SAIKOLOJIA YA MAISHA Na.Fr.SIMON R.LIBERIO, MWALIMU WA SAIKOLOJIA
MAISHA YA MWANADAMU YANAMUHITAJI MWANADAMU MWENZAKE
Saikolojia ya maisha ya mwanadamu ina Mambo mengi.Katika maisha ya mwanadamu Kuna Mambo mengi yanayokutuletea furaha au msongo kwa jina maarufu "stress". Kuna mengi sana duniani yenye kufurahisha.Kuna mengi duniani yanaweza kukukatisha tamaa.Kuna mengi duniani yanaweza kupunguza kasi na munkali wa kuleta Maendeleo tungeita KISAIKOLOJIA " kususia" au kususa. Mwanadamu ameumbwa kichwani mwake kumejaa kama stoo ya maboksi mbalimbali.
Maisha ya mwanadamu Duniani yanaweza kuwa mafupi au marefu.Mwanadamu wa Zama zetu za utandawazi, utandawizi, na utandawazimu.
MAMBO YANAYOWEZA KUKUPATIA UTULIVU WA MOYO KATIKA MAISHA.
1.FANYA UNACHOKIPENDA MAISHANI
Maishani kuna mambo mengi na vivutio hi vingi.Wataalamu husema, " Mirusi mingi humpoteza mbwa". Ukiishi bila malengo siku zote utabaki mtu wa kushika Hiki unaacha kila kitu.
2.Maishani jitahidi kufanya kazi kwa bidii na ujipatie riziki ya kila siku.Uache kuwa mtu wa kulaumulaumu.Acha kulaumu laumu watu.
3.MAISHANI ISHI MAISHA YAKO /ZAKUAMBIWA CHANGANYA NA ZA KWAKO (J.K)
Uishi maisha yako mwenyewe.Badala ya kumlaumu aliyekunyima chakula. Tafuta mbinu halari za kupata chakula chako.Azima hata madum chota maji.Uza maji hautalala njaa.Omba vibarua hata vya kulima mashambani hautalala njaa. Ukishangaa mjini utalima lami. Dunia ni gunia hakuna atakayekuhurumia kwa uvivu na kupuuza fursa. Hata Mimi sitakuonea Huruma kwa Upumbavu wako wa kufikiri kuwa maisha ni "isidingo" au "ze comedy".
4.UWE MBUNIFU KATIKA UJASIRIAMALI
Ulimwengu huu sio wa Bibi yako. Ni ulimwengu wa watu tena wwshindani.Ujasiriamali mwingi. Biashara kwa wingi. Siasa uchwara nyingi. "Figisufigisu" nyingi. roho mbaya nyingi. roho za mtakafujo.roho za mtaka vyote. roho Mtakavitu.Ndiye anayeutawala ulimwengu wa nope nikupe. roho msakatonge.roho gombania madaraka. roho gombania vyeo. roho mchafu wivu.Dunia ina mtima nyongo. Marekani haiwezi ikacheka cheka na Taifa la uchina na kinyume chake ni sahihi. Urusi haiwezi ikachekacheka na Taifa la Amerika na kinyume chake ni sahihi.Ndio hapo tunaweza tukakibaliana kuwa adui wa bodaboda ni bodaboda. Adui au hasimu wa mfanyakazi ofisini ni mwenzake hasa wafanyakazi wavivu, wakosa ubunifu.Waiba vyeti vya mitihani.Waingia kazini kupitia migongo ya baba na wajomba zao.Watu wanamna hii usiwape taarifa za Maendeleo yako.
5.MAHATMA GHANDI ALISEMA " KAMA HAUNA SURA YA KUTABASAMU KAMWE USIANZISHE DUKA ".
Saikolojia ya muuzaji na mnunuzi ni mguso na ukaribu wa watu wawili.Mwwnye kuhitaji huduma na mwenye hitaji wa "shekeri". Mfanyabiashara anapaswa kuwa mnyenyekevu. Angalieni wachaga hapa Tanzania. Mteja si mfalme tu bali Ni ndugu alisema Baba yangu Mzee Liberio Bahanza hotelini nyumbani Mabamba.
6. TAMBUA VIPAJI VYAKO KISHA KIFANYIE KAZI KIPAJI UNACHOKIONA KINATOA MATUNDA WAZI
Kama mwanzo nilivyoandika kuwa " kichwa cha mwanadamu kimesheheni maboksi mengi yenye fikra pembuzi nyingi". Kichwa cha mwanadamu na moyo wake hujazwa na ndoto kibao. Ndoto nyingi bila kuzitekeleza ni sawa na kuwa na meno yote tena mabovu.
7. SHIKA JAMBO MOJA NA ULISHIKILIE,KIFANYIE KAZI, PAMBANA, LIWEKEA VIPAUMBELE
Maisha yanadai utulivu. Ishi kwa kutimiza ndoto zako. Ifanyie kazi ndoto yako moja ya kwanza kishapo jiulize je ninachokifanya kinanipatia raha na utulivu wa moyo? Ili kuamini kile unachokifanya kinakupatia amani ni pale unaporidhika hapo ulipo hata kama si kwa kipato kikubwa sana, angalau unaweza ukajipatia mahitaji ya msingi yaani :Makazi nadhifu, chakula bora, maji safi, mavazi, ada ya kulipa kwa watoto shuleni kwa wenye watoto au unaoweza kuwasaidia.
8. JITAHIDI KUWAVUMILIA WATU WENYE "TABIA NGUMU" (HARD CHARACTER PEOPLE) AU "SPECIAL CHARACTER PEOPLE /COMPLICATED BEHAVIOUR.
Ninapoandika kuwavumilia watu wasumbufu na wenye tabia ngum. Yapo makundi mengi ya watu wenye tabia zao ngumu. Wapo walalamishi kwa kila Jambo.Wapo wanaopinga kila Jambo.Watu wa namna hii wanashida kichwani. Au uelewa wao wa kifikra ni mdogo sana. Watu wanamna hii hawana mpanuko mkubwa wa kimawaz. BeNa be hawana "exposure" tuseme ni washamba wa Mambo mengi. Hujifanya wajuaji wa kila jambo. Wapo wanaopenda wawajali huku wao hawana muda na wenzao. Wanaopenda kubembelezwa huku wao hawana muda na mtu. Wapo wanaopenda kuhurumiwa huku wao hawako tayari kuhurumiwa. Wapo wanaopenda waheshimiwe huku hawawaheshimu wenzao. Wapo wanaolalamikia wenzao huku wao ni mizigo kwa watu.Wapo wanaotaka kusikilizwa huku hawako tayari kuwasikiliza wenzao.
9.TIMIZA NDOTO ZAKO HAKUNA MWINGINE "WEWE"
Furaha yako itapambwa pale utakapokuwa umeishi ndoto zako, ni Kama katika Maandiko Matakatifu Mzee Simeon anatoa shukrani kwa Mungu kwakumvumilia akaishi maisha marefu sana mpaka amwone Masiha wa Bwana.Anasema "Sasa Bwana WAWEZA kumruhusu mtumishi wako aende kwa amani kwakuwa macho yangu yameuona wokovu wa Mungu wetu.
10. Epuka kujitengenezea maadui wako mwenyewe.Uwe na kauli njema. Uwe na simile. Mtu mzima hspigwi viboko. Mtu mzima huambiwa kiutu uzima.Hakaripiwi Kama dogo wa darasa la kwanza
11.Uwe tayari KUYAPOKEA Mambo magumu.Na zaidi ya yote ubaki na hekima ya Dini na Falsafa ya Watao kutambua kuwa unaweza ukavae koti au Sweta lakini hauwezi kuiondoa baridi. WAWEZA kuwasha taa na umeme lakini hauwezi kuiondoa Giza. Mwisho,Pokea hekima.@Fr.SIMON R.LIBERIO
Saturday, February 22, 2020
Wednesday, February 12, 2020
AKILI
TUCHUNGULIE UBONGONI MWA MWANADAMU BILA UPASUAJI,
KAZI NZURI NI IPI DUNIANI?
MBAGALA SPIRITUAL CENTER ,DAR
@ LIBERIO S.BAVUGUBUSA C.
KAZI NZURI NI IPI DUNIANI?
MBAGALA SPIRITUAL CENTER ,DAR
@ LIBERIO S.BAVUGUBUSA C.
Swali huenda likatuchanganya kabisa,au tuseme kuna kazi mbaya? Muuliza swali huenda angeuliza kazi harali na kazi isiyoharali.
Hata hivyo ,Ni vema kuwa mwaminifu kwa muuliza swali.Nakumbuka nikiwa shule ya msingi Mabamba ,Kibondo wilayani wakati huo shule ikiitwa Misheni.
Tulikuwa tukisoma kwa mashindano ili kila mmoja awe wa kwanza darasani.Nilifuata maelekezo ya Baba yangu alivyoniambia " Kamwe Shuleni mwanangu usiwe rafiki wa mambulula" watakubwetesha. Na hapo nikajichagulia marafiki wasio "mbulula"(wenye uwezomdogo darasani).
Kati ya wanafunzi darasa la Pili na la nne waliojiweza walikuwa kama wafuatao, Valeriani Mbweja, Verasius W.Teyumwete, Julius Batromeo( mtoto wa mkulima), Victor na Dickson A. Kibala, Adili Husein Tamim, Simon Njuguma,Tausi Athuman,nk. Hao walikuwa ni vikolezo vya kuhamasishana kufanya vizuri darasani.
Mara kadhaa tulijikumbusha ule wimbo wa akina Baraka,Neema na Misa, " What are you going to be " ? Maana yake Unataka kuwa Nani? Mmoja alijibu angependa kuwa "Mwalimu", mwingine alijibu angependa kuwa "nesi" ,Mwingine alipenda kuwa "mkulima".Kwa akili zanguza kitoto niliamini kuwa kila mmoja alichagua kazi aliyoipenda zaidi kuliko ile ambayo hakuitaja.
Hiyo ni mifano hai mara nyingi ninaitumia katika kuinuana kifikra, kiuchumi na kiutendaji.
Marthin Luther Jr. Mmarekani mweusi na Mwanaharakati wa haki za watu weusina wenye asili ya Afrika na walatino aliwahi kutushauri katika maisha kwa ujumla kuwa katika maisha kuna Mambo yatakayokufanya ufike pale ambapo ungependa kufika.
Moja,Ufanye kazi unayoipenda.Kimsingi Anza na kile unachopenda japo si mbaya ukafanya kile unachopendekezewa hasa "wahenga" wakubwa wako wameonelea kipaji ndani mwako.Ninampenda sana Mheshimiwa huyu na Mwanaharakati huyu Marthin Luther Jr,mawazo yake katika pointi hii amefanana na Mzee Gotama Budha aliyewahi kusema "Tunakuwa hivi kwa KUTOKANA na mawazo yetu" ndio kusema tuko hivyo kutokana na mawazo yetu. Ambapo Mwanafasafa wa Kichina Confucius katika karne ya 5 kabla ya Kristo anasema " Ukitaka kufanya Jambo lifanye kwa moyo, na ulitaka kwenda mahali nenda kwa moyo". Kumbe hata wahenga waliliona kwa kusisitizia kuwa hatunabudi kuchagua chaguo letu wenyewe. Ukifanya kazi ya kuchaguliwa binafsi naifananisha na la kuchaguliwa mchumba ili awe mama yoyo. Kumbe ni vema kufanya kile unachokipenda.Hiyo kazi unayoipenda ndio kazi yako nzuri.Kama sio nzuri ieache ili ukalime lami.Kishapo ujipimie mwenyewe joto la jiwe.Ndipo akili zitakapokusogea na kugundua ukweli wa Falsafa ya kutafuta kazi nako ni kazi.
Hata hivyo ,Ni vema kuwa mwaminifu kwa muuliza swali.Nakumbuka nikiwa shule ya msingi Mabamba ,Kibondo wilayani wakati huo shule ikiitwa Misheni.
Tulikuwa tukisoma kwa mashindano ili kila mmoja awe wa kwanza darasani.Nilifuata maelekezo ya Baba yangu alivyoniambia " Kamwe Shuleni mwanangu usiwe rafiki wa mambulula" watakubwetesha. Na hapo nikajichagulia marafiki wasio "mbulula"(wenye uwezomdogo darasani).
Kati ya wanafunzi darasa la Pili na la nne waliojiweza walikuwa kama wafuatao, Valeriani Mbweja, Verasius W.Teyumwete, Julius Batromeo( mtoto wa mkulima), Victor na Dickson A. Kibala, Adili Husein Tamim, Simon Njuguma,Tausi Athuman,nk. Hao walikuwa ni vikolezo vya kuhamasishana kufanya vizuri darasani.
Mara kadhaa tulijikumbusha ule wimbo wa akina Baraka,Neema na Misa, " What are you going to be " ? Maana yake Unataka kuwa Nani? Mmoja alijibu angependa kuwa "Mwalimu", mwingine alijibu angependa kuwa "nesi" ,Mwingine alipenda kuwa "mkulima".Kwa akili zanguza kitoto niliamini kuwa kila mmoja alichagua kazi aliyoipenda zaidi kuliko ile ambayo hakuitaja.
Hiyo ni mifano hai mara nyingi ninaitumia katika kuinuana kifikra, kiuchumi na kiutendaji.
Marthin Luther Jr. Mmarekani mweusi na Mwanaharakati wa haki za watu weusina wenye asili ya Afrika na walatino aliwahi kutushauri katika maisha kwa ujumla kuwa katika maisha kuna Mambo yatakayokufanya ufike pale ambapo ungependa kufika.
Moja,Ufanye kazi unayoipenda.Kimsingi Anza na kile unachopenda japo si mbaya ukafanya kile unachopendekezewa hasa "wahenga" wakubwa wako wameonelea kipaji ndani mwako.Ninampenda sana Mheshimiwa huyu na Mwanaharakati huyu Marthin Luther Jr,mawazo yake katika pointi hii amefanana na Mzee Gotama Budha aliyewahi kusema "Tunakuwa hivi kwa KUTOKANA na mawazo yetu" ndio kusema tuko hivyo kutokana na mawazo yetu. Ambapo Mwanafasafa wa Kichina Confucius katika karne ya 5 kabla ya Kristo anasema " Ukitaka kufanya Jambo lifanye kwa moyo, na ulitaka kwenda mahali nenda kwa moyo". Kumbe hata wahenga waliliona kwa kusisitizia kuwa hatunabudi kuchagua chaguo letu wenyewe. Ukifanya kazi ya kuchaguliwa binafsi naifananisha na la kuchaguliwa mchumba ili awe mama yoyo. Kumbe ni vema kufanya kile unachokipenda.Hiyo kazi unayoipenda ndio kazi yako nzuri.Kama sio nzuri ieache ili ukalime lami.Kishapo ujipimie mwenyewe joto la jiwe.Ndipo akili zitakapokusogea na kugundua ukweli wa Falsafa ya kutafuta kazi nako ni kazi.
Kazi nzuri ni ipi, ni ile ambayo itakudai Ufanye kwa bidii tena kwa masaa kibao.Kama Wachina hufanya kazi masaa mengi,mpaka kituo cha haki za kibinadamu Amnesty huthubutu kuingilia Kati kwani wao hufanya kazi kwa Falsafa ya "punda afe mzigo ufike" ningewatania akina " hung yang ping" kwamba hufanyakazi Kama watumwa wakilenga kumkimbiza "kidume" cha Dunia ndio Waamerika ambao juzi Rais Donald Trump alijinasibu kwa ngembe nyingi kuwa katika utawala wake ameirudishia heshima tena Amerika.Ha ha ha kibwagizo cha wiki hiki.
Mwanaharakati Marthin Luther anasema, kazi uipendayo ifanye kwa muda wa kutosha na zaidi ya yote kwa ueledi mkuu.
Kazi nzuri ni ile utakayotaka kuifanya ili mwisho wa siku "utusue" utoboe ,ama uyaone matunda yake Tena waziwazi kwa kuacha Falsafa au "legacy" kwa kimombo. Usifanye kazi ilimradi utokwe na jasho, jasho haliuzwi hata ukipiga "push up" au ukala pilipili za wahindi jasho litakutoka. Kazi nzuri itakudai kuhenyeka kweli.Itakutaka uifanye kwa moyo.
Mwanaharakati Marthin Luther anasema, kazi uipendayo ifanye kwa muda wa kutosha na zaidi ya yote kwa ueledi mkuu.
Kazi nzuri ni ile utakayotaka kuifanya ili mwisho wa siku "utusue" utoboe ,ama uyaone matunda yake Tena waziwazi kwa kuacha Falsafa au "legacy" kwa kimombo. Usifanye kazi ilimradi utokwe na jasho, jasho haliuzwi hata ukipiga "push up" au ukala pilipili za wahindi jasho litakutoka. Kazi nzuri itakudai kuhenyeka kweli.Itakutaka uifanye kwa moyo.
Kazi nzuri ni ile utakayokuwa umejiwekea malengo ya kukukombowa.Katika Kitabu kilichoandikwa na Robert T. Kiyosaki, "Rich Dad and Poor Dad'' kinaonesha tofauti ya mtazamo wa Mtoto wa mkulima(poor Dad) tuseme yeye anakwenda Shuleni ili aajiliwe huku mtoto wa Rich Dad (Tajiri) anakwenda shule ili ailinde pesa kiusomi na sio apate kazi ya kuajiliwa na mtu.Anakwenda shule ili apate akili zaidi ya kuilinda pesa asifilisike mpaka kizazi cha nne ndio hao wafanyabiashara Waasia. Wabongo sehemu kubwa tunajua kutafuna pesa tulizoachiwa KWENYE mirathi na uzuri wa Bahati pesa za mirathi tunazitafuna bila kuzihurumia,kwa kigezo kilekile cha kuzipata kwa nasibu na bila kuzihangaikia.Ndio kisa pesa za mirathi hazilipi na hazikufanyi uumize kichwa.
Lao Tse Tzu MDAU mkubwa wa Falsafa za akina Confucius aliwahi kusema katika kazi nyepesi jiandae kukutana na magumu ili uifanye kwa ueledi mkubwa na umakini. Huyu Mwanafasafa Mchina anataka kutukumbusha tufanye Mambo kwa umakini yaani "serious". Maandiko matakatifu yametoa "ole" kwa wale wajiaminio kipumbavu. Ole wao wajiaminio kipumbavu, Upumbavu ni uparambogo,kutaka kujifanya unajua huku hujui na hutaku kujua wala kufundishwa.
Maisha na kazi ningesema ni sawa na kuwa na barabara nzuri zimetengenezwa kwa ajili ya magari huku hakuna magaru na watu wenyewe waamue kupita vichakani. Wajerumani walikuwana Falsafa ya kupiga kazi na sio kubwabwaja midomo.Ndio kusema Matakatifu Benedikto alisisitiza juu ya Sala na kazi na sio kulialia bila kupigwa.Tuchape kazi bwana.
Turudi sasa kwenye simulizi la vijana Musa, Baraka na Neema.
Yule aliyesema, ATAKUWA MWALIMU.
Huyu atapaswa kurithisha Elimu toka kizazi hata kizazi.
Huyu atahitaji awe mwema na atapasika kuwa Mfano Bora kwa watoto na jamii.
Atapaswa akwepe madeni yasiyo na tija.
Atapaswa kujiwekea uzeeni hasa kwa kutunza pensheni zake.
Atapaswa kuwakwepa walevi wa mjini na vijijini.Kwani pensheni ikiisha wao ndio watakaokuwa wakwanza kukupiga majungu na kukuona mpuuzi wa mwaka.
Atapaswa ajenge nyumba ndani ya miaka kumi ya kwanza ya kuajiliwa.
Atapaswa awekeze pesa benki ikiwa ni Maandalizi ya Kuandaa ada za watotoAtapaswa anunue mashamba walau Kama ni ekari chache ziwe kumi na tano au zaidi.Panda miti itakyokoa uzeeni. Ningekuwa Mwalimu ningefanyaje? Historia inaonesha kuwa walimu husahaulika msinite Mwanaharakati " sitaki" wengi hata walionifundisha nawaona walivyo na maisha duni.Mitazamo duni.Makazi duni.Chakula duni.Mshahara kuisha katikati ya mwezi.
Nifanyeje.Kukuruka.Fuga kuku vijana wa kazi watabaki wanawatazama kwani ukichelewa kazini ' majipu" yatashughulikiwa. Pensheni ni ya kula kidogokidogo na sio gawio la ukoo.
Wote wawili waliotaka kuwa nesi na mkulima kiufupi nesi akidhi maadili ya utabibu, mkulima naye apambane na Kilimo cha tija, kulima kwa wakati, kupanda MBEGU Bora na tena kupanda mbegu katika mvua za mwanzo kama Hayati Mwl.Julius K.Nyerere alivyowashauri watanzania.
Maisha na kazi ningesema ni sawa na kuwa na barabara nzuri zimetengenezwa kwa ajili ya magari huku hakuna magaru na watu wenyewe waamue kupita vichakani. Wajerumani walikuwana Falsafa ya kupiga kazi na sio kubwabwaja midomo.Ndio kusema Matakatifu Benedikto alisisitiza juu ya Sala na kazi na sio kulialia bila kupigwa.Tuchape kazi bwana.
Turudi sasa kwenye simulizi la vijana Musa, Baraka na Neema.
Yule aliyesema, ATAKUWA MWALIMU.
Huyu atapaswa kurithisha Elimu toka kizazi hata kizazi.
Huyu atahitaji awe mwema na atapasika kuwa Mfano Bora kwa watoto na jamii.
Atapaswa akwepe madeni yasiyo na tija.
Atapaswa kujiwekea uzeeni hasa kwa kutunza pensheni zake.
Atapaswa kuwakwepa walevi wa mjini na vijijini.Kwani pensheni ikiisha wao ndio watakaokuwa wakwanza kukupiga majungu na kukuona mpuuzi wa mwaka.
Atapaswa ajenge nyumba ndani ya miaka kumi ya kwanza ya kuajiliwa.
Atapaswa awekeze pesa benki ikiwa ni Maandalizi ya Kuandaa ada za watotoAtapaswa anunue mashamba walau Kama ni ekari chache ziwe kumi na tano au zaidi.Panda miti itakyokoa uzeeni. Ningekuwa Mwalimu ningefanyaje? Historia inaonesha kuwa walimu husahaulika msinite Mwanaharakati " sitaki" wengi hata walionifundisha nawaona walivyo na maisha duni.Mitazamo duni.Makazi duni.Chakula duni.Mshahara kuisha katikati ya mwezi.
Nifanyeje.Kukuruka.Fuga kuku vijana wa kazi watabaki wanawatazama kwani ukichelewa kazini ' majipu" yatashughulikiwa. Pensheni ni ya kula kidogokidogo na sio gawio la ukoo.
Wote wawili waliotaka kuwa nesi na mkulima kiufupi nesi akidhi maadili ya utabibu, mkulima naye apambane na Kilimo cha tija, kulima kwa wakati, kupanda MBEGU Bora na tena kupanda mbegu katika mvua za mwanzo kama Hayati Mwl.Julius K.Nyerere alivyowashauri watanzania.
TUSOME VITABU
FAIDA 100 ZA KUSOMA VITABU
Na.Fr.Simon R.LIBERIO
"Vitabu" ni wingi wa neno Kitabu litokanalo na neno la asili la lugha ya kiarabu " Al kitaab". Falsafa na tunu nyingi za kimaisha huhifadhiwa vitabuni. Elimu huhifadhiwa kitabuni.Hekima kedekede nazo twazikuta vitabuni.Mapindunzi ya kiuchumi na njia mbadala za ujasiriamali tunazikuta vitabuni.Sala mbalimbali majuzu, haditji za Mtume Muhamad (S.A.W) twazikuta Kitabuni. Mafundisho ya namna njema ya kuishi Duniani kadiri ya Gotama Budha, CONFUCIUS na Tao wachina Wanafalsafa nao wote tunawakuta vitabuni. Falsafa za Anthen Ugiriki takribani katika karne ya tano Kabla ta Kristo tunawasikia walimu Kama Socrates waliokuwa walimu wa Aristotle na Plato na kishapo Aristotle akawa Mwalimu wa Albert Mkuu. Msomi wa vitabu vya watangulizi waandishi wake huongeza maarifa kwake. Mafundisho ,Kazi za Yesu Kristo Mungu na Mwanadamu kwa pamoja zarekodiwa katika vitabu tena tuite Al wainjili ( Injili Takatifu)
Tujifunze kupitia mifano ya mabingwa katika kufanya vizuri.
Bila shaka ukimtazama Rais Barack Hussein Obama amekuwa hivyo baada ya ushawishi wa Mwanaharakati Marthin LutherJR Dr. Rais huyo Mstaafu wa Taifa kubwa lijiitalo "kidume" mbele ya mataifa yetu madogo ya wakata nyasi.Alimwiga Kaka yake Mbantu Marthin Jr. akiyetembelea viunga vya Alabama, Kansas akipaza sauti ya mnyonge mweusi aliyekuwa haruhusiwi kupiga kura katika Taifa alilozaliwa kwa bahati mbaya kwani alikuwepo huko ikiwa ni matokeo ya biashara chafu ya watumwa.
Na.Fr.Simon R.LIBERIO
"Vitabu" ni wingi wa neno Kitabu litokanalo na neno la asili la lugha ya kiarabu " Al kitaab". Falsafa na tunu nyingi za kimaisha huhifadhiwa vitabuni. Elimu huhifadhiwa kitabuni.Hekima kedekede nazo twazikuta vitabuni.Mapindunzi ya kiuchumi na njia mbadala za ujasiriamali tunazikuta vitabuni.Sala mbalimbali majuzu, haditji za Mtume Muhamad (S.A.W) twazikuta Kitabuni. Mafundisho ya namna njema ya kuishi Duniani kadiri ya Gotama Budha, CONFUCIUS na Tao wachina Wanafalsafa nao wote tunawakuta vitabuni. Falsafa za Anthen Ugiriki takribani katika karne ya tano Kabla ta Kristo tunawasikia walimu Kama Socrates waliokuwa walimu wa Aristotle na Plato na kishapo Aristotle akawa Mwalimu wa Albert Mkuu. Msomi wa vitabu vya watangulizi waandishi wake huongeza maarifa kwake. Mafundisho ,Kazi za Yesu Kristo Mungu na Mwanadamu kwa pamoja zarekodiwa katika vitabu tena tuite Al wainjili ( Injili Takatifu)
Tujifunze kupitia mifano ya mabingwa katika kufanya vizuri.
Bila shaka ukimtazama Rais Barack Hussein Obama amekuwa hivyo baada ya ushawishi wa Mwanaharakati Marthin LutherJR Dr. Rais huyo Mstaafu wa Taifa kubwa lijiitalo "kidume" mbele ya mataifa yetu madogo ya wakata nyasi.Alimwiga Kaka yake Mbantu Marthin Jr. akiyetembelea viunga vya Alabama, Kansas akipaza sauti ya mnyonge mweusi aliyekuwa haruhusiwi kupiga kura katika Taifa alilozaliwa kwa bahati mbaya kwani alikuwepo huko ikiwa ni matokeo ya biashara chafu ya watumwa.
1.VITABU HUTUPATIA HAMASA YA KUJIFUNZA MAPYA
Hauwezi kusahau Michango ya wanafalsafa kama Aneximenes, Anaximander Wala Heraclitus katika Maendeleo ya medani za Falsafa za Anthene huko Ugiriki.Ndio maana tunasema " Let us learn from the Geneous" tujifunze kwa " Manguli" waliofanya vizuri katika tasnia mbalimbali ili tujichotee ueledi maridhawa. Padre TITUS AMIGU amekuwa hivyo Nguli na bingwa mwandishi Afrika na dunia KUTOKANA na Mwl.wake Padre Mwandishi wavitabu lukuki CHRISTIAN MUHAGAMA. Kumbe penye hatua ya maendele Kuna mtu nyuma.Nami mwandishi mchanga Tanzania, Afrika na dunia nimekuwa hivi mwandishi kwa kuvutiwa sana na kazi za Vitabu vya Padre Titus Amigu. Shikamoo Mzee Titus Amigu.Salute.
Kama Saikolojia ya makuzi ya mtoto(mwanadamu) huzaliwa Ni Tabularasa, hajui chochote, kumbe hata angekua na kujifunza mengi atabaki na deni la kutaka kujua mengi tena mengi sana. Kumbe sasa, kwa kusoma Vitabu mwanadamu atajiongezea ueledi mpana, kwa Mfano mie mwana wa mkulima Mwandishi mzaliwa wa mabonde kuinama ya kijijini Mabamba Kibondo mkoani Kigoma, ili nipasue anga vijana huita " next level" za kuwa mwandishi wa Kimataifa sina budi kukomaa na kusoma Vitabu vingi vya waandishi wa Kimataifa Kama akina CHINUA ACHEBE, WOLE SOYINKA, NGUGI WA THIONGO, JULIUS KAMBARAGE NYERERE, ASKOFU MKUU FULTON JOHN SHEEN ,SHAKESPEAR, BRIAN TRANCY, ROBIN SHARMA, BENJAMIN WILLIAM MKAPA, ROBERT KIYOSAKI, OBAMA BARACK, FR.DR. GEORGE KAITHOLILI, BILL CLINTON, ERNEST BONIFACE MAKULILO, BILL GATES, SEMZABA ,PATRUCE LUMUMBA wa Kenya niwataje tu kwa ufupi.
Kumbe sasa katika mafanikio yoyote lazima uwatazame watangulizi wako wamefanyaje.Waliwwzaje "kutoboa" waliwezaje kufanikiwa mpaka wakafikia walipofikia.Kwanini wewe nawe usifikie hatua hiyo? Kama wao waliweza KWANINI nawe usiweze? Kama wao walithubutu kwanini nawe usithubutu. Kwa maneno mengine tungesema Kama wao walijaribu kwanini nawe usijaribu?
Niseme, tu kwamba tunahitaji maono mapya, mitazamo mipya, ujuzi mpya,njia mpya za kuweza kutambua Mambo na kutatua changamoto kupitia mifano ya wenzetu waliokwishapiga hatua katika maisha.
.Elimu mpya hutupatia hamasa.
.Elimu mpya hutupatia mawazo mapya
.Elimu mpya hutupatia moyo pale tulipokata tamaa.
.Elimu mpya hutupatia fursa ya kukikosoa
.Elimu mpya hukuongezea morali ya utendaji kazi.
.Elimu mpya hukubadilisha, badala yakufanya kazi kwa mazoea.Unafanya kazi kea utalaam.
.Elimu mpya hutukosoa.
.Elimu mpya hukuimarisha katika hoja.
.Elimu mpya hukutofautisha na wenzako katika kuyakabili mazingira yako.
.Elimu mpya ni jawabu ya zile ulizoziita changamoto kuwa fursa.
Hauwezi kusahau Michango ya wanafalsafa kama Aneximenes, Anaximander Wala Heraclitus katika Maendeleo ya medani za Falsafa za Anthene huko Ugiriki.Ndio maana tunasema " Let us learn from the Geneous" tujifunze kwa " Manguli" waliofanya vizuri katika tasnia mbalimbali ili tujichotee ueledi maridhawa. Padre TITUS AMIGU amekuwa hivyo Nguli na bingwa mwandishi Afrika na dunia KUTOKANA na Mwl.wake Padre Mwandishi wavitabu lukuki CHRISTIAN MUHAGAMA. Kumbe penye hatua ya maendele Kuna mtu nyuma.Nami mwandishi mchanga Tanzania, Afrika na dunia nimekuwa hivi mwandishi kwa kuvutiwa sana na kazi za Vitabu vya Padre Titus Amigu. Shikamoo Mzee Titus Amigu.Salute.
Kama Saikolojia ya makuzi ya mtoto(mwanadamu) huzaliwa Ni Tabularasa, hajui chochote, kumbe hata angekua na kujifunza mengi atabaki na deni la kutaka kujua mengi tena mengi sana. Kumbe sasa, kwa kusoma Vitabu mwanadamu atajiongezea ueledi mpana, kwa Mfano mie mwana wa mkulima Mwandishi mzaliwa wa mabonde kuinama ya kijijini Mabamba Kibondo mkoani Kigoma, ili nipasue anga vijana huita " next level" za kuwa mwandishi wa Kimataifa sina budi kukomaa na kusoma Vitabu vingi vya waandishi wa Kimataifa Kama akina CHINUA ACHEBE, WOLE SOYINKA, NGUGI WA THIONGO, JULIUS KAMBARAGE NYERERE, ASKOFU MKUU FULTON JOHN SHEEN ,SHAKESPEAR, BRIAN TRANCY, ROBIN SHARMA, BENJAMIN WILLIAM MKAPA, ROBERT KIYOSAKI, OBAMA BARACK, FR.DR. GEORGE KAITHOLILI, BILL CLINTON, ERNEST BONIFACE MAKULILO, BILL GATES, SEMZABA ,PATRUCE LUMUMBA wa Kenya niwataje tu kwa ufupi.
Kumbe sasa katika mafanikio yoyote lazima uwatazame watangulizi wako wamefanyaje.Waliwwzaje "kutoboa" waliwezaje kufanikiwa mpaka wakafikia walipofikia.Kwanini wewe nawe usifikie hatua hiyo? Kama wao waliweza KWANINI nawe usiweze? Kama wao walithubutu kwanini nawe usithubutu. Kwa maneno mengine tungesema Kama wao walijaribu kwanini nawe usijaribu?
Niseme, tu kwamba tunahitaji maono mapya, mitazamo mipya, ujuzi mpya,njia mpya za kuweza kutambua Mambo na kutatua changamoto kupitia mifano ya wenzetu waliokwishapiga hatua katika maisha.
.Elimu mpya hutupatia hamasa.
.Elimu mpya hutupatia mawazo mapya
.Elimu mpya hutupatia moyo pale tulipokata tamaa.
.Elimu mpya hutupatia fursa ya kukikosoa
.Elimu mpya hukuongezea morali ya utendaji kazi.
.Elimu mpya hukubadilisha, badala yakufanya kazi kwa mazoea.Unafanya kazi kea utalaam.
.Elimu mpya hutukosoa.
.Elimu mpya hukuimarisha katika hoja.
.Elimu mpya hukutofautisha na wenzako katika kuyakabili mazingira yako.
.Elimu mpya ni jawabu ya zile ulizoziita changamoto kuwa fursa.
2.KWA KUSOMA VITABU TUNAJIFUNZA WENGINE WALIWEZAJE AU WALIFANIKIWA KWA NJIA ZIPI NA MIBADALA MINGI WALIYOITUMIA KATIKA KUKUPAMBANA NA CHANGAMOTO KATIKA HARAKATI ZA MAFANIKIO YAO.
Ni matumaini yangu ndugu msomaji wangu,utakubaliana nami kuwa vitabu kwa sehemu kubwa vimekuwa na malengo ya kujifunza kwa wale waliofanya vizuri.Mfano mzuri ni katika Kitabu cha "RICH DAD AND POOR DADY" kilichoandikwa na Dr.Robert T.Kiyosaki, miaka ya 1997, kikitafsiriwa "BABA TAJIRI NA BABA MASKINI".Kinang'amua mitazamo miwili kinzani ya akina Baba wawili. Baba Maskini anawahimiza mwanae kuwa, "mwanangu umezaliwa katika familia Maskini,utapaswa kusoma kwa bidii sana ufaulu ili uajiliwe na upate pesa.Huo ndio msimamo wa Baba Maskini.
"Baba Tajiri" anakuja na msimamo tofauti na mitazamo mpya na wa kimapinduzi ya kifikra. Anamwambia mwanae kuwa mwanangu umezaliwa kwwnye familia tajiri,Mimi Baba yako naelekea kuzeeka, utapaswa kwenda Shuleni ukasome kwa bidii tena usome namna ya kuendesha vizuri biashara ili ukifuzu masomo urudi nyumbani uendeshe kampuni za kibiashara.Natambua ukibobobea sana katika masomo ya biashara utaendeleza vizuri Kampuni hizo bila kufilisika. Haya ndiyo tunayoyaona kwa wafanyabiashara hapa Tanzania wenye asili ya Asia akina Bakhresa, Mo,Yusufu Manji huandaa vijana wao kimasomo na hivi hata biashara zao hufanywa kisomi.Shughuli zao huendeshwa kisomi kwani vijana wao huandaliwa Kama Kijana wa " RICH DAD " alivyoandaliwa na Baba take. Ndio MAANA utajiri wao si rahisi kutoweka hapa chini ya jua. Kufilisika si rahisi. Kwani TAYARI Kuna watu waliokwishaandaliwa kiueledi katika tasnia ya biashara, masomo na matangazo.Hapa tujikubali tu, kuwa kwa kukosa mipango.
Ni matumaini yangu ndugu msomaji wangu,utakubaliana nami kuwa vitabu kwa sehemu kubwa vimekuwa na malengo ya kujifunza kwa wale waliofanya vizuri.Mfano mzuri ni katika Kitabu cha "RICH DAD AND POOR DADY" kilichoandikwa na Dr.Robert T.Kiyosaki, miaka ya 1997, kikitafsiriwa "BABA TAJIRI NA BABA MASKINI".Kinang'amua mitazamo miwili kinzani ya akina Baba wawili. Baba Maskini anawahimiza mwanae kuwa, "mwanangu umezaliwa katika familia Maskini,utapaswa kusoma kwa bidii sana ufaulu ili uajiliwe na upate pesa.Huo ndio msimamo wa Baba Maskini.
"Baba Tajiri" anakuja na msimamo tofauti na mitazamo mpya na wa kimapinduzi ya kifikra. Anamwambia mwanae kuwa mwanangu umezaliwa kwwnye familia tajiri,Mimi Baba yako naelekea kuzeeka, utapaswa kwenda Shuleni ukasome kwa bidii tena usome namna ya kuendesha vizuri biashara ili ukifuzu masomo urudi nyumbani uendeshe kampuni za kibiashara.Natambua ukibobobea sana katika masomo ya biashara utaendeleza vizuri Kampuni hizo bila kufilisika. Haya ndiyo tunayoyaona kwa wafanyabiashara hapa Tanzania wenye asili ya Asia akina Bakhresa, Mo,Yusufu Manji huandaa vijana wao kimasomo na hivi hata biashara zao hufanywa kisomi.Shughuli zao huendeshwa kisomi kwani vijana wao huandaliwa Kama Kijana wa " RICH DAD " alivyoandaliwa na Baba take. Ndio MAANA utajiri wao si rahisi kutoweka hapa chini ya jua. Kufilisika si rahisi. Kwani TAYARI Kuna watu waliokwishaandaliwa kiueledi katika tasnia ya biashara, masomo na matangazo.Hapa tujikubali tu, kuwa kwa kukosa mipango.
3.KWA KUSOMA VITABU TUNAJIFUNZA UVUMILIVU WA KUISHI NA WATU WA AJABU NA PIA TUNAJIFUNZA NAMNA WATU WANAVYOWEZA KUTUVUMILIA USUMBUFU WETU.
Kwa kusoma Vitabu utakutana na majina Kama akina Bokasa, Nduli Idd Amin Dadaa, akina Osama Bin Laden na wengi wengi. Majina hayo ni maarufu sana.Nilipokuwa shule ya msingi Mabamba, tukiwa tunakimbia mchakamchaka kwa mazoezi asubuhi ," tuliimba " Idd Amin akifa Mimi siwezi kulia , nitamtupa Kagera awe CHAKULA cha mamba" nilitamani kufahamu kwanini tusimulilie na zaidi ya yote maiti yake iliwe na mamba" .Nyimbo nyingi ziliimbwa "Amini aaah aaah ameolewa ,wapiii aaah huko Ulaya ,wivu aaah aaaah wamukereketa". Hiyo ilikuwa ni Falsafa ya kuonesha ushenzi wa Nduli Idd Amin.
NI KWANINI WATU HAO PAMOJA KWAMBA WALIKUWA WASHENZI WANAKUMBUKWA?
Kwa kusoma Vitabu utakutana na majina Kama akina Bokasa, Nduli Idd Amin Dadaa, akina Osama Bin Laden na wengi wengi. Majina hayo ni maarufu sana.Nilipokuwa shule ya msingi Mabamba, tukiwa tunakimbia mchakamchaka kwa mazoezi asubuhi ," tuliimba " Idd Amin akifa Mimi siwezi kulia , nitamtupa Kagera awe CHAKULA cha mamba" nilitamani kufahamu kwanini tusimulilie na zaidi ya yote maiti yake iliwe na mamba" .Nyimbo nyingi ziliimbwa "Amini aaah aaah ameolewa ,wapiii aaah huko Ulaya ,wivu aaah aaaah wamukereketa". Hiyo ilikuwa ni Falsafa ya kuonesha ushenzi wa Nduli Idd Amin.
NI KWANINI WATU HAO PAMOJA KWAMBA WALIKUWA WASHENZI WANAKUMBUKWA?
Ubabe duniani haulipi. Ubabe duniani hauna maana. Kwanini turinge.Maringo yanatoka wapi? Kwanini uvimbe pua? Kwanini uvimbe kwapa kwa mwenzio? Kwanini umkanyage mwenzio?
Maisha yetu hapa duniani , hatukuja kutunishiana misuli. Hapa duniani hatukuja kutafuta " u miss umwamba" wala hatupo kuusaka ubabe na umame". "Ubabe" ni hali, tabia, maneno au matendo ambayo yanatoka kama povu la hasira.Ubabe ni ukorofi wa akina Baba duniani.
Maisha yetu hapa duniani , hatukuja kutunishiana misuli. Hapa duniani hatukuja kutafuta " u miss umwamba" wala hatupo kuusaka ubabe na umame". "Ubabe" ni hali, tabia, maneno au matendo ambayo yanatoka kama povu la hasira.Ubabe ni ukorofi wa akina Baba duniani.
DEFEND YOUR FAITH AS A CATHOLIC: CHUKI NI NINI?
DEFEND YOUR FAITH AS A CATHOLIC: CHUKI NI NINI?: CHUKI NI NINI? Kadiri ya Dr.Ann Landers: “Chuki ni kama Asidi, ambayo huaribu kile kifaa ambacho imehifadhiwa na huaribu chombo ambamo ime...
Thursday, February 6, 2020
MADINI YA NDOA
MADINI KUTOKA FHWF
______________________________________________
TOFAUTI KATI YA VIVUTIO VYA NDOA NA VIGEZO VYA NDOA
Tarehe: 06/02/2020, Alhamisi.
Mtunzi: Mr. Francisco Kagoma, Founder na CEO wa FHWF, Mwanafalsafa, Mwanasaikolojia, na Mshauri wa Changamoto Mbalimbali za maisha zikiwemo na ndoa.
👉🏽👉🏽👉🏽 Washirikishe wengine nao wapate MADINI motomoto kutoka FHWF, tuma maneno "MADINI YA NDOA NA FAMILIA" kwa Ma-Admin wa FHWF: Chief Admin +255767 818 542 na Co-Admin +255 716 669 895 ili wakuunganishe na FHWF (JUKWAA). SHEA SASA HIVI⤴️↗️
Habarini za leo wanandoa waliomo katika Ndoa tayari na wanandoa watarajiwa.
Wapo tunaochanganya kati ya vivutio vya ndoa na vigezo vya ndoa kama vile vingekuwa kitu kimoja. Ni ukweli kwamba vyote vina mchango wake katika ndoa.
Utasikia maneno kama una vigezo vya kuwa MKE au mume wangu? Na mtu haulizi eti una vivutio vya kuwa MUME au mke wangu? Tayari hapo kuna maana fulani inaingia ambayo inavitofautisha "vigezo" na "vivutio."
Licha ya kwamba "vigezo" huonekana kuwa na uzito zaidi kuliko "vivutio", dunia hii ingekuwa inayokera sana kwa maana tumeumbwa kwa namna inayovutia halafu eti nje yetu kusiwepo vivutio.🤷🏼♂️🤷🏼♀️
Kifalsafa, hapa tunaongea kuhusu substance (kiini/ kigezo) (what makes something/ somebeing to be what it is, yaani _kile kinachokifanya kiwe kilivyo_) na accident (kivutio) (what adds value or falls marginally to the thing, yaani kile kinachoboresha au kinachoongeza uthamani wa kitu). Inawezekana kiini na kigezo visiwe na maana sawa mathalani maana ya ndoa - kiini cha ndoa, au vigezo vya ndoa- maana hata katika matumizi hutumika vigezo vya ndoa au vigezo vya kuoana na sio kiini cha ndoa au kiini cha kuoana. Vigezo vya ndoa hukupeleka moja kwa moja kwenye dhana ya ndoa yaani kwenye kiini cha ndoa.
Tumewahi fundisha kupitia makala mbalimbali kuhusu ndoa ni nini mfano makala ya tar. 10/02/2019 NDOA NI NINI?. Tulisema hivi ndoa ni agano kati ya mwanaume (a man) na mwanamke (a woman) kuwa wanafungamana na kuungana ili kuwa mwili MMOJA, moyo (hisia) MMOJA, akili MOJA na roho MOJA, kwa ujumla kuwa kitu kimoja katika nyanja zote na nyakati zote za maisha yao au uhai wao. Tulikwisha toa ufafanuzi wa maana hiyo katika nyakati tofauti tofauti, usitoke jukwaani tovuti (fuhuwi.com) ikikamilika utaweza rejea tena.
Leo tuone tofauti iliyopo kati ya vivutio vya ndoa na vigezo vya ndoa
1. Tofauti katika dhana au maana
Dhana ya kivutio (attractive/ exciting thing) husema kivutio ni kile kinachotakiwa kuwepo au kilichopo tayari ili kukuhamasisha kufanya kitu fulani/ kufikia jambo fulani. Na dhana ya kigezo (criterion/ requirement) husema kigezo ni kile kinachotakiwa kuwepo ili jambo fulani lifanyike au lipatikane kwa usahihi.
Hivyo vivutio vya ndoa ni yale yanayayotakiwa kuwepo au yaliyopo tayari ili kukuhamasisha kuitafuta ndoa na kuipata yaani kumtafuta na kumpata mwenzi wa ndoa, kumtafuta na kumpata mvulana au msichana fulani na kufunga naye ndoa. na vigezo vya ndoa ni yale yanayotakiwa kuwepo ili kuwezesha ndoa ipatikane, ifungwe na idumu.🌝
2. Tofauti katika ulazima na umuhimu.
Vivutio vya ndoa si lazima viwepo bali ni muhimu kwani ndio vichocheo kwa vijana kuingia ndani ya ndoa, huiongezea ndoa thamani na kuipa ndoa hii radha tofauti na nyingine. Ndoa ni moja ila inavyojidhihirisha kwa wanandoa hawa ni tofauti na kwa wanandoa wengine. Vivutio vya ndoa huifanya ndoa iwe na sura au taswira nyingi za kuitazama au kujidhihirisha kwa watu.
Vigezo vya ndoa ni ni vya lazima kwani vikifuatwa ipasavyo ndivyo vinavyowasaidia wanandoa kukifikia kiini cha ndoa kilichoelezwa kwenye maana halisi ya ndoa (unini wa ndoa) - muunganiko kimwili, kihisia (kimoyo), kiakili na kiroho.
3. Tofauti katika kutumikiana
Vivutio vya ndoa na vigezo vya ndoa vyote hutumikia ndoa, vina mchango wake katika kuhakikisha ndoa zinaanzishwa, zinakuzwa, zinakomaa, na kuzaa ndoa nyingine (kuzaa wanandoa wengine).
Lakini vivutio vya ndoa hutumika zaidi katika kuanzisha wazo la ndoa kwa vijana, na kulichochea. Huwezesha kuanza kutafakari vigezo vya ndoa, vya kuoana ni vipi. Hivyo huwezesha vigezo vya ndoa kutafutwa na hata kumpeleka kijana katika kiini cha ndoa.
👉🏽 Vivutio vya ndoa ➡️ Vigezo vya ndoa ➡️ Kiini cha ndoa
Vivutio vya ndoa hutumikia kiini cha ndoa kupitia vigezo vya ndoa LAKINI vigezo vya ndoa hutumikia kiini cha ndoa moja kwa moja.
Nahitimisha makala hii kwa kusema kuwa vigezo vya ndoa hubaki ndani ya kiini cha ndoa, kiini cha ndoa na vigezo vya ndoa ni kama pete na kidole, ila *vivutio vya ndoa* hubaki nje ya ndoa, huipamba ndoa, huipa ndoa muonekano unaovutia.
Tuvipambanue vizuri vigezo vya ndoa na vivutio vya ndoa ni vipi ili tupate kutengeneza ndoa bora.
Makala zijazo zitavipambanua vigezo hivyo na vivutio hivyo ni vipi. Baki JUKWAANI _yajayo ndani ya FHWF na FUHUWI (fuhuwi.com) yanafurahisha na kuelemisha._
© Future Husbands &Wives Forum (FHWF), 2019 - 2020
______________________________________________
TOFAUTI KATI YA VIVUTIO VYA NDOA NA VIGEZO VYA NDOA
Tarehe: 06/02/2020, Alhamisi.
Mtunzi: Mr. Francisco Kagoma, Founder na CEO wa FHWF, Mwanafalsafa, Mwanasaikolojia, na Mshauri wa Changamoto Mbalimbali za maisha zikiwemo na ndoa.
👉🏽👉🏽👉🏽 Washirikishe wengine nao wapate MADINI motomoto kutoka FHWF, tuma maneno "MADINI YA NDOA NA FAMILIA" kwa Ma-Admin wa FHWF: Chief Admin +255767 818 542 na Co-Admin +255 716 669 895 ili wakuunganishe na FHWF (JUKWAA). SHEA SASA HIVI⤴️↗️
Habarini za leo wanandoa waliomo katika Ndoa tayari na wanandoa watarajiwa.
Wapo tunaochanganya kati ya vivutio vya ndoa na vigezo vya ndoa kama vile vingekuwa kitu kimoja. Ni ukweli kwamba vyote vina mchango wake katika ndoa.
Utasikia maneno kama una vigezo vya kuwa MKE au mume wangu? Na mtu haulizi eti una vivutio vya kuwa MUME au mke wangu? Tayari hapo kuna maana fulani inaingia ambayo inavitofautisha "vigezo" na "vivutio."
Licha ya kwamba "vigezo" huonekana kuwa na uzito zaidi kuliko "vivutio", dunia hii ingekuwa inayokera sana kwa maana tumeumbwa kwa namna inayovutia halafu eti nje yetu kusiwepo vivutio.🤷🏼♂️🤷🏼♀️
Kifalsafa, hapa tunaongea kuhusu substance (kiini/ kigezo) (what makes something/ somebeing to be what it is, yaani _kile kinachokifanya kiwe kilivyo_) na accident (kivutio) (what adds value or falls marginally to the thing, yaani kile kinachoboresha au kinachoongeza uthamani wa kitu). Inawezekana kiini na kigezo visiwe na maana sawa mathalani maana ya ndoa - kiini cha ndoa, au vigezo vya ndoa- maana hata katika matumizi hutumika vigezo vya ndoa au vigezo vya kuoana na sio kiini cha ndoa au kiini cha kuoana. Vigezo vya ndoa hukupeleka moja kwa moja kwenye dhana ya ndoa yaani kwenye kiini cha ndoa.
