Wednesday, January 29, 2020
DEFEND YOUR FAITH AS A CATHOLIC: Maisha ni sasa
DEFEND YOUR FAITH AS A CATHOLIC: Maisha ni sasa: Napenda kuanza kwa kusema kuwa ‘The means justify the end.’ Nikimaanisha namna ya maisha yetu ya sasa ndiyo yanayo au yatakayotuwezesha ku...
DEFEND YOUR FAITH AS A CATHOLIC: KIFO
DEFEND YOUR FAITH AS A CATHOLIC: KIFO: Sababu zinazoweza kupelekea Kifo [1] Kila mmoja wetu amekwisha kutambua ya kuwa kifo ni lazima tukipitie. Kwa kuwa hata katika uumbaji ...
DEFEND YOUR FAITH AS A CATHOLIC: AMRI ZA KANISA
DEFEND YOUR FAITH AS A CATHOLIC: AMRI ZA KANISA: Amri za Kanisa Kuna jumla ya amri sita za Kanisa. “Amri hizi za Kanisa zimepangwa katika fumo ...
AMRI ZA KANISA
Amri za Kanisa
Kuna jumla ya amri sita za Kanisa. “Amri hizi za
Kanisa zimepangwa katika fumo wa maisha ya maadili, zikifungamanishwa na
kulishwa na maisha ya Liturujia. Sheria hizi zilizowekwa wazi na mamlaka ya
kichungaji zina hali faradhi kwa lengo la kuwathibitishia waamini kiwango cha
chini kabisa cha lazima katika roho ya sala na juhudi ya maadili, katika kukua
katika mapendo kwa Mungu na jirani.”[1] Nazo ni zifuatazo kulingana na Misale ya
waumini:[2]
1.
Hudhuria Misa Takatifu Dominika na sikukuu
zilizoamriwa.
Inamtaka mwamini kutakatifuza siku
ya kumbukumbu ua fumbo la Ufufuko wa Bwana, lakini pia sikukuu kubwa za
kuheshimu mafumbo ya Bwana, ya Bikira Maria Mwenye heri, na ya Watakatifu.
Kwanza, kwa kushiriki adhimisho la Ekaristi ambamo jumuiya ya Kikristo inakusanyika,
na kupumzika na kuacha zile kazi na shughuli ambazo kwayo zingezuia
kutakatifuza siku hizo.[3]
Lakini pia mwamini apumzike kwa kuacha
kazi nzito.[4]
2.
Funga siku ya jumatano ya majivu; usile nyama siku ya
Ijumaa Kuu.
Ndugu
yangu unayesoma kitabu hiki, unapoongelea Jumatano ya Majivu huwezi kutupilia
mbali Kwaresima, maana Jumatano ya Majivu ndiyo mlanngo wa kutuingiza katika
Kwaresima. Kumbe hatuna Kwaresima pasipo Jumtano ya Majivu. Siku ya Jumatano ya
Majivu tunaanza rasmi kipindi cha Kwaresma ambacho kinadumu kwa muda wa siku
arobaini. Kwa nini siku arobaini? Waisraeli walikaa jangwani sku arobaini,
gharika kuu ilidumu siku arobaini, Yesu alifunga siku arobaini, kwaresma
inadumu siku arobaini. Miaka/siku arobaini katika Maandiko matakatifu inawakilisha
kipindi kamili cha mpito ambacho ndanimo jambo linaweza kufanyika na
likakamilika. Hivyo Kwaresma ni kipindi kamili cha mpito ambacho ndanimo
mapinduzi ya kiroho yanaweza kufanyika. Ni kipindi cha kufanya maandalizi ya
kuadhimisha sikukuu ya Pasaka. Na hivyo
kinaambatana na kupakwa majivu yatokanayo na matawi tuliyotumia Dominika ya
matawi; katika paji la uso kwa waamini lakini kwa Waklero kichwani. Katika
kipindi hiki mama Kanisa anatualika kufanya tathimini ya mahusiano yetu na
Mungu. Ni kipindi cha kufanya mapinduzi ya kiroho.Waamini tunahimizwa kwa
naamna ya pekee kuhudhuria liturjia ya leo.[5]
Majivu tutakayopakwa ni alama ya ukubali wetu kwamba sisi ni wadhambi, hatuna
thamani mbele ya Mungu na tunahitaji kufanya toba.
