Friday, October 11, 2019

TANZIA

TANZIA

Msimamizi wa Jimbo Katoliki la Mpanda mheshimiwa Monsinyori George Kisapa anatangaza kifo cha Frater Festo Ntalindanya kilichotokea jana tarehe 10/10/2019 akiwa anaendelea na matibabu huko Mwanza.

Frater Festo Ntalindanya alikuwa akiendelea na malezi na majiundo ya upadre na alikuwa anasoma Mwaka wa pili wa masomo ya Falsafa katika Seminari kuu ya Mtakatifu Anthony wa Padua - Ntungamo, iliyopo Jimbo Katoliki la Bukoba.

Mwili wake unatarajiwa kupokelewa Jimbo la Mpanda kutokea Mwanza jumapili ya tarehe 13 Oktoba na Maziko yatafanyika siku ya Jumatatu tarehe 14/10/2019 huko Mpanda - Ilembo katika eneo maalum la kuzika Mapadre

Ibada ya Misa Takatifu ya kumuombea Marehemu itafanyika katika Kanisa Kuu la Bikira Maria Imakulata, Jimbo la Mpanda.

Tunatoa pole zetu za dhati kwa Msimamizi wa Jimbo la Mpanda, Mapadre, Mafrateri wa Jimbo la Mpanda, Walezi na Mafrateri wote wa Seminari kuu ya Ntungamo, familia, ndugu, jamaa na marafiki, pamoja na jamii ya mafrateri wote Tanzania kwa kuondokewa na mwenzao.

Raha ya milele umpe Ee Bwana na Mwanga wa milele umwangazie, apumzike kwa amani, Amina.

©Classmates Lutakangwa na Maganga