Tumewahi fundisha kupitia makala mbalimbali kuhusu ndoa ni nini mfano makala ya tar. 10/02/2019 NDOA NI NINI?. Tulisema hivi ndoa ni agano kati ya mwanaume (a man) na mwanamke (a woman) kuwa wanafungamana na kuungana ili kuwa mwili MMOJA, moyo (hisia) MMOJA, akili MOJA na roho MOJA, kwa ujumla kuwa kitu kimoja katika nyanja zote na nyakati zote za maisha yao au uhai wao. Tulikwisha toa ufafanuzi wa maana hiyo katika nyakati tofauti tofauti, usitoke jukwaani tovuti (fuhuwi.com) ikikamilika utaweza rejea tena.
Leo tuone tofauti iliyopo kati ya vivutio vya ndoa na vigezo vya ndoa
1. Tofauti katika dhana au maana
Dhana ya kivutio (attractive/ exciting thing) husema kivutio ni kile kinachotakiwa kuwepo au kilichopo tayari ili kukuhamasisha kufanya kitu fulani/ kufikia jambo fulani. Na dhana ya kigezo (criterion/ requirement) husema kigezo ni kile kinachotakiwa kuwepo ili jambo fulani lifanyike au lipatikane kwa usahihi.
Hivyo vivutio vya ndoa ni yale yanayayotakiwa kuwepo au yaliyopo tayari ili kukuhamasisha kuitafuta ndoa na kuipata yaani kumtafuta na kumpata mwenzi wa ndoa, kumtafuta na kumpata mvulana au msichana fulani na kufunga naye ndoa. na vigezo vya ndoa ni yale yanayotakiwa kuwepo ili kuwezesha ndoa ipatikane, ifungwe na idumu.🌝
2. Tofauti katika ulazima na umuhimu.
Vivutio vya ndoa si lazima viwepo bali ni muhimu kwani ndio vichocheo kwa vijana kuingia ndani ya ndoa, huiongezea ndoa thamani na kuipa ndoa hii radha tofauti na nyingine. Ndoa ni moja ila inavyojidhihirisha kwa wanandoa hawa ni tofauti na kwa wanandoa wengine. Vivutio vya ndoa huifanya ndoa iwe na sura au taswira nyingi za kuitazama au kujidhihirisha kwa watu.
Vigezo vya ndoa ni ni vya lazima kwani vikifuatwa ipasavyo ndivyo vinavyowasaidia wanandoa kukifikia kiini cha ndoa kilichoelezwa kwenye maana halisi ya ndoa (unini wa ndoa) - muunganiko kimwili, kihisia (kimoyo), kiakili na kiroho.
3. Tofauti katika kutumikiana
Vivutio vya ndoa na vigezo vya ndoa vyote hutumikia ndoa, vina mchango wake katika kuhakikisha ndoa zinaanzishwa, zinakuzwa, zinakomaa, na kuzaa ndoa nyingine (kuzaa wanandoa wengine).
Lakini vivutio vya ndoa hutumika zaidi katika kuanzisha wazo la ndoa kwa vijana, na kulichochea. Huwezesha kuanza kutafakari vigezo vya ndoa, vya kuoana ni vipi. Hivyo huwezesha vigezo vya ndoa kutafutwa na hata kumpeleka kijana katika kiini cha ndoa.
👉🏽 Vivutio vya ndoa ➡️ Vigezo vya ndoa ➡️ Kiini cha ndoa
Vivutio vya ndoa hutumikia kiini cha ndoa kupitia vigezo vya ndoa LAKINI vigezo vya ndoa hutumikia kiini cha ndoa moja kwa moja.
Nahitimisha makala hii kwa kusema kuwa vigezo vya ndoa hubaki ndani ya kiini cha ndoa, kiini cha ndoa na vigezo vya ndoa ni kama pete na kidole, ila *vivutio vya ndoa* hubaki nje ya ndoa, huipamba ndoa, huipa ndoa muonekano unaovutia.
Tuvipambanue vizuri vigezo vya ndoa na vivutio vya ndoa ni vipi ili tupate kutengeneza ndoa bora.
Makala zijazo zitavipambanua vigezo hivyo na vivutio hivyo ni vipi. Baki JUKWAANI _yajayo ndani ya FHWF na FUHUWI (fuhuwi.com) yanafurahisha na kuelemisha._
© Future Husbands &Wives Forum (FHWF), 2019 - 2020
Wednesday, February 5, 2020
KANISA NA KUJINYONGA
Labda nikusaidie kupanua swali lako kwanza. Ungeuliza kwanini watu wanaojiua kwa kuondoa uhai wao, kanisa linakataa maziko yao kwa Misa Takatifu?
Kwanza tujue kujiua ni kufanya nini? Ni kitendo kilicho kinyeme na kutunza uhai wa Mwanadamu ambao sio mali yake na hivyo hana mamlaka nao. Ni kujiua moja kwa moja kwa makusudi kabisa kwa utashi wako mwenyewe.
Kanisa siku zote hata kesho, litabaki kinyume na mtu anayeondoa uhai wake mwenyewe kwasababu mbalimbali zikiwemo hizi hap;
1. Mwanadamu hana haki miliki ya uhai wala mwili wake mwenyewe bali amepewa kutunza mwili na uhai (stewardship).
2. Kujiua (Suicide) ni kosa la jinai dhidi ya wajibu wa Mwanadamu kwa jumuia yake na wale wanaomtegemea. Uhai wa Mwanadamu daima sio kwaajili yake mwenyewe bali kwaajili ya jamii nzima.
3. Kujiua ni kukiuka wajibu binafsi wa kujitahidi kufikia ukamilifu wa maisha yake ya kimwili na kiroho. Mtu anayeondoa uhai wake anajiondolea pia uwezekano wa maendeleo yoyote ya baadae.
Kwa maana hiyo basi, kwakuwa mtu kufikia uamuzi wa kujiua anakuwa amevurugwa kiakili (mental disturbed). Kanisa kwa kuangalia mazingira yote ya kujiua na bila kuathiri imani ya watu kwa kuleta makwazo, linapaswa kuangalia namna nzuri ya kushughulikia maziko ya Mkristo aliyejiua.
Angalisho, namna ya kuangalia mazingira na kushughulikia swala hilo kichungaji, haitakuwa na ufanano kwa matukio yote wala kwa majimbo yote au tuseme ulimwengu mzima. Tofauti zitajitokeza na ukiziona ni vyema kuchukua muda wa kujielimisha juu ya maamuzi yaliyochukuliwa na kanisa kabla ya kulaumu au kujipa wajibu wa kuhukumu.
Mungu atuhurumie.
Frt. Nzaro
Kwanza tujue kujiua ni kufanya nini? Ni kitendo kilicho kinyeme na kutunza uhai wa Mwanadamu ambao sio mali yake na hivyo hana mamlaka nao. Ni kujiua moja kwa moja kwa makusudi kabisa kwa utashi wako mwenyewe.
Kanisa siku zote hata kesho, litabaki kinyume na mtu anayeondoa uhai wake mwenyewe kwasababu mbalimbali zikiwemo hizi hap;
1. Mwanadamu hana haki miliki ya uhai wala mwili wake mwenyewe bali amepewa kutunza mwili na uhai (stewardship).
2. Kujiua (Suicide) ni kosa la jinai dhidi ya wajibu wa Mwanadamu kwa jumuia yake na wale wanaomtegemea. Uhai wa Mwanadamu daima sio kwaajili yake mwenyewe bali kwaajili ya jamii nzima.
3. Kujiua ni kukiuka wajibu binafsi wa kujitahidi kufikia ukamilifu wa maisha yake ya kimwili na kiroho. Mtu anayeondoa uhai wake anajiondolea pia uwezekano wa maendeleo yoyote ya baadae.
Kwa maana hiyo basi, kwakuwa mtu kufikia uamuzi wa kujiua anakuwa amevurugwa kiakili (mental disturbed). Kanisa kwa kuangalia mazingira yote ya kujiua na bila kuathiri imani ya watu kwa kuleta makwazo, linapaswa kuangalia namna nzuri ya kushughulikia maziko ya Mkristo aliyejiua.
Angalisho, namna ya kuangalia mazingira na kushughulikia swala hilo kichungaji, haitakuwa na ufanano kwa matukio yote wala kwa majimbo yote au tuseme ulimwengu mzima. Tofauti zitajitokeza na ukiziona ni vyema kuchukua muda wa kujielimisha juu ya maamuzi yaliyochukuliwa na kanisa kabla ya kulaumu au kujipa wajibu wa kuhukumu.
Mungu atuhurumie.
Frt. Nzaro
DEFEND YOUR FAITH AS A CATHOLIC: HURUMA NA MSAMAHA NI KUBWA ZAIDI KULIKO DHAMBI ZET...
DEFEND YOUR FAITH AS A CATHOLIC: HURUMA NA MSAMAHA NI KUBWA ZAIDI KULIKO DHAMBI ZET...: HURUMA NA MSAMAHA NI KUBWA KULIKO DHAMBI ZETU. TUMWIGE MUNGU KATIKA KUWASAMEHE WENGINE Maandiko Matakatifu yanaongea sana juu ya kutostahi...
DHAMBI MATOKEO YA AKILI NA UTASHI HURU WA MWANADAMU
SHUKRANI
Kwanza kabisa napenda kutoa shukurani
zangu za dhati kwa Mungu wetu aliye katika Utatu Mtakatifu, aliyeruhusu
yafanyike haya. Kwa maana hiyo ni kwa Neema na Upendo wake mkuu kuniwezesha,
kunitia na kunipa nguvu na maarifa hata nikafanikiwa kuanza na kukamilisha
uandishi wa hii kazi.
Aidha namshukuru sana Baba Askofu wangu
wa Jimbo Katoliki la Kigoma Mh. Joseph R. Mlola, ALCP/OSS, kwa ushauri wake
mzuri alioniambia wakati naandaa kitabu hiki.Nampongeza kwa kazi nzuri ya
kuendeleza kile walichokifanya Mitume wa Yesu yaani kulichunga kundi la kondoo
wa Bwana katika jimbo letu la Kigoma. Mungu Mwenyezi amzidishie na kumpa nguvu
na afya njema pamoja na ulinzi wake katika Utume huo alioitiwa.
Kwa namna ya pekee kabisa napenda
kumshukuru Msgr. D. H. Mbiku wa Jimbo kuu Katoliki la Dar- es salaam kwa
kukubali na kutumia muda wake kuipitia kazi hii na kuiona kuwa inafaa kwa ajili
ya wokovu wa Roho za watu walioko ndani na nje ya Kanisa, Baba nasema Ubarikiwe
sana.
Nitakuwa mchoyo wa fadhila kama
sitawashukuru Baba zangu Mapadre ambao wamekuwa pamoja nami bega kwa bega
katika kunielekeza mambo mengi ya kufanya ili kazi kuwa nadhifu. Kwa namna ya
pekee Pd. Vedastus Nyamurundwa (Jimbo Katoliki Kigoma), Pd. Titus Amigu (Jimbo
Katoliki Iringa), na Pd. Arnold Kinyashi (Jimbo Katoliki Same).
Nawashukuru wazazi wangu ambao pia
wamekuwa na mchango mkubwa kwangu katika malezi mpaka mimi kufika hapa, Mzee
Joseph Lutakangwa na Mama Anatoria Yilagera; Mwenyezi Mungu mwingi wa Huruma
awajalie maisha marefu na ya fanaka siku zote. Pia nawashukuru sana wadogo
zangu wote kwa kunitia moyo katika safari hii ya wito, Mungu mwenyezi awasaidie
katika masomo yenu na kufikia lengo la kila mmoja alilonalo katika masomo.
Shukrani za pekee kwa Frt. Innocent
Banyongere na Frt. Wilhard Kangero kwa michango yao ya Mawazo katika kuboresha
kitabu; nasema asanteni sana. Mwisho kabisa nawashukuru ndugu, jamaa, marafiki
na waamini wale wote ambao wamekuwa wakinitia moyo katika kuandaa kazi hii, zaidi
kwa majitoleo yao kiuchumi mpaka kazi kukamilika pia katika hatua hii niliyopo
kuijongea Altare ya Bwana. Nasema asanteni sana, maana wanasema moyo usiyo na
shukrani hukausha mema yote.
Tamati: KWAHIYO NAWASIHI, MIMI NILIYE
MFUNGWA KATIKA BWANA, MWENENDE KAMA INAVYOUSTAHILI WITO WENU MLIOITIWA; KWA
UNYENYEKEVU WOTE NA UPOLE, KWA UVUMILIVU, MKICHUKULIANA KATIKA UPENDO (Efe
4:1-2)
UTANGULIZI
Wapendwa sana ndugu katika Kristo napenda kuwakaribisha kwa
moyo mkunjufu kabisa katika kukipokea kitabu hiki ambacho ni tunda la
kurekebisha mienendo yetu. Ni kitabu kinachotuonyesha kwa kina zaidi namna
nzuri ya kumfasa Kristo.
Katika sura ya kwanza inatoa ufafanuzi wa kina juu ya maana
ya Dhambi. Pia katika sura ya pili inatupa ufafanuzi juu ya ahadi ya Mungu kwa
viumbe vyake alivyoviumba, japo kwa baadae vikajakumgeuka na kuvunja yale
maagano naye ya tangu mwanzo.
Katika sura ya tatu kinatueleza maisha ya sasa ya mwanadamu
namna aishivyo. Sura ya nne inaeleza juu ya mabadiliko ya sayansi na teknolojia
yanavyochangia kwa kiasi kikubwa katika kuendelea kumpotosha mwanadamu wa sasa
katika hii dunia.
Katika sura ya tano inatupa mang’amuzi mazito juu ya kushuka
kwa maadili. Sura ya sita pia inatupa somo juu ya uovu mkubwa unaoendelea
katika dunia hii ya karne ya 21, japo ni marudio ya yale yaliyowahi kutendeka
kipindi kilichopita katika agano la kale. Na katika sura ya saba ambayo ndiyo
ya mwisho, inatueleza namna mbalimbali ya kumrudia Mungu aliyemwumba wa vyote
kwa kuiga na kufata mfano wa Mungu.
Ni matumaini yangu kuwa utanufaika na
mafundisho yaliyomo katika kuendelea kuimarisha nafsi yako. Kwa namna ya pekee
naamini mara baada ya kupata ujumbe uliokusudiwa utakuwa chombo imara cha
kupiga vita dhambi, ili hata wale ambao bado wanaendelea kuishi katika giza kuu
wapate kuanza kuurudia mwanga. Na mwisho kabisa naomba baada ya kusoma kitabu
hiki ujaribu kutafari ule uovu wa tangu Sodama na Gomora pia Gharika ya Nuhu;
je! si ndiyo maisha yanayoendelea katika wakati huu wetu? Kwani unaona tofauti
yoyote?
Hapo tunaona;
“Tukisema kwamba hatuna dhambi tunajidanganya
wenyewe, wala kweli haimo ndani mwetu. Tukiziungama dhambi zetu, yeye ni
mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu
wetu.”[1]
SURA YA KWANZA
1.0 UFAFANUZI JUU YA DHAMBI
Hakuna
utata wowote juu ya uwepo wa uovu ulimwenguni. Tunaona na kusikia maovu mengi
yanatendeka duniani kwa njia nyingi. Mfano: mafarakano kati ya mataifa, magomvi
katika familia, magomvi mitaani, rushwa, ukabila, ujinsia, ubaguzi wa rangi,
mauaji, ndoa za jinsia moja, ushoga, ukahaba na mengine mengi. Namna zote hizi
za ukatili, mivurugano na utengano ambazo tunazishuhudia katika maisha ya kila
siku, zinapoangaliwa kwa jicho la kiteoliojia, yote yanachipuka kutoka katika dhambi.
Hivyo dhambi ipo ulimwenguni, na kunauwezekano wa kupinga upendo wa Mungu kwa
namna nyingi sana.
“Biblia
Takatifu inasema juu ya dhambi mara nyingi na kila mara na karibu katika kila
ukurasa” alisema X. Lean-Dufour. Dhambi pia inajadiliwa kila wakati katika
Katekisimu ya Kanisa Katoliki, kwa sababu mengi yaliyo kiini cha imani hayawezi
kueleweka bila kuielewa dhambi. Zaidi sana, ili kufuata nyayo za Kristo,
tunahitaji kuelewa vizuri madhara ya dhambi. Dhambi ina mapato mabaya sana
katika maisha ya binadamu, lakini mara nyingi ulimwengu unayafanya matendo ya
dhambi yaonekane yanavutia. Ndiyo maana watu wengi sana katika ulimwengu huu wa
sasa, wamejikita na kuwekeza katika vitu vihusianishavyo na dhambi.
1.1 Nini maana ya Dhambi?
Dhambi ni
kukataa kwa makusudi na kwa kujua zawadi ya upendo wa Mungu ya urafiki naye,
ambako kunasababisha kudhoofisha au kuvunjika kabisa kwa mahusiano kati ya mtu
na Mungu au kati ya mtu na mtu. Hivyo basi, kwa dhambi binafsi mtu anashindwa
kuitikia kwa usahihi zawadi ya mapendo ya Mungu na urafiki usiokoma wala
kubadilika maisha yote. Katika Biblia; Maandiko Matakatifu yanailezea dhambi
kama nguvu ambayo ipo katika maisha yetu. Nguvu hiyo ipo duniani ambayo ina uadui
na Mungu na mpango wake, maana tunaambiwa baada ya shetani kulaaniwa alishushwa
kuzimu ili akatujaribu kwa namna yote ile ipingayo Mungu. Kwa hiyo dhambi inajaribu
kuharibu mahusiano yetu na Mungu. Dhambi ni kinyume kabisa na upendo na
upatanisho ambao Yesu Kristo anaufunua pale msalabani. Hivyo, dhambi ni zaidi
ya kuvunja sheria kwa sababu ni uasi dhidi ya utu ule ambao tumeitiwa. Kwa
namna nyingine, dhambi, ni kuvunja miiko fulani iliyowekwa na Mungu kwa ajili
ya faida yetu wenyewe.
v Dhambi katika Agano la Kale.
Katika Agano la Kale tunaona msingi wa tabia ya dhambi, kwamba ni kuanguka kwa
wazazi wetu wa kwanza (Rej. Mwa. 3:1-24).
Pia dhambi inaonekana kuwa:
§ Ni
kuvunja sheria ya Mungu (Mwa 3: 3 – 6 )
§ Ni
dhara dhidi ya Mungu (2Sam 12:10, 15)
§ Ni (upumbavu) ujinga (Kumb 36:6, Isa. 29: 11)
§ Ni kukosa uaminifu (Isa 24:5)
§ Ni
kuabudu miungu wengine (Eze 20:7-8)
Katika
Agano la Kale, hakuna tamko bayana juu ya asili ya dhambi na jinsi
inavyorithishwa kutoka kwa wazazi wetu wa kwanza mpaka kwa jamii yote ya
binadamu. Hata hivyo habari ya kuanguka kwa binadamu katika kitabu cha Mwanzo
inaeleza hali ya binadamu ya kuwa na mazoea ya kuelekea dhambi. Pale wazazi
wetu wa kwanza walipotenda dhambi, ilikuwa ni kwa sababu walitaka kuwa sawa na
Mungu na bila Mungu (Mwa 3:5).
v Dhambi katika Agano Jipya.
Katika Agano Jipya inaonekana kama ni mgomo au kukataa upendo wa Baba (Rej. Lk 15). Mgomo huo una mizizi yake
katika moyo. Mawazo ya dhambi katika Agano la Kale yamechukuliwa na kuingizwa
katika Agano jipya na kuelezwa kwa kina.
§ Agano
Jipya linaeleza kuwa dhambi si kitu cha nadharia tu, bali ipo kweli, ni ugonjwa
ambao kweli unahitaji tiba. Ni ugonjwa ambao unahitaji mabadiliko kamili ya
maisha ya mtu. Hili linaonyeshwa bayana na mwito wa Yesu mwenyewe(Rejea Mk 1:15, 7:21-23; Mt 5:21-48)
§ Dhambi
ni kitu ambacho kipo ndani ya mtu, ambacho kwacho binadamu wote wanakuwa chini
yake (Rum 5:19). Dhambi ni hali ya
kibinadamu ambayo tiba yake ni neema za Kimungu (Rej Rum 7:13-25).
§ Dhambi
ni kama kitu cha binafsi, cha kijamii, na cha ulimwengu wote (Rej. Rum 3:9...), kwa sababu hii
binadamu wote wanakuwa daima kwenye vita.
1.2 Chanzo cha Dhambi
Dhambi
ya Asili. Mungu alimuumba mtu kwa mfano wake na sura yake na
akamfanya rafiki yake, na alipokea neema mbalimbali za kimungu.[2]
Lakini kama ilivyokuwa kwa Malaika, Adamu na Eva walijaribiwa na katika jaribio
hilo iliwapasa kutii amri ya Mungu. Hii ndiyo sababu ya amri tuliyopewa mtu
asile matunda ya Mti wa ujuzi, wa Mema na Mabaya:
Mti wa Ujuzi, wa mema na mabaya huonesha
kwa mifano mipaka ambayo mtu kwa vile ni kiumbe amewekewa asivuke. Tena
aikubali mipaka hiyo kwa hiari na aiheshimu kwa ujasiri. Sasa kwa nini Mungu
alimwacha mtu ajaribiwe? Jibu ni hili kwamba, kwa Adamu na Eva kuwa kamili
katika upendo wa Mungu, walihitaji utashi
huru; bahati mbaya sana, zawadi hii kutoka kwa Mungu ikaja kuwa upanga
wenye makali kuwili, ambao pia ungeweza kuwaelekeza kwenye uovu. Mtu
akishawishiwa na Ibilisi, aliachilia tumaini alilokuwa nalo kwa muumba wake lililoko
moyoni mwake, na kwa kutumia vibaya uhuru wake akakaidi amri ya Mungu. Hiyo
ndiyo dhambi ya kwanza ya mtu (Rej. Mwa
3:1-11; Rom 5:19). Tangu hapo, kila dhambi itakuwa ni kumkaidi Mungu na kukosa kutumainia wema wake.
Dhambi ya wazazi wetu wa kwanza ni kukosa utii. “…kwa
kuasi kwake mtu mmoja watu wengi waliingizwa katika hali ya wenye dhambi …” (Rum 5:19). Mzizi wa kukosa utii ni
kiburi au majivuno.
Ø Wazo la kwamba dhambi ya Adamu na Eva
ilikuwa ni ya kuzini ni la kupingwa kabisa kwani linapingana na ( Mwa 1: 28)
Kwa dhambi
hii mtu amejichagua mwenyewe badala ya Mungu, na kwa hiyo amemdharau Mungu. Mtu
aliumbwa katika hali ya utakatifu ili Mungu amshirikishe kikamilifu Uungu katika utukufu. Akishawishiwa na
shetani mtu huyu ametaka kuwa “kama Mungu” lakini “bila
Mungu mbele ya Mungu, na si kadiri ya Mungu.”[3]
Kwa hiyo,
itambulike kwamba dhambi ya wazazi wetu wa kwanza ilikuwa dhambi ya kukosa
utii.[4] Ni kwa
kukosa utii huko watu wote wamefanywa wadhambi. Na mzizi wa dhambi hii ulikuwa kiburi.[5] Hivyo
kiburi ni chanzo cha dhambi zote. Ndiyo maana Mt. Agustino anaelezea dhambi ya
Adamu kuwa ni kitu kiikubwa hata kisicholezeka.[6]
Ø Dhambi ya Asili imo katika
upungufu/ukosefu wa neema uliosababishwa na tendo huru la dhambi lililofanywa
na mkuu wa jamii ya binadamu (wazazi wetu wa kwanza)
Mtaguso wa Trento unatoa maana ya dhambi ya asili kama
ni kifo cha roho. Kwa namna hiyo, kifo cha roho kimo katika kukosa neema ya
utakaso, hivyo ndiyo kusema, dhambi ya asili ni ile hali ya kuwa na ukosefu wa
neema. Kwa hiyo, dhambi iliyorithiwa kutoka kwa Adamu kimsingi imo katika
kukosa neema ya utakaso. Na ukosefu wa neema ya utakaso ambayo kadiri ya
matashi ya Mungu lazima iwepo, inamaanisha kwamba hatia ya dhambi ya asili
inaonesha ni kugeukia mbali kutoka kwa Mungu yaani kumwacha Mungu.[7]
Kwa maneno mafupi kabisa tunaweza kusema kuwa, Adamu na Eva waliendeleza kwa vizazi
vyao asili ya kibinadamu iliyojeruhiwa kwa dhambi ya kwanza, ikiwa imeondolewa
utakatifu na haki ya asili. Ukosefu wa
utakatifu huu na haki ya asili huitwa “dhambi ya asili.”[8]
1.3 Uenezwaji wa Dhambi
Japo kuwa haijulikani kwa uhakika
kabisa namna gani dhambi ilikujakuwa sehemu ya hali ya maisha ya binadamu,
habari ya Adamu na Eva katika kitabu cha Mwanzo inafafanua kwamba binadamu
wanachagua wenyewe dhambi kwa uhuru kabisa na hivyo Mungu hahusiki kabisa na
dhambi ya binadamu. “Kwa maana siku utakapokula, hakika utakufa” (Rej. Mwa 2: 17).[9]
“Dhambi ya Asili inaendelezwa na asili ya kibinadamu ‘kwa kuzaliwa sio kwa kuiga,’ na hivyo ni
kwa kila mmoja”, isipokuwa Yesu na Maria. Ingawa dhambi ya asili ni ya kila
mmoja, hakuna mzaliwa wa Adamu anayeirithi dhambi hii kama kosa lake binafsi.
Watu wote wamo katika Adamu “watu wote wameshirikishwa katika dhambi ya Adamu,
kama watu wote walivyoshirikishwa katika haki ya Kristo. Hata hivyo, jinsi
dhambi ya asili inavyorithishwa ni fumbo tusiloweza kulielewa kikamilifu.”[10]
1.4 Aina za Dhambi
Kuna aina nyingi sana za dhambi. Maandiko yanatuambia “Matendo
ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu,
uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi,
ulafi, na mambo yanayofanana na hayo; katika hayo...” (Gal 5:19-21; 1Kor 6:9-10 au rej. Rum 1:28-32).
Dhambi zaweza kutofautishwa kutegemeana na kitu, kama linavyoweza kila tendo la
kibinadamu, au kutegemeana na fadhila ambazo dhambi zinapingana nazo, au kwa
kupita kiasi au upungufu, au kutegemea amri ambazo zinazivunja. Zaweza pia
kuainishwa kutegemea yule zinayemhusu: Mungu, jirani, au mtu mwenyewe.
Inawezekana kuzigawa katika dhambi za kiroho na kimwili au za mawazo, maneno,
matendo na kukosa kufanya. Kadiri ya mafundisho ya Bwana, mzizi wa dhambi umo
ndani ya moyo wa mtu, katika utashi wake huru, “Kwa maana moyoni hutoka mawazo
mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati, wizi, ushuhuda wa uwongo na matukano. Hayo
ndiyo yamtiayo mtu unajisi; lakini kula kabla hajanawa mikono hakumtii mtu
unajisi.”[11]
Moyoni pia hukaa upendo, msingi wa kazi njema na safi, ambao dhambi huujeruhi.[12]
Kuna aina mbili za dhambi ambazo hupimwa kutokana na uzito
wake. Aina hizo za dhambi ni:
o
Dhambi ya mauti
o
Dhambi
nyepesi
Tofauti kati ya dhambi ya mauti na dhambi nyepesi kama
ilivyo wazi tayari kutoka katika Maandiko Matakatifu (Rej.1Yoh 5:16-17), iliingizwa katika mapokeo ya Kanisa. Nayo yathibitishwa
na mang’amuzi ya watu.[13]
Ø Dhambi ya mauti.
Hii ni dhambi ambayo huharibu upendo katika moyo wa mtu kwa uvunjaji
mzito/mkubwa wa sheria ya Mungu, inamgeuzia mtu mbali na Mungu ambaye ndiye
kikomo chake kwa kupendelea kitu kidogo kuliko yeye. Dhambi ya mauti kwa kuwa
inashambulia ndani yetu msingi hai, yaani upendo, yataka juhudi mpya ya huruma
ya Mungu na uongofu wa moyo ambao kwa kawaida hukamilishwa kwa utaratibu wa
Sakramenti ya Upatanisho. Dhambi ya mauti kuithibitisha ni lazima jambo lake
liwe zito/kubwa, itendwe kwa ujuzi kamili (kwa akili) na kutaka/kutenda kwa makusudi
(kwa utashi).[14]
ØDhambi nyepesi.
Ni dhambi ambayo haivunji agano na Mungu, kwa neema ya Mungu inaweza
kutengenezeka kibinadamu. Dhambi nyepesi haimwondolei mkosefu neema ya utakaso,
urafiki na Mungu, mapendo, na furaha ya milele. Mmoja anatenda dhambi nyepesi
kama hashiki, katika mambo madogo, viwango vinavyoelekezwa na sheria ya
maadili, au anapokaidi sheria ya maadili katika jambo zito, bila ufahamu wote
au bila kutaka kikamilifu. Dhambi nyepesi yabakiza mapendo, ingawa inayaumiza
na kuyajeruhi. Na hivyo ni vema zikiungamwa kwani bila kuzifanyia toba kidogo
kidogo hupelekea kutenda dhambi ya mauti.[15]
1.5 Matokeo ya Dhambi
v Matokeo ya dhambi ya Asili,
yako katika maneno haya kwa ufupi: kwa
dhambi ya Adamu, binadamu alikoseshwa neema ya utakaso na asili yake
ilijeruhiwa.[16]
Dhambi hii ni katika kutokuwa na utakatifu na haki ya asili;
hata hivyo, hali ya asili ya binadamu haikuharibika kabisa: imajeruhiwa katika
nguvu zake za asili, ikitiishwa na ujinga, mateso, nguvu za kifo na maelekeo ya
dhambi. Kwani mwanadamu amepoteza Neema ya Utakaso na kufanya wote kurithi, pia
kajeruhiwa hulka yake aliyokuwa nayo toka mwanzo.[17] “Maelekeo
hayo ya dhambi huitwa tamaa mbaya”[18]
Ubatizo, unapotoa
uzima wa neema ya Kristo, hufuta dhambi ya asili na unamrudisha tena mtu kwa
Mungu. Lakini matokeo ya dhambi hiyo, hali ya asili iliyodhoofishwa na yenye
maelekeo ya uovu inabaki ndani ya mtu ikichochea mapambano ya kiroho.[19]
v Matokeo ya dhambi ya mauti.
Endapo haikuondolewa kwa toba na kwa msamaha wa Mungu, dhambi ya mauti ina
matokeo yafuatayo:[20]
ü Kupoteza mapendo na Mungu na kuondolewa
neema ya utakaso.
ü Kutengwa na ufalme wa Kristo.
ü Kifo cha milele cha motoni/ Jehanam.
ü Kunyimwa uzima wa milele.
ü Kutengana na Kanisa.
v Matokeo ya dhambi nyepesi.
Tukumbuke kuwa dhambi hizi lazima pia nazo zikaungamwa maana zinapoendelea
kutelekezwa hupelekea kuingia katika dhambi ya mauti. Ndiyo maana hata matokeo
yake hapa chini yanaonyesha bayana kwamba pia yanavunja uhusiano mzuri na
Mungu.[21]
ü Hudhoofisha upendo moyoni mwa mtu.
ü Huzuia maendeleo ya kiroho.
ü Zatuandaa kidogo kidogo kutenda dhambi
ya
mauti.
ü
Adhabu ya
muda toharani au hapa hapa duniani.
Kwahiyo, “katika macho ya Imani hakuna
baya lililo zito zaidi kuliko dhambi na hakuna kilicho na matokeo mabaya zaidi
kwa wenye dhambi wenyewe, kwa kanisa na kwa ulimwengu wote.”[22] Kwa
sababu hiyo tunapokea mwaliko huu siku zote ili uwe msaada kwa maisha yetu yote
katika Bula ya Mt. Yohane Paulo II, “Huruma ya Mungu haina mipaka, lakini
yoyote anayekataa kwa makusudi kupokea huruma yake kwa kutubu, anakataa msamaha
wa dhambi zake na wokovu unaotolewa na Roho Mtakatifu.”[23]
SURA YA PILI
2.0 AHADI ZA MUNGU
Ahadi ni neno ambalo limetumika mara
nyingi katika Biblia Takatifu. Katika Agano la kale tunamwona Baba yetu wa
Imani Abrahamu akiahidiwa juu ya uzao wake kuwa utakuwa kama nyota za Mbinguni
japo hata baada ya kupata taarifa Sara mkewe hakuamini juu ya ahadi hiyo na
kuiona haiwezekani katika uzee wao (Rej. Mwa 18:1-15). Lakini pia hata katika
Agano Jipya tunaambiwa na Kristo baada ya ufufuo wake kuwa; atapaa kwenda kwa
Baba yake ambapo anatuahidia kwenda kutuandalia makao ili atakakokuwa, nasi
tupatekuwako (Rej. Yn 14:1-4).
2.1 Nini maana ya Ahadi?
Kulingana na maelezo hapo juu, Ahadi
inaelezewa kuwa ni kiapo kinachodai utekelezaji kwa makubaliano unayokuwa
umeweka na mtu. Ndiyo maana mimi nachukulia ahadi kuendana sana na kiapo, japo
siyo kiapo kinachowekwa mahakamani laa hasha! bali kinachoweza kushuhudiwa
baina ya wahusika; mfano mtu anamwahidi mwenzake kitu fulani wakiwa katika
mazingira ya wao wenyewe, hapo Mungu anakuwa shahidi. Pia watu wengi kama
mashahidi pale mtu anapoahidi kitu katika sherehe kuwa atakitekeleza hapo
mashahidi ni watu wote waliokusanyika hapo, nae Mungu anakuwa katikati yao.
Hivyo, Ahadi ni kiapo kutoka kwa Mungu wanachoweka watu wengine kwa jina la
Mungu au kwa kusanyiko la watu kama mashahidi zikidai heshima, uaminifu, ukweli
na mamlaka ya kimungu. Ahadi hizi zinapaswa kuheshimiwa kwa haki. Mungu alikuwa
mwaminifu katika ahadi zake tangu kale ambapo kila alichokiahidi kwa watu wake
kilitekelezwa kikamilifu.[24] Nasi
kupitia Mungu alivyotenda, methali isemayo Ahadi ni deni itukumbushe kuwa
tunakila wajibu wa kutekeleza kile tunachokuwa tumeahidi.
Katika ahadi tunaaswa kutumia vizuri
viapo hivyo, tukirejea amri ya pili ya Mungu inayotukataza viapo vya uwongo.
Kutoa kiapo au kuapa ni kumchukua Mungu shahidi wa kile ambacho mtu
anakithibitisha. Ni kuutia ukweli wa kimungu kama amana ya ukweli wake mtu.
Kiapo kinapokuwa kweli na halali huweka wazi uhusiano uliopo kati ya maneno ya
mtu na kweli ya Mungu aliye ahadi yenyewe.[25] Kwa
maana hiyo tunamfanya Mungu awe shahidi na hivyo tunaposhindwa kutekeleza basi
tunathibitisha na kumfanya Mungu awe shahidi wa uwongo.
2.2 Ahadi ya Mungu kwa Watu wake.
Ahadi ya Mungu kwetu sisi; alituahidia
uzima wa milele. Ndiyo maana tangu uumbaji wa vitu vyote alisema kuwa “...akaona
kila kitu alichokifanya na tazama ni chema sana...” (Mwa 1:31). Lakini
pia Mwenyezi Mungu hakuishia hapo kwetu wanadamu akatuumba kwa namna ya ajabu
na ya kipekee sana “...Na tufanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu... (Mwa 1:26).” Mungu
akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wake Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke
aliwaumba” (Mwa 1:27).
Wema huu alioufanya na kuuweka kwetu
ilikuwa ni ishara ya kutuonyesha upendo wake mkuu ya kwamba hakutaka
alichokiumba kipotee bali kiwe na urahisi wa kufikia uzima wa milele.
Tunaposoma katekisimu ndogo ya kanisa katoliki katika swali la kwanza linauliza
juu ya lengo la kuumbwa kwetu.[26] Hivyo
lengo lake mahususi kwetu ni kuishi maisha ya kumpendeza tungali hapa duniani,
nasi tukapate kufikia ile ahadi tuliyoahidiwa na Kristo mwenyewe baada ya
ufufuko wake na kupaa mbinguni. Pia anatuonyesha katika hili anaposema “Bwana
ataniokoa na kila neno baya, na kunihifadhi hata nifikie ufalme wake wa
mbinguni. Utukufu una yeye milele na milele. Amina”.[27]
Kwahiyo kila mtu atambue kuwa mara baada ya kumaliza hija ya hapa duniani
tumeahidiwa kupokea ile tunu ambayo ilitekelezwa na Kristo mwenyewe aliposema
kuwa anakwenda kwa Baba kutuandalia makao, ili alipo yeye nasi tukapatekuwako
huko.[28] Kupaa
Yesu mbinguni daima tunaidhamisha ile Dominika ya 6 baada ya Ufufuko wake katika
kila mwaka wa Kanisa. Na hapo ndipo anaenda kutekeleza ahadi ile ya kwenda
kutuandalia makao mbinguni, ili nasi tupatefika huko.
2.3 Utofauti wa Mwanadamu na Viumbe wengine
Katika uumbaji Mwenyezi Mungu naweza
kusema alimpendelea sana Mwanadamu, na hii yote ilifanyika hivyo kwa lengo
maalumu. Yeye aliye kila kitu alimtambua mwanadamu kama kiumbe ambacho kilikuwa
dhaifu na hivyo kwa namna yoyote alipaswa aone namna ya kuja kukikomboa baadae.
Swali la kujiuliza mwenyewe kichwani, unadhani uko sawa na wanyama au viumbe
wengine walioumbwa na Mungu? Una ufanano
nao? Namna ya kuona vitu unadhani uko sawa nao? Unapo mtazama mnyama unamwona
kama wewe ulivyo? Katika kutafakari kwangu nimebaini vitu vifuatavyo ambavyo
naona tumetofautiana navyo mbali sana.
Mwanadamu kiumbe wa Pekee, Upekee wake hautokani na kuwa na roho laa hasha
ila ni kutokana na ukweli kuwa ameumbwa kwa sura na mfano wa Mungu tena ametoka
moja kwa moja udongoni na siyo kutoka wanyama wengine.[29] Hapa
kuna haja ya kuishi kindugu kwa sababu Mungu katufanya damu moja na yote
yaliyomo katika historia yanalenga umoja wa binadamu.
2.3.1 Akili na Utashi.
Katika uumbaji Mungu alimpatia
Mwanadamu akili ya kuweza kufikiri na kuelewa mambo katika upana wake na hivyo
aweze kutenda kulingana na ile kweli yake. Katika akili ya mwanadamu ndiko
kuliko uwanja mkubwa wa mapambano kati ya nafsi na ushawishi au majaribu kutoka
nje. Kama nafsi ikijeruhiwa huwa na udhaifu katika kupambana na majaribu.
Kutokana na udhaifu huo vishawishi au majaribu huweza kuishinda nafsi kwa
urahisi na hatimaye dhambi huingia. Nafsi iliyoshindwa na dhambi huwa mtumwa wa
dhambi. Utu wa ndani uliotawaliwa na dhambi, roho yake hushindwa kuunganisha
maudhui mema au baraka za Mungu kutoka kwa Roho wa Mungu.
Pia katujalia utashi ili tuweze
kupambanua mambo na kuona lipi jema na lipi baya. Utashi ni uwezo wa kipekee,
Mungu alimwumbia mwanadamu wa kuwa na hiyari au ridhaa ya kuamua bila
kushinikizwa. Kwa mfano; ingawa nyoka alimshawishi Eva ale tunda la mti wa
katikati ya bustani ya Edeni, alikini nyoka hakumlazimisha au kumsisitiza kula
tunda, ila yeye mwenyewe kwa hiyari yake alinyoosha mkono na kuchuma tunda na
kulila. Ni dhahili kwamba hamna kiumbe kingine kilichojaliwa Akili na Utashi zaidi
ya mwanadamu. “Bwana Mungu akasema, Basi, huyu mtu amekuwa kama mmoja wetu, kwa
kujua mema na mabaya; na sasa asije akanyosha mkono wake akatwaa matunda ya mti
wa uzima, akala, akaishi milele.”[30]
Viumbe wengine wamejaliwa Silika(instinct) yaani ukimwona mfano mbuzi amekula majani ikafika jioni
lazima awe na kiu na hivyo kitakachofanyika lazima atafute maji anywe; sasa
unapomkuta anakunywa huwezi kusema huyu mbuzi ana akili kweli kisa anakunywa
maji. “Lakini hao kama wanyama wasio na akili... (2Pet 2:14)” inaonyesha
kweli viumbe au wanyama wengine hawana akili tangu kuumbwa kwao.
Ni kwa hali hiyo hiyo ambapo tunaona
pia mfano pengine mtu ameanika nafaka nje ya nyumba na kukawa na mbuzi
mazingira yale, ili kuona kuwa hana akili anaweza kuja pale kutaka kula ila
ukamfukuza kwa kumrushia jiwe na akaumia ila akikimbia kidogo utamwona anaanza kugeuka
nyuma na kurudi tena. Kumbe angelikuwa na akili angalijiongeza hata kwa kutumia
msema usemao akufukuzaye hakwambii toka; japo kwa kumrushia mpaka jiwe yeye
haoni kana kwamba humtaki. Ukisema ana akili utakuwa unakosea, kumbe anafanya
hivyo kwa kuwa ndiyo silika yake au kwa lugha nyinginr ndiyo asili yake.
Mwanadamu tunamtazamia atende vitu kwa kutumia akili na utashi. Muda mwingine
anaweza akajisahau kama kiumbe aliyedhaifu lakini hatumtazamii afanye vitu
vibaya ambavyo vinakinzana na mpango wa Mungu.
Mwanafalsafa mmoja (Jeremy Bentham, 15
Februari 1748 – 6 Juni 1832) aliwahi kusema kuwa kila kitu mtu afanyacho
anapaswa kufanya kile tu kimleteacho furaha, na vile visivyomletea furaha
anajiepusha navyo. Sasa swali kulingana na mtazamo huo kwamba kwa mtu kila
afanyacho anakifanya akitaka kupata furaha, na yaliyomengi yampatiayo mtu
furaha ni mambo zaidi ya kidunia. Je! kuna mambo mtu anafanya ila hayana maana
kabisa kama kuua au kufanya matendo mengine ya kinyama kama ukatili, huyo nae
tunasemaje? Nae kwa matendo hayo anapata kweli furaha? Au anatofauti gani na
mnyama sasa tena mkali kama simba au chui? Swali hili likupe changamoto ya
kufikiri zaidi kwamba wale watu watendao kabisa matendo yaendanayo na wanyama
tena wanyama wa mwituni tunawaweka katika sehemu gani, je! Nao pia ni wanyama
au wako upande gani? Mzaburi katika zaburi ya 14 anasema, “Bwana akasema, je! Wote wafanyao
maovu hawana akili?[31]
ni swali aliuliza. Sasa mimi na wewe tungelijibu vipi? Jibu rahisi ni kwamba:
fanya mazuri na epuka mabaya (Do good and avoid evil), au fanya kile ambacho
nawe wapenda ufanyiwe na wengine. Kwa kufata hiyo kanuni ya maisha utajiepusha
na ugonjwa wa kanza ya kujipenda mpaka kujipendelea.
2.3.2 Mwanadamu amefanywa kidogo tu kuliko Mungu.
Kama nilivyotangulia kusema hapo juu,
Mwanadamu kwa upande mwingine ndiye aliyependelewa kwa namna ya ajabu kabisa
kuliko viumbe wote.[32] Lakina
pia katika maisha ya kawaida kuna msemo usemao kila kizuri hakikosi kuwa na
dosari au siyo kila king’aacho ni dhahabu. Licha ya yote mwanadamu aliyotendewa
na Mungu bado anakuja kuonekana kuwa ni msumbufu kupita viumbe wengine wote na
kumfanya Mungu aanze kujilaumu kwa kumwumba kwake na matarajio yake kwake
kupitia matendo, “Bwana akaghairi kwa kuwa amemfanya mwanadamu duniani, akahuzunika
moyo.”[33]
Kupitia Huruma na Upendo wake bado
anaendelea kumthamini kama kiumbe wake, hakuweza kusema basi amshushe kutoka
hadhi hiyo aliyokuwa nayo bali akamwacha na kuendelea kubuni mbinu zaidi za
kutaka kumwokoa. Hivyo mpaka sasa Mwandamu huyu ndiye anaeendelea kutangaza
utukufu wa Mungu kupitia mamlaka na hadhi aliyopewa tangu kuumbwa kwake licha
ya kuwa msumbufu sana. “Umemfanya mdogo punde kuliko Mungu...” (Rej.
Zab 8:4-8).
2.3.3 Kiumbe wa mwisho katika kuumbwa.
Katika uumbaji tunaambiwa kupitia
masimulizi makuu mawili. Simulizi la kwanza linapatikana ukisoma Mwa
1: 1-2:4a ambapo limetajwa kuonekana katika hali ya kitaalamu zaidi
kuliko simulizi la pili, tunaambiwa namna Mungu alivyoanza kuumba Ulimwengu.
Mbingu na Nchi tena Nchi tunaambiwa ilikuwa ukiwa na utupu; akianzia na siku ya
kwanza akaamuru iwe nuru nayo ikawa mpaka siku ya sita, siku ya mwisho katika
uumbaji anapomwumba mtu na siku ya saba tukaambiwa akastarehe. Simulizi la pili
juu ya uumbaji linapatikana kuanzia Mwa 2: 4b-25 ambapo tunaelezwa kuwa
limetaja taratibu sana namna ya zote za viumbe vilivyoumbwa na Mungu. Viumbe
vyote vyatajwa kana kwamba vingaliumbwa kwa juma moja tu. Siku ya mwisho wa
juma, ndiyo siku ya saba, Mungu alistarehe.
Hivyo kutokana na masimulizi hayo
mawili Mungu ametuonyesha kuwa sisi kwake tu watu wenye thamani kubwa sana
kuliko viumbe wengine wote. Ndiyo kusema kwamba hakutaka tuhangaike mara baada
ya kuumbwa kwetu bali tukute mambo yameshakaa safi (poa au mwake kwa lugha ya
kisasa). “………ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya sita” (Mwa 1: 26-31).
2.3.4 Kutawala vyote
Ni katika hali hiyo hiyo, Mungu aliweza
kumwumba siku ya mwisho ili kile alichokuwa ameshakiumba kikapate kumfaa
Mwanadamu. Hapo ndipo tunaona bado ule upendo wa Mungu kwa mwanadamu na ile
namna ya hali na mategemeo makubwa sana kwa Mungu kupitia kwa mwanadamu. Ndiyo
kusema kwamba namna ambayo alikuwa ameshanuia kuitekeleza wakati utimiapo
ilikuwa katika mpangilio mzuri na safi, hivyo Mungu hakutenda na wala hatendi
vitu kwa bahati mbaya bali kwake kila kitu kinamakusudi na umaana wake.
Katika Agano la kale tunaambiwa “Mungu
akawabariki, Mungu akawaambia ….mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa
angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi” (Mwa 1: 28). Pia “umemtawaza juu ya kazi za mikono yako;
umemvika vitu vyote chini ya miguu yake. Kondoo, na ng’ombe wote pia; naam, na
wanyama wa kondeni; ndege wa angani, na samaki wa baharini; na kila kipitiacho
njia za baharini” (Zab 8: 6-8).
Mwanadamu huyu ndiye aliyepewa mamlaka
hiyo ya kutawala viumbe vyote maana kwa neno lake Mungu viliwekwa chini ya
miguu ya mwanadamu. “Ee Mungu wa baba zetu, Bwana mwenye
kuihifadhi rehema yako, umevifanya vitu vyote kwa neno lako; na kwa Hekima yako
ukamwumba mwanadamu, ili avitawale viumbe vilivyoumbwa nawe, na kumiliki
ulimwengu katika utakatifu na kwa haki, na kutoa hukumu kwa unyofu wa moyo.”[34] Namna
nzuri inayomwezesha kuvitawala vizuri: ni kupitia vile vitu ambayo viumbe wengine
walikosa nikimaanisha kwamba tunapaswa kuvitawala kwa kutumia Akili na Utashi
tulivyojaliwa; kama zawadi ya pekee tuliyopewa. Na hivyo mwanadamu ndiye
aliyewekwa kuwa mfalme wa kutawala viumbe wengine wote ulimwenguni.
2.3.5 Mwenye sura na mfano wa Mungu
Mungu akasema, “Na tufanye mtu kwa
mfano wetu kwa sura yetu;...[35]
Tunaambiwa ya kuwa naye ameviumba kwa
taratibu ya ubora wao. Ameanzia viumbe hafifu hata mwisho akamwumba mtu mwenye sura na mfano wa Mungu, akamweka kuwa
mfalme wa ulimwengu wote.
Ni kwa mantiki hiyo, tunawiwa siku zote
kutendeana vizuri. Kwani sisi wote tu watoto wa Baba mmoja, tena tulioumbwa kwa
sura na mfano wake. Kwa kulitambua hilo kila mtu hapa duniani ni wathamani sana
mbele zake Mungu aliyetuumba. Na hivyo hatuna sababu yoyote itupasayo kuanza
kudharauliana. Hatuna sababu yoyote ya kuwa na majivuno na kujiona pengine
wengine ni bora zaidi kuliko wengine.
SURA YA TATU
3.0 MAISHA YA SASA YA MWANADAMU
Mara nyingi nimekuwa nikijiuliza sana
swali hili; kwamba hivi ndugu, jamaa na marafiki waliotutangulia mbele ya haki
mfano wakafufuka nini watakacho tueleza wanadamu wa sasa? Au watashindwa hata
kutueleza chochote kufuatana na mabadiliko yaliyoko sasa na kuona kwamba kila
kitu kwao ni kigeni kabisa? Mara nyingi kama una desturi ya kuongea na wazee wa
zamani ambao bado tuko nao, kuna vitu mpaka sasa haswa hawavielewi na hawajui
kwa hakika ulimwengu huu wa leo unaelekea wapi; maana kila wakivuta taswira ya
wakati wa ujana wao na sasa maisha yaendavyo wanaonyesha bayana kuwa hii siyo
dunia ile ya zamani waliyoishi katika ujana wao.