Katika
ulimwengu wa wayahudi majivu yalikuwa ni alama ya huzuni, masumbuko, uchungu au
uduni.[6]
Baadaye utamaduni huu wa kupakana majivu ulitumiwa na wakristo wa kwanza kama
alama ya toba. Mwaka 600 hivi, Gregory Mkuu aliifanya siku ya Jumatano ya
majivu kuwa siku ya kwanza ya Kwaresma na akaongeza urefu wa kipindi hiki cha
toba hadi siku arobaini. Miaka ya 800 hivi, baadhi ya makanisa yaliadhimisha
ibada ya Jumatano ya majivu kwaajili ya wadhambi waliokubuhu katika dhambi na
waliojulikana. Sasa pale walipoamua kufanya toba ndio walipakwa majivu. Hivi
wakati huu si wote walipakwa majivu ila tu wale walikuwa wadhambi waliojulikana
wazi, kama vile Malaya, wauaji, waasi n.k. Kuanzia karne ya 11, Kanisa
lilipanua ibada hii na kuwahusisha waamini wake wote na si wadhambi waliokubuhu
tu. Hatua za kuchukua ili tuweze kufanya vema mapinduzi ya kiroho, toba na
kubadilika. Tukubali kwamba sisi ni wadhambi. Tusipokubali kuwa sisi ni
wadhambi halafu hatutaona hitaji la kufanya toba na kubadilika. Ndio maana
tunapakwa majivu ikiwa ni alama ya kukubali kuwa sisi ni wadhambi hatuna
thamini mbele ya Mungu, na hivi tunahitaji kutubu. Kutumia misaada mbalimbali
ambayo itatusaidia kumrudia Mungu: Sala, kufunga na matendo ya huruma. Na hivyo
kwa kutambua tu wadhambi ndiyo maana tunapaswa kufunga siku hiyo ya Jumatano ya
majivu.
Lakini
pia usile nyama siku ya Ijumaa Kuu. Tukumbuke ndiyo siku Mkombozi wetu Yesu
Kristo anakufa msalabani. Na hivyo hatupaswi kula nyama kama waamini wenye
kutambua thamani ya wokovu wetu. Kwahiyo, ni siku ambayo waamini wanakuwa katika
huzuni, wakiomboleza juu ya kuondokewa na Mpendwa wao. Kama tujuavyo katika
hali ya maisha yetu ni kwamba nyama inatumika na kuthaminiwa kama chakula fulani
cha hali ya juu, yenye thamani na nzuri sana; ni katika uzuri huo watu wanaona
fahari na kuwafanya wafurahie. Mfano mzuri ni huu, ukitaka kuona au kusikia
sherehe fulani wanaisifia kuwa ilikuwa nzuri; wengi waseamao utasikia yaani
walijipanga kwelikweli: nyama ilikuwa ya kutosha kwa maana walichinjwa labda
ng’ombe watano (5) na kitakachofuata ni kinyaji, utasikia kulikuwa na pombe ya
kutosha kama ni ya kienyeji au bia au divai n.k. Kwa hiyo, hatunabudi kufunga
siku hiyo kula nyama.
3.
Ungama dhambi zako walu mara moja kila mwaka.
Pia sheria hii yahakikisha
maandalizi kwa ajili ya Ekaristi kwa kupokea Sakramenti ya Upatanisho.[7]
Hii inaonyesha mwendelezo wa kazi ya wongofu na msamaha wa Ubatizo.[8]
4.
Pokea Ekaristi Takatifu hasa wakati wa Paska.
Kama nilivyotangulia kusema, sheria
hizi za Kanisa kuwa inatoa walau kiwango cha chini. Kumbe amri hii yahakikisha
kiwango cha chini cha kupokea Mwili na Damu ya Bwana kuhusiana na sikukuu za
Pasaka, asili na kilele cha Liturujia ya Kikristo.[9]
Na hii inaenda sambamba na wale wanaoweza kushiriki Misa zaidi ya moja.
Waliowengi hawajui ya kuwa kama umemaliza Misa hii na ukampokea Yesu katika
maumbo ya mkate na divai, unapoenda Misa nyingine una haki ya kumpokea tena.
Siyo useme tu nimemaliza kumpokea Misa iliyopita na sasa sitaki au siwezi, wewe
mpokee labda kama unaona hufai pengine kiroho. Lakini kulingana na mazingira
unaruhusiwa kumpokea hata kama unajua kiroho ni mdhambi. Pengine ni kigangoni
na Padre amekuja kwa kuchelewa kwa sababu za kichungaji, basi usishindwe kwenda
kumpokea ilimradi tu ulikuwa umeshaweka nia ya kuungama kwanza. Na hivyo ukiwa
katika nia hiyo unaruhusiwa kukomonika, ila unuie kuwa mara baada ya kukomonika
basi unamtafuta Padre kwa maungamo. Ukifanya hivyo utakuwa hujatenda dhambi na
katika kumpokea Yesu maadam hujasitahilishwa basi inakuwa siyo kufuru na
unakuwa hujajitwalia hukumu yako.