3.1 Kuongezeka kwa uovu
Uovu ni kutenda kinyume na mpango wa
Mungu yeye aliyemwema siku zote. Na hivyo kuongezeka kwa uovu inatupa jibu la
moja kwa moja kuwa siku hizi wanadamu hawamchi Mungu wala kumwamini na kutenda
kadiri ya mapenzi yake.Ukizingatia kinachochochea zaidi ni kwamba watu
wamepozea hofu ya Mungu (No sense of sin), na hapo tumeshajijengea utamaduni wa
kutokuwa na aibu; yaani hatuna mshipa wa aibu tena.Mwanadamu na dhambi ni
mamoja.Na zifuatazo ndizo nguzo ambazo Mahatma Gandhi alizotoa:-
· Kwanza ni Siasa bila maadili. Madhara yake ni makubwa kweli kweli, ndipo hapo
tunaanza kukutana na maneno magumu sana hata kutamkika kama vile Rushwa. Hayo
yote yanapata upenyo kwa kushindwa kuwa na maandalizi mazuri, na kufanya siasa
ionekene ni kitu cha kujiingiza ili unufaike kirahisi; yaani pasipo kutokwa
jasho. Pia kwa kukosa uadilifu tunakutana na wanasiasa amabao wanaishia kuwa
waongo kweli kweli katika ahadi zao. Kwa kushindwa kutambua umaana wa siasa
watu wengine wanajiingiza huko kwa sababu wanajua kuongea sana, hivyo muda
mwingi wnajikuta wakishindwa kutawala ulimi wao: ndiyo kusema kwamba wanatafuta
uongozi kwa nguvu hata kwa kuahidi uongo au kutoa ahadi ya viyu ambavyo anajua
hatoweza kuvitekeleza. Tuwe waadilifu na wa kweli daima (Let’s be realistic). Ni
kwa namna hiyo hiyo hatuna sababu ya kutoa visingizio katika uongozi bali
kuwajibika kila mmoja kwa nafasi yake. Hatutaki tena kuwa na watu wasiojua
siasa wala hawawezi kuwa viongozi, maana John C. Maxwell anatupatia sifa za
kiongozi; ‘Kiongozi ni yule anayeifahamu njia, anapita na kuwaonyesha wengine.’[36] Hivyo
kwa kuwa na kiongozi asiyejua maadili yake, atatufanya nasi kuenenda vivyo
hivyo kwa kuwa ni kiongozi; maana wanasema kipofu hawezi kumwongoza kipofu
mwenzake, akimwongoza maana yake wote wanaenda kutumbukia shimoni.
· Pili, Ndoa bila mapendo. Tafsiri ya haraka haraka ya ndoa ni upendo. Ndoa
inayokosa upendo inaenda kuwa ndoano. Utakuta wengine licha ya ukristo wao
wanakimbilia talaka au kujiingiza katika ndoa za mitala. Mahatma Gandhi aliwahi
kusema, “Palipo na upendo pana maisha.”[37] Tulioko
katika ndoa tujitahdi kupendana hata ikitupasa kujitahidi kuulinda upendo huo
kwa gharama yoyote, maana ndoa ni chimbuko na kitalu cha miito yote. Hatuwezi
kupata watu wakuwekwa wakfu kama familia zetu hazina upendo, maana Mungu ndiye
Upendo halisi;[38]
hivyo hata kupata wahudumu wa kiroho kunaambatana na baraka na neema kutoka kwa
Mungu.
Tunapozungumzia
ndoa ni kitu cha kipekee kabisa kwani kinahitaji umakini wa hali ya juu kabla
ya kuamua. Kwa kuwa mhimili wake mkuu umejengwa na upendo, hivyo watambue
kupenda ni kuchagua na kuchagua ni kuamua. Kwa mantiki hiyo, maji ukiyavulia
sharti uyaoge. Sasa inashangaza kweli kweli ya kwamba, tumekuwa tukiona baadhi
ya wanandoa wakiishi kama vile Mwalimu na mwanafunzi wake au mtumwa na Bwana
wake; mara nyingine wakithubutu hata mmoja wao akimwita mwenzake mbwa, huna
kitu, mlala hoi, mpumbavu, nilikuoa bahati mbaya tu na mengine mengi kama hayo.
Lakini jiulize kwanini useme hata ulioa bahati mbaya tu? Je, hukufanya
maandalizi yoyote kabla ya kuamua hivyo? Sasa kama hukuweza kumshirikisha Mungu
katika kuamua kwako ulitegemea au unategemea nini? (What do you expect?) Sasa wewe ndugu yangu unayeanza kujipanga kwa
maisha ya ndoa, tafadhali mkumbuke na umshirikishe Bwana Mungu wako naye
atakujazi na kukusaidia katika kufanya uchaguzi na uamuzi mzuri. Kwa hakika
hakuna lisilowezekana mbele yake Mungu, kama kweli tukimwendea kwa Imani. Tukimwomba
kwa Imani kwa hakika yeye atatupatia chaguo halisi; litupasalo na kutufaa kwa
maisha yote mpaka hapo mwisho wa maisha yetu yaani kifo.
Sala hii itufae wote tunaohangaika na
kujua ni yupi kweli nimeumbiwa kuwa mwenza katika ndoa, kama kweli tukiwa na imani
na kuisali mara zote.SALA/OMBI LA KUPATA
MCHUMBA MWEMA.
Ee
Mwumbaji wetu, umewaunganisha watu katika ndoa takatifu. Nami natamani kupokea
sakramenti hiyo na kuambatana na mwenzangu wa ndoa maisha yangu yote. Kwa hiyo,
nakuomba ee Bwana, unisaidie kuchagua kwa hekima, nipate mchumba mwema, safi,
mwaminifu, nifuate Zaidi uzuri wa roho kuliko wa uso, Zaidi tabia njema kuliko
utajiri na umaridadi. Mioyo yetu iwe ya kulingana, nia zetu zipatane, tupate
kukaa pamoja kwa amani na kulea familia kwa kukuheshimu wewe na kupata Baraka
yako. Amina.[39]
Hivyo, ili ndoa izidi kusitawi
inahitaji kutawaliwa na uvumilivu unaoambatana na msamaha pasipo kuchoka;
Bryant H. McGill alisema “Hakuna upendo bila msamaha, na hakuna msamaha bila
upendo.”[40]Kumbe
kupitia ile maana ya ndoa niliyodokeza hapo juu inakuja kuthihirishwa kwa
maneno hayo, hivyo ndoa iliyojaa upendo na msamaha itadumu zaidi; maana
kitakachoifanya iwe ndoano kwa kuwa imeshikana kwa pendo ambalo haliwezi
kugawanyika kamwe.
· Tatu, Dini bila hofu. Kuna mtu anajiita ni mkristo ila kiuhalisia anakuwa
mkristo jina (In nomine persona). Hii ndiyo imetawala sana kwa sasa, unamamwona
mtu kanisani unadhani kuwa ni mwamini kweli, kumbe anatumia kigezo hicho
kufichia maovu yake. Anafanya hivyo ili kufumba mambo mengine, maana wahenga
walisema akumlikaye mchana usiku hukuchoma. Hivyo afanyacho ni kujaribu kuficha
na kutoanika hadhalani mambo yake. Kwa mfano, mtu anajua ametenda dhambi
fulani, lakini hataki kukimbilia sakramenti ya kitubio na mbaya zaidi kila adhimisho
lazima ampokee Kristo. Sasa mafundisho yanasema, ampokeaye Kristo pasipo
kujiandaa hupokea hukumu yake. Tujiepushe kufanya vitu kwa mazoea tafadhali, na
mbaya zaidi tukivifanya kwa kulalia mgongo wa kanisa au Dini.
Waraka wa Yakobo unatueleza kuwa Mtu
ajaribiwapo, asiseme, “Ninajaribiwa na Mungu”; maana Mungu hawezi kujaribiwa na
maovu, wala yeye mwenyewe hamjaribu mtu. Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa
yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa… (Yak 1:13-15). Kumbe maovu
yetu yanasababishwa zaidi na tamaa ambayo tamaa hupelekea mashina mabaya saba
yaliyo asili ya dhambi nyingi (Mizizi ya dhambi), kwa maana ni kama
mizizi inayochipukiza dhambi nyingine Zaidi.[41]
v Majivuno,
ni hali ya mtu kujisikia kuwa yeye
ndiye bora. Mwenye majivuno ataka kuvuna sifa kwa ajili ya nafsi yake. Mifano:
Malaika wabaya; walijivuna kwasababu ya akili na uzuri wao, mpaka wakamwasi
Mungu. Mtu tajiri kwasababu ya mali yake, anamnyima Lazaro chakula. Kwa hiyo
ndugu yangu kama nawe ni miongoni wa wenye majivuno tambua ya kuwa unakilema
cha Unyenyekevu yaani hutaki kujishusha zaidi unataka kukaa juu tu. Pia
tukumbuke kuwa ni katika hali hiyo ya majivuno (kujiona watu wa maana sana
kuliko wengine) inatupelekea katika kuotesha kiburi, ambavyo vyote havipendezi
machoni kwa Mungu aliye peke yake Mtakatifu.[42]
v Choyo,
ni hali ya kuwa na mkono wa birika;
yaani yeye hajui kutoa bali kupokea tu. Hivyo mwenye choyo hupenda mno fedha na
mali, pia anakuwa na moyo mdogo sana msimopatikana nafasi kwa wenzake. Mifano:
Yuda alikuwa na choyo ambapo kutoka kwake tunaona wizi, upungufu wa Imani,
uhai, ukosefu wa matumaini na mwisho kujiua mwenyewe. Pia Tajiri kushiba
mwenyewe na kumnyima Lazaro. Mimi na wewe mifano hii ituimarishe na kutujenga
upya, pia tukitambua kuwa mtu mwenye choyo amekosa Ukarimu. Pengine mambo
mengine yanapita mbali nasi bila kuyajua maana yake, kuna msemo usemao Kadiri
utoavyo ndivyo upokeavyo Zaidi.
v Uchafu,
ni hali ya kutokuwa nadhifu kiroho;
yaani kuwa katika dhambi. Mara nyingi uchafu huu unahusianishwa na mambo
yatokanayo na tamaa za kimwili ambayo ni makatazo kutoka kwa Mungu. Mfano: Watu
wa gharika kuu, kwasababu ya uchafu wao iliwapelekea katika uuaji. Mimi na wewe
tujichunguze vema na kuona ni mara ngapi tumeiheshimu na kuipa hadhi miili
yetu; ambayo kwayo tunaambiwa kuwa ni Hekalu la Roho Mtakatifu? Jibu najua unalo, hii siyo tu kwa vijana tu
ambao hawajaoa; nawe uliye katika ndoa ni mara ngapi umeitendea haki ndoa yako
kwa kuwa mwaminifu kupitia viapo ulivyoweka mchana kweupe mbele ya kadamunasi
Kanisani? Kama majibu yako yanaonyesha kuwa bado u mchafu, tambua ya kuwa
umepungukiwa au umekosa Usafi wa Moyo.
v Wivu,
ni kitendo cha kuwa na kinyongo na mtu
kwa kuwa tu amekuzidi kitu fulani. Tunaambiwa ya kuwa mtu mwenye wivu huwaonea
wenzake kwa sababu ya heri na mali yao. Ni katika wivu maendeleo ya kimwili pia
kiroho yanakawia na kudorora hususani kwa watu waishio vijiji wakijisadikisha
na ushirikina. Mifano: Kain alimwua nduguye Abel kisa wivu. Pia vijijini watu
wanashindwa kujenga nyumba nzuri wakihofia kurogwa au kwenda kumwabudu Mungu wa
kweli, kwa vitisho vya wazee wa mila ya kuwa mizimu itamlaani na kumwua. Sasa
je! Mimi na wewe ni wapi tunajikuta na wivu usio na maana? Tukitambua kwamba
mtu mwenye wivu anakosa upendo kwa wenzake. Hivyo, kama unakosa upendo kwa
wenzako ujue unakilema cha wivu yaana kwa maana nyingine hutaki maendeleo ya
watu wengine.
v Ulevi
na Ulafi, ni kitendo cha
kutumia aidha chakula au kunywa kupitiliza. Tukiongozwa na msemo usemao kila
chochote kilichopitiliza ni hatari; Kwa mantiki hiyo Mlevi hunywa sana, Pia
mlafi hula sana. Katika maisha yako je! Umeweza kutumia kila kitu kadiri
ipasavyo? Hivyo kama umeshindwa kujisimamia katika maisha yako mwenyewe ujue ya
kuwa unakosa fadhila ya Kiasi. Maana kitu kinaonekana na kuleta madhara baada
ya kupitiliza katika ule uhalisia wa kawaida.
v Hasira,
ni kitendo cha kuwa na hulika. Mtu
mwenye hasira hukasirika upesi tena bure (vitu visivyomaana). Japo katika
hasira tunaambiwa kuwa kuna hasira ya haki, pale unapomkaripia mtu kwa kumkuta
au kumwona akifanya vibaya. Mfano; Musa alipowaona waisraeli wakiabudu sanamu
alikasirika. Likini hasira nyingine ni hiyo ya bure ambayo haina maana yoyote,
mfano: Kain alikasirika sana baada ya kuona sadaka ya Abeli imepokelewa ila
yake ikakataliwa. Najua kama binadamu tumeumbwa kila mmoja na hulika yake,
hivyo kila mmoja anajijua hasira yake ni ya aje. Kama hasira yako inakutuma
katika vitu ambavyo si vya maana jua ya kuwa umekosa Upole. Kwa hiyo, mfano wa
kondoo afahamikaye kama mpole tujifunze kutoka kwake, hata kama tunapokutana na
maudhi makubwa basi tukubali kujishusha hapo tutakuwa kama kondoo. Ndiyo maana
wanashauri kuwa hata siku moja usije ukatoa maamuzi ukiwa katika hasira au
ufanye na kuamua kitu ukiwa katika hali ya hasira lolote linawezakutokea, maana
wanasema ‘hasira hasara’.
v Uvivu,
ni kitendo cha kushindwa kufanya kazi
zilizo ndani ya uwezo wako kwa sababu zisizo na maana (uzembe). Tukirejea
maisha ya wamonaki wao walianzia Ora et
labora (kazi na sala), hivyo kufuatana mwito huo wa kufanya kazi kila mmoja
aone kuwa ni wajibu wake na haki. “Kwa kuwa hata wakati ule tulipokuwapo kwenu
tuliwaagiza neno hili; kwamba ikiwa mtu hataki kufanya kazi, basi, asile
chakula” (2The 3:10). Tunapokuwa wavivu tutambue kuwa tumekosa bidii ya
kufanya vitu ipasavyo. Maana katika kufanya bidii tunajipatia maendeleo ya
kimwili pia kiroho, inatuonyesha utu. Misho katika maonyo tunaambiwa kuwa
“uvivu ni mama wa dhambi nyingi”
Kwa kumalizia, tunapokuwa tukisali sala
ile aliyotufundisha mwokozi wetu, tuifanye na kuwa kielelezo cha sala zote (Mt
6:9-15).Kumbe daima tusalipo tusali kwa moyo mmoja ili aweze kutimiza
lile ombi la tano lisemalo “Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na
yule mwovu.”(Mt 6:13). Daima tukiendelea kuisali kwa moyo radhi wa
Imani, matumaini na mapendo atatuepusha na hayo maovu.
3.2 Kukosekana kwa Upendo
Tukirejea katekisimu ndogo ya Kanisa
Katoliki juu ya Fadhila za Kimungu: Mungu ametaka tuweze kuitunza neema ya
utakaso vizuri na kushika ahadi ya ubatizo kwa wepesi kabisa. Kwa hiyo wakati
wa ubatizo wetu ametia fadhila za Kimungu
na vipaji vya Roho Mtakatifu rohoni mwetu. Hivyo kuna fadhila tatu za
Kimungu: Imani, matumaini na mapendo, ambapo hatuwezi kujipatia fadhila
hizi kwa nguvu zetu wenyewe, kwa maana ni vipaji vya Mungu vipitavyo tabia na
nguvu za kibinadamu. Kwa hiyo, Mungu amezitia rohoni mwetu fadhila hizi mara
baada ya ubatizo ikiwa ni pamoja na neema ya utakaso; pia tunayo lazima ya
kuzitunza kwa sala na matendo yetu.
Tujiepushe na Maisha bila sadaka. Mtu
anapenda kuishi maisha ya fahari tu, pasipo kujikatalia baadhi ya vitu ambavyo
siyo vya msingi katika maisha. Kwa mfano, unamkuta ni mtu anapenda kubalisha
kuvaa nguo kila baada ya masaa sita (6); hapo hapo anatokea au anahamasishwa
juu ya kujitolea kuchangia watu wasiojiweza kwa kutoa kiasi chochote kadiri
anavyoguswa. Ila anashindwa kuchangia chochote hata kutoa 5,000/= akifikiri
kwamba akitoa tu hiyo atavuruga mipango yake ya kuendelea kununua nguo. Kumbe
kinachomchochea kufanya hivyo ni kupenda sifa na kujionyesha kwa watu wengine,
akidhania kuwa akionekana na wale waliomzoea akibadili nguo mpya mara nyingi
watamwona ameishiwa au ni kabwela tu. Tujiepushe kufanya vitu ili tutazamwe na
watu, maana tunaambiwa amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwandamu; nasi
tusileweshwa kwa kupenda sifa za watu pia tuachane na umaarufu kwa vitu visivyo
na maana sana katika maisha. Maana ni pale tuonapo shida au kupata ugumu fulani
katika kuamua tunapata suluhisho kamili. Albert Einstein anasema “katikati ya
ugumu pana fursa.” Hivyo tusiwe wagumu kutoa sadaka kwa namna yoyote ile kwa
maana ni katika kutoa kuwa nasi tunapokea (It is in giving that we receive) Mt.
Fransisko wa Asiz alisema.
Muda mwingine tunajisahau sana juu ya
mapendo, tukisema tunampenda Mungu wakati tunawachukia wenzetu wala kweli haiko
ndani mwetu; maana huwezi kusema unampenda Mungu usiyemwona wakati mwanadamu
mwenzako unaemwona humpendi. Kumbe tunaalikwa kwanza kumpenda Mungu kupita
yote, kwani yeye ni Mpendevu kabisa. Maneno ya Roho Mtakatifu “Mungu
ni upendo, na mwenye kuishi katika upendo, anaishi ndani ya Mungu na Mungu
anaishi ndani yake.”(1Yoh 4:16). Kwa sababu hiyo “Basi, tumpende Mungu, kwa sasabu
yeye alitupenda kwanza.”(1Yoh 4:19). Vivyo hivyo ni kwa mapendo yake
Mungu ametuumba, ametukomboa na anatutakasa.
Utamwonyeshaje basi Mungu kuwa
unampenda? Ni kwa kushika amri zake. Yesu anasema “Mkinipenda, mtazishika amri
zangu.”(rej. Yn 14:15). Nayo maneno ya Roho Mtakatifu yanasema: “Kumpenda
Mungu, ndiko kuzishika amri zake. Na amri zake si nzito.”(Rej. 1Yoh 5:3).
Kwahiyo, Mkristu hodari ataonyesha mapendo yake pia kwa matendo yasiyoamriwa,
yaani yaliyo ya hiari.
Dhana msingi kabisa ya kuonyesha ukuu
wa upendo ya kwamba upendo hushinda yote ni huu, katika maisha ya Yesu hapa
duniani alikutana na majaribu mbalimbali mengine yakitoka kwa Mafarisayo,
Masadukayo, Waandishi na Wanasheria wakimwuliza katika hali ya kumjaribu juu ya
amri iliyo kuu kupita zote. Yesu anawafundisha kwa maneno haya: “Umpende
Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako
zote na kwa nguvu zako zote. Hiyo ndiyo amri iliyo kubwa nayo ya kwanza. Na ya
pili ni sawa na hiyo: Umpende mwenzako kama unavyojipenda mwenyewe.”(Rej. Mt
22:34-40, Yn 13:34). Kwasababu hiyo kila Mkristu anaalikwa kuishi
maisha ya upendo maana kwa kuishi hivyo dunia itabadilika na kuwa kitalu cha
Amani pia uovu kupungua, kwa kuwa kabla ya kumtendea mwenzako chochote utaanza
kujifikiria kwanza mwenyewe je! Unachotaka kumtendea, nawe utapenda au
utafurahi kufanyiwa vivyo hivyo. Kumbe mwaliko kwetu sote ni kuendelea kuishi
katika ile hofu ya Mungu (Rej. Rum 12:10). Maana alitueleza chochote
tukitendacho katika wale walio wadogo basi tunamtendea yeye. Kwa mantiki hiyo,
mapigano baina ya nchi na nchi, mapigano ya ndani ya nchi na pia migogoro,
kutothaminiana na kujaliana, kuwa watu wa visasi na mafarakano ndani ya familia
zetu ni ishara wazi ya kuwa watu hatupendani kabisa (hatuna upendo ndani, ndani
mwetu). Hivyo basi tujitahidi kuiishi tunu hii ya upendo na itaweza kubadili
maisha yetu kwa ujumla na dunia nzima. Naye mzaburi anasema katika Zaburi 133“Tazama
jinsi ilivyo vyema na kupendeza, ndugu wakae pamoja kwa umoja…maana huko ndiko
Bwana aliamuru Baraka, naam uzima hata milele” nasi tuone fahari kuishi
kwa umoja maana katika umoja kuna upendo usiogawanyika.
Kiini
chote cha mafundisho ya Imani na ufundishaji wake lazima vielekezwe kwa upendo
ambao kamwe hautakuwa na mwisho. Iwe kitu kinaelezwa kwa ajili ya ukweli wa
imani au kwa lengo la matumaini au wajibu wa utendaji wa maadili, upendo wa
Bwana wetu hauna budi kuonyeshwa daima, ili kila mmoja aweze kuona ya kwamba
kazi zote za fadhila kamili ya Kikristo hutokana na mapendo na hazina malengo
mengine isipokuwa mapendo tu(Katekisimu ya kirumi, utangulizi 10, KKK 25).
3.3 Kukosekana kwa Huruma
Neno msamaha au huruma siku hizi
limekuwa kama msamiati mgumu, maana watu wengi hawalijali na kuona kama linafaa.
Zaidi ya hayo yote tunajibidisha na vitu tunavyosema je! vinalipa au laa! kabla
ya kutenda. Neno huruma limetumika sana hata katika kuumbwa kwetu na kuwa hivi
tulivyo sasa ilikuwa tu kwa sababu ya huruma ya Mungu, ndiyo maana hakutaka
tuangamizwe na ghadhabu yake pindi tunapokuwa tumemkosea bali tukimbilie
msamaha wake kupitia sakramenti ya kitubio (upatanisho). “Mungu hakutuumba ili
tuangamizwe na ghadhabu yake… kwa maana yeye hapendi mtu yeyote apotee bali
wote wafikie toba… daima yupo tayari kumpokea kila ajaye kwake yeye mwenyewe
anasema; “Nirudieni mimi kwa mioyo yenu yote...” Yoeli 2:12-14. Yesu
alitupenda upeo na anatupenda ndio maana alijitoa mwenyewe afe msalabani ili
tupate wokovu. Kumbe basi usalama wetu upo katika huruma ya Mungu tu. “Wala
hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini
ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo” Mdo 4:12.
Pasipo huruma ya Mungu mtu hana thamani yoyote.
Bwana Yesu Kristo anaita watu wote waje
kwake akisema “Njoni kwangu ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami
ntawapumzisha. Jitieni nira yangu mkajifunze kwangu, kwa kuwa mimi ni mpole na
mnyenyekevu wa moyo nanyi mtapata raha nafsini mwenu; kwa kuwa nira yangu ni
laini na mzigo wangu ni mwepesi.”(Mathayo 11:28-30)
“Njoni kwangu nyote” maana yake ni
kwamba hambagui yeyote yule. Anayeitikia wito huu na kuja kwa Yesu hupata
huruma kuu ya Mungu. Hivyo basi mtu
yeyote asiseme moyoni mwake kwamba yeye amepangiwa kutokufika Mbinguni. Bila
kumbagua yeyote Yesu anatupokea, “kwa maana yeye hapendi mtu yeyote apotee bali
wote wafikie toba...”2Pet 3:9.
Tuepukane na kitu kinachoitwa Ushindani
bila huruma. Kwa kupoteza hofu ya Mungu, mtu yuko radhi kumwua mwenzake
ilimradi tu yeye aibuke kidedea au mshindi wa tukio hilo. Daima tujifunze kuwa
na wivu wa maendeleo, yaani kama unajua au unaona kitu Fulani huwezi ukubaliane
na hali yako tu; kama vijana wa kisasa wasemavyo kuwa pambana na hali yako.
Kumbe sasa ni muhimu kubadili mienendo
yetu inayomchukiza Mungu. Hakuna awezaye kumpendeza Mungu asipokubali
kujiachilia kwa Yesu Kristo na kumruhusu ayatawale maisha yake. Ni vizuri ifikie
wakati tumwambie Yesu “Bila wewe mimi siwezi”. Tujitahidi kufananisha matendo
yetu na ya Kristo Yesu, hapa ndipo tutaweza kujiachilia katika huruma yake. Na
huruma hii inaendana kabisa kwa ukaribu na upendo, hivyo hatupaswi kuwa kama
Petro aliyemwuliza Yesu kuwa ndugu yake akimkosea yafaa amsamehe mara ngapi? Na
akajipa jibu Petro lake kama kumdadisi Yesu Hata mara saba? Ila Yesu
anamwambia ya kuwa bado haitoshi mara saba, bali hata saba mara sabini (Mt
18:21-22). Huyu alikuwa Petro walau yeye aliona yafaa amsamehe nduguye
mara saba, je! Mimi na wewe tungeweza hata kufikia hiyo mara saba? Kwa muktadha
wa sasa tuliowengi tungeishia kusema tu kuwa tusamehe mara tatu yafaa. Kwa hiyo
msamaha au huruma haina kikomo wala kiasi, kila mmoja anaalikwa kusamehe kadiri
awezavyo: maana tunaambiwa tumepewa bure nasi tutoe bure. Mungu katujalia kuwa
watu wa huruma, nasi hatunabudi kusameheana pia kuhurumiana; tukiendelea
kuchukuliana misalaba.[43] Pia
tunaambiwa kuwa kadiri tufanyavyo huruma ndivyo Mungu pia atutendeavyo.[44]
3.4 Kupuuza wengine (Dharau)
Kwanini tufike mahali tudharauliane?
Kama viumbe dhaifu tunasahau ya kuwa sote tumeumbwa kwa mfano na sura ya Mungu (Rej.
Mwa 1:26). Bali tunapaswa kujivunia utajiri tulijaliwa na kuutumia
vema. Kwa mantiki hiyo kila mmoja amejaliwa karama na talanta mbalimbali,
ambazo ndizo zinazoendelea kututegemeza sisi katika kujiendesha katika maisha
ya hapa duniani (Rej. 1Kor 12:4-11). Ndiyo maana hata katika utume wa mamlaka ya
ufundishaji katika Kanisa umepewa kwa watu wachache ili kuhakikisha Taifa la
Mungu linadumu katika ukweli ambao ndiyo unaowafanya huru. Katika kutekeleza
utume huu Kristo amewapa wachungaji karama ya kutokosea katika mambo ya Imani
na maadili, na utekelezaji wake una namna nyingi kulingana na ngazi kama padre,
Askofu au Papa.[45]
Vivyo hivyo hata katika maisha ya kitawa, ngazi ya mabikira humweka mwanamke
anayeishi ulimwenguni ili akae katika sala, toba utumishi kwa ndugu zake,
kadiri ya karama husika zinazotolewa kwa kila mmoja.[46] Kwa
hiyo tujifunze kuthaminiana pasipo kudharauliana, tukitambua kuwa kila mmoja
wetu amejaliwa kitu cha kipee ambacho mwingine hana kabisa. Tukiendelea
kudharauliana kati ya mwenye nacho na asiye nacho, inamaana kwamba tunajifungia
milango ya kupokea zile heri nane, na hivyo Mwinjili Luka anatueleza kinaganaga
katika heri nne (Rej. Lk 6:20-22) na laana nne. Hizo laana nne ndilo tuzo la
huyu mtu anaedharau wenzake wasio na kitu atakachopata itakuwa ni kilio na
kusaga meno (Rej. Lk 6:24-26). Kumbe msemo usemao tujifunze kutofautiana
pasipo chuki, na kuchukuliana kwa upendo. Lakini yote haya tunayafanya pasipo
kujua kwamba tumeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu mwenyewe? Au kutotambua kuwa
Mungu amemjalia karama na kipaji cha kipekee kila mmoja wetu? Kwanini sasa
tudharauliane wakati tunajua hamna aliyemkamilifu au anayejitosheleza kwa kila
kitu isipokuwa Mungu tu? Nakuachia swali hilo msomaji wa kitabu hiki, na
ujaribu kujitafakari je! wewe binafsi upo sehemu gani?
SURA YA NNE
4.0 MABADILIKO YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA
Katika ukuaji wa mambo ya ulimwengu huu
yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na suala la mabadiliko ya sayansi na teknolojia.
Lakini pia tukumbuke kuwa hata hawa wanasayansi nao pia wameumbwa na Mungu, na
kujaliwa karama hiyo ya uvumbuzi na utengenezaji wa mambo mbalimbali. Lengo kuu
ni katika kumrahisishia mwanadamu katika harakati zake za kuendesha maisha yake
kwa ujumla. Mfano; utengenezwaji wa ndege, ambao unamwezesha mwanadamu takiribani
kuweza kufika karibu kila sehemu apendayo. Vivyo hivyo, palipo na mafanikio
changamoto hazikosi; ni kupitia mabadiliko ya sayansi na teknolojia ulimwengu
umeanza kupoteza vile vitu asili vilivyowekwa na Mungu. Kumbe mabadiliko haya
yamekuwa ni kama msumeno ambao hukata huku na huku, yaani mabadiliko haya
yameleta matokea ambayo ni chanya lakini pia hasi kwa dunia nzima.
Mtu mmoja ambaye anapingana na falsafa
(fikira), Ukristo (maadili) na Sayansi (ukweli); Friedrich Wilhelm Nietzsche (kuzaliwa
15-10-1844, kufariki 25-8-1900) alijiita Nabii kwa kutabiri kuwa kuanzia karne
mbili(2)zijazo dunia itakuwa katika matarajio ya mchakato usioepukika;
ukomunisti, mijini, kiwango kikubwa cha viwandani, elimu, vyombo vya habari na
utamaduni, utamaduni wa kisasa, kupambana na jadi na uhuru wa kibinadamu… Na
mpaka sasa kweli tumeianza karne ya pili tangu afariki dunia, na yale
aliyoongelea yameshaanza kutokea. Kwa wenzetu Nchi zilizoendelea walio wengi
sasa hawamtambui Mungu, na wameendelea kiasi kwamba wanaweza kubashiri na kujua
ya kesho. Kwa kushindwa kutambua na kuona uwepo wa Mungu, maana yake wamejiunga
na Nietzsche aliyehitimisha kwa kusema Mungu amekufa (God is dead). Sasa katika
sehemu hiyo tutaona mambo yanavyoenda sasa, nawe msomaji utaona kwamba
mwanadamu ni mtu wa hatari sana; mpaka ameshaanza kufanya vitu kinyume hata na
mpango wa Mungu aliounuia tangu mwanzo kupitia kwa wazazi wetu wa kwanza. Hivyo
katika sehemu hii tunaenda kuona jinsi gani teknolojia imechangia kwa kiasi
kikubwa katika mambo yahusuyo mauaji ya watu wasio na hatia. Pia katika kutafakari
janga hilo kubwa, tukumbuke kuwa mwenye mamlaka ya kuchukua uhai wa mtu ni
Mungu pekee.[47]
4.1Uharibifu mkubwa wa mazingira
Tukirejea katika kitabu cha mwanzo
tunaambiwa kuwa na tazama kila alichokiumba Mungu ni chema (rej. Mwa 1:31).
Wema unaoongelewa hapa si kitu kingine bali Mungu aliweza kukiweka kila kitu
katika hali yake ya kuweza kujiendesha.
Hali kadhalika, kila kitu kiliwekwa katika ukamilifu wake kulingana na
mpango wenyewe wa Mungu. Neno mazingira lina maana ya kila kitu kituzungukacho,
kama uoto, mawe, mito, bahari na mengine mengi yanayotuzunguka.
Kupitia mabadiliko ya sayansi na
teknolojia, viwanda vinavyotumika kuzalisha na kutengeneza mambo ya kumsaidia
mwanadamu ndivyo vinavyochafua hewa. Kadhalika moshi utokao viwandani muda
mwingine hutoka na viambata vyenye sumu, ambapo huenda kuharibu anga
(destruction of ozone layer) pia kuathiri mwanadamu pindi tu anapoivuta hewa
hiyo iliyochanganyikana na viambata vikali vya sumu. Pia inaweza kupelekea hata
kuathiri mfumo mzima wa uumbaji wa pili ambao mwanadamu amepewa na Mungu. Si
hivyo tu hata moto tunaotumia kuchoma msitu, kukata miti kwa kutumia misumeno
au shoka pia panga; vyote vimetengenezwa kupitia maendeleo haya ya sayansi.Kwa
kutambua hilo ndiyo maana mataifa yameweka mpango mkakati wa makubaliano ya
Paris juu ya mabadiliko ya tabia ya nchi, ambayo yanalenga kupunguza
uzalishwaji wa hewa na gesi chafu duniani.
Viongozi wa Kanisa kama nilivyosema
mwanzo kuwa Kristo amewapa karama na mamlaka ya kukosoa katika mambo ya Imani
na maadili, hivyo kipindi wanapoona mambo hayaendi vizuri wanakila sababu ya
kushauri na pia kukemea mapema kulingana na ule mwelekeo uonyeshao madhara. Baba Mtakatifu Francis katika mwaka wa
tatu wa Upapa wake tarehe ya 24/5/ 2015 sikukuu ya Pentekoste aliweza kuzindua
Bula ya Sifa kwako ee Bwana (Laudato si). Kazi yake ilitoa mwongozo wa
namna nzuri ya utunzaji wa mazingira kwa ulimwengu mzima. Bula ilipokelewa
vizuri sana na mataifa yenye nguvu duniani ikiwemo Marekani. Baba Mtakatifu
Francis hakuishia hapo akaanda sala ya kutukumbusha na kuelewa uzuri wa
ulimwengu huu ulitoka wapi, na hivyo tuone tuna kila sababu ya kuutunza.
SALA KATIKA UMOJA PAMOJA NA UUMBAJI.
Baba, tunakutukuza pamoja na viumbe wako wote.
Vyote vilitoka katika mikono yako mikuu. Vyote ni vyako, vimejazwa uwepo na
upendo wako mwanana. Sifa ziwe kwako!
Mwana
wa Mungu, Yesu. Vitu vyote vilitengenezwa kupitia kwako. Ulifanyizwa tumboni
mwa Maria mama yetu ukawa sehemu ya dunia hii na ukautazama ulimwengu huu kwa
macho yako ya kibinadamu ndani ya utukufu wa ufufuko wako, Sifa ziwe kwako!
Roho
Mtakatifu, kwa mwanga wako unaongoza ulimwengu huu kupitia pendo la Baba na
kuusindikiza uumbaji unapogumia kwa utungu. Unakaa ndani mioyoni mwetu pia na
unatuvuvia kutenda yaliyo mema. Sifa ziwe kwako!
Bwana
wa utatu, jumuiya ajabu ya upendo usio na mipaka tufundishe kukutafakuri wewe
katika uzuri wa ulimwengu kwani kila kitu kinasema juu yako. Amsha sifa na
shukurani zetu kwa kila kilichopo ambacho umekifanya. Tupe neema kujisikia
kuunganishwa na kila kilichopo.
Mungu
wa upendo, tuoneshe sehemu yetu katika dunia hii kama mikondo ya upendo wako
kwa viumbe vyote vya dunia hii kwani hakuna hata kimoja kinachosahaulika mbele
zako. Angalia wote wenye mamlaka na mali ili waiepuke dhambi ya kutojali, ili
wapende mali yetu ya pamoja, wawasaidie wanyonge, wawutunze ulimwengu huu
tunamoishi masikini na dunia vyote vinakulilia.
Ee
Bwana, tuteke kwa nguvu na mwanga wako, tusaidie tulindeaina zote za maisha,
Tujiandae kwa mustakabali bora kwa ujio wa ufalme wako wa haki, Amani, upendo
na uzuri. Sifa ziwe kwako! Amina.
Kadhalika tunaalikwa sote kwa pamoja,
kila mmoja kwa nafasi yake kutunza mazingira. Kwa kufanya hivyo tutakuwa tunaendeleza
ule uumbaji wa Mungu lakini pia zaidi tukiheshimu na kuifanya kazi ile
aliyotupatia kuvitawala vitu vyote. Maana tusipofanya hivyo tunaambiwa katika
vitu ambavyo havina uwezo wa kutoa msamaha ni Mazingira. Kwamba ukishayaharibu
mazingira usitegemee kuwa yatarejea au kurudi katika uzamani wake kama
yalivyokuwa. Kumbe tutambue kuwa tunapoyakosea haki mazingira yetu kwa
kuyatunza, kwa hakika lazima yatuadhibu. Ambapo baadhi ya madhara yatokanayo na
uharibifu wa mazingira ni pamoja na ukosefu au upungufu wa mvua, ukame, baa la
njaa, kiu, n.k
4.2 Mauaji ya makusudi.
Kuua ni kitendo cha kutoa uhai wa kitu
au mtu kwa namna yayote ile aidha kwa bahati mbaya au kwa kudhamilia. Katika
Maandiko Matakatifu neno kuua limetumika sana, tukianzia na Kisa cha Kaini kumwua
nduguye Habili kisa wivu tu baada ya ile sadaka ya Habili ya kuteketezwa
kupokelewa mbele ya Mungu (Rej. Mwa 4:1-8). Kadhalika Mungu
aliwaua wazaliwa wa kwanza wa wamisri baada ya Farao kukataa kuwaruhusu wana wa
Israeli (Rej. Kut 13:15). Pia tunaelezwa juu ya Mungu kuwaua wafalme
wenye nguvu akina Sihoni, Ogu (Rej. Zab 135:10-12; 136:18-22).
Tunaambiwa kuua kwake Mungu ilikuwa haki yake kufanya vile ili aweze kulikomboa
taifa lake teule la wana wa Israeli.
Mauaji ninayozungumzia ni yale
yatokanayo na vita. Vita hii inayoonekana katika mataifa yenye migogoro ya
kisiasa. Mara zote yanachochewa na ile kuwa na uhakika wa silaha ambazo ni
nzito sana na zimefanyika hivyo kupitia mabadiliko ya sayansi na teknolojia.
Taifa na taifa wanawekeana vitisho vya vita ili kujaribu tu kupima silaha zao
walizotengeneza zinauwezo gani wa kuleta madhara. Mfano, haya ndiyo yanayoendelea
katika Taifa la Korea kaskazini wakijaribu kufanya vitisho dhidi ya Marekani.
Kile kinachoendelea katika nchi ya Syria, kinasababishwa na kile kiburi cha
kuwa na silaha za kutosha kwa Rais Bashar Al Assad: ndiyo maana tangu mwaka
2006 vita vya wenyewe kwa wenyewe vinaendelea mpaka sasa havijamalizika, licha
ya mataifa mengine kuingilia kati ili kutaka kuinusuru Syria kwa kumwondoa Rais
bado hawajaweza sababu kubwa ikiwa amejiimarisha vema katika nyanja ya silaha
ambazo ni zao la mabadiliko ya sayansi na teknolojia.
Na kimaadili inasema kuwa katika hali
ya kujilinda unaweza kutumia vifaa vinavyoweza kumjeruhi adui yako, kuua kabisa
inayosemwa ni ile inayotokea bila kudhamiria kumwua. Mfano; unafyatua risasi
kwenye bunduki yako ukimlenga risasi ya miguuni adui yako lakini naye katika
kujihami akawa ameinama na hapo risasi ikapiga kifua akafaa, hiyo kimaadili
inaweza kuelezeka katika dhamira.
Mauaji yanayoendelea katika ulimwengu
huu wa sasa mengi yanachangiwa kuongezeka kwa kasi sana silaha mbalimbali;
kwani njia na vitu vitumikavyo kutekeleza unyama huo vimerahisishwa. Mfano mtu
mwenye chuki au nia mbaya nawe anaweza kukuangamiza tu atakapoanza kukuwinda
mara na kukuona sehemu ya maficho kidogo, kwa kutumia silaha (bunduki ndogo);
ambayo inamwezesha yeye kutembea nayo na haitoi sauti kubwa wakati wa
kutekeleza shambulio. Kadhalika tumeona majambazi wakitekeleza uporaji mara
nyingine kuua mara baada ya kuhisi kutambulika kwa kutumia silaha aidha ziwe za
jadi au bunduki. Yote haya hufanyika hivi kwa kuwa mtu akihitaji silaha ya
kununua kigezo ni pesa yake, kama anayo ananunua kwa nia ya kusema kuwa ni kwa
ajili ya kujilinda au usalama wake.
Pia tunaona na kushuhudia ajali za
barabarani zikiua watu wasiokuwa na hatia kwa kutojali sheria na kasi wakati wa
uendeshaji barabarani kwa baadhi ya madereva. Yote hayo yamesababishwa kwa
kiasi kikubwa na hayo mabadiliko ya sayansi na teknolojia, lengo hasa mahususi
yakilenga kumrahisishia mwanadamu katika kuendesha maisha yake. Kwa bahati
mbaya sasa mwanadamu huyo ndiye anatumia vitu hivyo vibaya, kwaajili ya
kutimiza haja zake binafsi.
Hivyo basi, tunapaswa kutafuta Amani
ambayo ndiyo huleta heshima na maendeleo ya mwanadamu kwa ujumla. Amani hii si
kutokuwako vita tu na wala haiwekwi tu kwa kushikiza usawa wa nguvu kati ya
wapinzani. Amani haiwezi kupatikana duniani bila usalama wa mali na watu, uhuru
wa mawasiliano kati ya watu, kujali hadhi ya watu na mataifa, na jitihada za
kuishi udugu (KKK 2304).Tuungane na Nabii Isaya anayesema “Amani ni kazi ya
haki na matunda ya mapendo.”(rej. Isa 32:17).
Lakini pia wale wanaoendelea kufanya mauaji hao watambue damu hiyo
wanayayomwaga inawalilia, kama ilivyokuwa kwa Kaini. Mungu alimwambia Kaini “sauti ya damu ya ndugu yako inanililia
kutoka katika ardhi” (Mwa 4:10).
4.3 Matumizi mabaya ya vifaa vya Mawasiliano
Mawasiliano ni kitendo cha kuchukua au
kutuma na kufikisha ujumbe kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine au kutoka
sehemu moja kwenda nyingine. Mtaguso Mkuu wa pili wa Vatikano; katika hati yake
ihusuyo Kanisa unatueleza namna nzuri ya kushirikishana mambo mbalimbali bila
ubaguzi kwa walei wote ukisema “Zaidi ya hayo, walei kwa kuunganisha nguvu zao
waweza kuponya taasisi na hali za maisha zinazochochea dhambi katika ulimwengu,
hivi kwamba wote waweze kufuata kanuni za haki ambazo zinarahisisha kutenda
fadhila badala ya kuwa kizuizi. Kwa kufanya hivyo wanapenyeza thamani ya
maadili katika utamaduni na kazi za binadamu.”[48]
Mfano halisi ni chombo cha mawasiliano
kiitwacho simu. Simu imekuwa ngangali na ngunguli katika uovu sana, nadhani
kupita kitu kingine zaidi. Simu kwa sasa baada ya kutumika kuwasiliana kwa
mambo yenye tija na manufaa; inatumika katika kupanga njama za uzinzi na uasherati,
wizi kwa namna ya pekee katika kutekeleza uharifu ikiwemo utekaji na ujambazi,
uongo ambao unatikisa na kusambalatisha mpaka familia. Na hii imekumba takribani
rika zote, si vijana si watu walio tayari katika maisha ya ndoa. Ndiyo maana
ndoa nyingi siku hizi tunaziona zikiharibika pasipokuwa sababu ya msingi. Zaidi
utasikia wameamua kuachana baada ya Mme au Mke kuchukua simu ya mwenzake, sasa
anachokutana nacho humo ndani hakielezeki kwa maana ya kuwa anaona na kujua
kuwa hayuko peke yake katika ndoa bali wengi.
Kama umewahi kushuhudia ni watu
wachache sana ambao wanaweza kuiacha simu tu nje nje, zaidi kama anaiacha tu
unakuta kaiwekea funguo (password) yaani kaiwekea namba ya siri karibu kila
sehemu. Na kwa nini haya yote kutokea katika wanandoa? Katika maisha ya sasa
watu wengi hususani vijana hawatambui tena utu wao uko wapi. Hivyo kupelekea
kudandia gari kwa mbele, licha ya kwamba tumeambiwa na Mhubiri kuwa kila jambo
linawakati wake (Rej. Mhu 3:1-8). Kwa hiyo, wanapokuja kubariki ndoa yao
wanakuwa kama watu wanaoigiza, maana hamna anayekuwa ametunza utu wake kabla ya
hapo. Mbaya zaidi kwa upande wa akina Dada ndiyo zaidi wanaathirika
kisaikolojia pale anapojikuta ambaye ameshiriki naye katika kumvua utu wake kwa
mara ya kwanza siye aliyemwoa. Tunaambiwa katika ndoa hiyo kuna mwingine hawezi
kukaa kwa utulivu, kama tujuavyo kuwa binadamu tuna hulka ya kukumbuka. Maana
kinachosababisha anakuwa ameshaweka agano la nafsi na mtu aliyemtolea ubikira
wake. Hivyo anapomkumbuka tu yule wa kwanza atajitahidi kumtafuta kwa namna
yoyote ilimradi tu ampate na aweze kutimiza haja yake. Sasa kifaa kitumikacho
kumtafuta mtu huyo tunaweza kumwita pengine mwana mpotevu ni simu kwa maisha ya
sasa, atajitahidi kuuliza kila mtu ambaye anaweza kuwa na namba yake.
Hali
kadhalika tunaambiwa kama vile ndoa nafsi mbili zinavyounganisha kwa pamoja au
zinavyoambatana, ndiyo inavyokuwa watu wanavyofanya ngono nje ya ndoa na kuunda
mshikamano wa nafsi unaopelekea kuwa utumwa wa kipepo. Muungano unatokea hapa
ulianzishwa na Mungu ili kuwafanya wanandoa wawili kuwa mwili mmoja mbele zake
(Mwanzo 2:24; Malaki 2:15; Mathayo 19:5-6), lakini ngono kabla ya ndoa na ile
ya nje ya ndoa inaweza kwa namna ya ajabu kushikamanisha nafsi ya mtu mmoja na
wengi. Kama mtu akifanya ngono na watu wengine zaidi ya mke wake, anaunda
mshikamano wa nafsi unaoweza kusababisha kila aina ya matatizo (ya kimwili,
kiroho na kiakili) kwa kuwa ngono si tendo la kimwili tu, lakini ni la kihisia
na kiroho pia. Sasa mshikamano wa nafsi unaotokea katika mazingira haya huwa
njia ambayo mapepo yanapitisha chochote wanachotaka kwenda kwa wale wahusika
ili wadumu katika kifungo au kuwadhuru.[49]
Kutokana na maelezo hayo juu, ndiyo
maana tunapata misamiati kama kuchepuka
siku hizi. Sasa niambie pale Bwana wake atakaposhika simu ya mkewe na kuona
kuna namba ameiweka ya mtu, jina lenyewe lilivyo linatia ukakasi na linaonyeha
muda mwingi ndo namba hiyo inafanya mawasiliano tu; nini kitatokea? Hapo jibu
rahisi ni kwamba atamfata mkewe na kumhoji juu ya mtu huyo kuwa ni nani na
anapojaribu kujitetea lazima aseme uongo ili abaki salama, hapo ndipo utasikia
kila siku ni fujo na migogoro tu ndani ya nyumba; mpaka kufanya uvumilivu
kufika kikomo mmoja anaamua kuondoka na hapo ndoa inaishia hapo. Maana
kinachoshangaza kama ni Mama amechoshwa na kipigo cha kila mara, siku akisema
anarudi kwao mwanamme naye siku hiyo hiyo naingiza jiko lingine ndani. Hii ina maana
kuwa wote inawezekana walikuwa na miradi sehemu mbalimbali ila kwa kuwa wanasema
siku za mwizi ni arobaini; basi aliyewahi kufikia hiyo siku ya arobaini ndiye
anaondoka. Hapo tujifunze fadhila ya uvumilivu na kuona kabla ya kumnyoshea
mwenzako kidole kimoja, jitazame nawe kuwa kuna vidole vitatu vinakuangalia;
tusiwe wepesi wa kuhukumu wengine bila kujitafiti kwanza sisi wenyewe.
Lakini yote hayo yamesababishwa na
msingi mbovu wa malezi, maana watu wa zamani wao walijua na kulelewa katika
misingi ya maadaili ya kabila husika. Kwao waliweza kukaa mpaka kukamilisha
ndoa yenyewe siku wanapopata Baraka za wazazi, yaani kuoana rasmi.Vijana
wenzangu tujifunze kubadilika, na kuwa na ule uchu wa kusema kama wa zamani
waliweza kwa nini mimi nisiweze! Hiyo itatutia nguvu na kutufanya kupiga hatua
mbele kidogo, japo utandawazi ndiyo dhana inayotawala sasa akili zetu pia
fikira zetu kwa muda mwingi.
4.4 Chanzo cha mahusiano mabaya
Mahusiano mabaya nayaanza kutokea pale
tu tunaposhindwa kutenga muda wetu kwa ajili ya kuwapa nafasi watu wengine.
Nikitolea mfano wa simu, siku hizi mtu anaweza kuwa anaongea na mtu mwingine
iwe ni katika stori au kuuliza kitu au kushirikishana; kinachoshangaza utakuta
mtu huyu anaendelea kuongea na mtu huyu akiendelea kuchati na simu yake. Hivyo,
ile ngazi ya uhusiano lazima ipungue maana mtu mwingine ataanza kumfikiria
mwenzake pengine amemdharau.
(i)Uhusiano
mwingine unaweza kuwa baina ya taifa na taifa, kwa kuwekeana uhasama.
Mfano: unakuta taifa hili
limejiendeleza katika kutengeneza silaha za masafa marefu, taifa lingine katika
kuzalisha bidhaa zitumiwazo na wanadamu kila siku. Lazima watu au mataifa haya
yaingie katika uhasama, ambapo mtengeneza bidhaa atamchukia mtengeneza silaha
tena kali na kuanza kujihami naye. Sasa nini chanzo cha mafarakano hayo?
Unakuta ni kupitia ujuzi huu wa sayansi na teknolojia kutofautiana tu, na hapo
huleta kutoelewana kati ya watu au mataifa.
(ii) Ushabiki wa kila kitu (Kiu na tamaa ya mali
na maisha ya kuiga).
Unakuta kijana kila
kitu kinachotoka au kutengenezwa na kuona kipya iwe ni mavazi au vifaa vingine
anajikuta anashadadia, licha ya kwamba pengine hana kipato cha kutosha. Kwa
kuwa anakuwa ni mtu wa ushabiki, kupenda sifa atafanya kwa namna yoyote ile ili
akipate atakacho. Sasa anapoamua kutumia njia mbaya kujipatia kitu hicho, moja
kwa moja anakuwa hajafanya mahusiano mazuri na mtu pengine aliyemwibia tu.
Tukitambua katika suala la maadili, kwamba kile kibaya kinachotendwa na mtu
mwovu mmoja aidha mwizi kinaleta madhara kwa jamii nzima; maana hakuna jamii
inayomkubali mwizi. Hivyo kijana aidha ajulikane kwa tendo hilo au asijulikane
moja kwa moja katika dhamira yake impe somo kuwa ameshajitenga na jamii yote
inayomzunguka.
(iii) Kanisa kujibebesha agenda ya uzazi wa
mpango.
Uhusiano huu unakuja
kuonekana mbaya baina ya Kanisa na Waamini pindi tu matokeo yake wengine
kutumia njia sahihi yaani kwa kutumia njia ya asili, lakini wengine wengi zaidi
kutumia njia chafu na mbaya za kisasa. Hii inakumba watu wengi zaidi na mbaya zaidi
unakuta hata wale ambao tunakuwa na matazamio nao makubwa katika kuielimisha
jamii (wasomi) wanatenda kinyume kwa kufuata njia ya asili (yaani kwa kufuata
mabadiko ya mwanamke katika mzunguko wake wa kila mwezi). Tuna kila sababu ya
kupiga vita kwa nguvu zetu zote njia hizo za kisayansi zinazokinzana na mpango
wa Mama Kanisa. Tuelimishane juu ya madhara yatokanayo na utumiaji wa vijiti,
sindano, vidonge na mara nyingine kuamua kutoa kizazi eti kisa kwamba watoto
uliojaliwa wametosha huhitaji wengine. Baadhi ya madhara ya kutumia njia hizo
za kisayansi, zinaweza kupelekea Kansa katika mkono wanapoziingiza hizo njiti,
pia Kansa ya Kizazi na muda mwingine kwa wale wanaothubutu hata kutoa kizazi
huishia kupata matatizo makubwa ya mahangaiko ya tumbo mpaka kufa kwao. Kwa nini
sasa tufikie mahali hayo tuyaruhusu? Kumbe tutambue kuwa Kanisa linapingana na
matumizi ya vidhibiti mimba (Contraceptive) maana vinaenda kinyume na mpango wa
Mungu katika kuendeleza kazi ya uumbaji.
SURA YA TANO
5.0 KUSHUKA KWA MAADILI
Siku zote uhuru humfanya mwanadamu kuwa
mtu mwadilifu. Na hivyo mtu anapotenda kwa kuazimia basi anakuwa ni Baba wa
matendo yake. Na hivyo matendo ya kibinadamu yanachaguliwa kwa makusudi,
kufuata hukumu ya dhamiri yanakuwa na sifa kimaadili. Kadhalika uadilifu wa
matendo ya kibinadamu hutegemea zaidi kitu,
nia na mazingira. Katika kitu tunaona
je, kilichochaguliwa ni chema ambapo utashi unajielekeza kwake kwa makusudi. Na
hili ndilo jambo la tendo la kibinadamu. Nia
hukaa upande wa mtu anayetenda. Kwa sababu hiyo nia hukaa katika chanzo cha
hiari cha tendo la kulainisha kwa njia za lengo lake, hivyo kufanya nia kuwa
kitu cha lazima katika namna ya kupima tendo kimaadili. Mfano: katika kutenda
jambo jema kwa jirani haigeuzi ile nia njema, na hivyo lengo halihalalishi
njia. Mazingira pia ni mambo madogo yanayochangia katika kuongeza au kupunguza
uzuri (adili) au ubaya wa tendo la kibinadamu. Yaweza pia kupunguza au kuongeza
wajibu wa mtendaji.
Kadhalika mazingira yenyewe hayawezi
kubadili sifa adili za matendo yenyewe; hayawezi kulifanya tendo kuwa jema au
sahihi ambalo kwa lenyewe ni baya.[50]
Changamoto zinazojitokeza na kuchochea kuporomoka kwa maadili, sehemu kubwa
inayoathirika ni mijini. Watu wakaao mijini naweza kusema ndipo kuna mizizi
hii, na hivyo mizizi hiyo kuanza kuambaa mpaka vijijini; inakuwa baada ya
kumaliza na kuwa imeshatapakaa sana. Hivyo baadhi ya changamoto zinazoelezwa
humu kwa wakazi wa vijijini bado tunaweza tusielewe vema nini hasa inamaanisha,
hususani changamoto zinazoenda hata kinyume cha asili. Ila tuyaelewe kwa moyo
na tuwe tayari kuyapiga vita maana mijini sasa yapo licha ya kuwa yanafanyika
chini chini.
5.1 Utandawazi
Utandawazi kwanza ni neno lililoanza
kutumika miaka ya 1990, likimaanisha kukifanya kitu kuwa katika kiwango cha
kimataifa na kukihamisha nje ya mipaka na kukifanya kuwa cha wazi na kikafanywa
na watu wa aina yote duniani.[51] Tunaweza
kusema kwa lugha nyepesi kwamba utandawazi ni mwingiliano wa kweli mbalimbali
ambao umefanya ukaribu wa kweli zaidi yaani dunia kuifanya kama kijiji.
Utandawazi umeleta mabadiliko makubwa kiutamaduni, kijamii, kiuchumi, kisiasa
na mengine mengi. Utandawazi pia una maana ya jambo linalolenga umiliki wa
fikira na wa kiutamaduni juu ya kusaidiana na kuungana yaani kuwa kitu kimoja,
kuondoa mipaka na masafa kati ya nchi na nchi, kukusanyika pamoja na kuleta
kitu kinachoitwa “kijiji ulimwengu.”[52] Hivyo kunapotokea
mwingiliano wa jamii zenye asili na mila tofauti lazima kutatokea shida aidha
pande zote au upande mmojawapo. Sasa kuna neno linatumika wakisema tunaenda na
wakati, sasa je, huu wakati unaoongelewa ndiyo ule Mhubiri anasema kuwa kila
jambo na wakati wake? Au ni ujinga wetu tu, kutotofautisha kati ya jana na leo
yaani kutenda vitu kulingana na mazingira husika kufuatana na kanuni na
taratibu za jamii yenyewe?
Mimi na wewe tuachane na Usasa
bila miiko. Wanasema, hakuna marefu yasiyokuwa na ncha. Baada ya malezi
kudorora tunaona kwamba, mlezi wetu mkuu sasa amekuwa ni utandawazi; ambapo
daima tunadai kuwa tunakwenda na muda ila kiuhalisia hatuna utandawazi bali
utandawazimu. Kwamba wewe jinsia ya kike kuvaa sketi fupi au nguo za kuonyesha
maumbile yako na muda mwingine nyingine zikitoa baadhi ya viungo nje; pia jinsia
ya kiume kujindanganya kuwa umevaa suruali wakati unatembea ukionyesha nguo
yako ya ndani au kuvaa suruali za kubana ni kukosa adabu. Sasa lazima tutambue
kuwa kila kitu kina mipaka yake, sote tupambane kutokomeza utandawazimu huu.
Maana ni katika umoja tunaweza. Lakini tatizo kubwa ni kwamba tunakuwa au
tunavutwa na umoja katika mambo ya upuuzi, ila yale mazuri, ya msingi
tunatengana. Hii itufumbue macho na kuona kwamba kuna nguvu ya shetani ndani
mwetu inayotuongoza.
Pia kwa uelewa wangu mambo hayo
nayaambatanisha na suala zima la mkumbo (mob), yaani kwa kuona mtu fulani yeye
yuko hivi nami nakuwa kama yeye. Haya mambo ya kushadadia vitu hivi ndiyo
hutupumbaza zaidi na kushindwa kuona na kufikiri hali husika katika mazingira
yako, mila na desturi na utamaduni kwa ujumla unakichukuliaje kitu au kitendo
hicho. Tunahitaji kutumia busara katika kuona mambo haya na kuamua, ili kuweza
kupunguza wimbi lililopo katika maisha ya sasa.
Angalia namna ya uvaaji siku hizi pande
zote, je! Unaendana na uvaaji wa maisha ya zamani? Maandiko Matakatifu
yametupatia majibu sahihi ya namna anavyopaswa kuvaa mwanamke, ambayo ndiyo
namna nzuri na adilifu. “Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa
mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka
nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani.”(1Tim 2:9).
Jiulize kweli wanawake wa sasa wanavaa nguo za kujisitiri? Asilimia kubwa ndiyo
wanaokiuka hiyo: huvaa nguo fupi, za kubana na zenye kuwekewa mipasuo mirefu ya
nyuma na mbele. Pia ndiyo mpango mzima sasa kwamba mwanamke nywele, kila leo
mpaka fujo katika familia lazima kwende saloon kusukwa; huko ni kupoteza muda
tu kwa kwenda kusikiliza na kusimulia mambo ya watu wengine (kusengenya) hiyo
ndiyo hulika ya Wamama. Kadhalika, siku hizi mwanamke huyo huyo ndiye yuko
tayari kulala njaa ilimradi aonekane amevaa nguo za thamani kubwa.
Tukienda mbali zaidi tumefikia hata
hatua ya kuvaa nguo zisizo za sifa zetu. Naliongea hili kwa masikitiko makubwa
sana, kwani uvaaji wa nguo zetu unaendana na maumbile yetu katika namna ile
tulivyoumbwa. Kwa mfano uliowazi kabisa, akina Mama, Dada na Mabinti katika
ujumla wake jinsia ‘Ke’; tunawaona wanavaa suruali. Suruali hizo kimaumbile tu
zipo kwa ajili ya jinsia ‘Me’. Kumbe tujiepushe na mavazi yasiyotuhusu, zaidi
tujikite katika mavazi ya hulka zetu kulingana na jinsia zetu na namna ya
maumbile yetu yanavyoturuhusu. “Mwanamke asivae mavazi yampasayo mwanamume,
wala mwanamume asivae mavazi ya mwanamke; kwa maana kila afanyaye mambo hayo ni
machukizo kwa Bwana, Mungu wako.”[53]
Kadhalika mwanamke anaambiwa kuwa hana
ruhusa ya kumtawala mwanaume, je! ni wanawake wangapi wanatekeleza agizo hilo?
(rej.
1Tim 2:11-12). Siku hizi tunawaona akinamama wanaopiga waume zao, pia
tunasikia wanawake hao hao wakitafuta haki sawa kwa wote. Lakini wamesahau ya
kuwa hata Maandiko Matakatifu yaliweka bayana hata shughuli zimpasazo mwanamme
pia mwanamke, kama kweli ni haki sawa kwanini ziliwekwa bayana kwa kutengwa kwa
kila mmoja? (rej. Mwa 3:16-19; 1Tim 2:11-14). Kwa hiyo kuna vitu vingine
tunaanza kuvipigia tu kampeni aidha baada ya kusikia kwa watu wengine hususani
kutoka mataifa yaliyoendelea na kuviweka kwetu, pasipo kutambua asili yake iko
wapi.
Upande wa wanaume, namna ya uvaaji
imeshabadilika tena. Uvaaji wa suruali za kubana, uvaaji wa milegezo (yaani kata
‘k’) na unyoaji wa mitindo ya kigeni. Katika waafrika tulikuwa na namna
zinazofanana kiutamaduni tangu zamani, lakini sasa tamaduni hizo hatuna tena
sasa zimetoweka. Unyoaji wa nywele ulikuwa ukitumia zaidi nyenzo tata, yaani
mikasi ambapo kichwa kiliwezeshwa kunyolewa katika ustandadi wa kipimo kimoja
(kiwango kimoja). Lakini sasa baada ya upatikanaji wa nyenzo rahisi sana mtu
anaweza kunyoa awezavyo, ndiyo maana utaona mara mtu amenyoa kiduku. Sasa kwa nini
kiduku ambacho hakikuwepo tangu zamani? Utaambiwa alimwona mchezaji wa timu fulani
amenyoa hivyo naye akavutiwa kunyoa hivyo. Kumbe kinachoendelea na kutusumbua
sana ni suala la ushadadiaji (ushabiki usio na maana) wa vitu pasipo kujua
umaana wake.
Siku hizi kitu kinachotumaliza ni uvivu
ambayo ni moja ya mzizi wa dhambi. Watu tumekuwa wazembe sana wa kutotaka
kujishughulisha na ufanyaji kazi. Mtakatifu Paulo anasema na asiyefanya kazi na
asile (rej. 2 The 3:10). Sasa ile roho ya mtu
kutaka vitu vya mtelemko ndiyo imekuwa sana, na kusababisha au kuwa chanzo cha
matatizo mengi sana ya sasa.
Tunajikuta tunajiingiza katika hali ya maisha
bila msalaba. Kuna mwanafalsafa mmoja anaitwa Plato, alisema “Uhai
usiofaa haukustahili kuishi” (Unexamined life is not worthy living). Vivyo
hivyo mpiganaji maarufu Bruce Lee alisema “Usiombe kuwa na maisha rahisi, bali
omba nguvu za kukabili maisha magumu.”[54]
Matokeo
ya kupenda vitu rahisi.
v Ongezeko
la maovu, mfano: wizi,
ujambazi na kadhalika. Kwa sababu mtu hataki tena kufanya kazi ila bado
anatamaa ya kuishi, atafanya awezalo kuhakikisha walau anapata mkate wake wa
kila siku. Sasa katika utafutaji wake kwa kuwa ni mtu ambaye hapendi kazi,
anapenda vitu rahisi tu anaweza kutumia hata njia ya kuiba ilimradi tu aokoe
uhai wake. Kumbe wizi huo ni kwa sababu hapendi kujishughulisha, ambayo ni
matokeo hasi yasababishwayo pengine na walezi katika kipindi cha makuzi yake.
Ni mtoto amezaliwa anakuta kila kitu kipo, wazazi wanamwambia wala usifanye
kazi yoyote mwanetu wewe tulia tu kula bata. Sasa waliokuwa wakimtia kiburi cha
kutofanya kazi wanapotoweka na kila kitu, hapo ndipo mtu anaanza kutaabika na
kushindwa kuona afanyeje; mwisho wa siku anaona kuiba itakuwa rahisi maana
kushika jembe hawezi wala kufanya kazi yoyote ile itakayomfaa.
v Mimba
za kabla ya ndoa, Mfano:
mimba katika hali ya uanafunzi au mimba za utotoni; huchangiwa zaidi na
upokeaji wa zawadi mbalimbali kwa mwanafunzi, ambapo muda fulani anapata fursa
ya kumbana ili amlipe vyake na kwa kuwa hana uwezo huo wa kurudisha basi namna
iliyowazi kwake anaona bora atoe utu wake.
Haya tunayashuhudia
zaidi katika shule zetu za sekondari, ambapo unakuta ni binti anasoma umbali
ambao japo siyo mrefu ila kwa sababu ya kujidekeza anaamua kupanda aidha
bodaboda au tax kuweza kumfikisha shule. Kwa kuwa familia zetu tunazijua ni
masikini, hivyo hawawezi kuhimili gharama za kila siku na binti kwa kuwa
amezoea hivyo kusema hata atembee hawezi; anafanya kila mbinu ilimradi aendelee
kufika shule kirahisi na kujikuta tayari yuko kwenye mkataba na dreva tax au
bodaboda sasa. Kadiri mazoea yanavyozidi, wanaamua kujihararishia ndoa mwisho
wa siku utashangaa binti tayari ni mjamzito. Lakini nasi vijana tunaojiingiza
katika wimbi hilo la mapenzi kabla ya muda wetu, tafadhali naomba tutambue kuwa
tendo la ndoa ni marupurupu ya wanandoa tu.
v Mimba za Utotoni
Kwa
mujibu wa Mafrt. BONAVENTURA MAHEHELA na BENEDICT KAGWA mwaka 2015 juu ya mimba
za utotoni, wanaanza kwa kujiuliza swali msingi hili; Nini maana ya mimba za utotoni? Mimba za utotoni ni zile
zinazo tungwa kabla ya umri unaomruhusu msichana kupata mimba kwa kuwa anaelewa
wajibu huo wa mzazi. Kwa hali ya kawaida, mwanamke anayeeleweka kupata uja
uzito ni yule aliyefikia umri wa kuwa mtu mwenye kuweza kubeba majukumu ya mama
wa familia. Sio kupata mimba msichana angali mtoto yaani anakuwa ‘mtoto mwenye mtoto!’
Sababu za mimba za utotoni.
Sababu
nyingi zinazoweza kutajwa katika jambo hili ni za ukurupushaji wa maadili ya
Kanisa na yaliyo mema kwenye jamii. Nyingine zinatokana na utukutu au
kudanganyana kati ya vijana wenyewe. Wengine wameingia kwenye matatizo ya
kutaka kujaribu kila kitu maishani. Kuyakimbilia mambo bila kujua nini
wanakikimbilia.
· Maisha magumu (hali
ya uchumi kwa baadhi ya familia).
Wasichana
wakati mwingine hujiingiza katika mahusiano ya kimapenzi wakiwa watoto wadogo.
Hii ni kwa sababu ya kutaka kutimiza mahitaji yao, kwani familia zilizo nyingi
zinakuwa na uwezo mdogo wa kutimiza mahitaji ya msichana, hivyo binti anaamua
kujiingiza kwenye ngono akiwa mtoto mdogo na matokeo yake ndiyo ndoa za
utotoni.
· Elimu kwa watoto wote
Katika
kipengee hiki tulitazame suala hili kwa namna mbili; kwanza kabisa; katika Familia.
Familia zilizo nyingi hazipati muda mzuri wa kukaa na watoto wao kwa ajili ya
kuwaelimisha mambo ya duniani hapa. Familia hazina muda wa kuwaelimisha watoto
wao kwamba mtoto kujiingiza kwenye mahusiano akiwa mdogo ni kosa kubwa sana.
Kukosekana kwa fundisho hili kumepelekea watoto walio wengi wanajiongoza
wenyewe tu. Tukijaribu kulinganisa watoto wa sasa na kipindi cha nyuma ni
tofauti, maana kipindi cha nyuma vijana walikuwa pia wakipata elimu kupitia
JANDO na UNYAGO.
Pili, Shule.
Shule pia kwa namna nyingine zinachangia kusababisha mimba za utotoni kutokana
na ufundishaji wa mfumo wa uzazi hasa shule za msingi. Kuna mafundisho mengine
kwa asili yake, yanavunja ukuta wa malezi bora, yanabomoa nguzo ya malezi bora
kwa vijana. Mathalani mtoto mdogo anafundishwa juu ya matumizi ya Kondomu,
uzazi wa mpango kwa njia ya vidhibiti mimba kama vile vipandikizi nk. Anapo
yapata haya, tukumbuke kuwa haya pati kwa nguvu ile ile yale yaliyo ya kinyume
chake yaani yenye kuonesha athari zake (hususana mafundisho ya Kanisa).
· Mitandao (utandawazi)
Mitandao
ni chanzo kikubwa kabisa cha kusababisha mimba
za utotoni kwa watoto wengi kwa sasa. Hii ina jidhihirisha hasa
tunapoona watoto wadogo wanaingia kwenye internet
na kupakua picha za uchi na kuangalia. Hii inawapelekea kuwaka tamaa na kutaka
kufanya au kujaribu na kuwasababisha kupata mimba zitokanazo na udadisi wao juu
ya mambo wayaonayo mtandaoni.
· Kupuuzia mila zetu na kufuata za kigeni
(kugenishwa)
Tufikapo
mahali tukayaona yakwetu kuwa ni mavi na
ya wengine kuwa ni dhahabu hapo tujue
kuwa tunauvua kwa kuusaliti utu wetu kama Watanzania na wenye tunu zao msingi
na kunadi za mataifa mengine. Na ukweli unaonesha kuwa nyingi kati ya hizi
tunazokopa kwingine ni za hovyo. Hii nayo inajidhihirisha hasa kwa watoto wa
kike. Tukilinganisha kwa sasa na zamani tunagundua kabisa kuna upuuzaji wa
tamaduni na mila zetu, maana watoto au wasichana wanakaa na kuvaa sketi tupu
tofauti na mila zetu. Na hii inasababisha tamaa kwa wanaume walio wengi.
·
Utamu wa dhambi
Sifa mojawapo ya dhambi ni hii ya kuwa
tamu. Dhambi yoyote ile iko kama dawa kali ambayo imewekwa juu yake vitu vitamu
(sweet coating) ili kuleta utamu kwa mmezaji lakini ndani yake kuna
uchungu. Kumbe na dhambi inaonekana kuvutia, inaonekana kubeba utamu kwa juu
lakini ukishaitenda kama dhamiri iko hai, utaonja machungu ya dhambi. Kabla ya
kutenda mawazo yote huleta uzuri wa jambo lakini mara baada ya kulitenda
unaingia kitu kiitwacho ‘majuto.’ Na majuto siku zote ni mjukuu, yaani huja
baada ya tendo baya. Kwahiyo, vijana wengi wamekuwa wahanga wa jambo hili maana
waliona utamu wa mahusiano, wakahusiana kweli na mwisho wakapata malipo ya
mahusiano yao (ujauzito kwa msichana kabla ya ndoa)! Utamu huu wa dhambi,
umepelekea wengine kubobea katika tamaa za uzinzi, ukishabobea namna hiyo
mwendo mdundo ni kutenda dhambi hii na huyu, kesho na yule. Hapo dhambi inazaa
dhambi (sin begets sin) na inapata mpaka wajukuu ambao majina yao
ni ‘dhambi!’
·
Kukaidi na kuvunja Amri za Mungu
Vijana kama tunamwogopa Mungu na kumpa
heshima yake stahiki, tutamsikiliza asemapo ‘acha hili, tena hili, litende
hivi.’ Katika amri VI ya Mungu tumekatazwa kuzini (Kut. 20:14). Kwenda kinyume
na hiyo amri ndipo wenzetu (vijana) wameishia (vijana) kupata ujauzito kabla ya
wakati (ndoa). Kijana ukishindwa kuitii amri ya Mungu utafanya kila aina ya
uovu maana huna uoga na utii kwa Mungu, na hapo hutafaidika na lolote ulitendalo
zaidi ya kupata athari za ukaidi.
·
Kupenda kujaribu jaribu kila mambo/ kitu (negative
curiosity)
Kujua jambo au mambo si kosa kosa ni
kujua hata kabla ya muda mwafaka wa kuyajua baadhi ya mambo. Mtoto mchanga
akizaliwa anajua mambo pole pole tena kwa kiwango cha umuhimu wake. Cha kwanza
kabisa ni kujua chakula chake kiko wapi (kifuani mwa mama wake), jambo la pili
ni namna ya kukila chakula hicho. Sasa kwa mfano wa mtoto mchanga huo, nasi
vijana tuweni na shauku nzuri ya kujua mambo na vitu. Ukiwa mwanafunzi, jua
yamhusuyo mwanafunzi barabara na mengine yanayokujenga ungali mwanafunzi. Cha
ajabu na cha kusikitisha ni pale mwanafunzi tunayomwona kwa nje amevalia sare
safi na daftari mkononi kumbe hapo alipo anajua mambo ya ngono, mambo ya
mapenzi kuliko hata walio kwenye kitengo hicho (wana ndoa). Kwanini tusiwe na
kauli hii moja ya kuwa ‘ya Ngoswe mwachie Ngoswe.’ Kujaribu jaribu huko
wengine wamejaribu kufanya mapenzi na matunda yake ni mimba kabla ya ndoa.
Jambo hili kwangu ni ‘missing the target!’ usijaribu ukali wa sumu kwa
kuilamba kijana mwenzangu. Siyo lazima ufanye mapenzi kabla ya kuoa ili uje uoe
bila shida yoyote. Utunze mwili wako kwaajili ya aliyeandaliwa kwako na Mungu.
Fikiria raha na furaha utakayoikuta kwa mwanamwali bikira aliyejitunza kama
zawadi kwako, naye je, atafurahije akigundua yeye amekuwa wa kwanza kwako?
·
Ushawishi wa marafiki (mob/company)
Kuna ukweli kwamba kuna watu kama
bendera, ‘hufuata upepo.’ Na wengine ni kama toroli, ‘lazima
wasukumwe na wengine.’ Na wengine ni kama maji, ‘lazima wafuate mkondo.’
Haya siyo maisha vijana wenzangu, tusimameni wenyewe wakati mwingine. Usione
fulani anafanya kitu fulani nawe bila kufikiria ukaenda kukifanya huko nyumbani
ndiyo maana kwenye mieleka utakumbushwa ‘stay safe, don’t try this at home.’
Usifuatane na kikundi cha wazinzi, watakuambukiza uzinzi. Usifuatene na kampani
ya watongozaji wanaojiona wao kuwa jogoo wa kila mtetea, utalazimika kuwa jogoo
moja wapo la kutongoza mtetea. Usiwe katika kundi la wanaopenda tu kusikia ‘SSSSSSS’
miluzi ya wavulana ndipo wanafurahi. Hawa mimi nawaita jamvi la kila mgeni.
Ukikaa nao utaishia kuwa jamvi la mgeni fulani. Tusiwe na roho ya kujaribu kila
kitu mengine tuseme ‘hili jambo hata siliwezi, na hili hata kama naweza
kulifanya, silifanyi.’
·
Kuogopa kuuziwa mbuzi kwenye gunia
Huu nao ni ukweli ambao nisipousema
sitakuwa huru kamwe. Kuna vijana nilishaongea nao kuhusu masuala ya kufanya
mapenzi kabla ya kuoa/kuolewa, walinieleza wazi kuwa ‘leo hii hakuna msichana
mkweli, wala hakuna mvulana mkweli, kumbe kuwa salama na unayetaka kumwoa au
kuwa na uhakika kwamba mambo ya ndoa unayaweza, kipimo ni kufanya mapenzi
kadiri uwezavyo.’ Kweli inasikitisha! Na hapa kama mpo, mnanisikitisha sana,
lakini kwa kuwa siwadhanii hivyo ngoja nisonge mbele nikiwatumia ninyi kama
mabalozi wangu huko mwendako. Wengine wanaenda mbali zaidi na kudai hata kupata
mtoto kwanza ili wajue kama wakioana wanaweza kupata watoto au la! Ukiyaweka
pamoja masuala haya, utafika kituo cha mwisho ukute vijana wengi sana leo
wameingia kwenye uwanja huo wa walioharibikiwa!
·
Utandawazi
na athari zake hasi
Mambo yamerahisishwa sana na
utandawazi. Lakini pia yameharibiwa sana kwao huo utandawazi. Ambayo
hayakuwezekana zamani, leo yanawezekana. Mazuri kwa mabaya yote yanawezekana
leo kwa hii sayansi na teknolojia. Hapo hata mengine kati ya tuliyoyaona hapo
juu yamepata kichocheo (catalyst) chake mfano ‘negative curiosity, mob, and
bad company.’ Kuna msemo huu kwamba ‘google tu utaipata mubashara, usije
ukaaibika siku ya mechi kwa kuonekana huyajui mambo, google tu ujinoe, usije
ukazidiwa ndani ya dakika 5 za mchezo kwa kutokuzijua njia, namna, google tu
ungali kwenye zoezi ili kwenye mechi uoneshe umahiri na hutoachwa kamwe.’
Vijana wamegoogle na hakuna walichobakiza nyuma. Wamejua mambo na mambo
yamewajua, wamejuana kwa maneno mengine. Ngono za kwenye simu, zimewaandaa kwa
ngono mubashara siku watakapoonana. Takataka zote password yake iko kwa google.
Google huyu hana huruma, amewaacha wasichana wengi wajawazito na wengine hata
leo hii wanalia kilio kikuu. Sisi nasi twataka kujiunga nao?! Angalia sana
kijana ‘unagoogle nini?’
·
Kudanganyika
na kutaka kuudhihirisha upendo kwa ngono
‘Kama kweli unanipenda…’
Kinachomaliziwa hapo, ni sadaka ya mwili wako kwa mwenzako. Eti, ndugu vijana
wenzangu, mimi kukupenda wewe dada mpaka tulidhihirishe hilo kwa mapenzi? Wewe
kumpenda kijana wa kiume/kike mpaka mfanye mapenzi ndipo ijulikane kuwa
mnapendana? Kipimo cha upendo ni kupenda bila kipimo. Kupenda bila kikomo. Na
Mt. Mama Tereza wa Kalkuta anasema kipimo hicho ni kutokuwahukumu watu. Anasema
‘ukiwahukumu watu, huna muda wa kuwapenda.’ Vile vile anasema ‘penda
mpaka uumie.’ Hajasema fanya mapenzi na umpendaye na hapo mtajua
mnapendana. Kama kweli unampenda, utauheshimu utu wake, utaiheshimu na
kuithamini kesho yake. Hutamchezea. Vijana msihadaike, hakuna upendo wa kweli
kwa rushwa ya ngono. Huko kuna wengi waliofanya hivyo na wakaishia kupata uja
uzito kabla ya ndoa. Je, walioana? Upendo wao je, uliendelea? Baada ya kuzini
huja majonzi, huzuni, masikitiko. Msidanganyike mkaishia kubeba mikono vichwani
mwenu. Mtu akikupenda na akadai uhusiano wa ngono ili kudhihirisha pendo lenu,
huyo hakupendi anapenda tendo la ngono juu ya mwili wako yaani amekushusha
mpaka kwenye hatua ya kuthamanishwa na ngono, bila hiyo wewe si kitu! Hii ni
mbaya sana. Upendo wa kweli hauko hivyo. ‘PENDANENI KAMA VILE MIMI NILIVYO
WAPENDA NINYI.’ Ni ujumbe wa Kristo tunayejiandaa kushuhudia ufufuko na ushindi
wake. Wengine ni waongo, walaghai tu, madebe matupu tu ambayo hayaachi kutika.
·
Mmonyoko
wa maadili
Hapo kale iliaminika kuwa msichana
mwenye heshima alikuwa yule ambaye hakumjua mume mpaka alipoolewa. Ndiyo maana
hata mama wetu Bikira Maria alipoambiwa atachukua mimba na kumzaa mtoto,
alistaajabu na hata kumwuliza mjumbe wa Mungu “Itawezekanaje maana mimi simjui
mume” (rej. Lk. 1:34)? Leo ndugu mkubali au mkatae, mgune au mnong’one,
kuna hata wazazi wanao wahimiza watoto wao wakike na wakiume kuwa na
maboyfriend na magirlfriend ili siku ya siku wasiwaaibishe. Wengine mpaka
wanawatafutia watoto wao marafiki wa kimapenzi eti wanasema ‘ni bora awe naye
mmoja wanayeaminiana kuliko awe na kijiji cha wapenzi.’ Kuna kaya nyingine
msichana akitembelewa na rafiki wake wa kiume, mama kama alikuwepo anawaaga
kabisa ‘kuweni huru tu watoto wangu, mimi natoka kidogo, kijana wangu jisikie
nyumbani baba eee! Wangine huwaasa binti zao kufanya hima wasiwaangushe wazazi
wao, yaani wafanye kitu cha ukweli.’ Katika mazingira hayo, maadili yetu yako
wapi? Mama anarudi nyumbani anauliza ‘ehee Neema niambie mwanangu mkwilima
wangu vitu, jogoo anawika mjini?’
Hapo tumezibiip mimba za ujanani kabla
ya ndoa, na tusitegemee muujiza, lazima vema iwepo tu (mimba itiki) kama siyo
kwenye tendo la kwanza basi moja wapo kati ya mtakayofanya. Watoto
wataambulisha wapenzi wao bila wasi wasi kabisa eti uhuru wa kuhusiana! Ujinga
uliogubikwa na giza totoro siku zote utalenga katika matendo kama hayo. Malezi
mabaya katika ngazi ya familia, shuleni, na kwenye taasisi mbali mbali
yatafungua njia kwa vijana wetu kuogelea katika uhuru wa kimapenzi. Vijana
mtateketea huku mnaona. Mimba zitazidi kuwa nyingi kila kukicha. Mila potofu
katika familia, mitaa, vijiji vyetu nazo haziko mbali katika kubomoa mahusiano
kwa vijana wenzetu. Siku hizi watu hawahangaiki na malezi ya mtoto wa jirani
kama ilivyokuwa kale kwamba ‘mtoto wa familia fulani alikuwa mtoto wa jamii.’
Leo mtoto wa familia ni mtoto wa baba na mama wake walio mzaa! Kweli vijana
kama nanyi mna mwono huo, mnawadharau walezi, wakubwa wenu nje na wazazi wenu
wa kibiolojia, mmepotoea na karibu mnaishia kabisa. SWALI: KAMA MISINGI
IMBEBOMOLEWA, MWENYE HAKI ATAFANYA NINI? (Zab. 11:3). Nimetambua kuwa
NILIKOSEA, NIMEKOSEA, sasa naamua SITAKOSEA TENA maana…
·
Ubakaji na ubakwaji
Huyu mnyama aitwaye ‘ubakaji’ naye ni
miongoni mwa wanaochangia mimba za kabla ya ndoa. Yeye hajui cha malengo na
ndoto za kijana. Ni tinga tinga, bomoa bomoa la ndoto na malengo ya vijana. Na
zaidi ya hayo linaweza kumkumba hata mama mkubwa tu. Kuna mimba nyingi tu
vijana wenzangu zitokanazo na matatizo ya wanaume kuwabaka wanawake au
wasichana. Tendo hili ni la kinyama. Ni dhidi ya utu, ubinadamu. Ewe kijana
unaye nisikia hapa leo, nakuomba na nina kusihi sana, usiwe miongoni mwa
wabakaji. Hao ni wauaji wa dada/mama wetu. Kubaka kumeacha matatizo mengi sana
ya kisaikolojia, kimwili, na kiafya. Kimaisha kwa ujumla kuna vilio vingi vya
wenzetu waliobakwa na hali zao kimaisha leo ni mbaya sana hata wale ambao hali
zao ni nzuri wakikumbuka tu ‘lakini nilishabakwa mimi,’ wanaumia sana.
Tendo hilo linaamsha mateso yote waliyoteswa na kuteseka kwayo tangu siku ya
kubakwa. Wengine walijiua! Wengine waliua watoto wao tumboni! Wengine
walijifungua kisha wakawatupa wachanga wao! Yote haya chanzo ni wavulana, ni
wanaume. Leo, vijana wakiume mnaamua nini mkishalisikia jambo hili? Wasichana
mnasemaje kuhusu kaka/baba wafanyao hili? KAULI MBIU YETU…
v Mhusika/ Wahusika
· Wasichana
wenyewe
· Wavulana
walaghai
· Akina
mama wenye malezi mabaya (walezi bora liende)
· Akina
baba ndumila kuwili (fataki)
· Jamii
kulifumbia macho
· Serikali
kukaa kimya au kutokufuatilia kwa nguvu zake zote kesi za namna hii za kuwapa
mimba binti wa shule au binti wadogo
· Wakati
mwingine hata walimu mashuleni huwa chanzo (kuna walimu wana wapenda na
kuwataka kimapenzi wanafunzi wao-mchungaji anakula kondoo wake mwenyewe)!
v Athari/ hasara za mimba kabla ya wakati
(Ndoa)
Katika ukurasa huu, lengo letu siyo tu
kutoa hofu kwa vijana wenzetu ila ni kutaka kuonesha kuwa jambo hili
halikubaliki, ni hatari, linaleta maafa makubwa kwa mtu mmoja (mhusika), kwetu
vijana wenzake na jamii kwa ujumla. Tukisha yaeleza madhara/athari za mimba za
kabla ya ndoa, ni imani na mategemeo yetu kuwa HAKUNA KIJANA KATI YETU HAPA NA
HATA TUTAKAO KUTANA NAO NA KUWASHIRIKISHA HAYA, ATAKAYEPATA MIMBA KABLA YA
NDOA. Lakini hatuachi mwanya wa kutumia kila njia kuliepa hilo ati kwakuwa
tumekubaliana hakuna mmoja wetu atafanya hivyo, sasa aje apatikane mmoja au
wawili halafu kwa kutuogopa sisi vijana wenzao wa kongamano hili aishie KUTOA
MIMBA ili tusimwone. Ndugu, kumbuka kuna anayekuona kila siku “MUNGU PEKE YAKE”
na hata hivyo ana uwezo wakutuonesha yaliyofichika. Athari hizo ni nyingi, sisi
leo tunakupeni hizi chache na nzito:-
¨
Kuwa
mhanga wa dhambi (ulizini ndipo ukapata ujauzito)
Matunda ya uzinzi siyo matamu hata
kidogo. Kila tunda la uzinzi ni angamizo kwa ustawi wa maisha ya mtu. Mimba
kabla ya ndoa ni tunda moja wapo. Wasichana wengi waliojikita katiaka uzinzi,
wameishia kuvuna humo uharibifu. Magonjwa na kuharibikiwa kimaisha ni kati ya
matokeo. Na mimba kabla ya ndoa inatokana na uzinzi lakini yenyewe ni halali
yaani huyo mtoto siyo haramu. Uzinzi kwanza (dhambi) kisha mimba (matokeo).
¨
Kuathirika
kisaikolojia
Mwathirika wa mimba kabla ya ndoa
anapatwa na msongo wa mawazo stress. Kila akifikiria anaona kuwa mambo
hayaendi na chimbuko analiona katika tendo la kupata mimba. Hata akishindwa
jambo fulani yeye fikra zake anazielekeza kwenye huo ujauzito tu. Kisingizio
‘isingekuwa hii mimba, ningefanikisha jambo hili, asingekuwa yule mvulana/baba,
ningeweza kuvuka janga hili.’ Mawazo hayo na mengine mengi, hufanyika kwake
wimbo wa kila siku na kila mahali. Hata ndoto zake za mchana na usiku
huathiriwa na jambo hilo. Anakuwa na tabia ya kuhama hama kimawazo, katika
fikra na hata kwenye maneno na utendaji wake. Ama kweli mimba kabla ya ndoa, ni
ajira yenye matatizo mengi!
¨
Kuwa
mama mtoto (mtoto mama/mama ambaye bado ni mtoto)
Hapa tunamwona mhanga yaani binti mdogo
ambaye amebeba hadhi ya kuwa mama mtoto. Lakini umri wake unamweka kwenye kundi
la watoto bado, au tuseme msichana bado wa kuwa shuleni kwa mwendo wa kawaida
wa maisha. Yeye ni mtoto bado, lakini ana mtoto wa kuzaa yeye siyo mtoto wa
dada au mama wake. Ni mtoto mwenye mtoto wa kuzaa! Anahitaji malezi ya wazazi
wakati huo huo na yeye anapaswa kulea kichanga chake. Hapo ndipo wengine
huchanganyikiwa kabisa. Hebu fikiria, unamkuta binti ana mtoto mdogo
aliyembeba na analia kweli kweli pale ushindwapo kuvumilia na kwa huruma
unamwambia ‘wewe binti, mpeleke mtoto kwa mama wake akanyonye. Kumbe binti
huyo ndiye mama, atajisikiaje? Nawe je, ukigundua kuwa yeye ndiye mama mwenye
mtoto, utajionaje? Hili ni tatizo. Mtoto kuwa mzazi, kimawazo bado hajafikia
kutatua shida za wazazi, ki uchumi hajajikwamua bado, kijamii pia anaonekana
kuwa kioja. Huku ni kuingia kwenye majukumu mazito na yasiyo saizi ya mbebaji maana
siyo muda wake. Kweli yasiyo yetu yakiwa yetu mengine huumiza sana.
¨
Kutengwa
na familia, ndugu, jamaa na marafiki
Athari hii imejikita kwenye ukweli
kwamba, wale wasio pendezwa na tabia chafu namna hiyo, wengine wao hawana
mshipa wa uvumilivu. Wakiwa ni wazazi, wanaweza kumfukuza nyumbani binti wao.
Wakiwa ndugu, jamaa na marafiki wanaweza kumtenga na kumwacha ajijue mwenyewe.
Yaani wanachukizwa na tendo lenyewe pamoja na mtu mwenyewe. Kauli chafu zote
huelekezwa kwa binti huyu, ‘tuondolee hapa tumbo lako hilo kama mtu mwenye
utapia mlo, loo! Mwanamke kitambi bibieee, peleka huko kitambi chako, wewe si
kampani yetu, usitufuate fuate kama nzi best usije ukatutia aibu tukaoneka kama
wote wazinzi jinsi ulivyo wewe.’ Hayo na mengine mengi, huwasibu vijana wenzetu.
Ewe binti uko tayari kwa hayo? Wewe kijana wa kiume, kuwa mstari wa mbele
kusema ‘hutakuwa miongoni mwa walaghai.’
¨
Kuachwa
na aliyekupatia ujauzito
Nje na kutengwa na familia, ndugu,
jamaa na marafiki, kuna adha hii moja kwamba, kwa wale wanaodanganyana kwamba ‘mimi
nitakuoa, nizalie mtoto nitamtunza na wewe pia,’ mambo yanapozua mambo
(ujauzito ukiingia bila hodi-kabla ya ndoa) kuna kugeukiana na kuonana kama
mmoja ni shetani wa mwenzake hasa mvulana au mwanamume. Fikirieni kuwa wote
mnasoma halafu mmepata ujauzito, nani yuko tayari kusema ‘tuache shule tukalee
mtoto wetu.’ Ni mvulana yupi atakuwa tayari kuukubali ujauzito huo kuwa ni
wake? Wengi kama siyo wote wana kataa na hapo binti anabaki mbeba lawama zote
kana kwamba alijipatia huo ujauzito yeye peke yake. Wengi wakifika hapo, hukata
tamaa na hata kuchukua maamuzi mabaya yaliyo kinyume.
¨
Kukosa
nafasi katika masomo na kazini pia
Kuna wasichana wengi walipoteza nafasi
zao za masomo kwa kuwa wajawazito wangali shuleni. Wengine walifukuzwa shule.
Wengine wazazi wao walikataa kata kata kuwaendeleza kielimu katika ngazi au
hatua yoyote. Leo Serikali inapambana kuwapa nafasi tena wasichana kama hao.
Sijui faida yake na umuhimu wake maana naogopa isije ikawa kwa upande mwingine
wanaacha mwanya kwa vijana kufanya tu mapenzi maana shule ipo tu hata kwa waja
wazito. Na wenye watoto. Wengine walimwaga unga maafisini kwa kuwa na ujauzito.
Zote hizi ni athari hasi. Na hilo linapotokea
kuteketea kwa ndoto za kijana za maishani huwa ni pai (yaani lazima iwe
hivyo).
¨
Kubaki
nyuma kimaendeleo
Maendeleo yoyote yana viashiria vya
kijitambua na kufanya yaliyo sahihi. Vile vile yana viashiria vya muda
uliotumika vema. Kwahiyo, katika masuala ya mimba kabla ya ndoa, hatuwezi
kuubeza ukweli kwamba wahusika walishindwa kujitambua wao ni akina nani (mfano,
kijana ambaye hajaolewa nk), walishindwa kujua wako wapi (mathalani shuleni
nk), walishindwa kutambua kuwa muda wao kwa wakati huo ulikuwa rasmi kwa kuishi
maisha ya wale ambao hawajaolewa ‘kutokujihusisha na mapenzi nk.’ Kwa hiyo
hawakuutumia muda wao kwa mambo msingi. Mioyo yao ilisukuma vingine siyo
damu kama asemavyo MSANII LAMECK DITTO. Akili yao ilipata ajira kwa yasiyo
msingi. Miili yao ilitumika kama pango la mapenzi. Katika hali kama hiyo,
usitegemee maendeleo ya maana. Utabaki nyuma tu kama kitako cha bunduk, nyuma
tu kama kisogo, nyuma tu kama mgongo. Utabaki kuusingizia ujauzito kwa kila
anguko lako. Kweli ‘mbaazi ikikauka husingizia jua!’
¨
Kuingia
kwenye maamuzi mabaya kwa mwenye mimba
Mambo yote yanaweza kuwa kenda, na kumi
ni kufanya maamuzi mabaya. Ubaya wa maamuzi haya ni kwanza kwa mtu binafsi, au
kwa aliyempatia ujauzito, waliomdanganya, aliyetumboni mwake (mtoto), anaweza
hata kuichukia jamii kwa sababu zake binafsi na kuona kuwa haikutimiza wajibu
wake katika kuwafunza vijana maadili. Mbaya zaidi, anaweza kumlaani hata Muumba
wake. Chukulia mfano Mzaburi anasema “Kinacho niuma zaidi ni kwamba Mungu hana
nguvu tena” (Zab. 77:10). Haya yaweza kuwa mawazo ya binti aliye katika
hali hiyo. Sasa naomba niyaainishe hapa bila kusema chochote maana
yanajitoshereza:-
ü Kujinyanyapaa mwenyewe (I have no
any shadow of value)
ü Kukata tamaa na maisha (Nothing is
possible any more for me)
ü Kutoa mimba/kuua (This is the only
solution I can opt for)
ü Kutupa watoto waliozaliwa (To hell
with it)
ü Kujinyonga/kujiua (It’s better I
take a long and deep rest)
ü Kuwachukia wanaume wote na hata
kutokuwa tayari kabisa kuolewa maishani (Single life is my vocation in
life/I don’t want troubles)
v Suluhisho/ Mwarobaini
Nani sasa Amfunge Paka Kengele?
MIMI, WEWE, HATA NA YULE…
Tumekwishaona maana ya mimba kabla ya
wakati (ndoa), chanzo chake, sasa tuangalie namna ya kumfunga paka kengele ili
kila asogeapo, tujue kuwa yuaja adui yetu vijana, adui wa ndoto zetu na adui wa
uhusiano wetu na Muumba wetu. Njia moja kubwa sana yakusuluhisha tatizo hili ni
kuepa na kukaa mbali kabisa na sababu zinazopelekea vijana kuwa na mimba kabla
ya wakati (ndoa). Na nyingine ni hizi tunaongezea:-
Ø Kumcha Mungu na kuwa na hofu naye
“Kumcha Mungu ni mwanzo wa hekima” (Mit.
1:7). Vijana wenzangu tukimcha Mungu, tutakuwa wana wema. Tutaishi katika
nuru ambayo ni Kristo mwenyewe (Yn. 8:12). Kumcha Mungu ni pamoja na
kuzishika amri zake na KUTOKUZINI ni moja wapo ya amri hizo. Usipozini
utaondokana na matokeo yake yote mabaya. Utakuwa kijana jasiri na mwenye SUBIRA
ivutayo heri. Anza leo. Hujachelewa. Usisubiri kesho. Kumbuka ‘ngoja ngoja
yaumiza matumbo.’
Ø Kumwomba Mungu Roho Mtakatifu akupatie
mapaji yake ili uwe na mang’amuzi sahihi (Isa. 11:2)
Mapaji ya Roho Mtakatifu ni zawadi na
silaha zetu za mapambano. Omba upewe hekima, akili, shauri, imara/nguvu,
elimu, ibada na uchaji wa Mungu. Ukiwa nayo haya utatenda yote yaliyo
mazuri na utajiepusha na yote yaliyo mabaya. Omba pia matunda ya Roho Mtakatifu
ambayo ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhila, uaminifu,
upole, na kiasi (rej. Gal. 5:22-26) yakusindikize katika kuwa
mwanadamu mwema kati ya wanadamu wengine wema na utaufanya ulimwengu uwe mwema
pia. Hii ni misaada ya ufuasi katika maisha. Ni kinga dhidi ya dhambi na yote
yaliyo mabaya.
Ø Sali daima ili Mungu akupe nguvu ya
kwanza kuepa nafasi za dhambi (Lk. 22:40) pili kuishinda dhambi kwa wema na
kuikimbia (Yak. 4:7-8)
Sala iliyosaliwa vizuri hufungua mioyo
ya wasalio na huifungua mbingu ili aishie huko aisikie maana hupaa mpaka kwake kama
moshi wa ubani (reje. Zab. 141:2). Tukimwomba Mungu katika ujana wetu,
hatatuacha tuangamie kwa mahusiano mabaya. Kwake hakuna lisilowezekana kwa
aombaye kwa imani (Lk. 1:37, 18:1). Kama huwezi kuacha uzinzi, Mungu
hajashindwa kukutoa huko mwombe tu. Kama unaona huna nguvu za kujinasua kutoka
huko, mwombe tu atakuwezesha. Tuombeni bila kukoma na hata tukipewa tuombeni
tu. Tuombeni mpaka kitu kitokee hiki ndicho kirefu cha PUSH [Pray, Until,
Something, Happens]. Kijana mwombe Mungu ili nguvu ulizo nazo zitumike
vizuri kwa malengo mazuri. Ukiomba utapewa (omba nguvu ya kuepuka au kuacha
uzinzi), ukitafuta utapata (tafuta namna ya kukaa mbali na dhambi kutoka kwa
Mungu utapata), ukibisha hodi utafunguliwa, (bisha hodi kwa neema za Mungu
uushinde uzinzi nawe utaushinda).
Ø Mtukuze Mungu katika mwili wako maana
ni Hekalu lake (1Kor. 6:19-20, 2Kor. 6:16)
Miili yetu ni mahekalu ya Roho
Mtakatifu. Tuitumieni kumwenzi Muumba wetu. Milango yetu ya fahamu itoe
ushirikiano katika kumtukuza Mungu. Tuyaone yaliyo mema, tuyasikie yaliyo mema,
tuyashike yaliyo matakatifu, tuyanene yaliyo asili ya wokovu wetu na wa
wenzetu. Tukifanya hivyo tutajiweka pembeni ili kuepusha msongamano katika
msafara wa wazinzi. Na mimba za kabla ya ndoa zitaisha kabisa kwetu na kwa
wenzetu ujumbe utawafikia maana Injili ni kuishi siyo kuhubiri tu kwenye
marufaa.
Ø Kushika mafundisho ya Kanisa
Kanisa Katoliki ni mama na mwalimu,
tukilifuata tutafikia kule ambako Mungu ametuandalia makao maana lenyewe ni
sakramenti ya watu wote wenye kuuhitaji wokovu.[55] Kanisa
linakataza kile ambacho Mungu alikataza “USIZINI.” Tulisikilezeni maana
halikosei katika kutufundisha sisi wana wa Mungu. Makatazo ya Kanisa ni
kwaajili ya wokovu wetu na wa wenzetu.
Ø Elimu bora ya mahusiano
Kanisa na dini mbalimbali zishirikiane
kuwaandaa vijana katika maisha ya uadilifu na maisha ya kimahusiano. Vijana
watajua nini wafanye wanapotaka kuingia kwenye maisha ya ndoa. Na wafanye nini
kabla ya ndoa. Serikali pia iwe na utaratibu mzuri wa kuwaandaa vijana ambao ni
taifa la kesho. Mitaala iwe rafiki katika mahusiano siyo kuwapotosha watoto na
kuwabomoa kwa mafundisho potofu kama mpango unaoendelea sasa wa kutaka kuruhusu
mpango wa uzazi na vidhibiti mimba kwa vijana wa umri miaka 10 hadi 19 na
kuendelea.[56]
Kwa rejea tusomeni (1Kor. 7:32-33). Kila mmoja wetu leo hii namwomba
sana chonde chonde, awe macho na kupinga yote yaliyo kinyume na maadili yetu
kama huu mswaada wa kuruhusu mafundisho yenye kuruhusu vijana wadogo kabisa
wafundishwe na waanze kutumia vidhibiti mimba chini ya mwavuli wa “SEXUAL
REPRODUCTIVE HEALTH AND RIGHTS-SRHR (AFYA YA UZAZI NA HAKI)." Huu ndio
mswaada wenyewe. Tukilala leo, tutaamka kesho ukiwa kazini!