5.
Saidia Kanisa Katoliki kwa zaka.
Ina maana ya kwamba waamini wana
wajibu na kazi ya kusaidia kutoa mahitaji ya Kanisa kila mmoja, kadiri ya uwezo
wake.[10]
Zaka hii inapaswa kutolewa fungu la kumi la kile unachojaliwa au ulichojaliwa.[11]
6.
Shika sheria Katoliki za ndoa.
Lakini kwanza tutambue kuwa ndoa ni
sakramenti kwa wakristo na hasa kwa wakatoliki. Ndoa ni agano kati ya mtu mume
na mtu mke. Ndoa ni aganao linalowafanya wanandoa kusihi pamoja kwa maisha yao
yote.[12]
Kwa kweli nakosa hata nguvu za kuongelea juu ya amri hii. Walio wengi naamini
ni mashahidi, ya kwamba amari hii haitendewi haki na wale wenye kuitendea haki.
Sina uhakika ni watu wangapi ambapo kwa uwazi kabisa tukiwauliza juu ya amri
hii kama wanaijua vilivyo; hususani wanandoa. Mama Kanisa katuwekea sheria
jumla mia moja na kumi na moja (111) za ndoa.[13] Sheria zenyewe hizi zimegawanyika katika
sehemu kumi (10) kwa kadiri ya Kitabu cha kanuni ya Kanisa Katoliki toleo la
pili la mwaka 1983.
a)
Mtazamo
wa kichungaji na nini kinatangulia maadhimisho ya ndoa (Pastoral care and what
must proced celebration of marriage)
b)
Vipigamizi
vya ndoa kwa ujumla (Diriment impediment in general)
c)
Vipingamizi
vya ndoa moja kwa moja (Diriment impediment specifically)
d)
Makubaliano
ya ndoa (Matrimonial consent)
e)
Nguvu
ya ndoa (Force of marriage)
f)
Ndoa
mchanganyiko (Mixed marriage)
g)
Kuadhimisha
ndoa wa siri (The secret celebration of marriage)
h)
Athari
za ndoa (Effects of marriage)
i)
Kuwatenganisha
wanandoa kwa muda (Simple separation of spouses)
j)
Kuhalalisha
ndoa ambayo haikuwepo (The convalidation of marriage).[14]
[1] KKK Na. 2041.
[2] Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania,
Misale ya Waamini, Toleo la Kumi, TMP Book Department, Tabora- Tanzania, 2008,
uk. 1077.
[3] Rej. MSK. Na. 1246- 1248.
[4] Rej. KKK Na. 2042.
[5] Rej. Katekisimu ndogo ya Katoliki
Jimbo la Iringa, Na .97, 100.
[6] Rej. Ayu 2: 8, 30: 19; Zab 102: 10.
[7] Ibid.
[8] Rej. MSK. Na. 989, 719.
[9] Rej. Sheria za Kanisa Katoliki, CIC
Na. 920, 708, 881.
[10] Rej. Sheria za Kanisa Katoliki, CIC
Na. 222, 1249-1251, 882, 25.
[12] Rej. Elias Nada, Karne ya Ishirini na Moja na Ndoa za Kikristo, Sayansi, Maisha ya
Familia na Ndoa, Chapa ya pili, Timia Printers, Moshi, 2015, uk. 25.
[13] Rej. Sheria za Kanisa Katoliki za
Ndoa, Mada ya saba Ndoa (CIC 1055-1165).
[14] The Code of the Canon Law, New
Revisedd English Translation, Harper Collins Publishers, Newsland, 1983,
237-258.
[15] Eze 18:23-28.
Tuesday, January 28, 2020
KIFO
Sababu zinazoweza kupelekea Kifo[1]
Kila mmoja wetu amekwisha kutambua ya
kuwa kifo ni lazima tukipitie. Kwa kuwa hata katika uumbaji (uhulushi) tunajua
ya kwamba mwanadamu ni mwili na roho. Mara tu baada ya kutungwa kwa mimba, basi
Mungu mwenyewe ndiye aiwekaye roho hiyo. Mwili daima unakufa, lakini roho kamwe
haifi. Ndiyo maana mtu baada ya kufa mwili ule unaoza kwani umeumbwa kwa
kitufaa (matter or material). Kwa lugha nyingine ni kwamba; ‘material body or
things normally corruptible, hence decay’.[2]
Kwani kupitia kuonja mauti, ndiyo njia pia itupasayo kufika kwa Baba. Huko
ndipo tutaenda kuishi na kustarehe kwa umilele. Sasa kwa kuwa kifo ni matokeo
ya dhambi ya asili waliyoifanya wazazi wetu wa kwanza yaani Adamu na Eva.