Ø Semina na Warsha mbali mbali
Hizi ni nyenzo za kufundishia na
kuelimishia. Leo tunatoa semina, lengo ikiwa ni kutoa rai, kutoa dira na kutoa
mwelekeo mwema. Tuna imani kuwa haya yatachachusha donge zima la kujikomboa na
kuondokana na mahusiano mabaya kati yetu vijana. Matumaini yetu ni kwamba baada
ya semina hii, kutakuwa na kumwongokea Kristo kwa vijana wote. Amka kijana,
zinduka kijana. Vuna kitu leo kwaajili ya kesho. Tupendeni kuhudhuria semina na
warsha mbali mbali na tuwavuteni na wengine wengi wazipende semina ili
wanufaike kama ninyi kwa juma hili. Nanyi kaweni chumvi na nuru huko (Mt.
5:13-14), mashuleni, majumbani kwa kutoa semina elekezi. Mkifanya hivyo
kwanza kwa kuishi vizuri ninyi na pili kuseminisha, watu watayaona matendo yenu
mema na watamtukuza Mungu Baba wa mbinguni. Kumbukeni ‘mmepewa bure, katoeni
bure.’ Kumbukeni ‘ninyi si maskini hivyo kwamba hamna cha kutoa kwa vijana
wengine.’
Ø Jitambue
Jitambue wewe ni nani na uko wapi,
unafanya nini, kwanini, kwa wakati gani, sehemu gani, na kwa njia ipi? Kama
wewe ni mwanafunzi, zingatia masomo kwanza, “MAPENZI NA SHULE HAVIPIKIKI CHUNGU
KIMOJA” Neno la Mungu linasema “Mshike sana elimu, usimwache aende zake…”
(Mit. 4:13). Mambo mengi sana yamefikichika kwenye siri hii ya
kujitambua. Nawe itumie uvune matunda mengi katika ujana wako leo. Na utaepa na
kukwepa mimba hizo.
Ø Malezi bora nyumbani
Nyumbani ni shule ya kwanza ya malezi
na imani. Maadili na staha njema ya kila mtu yanategemewa kutoka nyumbani. Kama
ni kuharibikiwa kwa mambo ni huko na kama ni kujenga nyumba bora ya maadili ni
huko. Mahusiano mema yajengwe kwenye familia. Msingi bora wa maisha ujengwa
huko. Wazazi na kaka/dada wawe mfano wa kuigwa kwa wadogo wao. Sio jambo la
kifamilia baba kuleta kimada pale mama atokapo. Au mama kuleta kidume pale baba
atokapo. Kwa vyovyote vile hiyo ni sumu wazazi wanayoimwaga mbele ya watoto
wao. Watoto wakiulizia jibu ni ‘anti, mjomba.’ Ndiyo maana YAMOTO
WALIIMBA UKWELI KABISA JUU YA ANKO JONI. Niseme nisiseme nisieme…semaaaa.
Chondo chonde, vijana tuvuneni mema nyumbani hata kama mabaya yanaweza kuwa
mengi zaidi. Nanyi mkija kuwa wazazi hapo kesho, kuweni kioo safi.
Ø Ilishe dhamiri yako kwa mafunzo mema,
mawazo mema na matendo mema ili ikulinde katika kuenenda vema
Fuata maongozi ya roho zaidi ya yale ya
mwili (Rum. 8:8-11). Dhamiri ni mwamuzi mwenye haki akitunzwa ndani ya
mahakama safi na salama yaani ‘kupewa taarifa na malezi bora siku zote.’
Dhamiri haiweze kukukana kama utailea vizuri na kuikuza vema. Hii ni sauti ya
Mungu ndai yetu. Ni madhabahu yetu ya kutenda matendo makuu na mazuri yenye
kumpendeza Mungu na jirani. Dhamiri ndiyo itakuambia “USIFANYE HILI NI BAYA.”
Ukiisikiliza utashinda hata vishawishi vya mimba kabla ya ndoa. Ukiipinga
haitakulazimisha lakini mara baada tu ya tukio itasikika ikikuambia “UMEFANYA
NINI? UMEFANYA VIBAYA! UMETENDA DHAMBI! LAKINI NILIKUARIFU MAPEMA HUKUTAKA
KUNITII MIMI! ONA SASA!” Tupendeni kuzisikiliza dhamiri zetu. Dhamiri njema ni
usukanai wa maisha.
Ø Kuacha kuiga iga kila kitu/mambo
Kuna mambo mengi sana yanatushawishi
kuiga kutoka kwa watu, lakini tuweni na mipaka katika kuiga. Waswahili wanasema
“Ukiiga kunya kwa tembo utapasuka msamba.” Kuna vijana wengi wameharibikiwa
katika maisha na mahusiano baada ya kuona yafanywayo kwenye filamu na sehemu
nyingine. Kutoka huko wanaanza nao kufanya kama walivyoona. Hapo utakuta
kubusiana kila waonanapo, kutomasana tomasana kwenye maficho hasa wawapo peke
yao tena kwa kuibia. Matendo hayo na mengine mengi, yanawasha moto ambao fukuto
lake na joto lake linaweza kufikia kwenye hatima mbaya. Maana ndizi mbivu
ukizitomasa zinaweza kudondokea kiganjani, zikifika hapo, mdomo nao utatamani kuzitia
gegoni, na hapo kutafuna huwa ni ajira ya muda huo. Angalia sana, ‘safari moja
huanzisha nyingine.’ Kama ni nzuri itakupeleka kuzuri na kama siyo nzuri
itakupeleka kwingineko.
Ø Kuwa na subira ivutayo heri
Wahenga walisema “Haraka haraka
haina baraka, haraka haraka ya mbwa huzaa watoto vipofu.” Vumilia kama una
ndoto njema yakuwa baba/mama wa familia kesho. Ishi vema leo ili kesho uwe
mume/mke mwema na baba/mama mzuri wa familia. Subira yavuta heri. Kuwa na
saburi. Usiyakimbilie mapenzi, ukifanya hivyo utayapata na unaweza ukaovertake
kabisa. Lakini ujue ajali utakayoipata siyo ndogo kamwe, ni kifo cha mende.
Ukisubiri utafanya mambo yako kitaalam kwa muda mwafaka na kwa utakatifu wa
masuala. Subira ni fadhila, ipalilie, ijenge, ilinde ikulinde. Ukiweza kusubiri
utakuwa umepiga hatua nzuri sana katika ukombozi wako.
Ø Kuepa mahusiano ya ngono kabla ya ndoa
Epuka, jiepushe na biashara hii ya
mapenzi kabla ya ndoa. Muda wa kufanya hivyo utafika utakapo kuwa mume/mke
halali wa mwenzi wako. Kwanza mtafurahia maana mtakuwa ndani ya sakramenti. Na
sakramenti yoyote ile ina neema iliyowekwa ndani yake na Kristo. Hapo hamtakuwa
wazinzi tena bali wapendanao, wanaokula ndoa yao kwa lengo la kukamilishana na
hata kupata watoto Mungu akibariki pendo lao au akikusudia hivyo kwa sifa na
utukufu wake. Dawa ya moto ni moto, na dawa ya kuepa mimba za janani yaani
kabla ya ndoa ni kuepa mahusiano ya kimapenzi kabla ya ndoa. Inawezekana kabisa
wala usiwe na mawazo ya wachache waliokosa dira ya maisha ‘eti usipofanya
mapenzi, utaugua, utashindwa kuwa mchangamfu, utakuwa zezeta, utashindwa hata
ukijakuingia kwenye ndoa.’
Ø Penda kufanya kazi
Jitahidi kauli yako ioane na ya
mheshimiwa Rais JPM “HAPA KAZI TU.” Nawe sema “KWANGU KAZI TU MENGI-NO SPACE,
NA YA MUHIMU, MUDA UKIFIKA YATAFANYIKA.” Kumbuka wazungu wanasema “An idle
mind is the devil’s workshop.” Do you want to be one of them? No please,
undo your wish. Wish for good and the good will follow you. Ukipenda kazi
utaepuka mawazo machafu, utatenda yaliyo mema. Waza mema, nena mema, tenda mema
nayo yatakufuata nyuma yako.
Ø Palilia fadhila za kibinadamu (Busara,
Haki, Uhodari/Nguvu, na Kiasi)
Kuwa nazo hizi katika kila jambo. Fanya
lililojema. Ulifanyapo lifanye kwa busara, haki, uhodari na kiasi. Ukihitimu
katika hili, hata mahusiano yako yatakuwa mazuri yaliyojikita kwenye busara,
haki, nguvu na kiasi. Hutofanya jambo lolote bila kipimo tarajiwa, wala
hutolifanya kwa kiwango cha chini.
Ø Kubali kukosolewa na wenzako
Unaweza kudhani kuwa uko kwenye njia
sawa katika maisha na matendo yako kumbe uko nje ya maadili ya jamii, uko
kushoto mwa ukweli. Sikiliza watu, ujitambue, watu ni kioo cha matendo yako,
wasikilize wanapokuambia ukweli hata kichaa akisema kitu kwako usikibeze
kwasababu yeye ni kichaa, chukua ujumbe. Ukisikiliza ushauri mzuri hutaingia
katika maovu tunayoyapigia kampeni za kuyatokomeza hapa leo kwenye semina na
kongamano letu.
Ø Soma alama za nyakati (Lk 12:54-56)
Katika hili jifunze kutoka kwa waliao
leo. Usije nawe ukaingia kwenye kilio chao kana kwamba hukuwaona wakilia na
kana kwamba hukujua kwanini wanalia. Waswahili wanasema “Mwenzako
akinyolewa, zako tia maji.’ Sasa wewe kutia kwako maji ni kujihadhari na
wanaume au wavulana walaghai. Ukitaka kufanikiwa waliofanikiwa watakupa hamasa
juu ya nini ufanye, ufanyeje ili nawe ufanikiwe. Lakini ukitaka kufanikiwa
zaidi, jifunze kwa walishindwa. Hao watakufunza viunzi vya kuruka ili usianguke
au usijikwae ukaishia walipoishia wao. Habari ya Ngoswe na Mazoe kwenye Kitabu
“NGOSWE: PENZI KITOVU CHA UZEMBE,” mimi ilinifunza kuwa mapenzi ni sumu ya kazi
zetu. Mazoea alitumbukia katika mapenzi na Ngoswe na hatimaye Ngoswe aliunguza
takwimu zote za Sensa. Ukiona vitu kama hivyo, vinakuamsha kutokufanya kama
wao. Na ufanyapo kinyume chao, umefanya vizuri na hapo umeruka kiunzi. Kwa
upande wa mapenzi kabla ya ndoa, umekwepa mitego ya yote yatokanayo na mapenzi
hayo ‘mimba kabla ya ndoa’ ikiwa ni moja kwa kutaja. RUKA KIUNZI, KIJANA, MAKE
SUCH A LONG JUMP IN LIFE.
Ø Usidanganyike (Mk 13:5)
Jitahidi kuwa mjanja katika maisha.
Epuka kupenda kubembelezwa kwa kila jambo na kila wakati. Wengine walianzia
huko kwa kutaka kubembelezwa, wakaishia kuwekwa kwenye mapaja kama Samsoni kwa
Delila. Mwisho wake, walienda hatua kubwa zaidi kwa ubaya (mapenzi) na kwa kuwa
muda ulikuwa haujafika, waliiharibu kesho yao ambayo ndiyo leo tunayoizungumzia
hapa. Sema SIDANGANYIKI. Nawe kijana wa kiume usimdanganye binti wa watu.
Mheshimu na heshimu utu na maisha yake. Mnapokuwa mabwenini wasichana kwa
wavulana mna mengi sana ya kufanya kuliko kuwaza na kuwaka tamaa za mapenzi tu.
Mtaharibu mambo. Na mtaishia kupotea. Kila mmoja aishi kwa adabu njema na hiyo
iwe chombo chake cha kusafiria katika maisha, usafi uwe vazi lako. Mchana na
usiku mtu asikudanganye.
Ø Usiwe mtumwa wa malimwengu na dunia hii
(Rum. 12:2)
Ulimwengu una ajira nyingi sana hii ya
mapenzi kabla ya ndoa ni moja wapo, usiutumikie ulimwengu katika ajira hii,
mshahara wake ni mimba za utotoni, mshahara wake ni UKIMWI. Mshahara wake ni
mauti. Ulimwengu una matamu mengi sana, hili la mapenzi linaweza kuonekana
nambari wani, lakini ukishaonja utaona kuwa siyo ukweli kama bado dhamiri yako
inasema ‘NDIYO-HAPANA, SAHIHI-SI SAHIHI, VEMA-KOSA, FANYA-USIFANYE, KAMA
AMBAVYO SAA HUSIKIKA ‘TIKI, TIKI, TIKI.’
Ø Kujitambua na kutenda mambo msingi kwa
muda maalum
Napenda nikupe ushauri huu bure kabisa,
Wazungu wanasema “first things first” Jitahidi ufanye yaliyo ya lazima
na kwa muda wake. Unaweza ukawa unafanya jambo zuri na takatifu kabisa lakini
kama ni nje ya muda unaweza kupoteza lengo. Kumbuka hautabaki msichana siku
zote au mvulana siku zote. Ishi vizuri muda huu ungali na nguvu nyingi kesho
yaja unaweza ukutwe huna akiba ya matunda mema ya ujanani. Anza leo. Ukichezea
ujana wako leo, fainali iko uzeeni, yaani kesho. Cheza vizuri leo ungali
kijana. Fanya yaliyo sahihi. Hutajuta fainali ikifika.
Ø Kuwa na msimamo thabiti na simamia
maamuzi mazuri na sahihi bila hofu yoyote
Usiposimama kwa lolote utaanguka kwa
lolote. Simama katika ‘hapana kwenye masuala ya kipuuzi.’ Na hapana yako iwe ya
kweli, siyo hapana nje kumbe ndani unasema ‘ulichelewa wapa kaka/baba?’
nilikungoja kwa shauku, loo! Sasa Mungu anipe nini? Na usisimame kwa miguu ya
mwenzako, yeye ni yeye na wewe ni wewe. Usitumie vionjo vyake kuishi maisha
yako. Kama anapenda ngono, siyo ufunguo wa maisha yako wewe kuishi kwa kupenda
ngono. Amua sasa.
v Ushauri nasaha
“Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa
huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu,
yakumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana” (Rum. 12:1). Naanika
ujumbe huu hadharani, kijana mwenzangu mwone kijana mwenzako kuwa dada/kaka
kwako. Kwa mkubwa mwone kama mama/baba kwako. Husiana nao vizuri. Usikosee na
kuwaona ‘girlfriend/ boyfriend’ ‘mume/ mke.’ Waheshimu katika mtazamo huo.
Ukimwona dada/kaka ndani ya kijana mwenzako, hutomkimbilia kwa mapenzi.
Utamkimbilia kwa uhusiano mwema. Na kama mmependana kwa lengo la kuoana,
taratibu zipo za kikanisa, kijamii, zifuateni na ipo siku mtakuwa mume na mke
nje na hapo ni uzinzi. Ni kuvunja amri ya Mungu, ni dhambi. Epa dhambi.
Usikimbilie kumwona kijana mwenzako kama WIFE/ HUSBAND MATERIAL wa leo kumbe
unataka kumchezea tu.
Urafiki tuujengao utusadie kukua,
kujilea, kujitambua na kuhusiana. Kijana mwenzangu jenga urafiki mwema, wenye
afya, wenye asili ya Kimungu “Siwaiti tena watumwa, nawaita rafiki maana yote
niliyoyasikia kwa Baba yangu nimearifu” (Yn. 15:15). Epa, epuka marafiki
wabaya “tufanye tu, mbona hata wengine hufanya, haiui kufanya” marafiki wa
namna hii, ni kama kivuli giza likiingia wanatoweka (ukishawatimizia matakwa
yao huwaoni tena). Soma neno hili la Mungu (YBS 6:7-17) likusaidie
kuchagua marafiki wema na wazuri. Marafiki hao hufurahi wakikuona unaangamia
nawe usijikaze huku unateketea (Rej. Mit. 1:10).
Nawaomba vijana wenzangu, kila mmoja
awe mlinzi wa mwenzake, kila mmoja awe msaada kwa mwenzake kutenda mema. Kila
mmoja awe mwalimu kwa mwenzake ili amfundishe kuwa ‘uhusiano kati ya mtu na mtu
siyo kwa njia ya mapenzi tu. Na tujaribuni kuwaonesha wenzetu athari za
mahusiano ya mapenzi kabla ya ndoa. Wakizitambua wapo watakaoacha mapenzi kabla
ya ndoa na hata wakitokea wakaidi ambao hawafaidi mpaka siku ya idi kama
wasemavyo Wahenga, basi kwa upande wa mwalimu, yeye ajue wazi kabisa kuwa
amekuwa mtumishi mwema na mwaminifu na ametenda kwa mujibu wa wajibu wake.
Hutajuta wala hutasutwa dhamiri kwenda kuungama kwa kutoa elimu hiyo, lakini
ukiacha na mwenzako akapotea, sala ya kutubu kipengee cha ‘…kwa kutotimiza
wajibu” kikutangulie kusema ‘nimekosa mimi, nimekosa mno...” Vijana
wenzangu, tukitaka kufanikiwa katika maisha, tumwigeni Kristo aliye njia,
ukweli na uzima (Yn. 14:6), yeye pekee ndiye ufunguo wa maisha yetu
tukimfuata yeye tutafanikiwa katika maisha na tutazikomboa nafsi zetu.
Imetokea
umechanganya mafaili na mimba imeweka vema (imeingia) ufanye nini?
a)
Usiitoe
huyo kwetu wana uhai ni binadamu mwenzetu, ni mali ya Mungu, ni zawadi kutoka
kwa Mungu, kwako wewe mzazi ni mtoto, na kwa Mungu ni kiumbe chake alichokijua
tangu hujakibeba tumboni mwako (rej., Yer. 1:4) na amemuumba kwa sura na
mfano wake kwa malengo maalum (rej., Mwa. 1:26, KKK na. 2002).
b)
Uhai
wa hicho ulichokibeba ni bora mara kumi elfu kuliko ujana unaouhofia
kuharibika, kuliko masomo unayofikiria kuyakosa, kuliko ajira unayohofia
kuimwaga chini, kuliko kampani ya mabesti wako unayoiona iko matatani.
c)
Kumbuka umependelewa kuwa mama mtoto mtarajiwa
na baada ya muda wa miezi hiyo kenda tu unakuwa. Umeshirikishwa uumbaji na
Muumbaji wa kwanza na mkuu (Mungu Baba). Shirikiana naye akushirikishaye upate
neema na heri kama wanawake wengine waliozipata (rejea mama wetu Maria ‘umejaa
neema…umebarikiwa…Lk. 1:28, 42).
d)
Mimba siyo ugonjwa wala dhambi, ugonjwa na
dhambi ni kuitoa.
Nawapeni nguzo za kuishinda njaa na kiu
ya miili yetu. Tuwaigeni watakatifu vijana walioishinda dunia na matamu yake
kwa usafi wa moyo. Walibaki mabikira tangu kuzaliwa mpaka kufa kwao. Mfano, mt.
Terezia wa mtoto Yesu. Mwenye heri Anuarite, watakatifu akina Anyesi na wengine
wengi. Hao watatufunza kuona kuwa inawezekana kuishi kiaminifu bila kuchafua
usafi wa moyo. Kama kijana mpaka ninavyoongea hivi unaumia maana umeshatibua
mambo yaani kwako wewe kuishi si Kristo bali ni mapenzi, nakubeba kwa upendo
mpaka kwa mt. Agustino ambaye kwa maisha yake, hakuna mwanamke aliyekatiza
macho yake akampendeza halafu akamwacha aende zake, lakini mwisho wa siku
alimwongokea Kristo nakusema “Nimechelewa mno kuutambua uzuri wa tangu kale!”[57] Na hapo
anatambua jambo hili lililogusa kiu ya roho yake “Umetuumba kwaajili yako
Bwana, na roho zetu hazitatulia mpaka zitulie kwako.”
Kwa kuwaangalia hawa, tutafuteni
majawabu ya maswali haya:
(1)
Nimejiandaaje
kwa maisha baada ya maisha? Ninaendelea kujiandaa au najiandaa kwa kinyume
chake?
(2)
Kwa namna
ninayoishi na jinsi ninavyohusiana ana wenzangu, nikifa leo, mimi ni wa sehemu
ipi kati ya mbinguni alikoenda Kristo kunitayarishia makao (Yn. 14:2) au
motoni kwa shetani na malaika wake? (Mk. 9:48).
Ukipata jawabu zuri leo, usibweteke
nalo nakucharaza maisha kumbuka “ajidhaniaye kuwa amesimama aangalie asianguke”
(1 Kor. 10:12). Tujiulizeni maswali hayo kila siku, hata unapoenda
kulala, uamkapo, utembeapo njiani jiulize. Hata uendapo kwenye utekelezaji wa
appointment zako za kimahusiano kama tulivyoelezwa na msemaji wa kwanza,
jiulize maswali haya. Maswali haya yatatusaidia, kuepa nafasi za dhambi
zitokanazo na mahusiano mabaya. Maana kuna wakati kila ukimwona
msichana/mvulana unamtamani kwa mapenzi. Hayo siyo maisha ya wana wa Mungu
ndugu nakwambia.
Ifike mahali ukimwona msichana amepata
sifa zote za vionjo vyako, mwonee tamaa na kiu yakumtakia siku moja kwa jinsi
anavyoishi aweze kuwa mtawa/sista au ukimwaona mvulana na namna anayoishi,
umwazie mema mathalani yeye siku moja kuwa padri wa kazi ya Mungu au mtawa wa
kiume. Au hata mama/baba mzuri wa familia yaani kanisa la nyumbani. Na hapo
utamheshimu kila mtu na hutomvunjia au kumharibia kesho yake anayoiandaa leo.
LET’S BUILD TRANSFORMATIVE SELF DESIRES IN OUR LIVES. SURELY WE SHALL MAKE IT
ONE DAY. GET MY WORDS CLEARLY. Ukiwa na tamaa njema yenye kubadili mwelekeo
kuutoa kwenye ubaya kuupeleka kwenye uzuri, utakuwa umeanza kuishi maisha ya
wana wa Mungu, maisha ya kiadilifu. Na kesho yako itakuwa yakung’ara, na mbingu
itakuwa ndiyo mede uitafutayo.
Usukumani tulikuwa tunawimbo kipindi
cha kulima, ambao maneno yake kwa Kiswahili ni haya:
Kiatu changu kimetangulia kwa wanawake,
binti kiuno, nipe titi ninyonye, nimelogwa, nimelogewa vitu hivi.
Hapa unaweza kuona hamasa na kujitetea
kutenda mabaya. Change the mind, transform your desires, transform your
thoughts, the way you think affects your today and tomorrow and can affect you
to the end of your life whose destiny is a complete loss! What is life if not
reaching our Creator?!!
v Hasara
· Inawezekana
kupelekea mauaji (utoaji mimba)
· Inapelekea
mshichana kukosa haki zake za msingi kama msichana (kukatisha masomo yake)
· Pia
inaweza kumpelekea msichana kuathirika kimahusiano, kiafya kutokana na kupata
mimba pasina kufikia umri stahiki
· Familia
wakati mwingine zinapata mizigo ya kuanza kulea mtoto aliyepata mimba pamoja na
mimba yake (yaani yeye binti na kichanga chake)
· Pia
msichana mwenyewe anaweza kuingia kwenye kishawishi cha kujiua endapo atatengwa
na jamii au kuonekana kioja katika jamii
· Kuacha
fundisho baya kwenye jamii (mtoto anakuwa na mtoto)
Nini kifanyike?
§ Lazima
kuimarisha elimu ya msingi na sekondari na kuhakikisha wote wanaohusika
wanaipata
§ Elimu ya
uzazi itolewe kwa wanafunzi wa umri husika kuanzia umri wa miaka 10 n.k.
§ Walimu
wa kutoa elimu ya uzazi wathibitishwe kuwa watu wenye maadili mema na wenye
weledi na taaluma hiyo
§ Kukumbushia
wazazi wajibu wao kwa watoto wao. Kwa njia ya semina na makongamano mbali mbali
§ Kuzuia
uhamasishaji wa wazi wazi au kwa njia yoyote ile wa matumizi ya mipira
(Kondomu) kwa watu wote
§ Kutambua
nafasi ya mafundisho ya dini na kuyazingatia
§ Serikali
izingatie kwa kuheshimu mafundisho ya kimaadili ya watu wake mfano ikikatazwa
matumizi ya Kondomu. Watu wasiaminishwe na vyombo vya habari juu ya ufanisi wa
vifaa hivi
§ Adhabu
kali kwa wahusika (anayempa mimba msichana mdogo na msichana aliyepewa mimba
kwa hiari)
§ Kuimarisha
ulinzi wa watoto mashuleni, nyumbani na kokote waliko watoto wa kike kuepuka
mazingira hatarishi hususani ya kubakwa. Mtoto adhaminiwe na kijiji awe mtoto
wa wote katika suala la kulindwa na kutunzwa yaani mzazi na jamii kwa pamoja
wafike hapa kwa kukiri kuwa “MTOTO WANGU NI MTOTO WA WETU.”
Maoni yangu
·
Tamaa ya Pesa, Mali, Vitu
Waswahili wana msemo ‘Tamaa mbele,
mauti nyuma.’ Katika umri wa ujana kuna bahari ivumayo mioyoni mwetu vijana
nayo ni bahari ya tamaa ya pesa, mali na vitu vya thamani kubwa. Wengi wetu leo
tunatamani, simu nzuri, gari zuri, kompyuta, mavazi mazuri, nyumba nzuri na
vitu vingine vingi tu vya namna hiyo. Tamaa hiyo siyo lazima iwe mbaya kama una
malengo mazuri ya kufanya kazi ili uje umiliki vitu hivyo. Sasa upande wa pili
wa shilingi ndio unaoleta adha. Kama wewe mvulana unamdanganya msichana kwa
kutumia vitu hivyo ambavyo vingine huna ukiwa na lengo la kumpata binti wa watu
kimapenzi, hapo umekosea ndugu. Na hata ninyi wasichana kama mnaitoa miili yenu
kwaajili ya kupata vitu hivyo, kupata alama nzuri darasani, na mengine mengi,
wewe pia umekengeuka. Katika kuhadaana huko, ndiko kuna mavuno ya mimba kabla
ya wakati na hatima yake hakuna ndoa hapo. Zaidi ya hayo kuna kuwa na
kutukanana na kujengeana chuki na vinyongo. ‘Asingekuwa yeye, asingekuwa
fulani, nisingekuwa na maisha mabaya namna hii!’ Wengine wanasema ‘ningejua!’
5.2.1 Tamaa
Na
Frt. Aresius Ngemera mwaka 2015 alikuwa na hiki cha kutueleza katika maada yake
juu ya tamaa.
Katika Maisha yetu wanadamu, ni mengi tunayokumbana nayo kama sehemu ya maisha
yetu haya, mengine yakionekana yenye tija kwetu na mengine tukiyaona kama
kikwazo katika kutengeneza maisha ambayo tunaamini Mwenyezi Mungu ametupangia.
Vifo, ukame, njaa, vimbunga, magonjwa, na mengine mengi, hutufanya tuhuzunike
na wakati mwingine kuwaza kuwa huenda Mungu ametuacha. Katika hali kama hiyo,
tunaweza kuchukua hatua mbalimbali kutokana na hitaji la kila mtu, hatua ambazo
zinaweza kuleteleza matendo yaliyo mema na pengine yaliyo mabaya. Mojawapo ya
tunayoweza kuyafanya kutokana na hali hiyo ni Tamaa ya mali. TAMAA YA MALI NI
NINI? Inafanyaje kazi ndani ya mwanadamu na ina matokeo yapi? Haya ni baaadhi
ya maswali ambayo tunalenga kuyajibu katika makala hii, tushirikiane kwa pamoja
tuone ni lipi twaweza kufahamu juu ya tamaa ya mali.
Ukiamka
asubuhi ukaanza safari yako kuelekea katika kituo chako cha majukumu yako ya
siku, ni wazi utapishana na watu wengine wenye safari kama hiyo ya kwako.
Kadhalika utaona vitu vingi ambavyo, kati ya hivyo waweza kuona vinavyovuta
hisia zako. Ni kawaida yetu wanadamu kujikuta unaiambia nafsi yako kwamba ‘nguo
ile ni nzuri’ ‘huyu ana gari zuri’ ‘kile kiatu kinafaa kwa mwanangu’ ‘yule dada
anapendeza machoni’ na mengine kama hayo ambapo bila kijishauri, utajikuta
unajisemea tena moyoni kwamba ‘ningekuwa na pesa ningenunua ile nguo’
‘nitatafuta pesa nimnunulie mwanangu hicho kiatu.’ ‘Yule dada angepita karibu
ningemsemesha walau’ na mengine kama hayo kulingana na kile unachokiona. Tendo
unalofanya mpaka wakati huu ni kujaribu kuieleza nafsi yako hisia zako kutokana
na msukumo unaoupata kutoka katika uhusiano wa uliyoyaona na unayoyahitaji.
Huu
msukumo ndio twaweza kuuita Tamaa kwa maneno mengine. “Nilipoona vazi moja zuri
kutoka shinari kati ya nyara, shekel mia mbili za fedha na mchi wa dhahabu
wenye uzito wa shekel hamsini, nikavitamani na kuvichukua, nimevificha ardhini
ndani ya hema langu, na fedha iko chini ya vitu hivyo” (Yoshua 7:21).
Tamaa ni nini basi? Katika makala yake Apolinary Macha,
anatwambia kwamba tamaa ni hali ya uhitaji wa kitu fulani kiasi kwamba mhitaji
anaamini kwamba upatikanaji wa kitu hicho ndio upatikanaji wa furaha yake.
Macha anaendelea kutuambia kwamba, unapopata ulichotamani kimoja, ghafla,
uhitaji wa kitu kingine cha namna hiyo ama tofauti na hicho unakujia. Bila
kuchelewa unaanza safari ya kuikamilisha tamaa hiyo kwa kukitafuta kitu hicho
kadiri ya uwezo. Safari hiyo huendelea mpaka mwisho wa maisha ya mwanadamu
kwani kila siku kuna kitu kipya cha kutamani. Tamaa kwa maana hiyo, haina
mwisho kwani pamoja na mengine, haitupatii furaha ya kudumu. (rej. 1Yoh.
2:15-17). Tamaa hutoka moyoni ingawa
ukamilisho wake hutegemea sana utendaji wa milango ya fahamu. Na kila mwanadamu
awaye yote hupatwa na tamaa (rej. Yer. 6:13). “Basi nasema: Enendeni kwa Roho,
wala hamtazitimiza kamwe tama za mwili. Kwa sababu mwili hutamani ukishindana
na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi
kufanya mnayotaka.”[58]
5.2.2 Mali
Yawezekana
kuwepo namna nyingi za kuelezea maana ya mali, lakini sisi tutajikita katika
kuelezea ile isemayo kuwa, mali ni kitu chochote kinachomilikiwa. Umiliki
katika maana hii, unaweza kumanisha mamlaka ya mtu ama kikundi cha watu kama
vile familia, ukoo, kijiji, mkoa, nchi na mengine mengi juu ya mali husika.
Mali katika muktadha huu, inajikita hasa katika kumanisha kitu kinachoonekana
na kitu chochote anachomiliki mtu ni mali yake.
Ø Tamaa ya Mali
Baada ya
kuona maana ya tamaa na maana ya mali, twaweza sasa kujaribu kuangalia nini
hasa maana ya tamaa ya mali ambalo ndo suala msingi katika mjadala wetu. Bila
shaka tayari tuna dhana kuwa tamaa ni hali ya kuhitaji kumiliki kitu, na mali
ni kitu chochote kinachomilikiwa na mtu. Hivyo tamaa ya mali yaweza kumanisha
hitaji alilonalo mtu juu ya kitu kingine ambacho kwa wakati huo si mali yake.
Wahanga
wa hali hii ya kuhitaji kumiliki mali ni watu wote ambao kutokana na mahitaji
ya wakati hawajafanikiwa kuwa kitu hicho wanachokitamani, ama walichonacho
hakikidhi mahitaji yao. Hali hii ya uhitaji, yaani tamaa ya mali yaweza
kuendelea kwa kitu kilekile ama kitu kingine kutokana na uhitaji wa mhusika ili
aweze kutimiza ile furaha yake.
§ Mgawanyo wa tamaa ya Mali
Katika
upana wake, tamaa inaweza kugawanyika katika vipengele ama aina mbalimbali,
japo zinaweza kuwa na uingiliano wa nama fulani. Kuna tamaa ya madaraka, tamaa
ya uzima wa milele, tamaa ya kazi nzuri, tamaa ya mali, na nyinginezo. Katika
mjadala wetu, tunaongelea tamaa ya mali ambayo kama sehemu ya tamaa, nayo
inaweza kugawanyika katika mchanganuo wa aina mbili ambazo ni Tamaa nzuri ya mali na Tamaa mbaya ya mali.
Magawanyo huu unaletwa na kile tunachokiita lengo la tamaa husika.
ü Tamaa nzuri ya Mali
Hii ni
hali ambayo mtu hutamani kumiliki kitu kwa ajili ya matumizi mazuri kwake na
kwa jamii inayomzunguka, na mtu huyo hutumia njia ama mbinu njema kukipata kitu
hicho. Hapa tunaangalia ni kitu gani mtu anatamani na ni kwa sababu gani
anakitamani, baadaye tunachunguza
uwezekano wa yeye kukipata kwa namna iliyo halali. Mfano, anayetamani
kupata fedha ili anunue nguo ama ajenge nyumba na anatafuta pesa hiyo kwa njia
ya kujishughulisha na kilimo anakuwa anatekeleza tamaa nzuri ya mali.
ü Tamaa mbaya ya Mali
Hii ni
hali ambayo mtu hutamani kumiliki kitu, si kwa sababu ya nia nzuri ya matumizi
bali kwa sababu ndugu yake ama jirani yake anacho nayeye hana. Katika hali kama
hii, mtamani husika huwaza katika kuhakikisha anapata kile alichonuia ama
kikubwa zaidi ya kile, kwa nia ya kumkomoa ama kumtambia mtangulizi wake. Njia
za kupata ama kukidhi tamaa hii ya mali, zaweza zisiwe njema kwani, mhusika
yuko tayari kutumia njia yoyote ile ilimradi atimize ama apate anachotaka. Hii
yaweza kupelekea mtu mmoja kumkanyaga kanyaga mwenzake ili tu aweze kupata kile
anachokitamani. Ndiyo maana mtu mmoja aliwahi kusema “Kama kusali kwako kwa
kupiga magoti ni kumkanyaga mwenzako, bora uache tu.” Kama nia yako ya kupata
mali inakupelekea kumuua ndugu wetu mlemavu wa ngozi, ni vema akaghairi
mwenendo wako mbaya upate kulinda uhai wa mwenzako na wako pia, ni bora kuwa
maskini wa mali kuliko kuwa tajiri kwa njia ya kumuua mwenzako. Hali hii yaweza
kuambatana na wizi, mauaji ama mafarakano baina ya washusika. Hii tamaa ina
mizizi yake katika kutoridhika na kile mtu alichonacho. Hizi tamaa zote
hutokana na nini?
5.2.3 Sababu za Tamaa
Katika
nafasi ya mtu mmoja mmoja, tamaa yaweza kuelezwa kuwa na visababishi vya
kutosha, kwani ni mara chache tamaa ya huyu ikawa sawa na tamaa ya yule, hususani
katika masuala ya lengo la tamaa hiyo. Hapa kuna baaadhi tu ya mambo yanayoweza
kuwa miongoni mwa visababishi vya tama:-
¨ Hitaji la kibinadamu
Hapa
tunaongelea ile hali ya uhitaji wa vitu ambayo kila mwanadamu anayo kutokana na
mazingira yake. Ni hali ya kawaida mwanadamu kuhitaji chakula kizuri, malazi
mazuri, mavazi mazuri na kila kitu ambacho kwacho anapata furaha anayoihitaji.
Hali hii tunaweza kuiweka katika kipengele cha matendo ya binadamu ambayo
anayafanya pasipo hiari na hivyo katika shughuli zake za kila siku anajitahidi
kupigana ili ayapate kwa manufaa ya maisha yake ya hapa duniani.
¨ Ufahari
Hii ni
hali ambapo mtu ana kiasi fulani cha mali kama milki yake lakini hajaridhika na
kiwango hicho cha mali alichonacho. Katika hali ya kutoridhika, mtu huyo
anaamini kuwa bado ana uwezo wa kupata mali zaidi ya ile aliyonayo na hivyo
akaweza kujipatia sifa ya utajiri kutoka kwa jamii inayomzunguka. Mtu huyo
atafanya kila jitihada ili aweze kupata mali nyingi zaidi akiamini atapata
ufahari anaoutamani (rej. Lk. 12:16-20).
¨ Matabaka/ Utofauti katika umiliki wa Mali
Hapa
tunazingatia kigezo kwamba binadamu tunatofautiana katika kiwango cha mali
tunazomiliki. Kuna wenye mali nyingi na wengine kidogo, wengine wana mali bora
kuliko za wengine, na wengine hawana kabisa kile wanachohitaji kama mali zao
kutokana na uwezo mdogo, lakini wote tunajikuta katika mazingira ya aina moja.
Katika mazingira haya, yule ambaye anajiona hana kile anachohitaji wakati
anakiona kwa jirani mwenye vingi zaidi, atashawishika kufanya jitihada ili naye
aweze kupata mali kama hizo au hata zaidi yake. Huku ni kujifunza kwa
waliofanikiwa kupiga hatua katika maisha. Ni hali ya kuiga yaliyo mazuri na
yafaayo kuigwa kwa maendeleo ya mtu binafsi na jamii nzima.
¨ Tofauti katika ubora wa Mali
Hii
inaendana kwa kiasi fulani na ile ya matabaka, katika mazingira kwamba, mwenye
uwezo mkubwa hutafuta kitu chenye ubora mkubwa wakati mwenye uwezo mdogo
ananunua kile kinacholingana na uwezo wake; kila mbuzi hula kwa kadiri ya urefu
wa kamba yake. Tofauti hizi huamsha hali
ya kawaida ya binadamu ya kuhitaji kilicho bora kwa matumizi yake. Yule
mwenye kitu chenye ubora mdogo atapigana kuhakikisha anapata hicho chenye ubora
zaidi kadhalika na mwenye bora anatafuta kilicho bora zaidi na hivyo tamaa
inaanza kupaliliwa. Hii ni tamaa ambayo ni matokeo ya kuwa na kitu na kutamani
kuwa nacho zaidi na zaidi (kwa wingi wake au ubora wake). Wana uchumi husema
“Jinsi unavyokuwa na mali nyingi ndivyo unavyotamani kuwa nazo nyingi zaidi, na
hata namna ya kuzipata hukua na fursa pia huongezeka.” Ingekuwa ni kuliangalia
suala hii kwa jicho la Kibiblia tungeweza kusema pasina wasi wasi kuwa “Aliye
nacho ataongezewa, na yule ambaye hana, hata kile alicho nacho atanyang’anywa.”
5.2.4 Faida za Tamaa
Katika
lenyewe, neno tamaa halina ubaya ndani yake isipokuwa tu pale mtu anapokuwa
ametumia tamaa hiyo kutekeleza yaliyo mabaya. Kutamani kitu ambacho kwa hatua
halali unaweza kukimiliki ni hatua mojawapo katika kufanya jitihada binafsi za
kimaendeleo. Hakuna maendeleo ya kweli bila tamaa maana hata kuendelea huja
mara baada ya kuwa na tamaa ya kupata maendeleo. Hii ikikosekana, hakuna ndoto
ya kumwezesha mtu kupiga hatua ya mafanikio. Hata kama angepata mchawi wa
maendeleo, bado angejikuta anaogelea kwenye dimbwi lenye sumu kali ya mchawi wa
kutokusonga mbele kimaendeleo. Atabaki anachapa miguu pale pale tu (mbele
haendi wala nyuma harudi).
Hali hii
katika maendeleo ni mbaya sana maana inaua matumaini ya kimaendeleo. Inavunja
moyo wa kuyatafuta maendeleo. Inaifunika imani ya kuendelea kwenye dimbwi la
kuridhika na hali iliyopo kitu ambacho ni sumu na inaua hata kama itaonekana
kuwa ni kwa mwendo wa kobe maana Wahenga walishasema “Pole pole ya kobe
humfikisha mbali.” Hii ni tofauti na
kutamani mali ya mtu mwingine ambayo hata Maandiko Matakatifu katika kitabu cha
Kutoka 20:17, yanazuia.
Unaposhuhudia
maendeleo ama mafanikio ya jirani yako, nia ya kufanya vivyo hivyo (ambayo
ndiyo tamaa) inakujia na kukutia nguvu na hamasa ya kuhangaika ili kufikia
hatua ya mwenzako na pengine zaidi. Hili ni zao zuri la uwepo wa hali ya
kutamani maishani mwetu. Bila hii aina ya tamaa dunia isingekuwa imefikia
ubunifu, udadisi, na mafanikio yaliyopo leo. Na hata kwenye jamii zetu mambo
yangebaki kama yalivyokuwa enzi za zama za kwanza/za kale za mawe au hata kabla
yake! Lakini kila iitwapo leo, watu wanapiga hatua mbele. Aliyeanza na simu ya
tochi, leo anatamani au amesha nunua simu ya tachi au almaarufu smart phone.
Aliyekuwa
na baiskeli mwaka jana, leo ana ndoto ya kununu bodaboda maana mtaani alimo
wanaume wenzake karibu wote wana bodaboda na akiaangalia kuwa wengine aliwazidi
kiuwezo, hapo ndipo anatamani hata kuleta pikipiki kadhaa au kilav4 chake.
Aliyekuwa na mtaji wa laki tano (500,000/=) leo hii anapigia kuongeza mtaji
wake ufikie Milioni moja (M1) kama jirani yake au hata zaidi. Staili hii ya
tamaa ni ile inayofuata kaulimbiu ya “KAMA.” Mfano “KAMA WENGINE WAMEWEZA
KWANINI MIMI NISIWEZE? KAMA YEYE AMEWEZA NA TULIKUWA SAWIA NAYE, KWANINI MIMI
NISIWEZE?” Msanii aliyekuwa na nyimbo chache chini ya album, leo ana ndoto ya kuzindua album yake. Na kweli watu wamefika mbali kwa tamaa kama hii. Hata
baadhi ya waandishi mashuhuri leo walianza na tamaa ya kuandika kama waandishi
fulani fulani kama akina William Shakespeare, Eric Shigongo, Mhe. Pd Titus
Amigu, Mhe. Pd Dk Faustine Mwikila Kamugisha kutaja japo wachache.
5.2.5 Hasara za Tamaa
Licha ya
mazuri mengi tunayoweza kuyapata kutokana na kutamani, maelekeo mengi ya tamaa
zetu ni katika hasara. Pengine hii ni kwa sababu ya malengo tunayokuwa nayo,
ama mbinu tunazotumia kukidhi haja hizo. Tujaribu kupitia baadhi ya hasara
zitokanazo na tamaa.
Ø Tamaa huondoa hofu ya Mungu
Hali hii
inajitokeza pale ambapo mtu hutenda mambo yatokanayo na tamaa yake, yaliyo
kinyume na mapenzi ya Mungu. Nabii Ezekiel katika Maandiko matakatifu anasema
“Ndani yako wamepokea rushwa ili kumwaga damu, umepokea riba na faida, nawe kwa
uchoyo umepata mapato kwa kuwadhulumu jirani zako nawe umenisahau mimi, asema
Bwana Mungu” (22:12). Tunapo endekeza tamaa zetu, hatuna namna ambapo tutaepuka
kutoutii uwepo wa Mungu maishani mwetu.
Ø Mauaji
Nabii
Yeremia Katika Maandiko matakatifu anasema “Bali macho yako na moyo wako hauna
utakalo ila kutamani, na kumwaga damu isiyo na hatia na kudhulumu na kutenda
jeuri (22:17).” Tamaa ya mali inaweza kutushawishi hata kuondoa uhai wa mtu
asiye na hatia, hasa pale ambapo tamaa zetu zinazidi uwezo wetu wa kufikiria;
pale ambapo mafanikio ya mwenzako yanaonekana ni kikwazo kwako. Suluhisho pekee
katika hali hii laweza kuwa ni kuondoa uhai wa watu wasio na hatia. Hapa ndipo
usahihi wa kauli hii hujidhihirisha ‘akili na utashi wa mtu unagubikwa na tamaa
ya mali, anaona lolote linalomwezesha kufika anakotaka ni jema na analifanya
kwa haraka na kwa wepesi!’
Ø Wizi
Tamaa
inapozidi na kutaka kutekelezeka katika namna ya haraka, mwenye kutamani
anaweza kujikuta hana namna nyingine ya kupata mali hiyo anayoitamani ispokuwa
kwa wizi. Kuiba ni uvunjifu wa Amri za
Mungu (rej. Kut. 20:15) na pia ni ukiukaji wa sheria za nchi zinamzozuia mtu
kumnyima mwingine haki yake ya kuishi.
Ø Malumbano
Nabii
Isaya anasema “Kwa sababu ya uovu wa kutamani kwake, naliona hasira nikampiga,
nalificha uso wangu nikaona ghadhabu, naye akaendelea kwa ukaidi kuifuata njia
ya moyo wake mwenyewe (57:17)”. Pia Nabii Mika anasema “Nao hutamani mashamba
na kuyashika, na nyumba pia, nao huzichukua, nao humwonea mtu na nyumba yake,
naam, mtu na urithi wake (2:2).” Mtume Yakobo naye anasema “Vita vyatoka wapi
na mapigano yaliyoko kati yenu yatoka wapi? Si humu katika tamaa zenu zifanyazo
vita katika viungo vyenu?... (4:1-5)”. Aya zote hizi kutoka katika Maandiko
matakatifu zinaonesha ni kwa namna gani tamaa huleta malumbano na mafarakano
baina yetu sisi wanadamu. Tamaa inatutenganisha mtu na mtu, ndugu na ndugu. Ni
kwa tamaa mbaya ya mali namna hiyo Yuda Iskariote alimsaliti Bwana wake! Nasi
leo ni akina Yuda Iskariote kwa kusaliti utu wa wenzetu, haki za wenzetu, mali za
wenzetu na mambo mengi kinyume na taratibu za Kikanisa na Kiserikali.
Tumejeruhi mara mia zaidi kuliko kuponya kwa silaha yetu ya tamaa. Tumeiruhusu
tamaa iwe risasi yetu ndani ya bunduki yetu (akili na utashi) na hivyo kuitumia
si kwa kuua wanyama, bali binadamu wenzetu!
Ø Dharau
Mwenye
tamaa ya mali huambatana na majivuno na kupenda sifa za kila wakati. Mtu mwenye
tamaa ya aina hii hupenda watu watambue uwepo wake katika jamii kwani anaamini
mali alizo nazo ndio utajiri wa kuweza kumtiisha kila awaye chini yake. Mzaburi
anasema “Maana mdhalimu hujisifia tamaa ya nafsi yake, na mwenye choyo humkataa
Bwana na kumdharau” (Zab. 10:3). Tamaa ya mali inaweza kutufanya tuwaone
wengine si kitu kwetu na mbaya zaidi kusahau uwepo wa Mungu katika maisha yetu.
Tamaa ya mali hutufanya tuwaone wenzetu kuwa ni chombo, ni daraja la kufikia
mahitaji yetu. Hiyo tamaa hutufanya tusiione thamani ya wenzetu katika maisha
yetu. Hutupofusha na kutuacha maskini wa pendo la Mungu linalotualika kumpenda
na jirani wetu kama tunavyojipenda sisi wenyewe.
5.2.6 Suluhisho juu ya Tamaa
Katika
ufupi wake, mpaka sasa tumeona ni kwa jinsi gani tamaa ya mali ama kutamani kwa
ujumla kunavyoweza kuvunja amani yetu wanadamu, hasa kama watu wanaoishi kwenye
jamii moja na watu wa Baba mmoja, Baba yetu wa mbinguni. Hivyo hatuna budi
kujiepusha na tamaa zetu mbaya za mali. Luka katika Injili anasema “Angalieni,
jihadharini na choyo maana uzima wa mtu haumo katika wingi wa vitu alivyonavyo”
(12:15). Yafuatayo ni baadhi ya mambo tunayoweza kuzingatia ili kuepuka tamaa
mbaya ya mali:-
· Upendo kwa Watu Wote
Upendo
ni silaha kubwa sana tuliyonayo sisi wanadamu, inayotusaidia kutambua uwepo wa
Mungu maishani mwetu na katika maisha ya jirani zetu. Amri za Mungu
zinatuhimiza kupendana. (tazama Lk 10:27; Rum. 13:8-10). Tukipendana
hatutafarakana kwa sababu ya tamaa ya mali. Mtume Paulo kwa Warumi anaseka
kuwa; “Tumtegemee Mungu na tuachane na kupenda tamaa za dunia (13:14).
Tukifanya hivi tutakuwa tunatengeneza jamii yenye furaha na upendo, yenye
ushirikiano hata katika shida zetu. Hebu tuimbe kwa pamoja wimbo huu mzuri na
wenye ujumbe mzuri pia:
Kiitikio
Tukipenda wenzetu, Kati yetu Mungu yupo X2
1.
Aliyetufanya tuwe ndugu, Ndiye Yesu ndugu yetu, Chuki yote
na hasira, Kati yetu ziondoke.
2.
Tukipenda Mungu wetu kweli, Tuanzie na nduguze, Audhiye
mmoja wao, Mapendoye si ya kweli.
3.
Tuwe moyo mmoja, roho moja, Tuwe pia kundi moja, Tupendane
kama vile Yesu alivyotupenda.
4.
Furahini nyote, binadamu, Mwimbieni Mungu wetu, Amri yake ni
nyepesi, Neno lake: kupendana.
5.
Kati ya ugomvi na fitina, Na katika kasirani, Mungu wetu
hapapendi, Mungu wetu wa amani.
6.
Yesu Kiongozi wetu mwema, Amri yako twaijua, Washa nyoyo za
Wakristu, Wapendane siku zote.[59]
· Kuutafuta Ufalme wa Mungu
Mtume
Paulo kwa Wakorintho anasema; “Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme
wa Mungu? Msidanganyike, waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala wazinzi,
wala walawiti, wala mashoga, wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala
watukanaji, wala wanyang`anyi” (1Kor. 6:9-10).