Zifuatazo zinaweza zikawa sababu ambazo zinaweza kupelekea kifo, kwa kila mmoja
wetu. Japo ni fumbo kwetu kama wanadamu kutambua tutakipitia kifo kwa njia ipi.
Ila uhakika tulionao tu ni kwamba lazima kifo tukipitie.
1 Magonjwa
Kama tutambuavyo mapisi (historia) ya
Adamu na Eva kule bustanini, ya kuwa waliishi vizuri na wanyama tena. Lakini
baada ya kukosa utii, Mungu aliamua kuwafukuza bustanini na kuwapa mapigo
kadhaa. Kama tutambuavyo ya kuwa hata dhahabu hujaribiwa kwa moto, ndivyo hivyo
nasi tunakutana na magonjwa mbalimbali ili kuyafanya maisha yaende cha
mikikimikiki. Kwa hiyo, maisha yetu kutokana na waandami (watangulizi) yaani
wazazi wetu wa kwanza, nasi hatunabudi kuyapokea mahangaiko, mateso yatokanayo
na maradhi. Kwani ardhi yote imelaaniwa kwa sababu wazazi wetu, vivyo hivyo
nasi tunapatwa na yale aliyosema Mungu kama laana juu yetu.
Sasa katika maisha yetu tunaona na
kushuhudia watu wengi wakifa kwa sababu mbalimbali za magonjwa. Na
kinachosikitisha zaidi ni kwamba wakati huu watu wamekuwa wengi na magonjwa
nayo yameongezeka sana. Kuna magonjwa ya aina mbalimbali ila zaidi ni ya
kuambukizwa na yale yasiyoyambukizwa. Lakini yote katika yote unachelewa kupata
huduma basi ugonjwa ukawa umeshamaliza au umeshatawala mwili kwa kiasi kikubwa
basi hata matibabu unayowekupata yanaweza tu kukusaidia kusogeza siku au hata
masaa. Magonjwa ambayo ni tishio sana kwetu mpaka sasa ni Mgandamizo wa damu
(Presha), kisukari, ugonjwa wa moyo, saratani au kansa, UKIMWI pia malaria.
Haya kwa kiasi kikubwa yamekuwa changamoto sana siku hizi. Mbaya zaidi
yaliyomengi yanayoonekana kuwa kama tishio kwa kipindi hiki, mengi yanachangiwa
na matumizi ya vyakula. Tunajikuta tumelalia kula vyakula vya kisasa (vyakula
vinavyopita viwandani) zaidi kuliko vile vya asili. Vyakula vilivyojaa sana
mafuta.
Tahadhari ni kwamba watu waanze kuwa na
mazoea ya kupima na kuchunguza afya zao mara kwa mara ili kujua maendeleo ya
afya zao. Hii isifanyike kwa ratiba bali iwe kila mara unapopata nafasi ya kufanya
hivyo basi fanya. Kwani unapogundulika unatatizo fulani na ukawa tayari kufuata
maelekezo ya Madaktari, aidha kwa kuacha kula aina fulani za vyakula au kwa
kula aina fulani tu za vyakula basi utakuwa katika nafasi nzuri ya kuuweka
mwili wako katika mazingira safi ya kupamabana na maradhi mengine ambayo
yanaweza kujitokeza.
Lakini pia kuna maradhi mengine sisi
wenyewe tumekuwa chanzo cha kuyasababisha. Kwa mfano kuna magonjwa ya mripuko
ambayo unakuta chanzo chake kikuu ni kushindwa kutunza mazingira yetu salama.
Hali tukitambua kuwa tukiyatunza mazingira hakika nayo pia yatatutunza. Kwa
mfano kuna watu wanakufa kwa sababu ya mripuko wa ugonjwa wa Kipindupindu au
Ebola. Sasa mtu watu hawa waathirika wanapokosa msaada wa huduma ya haraka
lazima tuwapoteze, maana hamna namna. Kwa hiyo, tuwe makini na tutunze
mazingira yetu nayo yatatutunza na kutuweka salama.