Tena,
Mtume Paulo anawaambia Warumi kwamba; “Dhambi isitawale ndani ya miili yenu
ipatikanayo na mauti, hata mkazitii tamaa zake” (6:12). Waraka wa pili wa Mtume
Petro kwa watu wote umeandikwa kuwa “Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa
mno, za thamani, ili kwamba kwa hizo tupate kuwa washirika wa Umungu,
tukiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa” (1:4). Mwinjili
Luka anatupa kilele cha haya mawazo yote kuwa tuutafute kwanza ufalme wa mbingu
na mengine tutapata kwa ziada (12:31 soma pia Tito 2:12-13).
· Kuridhika na kidogo tulichonacho
Kuridhika
ni tabia tunayopaswa kuijenga sisi wanadamu, licha ya uhitaji wowote tunaoweza
kuwa nao. Waraka kwa Waebrania unatuambia kuwa; “Msiwe na tabia ya kupenda
fedha, muwe radhi na vitu mlivyonavyo, kwa kuwa yeye mwenyewe amesema,
sitakupungukia kabisa wala sitakuacha kabisa” (13:5). Tena katika waraka wa
pili wa Mtume Petro kwa watu wote imeandikwa; “Kwa hiyo vifungeni viuno vya nia
zenu na kuwa na kiasi, mkiitumainia kwa utimilifu ile neema mtakayoletewa
katika ufunuo wake Yesu Kristo. Kama watoto wa kutii, msijifananishe na tamaa
zenu za kwanza za ujinga wenu (1:13-14)”. Kana kwamba nataka kumuua mbu kwa
kutumia greda! Yohane Mbatizaji pia alipofuatwa na makundi yale matatu ya
waliohitaji msaada wake kwa kumwuliza “TUFANYE NINI?” yaani (watu wote, watoza
ushuru na maaskari) aliwaambia watu,
watoza ushuru, na maaskari kila mmoja “mwenye kanzu mbili ampe asiye na
kanzu, mtu yeyote mwenye chakula ampe yeye asiye na chakula, msitoze zaidi ya
kilichopangwa, msiwatishie watu, msiwakaripie watu, ridhikeni na mishahara yenu
(rej. Lk 3: 7-14)”. Tukumbushane ule wimbo wa Msanii wa kizazi kipya anayesema
mahali fulani kwenye wimbowe:
Tukipata twashukuru,
Tukikosa twalala.
Anachotufunza
kijana huyu ni kuridhika na kidogo cha halali ulicho nacho. Pili, kuwa na
shukrani kwa Mungu mpaji wa vyote, kidogo au kikubwa tumevipata toka kwa Mungu,
tushukuru basi kabla hatujayakausha mema yote kwa kuwa na moyo uso shukrani.
Na Mzaburi
ana haya ya kutuambia:
Sikilizeni
jambo hili enyi watu wote, tegeni masikio enyi wakazi wote wa dunia; sikilizeni
nyote wakubwa kwa wadogo, watu matajiri na fukara. Maneno yangu yatakuwa
mazitomazito, nami nitasema maneno ya hekima…Watu waovu hutegemea mali zao,
hujisifia wingi wa utajiri wao. Lakini mwanadamu hawezi kamwe kujikomboa
mwenyewe; hawezi kumlipa Mungu bei ya maisha yake, maana fidia ya maisha ni
kubwa mno. Hawezi kutoa kitu chochote kinachotosha, kimwezeshe aendelee kuishi
daima, asipate kuonja kaburi. Yeye afahamu kuwa hata wenye hekima hufa,
wapumbavu kadhalika na watu wajinga. Wote hao huwaachia wengine mali zao.
Makaburi ni makao yao hata milele; ni makao yao vizazi hata vizazi, ingawa hapo
awali walimiliki ardhi. Binadamu hatadumu katika fahari yake, atakufa tu kama
mnyama. Hayo ndiyo yawapatao wanaojiamini kipumbavu, ndio mwisho wa wale
wanaojivunia mali zao... Usihangaike ukiona mtu
anatajirika, wala mali yake ikiongezeka zaidi na zaidi, maana atakapokufa
hatachukua chochote, mali yake haitashuka huko chini pamoja naye. Ajapojikuza
katika maisha haya, na kusifiwa kwa sababu ya kufanikiwa, atajiunga na wazee
waliomtangulia kufa, ambao hawawezi tena kuona mwanga. Binadamu hatadumu milele
katika fahari yake, atakufa tu kama mnyama (Rej. Zab. 49).
5.2.7 Ndoa za Utotoni
Lakini pia tukumbuke kuwa uovu huo
tumeuendekeza sisi wenyewe kwanza kwa kukimbilia familia bila malezi.
Fikiria vijana ambao wameoana katika umri mdogo, hivyo hata watoto watakaozaliwa
watalelewa kitoto-kitoto. Kwa kuwa wanasema kukua ni kuona mengi, kwao
hawajaona mengi ni dhahili; hata namna ya kujiweka katika maisha hawaitambui
vizuri, zaidi utawasikia wakizungumzia kula bata tu (they do not have exposure
to life).
Tunapokuwa na mimba za utotoni
tunategemea pia kuna ndoa za utotoni pia katika maisha ya baadhi ya jamii. Kwa
kuungana na Frt. Ludovick
Frimi mwaka
2015, juu ya ndoa za utotoni alikuwa na haya ya kutueleza:-
Maana ya
Ndoa ni makubaliano ya hiari baina ya mwanamume na mwanamke. Na haya
makubaliano yasiwe ni kwasababu fulani fulani bali yawe yametoka kwao wenyewe.
Ndoa za utotoni ni ndoa zinazofungwa bila makubaliano baina yao (vijana)
wenyewe bali ni kwasababu mbalimbali kama vile kulazimishwa na wazazi, walezi
nk. Wakati mwingine pia wahusika wanaweza kushawishiana wao wenyewe kwasababu
ya kufuata mkumbo mfano, wenzao waliosoma nao wameoa na kuolewa. Kwasababu ya
umaskini au kwasababu ya ujinga wa wazazi au walezi wenyewe. Ni ndoa
zinazofungwa huku wahusika wakiwa chini ya umri wa kuoa au kuolewa. Wakiwa bado
hawaja fikia umri wa kuwa baba au mama wa familia.
5.2.7.1 Sababu
zinazopelekea Ndoa za utotoni
Kuna
sababu lukuki. Tuone japo chache:-
¨ Ujinga
¨ Umaskini
¨ Mila
potofu
¨ Tamaduni
za ukandamizaji
¨ Wafuata
mkumbo (kutaka kutambulika katika jamii kwamba na wao wamo)
¨ Imani
potofu mfano, ‘kuozesha binti mdogo kuna faida kubwa maana ana mvuto mkubwa kwa
wanaume wengi wenye nia ya kuoa’
¨ Mategemeo
makubwa mno ya kimapato (kuozesha binti mdogo kuna fungua mlango wa mafanikio
na utajiri-ng’ombe au mahari wengi watatolewa)
5.2.7.2 Washiriki
¨ Wazazi
¨ Walezi
¨ Ndugu
¨ Jamaa
¨ Jamii
¨ Watoto
wenyewe
5.2.7.3 Hasara
Hasara
ni nyingi mno hata zisipo tajwa hapa zinajulikana. Lakini kwa uchache kabisa
tutaje hizi hapa:-
¨ Kuvunjika
kwa ndoa hizo mapema kabisa
¨ Kupata
matatizo kwenye kipindi cha uja uzito na kujifungua
¨ Kuwa na
familia za watoto wenye watoto wenzao
¨ Kumkosesha
haki zake msingi kama elimu
¨ Mateso
mengi kwenye ndoa hizo (hasa pale wanapo gundua kuwa waliingia kwenye maisha
hayo wangali bado)
¨ Kutokujua
masharti ya ndoa na miiko ya ndoa
¨ Kuonekana
kama waigizaji tu kwa kufanya mambo ndivyo sivyo (mambo mengi ya ndoa yana kuwa
hayajulikani kwao)
5.2.7.4 Dawa ya tatizo
Tusaidiane
kuzibaini japo chache ili tutibu ugonjwa huu hatari kwa Taifa letu (vijana
wetu):-
¨ Elimu
itolewe juu ya ndoa za utotoni na matatizo yake
¨ Kuwasaidia
wazazi namna ya kuondokana na umaskini kwa njia nyingine nje na hiyo ya kuwaoza
watoto wadogo
¨ Kuacha
mila potofu
¨ Vijana
wenyewe wafike mahali hasa wale wa kike waseme ‘hapana, mimi bado, muda ukifika
nitaolewa’ hata wale wa kiume kuna wanao lazimishwa na wazazi wao kuoa ili nao
wajitegemee. Ngoja nikupe mfano mmoja yaliyo jiri kwenye familia moja
Usukumani:
Baba: Ng’wanone ihaha wakulile ‘tolaga lulu nang’ho wizugile
nose ukukilanija’ (mwanangu sasa umekuwa mkubwa, oa sasa nawe upate jiko
mwishowe utapitiliza)
Kijana: Sawa baba. Lakini unkima nakumpandikila hali? (sawa baba.
Lakini nitampata wapi mwanamke)
Baba: Uyukayelayela ng’wanone ukumpandika nunene umayu wako
nakampandika chene (uwe unatembea tembea mwanangu utampata tu hata mimi
nilimpata mama wako hivyo)
Kijana: Sawa baba intondo nakwandya kuchobha nane napandike
ng’wichane (sawa baba kesho nitaanza kutafuta nami nipate mwenzangu)
Kweli kesho ilipofika kijana alimwaga babaye na kuomba
baraka zote ili akafanikiwe.
Kijana: Baba uko nakaja, nakashika mhola lakini natampandikile
unkima wakutola (baba kule niliko enda nilifika salama lakini sikumpata
mwanamke wa kumwoa)
Baba: Pole ng’wanone. Lakini ishi wagwandyaga umhayo,
ukumpandika nduhu tabu nintondo ulaje hangi nyandone (pole mwanangu. Madam
umeshaianza kazi hapana tabu utampata tu na kesho tena uende tena kijana wangu)
Kesho yake kweli kijana kama siku ya jana yake alifanya
vivyo hivyo. Lakini hakufanikiwa tena. Alifanya hivyo kwa muda mrefu sana
hatimaye akachoka mithiri ya sungura kusema ‘sizitaki mbichi hizi.’
Kijana: Bhabha, unene nanoga lulu eshi natumpandikaga unkima uwa
kutola! (baba, mimi nimechoka sasa maana simpati mwanamke wa kumwoa!)
Baba: Hama ulihaya wite ki lulu nyandone? (sasa unataka ufanyeje
kijana wangu?)
Kijana: Napandikaga iwazo bhabha (nimepata wazo baba)
Baba: Iwazo ki ng’wanone? (ni wazo gani mwanangu?)
Kijana: Angu lulu usengi duhu nantole eshi atatoliwe aliyo nsoga
gete kukila nabhabho naliyubhabhona ulu naja kuchola wakutola (si hata shangazi
tu yamkini hajaolewa na hata hivyo ni mzuri sana kuwazidi hata wale ninao waona
nikienda kumtafuta wa kumwoa)
Baba: Ulintumbafu gete nyandebhe untole llumbu lyane! (wewe ni
mpumbavu sana kijana umwoe dada wangu!)
Kijana: Bhabha bhuli ubhebhe untolile umayu wane? (baba kwanini
wewe umemwoa mama wangu?)
Naomba
nisikuchoshe sana. Mfano huu nilio utoa usukumani inawezekana pia uko sehemu
nyingine hata kwa namna nyingine. Utufunze hasa vijana, kusema ‘bado muda
ukifika nitaoa tu au nitaolewa.’ Vijana kuweni na msimamo msiwe kama bendera
‘kufuata upepo.’
¨ Mtoto wa
kike asitumiwe kama mradi au tega uchumi kwa njia ya kudai mahari (hasa
ng’ombe)
¨ Katekesi
ya kina juu ya majukumu na haki za wana ndoa-wanaofunga ndoa wafikie umri wa
kuweza kuyakabili majukumu hayo
Hitimisho;
Ndoa za utotoni ni haramu, si haki kwa watoto kulazimishwa kuingia katika
maisha na wito huo msingi wa miito mingine kabla ya kufikia umri stahiki. Wazazi
na jamii wanapaswa kupewa elimu yenye asili ya ukombozi ili watoto hasa wa kike
walindwe pasina haki zao kukanyagwa kanyagwa kama mavumbi chini ya viatu vya
mvaaji. Wakikua watachagua wao wenyewe ni maisha gani yatakayo wawezesha kumjua, kumpenda na kumtumikia Mungu wao.
Na endapo watachagua ndoa, itakuwa safi maana umri utakuwa ni rafiki kwao
kufanya hivyo na hakutakuwa na matatizo kama tulivyo yabainisha hapo juu.
Jamii
imeishia kuvaa sketi fupi kimaadili kwasababu ya kukithiri katika mambo machafu
kama hili la kuozesha wanajamii wake katika umri mdogo. Hili ni janga kubwa
sana! Tupigeni vita ndoa za namna hii na kwa pamoja tutashinda. Jamii
iziwajibishe familia zenye wazazi wanao walazimisha watoto wao kuingia katika
maisha ya ndoa wangali wadogo bado. Familia pia ziseme hapana kwa watoto
wanaoonesha mwonekano wa kutaka kuoa au kuolewa katika umri mdogo. Watoto
wenyewe pia wawe mstari wa mbele kusema ‘nitasubiri hata kama mazingira
yananilazimu kuoa au kuolewa.’
Kila
mmoja wetu akitimiza wajibu wake, tutaishinda vita hii. Familia moja moja iwe
kali na tayari kuwachukulia hatua wote wanao fika nyumbani kwa lengo lwa kuoa
binti wadogo wadogo. Iwakamate na kuwapeleka mahakamani na huko sheria ichukue
mkondo wake dhidi ya walaghali wa mapenzi kama hao, waharibuji wa maana ya wito
wa ndoa kama hao. Tukumbuke yaliyotokea kwenye Biblia Kitabu cha Mwanzo pale
Yakobo alipoenda kwa Mjomba wake Labani kuoa akimtaka binti mdogo amwoe kabla
ya dada wake. Labani alikataa akasema “HAVITENDEKI HIVI KWETU, KUMTOA MDOGO
KABLA YA MKUBWA; TIMIZA SIKU ZAKE SABA, NASI TUTAKUPA HUYU NAYE KWA UTUMISHI
UTAKAONITUMIKIA, MIAKA SABA MINGINE” (Mwa.
29:26-27).[60]
Kanisa
kwa nafasi ya pekee sana lina sauti ivumayo kwa nguvu sana. Likemee jambo hili.
Liweke vizuizi vya hapana kwa watoto kama hao. Na isitokee kwa vyovyote vile
ndoa kama hizo zikafungwa ndani ya Kanisa letu moja, takatifu, katoliki na la
mitume. Itakuwa aibu kubwa sana kufanya hivyo. Nilifurahishwa sana na tukio
lililooneshwa na chombo cha habari ITV juu ya uamuzi wa mahakama kuwakamata
wahusika wa ndoa kati ya vijana wadogo kabisa (mvulana alikuwa amemaliza darasa
la VII na msichana alikuwa darasa la VI). Jamii ililisimamia suala hili na
kuhakikisha linafika kwenye ngazi ya juu.
Na ndugu
wenzangu Wasukuma kuna mtindo wa msichana anapomaliza tu darasa la VII siku
hiyo hiyo masaa ya jioni jioni ananyakuliwa kama kifaranga kinyakuliwavyo na
mwewe. Tunaita “KUBOLWA.” Hapa ndugu Wasukuma wenzangu tumeshindwa, tuamke
sasa, tuzinduke, tutoke usingizini, tuseme hapana. Nilipo fuatilia suala hili
nilihakikishiwa kuwa huwa ni mpango wa muda mrefu kati ya mama na binti wake na
mpenzi wake mtarajiwa. Na bahati mbaya sana kijana wa kiume awe ameshampa na
Khanga mama wa binti, hapo hata binti angejifaragua namna gani ataenda tu. Wasukuma
wana msemo “ATASHENG’WA TU” huu hutumika pale ng’ombe anapokuwa mkali
kukamuliwa na mkamuaji anasema ‘ATAKAMULIWA TU.’ Anaweza kuhahikishiwa kuwa
hata nguo zake zimeshatangulia na nyingine zitamkuta huko. Wengine nilisikitika
zaidi kusikia kuwa hata kwenye mitihani yao ya shule za msingi waliambiwa
wajitahidi kutokufaulu na ole wao wangefaulu yangewatokea puani. Kumbe
waliandika andika tu! Bora liende.
v Magonjwa. Kadhalika kupenda vitu rahisi
imepelekea kuibuka kwa magonjwa mbalimbali, mfano: kisukari, presha,
kiribatumbo, ugonjwa wa moyo na mengineyo. Haya ni baadhi ya magonjwa
tunayojisabishia sisi wenyewe kwa kutojali afya zetu kupitia kazi za kufanyisha
mwili mazoezi. Maana ni katika kazi, afya ya mwili na akili inajengeka vizuri.
Kumbe tukirejea hata kwa Mwasisi wa taifa letu
Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika moja ya hotuba zake aliwahi
kusema “Kazi ni kipimo cha utu.”
Hivyo kila mtu anao wajibu wa kufanya kazi kwa manufaa au kwa ajili ya
kunufaisha mwili wake, katika kupambana na maradhi mbalimbali. Tuweni watu wa
kujituma na siyo legevu yaani eti tunajiita watoto mayai. Kumbe tuachane na
dhana potofu hiyo, tukijua kabisa hatunabudi kufanya kazi. Hii inatupelekea pia
kuungana na Mhe. Dr. John Pombe Magufuli
Rais wa amamu ya tano wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania katika sera yake ya “Hapa Kazi Tu”, nikiihusianisha na
umuhimu wa kwamba kazi au mazoezi ni afya.
5.3 Ulegevu katika Mila na Desturi
Lazima tukubaliane tu na hali yenyewe
kwamba, maisha ya sasa ni tofauti na ya zamani. Kadhalika namna ya kuelekeza na
kutoa maadili kwa zamani ilikuwa kitu cha lazima, ila kwa sasa hata wazazi
hawana muda wa kukaa na watoto wao kuwajuza juu ya mambo ya zamani. Na hapo
utaona kuporomoka kwa taasisi msingi ya malezi ambayo ni familia, kumechangiwa
na Utandawazi. Muda wa jioni au wa kupumzika wameketi barazani unakuta si Baba,
si Mama wala si Mtoto kila mmoja anaendelea na shughuli za mtandaoni tu. Wakati
kipindi hicho hata maswala ya Televisheni hayakuwepo na hivyo ilikuwa tu giza
likikaribia wanafamilia wote wapo Nyumbani na hapo hadithi ziliweza kusimuliwa
sana huku wakiendelea kuota moto. Siku watu wa nymba moja hawana muda wa
kuwasalimia watu wa ndani ya nyumba yao. Zaidi anaanza na aliyeko mbali nae.
Hello……umeamkaje ndugu yangu? Na pengine hata yule ambaye amelala naye
hajamwambia, umelalaje?
Malezi
bila mila. Ikitokea ukaulizwa
mila za kabila lako hususani zile zihusuyo malezi utaweza kujieleza? Swali hilo
naamini linaweza kuwa gumu, labda kwa wale wachache ambao wamekaa sana kijijini
katika malezi yao. Ila asilimia kubwa imepoteza mila hizo baada ya kupita
shule, yaani ni kijana ametoka chuo pengine kwa sababu ya kuingiliwa au
kuvamiwa na utandawazi anaona au kujiona hana hadhi ya kuongea tena na wazee.
Hali hiyo imesababisha vijana waliowengi kukosa malezi yaliyokuwa yanawaandaa
kuwa watu wazuri katika maisha yao ya baadae. Kwa mfano kulikuwa kuna mila na
desturi ya jando na unyago; hii iliweza kuwaelimisha vijana namna ya kuishi
vizuri katika maisha yao ya ndoa. Ndiyo maana hapo awali hapakuwa na migogoro
ya kifamilia sana kama siku hizi. Tuanze kurejea taratibu katika mila na
desturi zetu za awali ili kunusuru kizazi cha sasa pia cha baadae, na hii iende
samabamba na yale mazuri tu; mabaya tuachane nayo yakiwemo ya ukeketaji ambapo
hata kibiolojia kinachofanyika ni ukatilii. Tujishikamanishe na yale
yatakayojenga familia zetu upya.
Chanzo kikubwa cha kuporomoka maadili
ni kutowajibika ipasavyo kwa taasisi msingi ya malezi yaani familia. Wazazi
wengi sasa hivi hawajui wala hawatambui wajibu wao, anachojali tu ni kutafuta
riziki ya kila siku. Ni kweli ni jambo jema, ila inafikia ni Mama wa familia
eti kisa shughuli za utafutaji za hapa na pale anamaliza wiki nzima hajui
watoto au mtoto anashindaje nyumbani. Kwani yeye anachofanya anaondoka alfajiri
sana na kwenda katika shughuli zake akiwaacha watoto bado wamesinzia, wakati wa
kurudi pia anarudi usiku ambapo anawakuta watoto wameshasinzia; zaidi
akijitahidi atauliza mfanyakazi tu watoto wamesinzia wakiwa wamekula au wameoga?
Huishia hapo tu baada ya kujiridhisha kuwa hawajalala njaa, kuhusu malezi
mfanyakazi ndiye atakayefanya.
Kwa hiyo wazazi huwafanya wafanyakazi
wa ndani kuchukua majukumu mazito ya kulea kabla ya wakati wao, kumbe malezi
yanayotolewa hapo si rafiki sana ukizingatia ni mtoto analea mtoto mwenzake.
Pia kwa kuwa mzazi hana muda na watoto wake hata shuleni walimu wanabebeshwa
kulea watoto ambao ni wasumbufu sana, hawasikii wala kuambilikika; kwani malezi
bora na msingi yanaanzia katika familia. Sasa mzazi huyu ambaye amebanwa sana
na shughuli za utafutaji hata kumsahau mwanae kiasi hicho, unadhani ni lini
atapata muda wa kuongea na mwanae na kumsimulia maisha yaliyokuwa wakati wao?
Wazazi tujitahidi kuwa na kiasi pia kufikiria nini tunakijenga kwa watoto wetu,
maana unapoendelea hivyo ujue unamharibu mtoto kwani unampatia uhuru kabla
hajakomaa. Matokeo yake utaona mara ameshapata mimba, ana maambukizi ya virusi
vya ukimwi; kumbe yote hayo tunayababisha wazazi wenyewe.
5.4 Elimu ya Magharibi
Ninapoongelea elimu ya magharibi nina maana
ya elimu tuipatayo shuleni ambayo tumeipokea kutoka kwa wenzetu waliotutangulia
kimaendeleo yaani Nchi zilizoendelea. Sasa kama siku zote tusemavyo kila chenye
faida hakikosi kuwa na hasara. Ni kweli kwamba kile tunachokipata kinatusaidia
katika kuendeleza maisha yetu kwa vitendo pia nadhalia. Lakini siyo kila
tunachokisoma na kukielewa kwa nadhalia tukiweke katika matendo, maana kwa
kufanya hivyo ndipo tunaanza kupata matatizo mbalimbali.
Hususani masomo ya sayansi tunapaswa
kuyaelewa na kuyafanyia kazi kwa umakini wa hali ya juu. Kuna somo la Biolojia linamwelezea mwanadamu
kadhalika wanyama na mifumo yao yote namna inavyofanya kazi. Mfano wa mfumo wa Uzalishanaji unaongelea namna nzima ya
ile kazi tuliyopewa ya uumbaji wa pili (rej. Mwa 1:28). Sasa mwanafunzi
asiyemwangalifu akishajua ahaa! kumbe katika mzunguko wake wa mwezi kuna siku
ambazo yuko huru anaweza kushiriki ndoa ya kabla ya wakati na asidhulike, basi
anafanya mara ya kwanza kama majaribio akisema liwalo na liwe. Hivyo inapotokea
kweli hajapata ujauzito, siku nyingine atarudia tena na tena mwisho wa siku
akajikuta ni gwiji katika mchezo huo. Maana tunaambiwa kuwa sumu ya penzi
ukishailamba hata kwa maziwa huwezi kupona, na bandubandu huisha gogo; hivyo
inaweza kumpelekea hata katika ukahaba.
Elimu
bila tunu. Yaani
katika maisha ya kawaida tunatazamia kumwona msomi anafanya au akitenda
kulingana na alichosoma, sasa unapomwona msomi mfano mwenye shahada anatenda
sawa na mhitimu wa darasa la saba; mmh! hapo lazima kuna tatizo. Kwa maana
nyingine hakuna alichoambulia licha ya kusoma kwake, zaidi tutamwona kama
alienda shule kutembea au kukua shuleni. Ni kwa mantiki hiyo tunataraji kumwona
msomi akiishi na kuenenda kisomi katika maneno na hata matendo yake. Yaani kile
alichokisoma anakiishi na kuwafanya watu wengine waige kutoka kwake yale yote
ya msingi. Angalisho, siyo kusoma kwako sasa kukufanye uwadhalau wengine na
kuwaona hawafai hata kuishi kwa kuwa hawajui mambo mengi. Jitahidi uishi uasili
wako (be natural), usianze kujivisha pembe za majivuno mpaka kufikia kuwadhalau
waliokuwezesha mpaka kufikia hapo ulipo. Hivyo tujifunze kwa Albert Einstein
aliyesema ‘Elimu ni kile kinachobaki kwa mtu baada ya kusahau alichojifunza
shuleni.’ Hapa alitaka kutupa somo kuwa elimu siyo kile kilichoko kwenye
madaftari na vitabu bali kile kilichopo kichwani au kinachobaki ndani mwako na
ukakiishi.
Kwa hiyo wito wangu kwa wazazi,
wajitahidi kuwaeleza watoto wao kinagaubaga pasipo kumng’unya maneno hali
halisi ya maisha ya nyakati hizi na madhara yake. Na watoto nao tuwe tayari na
kuwasiliza wazazi wetu maana hao ndiyo Mungu wa pili hapa duniani. Hivyo kama
tukishindwa kuwasikiliza yale wanayotuasa maana yake hatuwaheshimu, kama
hatuwaheshimu tunajipunguzia miaka ya kuishi duniani; Amri ya nne ya Mungu (rej.
Kut 20:12). Pia tunaaswa kuwa asiyefunzwa na Mamaye hufunzwa na ulimwengu,
kumbe tuwe wasikivu siku zote na kupokea kile tunachoelezwa na wakubwa wetu.
Kila mtu asiwe wa kutaka kila kitu akisikiacho akionje au kukijaribu kwanza,
bali tuongozwe na busara na hekima katika kufikiri. Tuutumie msemo usemao
“Fikiri kabla ya kutenda” balabala, ukimaanisha kuwa kabla ya kutenda uwe
umeshaona faida na hasara zake. Na hapo ndipo ufanye uchaguzi sahihi.
Matokeo
hasi ya Elimu ya Magharibi
v Uasherati.
Kulingana na ufafanuzi wa kamusi ya
kisasa inasema kuwa ni kujamiana kwa hiari kati ya watu ambao hawajaoana (yaani
kati ya mtu ambaye hajaoa au kuolewa). Katika agano la kale, dhambi zote za
ngono ikiwemo uzinzi zilizuiliwa na sheria ya Musa na desturi ya wayahudi. Na
hivyo katika Kiebrania neno uzinzi lilitafsiriwa na kutumika katika mazingira
kama ya ibada ya sanamu.[61] Ndiyo
maana ukisoma 2 Nya 21:10-14 tunaambiwa kuwa Mungu alimpiga Yehoramu kwa
kuwaongoza watu katika ibada ya sanamu. Pia Ufu 17:1-2 tunaambiwa kuwa
uasherati umeenea duniani mwote. Hivyo basi kwa maisha ya sasa tumekuwa
tukishuhudia Kaka na Dada zetu walioko shuleni wakisahau na kupoteza dira yao
ya kuwa shuleni. Na matokeo yake tunawashuhudia aidha kabla ya kumaliza au mara
baada ya kumaliza tukiwa na matarajio makubwa juu yao, wanatuletea aibu katika
familia aidha ya mimba au magonjwa. Kwa nini niiite aibu ya mimba? Mimba
yenyewe kama yenyewe siyo mbaya na haina hatia, ila aibu yake iko kwa aliyebeba
mimba hiyo au aliyebebesha mimba hiyo; kwa maana imepatikana kimagendo yaani ni
haramu, kwa kuwa haijapatikana kihalali na kwa wakati husika.
5.4.1 Maambukizi
Tujiunge
na Frt. Richard Nyonga mwaka 2015, anayetoa ufafanuzi wa Maambukizi yatokanayo na mapenzi au tokeo la ngono si salama.
Maambukizi
ni hali ya ugonjwa kuenewa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine. Kuna
njia mbali mbali ambazo zinaweza kupelekea kuenea kwa ugonjwa kwa kasi zaidi
kama vile upepo (air borne diseases),
vijidudu, maji (water borne diseases), kugusana (contagious diseases), kufanya
tendo la ndoa nk.
o
Aina za
maambukizi
Magonjwa
yanayotokana na mapenzi yapo mengi sana. Hapa najikita kueleza yale
yanayosababishwa na vijidudu (viral
diseases). Maambukizi hayo ni kama yafuatayo:-
Ø Kisonono
Ugonjwa
huu huenezwa na vijidudu aina ya Gonococcae.
Wahanga katika ugonjwa huu ni wote wanaume na wanawake wanaoshiriki mapenzi na
mmoja wao akawa ni mwathirika tayari na yule ambaye kabla ya tendo la ngono
hakuwa mwathirika basi huwa yaani kwa tendo hilo, humwambukiza na mwingine.
Ugonjwa huu kwa asilimia kubwa huwakumba vijana wanao wekeza nguvu zao nyingi
katika mapenzi.
Ø Kaswende
Hii ni
aina nyingine ya maambukizi yatokanayo na mapenzi. Ugonjwa huu pia huhusisha
wote wanaume na wanawake pale mmoja kati ya washiriki anapokuwa ameathirika na
ugonjwa huo. Vijana hawako nje ya maambukizi hayo. Tungeweza kusema wanacheza
namba inayoongoza mashindano.
Ø UKIMWI
Ugonjwa
huu pia husababishwa na kufanya mapenzi japo sababu nyingine zinaweza kuchangia
kama vile kuchangia vitu vyenye ncha kali kama vile nyembe, kupewa damu ya mtu
mwenye virusi vya ugonjwa huo nk. Lakini kwa asilimia kubwa sana ni kwa njia ya
kufanya mapenzi na mtu mwenye VVU.
o
Mhusika/Wahusika
Ø Vijana
Ø Wanandoa
wachepukaji
Ø Wanaofanya
mapenzi kwa utafiti (sex for curiosity)
Ø Wanaofanya
mapenzi kwa biashara (sex for business)
Ø Wanaokaa
mbali na wenzi wao kwa muda mrefu mathalani madereva wa magari makubwa
Ø Wadada
wanao jiuza (dada poa) na akina kaka au baba wanaishi maisha ya ufanyaji ngono
na kila mtu
o
Hasara zake
Ø Maambukizi
haya yanaweza kusababisha utasa kwa mwanamume na pia kwa mwanamke na kumpelekea
asiwe na uwezo kabisa wa kubeba mimba kwa mfano, Kisonono.
Ø Pia mama
mwenye Kisonono, kipindi cha mimba mtoto atakayezaliwa kuna uwezekano mkubwa
sana wa kuwa kipofu asipopatiwa tiba mapema
Ø Mtoto
anaweza kuzaliwa amekufa (still birth) hasa kwenye gonjwa la Kaswende.
Ø Hasara
nyingine ambayo ni ya kiuchumi ni kupoteza hela nyingi sana kwasababu ya
matibabu kwa mfano, Kisonono kinapokomaa, mgonjwa huyo hasa wa kiume mirija
huziba na hupata shida katika kupata haja ndogo, hivyo mahitaji ya kimatibabu
ya hali ya juu huchukua hatamu
Ø Kifo na
vifo vingi katika jamii. Tumepotelewa na wapendwa wetu wengi sana katika jamii
kwasababu ya maambukizi haya
Ø Ugomvi
katika familia
Ø Kuvunjika
kwa familia mara baada ya kugundua kuna ukosefu wa uaminifu kati ya mwenzi au
kuogopa kuambukizwa hasa UKIMWI usio ponyeka
o
Mwarobaini
wa tatizo
Mwarobaini
pekee kwa tatizo hili ni kuvaa vazi la uaminifu, na kujiepusha na kufanya
mapenzi kabla ya ndoa au nje ya ndoa kwa wanandoa na kwa wasio na ndoa kuacha
kabisa kujihusisha na mapenzi. Ushauri mwingine, kwa wana ndoa ikigundulika
mmoja ni mwathirika, awe na upendo wa thati kwa mwenzake asiwe mfereji wa
kuiangamiza familia nzima. Wana ndoa wapime mara kwa mara ili wajue afya zao na
kuendelea kuishi kwa upendo kila mmoja akidhamiria kumlinda mwenzi wake na siyo
kuleta UKIMWI au maambukizi mengine nyumbani. Itambulike wazi kuwa ni kosa
kubwa kujua kuwa ‘umeathirika na unakomaa mpaka na mwenzako athirike pia, huu
ni uuaji wa kukusudia kabisa!’
o
Maoni
yangu na ushauri
Ø Elimu
siku zote ni ya muhimu sana, itolewe kuhusu maambukizi haya na namna
yanavyoambikizwa ili watu wajue kuyaepa si kiujanja ujanja (kwa mfano kutumia
mipira ya kiume na kike) bali kwa kuzingatia taratibu stahiki
Ø Tunu za
wanandoa zisisitizwe kwa wanandoa mfano, uaminifu, upendo wa dhati kwa mwenzi
wa mtu, uvumilivu nk
Ø Watu
wautumie vema uhuru wao maana uhuru usio na mipaka ni utumwa na uhuru wa
kufanya mapenzi bila kufuata mafundisho ya Kanisa na maongozi mema ya jamii ni
kujaribu kina cha maji kwa mguu wako mwenyewe
Ø Kanisa
liongeze na lipanue wigo wake wa kimafundisho ili liweze kuwafikia watu wengi
na kuwanusuru na hatari hii
Ø Kila mtu
awe mlinzi wa mwenzake
Ø Tusidanganyike
kwa matangazo lukuki ya baadhi ya vyombo vya habari vingine ni vya serikali
kabisa kuwa:-
1) Kuna ngono salama (kwa kutumia mipira-Kondomu)
2) Kuwa na mwenzi mmoja hata kabla ya ndoa
wakupozea injini (hapa ni kama kumpelekea mbuzi wako muuza supu), vipi kama
huyo mmoja uliye naye naye anawake mmoja hamtafika watatu?
3) Matangazo mengi yanapotosha umma. Fuatilia
matangazo ya PSI utagundua kuwa kuna viashiria vya kutumaliza. Wengine
wanasisitiza “kama kweli unampenda utamlinda. Mpenzi wangu nakupenda
nitakulinda na kinga nk, mimi na mwenzi wangu tunapendana na hivyo tunatumia
Kondomu-wewe je? nk”
5.5 Ukosefu wa vitu
asilia
Asilia ina maana ya mwanzo au halisi.
Kulielewa neno asilia ngoja tuone Waraka kwa Wafilipi inasema “Yesu
kwa asili alikuwa daima Mungu……” (Rej. Flp 2:6). Asili inaonyesha ni
kitu tangu mwanzo kilikuwa na namna fulani, na hapo Yesu anaongelewa kuwa ni
uhalisia kwamba tangu mwanzo kweli alikuwa Mungu.
Katika maisha yetu neno asilia limekuwa
likitumika kama kitu chenye kuhusisha mambo ya tamaduni. Mifano; utasikia
wakisema asili ya wachagga ni pesa tu, au asili ya wasukuma ni kupenda kula
ugali, pia mara asili ya Muha ni mtu wa kufanya kazi ngumu na mengine mengi.
Sasa uasilia ninaoongelea mimi umejikita katika hali ya ulaji wa chakula,
ambapo kila kabila au ukoo fulani ulikuwa unavyakula asilia walivyokuwa
wakivitumia kujipatia nguvu za kuendelea kuishi. Mifano; Waha walipenda kutumia
Ugali wa mtama na viazi vikuu kama chakula cha asili, Wachagga ni Kimbo
(huchanganywa ndizi na maharagwe); Wasukuma ni Viazi, Makande na Michembe;
Wahaya ni Ndizi; Wairaqw ni Ugali na Makande; Wapogolo ni Wali; Wapare ni
Makande; Wammalila ni Ndothani (viazi mviringo). Lakini sasa hivyo vyakula bado
wanavitumia? Jibu ni hapana vimeshaachiliwa, kupuuzwa na kutupiliwa mbali; kwa
kisingizio kwamba vimeshapitwa na wakati.
Ni katika ile hali ya kudharau vitu vya
maana vya zamani, ambapo imepelekea na kuchangia katika kushuka kwa maadili.
Moja ya madhara yatokanayo na upuuzwaji wa vyakula asilia ni Watoto kuanza
kubarehe mapema sana. Kibiolojia mvulana anaanza kubarehe akiwa na umri wa
miaka 14, na msichana kuanzia miaka 11. Sasa inatoa picha gani pale tunaposikia
vyombo vya habari vikitoa taarifa ya msichana kupata ujauzito kwa kulawitiwa
akiwa na umri wa miaka 8? Kwa hiyo itupe
somo kuwa vyakula hivi tunavyotumia vya kisasa vinasindikwa viwandani na
utunzaji wake unaambatana na utumiaji wa kemikali. Kadhalika tunapovitumia sisi
vinaenda kufanya vurugu na kemikali tulizonazo mwilini, na zinapounganika ndipo
zinaenda kuharibu baadhi ya mifumo ya ukuaji wa mwanadamu. Na madhara tunaanza
kuyaona mapema hata katika nyanja za ukuaji, kama ni msichana kufikisha miaka 5
tu tayari unaona baadhi ya viungo vyake vimeshachipua. Hali kadhalika kwa
wavulana inakuwa hivyo, yaani unakuta bado mdogo ila anafahamu mambo mengi ya
kidunia kupita hata wakubwa wake.
Tukumbuke vyakula asilia havikuwa
vinapita na kusindikwa viwandani au katika upandaji wake haukuwa wa kutumia
madawa ya viwandani. Kumbe kama sehemu ilionekana haina rutuba ya kutosha
waliweza kutumia mbolea asilia kama samadi
ambayo kwayo haikuwa na madhara kwa watumiaji. Sasa basi, kupitia mabadiliko ya
mapema watu wakiwa bado watoto; hata katika ukuaji wake ukifuatilia utaona
mabadiliko ya mwili yanatokea mara hata kabla ya kufikia ule muda wake. Hivyo
na kujikuta maadili kuporomoka bila kujua chanzo, kinachangiwa na ulaji wa
vyakula vya kisasa; ndipo tunaona kuwazia mapenzi wakiwa bado na umri mdogo.
Hatupaswi kuwalaumu sana ila kuwaelimisha namna ya kujikwamua katika janga hilo
pengine la ukahaba.
5.6 Uwajibikaji hafifu wa kila mtu
· Viongozi
wa Kiroho.
Mara nyingine tunaweza kuumiza na
kugongagonga vichwa vyetu tukitafakari ni kwa namna gani viongozi wa dini au
kiroho wamechangia katika ushukaji wa maadili. Huo ni ukweli usiopingika ya
kuwa kila mmoja anaowajibu wa kufanya kulingana na nafasi yake katika jamii
hata pia katika mazingira anayokuwepo kwa wakati huo. Lakini sasa tukumbuke
hamna mtu mwenye wajibu mkubwa sana hapa duniani kama kiongozi wa kiroho, moja
kwa moja hapa naongelea Mtawa, Shemasi, Padre na Askofu. Kwa nini naamua kusema
hivyo? Kiongozi wa mambo haya ya dunianai au kimwili anashughulika zaidi na
kitu kipitacho; ndiyo maana tunasikia mwili haufai kitu bali roho ndiyo itutiayo
uzima. Hivyo basi Padre kama kiongozi wa kiroho anatuelekeza na kutusaidia
kuufikia uzima wa milele.
Ni kwa mantiki hiyo tunajua ya kuwa,
Padre ni Kristo mwingine (Alter Christus); kama ilivyokuwa kwa Kristo kuwa kazi
yake kubwa mpaka kuja duniani ilikuwa kutukomboa sisi wanadamu: vivyo hivyo kwa
Padre naye anashirikishwa kazi ile ile ya Kristo ya kutaka kumkomboa mwanadamu
kupitia Mamlaka aliyopewa na Kanisa zaidi kabisa kupitia Masakramenti. Sasa
uchangiaji wa Padre katika dimbwi hili la mporomoko wa maadili ni pale kama
kiongozi wa kiroho anapoona watu wanaishi hali zisizompendeza Mungu na akaamua
kupuuzia au kukaa kimya tu; asitake kukemea na kukalipia. Hapo anaonyesha
dhahili na kuchangia maadili kuzidi kumomonyoka tu; kama tuonavyo ardhi ikimomonyoka
hususani kipindi kama cha mvua (masika). Pia ni kwa namna hiyo Mt. Maria Viane
aliona umuhimu wa Padre katika jamii na kusema “Mahali ambapo Padre anaweza
kupaacha kwa muda wa miaka 20, atakuta watu wanaabudu hata miti arudipo”.
Alisema hivyo kutuonyesha kuwa Padre katika mambo yahusuyo maadili na yote
yampendezayo Mungu yeye ndiye mtaalam haswaa!
Changamoto inaanzia sasa wapi mpaka
Kiongozi wa Kiroho asikemee? Katika somo la Litrujia Takatifu katika Utunzaji
wa Litrujia katika Seminari (In ecclesiasticum Futurorum: 1979) inasema juu ya
dalili kwa mseminari kuhusu jinsi ya kuundwa kwa nia mbili; kwanza: haja ya
kukuza maagizo sahihi ya makuhani wa baadaye ili waweze kufanywa zaidi ya
kuchagua kuelewa wazi tabia na nguvu ya Litrujia Takatifu mpya na hivyo
kuyafanya maisha yao ya kiroho na katika mwenendo wao wa kila siku na
kuwasiliana kwa uzuri na waamini. Hivyo wakati wanapoelewa huwapelekea
kujitambua wenyewe na baadaye kugeuzwa na kuwageuza watu wengine katika
mitazamao yao mibovu ya kimaisha.
Pili, msisitizo mkubwa juu ya malezi ya
Litrujia katika seminari unahitajika ili kukabiliana na matatizo mapya ya
mafundisho yanayotokana na kuongezeka kwa jamii; ambapo inapelekea watu kuamua
kuishi maisha watakayo. Mt.Tereza wa Culcuta aliwahi kusema kuwa “Mtu anatoa
kile alichonacho”. Pia mwanafalsafa mmoja (Ludwig Wittgenstein) katika kitabu
chake (Tractatus Logico) anasema “whatever can be said at all can be said
clearly and whereoff one cannot speak therefore one must be silent” Maneno yote
ya watu hawa yanataka kutufumbua na kututafakarisha ya kuwa; Imani bila matendo
imekufa, hivyo mfano mimi ningekuwa tayari ni Padre lazima tu iniwiye vigumu
kukemea kitu ambacho hata mimi kukiishi siwezi. Kwa mfano mimi nakuwa Padre
ambaye sina upendo kwa watu wote yaani wale niwajuwao na nisiowajua na hivyo
nakuwa na ubaguzi: nachangamkia wale ninaofahamiana nao tu. Sasa itakuwa vigumu
sana kusimama na kuwaambia wengine waishi upendo kwa kumwiga Kristo yeye
aliyetupenda upeo. Hivyo lazima nitaona aibu na kuamua kukaa kimya pasipo
kukemea. Na hapo taifa la Mungu litakapozidi kuishi kwa kujitenga na kukaa
mbali na Mungu: wakati mchungaji wanae ila hatekelezi wajibu wake ipasavyo mimi
kama Padre nitakuwa nahusika moja kwa moja katika kuliteketeza taifa la Mungu kwa kushindwa kumfasa Kristo
kiaminifu.
Sasa changamoto hii inatokea baada ya
Kiongozi wa kiroho pengine tangu akiwa bado mlelewa hakuwa makini na kufuata
kile anachofundishwa na walezi wake. Hivyo anapokuwa katika kituo cha utume
wake mambo kama hayo yanatokea tu kiurahisi. Maana wahenga walisema samaki
mkunje angali mbichi, sasa anapojikuta muda umeenda kuna vitu inakuwa vigumu
kusema anaaweza kuvipokea na kuvifanyia kazi. Licha ya kujua kuwa Binadamu hubadilikabadilika
(Man is dynamic).
·
Jamii nzima kwa ujumla.
Hatuwezi kuongelea jamii pasipo
Familia. Na hivyo jamii inaundwa na familia. Sasa ufanisi wa familia kiroho na
kimwili unategemea zaidi uwajibikaji baina ya wanafamilia; kwa kuwa msingi wake
upo katika kutimiza wajibu. Pale inapotokea kwamba, wazijengao familia
hawatimizi nyajibu zao, familia kwa ujumla na jamii nzima zinakosa mwelekeo
katika nyanja zote (kiroho, kijamii pia kiuchumi). Na matokeo ndiyo hayo
yanayopelekea yafuatayo kwa maadili kushuka na madhara yake yanakuwa makubwa
katika familia na jamii nzima.[62]
Ø Kuongezeka kwa matendo maovu katika
jamii kama wizi, ujambazi, ugaidi, ualawiti, ubakaji, n.k
Siku hizi yanazuka maovu yanayoathiri
maisha ya vijana na maisha ya weneye ndoa. Nayo ni mengi. Baadhi yake ni wizi,
utovu wa nidhamu, kukoseana heshima, ulevi, uasherati, makwazo kwa watoto;
kudekeza watoto; kuwakatili watoto, kukosa mahitaji ya lazima; maovu ya kuzuia
ama kuharibu mimba; magonjwa ya zinaa na mengine mengi.[63]
Ø Malezi duni kwa watoto. Ikumbukwe ya
kuwa malezi hafifu kutoka kwa wazazi na walezi pia yanapelekea uwepo wa watoto
wa mitaani, umalaya, uasherati, mimba za utotoni, matusi, uvaaji mbovu, dharau,
kiburi, uvivu, n.k. Na hivyo kupelekea washindwe hata kufikiria juu ya kuoa au
kuolewa kwa kuwa hawana elimu ya kutosha ya maisha ya ndoa. Maana kwa
kukosekana tu heshima, mtoto anakataa na kushindwa kumsikiliza mzazi au mlezi
wake anapokuwa anamweleza mambo ya kumjenga hapo baadaye.
Ø Vifo vya mapema. Tukumbuke kuwa siyo
kila kifo ni mpango wa Mungu; bali vingine vinatokana na mtu au mpango na
maamuzi ya mtu pale anapoamua kuishi maisha atakayo yeye, maisha yaliyokosa
hofu ya Mungu na hivyo anaachana na maadili. Mfano ni ajali zitokanazo na ulevi
wa pombe na madawa ya kulevya kwa baadhi ya madreva, harakati za utoaji mimba,
magonjwa ya zinaa kama UKIMWI. Hayo yote naweza kusema yanakamilika kwa ule
msemo usemao “asiyefunzwa na Mamaye, hufunzwa na ulimwengu”. Kwamba mtu
anaposhindwa kufuata yale anayoelekezwa kutekeleza au kufanya matokeo yake
ndiyo hayo kuwa lazima aingie katika matatizo makubwa, ni kwa matokeo hayo basi
alililia wembe nao umemkata; maana hakutaka kuwa msikivu kwa aliyoambiwa.[64]
Sasa wito wangu kwa wote baada ya kuona
changamoto hizo tena zilizo nyingi, kama Wakatoliki tunapaswa kuinuka kutoka
usingizini na tuanze kujikita katika kusoma maneno ya Maandiko Matakatifu. Kwa
mantiki hiyo tufanye neno la Mungu ndilo liwe chakula na kinywaji chetu, maana
ni katika neno tunajipatia hekima ya Mungu. Yatupasa kuifanya Biblia kuwa kama
Kitembea Nasi “VADE MECUM”. Ni vema kuhusianisha Biblia na matukio katika
Biblia na maisha yetu ya sasa. Mtazamo wetu unapaswa uwe wa kisasa hasa katika
kuwa na mazoea ya kufanya tafakari ya masomo katika Biblia ikiwezekana kila
siku iendayo. Mwisho, wote kama Wakatoliki na wakristu kwa ujumla tunapaswa
kuiga maisha ya watangulizi wetu hasa wale waliofanya mema katika ulimwengu
huu. Mfano huu bora tutaupata pindi tu tutakapofuata maisha ya watu wenye
kumfasa Mungu, na haya tutayapata pale tu tutakapokuwa na mazoea ya kusoma
Maandiko Matakatifu. Kwa kusoma Maandiko Matakatifu tutaweza kuona ni wapi
ulimwengu ulianzia, ulipitia na ulipo.
Thamani yetu machoni pa Mungu ni kubwa
sana; nasi tusiipoteze kwa matendo yetu maovu, lakini thamani hii itaweza kuboreshwa
endapo tutakuwa wenye kufuata mashauri ya Mungu, na mashauri haya hupatikana
kwa njia ya kutafakari Neno lake yaani Biblia. Zamani zile Mungu alinena na
wazee wetu na Manabii nao wakayaweka katika maandishi yale yote Mungu aliyonena
nao. Waebrania waliweza kudumisha uhusiano bora na Mungu kwani hawakuweza
kufahamu siku ambayo Mungu angeweza kuzungumza nao. Kadhalika nasi tunapaswa
kuwa na uhusiano bora na Mungu hasa kwa njia ya sala na matendo mema yenye
kujaa uangavu na maadili safi. Hatujui siku wala saa ambapo Mungu
atakayotuondoa ulimwenguni humu.[65]
SURA YA SITA
Kuna mambo mengi sana ambayo kwa sasa
yanaitesa dunia, na binadamu ndiye mhanga au mateka wa mambo hayo. Sasa tatizo
limeshajitokeza na lipo, nini tunapaswa kufanya katika kuinusuru dunia hii?
Maana katika uhalisia kamili yaliyokuwa yakifanyika kipindi cha sodoma na
gomora (rej. Mwa 19:1-28) pia kipindi cha Gharika kuu (rej. Mwa 6:1-22) ndiyo
sasa yameshaanza kushamili.
6.1
Utoaji mimba
Katika uuaji unaojikita katika Utoaji
mimba nauona kana kwamba ni uuaji wa makusudi kwa wasichana na baadhi ya
wanawake wa siku hizi. Ni kuua kwa
kudhamiria mtoto aliyemo tumboni mwa mama yake kwa njia yoyote ile na kutoa nje
vipande vipande vya mwili au mwili wote ukiwa maiti. Uhai wa mtoto unakatizwa
kabla ya kuzaliwa; mama anamkatalia mtoto wake haki yake ya kuishi, yaani kuwa
hai. Kwa lugha rahisi kutoa mimba ni kuua kama kuua kwa aina nyingine
tunayoweza kufikiria. Mara zote ndiyo maana unakuta wanatoa sababu kama hizi
ilimradi tu wajitetee: Afya ya mama, Mtoto anaweza kuzaliwa na ulemavu, Mimba hii imetokana na kubakwa au ni ya ndugu wa damu (Baba au Kaka),
Siko tayari kuwa na mtoto sasa, Naogopa mtoto atabadilisha maisha yangu,
Nimetelekezwa, Nimezaa watoto wote niliowahitaji.
Lakini mimi
nasema hamna sababu yenye mashiko, maana hata hiyo ya kiafya muda mwingine mtu
anaweza akadanganya ili tu aitoe mimba kwa kisingizio.
Maandiko Matakatifu yanatuhimiza sana
katika utunzaji na ulindaji wa uhai wa kila mtu. Kwa Msichana au Mwanamama hana
sababu yoyote ya kukatisha uhai wa mtu mwingine, isipokuwa Mungu mwenyewe
anapokuwa amempenda angali tumboni kumchukua yaani mimba kuharibika kwa
uhalisia.[66] Hivyo Mungu katika hilo anaafiki na
siyo kuharibu mimba kwa makusudi. Hivyo Mungu awachukia wauaji na wale wote
watendao maovu (rej. 1Tim 1:9; Ufu 22:15)
Tukumbuke kuwa hamna damu inayopotea tu
bure, hivyo anaethubutu kufanya hivyo hiyo damu itamlilia mpaka mwisho.
Tukiangalia Kaini baada ya kumwua nduguye Abeli, Mungu anamwambia Kaini “sauti ya damu ya ndugu yako inanililia
kutoka katika ardhi” (Mwa 4:10). Lakini pia tunaambiwa katika Maandiko
Matakatifu kwamba, hata zile roho wa wale walioko kwenye madhabahu ya Mungu
mbinguni yaani watakatifu wanalia wakisema “Ee Mwenyezi, Mtakatifu, mwenye kweli, hata
lini kutokuhukumu, wala kuipatia haki damu yetu kwa hao wakaao juu ya nchi?”
(Ufu 6:10).
Wachangiaji wa mauaji haya ni kila mtu
kulingana na nafasi yake aliyonayo. Kulingana na maelezo ya Frt. Audax
Ndalahwa katika juu ya Prolife (kulinda uhai) kuwa ‘Nani washiriki wa utoaji
mimba’ tarehe 03-04-2015; alikuwa na haya ya kusema:-
Akiongozwa na dhana hii “NAONA KIU” (Yn 19:28)
Kauli hii ni ya Bwana wetu Yesu Kristo
akiwa Msalabani katika harakati za kuutetea UHAI wetu, ukombozi wetu, utu na
thamani yetu tuliyoipoteza kwa sababu ya dhambi zetu. Ni kauli fupi kuliko
kauli au maneno yote (7) aliyosema akiwa Msalabani lakini ina uzito na ujumbe
mahususi sana kwetu leo. “NAONA KIU.” Kiu ya Yesu ni kutuvuta sote kwake, ili alipo
Yeye, nasi tuwepo. Yeye alisema, “Nami nikiinuliwa juu ya nchi, nitawavuta wote
kwangu” (Yn 12:32; 8:28). Mimi na wewe tuna kiu gani katika dunia hii? Je, ni
kiu ya kinywaji (moto/baridi), ni kiu ya kufaulu mitihani na kuwa wanafunzi
bora? Ni kiu ya kuwa tu padre? Ni kiu ya kuwa na mali na vitu vingi vya
thamani? Lakini zaidi ya hayo, naomba tujiulize jambo hili, “Mimi nina kiu ya
KUUJUA, KUUPENDA, KUULINDA NA KUUTETEA UHAI ULIO ‘ZAWADI YA MUNGU NA MALI YA
MUNGU?’” Tukiwa na Kiu ya kuulinda UHAI, karibuni tuchukue hatua.
Karibuni sasa tukiongozwa na neno hili
la tano (5) la hotuba ya Yesu Msalabani, tuwaangalie WAHUSIKA/WASHIRIKI WA
UTOAJI MIMBA.
Tujiulize maswali haya mawili kama gia
yetu yakuondokea:-
v Nani
hutoa mimba?
v Je,
mtu mmoja anaweza kutoa mimba?
Majibu ya maswali haya yanaweza
kutofautiana kutokana na mtazamo kati ya mtu na mtu. Karibuni sasa tusafiri
pamoja katika kuyadadavua maswali haya na kuyatafutia majawabu yake.
ü Kwanza ni SHETANI
Katika orodha ya wachangiaji wengi,
nimependa kumpa nafasi ya kwanza huyu mhusika. Huyu hutoa msukumo wa ndani
kabisa mwa mtu. Msukumo wake ni wa namna ya kupendekeza, kama vile mtu
anavyotoa ushauri kwa mwenzake. Shetani hutumia maneno lukuki matamu na yenye
mvuto mkubwa. Husema, ‘fanya tu chapu!
Kwa haraka na kwa wepesi, ni rahisi sana
kama kumsukuma mlevi, usiogope wewe
sio mtu wa kwanza kufanya hivyo, wengine wengi tu wameshafanya na
wakafanikiwa, kuwa mjanja-zeeka
mwili usizeeke mawazo na uamzi, usichelewe
kijusi hiki kinakua, utaaibika
mrembo, ona sasa unavyoonekana! Umekuwa ‘shapeless.’ Akisha kulainisha kwa maneno yake ya uongo yaliyo
katika ofisi yake ya “baba wa uongo” ( Rej.,Yn 8:44), hukusindikiza mwanzo
mwisho na akisha hakikisha kila kitu
kimeenda 100 kwa 100, yeye hutoweka na kubaki kando akijipa HEKO kwa utume
mzuri! Je, mimi na wewe leo tunachagua kumpa kampani Shetani katika hili? MIMI
SIMO, WEWE JE?
ü Pili ni MAMA/DADA MJAMZITO
Mama wa Mtoto. Mtoto yumo
tumboni mwake, ni mama yake kwelikweli; anafanya uamuzi (uwe wa hiari au wa
kulazimishwa); ndiye anayemwambia mganga ua mtoto huyu; simtaki.
Huyu
ni mshiriki mwingine mkubwa tu katika uovu huu usio vumilika hata chembe
kidogo. Kwa kweli mama/dada mjamzito ndiye anayekuwa na dhamana ya kubeba UHAI
ambao ni “ZAWADI YA MUNGU, MALI YA MUNGU.”
Lakini cha ajabu na cha kushangaza, ‘mbeba mkoba leo anadiriki kumiliki mkoba!’ Mkoba huu (UHAI) ni wa Mungu, amemkabidhi mama/dada huyu aushikilie bila mastahili. Amepewa zawadi ya kuulinda kwa muda mwafaka kwa ajili ya lengo maalum kuujaza na kuutawala ulimwengu agizo la kwanza kwanza kabisa la wazazi wetu wa kwanza (Rej., Mwa 1:28), ‘Zaeni mkaongezeke.’ Mshiriki huyu hufikia hatua au uamzi huu mbaya baada ya kusikia mashauri mabaya ya mshiriki nambari moja kama tulivyoona hapo awali. Amempa Shetani nafasi! Lakini amempa Mungu kisogo na kumwona hana jipya!
Lakini cha ajabu na cha kushangaza, ‘mbeba mkoba leo anadiriki kumiliki mkoba!’ Mkoba huu (UHAI) ni wa Mungu, amemkabidhi mama/dada huyu aushikilie bila mastahili. Amepewa zawadi ya kuulinda kwa muda mwafaka kwa ajili ya lengo maalum kuujaza na kuutawala ulimwengu agizo la kwanza kwanza kabisa la wazazi wetu wa kwanza (Rej., Mwa 1:28), ‘Zaeni mkaongezeke.’ Mshiriki huyu hufikia hatua au uamzi huu mbaya baada ya kusikia mashauri mabaya ya mshiriki nambari moja kama tulivyoona hapo awali. Amempa Shetani nafasi! Lakini amempa Mungu kisogo na kumwona hana jipya!
Anaichezea
kwa hiari kabisa au hata kwa kushinikizwa, zawadi ambayo si wote wamewapewa na
Mungu, ‘zawadi ya kuwa na kuitwa ‘MAMA (f).’ Kwa maneno mengine yeye husema,
‘UA KITU HIKI, FLASHI UCHAFU HUU, MWAGA OIL HII, SIKITAKI NA SIKIHITAJI! Na kwa
hali ya kawaida hutoa sababu lukuki za uhalalishi wa uovu huu, uhalalishi huu
huuitwa, ‘VISINGIZIO.’ Navyo ni pamoja na hivi: mimi bado ni msichana mdogo mno, sitaki kuwa na mtoto sasa, sitaki
kuitwa mama kwasasa, mwenye mtoto
(baba) amemkataa, bado niko masomoni,
nyumbani hawatanielewa, nitachekwa sana, nitazeeka mapema, nitakosa thamani (market-soko), nitashindwa
kula ujana, nitakosa kampani, nina hali ngumu ya kimaisha, sitaweza kumtunza
mtoto huyu, nilibakwa tu, aliyenipa mimba hii ni baba yangu mzazi (kaka yangu
wa damu), nina mtoto mchanga nitaambiwa ‘nazaa kama nguruwe/siyo mradi wa
kujivunia kuzaa haraka haraka na kwa wingi huo.’
Visingizio
vingine ni pamoja na; nimeipata mimba
hii nje ya ndoa-nitampoteza mume, wazazi wamenilazimisha kutoa, nimepata
mimba uzeeni. Na mengine mengi ya namna hiyo. Lakini tukubali tusikubali hakuna
hata kisingizio kimoja ambacho chaweza kuwa na uzito kama sababu ya kuuruhusu
mpango wa Mungu, kuupenda na kuulinda uhai utokao kwa Mungu peke yake.
MAMA/DADA Yesu alikuonea wewe KIU ili aukomboe UHAI wako. Je, wewe humuonei KIU
mtoto wako mwenyewe ili uje umwone siku moja alivyomzuri, akikulanda wewe/mume
wako/wazazi wenu? Isikie sauti hii ya huruma moyoni na kwenye dhamiri yako “NAONA KIU.”
Huyu
anaweza kuwa baba kwa maana halisi ya umri wake au kijana tu amepata mwanya huu
wakuwa mzazi. Huyu naye haepuki sura hii ya ushiriki/uchangiaji. Ushiriki wake
waweza kuwa wa moja kwa moja au kinyume chake. Anaweza kumshawishi mpenzi wake
kufanya hivyo, na hata akikataa kwakuwa yeye ameamua hivyo, anaweza
kulazimisha! Anaweza kushawishiwa pia na mpenzi wake juu ya uamzi huu mchafu
kabisa (ambao hata wanyama wadogo/walio chini yetu hawafanyi) kuchukua uamzi
huu nayeye kwa kujidai kuonesha upendo kwa mpenzi wake (kumbe upuuzi) anaafiki
na hata kutoa pesa kwaajili ya ufanikishaji wa adhma yao mbaya. Anaweza hata
akamsindikiza mjamzito wake kwenye kituo cha afya ili ahakikishe kweli kuwa
ameenda kutenda kama walivyokubaliana. Mchango wake ni ‘mchango-mtambuka,’
anaweza kushiriki kwa kumtelekeza mjamzito wake kama tulivyoona kisingizio
kimojawapo hapo juu. Lakini liwe liwalo, atakuwa ameshiriki vizuri kabisa
kufanya kitu kibaya kabisa (UUAJI). Kutupiana mpira kwa akina Adamu na Hawa na
Nyoka (Rej., Mwa 3:12-13), hupata mwendelezo hapa. Huyu naye hutoa visingizio
au sababu ili kuhalalisha uhitaji msingi wa zoezi hili bovu kabisa. Anaweza
kudai: bado sijafikia umri wa kuwa na
kuitwa baba sasa hivi, bado nasoma,
nitakuwa na mzigo mkubwa sana, huyu
dada/mama ni mwongo alipaswa kuniambia kuwa yuko kwenye siku zake za hatari,
amelikoroga mwenyewe acha alinywe (atoe mimba), nitafungwa jela (maana binti huyu ni mwanafunzi bado/ mama huyu ni
mke wa mtu), nitachekwa na vijana wenzangu, nitakosa kampani ya vijana wenzangu
hata wazee hawatanipokea maana mimi damu bado ya moto, nitapoteza wasichana wengi/wanawake wengi (kama ni mchepukaji), mke
wangu ataniacha na familia (kama ni mume wa mtu).
Kuna
sababu nyingi mno kama walivyo wavulana na wanaume wengi tu katika uso huu wa dunia.
Lakini hata hivyo sababu hizi zilizo hitimu kwa vigezo vya uovu kamwe haviwezi
kuwa na mashiko yoyote ya kupelekea kuutoa UHAI (kuua). ‘NAONA KIU.’ Kijana mwenzangu, ewe baba, kiu hii ilikuwa ya Yesu
kwako wewe, na ni kiu Yake kwa huyu binadamu mwenzako aliyetumboni mwa huyu
mpenzi wako. Je, unataka kumpa Yesu Siki kwenye Sifongo? Huoni Kiu ya kuyaona
matunda ya kazi yako? Unapenda kulima tu lakini hupendi kuvuna? Iruhusu basi
kiu ya mwanao mpenzi ya kumwona baba uso kwa uso itimie baada ya mwezi wa tisa
(9) ya kuwa kwenye tumbo zuri la mpenzi wako (mama wake).
ü Nne ni DAKTARI/NESI/MTOA DAWA
Huyu
naye ni mshiriki wa kitaaluma. Nimsomi na kioo cha jamii. Ni tegemeo la
wahitaji (wagonjwa), ni mtu anayeleta matumaini ya kuishi pale ambapo mtu
amepoteza matumaini kwa ugonjwa. Je, hufanya hivyo muda wote na kwa mtu yeyote?
Wewe mwenzangu unayetamani sana kuwa yeye (daktari/nesi) kwa siku za usoni, una
adhma hiyo? Napasua jipu. Ukweli umejidhihirisha kuwa, hapa na pale, kwa huyu
na yule wataalam hawa wamekuwa waharibifu. Mchango wa watu hawa mara nyingi ni
ule wa moja kwa moja na wakati mwingine (kwa nadra) huvaa vazi la watoa ushauri. Lakini ‘tuliite koleo ni koleo tu na siyo kijiko
kikubwa.’ Sababu, nia na kusudi la kumwita huyu mhusika “MUUAJI” tunayo. Hii
ni kwasababu yeye ndiye anayekamilisha nia ya washiriki 2 na 3 kuwa kitendo.
Kama ni vidonge (sumu) vyakunywa, ndiye anayevipitisha na hata kuvitoa, kama ni
kumkatakata binadamu mwenzetu ambaye hajazaliwa bado, yeye ndiye anayevaa
‘gloves’ na kushika mikasi tayari kwa kutekeleza uovu huu. Tunamlaumu sana
huyu, maana angeweza kusema ‘hapana,’ na hapana yake ikanusuru maisha ya
mwenzetu.
Kwa
taaluma yake, yeye ndiye anayetoa matumaini na kumwaminisha mtoa mimba kuwa,
‘utoaji wa mimba ni kitendo cha kawaida kabisa tena hakichukui muda, ni dakika
sufuri tu, hakina madhara yoyote, wala hakuna maumivu yoyote ni kama kutema
mate tu, hauumii bali unajisikia raha kwamba umetema mate.’ Kwa upande mwingine
mhusika huyu ni halali kwa lawama zetu kwani yeye ndiye anayemhadaa mama/dada
mjamzito kuwa ‘kilichoko tumboni siyo mtoto na hivyo siyo mtu, ni nyama nyama
tu, ni damu damu tu sawa kabisa na damu ya mwezi (hedhi), ni mnyama fulani
fulani tu, ni mlemavu nk.’ Ni huyu anayeitumia vibaya taaluma yake kwa
kuwadanganya wajawazito kuwa, ‘kiumbe hicho hakijaumbika, hakijaifikia hatua
stahiki ya kuwa mtu/binadamu kama sisi, ni kama kiluwiluwi chenye kichwa
kikubwa na mkia mdogo! Kwa haya na mengine mengi, mganga/daktari/nesi hakwepi
shitaka na kilio chetu watetea uhai kuwa ‘YEYE NI MUUAJI NAMBARI MOJA.’ Hata
hivyo, ‘NAONA KIU,’ bado ni sauti
tunayomuasa kuisikiliza kila mara, awe anakula, anakunywa maji, anatembea, ili
ikitokea hali inayotoa msukumo, ‘asimpe nafasi mwenye risasi bila bunduki kumpa
yeye risasi nakuitia kwenye bundukiye na kumuua mtu asiye na hatia’ (mjamzito
mwenye nia hiyo akija kumwomba ushauri asikubali kutenda jambo hilo).
Wapendwa sana wazazi wetu wana
ushawishi mkubwa sana karibu katika kila kitu katika maisha yetu sisi wana wao.
Katika mazuri na mabaya mchango wao haukwepeki, ama wayakemee mabaya (ushiriki mzuri) au wayanyamazie kana
kwamba hawayaoni (ushiriki mbaya).
Katika uwanja huu wa utoaji mimba, wazazi kwa ukali wao, kutokuwasikiliza
watoto wao, kutokuwasamehe katika makosa yao, kutokuwaelekeza namna ya kuingia
katika utu mzima n.k wanajikuta wako
kwenye bahari na siyo tu jito ya kutoa msukumo kwa watoto wao kufanya maamuzi
mabaya ya mauaji. Mathalani binti anajiuliza, ‘baba alivyomkali yule, nitabaki
mtu kweli? Kama alisikia tu niko kwenye mahusiano na fulani nilitishiwa kifo!
Sembuse hii leo nimeleta aibu ya kuwa mjamzito na ninasoma kwa pesa yake!’ Kwa
upande mwingine wa shilingi, binti anajiuliza, ‘ni kwa maneno gani nitamweleza
mama anielewe jinsi alivyokuwa mstari wa mbele wa kuniasa na kunikanya juu ya
kutokujihusisha na mapenzi mpaka akaapa kuwa ikitokea tu nimepata mimba
nitambue bayana kuwa sina mama na hapo ndipo utakuwa mwisho wa safari yangu ya
masomo nami nikaapa nikimdhihirishia kuwa kamwe sitamwangusha. Leo hii ninavielelezo
vyote na kiambatanishi vyakuwa nimeshiriki ngono, nina mama kweli? Nina shule
kweli? Na yeye ndiye baba na mama wangu?
Kwa hali ya kawaida, maswali mazito
kama haya humpelekea binti kuwa na msongo mkubwa wa mawazo, anakosa afanye nini
na mwisho hujikuta amekuwa ‘duka la
shetani’ maana ‘akili isiyo na
chakujishughulisha nacho, huwa duka la shetani.’ Na hapo mshiriki nambari
moja hutoa majibu kwanza, mepesi, marahisi, yanayowezekana (practical),
yanayomsaidia huyu binti kutoka katika hali hiyo kama tulivyoona mwanzoni. Pili
hushiriki vema kabisa mpaka kwenye ngazi ya kumwonesha njia, na
daktari/mganga/nesi aliyebobea/maarufu kwa shughuli ya utoaji mimba. Kana
kwamba haitoshi-humsindikiza binti huyu mpaka sehemu husika na kumpa ujasiri
wote, wote kabisa akijichukulia uoga wote mabegani mwake.
Jua lizamapo, binti huyu huishia kumwua
mwanae, labda mwanaye wa pekee kabisa (kama alikuwa na nafasi moja tu ya
kuzaa), msaidizi wake wa kesho, mtu wa kumlea na kumtunza uzeeni mwake,
kiongozi mkubwa tu wa dini au serikali n.k. ‘NAONA KIU.” Wazazi kuweni wazazi jua linapochomoza na jua
linapozama. Wapokeeni watoto wenu katika hali zote na muwasaidie katika
mafanikio na maanguko yao. Wahenga wanasema ‘mwanao akishika mavi, haumkati mkono la, bali unamnawisha vizuri.’
Au ‘nzi akitua kwenye maziwa yako,
chukua kijiti mtoe halafu kunywa maziwa yako.’ Hii yafaa kuwa KIU yenu kwa
watoto wenu na ustawi wa maisha yao.
ü Sita ni NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI
Hawa
nao ni wadau wakubwa katika janga hili. Mchango wa hawa ndugu ni ule wa
kumsaidia mtu kuingia kwenye majuto kamili kwa kumzomea kutokana na ujauzito
wake akiwa: mwanafunzi, msichana mrembo/mbichi/damu moto/mwenye mvuto kuliko
hata wao, mke/mshikaji wa mtu mwingine, bado ananyonyesha kichanga kingine, ana
umri mdogo mno (binti) au mkubwa mno (mama). Vitisho vingine ni vya kumtenga
kwenye kampani yao. Wakisha mfikisha kwenye majuto ambayo ni mjukuu, humpa
ushauri juu ya nini cha kufanya, namna ya kukifanya, muda wa kukifanya, sehemu ya
kukifanya na sababu ya kukifanya. Wao, Shetani, yeye (mhusika) pamoja na
Daktari hufikia mwisho la reli (kuua). Na hapo hata walio masikini huwa
matajiri wa kutoa pesa kwa ajili ya ufanisi wa zoezi zima. ‘Akufaaye kwa dhiki
ndiye rafiki wa kweli.’ Akikufaa katika kutoa mimba huyo ni ‘adui wa kweli.’
Utanishauri nisiue kama wewe unauchukia uuaji.
Hata
hivyo, ‘NAONA KIU.’ Bado ni sauti ya
mchungaji wetu Bwana Yesu kwao. Anawaonea kiu ya kuwatoa katika uovu wao,
anataka kiu yake ioane na kiu yao ya kuupenda na kuupa nafasi ya kwanza uhai,
‘Zawadi ya Mungu, Mali ya Mungu.’
ü Saba ni VYOMBO MBALIMBALI
(i)
BUNGE
Hiki ni chombo ambacho tunajua kina
fanya kazi ya kutunga sheria za nchi. Kumbe mchango wake katika janga hili la
utoaji mimba umejikita hapo hapo kwenye utunzi wa sheria za nchi. Hata hivyo
huko nako kuna watu siyo malaika wanaoifanya kazi hiyo ya utunzi wa sheria za
nchi. Ni walewale tulio waona hapo
mwanzo (baba/mama), na kama wamepotoka hawawezi kutunga sheria ambazo
zimenyooka na ziko kwa manufaa ya wananchi. “Hauwezi kuchuma chungwa kwenye
mpera, mtu au kitu hutoa alicho/kilicho nacho.’ Kama watuambiavyo Walatini, ‘Nemo dat quod non habet=No none gives
what he does not have=asichonacho hatoicho/hakuna mtu atoaye asicho nacho.’
Mchango wa Wabunge bungeni uko katika
kutoa miswaada ambayo hupitiwa na kuwa sheria baadaye. Miswaada hii ikipita na
kuwa sheria na kama iliruhusu utoaji wa mimba, basi hapo kuua huhalalishwa.
Wakati mwingine ni kushindwa kwao kutunga sheria ambazo huwalinda binadamu
wenzetu hawa wasio na sauti ya kujitetea (wachanga wa tumboni). Kwahiyo kwa
kutunga sheria mbovu au hata kulifumbia macho suala hili, mchango wao huwa wazi
kabisa kwamba ‘nao ni wauaji.’ Na kwa mantiki hiyo, “NAONA KIU,” hubaki kuwa mwaliko kwao juu ya kuchukua uamzi mzuri wa
kuulinda uhai wa ndugu zao. Binadamu ambao baada yao, wengine ndio watakao
ingia bungeni na kutunga sheria za kuwalinda wao wakiwa wazee. Wabunge na
mtakaokuwa Wabunge kesho, oneni kiu ya kuupenda uhai ulio ‘Zawadi ya Mungu,
Mali ya Mungu.’
(ii)
MAHAKAMA
Hiki ni chombo kinachosimamia sheria.
Huhakikisha kuwa sheria inakidhi mahitaji ya kuwa sheria kwa kila mtu, na
huhakikisha kuwa hakuna aliye juu ya sheria. Kwahiyo, chombo hiki hukakisha
kila mtu ana usawa na mwenzake kisheria awe mzee kabisa, baba/mama wa makamo,
kaka/dada, mtoto aliyezaliwa na aliyetumboni pia. Kinachoshangaza ni kuona
kwetu pale ambapotunaitegemea Mahakama kufanya kazi za namna hiyo na nyingine
nyingi za jinsi hiyo-hazifanyiki. Na pale ambapo hali iko hivyo, kinyume chake
hudhihirika machoni petu. Watu wengine kuwa juu ya sheria (mathalani viongozi
wa serikali na watoto au ndugu/jamaa na marafiki zao wa karibu pamoja na
matajiri). Kwa mtiririko huo kuna kuwa na wenzetu ambao hawana haki yoyote
kisheria, hawana utetezi (hususani watoto ambao hawajazaliwa bado na wale ambao
bado wadogo hawawezi kujitetea).
Kwa mhitasari, mahakama inaweza
kushiriki kwa namna zifuatazo: kushindwa kutoa hukumu zinazowalinda watoto,
kupitisha sheria ili itumikie maslahi ya watetezi wa kifo, kushindwa (kwa
kufumbia macho) kutoa adhabu kali pale ambapo utoaji wa mimba umetokea,
kuungana na watetezi wa kifo katika mauaji ya watoto wachanga.
Kilio cha Yesu, bado kinasikika leo
hii, “NAONA KIU.” Wakiruhusu kilete
mabadiliko mioyoni mwao. Ili nao wapate kiu ya kuisimamia vema sheria izuiayo mauaji
ya wapendwa ndugu zetu wasio zaliwa bado. Watoto hawa nao wanakiu ya kuuona
ulimwengu pamoja na ndugu zao. Ni haki yao msingi kabisa kuzaliwa kabla ya haki
zingine zozote (zingine hufuata baada ya hii).
(iii)
MASHIRIKA (mfano PSI, USAID, MARIE STOPES)
Kauli zao nyingi ni za ulaghai na uhamasishaji
mathalani “TUMIA KONDOMU, JIEPUSHE NA NGONO ZEMBE UKIMWI UNAUA.”
Mashirika haya yaweza kuwa ya Umma au
ya watu binafsi. Kwa ushawishi wake wa pesa yanaweza kufanya kitu ambacho ni
hatarishi kwa maisha ya mtoto aliyeko tumboni mwa mama yake.
Kwa kifupi sana haya huweza kushiriki
kwa njia mbalimbali. Baadhi ya njia hizo ni pamoja na:
· Kuhamasisha kupitia kampeni na programu
mbalimbali vitendo vya utoaji mimba.
· Kutumia fedha nyingi kuwateka watu
kifikra ili wakubaliane na uamzi na maadhimio yao.
· Kuziteka mamlaka za serikali, bunge na
mahakama kwa lugha ya ulaghai na fedha nyingi ili zitumikie itikadi za
utamaduni wa kifo.
· Kutumia lugha inayomfanya duni/mnyonge
binadamu aliye tumboni ili aonekane kuwa sio mtu na hivyo kuwa rahisi kumwua.
· Kutoa taarifa zisizo za kweli juu ya
wingi/idadi kubwa ya watu katika uso wa dunia, lengo likiwa ni kuhalalisha
utamaduni wa uuaji wa ndugu zetu walioko tumboni mwa mama zao.
Kwa hiyo, mchango wao mkubwa ni wa
ushawishi. Lakini ni ushawishi mbaya, usiolinda maslahi ya mtoto mchanga
aliyeko tumboni. Je, wakuu wa Taasisi hizi, dhamiri zenu hazisikii kilio hiki “NAONA KIU,” cha Mkombozi wetu Yesu
Kristo kwa kila mtu? Anaona kiu ya kila mtu kuishi huru, kwa amani kama
istahilivyo wana wa Mungu Baba yetu wa mbinguni.
(iv)
TAASISI NA ASASI
Sanjari na Mashirika mbalimbali, kuna
nafasi ya Taasisi na Asasi lukuki ambazo kama sehemu ya jamii, zinaweza kuwa na
mchango hasi katika ustawi wa maisha ya watoto wachanga. Na kwa mantiki hiyo mwisho
huwa ni mbaya (uuaji). Tuangalieni kwa mhitasari mchango wa Taasisi/Asasi:
Ø Kwa kuweka na kutekeleza
sheria/kanuni/taratibu za kuwafukuza wanawake wapatao ujauzito katika hali
isiyo rasmi (mwanafunzi au mke wa mtu nje ya ndoa yake) na hivyo huwashauri
kutoa mimba.
Ø Mgawanyo pendelevu wa kazi/ajira.
Kuwabagua wajawazito kana kwamba ujauzito ni kikwazo katika kufanya kazi (mfano
Bosi anayemfukuza katibu wake baada ya kupata mimba!)
Ø Kuna wakati pia wanawake wanakumbwa na
changamoto ya ajira zinazoendana na masharti mazito kwa madai ya wanawake wenye
maumbile fulani fulani tu. Hii huwa hatari pale wanawake nao wanapoingia moja
kwa moja katika utekelezaji wa vigezo na masharti hayo yanayohitaji
kuzingatiwa, na ikitokea mwanamke amepata mimba basi yuko tayari ‘kwa udi na
kwa uvumba’ kuitoa mimba hiyo ili abaki na umbo linalomruhusu kuendelea kukidhi
matakwa ya mwajili/waajili wake!
Ø Mitazamo ya kumwona mwanamke mjamzito
kama mzinzi nambari moja katika jamii. Hali hii hujitokeza zaidi katika Taasisi
za dini. Hii ni sababu nyingine ambayo nayo huchangia wanawake wengi kufikia
uamzi wa kutoa mimba ili wasiabike katika kanisa kwa kufananishwa na yule
mwanamke mzinzi katika Injili ilivyoandikwa na Yohane (Rej., 8:1-11).
Yesu anatuambia leo, “NAONA KIU,” kwaajili ya mabadiliko yako
ya ndani, ya kiroho na kimwili ili tuupende na kuuthamini uhai “Zawadi ya
Mungu, Mali ya Mungu.”
(v)
WANASAYANSI
Tunamshukuru Mungu kwa zawadi ya
wanasayansi katika dunia. Kwa upande wa wataalam wa mambo yahusuyo mimba na
mtoto mchanga na maendeleo yake mpaka kuzaliwa. Tunawashukuru sana kwa
kutufumbua macho na kutupa uelewa juu ya mimba inavyotungwa, kukua kwa mtoto
tumboni mwa mama yake. Kujua umri wa mimba/mtoto na jinsia yake
(wakike/wakiume), mzunguko wake tumboni mwa mamaye, kama ana ulemavu au la
anavyogeuka geuka tumboni nk.
Lakini sijui ni kwasababu ya sifa zetu
kwao ‘tembo wamelitia maji!’ Na
mwisho wake wameleta balaa, janga, tishio na hatari katika jamii. Na kwasababu
hiyo, hawa nao tunawatambua katika mtiririko wa wale wanaoshiriki kutoa mimba.
Tunaweza kusema kwa haki na uhuru kamili kabisa kuwa, “hawa ndio wanaotengeneza madawa au vifaa vya kutekelezea adhma ya wale
wanaotamani kutoa mimba.” Kwa upande mwingine tunausahihi kusema kuwa
“wasingelikuwa hawa wataalam kwa udadisi wao wa kujaribu jaribu hiki na kile,
kusingekuwepo na uhakika wa moja kwa moja juu ya utoaji wa mimba.”
Wamewadhihirishia watu kuwa, jambo hili linawezekana kabisa kwa asilimia mia
moja na halina madhara, mtu anaweza akatoa mimba kadiri awezavyo, ni rahisi
sana kama kumsukuma mlevi tu, ni jambo la kufanya ‘body cleanliness’ na hivyo hakuna cha kuogopa wala kustaajabia.
Kutokana nao tumekuwa na majanga mengi kama vile:
Enyi
wanasayansi, kumbukeni utalaam mlio nao ni zawadi kutoka kwa Mungu ambayo
hutokana na uhai aliowapa Mungu. Kwanini hamtaki dunia ijipatie wataalamu
wengine kutokana na watoto wanaozaliwa leo? Ndiyo maana sauti ya Kristo
inajirudia tena kwa huzuni zaidi, “NAONA
KIU.” Tuisikieni na tuwasheni mishumaa ya kuulinda uhai, “Zawadi ya Mungu,
Mali ya Mungu,” dhidi ya giza hili totoro la mauaji ya wapendwa ndugu, rafiki
na jamaa zetu.
(vi)
VIONGOZI WA DINI
Unaweza kunishangaa kwamba nimepata
wapi ujasiri wa kuwahusisha na viongozi wa dini katika mkanda huu wa mauaji.
Nisamehe ndugu yangu, lengo ni kuutetea uhai huu siyo kufunika kombe
mwanaharamu apite (kulinda sifa ya kiongozi kwa gharama ya kuutoa uhai), ili
kila mtu aulinde awe ni mtu wa dini au la! Wajibu uko palepale, “Ukiona chura anaruka mchana, ujue
anajambo/chura haruki mchana bila sababu,” wanatuambia Wanigeria. Kumbe
nami ninajambo ambalo nataka kukujuza. Viongozi wa dini wanahusika moja kwa
moja katika filamu hii ya utoaji mimba kwa njia zifuatazo:
Ukimya wao. Viongozi wa dini ni sauti ya wengi, na
‘sauti ya wengi (katika jambo jema) ni sauti ya Mungu,’ wanatuasa Walatini (vox
populi vox Dei). Kwahiyo ukimya wao badala ya kukemea usiku na mchana mauaji ya
watoto wachanga, huua mara dufu zaidi kuliko wahusika wengine. Maana ukimya wao
huwaacha waumini wao njia panda na huwaachia maswali mengi, mfano, “Je, kutoa
mimba ni dhambi mbele za Mungu?” Mbona sijawahi kumsikia kiongozi wetu akisema
chochote juu ya hilo? Akina Thomaso, hawajaisha makanisani. Mpaka wasikie
Paroko/Padri/Mchungaji/Kiongozi yeyote wa dini amesema nini ndipo watende bara
bara.
Kushindwa kutoa katekesi toshelezi. Tatizo hili hupelekea kudumaa au hata
kufa kwa dhamiri za waamini wao na hivyo kuhalalisha hata maovu kuwa mema ili
wayatende pasipo kusutwa na sauti ya Mungu mioyoni mwao.
Kwamfano, tunaweza kujiuliza maswali
kadhaa, “hivi watumishi wa Mungu (viongozi) walikuwa wapi wakati Bunge la
Uingereza, Marekani, Afrika Kusini ilipojadili kupitisha sheria za kuruhusu
kuwaua binadamu wachanga katika umri ambao wangehitaji kulindwa na kutetewa?
Kushiriki moja kwa moja. Hii ndiyo balaa kubwa zaidi kuliko
inavyodhaniwa. Imeonekana hapa na pale hata kwa kusikia maana asije mtu
akanishitaki kuwa kusikia tu haitoshi. Maandiko yanatuambia ‘imani huja kwa
kusikia’ (Rej., Rum 10:17). Tumesikia kuwa kuna baadhi ya viongozi wa dini
wameshiriki katika mapenzi na waamini wao, na ilipotokea kudhihirika kwa upendo
wao (tunda la upendo wa kindoa) wameishia kuficha aibu kwa kuvunja amri ya tano
(5) ya Mungu baada ya kuivunja ile ya sita (6). Tusikate tamaa wala tusione
kuwa ni jambo jema kufanya hivyo maana hata viongozi wetu wanafanya! Tuipeni
nafasi sauti ya Mungu isikike tena na tena katika masikio ya mioyo yao “NAONA KIU.” Na sala zetu zitawasaidia
kuisikia zaidi na zaidi. Inawezekana kabisa.
(vii)
MIMI NA WEWE
Ni imani yangu kuwa kama vile
ulivyonishangaa hapo juu, na hapa pia utanishangaa kwamba ‘hata mimi pamoja na
kuwachambua wenzangu, bado kumbe hata na mimi ni mmoja wao.’ Mimi ni muumini wa
falsafa hii, Sheria ni msumeno, hukata
huku na huko. Labda unaweza hata kuhamaki kuwa nimekushitaki kwa kosa
usilohusika au kujiuliza, ‘amenijuaje kuwa nilitoa mimba? Ametambuaje kuwa
nilimlazimisha yule rafiki wangu wakike kutoa mimba? Ni nani amemwambia kuwa
mimi ndiye niliyempa wazo na hata kumpeleka kwa mtaalam?’ Na maswali mengi ya
namna mbalimbali. Kumbe mimi na wewe tumo kwa namna ya pekee katika janga hili.
Hii ni kwasababu:
v Mimi na wewe tumekaa kimya asubuhi
mpaka jioni, Januari-Desemba. Lakini tunasikia mambo yanaendelea tena wakati
mwingine kwa watu wetu wa karibu kabisa. Lakini bado tumeogopa kuambiwa
“Kikulacho kinguoni mwako.” Tunabembeleza urafiki wa Kaysari!
v Mimi na wewe tumefumba macho yetu
tusione yanayoendelea lakini tunawafahamu wanaofanya unyama huu. Tumetumia
nguvu nyingi sana kuyawekea macho yetu mapazia meusi!
v Inawezekana mimi na wewe tumetoa fedha
kumsaidia rafiki yetu/mpambe wetu kutoa mimba. Tumemsindikiza au kumpeleka kwa
wataalam. Mimi na wewe tumekuwa washauri na watoa ushuhuda kuwa jambo hilo
linawezekana kabisa jambo la msingi ni kusema tu ‘NDIYO,’ tufanyeni haraka
iwezekanavyo!
v Tumemchukulia hatua gani ya kisheria
binti/mama anayetoa mimba? Tumemchukulia hatua gani ya kisheria daktari
anayeifanya kazi hiyo ya kutoa mimba na anafahamika mtaani kwetu? Tumemchukulia
hatua gani kijana wa kiume/baba anayewapa mimba wasichana/akina mama kana
kwamba anatoa ruzuku? Au ndo tumekuwa redio ya kumtangaza kuwa ni mtaalamu
sana, akimfanyia mtu habahatishi-bali ni kawaida yake.
Mimi
na wewe leo, Kristo anatualika kuisikiliza kwa utulivu mkubwa kabisa sauti ya
kilio chake msalabani, “NAONA KIU.”
Tuisikiapo sauti hii leo, tusiifanye migumu mioyo yetu. Tuifungue na tufanye
mabadiliko leo. Nasi tuwe na kiu ya kuwaona duniani hawa watoto wachanga,
wengine ni wadogo zetu na kwa wengine ni watoto wao wadamu kabisa.
Kumbe tujue
na tutambue kuwa, kitendo cha kushiriki tendo la ndoa lengo siyo kutuliza tamaa
za mwili bali kuendeleza uumbaji. Na hivyo inapotokea aidha mtu amepata mimba
bahati mbaya hana sababu yoyote ya kutaka kuiharibu mimba hiyo, zaidi mtu
akiwezakufanya hivyo basi anajaribu kukwepa majukumu tu. Tuwe mashahidi wa Kutetea Uhai, kutofumbia
Macho Ukweli, tuufichue ukweli, Kuandika, kuongea na kutumia vyombo vya habari
kutetea uhai. Muhimu zaidi Kusali na kuombea watu wabadilike. Kama nilivyotangulia kusema hapo juu mwenye
mamlaka ya kutoa uhai wa mtu ni Mungu pekee, vitu vingine vyovyote visiwe
sababu ya sisi kujichukulia mamlaka isiyotuhusu.
NINI KIFANYIKE? Kila mmoja
kwanza atambue Uhai ni zawadi kutoka kwa Mungu na ametutungia sheria ya kuwa
tuulinde. Mwandishi Benjamini Mbowe anasema, Ni lazima tujue sisi tumepewa tu
uhai tuutunze siyo wa kwetu, hivyo yatupasa tuulinde ipasavyo hata kwa gharama
kubwa.[67]
Pia tunaelezwa kuwa kuua au kujiua kunapingana na mapendo ya Mungu, hivyo kila
mmoja wetu atambue kuwa anawajibu tu wa kuutunza uhai; maana Mungu pekee ndiye
anayetawala uhai.[68]
6.2 Mapenzi ya jinsia moja
Kuna wakati kitu hicho kinanifikirisha
na kunikera sana ninaposikia baadhi ya watu wanadhubutu eti kusema ‘ndoa za
jinsia moja.’ Maana kiukweli kila nikazanapo kujitahidi kusoma vitu mbalimbali
ili kuongeza wigo wa kuelewa vitu katika karne hii ya 21, bado napata
kigugumizi hata kuthubutu kuungana na wanaosema ‘Mapenzi ya jinsia moja.’ Ni
kutokana na uhalisia kamili wa neno ‘Ndoa’ maana ni mahusiano ya Mume na mke
(jinsia tofauti) na daima kunapatikana zao la mahusiano hayo kama ilivyo asili
na utu wetu. Na hivyo maingiliano ya watu wa jinsia moja haipo katika kanuni
yoyote ya maumbile, labda kama ni zao la sayansi fulani na tafiti zilizofanyika
zikaleta zao hilo.
Hata hivyo ni kitu kisichoeleweka kwani
kinaenda kinyume cha asili (Nature). Sasa kama wanadamu tuko tofauti na wanyama
wengine wote kwa sababu tu kujaliwa akili na utashi, hivyo tunafikiri (Man is a
rational animal). Lakini sasa kama wanyama tu wengine walioko chini yetu katika
mambo yote na wahafikiri (Irrational animal), lakini hata siku moja sijawahi kuona
mnyama kakengeuka asili yake; yaani dume kaambatana na dume mwenzake au jike na
jike mwenzake. Na hivyo mfano huu utufumbue macho tena ili tuwezekuona vizuri,
kama wanyama hawajaweza kupingana na asili (nature) na hawafikiri. Je!
inakuwaje kwa mwanadamu anayefikiri kufanya vitu ambavyo hata wanyama wengine
hawajawahi kutenda na sina matumaini kama watakuja kutenda kinyume na asili.
Kwa mfano tumezoea kuona mtu ana miguu na mikono miwili, sasa ikitokea
akapatikana mwenye mikono mitatu kwa hali ya waziwazi tunaona ni kitu cha
ajabu, siyo kawaida (abnormal). Maneno yenyewe hayana hata radha kabisa kusikia
mapenzi za jinsia moja. Maana yake ni kwamba ni wapenzi wa jinsi moja (mwanaume
na mwanaume au mwanamke na mwanamke). Nashindwa nikuelezeje kwa undani mpaka
unielewe, lakini kwangu nasema ni ndoa za kishetani kabisa. Maana haimo katika
ile asilia ya Mungu, yeye aliwafanya mwanamme na mwanamke na kuwaunganisha kwa
tendo la ndoa. Kumbe kitendo kinachofanyika kiko kinyume na ile asili ya Mungu,
hivyo ni dhambi kama dhambi nyingine (rej. 1Tim 1:10). Licha ya baadhi ya
mataifa kupitisha kuwa haki kuanzia miaka ya 2000, zaidi ni nchi za ulaya na
Amerika mfano; Uingereza, Marekani, Ujerumani, Hispania na hata Afrika Kusini.[69]
Wewe unaenisikia jitahidi kupiga vita hiyo
mbaya na ya aibu sana ya kumkosoa vikali Mwenyezi Mungu (rej. Mwa 2:18-19; 23-24).
Daima ongozwa na Neno la Mungu, ndipo utaona ya kuwa tumesharudi sodoma na
gomora (rej. Mwa 19:1-8) pia gharika kuu (rej. Mwa 6:1-4), tunaonyeshwa kuwa
watu hao waliishi kama wanyama kabisa. Sasa nasi tumekwisha anza kuishi kama
wanyama, na hatari zaidi inayojitokeza ni kutaka kusambaza uchafu huu kila
taifa. Mataifa yaliyoendelea yanaanza kutoa masharti juu ya utoaji wa misaada
kwa mataifa yanayoendelea, wakiwataka ya kuwa ili wawape misaada au mikopo yenye
nafuu kwanza wahalalishe mapenzi ya jinsia moja, mara utoaji mimba pia upokeaji
wa vidhibiti mimba.
Sababu
na dalili zinazoweza kuchangia na kupelekea mapenzi ya jinsia moja
Kwanza kabisa ndugu zangu lazima
tutambue kuwa uchafu huu hautokei ghafla kama mwizi au kama unavyoweza kuona
mwanga pale tu unapowasha soketi, bali huanzia kabisa mwanzo wa makuzi ya
mtoto. Hivyo, mchango mkubwa unaweza kutokana na wazazi pengine kwa kutokujua
na kuwapatia malezi bora watoto. Zifuatazo ni baadhi ya sababu ambazo zinadaiwa
kupelekea na kuchochea mapenzi ya jinsia moja, wazazi wasipokuwa makini na
dalili hizo.[70]
v Zawadi
nyingi (zilizopitiliza) katika uhusiano wa Mtoto na Mama yake (A more rewarding relationship with
the Mother). Kama Mama anakuwa na utaratibu wa kutoa zawadi kwa wanawe (wa
kiume) mara nyingi, ina maana watapendelea kumpenda Mama yao zaidi. Tokea hapo
wanaanza kutengeneza aina fulani ya tabia kati yao, ambapo kuna ambao
watapitiliza ule upendo na kujikuta wanaanza kuwa na tabia za kike. Mara ni
mvulana anapenda kukaa karibu na Mama na kujikuta anaanza kutenda kama Mama
yake katika kupika, kuosha vyombo. Hapo hapo ndani ya watoto hao wapo ambao
watapenda kuonekana ndiyo wanaume, na hivyo inapotokea tofauti hizo kati yao;
wanaweza kujikuta wanatengeneza hali ya mvuto kati yao. Na hivyo kitakacho
tokea baina yao ndiyo laana hiyo tunayoaswa kuipiga vita.
v Upungufu
wa Baba wanaokalipia (Lack of
salient Fathers’). Hii ina maana ya kwamba Baba kushindwa kuonyesha ule uwanaume
(Masclinity) kwa vijana wake wa kiume. Kwa mfano kuna baadhi ya makabila
walikuwa na utaratibu wa Baba wa familia kuchukua mtoto wake wa kiume na kwenda
nae aidha kumwonyesha namna ya kushiriki kuchinja mbuzi, kuwinda na katika aina
yoyote ya utafutaji. Hii ilianza kumjengea mtoto huyo ile thamani ya kuanza
kuhisi ni mwanaume tangu mapema, japo aliweza kushirikishwa aidha kwa kushika
mguu wakati wa kuchuna ngozi na baadaye kupewa nyama ili azifikishe nyumbani.
Sasa kama Baba anashindwa kumtengenezea mazingira ya hivyo mwanaye na kujikuta
anaambatana na Mamaye muda mwingi, inaweza kupelekea tatito hilo kwa baadaye.
v Kushindwa
kuhimiza kujitawala na kufanya maamuziadilifu (Failure to encourage autonomy). Ina maana ya Baba
kushindwa kumulika kwa vijana wake ile hali ya uimara wa uwanaume katika kufanya
maamuzi. Hivyo Baba anapaswa kuwatengenezea na kuwamulikia vijana kwa kuwapatia
mazingira ya mahusiano ya kujitegemea, na siyo kujilegeza kwa mtoto wa kiume.
Kumbe, Baba anaposhindwa kumdhibiti mtoto wa kiume na akawa tepetepe au kijana
wa kujilegeza basi inaweza kumpelekea katika uovu huo.
v Kutokuwepo
kwa Baba katika familia.
Hali hii inapelekea katika matokeo kama ya kutegemea, ukosefu wa kukaguliwa
(assessor) au ukosefu wa uimara wa uwanaume katika familia. Hayo yote kwa
kuyazingatia Mama hawezi peke yake, maana yanategemea uwepo wa Baba. Sasa
anapokosekana watoto wanaweza kujikuta wameendana zaidi katika mambo ya jinsia
ya kike, ambayo ni hatari sana.
v Upungufu
wa shule za mchanganyiko (Lack
of co-education schools). Kwa namna ya kipekee watoto wanajikuta katika dimbwi
hilo wakiwa katika mazingira ya shuleni. Mfano wazazi wanaamua kumpeleka mtoto
shule ya bweni kuanzia chekechea mpaka kidato cha sita ni shule hiyo hiyo na ya
wavulana tu au wasichana tu. Sasa kupitia maisha hayo yanamnyima mtoto fursa
wanasema ya kusafisha macho, na mbaya zaidi kwa wale wa mjini zaidi ndiyo
inakuwa mbaya sana, mtoto anaporudi kwa ajili ya likizo anabaki ni wa kubaniwa
ndani; kama ni mwalimu anakuja kumfundishia humo humo ndani ya geti mpaka
anarudi shule ratiba yake ni hiyo tu. Hivyo, hata kisaikolojia anajikuta
anaathirika, kumbe wito wangu kwa wazazi wazingatie malezi bora pia watambue
kuwa malezi bora si shauri ya kumfungia mtoto ndani ya geti; ambayo mwisho wa
siku inampelekea kuitwa mtoto wa geti kali. Tubadili mitazamo yetu tafadhali.
Wito wangu kwa wewe msomaji unayesoma
kitabu hiki kikufumbue macho na kuona mbali zaidi. Utagunduaje kuwa umeanza
kuona mbali? Ni pale tu utakapoanza kupiga vita na kukemea kitu hicho kwa nguvu
zako zote, ambapo inawezakana katika kuelimisha watu ambao hawajapata nakala
hii ya kitabu ili nao waweze kutambua na kujiepusha na laana hii mbaya. Nimeamua
kuiita laana tena mbaya maana inakinzana na asili ya mwanadamu tangu kuumbwa
kwake. Nikiamini kwa nguvu zetu wenyewe hatuwezi, tuungane sote kwa pamoja
katika kumwomba Mwenyezi Mungu atuepushe na balaa hili, maana linazidi
kushamili kila mahali; licha ya kuona kuwa lilianzia kwa wenzetu Nchi
zilizoendelea. Pia tukumbuke kuwa hata wao wakati linaanza halikupokelewa
haraka na kupitishwa na serikali, vivyo hivyo nasi tatizo hilo limeshaanza japo
serikali haijahararisha au kuruhusu kitu hicho kufanyika hazalani. Tuendelee
kuliombea taifa letu na nchi zote ambazo hazijakubaliana na jambo hili chafu
wabaki na msimamo huo hata mwisho wa dahari.
6.3 Watu kuuza utu
Ninapoongea juu ya mtu kuuza utu wake,
nina maana ya kuufanyia mwili ambao ni hekalu la Roho Mtakatifu kama aina
fulani ya udharirishaji; kwa mfano wale wanaofanya biashara haramu ya ngono.