2 Ajali
Si kila ajali inatokea kwa sababu ya
uzembe wa wale wenye dhamana ya kuongoza vyombo hivyo vya safari. Lakini zilizo
nyingi chanzo kikubwa ni uzembe wa wahusika. Kuna aina mbalimbali za usafiri
ukiwemo wa nchi kavu (Barabarani), majini pia angani. Sasa mara nyingi utakuta
ni uzembe wa Dreva ama Nahodha ama Lubani kushindwa kuwa makini wakati
anaongoza chombo. Na hii inatokana na kuwa na mawazo tawanyishi. Yaani mawazo
yake muda fulani yanakuwa yametawanyika, badala ya kuwaza kile chombo
anachoongoza anawaza yaliyo nje ya pale. Sasa hali hiyo inapoendelea inaweza
kumfanya apoteze mwelekeo. Apotezapo mwelekeo tu, maana yake anaposhindwa kufuata
vigezo na masharti ya uongozaji basi utasikia ajali imetokea.
Si hivyo tu, bali wakati mwingine
inatokana na uchakavu wa vifaa au vimbo hivyo. Yaani unakuta ni chombo cha
usafiri na kila siku au kila mara kiko safarini, kwa bahati mbaya uangalizi
unapokuwa hafifu au mdogo. Sasa kama hamna uangalizi (kufanya service), kuna
siku kinaweza kuwa kibovu na kwa kuwa hakina uangalizi wa mara kwa mara au
kabla ya kuanza safari; basi mwisho wa siku kikiwa safarini na tatizo
limeshakuwa kubwa utasikia kimepata ajali na watu kadhaa wamefariki dunia papo
hapo na wengine kadhaa wamejeruhiwa. Kwa hiyo, kuwa na muda wa kuwa
tunavihakiki ubora wake ni muhimu sana.
Mara nyingine pia mazingira ya hali ya
hewa yanaweza kusababisha ajali. Kuna wakati hali ya hewa ndani ya maji
inachafuka yaani unakuta mawimbi yameongezeka na chombo kiko safarini au chombo
kiko angani na huko kinakutana na kani ya mvutano na hivyo kupelekea chombo
hicho kupoteza mwelekeo. Hatimaye kinashindwa kumudu au kukabiliana na hali
hiyo, basi kinabaki kuongozwa na hali ya hewa ya wakati huo. Na baadaye
utasikia kimepata ajali. Kama tujuavyo Meli ya Mv. Bukoba ilivyozama tarehe
21-05-1996 na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 800.
Lakini pia sababu nyingine ya ajali
inakuwa ni Dreva mwenyewe asiyejali mwendokasi. Mfano ulio hai ni huu, kuna
aina tatu za Madreva; Dreva Kenge (huyu ni Dreva wa kukurupuka, pasipo kujali
ubora wa chombo chake pia mwendokasi), Dreva Nyoka (huyu anaendesha kwa
kupindapinda, yaani anaenda kwa kukatakata makona mfano anataka kumpita
mwenzake shemu mbaya au isiyoruhusiwa na akiwa katika mwendokasi), na wa mwisho
ni Dreva Kinyonga (huyu ni Dreva anayeendesha kwa usalama na anafuata kanuni
zote za barabarani vizuri). Kumbe mwendokasi unapelekea wakati mwingi ajali,
maana anapokutana na kona kali na yuko mwendokasi lazima limshinde kukata kona,
mwisho wa siku gari litamshinda kumtawala na kuanguka au kupindukapinduka.
Ajali nyingine zinakuwa za mtu husika
mwenyewe. Pengine ni fundi umeme. Sasa akiwa yuko juu ya nguzo akateleza na
kuanguka, kwa bahati mbaya akaangukia sehemu mbaya. Kumbe inaweza kumpelekea
katika kifo. Wakati mwingine watoto wanapenda kukwea juu ya miti yenye matunda
misimu yake ikifika. Sasa inatokea wakati fulani akiwa amekwea anakanyaga tawi
vibaya au tawi alilokanyaga bila kujua likawa limeshakauka. Mwisho wa siku anajikuta
ameshashuka nalo chini. Na pengine mazingira ya pale chini yakawa hayako
vizuri, basi anapoanguka vibaya basi inaweza kumpelekea katika kifo.
3 Vita
Kinyume cha vita ni amani. Kwa hiyo,
kwa maneno mengine vita ni ukosefu wa amani. Kumbe vita inaambatana na utumiaji
wa nguvu kupita kiasi (yaani silaha). Vita kwa yenyewe siyo kitu kizuri, kwani
mara zote inaenda sambamba na umwagaji wa damu kwa watu wasio na hatia au wenye
hatia. Licha ya kwamba katika maadili inaongelea katika sababu yenye haki, basi
kwa haja ya hali ya kujihami n akujilinda basi itumike. Lakini katika yote,
licha ya sababu inayotambulika hata kimaadili. Bado vita lazima ihusishe
mauaji. Kwa mfano wa vita ya kwanza ya dunia mwaka 1918, pia tazama mauaji ya
kimbari (Mauaji dhidi ya Wtutsi) kule Rwandwa kati ya 7-04 mpaka 15-07 mwaka
1994. Sasa takribani watu 500,000 mpaka 1,000,000 waliuawa. Kati yao asilimia
70 wakiwa Watutsi;[3] vita
zote hizi zilihusisha mauaji ya watu wengi sana. Tusiende mbali sana hata kwetu tukikumbuka vita ya Tanzania na Uganda
(Vita vya Kagera) dhidi ya Idi Amin Dada iliyodumu kwa muda miezi sita, kuanzia
mwaka 1978 mpaka 1979. Inasadikika takribani Askari wa Tanzania 373, Raia pia
takribani 1500 na Askari 600 miongoni mwa 3000 wa Libya nao waliuawa.[4]
Ilihusisha vifo vya watu wengi tu. Na katika hao wapo waliokuwa hawana hatia lakini
wengine walikuwa ni wenye hatia.
4 Mamlaka
Katika nchi basi serikali imetoa
dhamana kwa chombo fulani kushughulikia mambo kama hayo ya utoaji wa uhai. Kwa
mfano nchi ya Tanzania imetoa mamlaka
katika vyombo viwili kwa wale wanobainika kuwa waharifu. Kuna chombo cha
Mahakama, ambayo ndiyo inayotoa hukumu kwa watu wanaobainika kufanya makosa
makubwa. Lakini utekelezaji wa agizo la mahakama unafanya na chombo cha
Magereza. Kumbe, pale mtuhumiwa anapokuwa amehukumiwa kifo yaani kunyongwa na
mahakama; ni jukumu la Magereza kuteke agizo hilo kwa mujibu wa mamlaka
waliyonayo. Sasa utekelezaji wa mamlaka huo unapofanyika, basi hupelekea kifo
kwa mtuhumiwa.
5 Kujitoa mhanga
Tumekuwa tukisikia mashambulio
mbalimbali yanayotekelezwa na vikundi mbalimbali katika nchi fulani.
Mashambulio haya ndiyo kusema kwa lugha nyingine ugaidi. Utekelezaji wa kujitoa mhanga huu
unawezakunywa na mtu mmoja, kwa kutumia silaha za miripuko; ambapo anatekeleza
shambulio hilo la kujitoa mhanga akiwa katika mazingira ya kuzungukwa na watu
wengi. Ni dhamiri ya kuwa kwa kutenda hivyo anajikuta kajiua na kuwaua wengine
wengine. Kwa mfano tumekuwa tukisikia vikundi kama Alshababu kule Nchini
Somalia, Boko haram kule Nchini Nigeria, Alkaida na vingine vingi. Ambavyo mara
kadhaa vimekuwa vikiripotiwa kufanya mashambulizi ya kujitoa mhanga katika njia
kadhaa. Kumbe kwa kitendo cha kujitoa mhanga tayari kinaambatana na mauaji ya
watu.
6 Umri mkubwa
Hiki ni kifo cha asili (natural death).
Kama tujuavyo kuwa uhai tumepewa na Mungu na unatoka kwa Mungu. Vivyo hivyo na
maisha yetu yote yako kwa Mungu, kwani ndiye ajuaye ni katika umri gani basi
tutapaswa kuyiacha dunia hii. Kwa hiyo, siyo wote walioandikiwa kufikia uzeeni,
bali wale wachache. Sasa unapokutana na Mzee kabisa aliyekula chumvi ya kutosha, yaani aliyefikia
hatua ya kulelewa kama mtoto maana hajiwezi kwa lolote. Basi anapokufa tunaona
kuwa ni kama haki yake, kwani umri wenyewe unaruhusu. Na watu wa namna hii mara
nyingi huwa wanakufa wakiwa usingizini. Yaani kabla ya kulala mmeagana vizuri
na hakuwa na tatizo au ugonjwa, ila asubuhi mnaamka kwenda kumjulia hali
mnakuta ameshakufa. Kumbe umri unapokuwa wa kutosha basi mwisho wa siku zile
seli nazo zinachoka mpaka kufikia hatua ya kutojiweza, hatimaye kupelekea kifo.
7 Majanga ya asili
Majanga ya asili wakati mwingine
tunajitafutia vifo kupitia yenyewe aidha kwa kutokujua au kwa kujua. Kwa mfano
mtu anaamua kwenda kujenga bondeni ambapo anajua mafuriko yakitokea hawezi
kubaki salama, lakini anapoambiwa na kutahadharishwa ya kuwa anapaswa ahame ila
yeye anabakia huko. Yakumkuta yakifika licha ya kuwa ni majanga ya asili lakini
yeye kajiweka katika mazingira ya kukumbwa na matatizo. Kuna majanga ya
kumbunga, tetemeko la ardhi, Tsunami, njaa, ukame pia miripuko ya Volkano. Haya
yote ni baadhi ya majanga ya asili, hivyo yanapotokea kwa hakika hayawaachi
watu salama. Kuna baadhi wanaenda nayo, yaani kifo kinawakabili. Hatuwezi
kuyaepuka kwa kweli zaidi tunaaswa tu kuchukua tahadhari. Kwa mfano tetemeko la
ardhi lililotokea mkoa wa Kagera mwaka 2017 lilisababisha maafa makubwa, watu
kupoteza nyumba zao na mali zao pia wengine walipoteza maisha (walikufa).
8 Kifo cha maamuzi binafsi
kuna watu tumekuwa tukiwaona au kusikia
au hata kushuhudia wakipoteza maisha aidha kwa kujitakia au kwa kutojitakia.
Wale wanaojitakia ni kama wale wanaofikia hatua ya kukata tamaa ya kuishi, na
mwisho wa siku wanaamua kuchukua uamuzi aliouchukua Yuda Iskalioti wa kujiua
kwa kujinyonga. Sasa watu wa hivi mimi nawatazama katika mwono huo, ya kuwa
wamejitakia. Lakini kuna wale wanakufa bila kujitakia. Kwa mfano unasikia mambo
ya utoaji mimba ambao ni dhahiri ni kuuwa tu. Au mwingine anajifungua vizuri
mtoto lakini mwisho wa siku anaamua kumtupa chooni au kichakani. Hicho nacho ni
kifo cha mtu asiye na hatia na hakujitakia.
[1] Rej. Richard A. Kungi, Kupata nguvu Saa ya Majonzi, Maana na
Uponyaji katika Kifo cha Umpendaye, FGD Tanzania Limited, Dar es salaam,
2018, uk. 4-12.
[2] Ludwig OTT, Fundamentals of Catholic Dogma, J. C. Bastible (ed), P. Lynch
(trans.), Tan books and Publishers, Inc, Rockford, 1960, uk. 96-100.
[3] WIKIPEDIA- Rwanda
genocide, https://en.m.wikipedia.org/wiki/Rwanda-genocide, retrived on
12/05/2019.
[4] MWANANCHI, https://www.Mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Yusufu-Lule-aondolewa-madaraani-30/1597296-4925576-format-xhtml-uwyeepz/index.html, recited on 12/05/2019.
Wednesday, January 22, 2020
Maisha ni sasa
Napenda kuanza kwa kusema kuwa ‘The means justify the end.’ Nikimaanisha namna ya maisha yetu ya sasa ndiyo yanayo au yatakayotuwezesha kuiona ya kesho. Maneno mengine, ni kwamba maisha tuishiyo leo ndiyo yanayotabiri kesho yako wewe, mimi na yule. Kwa hiyo namna ya kuishi kwetu leo, inatupatia fursa ya maandalizi ya maisha ya hapo baadaye mara baada ya maisha ya hapa dunia. Kwa mantiki hiyo, tuna kila sababu ya kujitahidi kuishi maisha ya kulenga hapo baadaye itakuwaje. Kufikiri zaidi (foresee or aim high) itakuwaje, na kama umeshaanza kuishi kwa kuona na kutenda kwa kuangalia au kulenga juu ya mwisho wako ni vizuri.
Endelea na kasi hiyo, kwa kusonga mbele
na usirudi nyuma kamwe (Ever forward never backward). Kama mwaliko wa siku zote
wa Mheshimiwa Rais Dr. John Joseph Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania mara zote anavyopenda kutuasa kama wananchi kuwa tusibaki
kutazamana tu bali anasema “Wewe chapa kazi tu.”
Pia tukiongozwa na methali isemayo,
‘Ngojangoja yaumiza matumbo’ tuchangamkie fursa kwani wakati wenyewe ndiyo huu
wa kufanya na kuandaa maisha yetu ya hapo baadaye kuwa mazuri. Tusikae
tukabweteka mpaka kufikia wakati ule wa NINGE…. Ninge…. Hii huja mwisho wa
safari, ambapo tunakuwa tumeshachelewa na haiwezekani tena. Kama tusemavyo kuwa
‘maji yakishamwagika huwa hayazoleki.’ Ni kwa mantiki hiyo hiyo tunaona mfano
ule wa mtu tajiri na Lazaro. Tajiri anvyomlilia Ibrahimu kwa kumwomba amtume
basi aende duniani ili awambie juu ya hali aliyokuwa akipitia ili basi nao
wasiweze kuingia huko. Lakini tunaambiwa kati yao wametenganishwa na shimo
kubwa, na hivyo haiwezekani. Kwa kuwa kuna wengine walioko huko dunia basi
wasipowasikiliza hao nao pia wataingia kwa tajiri alipokuwa. Hapa anatufundisha
kuwa haiwezekani tena kurudi nyuma, na hivyo tusiisubirie hiyo
ninge….tukajikuta tumeshachelewa sana.[1]
Kumbe kwa kuwa mimi na wewe bado tuna nafasi ya kujirekebisha basi tufanye
hivyo; kabla ya NINGE… haijaja kusikika masikioni mwetu maana muda utakuwa
umeshaisha tena wa kusema tunaweza kurekebisha maisha yetu.
Na hivyo kama wasemavyo kuwa ‘Bahati ya
mwenzio usiilalie mlango wazi.’ Kuna mtu mwingine anapenda kuyafanya maisha
yake kuwa ya mazoea. Tafadhali, mwanadamu daima ni mwili na roho pia mwanadamu
hulka yake ni kubadilikabadilika kama kinyonga. Kubadilikabadilika huku ni kule
kutoka hali hasi na kwenda hali chanya. Mfano mtu ameshauriwa kuuacha
mwenendowake mbaya na afanye hivyo kweli kwa kubadilika au kubadilisha mwenendo
wake. Si hivyo tu, ni busara ya kawaida kwamba unapoenda sehemu ukawakuta
wanaomboleza basi nawe jiunge nao katika maombolezo hayo. Na kwa kufanya hivyo
kile kinachofanyika pale ni kwa manufaa ya jamii nzima, wala siyo cha mtu
binafsi.
Sasa, kuna watu wengine kupitia mazoea
tunashindwa kuelewa somo hilo juu ya mabadiliko. Kwa mfano, kuna mtu
anamchukulia mtu fulani kuwa wa mfano kwake katika maisha; mbaya zaidi mtu yule
maisha yake ni ya ajabu ajabu. Kwanini sasa aige maisha hayo? Ukifuatilia
utakuta wanatabia zinazoendana au kukaribiana. Wana namna zinazoendana katika
yale wayapendayo na yale wasiyoyapenda katika maisha yao. Na huu kwa hakika ni
mfano uliohalisi, kwamba jaribu kuchunguza wale watu waliomarafiki. Utakuta
kuna kitu wanashirikiana aidha kitabia na mwenendo mzima wa maisha.
Kumbe tambua kuwa kila mtu anabahati
yake kuanzia leo. Sasa wewe utasema naishi hivi kwa maana hata fulani anaishi
hivi na maisha yanaenda. Ila jua kila mmoja alizaliwa kwa mama yake pekee, si
hivyo tu tena kila mmoja alizaliwa peke yake, anaishi peke yake, atakufa peke
yake na mwisho atazikwa pekeyake. Kwa kujua hilo ndiyo maana kila mtu anakuja
na bahati yake. Kwa hiyo, haya malimwengu yasikusumbue kabisa; kwa kuwa
tumeyakuta. Kwani tumezaliwa tuli uchi na tutarudi vivyo hivyo.[2]
Huyu rafiki yako, swahiba, shosti wote umewakuta tu. Kumbe huna sababu yoyote
ya kumfanya mtu huyo awe kama mungu-mtu. Ndiyo maana ukiwa mtu wa kuchukua na
kuiga kila kitu kama kilivyo (copy and paste) kwa mwingine unaweza kuishia
kubaya. Maana huwezi yeye ameandikiwa nini na Mungu, maana yeye tunaambiwa
alitujua tungali tumboni mwa mama zetu.[3]
Ndo hiyo utashangaa mwenzako, licha ya maisha yake mabaya aliyokuwa anaishi ila
dakika za mwishoni anamrudia Mungu; ila wewe isitokee hivyo. Kwa hiyo
tujihadhari sana katika maisha yetu. Tujiepushe na kuiga kila kitu bali yale
yaliymazuri basi tuyaige na kuyafuata. Lakini katika yale yanayoweza
kutupotosha au kutupeleka katika njia isiyo sawa, ambayo inaweza kututenga naye
Mungu; basi hatunabudi kuyatupilia mbali. Kwa maneno mengine hatunabudi
kuachana nayo tena moja kwa moja.
Subscribe to:
Posts (Atom)