Haya ni baadhi ya mambo ambayo Mungu aliyachukia mpaka kufikia muda wa
kuangamiza watu wake kama kule Sodoma na Gomora, pia kipindi cha Gharika kuu.
Hivyo kadiri yanavyozidi kuenea kutoka mji na mji basi tusibaki kuyafumbia
macho tukemee kwa nguvu zote, maana ni dhambi na siyo kwamba kwa kukemea
tutakuwa tunawahukumu wahusika. Tukumbuke kuwa ukweli siku zote utatuweka huru (rej.
Yn 8:31-32).
Kwa upande wa wanawake wale wanaojiuza
au kuuza utu wao wanaitwa Makahaba, kitendo kinaitwa Ukahaba. Ukahaba limetokana na neno la kiarabu qahabatun
ikimaanisha malaya. Ukahaba ni tendo la kufanya ngono nje ya ndoa au uhusiano
unaokubalika katika jamii, tena na watu mbalimbali na kwa malipo.
Kwa nini niseme ni uhusiano
unaokubalika katika jamii wakati kitendo chenyewe hakifai? Kwa sababu kwa ndugu
zetu walioendelea zaidi kwao wamesharasimisha na hivyo ni kitu kinachoeleweka
na kukubalika hata na serikali zao. Tunaambiwa baadhi ya nchi hao makahaba kwa
kitendo hicho cha ukahaba kinajulikana kama biashara kama biashara nyingine
halali uzifahamuzo, mpaka serikali inajivunia kodi kupitia mapato ya watu hawa.
Sasa watendaji wanaopokea malipo huitwa kahaba au malaya; washiriki wanaotoa
malipo huitwa wateja. Lakini kama ukahaba unaendeshwa katika nyumba maalumu
mahali hapo panaitwa danguro.[71]
Aina
za Ukahaba. Kimsingi
kuna aina mbili za ukahaba; Malaya anajifanyia kazi mwenyewe na Malaya anafanya
kazi chini ya usimamizi wa mtu mwingine.
Ø Malaya
anajifanyia kazi mwenyewe.
Hapa tunajuzwa kuwa mtu huyu anaamua mwenyewe bila shuruti kufanya tu. Huyu
mara nyingi utamkuta akitembea barabarani, kusubiri kwenye klabu au kwa
kutangaza namba ya simu. Pia hata kupitia intaneti wanajitangaza na kukutana na
wateja mahali mbalimbali.
Ø Malaya
wanaofanya kazi chini ya usimamizi wa mtu mwingine au watu wengine. Hali yao inaweza kufanan na aina ya
ajira wakilipwa kwa kila tendo la ngono kutoka kwa msimamizi anayepokea fedha;
au wanatakiwa kutoa malipo kwake kutokana na mapato yao. Kundi hili mara nyingi
linapatikana katika danguro, lakini wako pia barabarani katika maeneo maalumu
wanapotazamiwa na kuwadia. Katika kundi hili kuna hasa aina ya utumwa wa
kingono, ambapo mabinti na wanawake wanalazimishwa kujiuza kwa wateja. Mwaka
2009 Umoja wa Mataifa ulikadiria kwamba 79% za watu wanaouzwa ni kwa ajili ya
biashara ya ukahaba, ambayo imekuwa hivyo biashara ya watumwa kubwa kuliko zote
za historia ya binadamu. Kila mwaka watu 800,000 hivi wanavushwa mipaka ya nchi
zao kwa ajili hiyo, wakiwemo hasa wanawake wale wenye umri chini ya miaka 18
wakiwa hadi 50%.[72]
Wazazi tujihadhari sana, usije ukakurupuka kumtoa mwanao kuwa anakwenda nje ya
nchi kapata kazi ya ndani, tambua wimbi hili linaendelea na kukua siku hadi
siku kwa sababu hiyo ya uwongo. Kwa hiyo mtoto anapofika huko ndipo anajikuta
analazimishwa kufanya kazi hiyo, kwa kuwa hana namna nyingine ya kufanya wala
hawezi kutoroka basi anajikuta ametumbukia katika giza hilo.
Watu hawa ni wale ambao siku hizi
kwenye miji mikubwa unakuta ikifika jioni wanatengeneza kijiwe chao kwa
biashara hiyo, na kila mmoja anabei yake kulingana na ule mwonekano wa nje wa
maumbile yake. Kwa mara ya kwanza ukisikia hivyo unaweza usiamini, maana
unaanza kujawa na maswali kuntu mfano: umeonyeshwa au umemwona hata mmoja wapo
wa wanawake wanaojiuza namna alivyo tu, utasema hivi huyu naye na urembo wake
amekosa mwanaume wa kumwoa? Au amepungukiwa nini mpaka ajidharirishe hivyo?
Hayo ni baadhi ya maswali ambayo unaweza kujiuliza baada kumwona au kuwaona
watu wa aina hiyo ya kujiuza.
Lakini tatizo kubwa siyo amekosa nini,
bali ni tabia yake ambayo imejengeka kupitia katika kipindi chake cha malezi.
Hivyo walezi wajitahidi wanao wazipitie hatua zote za ukuaji wa mwanadamu,
maana wakishindwa kufanya hivyo madhara yake ni makubwa sana kwa baadaye; pia
namna ya gharama ya kuweza kumsaidia inakuwa juu sana. Nimefanya utafiti wangu
kwa mji wa mwanza walio wengi wanafanyia biashara yao haramu pale mjini mtaa wa
makoroboi, pia katika mji mdogo wa
kasulu kijiwe chao kinaitwa makaburi wazi.
Kila mmoja anapaswa kupiga vita jambo hilo kama Mungu ambavyo hakulichekelea
bali kulichukia na kulipiga vita sana (rej. 1Tim 1:10).
Sasa kwetu ni biashara ambayo ni
haramu, yaani haijapewa utambulisho kamili na kukubalika. Lakini ukienda katika
baadhi ya mataifa inatambulika kama biashara halali, na hivyo serikali
inajipatia hata mapato kupitia biashara hiyo kodi ya ushuru.
Madhara
yake sasa hususani kiafya, siyo siri ni
chanzo kikubwa ambacho kinaweza kueneza maradhi mbalimbali ya zinaa kwa kasi zaidi.
Kwa upande wa akina Baba nao wanaojiuza
wanaitwa Mashoga. Yaani ni
vitu ambavyo hata kuvielezea lazima uone aibu maana siyo vitu vya kawaida
kuvisikia, maana vinazidi hata unyama. Kwa mfano; mimi sijawahi kuona mnyama
dume anamtafuta dume mwenzake, au mnyama jike anapoingia katika joto lake
hawezi kumtafuta jike mwenzake. Sasa hawa wanaume wanaotafutana wako katika
upande gani? Wafanyao mambo hayo wote wanadhambi sawa na wafiraji maana watenda hayo kinyume na maumbile (rej. Rum 1:24-27;
1Tim 1:10). Kwa hiyo mwanadamu anayeweza kutenda vitendo ambavyo asili (nature)
yenyewe inakataa, hiyo moja kwa moja ni kazi ya shetani.
Kadhalika mtu huyo haanzi mara moja tu,
bali tabia hii mbaya inaanzia angali mdogo sana. Hii imewaathiri zaidi wale
watoto tunawaita wa geti kali, kwamba ni mtoto yeye ni wa kutoka na kwenda
sehemu kwa kupelekwa na baada ya shughuli anarudi aidha kama ni mwanafunzi.
Kumbe kumjengea mazingira hayo ya kumbana sana, inafika hatua wazazi wanapokuwa
wametoka na kwenda sehemu basi nao wanabaki wakifanya yao. Kumbe chimbuko lake
mara nyingi yanaanzia ndani ya familia kulingana na mazingira aliyopitia katika
makuzi yake. Mfano; unakuta ni binti tayari ameshaolewa, ila kila anapofanya
tendo la ndoa lazima amwambie mmewe tena kufanyika kinyume cha maumbile. Kumbe
wito wangu kwa wazazi na walezi wawe makini na malezi wanayotoa, kumbana mwanaye
siyo suluhisho la yeye kujiepusha na majanga ya sasa bali kumfanya atafute
namna nyingine ya kuweza kujituliza na mahangaiko yake.
Pia kuna suala la usafirishaji haramu wa binadamu. Hili nalo liko mbioni kustawi kama
nyasi, maana kasi yake ni kubwa sana ya namna ya ushawishi. Tusiwe watu wepesi
wa kuamini kila mtu, ndiyo maana tunaaswa kuzijaribu roho, kwani siyo kila mtu
ni mwema au anakuwazia mazuri; wengine wanakuwazia mabaya daima na furaha yao
ni kuona umeshindwa (rej. 1Yn 4:1). Sasa tumefika mahali mtu anakwambia nataka
nikupeleke nchi ya Oman ili uwe unanisaidia kazi za biashara, sasa unachokosea
hauulizi hata swali; ila unachojua na kufurahia ni kwamba unaenda nje ya nchi.
Sasa matokeo yake uliyemwamini akiishakukufikisha anakupa kazi za
kukudharirisha mara ya biashara ya ngono, mara kufanya kazi za ndani kama
kijakazi; kwa kuwa huna namna wala jinsi unapambana na hali yako huko.
Tahadhari kwa wote, tafadhali tusiwe watu rahisi kiasi hicho cha kuonyesha
ushamba uliopitiliza. Mwisho wa siku umetolewa huku ulipokuwa unafanya kazi kwa
amani na kulipwa vizuri, sasa unakwenda kufanya kazi bila amani na malipo yako
ni majaliwa kuyapata. Wakijua ukilipwa tu basi unaweza kurudi nyumbani, hivyo
wanaamua kukukomoa. Sana sana hii imeathiri vijana wadogo ambao wanapelekwa
nchi za kiarabu wakiahidiwa kwenda kufanya kazi fulani, ila wafikapo hukuta
mambo yako tofauti na matazamio yao; tujiepushe na tamaa zisizo za msingi.
Tujihadhari sana maana ni ukiukwaji hata wa haki za binadamu kumgeuza mtu kuwa kama
biashara au bidhaa, yaani unaamua kumuuza au kuuza utu wake.
6.4 Imani potofu
“Basi Imani ni kuwa na hakika ya mambo
yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.”[73] Lakini katika Imani potofu inautofauti
juu ya yale wanayoyaamini, kwani yako kinyume na mipango ya Mungu. Kwa nini
nasema hivyo? Kwa sababu ni kupitia Imani potofu tunasikia mauaji, mafarakano
baina ya familia, ambapo vyote hivyo vinakinzana na mpango wa Mungu.
Matokeo ya Imani potofu kwanza ni uchochezi
wa mauaji. Tunasikia mauaji ya aina mbalimbali yanayohusisha Imani
potofu za kishirikina. Mfano; mkoa wa shinyanga mara kadha zimekuwa zikitolewa
taarifa za mauaji ya vikongwe wenye macho mekundu, kwa tuhuma za kuwa wao
ni wachawi. Pia mauaji ya ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi yaani Albino,
kwa tamaa ya kupata mali kupitia baadhi ya viungo vyao kukatwa au kuondolewa
kabisa. Lakini pia tumesikia mauaji yanayosababishwa na ushirikina ikidaiwa kuwa
kwa kupata kiungo fulani cha mtu utapata mali nyingi sana.
Haya yote yamechangia katika kuchelewa
kwa upatikanaji wa maendeleo ya sehemu husika, maana nguvu kazi yenyewe ndiyo
inazidi kuteketea. Sasa tujiulize kupitia vitendo hivyo je! kuna kweli ndani
mwake? Licha ya kwamba uchawi hata Biblia inautambua kuwa upo (rej. Ufu 22:15),
japo siyo kwa mantiki hiyo inayotumia mauaji eti kujipatia kitu fulani.
Pili ni kudorora kwa maendeleo. Ni katika Imani potofu sasa watu
wanaimani katika ushirikina, hivyo kuna sehemu mpaka sasa kama unajipenda
huwezi kujenga nyumba ya bati. Utaambiwa ukiijenga tu huwezi kumaliza siku
nyingi lazima wakuloge, ili wakuone sasa mali zako utaziachia nani na kufanya
wote mwonekane kama kitu sawa ndani ya jumuiya. Na wanasema maneno yanaumba,
kumbe kuna vitu vinatuharibu hata kisaikolojia. Mtu anapokwenda kwa mganga wa
kienyeji anaweza kuambiwa ukikutanisha macho na mtu fulani basi lazima uanguke
chini kwa sababu ndiye mbaya wako. Sasa kwa kuwa maneno yanaumba na kuchanganya
na hali ya kisaikolojia, kweli lazima hali itokee hivyo nawe upate kuamini. Kwa
hiyo unakuta ni kama unachezewa mazingaombwe tu au viini macho.
Imani potofu inaenda mbali zaidi kwani
kila mtu anayo namna ya kufikiri na kuelewa mambo, kama ambavyo Pd. Titus Amigu
anavyoeleza katika kitabu chake cha Ushirikina na Imani potofu. Kuna imani kali
zilizosambaa kati ya watu. Mtu akiamka amechoka asubuhi anasema
“wachawi” wamemfanyiza kazi labda amebebeshwa mizigo kama punda au kulimishwa
shamba la mwingine. Wengine wanaamini kwamba
gizani wamejaa wachawi, na hivi usiku si wakati mzuri kwa mtu. Wengine
wanaamini kwamba bundi, fisi na mbweha ni mifugo ya “wachawi”. Wengine wanaamini kwamba mtu kutembea uchi usiku ni
kitendo cha uchawi. Wengine wanaamini vigezo vingi vya “wachawi” hasa macho
mekundu, kibiongo, mapengo, kilema na uzee mkubwa. Haya yanawatia watu hofu na
hivyo wanaanza kuumwa kimwili au kisaikolojia.
Kama imani, wapo wengi wanaosadiki kila hadithi
inayosikika juu ya uchawi na ushirikiana. Kumbe hadithi nyingi zinazosimuliwa
ni za ubunifu tu. Ukikaba uthibitisho utagundua mambo. Hadithi zingine hazina
hata majina ya wahusika. Zingine hazitaji tarehe wala mahali zilipotokea. Labda
kuna mahali watu walifungukiwa mlango mlimani wakaingizwa ndani kujifunza kitu
fulani. Ukiuliza wapi na nani walikuwepo, utazungushwa tu.
Bado chini ya imani kuna mambo mengi wanayoamini watu
katika njaa yao ya kujipatia nguvu za pekee za pekee tu. Utawasikia watu
wakisema kwamba kuna watu wanaruka usiku, wengine kwa nyungo, wengine kwa fisi,
wengine kwa kuingia ndani ya pembe ndogo. kuwa na televisheni. Mambo mengine
yanayowafanya wengine waamini kwamba kuna “uchawi” ni matendo ya vichaa tu.
Utasikikia nimemwona mtu akikimbia msituni kwenye miiba bila kujali. Au kwamba
amemwona mtu akijikatakata na kujitoa damu. Sasa mambo kama haya ni matendo ya
kichaa. Ubongo wa mtu una mawimbi aina nne: alpha, beta, gamma na delta.
Mawimbi haya yakitibuliwa kwa sababu ya ugonjwa au kemikali fulani mtu huonesha
tabia za ajabu ajabu, tabia ambazo kwa waoga husema ni mambo ya kichawi. Kumbe
si hivyo. Zaidi ya hayo, kuna wengine hudhani kuna uchawi kwa sababu ya
kujikuta usiku wakipigwa, kukatwakatwa au kufukuzwa na watu au viumbe
visivyojulikana au pengine vinavyojulikana kabisa. Kumbe hizo ni ndoto maalumu
tu. Jina la ndoto hizo za kutisha ni majinamizi, nazo zisichukuliwe kama
ushahidi wa uwepo mambo ya “kichawi”. Ni mtindo mwingine wa ubongo kufanya kazi
kwa fujo kunakotokea usiku usingizini. Mambo ya kwenye mtima hujiibusha kwa
fujo kutokana na kuchozwa kwa ubongo ama na ugonjwa au kemikali zenye athari.
Mambo mengine chini ya imani ni mambo ambayo msingi wake
ni kudhaniana kusiko na misingi ye yote ile. Hapa utawakuta watu wakituhumiana
vijijini na mijini. Karibu kila mwenye mambo ya kushangaza anadhaniwa ni
“mchawi”. Mzee aliyeishi kuwashinda wenzake anadhaniwa “mchawi”. Mtu mwenye
mapengo makubwa anadhaniwa “mchawi”. Mtu mwenye kibiongo anadhaniwa “mchawi”.
Mtu mwenye macho mekundu anadhaniwa “mchawi”. Mtu mwenye masikio au vidole na
kucha za ajabu anadhaniwa “mchawi”. Na kwa jinsi hii, kikitokea kitu cho chote
kikubwa na kushangaza watatuhumiwa hao wanaodhaniwa kuwa “wachawi”. Mtindo huu
wa mambo si mzuri kwani unawaonea watu pasipo ushuhuda wo wote.
Halafu chini ya imani kuna mambo mengi tunayoyasikia au
kuyaona yaliyo mapato mabaya ya kuchanganya imani hasa upagani na Uislamu.
Katika upagani watu wanasadiki kwamba kwenye giza wamejaa “wachawi” na hao
wanatembea huko na huko kuwanga nyakati zote za usiku. Wapagani wanaendelea
kusadiki kwamba usiku “wachawi” wanaruka kwa nyungo, mikeka, pembe ndogo ndogo,
wanawapanda fisi kwa tumbo na kadhalika. Si hayo tu bali kwamba usiku “wachawi”
wanaitana kwa milio ya filimbi ambazo ni sehemu za siri za wanaume. Pia kwamba
wanafanya mikutano ya kupanga kuwaloga watu na kufanya karamu za kula nyama za
watu. Haya anapoyasadiki Mkristo anachanganya imani. Ukristo haufundishi wala
kuamini katika mambo kama haya. Uislamu unawaambia wafuasi wake kwamba uchawi
umefundishwa duniani na malaika Haruti na Maruti. Wenyewe wanasema kwamba kiasi
kilichofundishwa na malaika hawa ni asilimia kumi tu. Kwa hali hii, Waislamu
wenyewe huulizana, mambo yangelikuwaje kama huo uchawi ungelifundishwa asilimia
zote mia.
Mwishowe chini ya imani ni taarifa mbalimbali za filamu,
video, magazeti na maelezo ya watoto. Kuna mengi ambayo watu wanasadiki kwamba
yapo kutokana na filamu, video, magazeti na maelezo ya watoto. Wengine wakiona
picha za ajabu ajabu za filamu au video hudhani kwamba picha hizo ni ushahidi
wa uwepo wa “uchawi”. Watu hawa hawayajui mambo ya kompyuta. Kompyuta inaweza
mengi sana. Inaweza kutumiwa kuunganisha picha mbili zisizohusiana kabisa.
Ndipo inaweza kuweka pamoja picha mbili. Alipo mtu unaweza kuona baada ya muda
mfupi pana nyani. Au unaweza kumwona mtu ndani ya chupa na kadhalika. Haya yote
ni ufundi wa kuunganisha picha kwa haraka na wala si ushahidi wa uwepo wa
“uchawi’. Hali kadhalika video.
Mintarafu magazeti wala hakuna lo lote la pekee. Watu
wanaweza kuzusha habari za kutisha na vile vile kuziambatishia picha za
kutisha. Tufahamu wote kwamba magazeti ni miradi. Kila habari inayowavutia watu
inaweza kununuliwa ili kulifanya gazeti liuzike sana. Magazeti hasa yale
yanayoitwa ya udaku mathalani WATU, SANI, JUMATATU na IJUMAA huwa na habari
nyingi za namna hiyo.
Maelezo ya watoto nayo yanawapambisha moto baadhi ya watu
hapa duniani. Huondokea katika vitambo fulani vya maisha, watoto hujitokeza na
kuanza kuzungumzia habari za “uchawi” na matendo ya “wachawi”. Watoto hao husimulie
eti wanavyoruka usiku na wazazi au watu wengine kutumia fursa hiyo kuwaloga
binadamu wenzao. Maelezo ya watoto kama haya huwafanya watu wengine waamini katika uwepo wa “uchawi”
wakati si kweli. Kama tulilolisema kuwahusu wakubwa, tunasema hilo hilo kuhusu
watoto.
Ubongo wa mtu, hata ule wa mtoto mdogo hufanya kazi
katika mawimbi aina nne: alpha, beta, gamma na delta. Kumbe mawimbi haya
yakitibuliwa kwa sababu ya ugonjwa au kemikali fulani mtu huweza kuzungumzia
habari ya ajabu ajabu, habari ambazo kwa waoga husema ni ushahidi wa mambo ya
kichawi. Kumbe si hivyo. Wafuatilie watoto hao hao baada ya miaka walao
ishirini, uwaulize habari hizo hizo, watakukatalia na wataonea aibu kuhusika
nazo. Wengine wanaweza kukasirika kabisa ukiwaulizia habari walizozisimulia
wakati wa utoto wao kwani hakumbuki lo lote ukubwani mwao. Mimi ninamfahamu
walau mtoto mmoja ambaye alipokuwa na umri wa miaka mitatu hivi alikuwa akisema
mambo ya ajabu ambayo hata sisi wakubwa hatukuyajua ameyapata wapi. Kumbe baada
ya miaka ishirini hivi, tulipomuuliza habari zile zile alikuwa akikasirika sana
kwa vile alikuwa hakumbuki lo lote katika hayo tuliyomwambia kuwa alikuwa
akiyasema.
Pilikapilika
Chini ya pilikapilika, kuna pilikapilika nyingi ambazo
msingi wake si lo lote isipokuwa elimu ya siri. Watu hujielimisha habari za
siri kama vile vitu vinavyowavuta ndege kama bundi na njiwa, wadudu kama siafu
na nyuki na wanyama kama vile nyoka na simba. Basi elimu hizo za siri ndizo
hutumika kufugia au kuwaleta bundi, njiwa, siafu, nyoka na simba mahali. Bundi
hupenda mwanga na harufu za mizoga, hivi hufika po pote penye vitu hivyo.
Mwanga huwasaidia kuona panya na harufu huwasaidia kujua kilipo chakula. Hivi
anapoumwa mtu sana, si mara haba bundi kufika. Hufika hapo si kwa ajili ya mgonjwa
aliye mahututi bali kwa ajili ya ule mwanga ambao wauguzaji huwa nao. Yeye huja
apate kusaidiwa kuwaona panya. Aidha hufika hapo kwa sababu mara nyingi mgonjwa
mahututi haogeshwi na kwa namna hiyo anatoa harufu ambayo bundi hudhani ni
mzoga wa kula. Basi mahali kama hapo akifika bundi na kuimba wauguzaji hudhani
ameletwa na “wachawi”. Vivyo hivyo mgonjwa mwenyewe. Kumbe kwa dhana hiyo,
mgonjwa hujipandishia msukumo wa damu (BP) na kumfanya asifike asubuhi. Ndipo
mgonjwa akifa, wauguzaji na jamaa huanza patashika ya kumsaka “mchawi”
aliyemuua mgonjwa. Wapi na wapi! Njiwa hufugwa kwa chakula. Nyoka na simba
huletwa mahali kwa majani yanayonukia kama nyoka au simba jike. Kwa kuvuta
nyoka huko Iringa hutumiwa majani ya mti unaoitwa mgegeluka. Kwa simba kuna
majani yake. Kwa siafu ni chakula kile wanachokipenda. Kwa nyuki ni mpako wa
asali yao. Mambo ya elimu ya siri hayaishii kwenye kuwaita ndege na wanyama tu.
Wawindaji hujua kwamba kila mnyama dume ana eneo la milki yake. Ukipiga mluzi
wa aina fulani mwenyewe atakuja pale kuangalia nani anatia fujo. Hapo mara
hupigwa risasi au kupigwa mshale au mkuki. Aidha vifaru huchukia moto na
ukiuwasha ni sharti waje kuuzima. Nyati huchukia mlio wa aina moja kwa mfano
mungurumo wa gari linalozizima. Bais moto humvuta kifaru na mungurumo wa
kuzizima humvuta nyati.
Katika kutabiri mvua, mambo ni ya namna hiyo hiyo.
Wanaojidai kutabiri mvua hutaza mawe. Wakiona yana unyevu, huwaalika watu
watolee sadaka. Kumbe ule unyevu ndio unaowaambia kwamba anga na mawingu
yamejaa unyevu ambao punde utaanguka kama mvua. Kwa hali hiyo wao hawanyeshi
mvua ye yote isipokuwa ni mabingwa wa kujua lini mvua imekaribia kwa kadiri ya
maandalizi aliyoyafanya Mungu mwenyewe. Mvua ni chini ya Mungu mwenyewe na wala
si chini ya binadamu fulani. Ndiyo maana wale wanaojifanya wanyeshaji mvua,
hawawezi kufanya lo lote jangwani, mathalani huko Sahara, mahali ambako Mungu
haandai mvua kama anavyofanya katika sehemu nyingine za dunia. Hatimaye, elimu
ya siri ndiyo inayotumika katika utengenezaji wa televisheni zile zinazoitwa za
asili. Wakati baadhi wakitumia nuru za maji, vioo na vivuli wengine hutumia
pombe kali. Basi katika maji au vioo taswira hubanwabanwa na kumghilibu
mtazamaji aone kile alichoambiwa atakiona. Zile televisheni za asili
zinazotengenezwa kwa pombe kali huwalewesha watu. Kutokana na kulewa, watu
huona mambo yasiyokuwapo katika uhalisia.
Chini ya
pilikapilika kuna mengi yaliyo na msingi wake katika matisho ya waoga. Lishe ya
mambo ya kishirikina ni woga. Mtu anayesadiki katika mambo ya kishirikina huwa
“amelogeka” walao kwa asilimia hamsini. Mtu anayemwogopa mtu fulani, akioneshwa
kidole na yule anayemwogopa au akiambiwa naye, “kesho utakufa”, hushikwa na
kihoro na kihoro hiyo hugeuka ugonjwa wa mwili au wa moyo wa kumkatishia maisha
yake. Woga unaua. Kwa Waislamu hilo ni wazi kabisa. Shughuli za albadiri (dua
mbaya) hupata nguvu katika woga wa mlengwa. Mwislamu akiambiwa atasomewa
albadiri, hushikwa na kihoro cha mwaka. Halafu akisomewa kweli, huvunjika moyo
na kudidimia nguvu yote. Ndipo mtu hufa. Kumbe kwa watu wasio Waislamu, labda
Wakristo wasiokuwa na woga huo, albadiri hushindwa kabisa kufanya kazi kwani
haiwatishi hata kidogo. Katika woga, watu wanaogopa mengi. Ukimchukua chura
ukamfunga kitambaa chekundu kiunoni na kumweka chumbani kwa mwoga atashikwa na
woga mkubwa kabisa. Kesho yake ukimwekea mjusi aliyefungwa miguu na kuwambwa
msalabani mwoga atatishika mno. Asubuhi yake ukimwekea budi aliyevikwa shanga
shingoni, hata kinyesi kitamtoka. Ukizidi hapo ukamwekea furushi lililochomekwa
manyoya marefu, mtu yule atatishika hata kiasi cha kuhama kijiji au mji.
Kuna pilikapilika zingine ambazo msingi wake ni matumizi
ya mapaji ya pekee ambayo wachache wamejaliwa hapa duniani. Kuna watu fulani
fulani mathalani hawadhuriki na nyuki hata wakiumwa na nyuki elfu. Aidha wapo
wengi hata wakipigwa na umeme volti 380 hawadhuriki. Idadi ya watu hao ni ndogo
sana, labda mmoja kati ya elfu. Wakiamua kutumia mapaji ya namna hiyo kwa
manufaa yao huweza. Hakika watu kama hao huweza kufanya vituko kadha wa kadha
ambao sisi wengine huhitimisha kwa dhana ya kwamba ni “wachawi”. Wasiodhurika na nyuki huweza kulala hata na
nyuki au kuwachukua nyuki katika magunia kana kwamba wamechukua inzi. Wale
wasiodhurika na umeme wa kiasi kikubwa kama nilichokitaja huweza kuchezea nyaya
za umeme kiasi cha kutustaajabisha wewe na mimi na hata kutembea juu ya waya wa
umeme bila viatu. Basi wengine wanapoyaoona mambo kama hayo hutishika na kwenda
huko na huko kutangaza kwamba wameupata ushahidi wa uwepo wa “uchawi” kumbe sivyo.
Katika pilikapilika kuna mambo mengi tunayoyasikia au
kuyaona yenye msingi wake kwenye mbwembwe zilizoongezwa kwenye dawa za kawaida
tu. Dawa za asili si mbaya kwa zenyewe. Mungu ameziweka kwenye majani, miti,
mizizi na vyakula ili zitutibu na kuturejeshea uzima uliotetereka. Hakuna mtu
mwenye busara anayeweza kuzidharau (rejea YbS 38:1-14). Hata hivyo kuna waganga
wengine wanaoongeza mbwembwe nyingi na za kutisha ili waongeze bei ya dawa zao
na wao wenyewe wajipatie umaarufu. Dawa ya tumbo la kawaida la kuhara ni pamoja
na kutafuna majani machanga ya mpera na kunywa maji yaliyochanganya kidogo na
udongo wa mfinyanzi. Lakini kwa dhamira ya faida binafsi, waganga wengine
huanzia kwenye kuwaeleza watu kwamba wametiwa vitu mwilini, machoni au
masikioni. Ndipo unapoweza kuwasikia watu wakiambiwa eti wametiwa mahindi
machoni, au misumeno magotini, au vyungu matumboni na watu wanapikia pombe
humo. Basi waganga hao hujidai kufanya madhehebu ya kuvitoa vitu hivyo pale
wanaposema vimewekwa. Kwa kelele, kuimba na miruko wanafanya udanganyifu wa
kutoa mahindi machoni, au msumeno magotii au vyungu matumboni. Ajabu ya watu
tunaoamini ushirikina ni jinsi tunavyoshindwa kujiuliza maswali mengi. Chukulia
suala la mtu kuwekewa kitu mwilini. Mbona mtu ukiingiwa na mchanga mdogo tu
machoni, huwi na raha hadi mchanga huo upulizwe nje? Mbona mtu ukichoma mwiba
mdogo kidoleni, huwi na raha hadi mwiba huo mdogo utolewe? Iweje basi mtu awe
na punje za mahindi machoni au msumeno gotini na chungu cha kupikia pombe
tumboni. Tunaaminije jambo kama hili?
Katika pilikapilika kuna mambo mengi tunayoyasikia au
kuyaona yenye msingi wake kwenye namna za kuloga. Utawakuta watu wakijaribia
kuwaloga wengine. Kati ya formula zilizopo za kuloga nyingi zinatumia vitu vya
yule anayekusudiwa kulogwa, mathalani mate yake, nywele zake, nguo zake na
kadhalika. Au zinahusisha vitu vilivyogusana naye, mathalani mchanga
alioukanyaga na kuacha nyayo au maji aliyoyaoga. Vitu kama hivyo wakivipata,
wenyewe wanaojidai walozi, huvifutika kwenye kitambaa na kuvidunga sindano huku
wakitoa dua mbaya, kwa mfano, “Huyu mtu apatwe na kifo ghafla” au “Huyu mtu
apatwe na maradhi yasiyopona, augue na kuugua””.
Basi kwa ajili ya kubahatisha kuloga hivyo, utawaona au
utasikia jinsi watu wanavyotafuta vitu vya wenzao kama hivyo tulivyovitaja sasa
hivi. Wengine wanachotwa mate usiku, au wanakatwa nywele usiku au nguo zao hasa
zile za ndani zinaibiwa, nyayo zao za mchangani zinachotwa au maji waliyoyaoga
yanachotwa huko bafuni au chooni. Sasa, ndugu yangu, ukiyaona au ukisikia mambo
haya yanatendeka usidhani kuna nguvu zo zote za pekee hapo. Ni kusumbuka na
upepo tu. Hakika kama mtu akavichukua vitu vyako na kufanya hivyo, wakati wewe
huna habari, huwezi kudhurika wala chembe. Lakini ikiwa umegombana na mtu na
mtu yule amekutisha hadharani wakati wewe unaoogopa mambo ya kishirikina,
nakwambia utaanza kweli kuugua. Utaanza kuugua, si kwa sababu ya nguvu ya pekee
isipokuwa kwa sababu ya woga wako mwenyewe. Kifupi, utaanza kuugua kisaikolojia
kwani chakula au mbolea ya mambo ya kishirikina ni woga wa yule anayetishwa. Anayetishwa
akiwa mwamba wa kujiamini matisho yale huwa kama ngumi ya mtoto ukutani. Basi
uwe mwamba wa kujiamini, ndugu yangu.
Wengine huhangaika sana wakiona nywele zao zimenyolewa
usiku au nguo zao za ndani zimetoweka. Hupita huko na huko kuulizia. Kwa vyo
vyote, ndugu yangu, ukipatwa na mambo kama hayo ujue mtu anayekufahamu au mtu
aliye karibu nawe nyumbani au chumbani amehusika. Kama unataka kumwita “mchawi
wako” wala usimtafute mbali. Ni huyo huyo mwenzi wako au jirani yako. Huyo huyo
yumo katika mradi mbaya dhidi yako! Mtu wa mbali asiyekufahamu au kukukaribia
hawezi kukufanyia vituko kama hivyo. Wala wewe huwezi kwenda mbali kama New
York, usiku na kufanya vituko kama hivyo. Au mtu asiyeishi Washington au Marekani
hawezi kumfanyia Raisi wa Marekani vituko kama hivyo. Hata White House yenyewe
ilipo haijui! Au hawezi kumfanyia Malkia wa Uingereza, hata Birmgham Palace
yenyewe ilipo hajui!
Tuzidi kuongea. Katika pilikapilika kuna mambo mengi
tunayoyasikia au kuyaona yenye msingi wake kwenye mazingaombwe. Unajua,
mazingaombwe yakiwa rasmi wanaoyafanya hujipatia fedha za viingilio
wanapoyaonesha. Wafanya mazingaombwe wanafanikisha shughuli zao kwa njia tatu.
Kwanza kabisa, wao huua macho ya watu yasiweze kuvifuatilia vitendo vyao vya
kijanja. Basi ukiwaona wanawakazia watu macho na kusema, “pache pu” wanakusudia
hilo. Nakwambia hawaanzi kucheza mazingaombwe yao mpaka hilo la kwanza
lifanyike. Kwa watoto hili linafanyika kirahisi sana. Kisha kuyaua macho,
wanakuja na la pili, ndiyo kufanya vitendo kwa haraka sana. Wao wanaweza
kuyafanya mambo mawili au matatu wewe katika kufiwa macho ukaona kitendo kimoja
tu. Kishapo kuna la tatu lao. Ni matumizi ya dawa fulani fulani, lakini si dawa
zenye nguvu za ajabu sana. Wao huweza kuwa na dawa kwa mfano inayomletea mtu
usingizi na hiyo hiyo kumtia kichefuchefu kiumbe. Dawa kama hiyo hutumika sana
katika michezo na nyoka. Mtoto mdogo anaweza kupakwa dawa hiyo na kulala. Ndipo
nyoka huweza kuanza kummeza mtoto yule. Lakini dawa ile ile itamtia nyoka
kichefuchefu na hivyo kumtampika mtoto mara moja. Hayo yote yanatakiwa
yatendeke ndani ya dakika 45. Muda ukizidi hapo au dawa ikiwa imeisha nguvu
yake, maana yake mtoto amekwenda na maji. Kwa hali hiyo maandalizi ya mchezo
kama huo lazima yafanyike kwa makini na ubora wa dawa lazima uhakikishwe.
Pamoja na dawa za namna hiyo ni matumizi ya vitu vya kudanganyia. Kati ya vitu
hivyo ni taa za rangi mbalimbali, michuzi myekundu ya nyanya, maboksi ya umeme
na upindaji wa mikono na viganja. Taa zinasaidia sana katika michezo kama ile
ya kumgeuza mtu jinsia, labda mwanaume aonekane kama mwanamke. Michuzi myekundu
ya nyanya ndiyo inayotumika sana katika michezo labda ya kuchinja watu au
wanyama. Maboksi ya umeme ndiyo inayotumika katika kuwashitua watu na
kadhalika. Basi hayo ndiyo mambo ya mazingaombwe ya hadhara wanayolipia watu.
Na haya huweza kufundishwa mashuleni watu wakajifunza. Kabla na hata wakati wa
Yesu, watu waliweza kujifunza hayo huko Misri na siku hizi ukitaka unaweza
kwenda kusomea huko jiji Brazaville, Kongo.
Kumbe, kuna mazingaombwe mengine ambayo watu wabaya
wameyagundua wenyewe kwa utundu wao. Hayo huyaficha na huamua kuwatishia au
kuwahangaishia wenzao. Hayo basi si nguvu zo zote za pekee. Mifano michache ni
kama ile ya kuona mtu amegandishwa kitini au mawe yakirushwa na kudondokea
mahali fulani. Kugandishwa kitini kunafanyika kwa kughilibiwa mawazo yako na
matumizi ya gundi kidogo. Kurushwa kwa mawe kunafanika kama kawaida ila watu
mnasadikishwa kwamba yanakotokea hakujulikani. Mkiwa makini na kupima mlalo wa
jiwe linaloruka, mnaweza kugundua mara linakotokea na mkichunguza vyema
mtamwona anayerusha.
Kuna bado mengi ya kusema au kuandika. Usichoke sikiliza
au soma.Katika pilikapilika kuna mambo mengi tunayoyasikia au kuyaona yenye
msingi wake kwenye sarakasi. Ukisikia
habari za watu kutembea juu ya paa usiku, usihangaike ni kitendo cha sarakasi
tu. Wala hakuna nguvu ya pekee ye yote. Watu hutumia rungu za mianzi mirefu
walizoviringishia nguo au matambara au huwaweka wanayamba wadogo waitwao komba
kufanikisha hilo. Kwa rungu mwanadamu anaweza kuigiza hatua hizo au komba
akitembea juu ya paa, hatua zake utadhani zinafanywa na binadamu. Hilo ni jambo
la ajabu, lakini halina nguvu za pekee ndani yake kiasi cha kwamba wewe
ushtuke. Na kumtoa nje binadamu aliyelala ndani wala hakuhitaji nguvu za pekee.
Kuna mbinu kadhaa. Mojawapo ni kumwinda mtu anayeota ndoto za kutembea afanye
hivyo siku unapotaka watu wajue. Unajua kuna wengine hutoka nje wenyewe na
kutembea huko na huko wangali usingizini. Hawa watu wazuri kwa mradi wa kuwatoa
watu nje ya nyumba usiku. Wanatoka nje wenyewe, kusifiwa wanasifiwa watu
wanaodhaniwa kuwa wachawi! Lingine ni kuingia ndani ya nyumba ya mkusudiwa
kungali mapema bado. Akifunga mlango wake na kulala, wewe ifikapo saa za
manane, unafungua na kumtoa nje. Kama hajalala vizuri unamwongezea dawa ya
usingizi ya majani au ya madukani. La sivyo ni kuufungua mlango wa mkusudiwa
usiku wa manane. Kufungua wala hukufanyiki kwa matako kama wanavyodai
wavumishaji wa habari kama hizi. Kufungua milango kunafanyika kwa funguo bandia
au kwa vijijini ambako milango hufungwa kwa miti, ni kitendo cha kujua namna ya
kuondoa miti hiyo tu. Kwa sarakasi kama hizi, mtu anahitaji kumfahamu sana yule
mkusudiwa, mahali anapolala na jinsi anavyochoka. Kifupi, mkusudiwa na
mazingira yake lazima vifahamike sana ili mkusudiwa afanyiwe “timing”. Bila
“timing” sarakasi kama hizo hazifanikiwi. Mintarafu usingizi, kila mtu hulala
usingizi kwa kusiganisha uzito. Mtu anaanza usingizi mzito kwa masaa mawili,
halafu usingizi mwepesi kwa masaa mawili na kuendelea. Ndipo kwa kawaida, kwa
walio wengi, usiku wa manane ndiyo wakati wa usingizi mzito. Hapo hata wezi
wanajua na huweza kufanya vituko vyao vya wizi. Sasa kama wezi wanafanya
vitimbi kwa “timing” tutashindwa mimi na wewe tukikusudia kumtisha mtu
tunayemkusudia!
Zaidi ya haya niliyosema, ndugu yangu, katika
pilikapilika kuna mambo mengi tunayoyasikia au kuyaona yenye msingi wake kwenye
masharti magumu. Jambo hili wala halihitaji maelezo marefu. Unaweza kusikia
mambo ya ajabu ajabu ambayo ndani yake hakuna lo lote. Mtu anaweza kupewa dawa
akaambiwa: “Unapotumia dawa hii, mtoto wako asilie” au “Mkitaka kushinda mechi
ijayo, kwanza usiku mkalale makaburini na kishapo wakati mnaingia kiwanjani msigeuke nyuma au msipitie mlango mkubwa bali
rukeni ukuta kwa upande wa kulia mwa goli”. Au unaweza kusikia: “Mkitaka
kufaulu mtihani mtafute paka mweusi umtoboe macho” au “ Weka mfukoni mwako
kipande cha sanda ya marehemu wa mwisho kuzikwa kijijini kwenu” na kadhalika.
Sasa haya yote na mengine ya namna hii, hayana ndani yake nguvu ye yote ya
pekee ni kufukuza upepo tu.
Basi ukimwona mtu anahangaika mtoto wake asilie, usidhani
kuna lo lote la pekee nyuma yake, ni kama hivyo amepewa sharti gumu na mganga
wa kienyeji tu kusudi mambo yasipoenda sawa na dawa aliyotoa mtumiaji amtwike
lawama mtoto wake atakayelia.
Basi ukiwaona watu wanahangaika kulala makaburini kabla
ya mechi, usidhani kuna lo lote la pekee nyuma yake, ni kama hivyo wamepewa
sharti gumu na mganga wa kienyeji tu kusudi mambo yasipoenda sawa na dawa
aliyotoa watumiaji wamtwike lawama mwenzao fulani atakayekataa kulala
makaburini.
Hali kadhalika ukiwaona wachezaji wanahangaika kuingia
kiwanjani pasipo kugeuka nyuma, usidhani kuna lo lote la pekee nyuma yake, ni
kama hivyo wamepewa sharti gumu na mganga wa kienyeji tu kusudi mambo
yasipoenda sawa na dawa aliyotoa watumiaji wamtwike lawama mwenzao atakayegoma
au atakayeshindwa kufuata sharti hilo.
Ama ukiwaona wachezaji wakikataa kupitia mlango mkubwa na
badala yake wanaruka ukuta kwa upande wa kulia mwa goli, usidhani kuna lo lote la pekee nyuma yake, ni
kama hivyo wamepewa sharti gumu na mganga wa kienyeji tu kusudi mambo
yasipoenda sawa na dawa aliyotoa watumiaji wamtwike lawama mwenzao atakayekataa
au kushindwa kufanya hivyo.
Aidha, ukimwona mwanafunzi au wazazi wa mwanafunzi fulani
wakihangaika kumtafuta paka mweusi au ukisikia wamemtoboa macho macho paka
mweusi, usidhani kuna lo lote la pekee nyuma yake, ni kama hivyo wamepewa
sharti gumu na mganga wa kienyeji tu kusudi mambo yasipoenda sawa na dawa
aliyotoa watumiaji wajilaumu wenyewe kwa kile watakachoshindwa kufanikisha kama
ilivyoelekezwa na mganga husika.
Mwishowe, ukimwona mtu makaburini anahangaika kutafuta
kipande cha sanda au ukisikia kuna mwanafunzi aliweka mfukoni kipande cha sanda
ya marehemu wa mwisho kuzikwa kijijini kwake, usidhani kulikuwa na lo lote la
pekee nyuma yake, ni kama hivyo alipewa sharti gumu na mganga wa kienyeji tu
kusudi mambo yasipoenda sawa na dawa aliyotoa mtumiaji ajitwike lawama mwenyewe
kwa kushindwa kutimiza kilichokuwa kigumu.
Ndipo ninakuambia, si mara haba unaweza kuwaona watu au
kusikia habari za ajabu ajabu kumbe zilikuwa mahangaiko ya watu kutaka kutimiza
yale waliyoambiwa na waganga wa kienyeji. Ndiyo mambo kama ya kuwabaka maajuza
au kuwanajisi watoto wachanga, kukata mikono ya maalbino, kuwaua watu
waliozaliwa peke yap katika matumbo ya mama zao. Au mambo ya kuzika vichwa vya
ng’ombe kwenye machimbo na kuuchukua mayai ya bundi mifukoni. Hayo yote ni
pilikapilika za watu wanaotafuta utajiri au bahati kwa kadiri ya ushauri wa
waganga wa kienyeji. Kumbe katika hayo hakuna nguvu ye yote ya pekee bali
kubahatisha bahatisha tu. Usihangae na habari zake.
Tukizidi kuweka wazi habari za pilikapilika zinazoonekana
au kusikika duniani hapa, acha nikuambie kwamba katika pilikapilika hizo kuna
mambo mengi yenye msingi wake kwenye mipango ya kughilibu. Kifupi, ninataka
nikujuvye habari za ushirikiano watu wanaoufanya na wengine tukababaika.
Unaweza kuona au kusikia mganga au mtu fulani anaweza kusema anachoumwa mgonjwa
bado akali mbali. Hapo usidhani mtu yule ana nguvu za pekee. Mara nyingi mtu
yule huwa amewapanga watu wa kumletea habari za wagonjwa bado wakali mbali.
Ukitaka kujua hilo, nenda kwa mganga wa namna hiyo ghafla huku ungali mzima kabisa. Hapo utaona jinsi
atakavyojaribu kukuepa au kubuni buni mengi anayodhani kati yake moja wapo
utalikubali kama kweli.
Aidha kwa mipango ya ushirikiano, unaweza kubaini vyema
wanachofanya wale wanaojiita “wanyoa wachawi” vijijini. Timu ya watu, mara
nyingi vijana wa kiume hukubaliana kumpandisha mmoja wao kama mganga mkuu.
Pamoja naye wengine hujidai kuwa wasaidizi wake. Wakipita huko na huko wanakuwa
makini sana kumlisha kwa taarifa mbalimbali kuhusu watu au vijiji
wanavyotembelea. Kama wakitaka kujidai kufichua vifaa vya “wachawi”, hao
wasaidizi ndio wanapita huko na huko kuzika vifaa vyao wao wenyewe kusudi
asubuhi mganga wao mkuu ajidai kuvifichua. Basi ni hasa wasaidizi wa mganga
wanaomsaidia mganga wao mkuu kuwadanganya watu. Wakitaka kucheza mchezo wa
kuongeza fedha kwa mfano, ni wasaidizi wanaoleta fedha zao. Wewe ukiowaona wao
wanasaidiwa kwa namna hii au ile, unaweza kudanganyika kwamba wao walikuwa
wateja kama wewe na hivyo wamefaulu. Kumbe siyo, fedha ni za kikundi chao wenyewe.
Wewe ukiweka au ukitoa fedha zako kuwaiga wao, ndiyo hizo watakazojichukulia
kwa kadiri ya mahesabu yao. Usiwafuate watu kama hao, utakuwa mjinga ndiye
aliwaye. Kwa maneno mengine, ukiyasikia au kuyaona mengine yakitendeka, ujue ni
mchoro wa kitapeli uliokusudiwa utapeliwe wewe.
Mambo mengine ninayotaka kukueleza yanatupeleka karibu
mwishoni mwa maelezo yangu kuhusu pilikapilika mbalimbali zilinazopatikana kati
ya watu wanaojishughulisha na ushirikina duniani hapa. Ninakwambia hivi, katika
pilikapilika za duniani hapa kuna mambo mengi tunayoyasikia au kuyaona yenye
msingi wake kwenye kujitafutia nguvu za pekee au bahati. Watu wengi, hasa
katika nchi zetu zinazoendelea wamebanwa na maisha magumu. Jinsi ya kujinasua,
watu wengi hawajui. Ndipo hujaribu hiki na kile kwa fikra za mlinganisho
wakidhani wataangukiwa na “ngekewa”.
Basi wengine utawasikia au utawaona wakinywa damu ya watu au ya paka.
Hao hufikiri labda damu ya mtu au ya paka ni ya pekee na huenda italeta bahati.
Wengine hubahatisha bahati yao kwenye kuwa, kuvaa au kubeba hirizi fulani. Hapo
unaweza kuona hiziri za kila kabila, rangi na urefu. Zote hizo si lo lote.
Ndani ya hirizi hakuna kitu kinacholeta bahati. Nini, kijiti, mchanga, kipande
cha jiwe, punje ya nafaka, maharage au kunde?, Wengine hubahatisha labda nguvu
za pekee zitatoka kwenye kumbaka ajuza fulani au kumnajisi mtoto fulani.
Wengine hubahatisha labda nguvu za pekee zitatoka kwenye
ngozi ya binadamu. Basi utawaona hao wakiwachuna wenzao ngozi na kutengenezea
hirizi.
Wengine hubahatisha labda nguvu za pekee zitatoka kwenye
kujiacha wachafu. Basi hao utawaona wakikataa kuoga au kujitunza katika usafi.
Wengine hubahatisha labda nguvu za pekee zitatoka kwenye
viungo vya akinamama. Hawa utawaona wakitafuta kwa udi na uvumba ndevu za akina
au kuwakata viungo vyao kama vile via vya uzazi na matiti.
Wengine hubahatisha labda nguvu za pekee zitatoka kwenye
viungo mbalimbali vya binadamu. Ndipo unaweza kuwaona au kuwasikia watu
wakitafuta mapafu ya watu, au mioyo yao au via vyo vya uzazi au matumbo yao au
mifuko yao ya chakula, macho, masikio na kadhalika.
Wengine hubahatisha labda nguvu za pekee zitatoka kwenye
vichwa vyenye upaa. Hao ndio wanaotumia vichwa vya binadamu vyenye upaa kuvulia
dagaa maziwani au labda kama huku Afrika ya Kusini kulindia stoo zao
zilizojazwa bidhaa au mali.
Wengine si kwamba wanatafuta bahati ya pekee ila katika
ujanja wao hujisingizia kutoka sehemu zinazoogopwa na watu. Unajua watu wengine
huziogopa sehemu fulani fulani za dunia na mtu akisikika kwamba anatoka huko
wengine hudhani ana nguvu za pekee. Basi kwa hilo utaona watu wakijisingizia
kutoka sehemu kama hizo. Madhalani wapo wanaojisingizia kutoka Sumbawanga,
wengine Baria au Gambush, wengine Malawi, wengine Msumbiji na kadhalika.
Ukichunguza sana, sehemu hizi si lo lote isipokuwa ni sehemu za nyuma kielimu
na kwa hali hiyo watu wake wamelimatia sana katika ushirikina. Hata hivyo,
kulimatia huko, hakuwapi nguvu ye yote ya pekee isipokuwa kelele zisizo na
maana. Ukiwa mbali utasikia watu wa huko wanaweza kutengeneza mvua au kutuma
radi au kuwatega wanaume wanaozini na wake wa watu au kuonesha mambo katika
televisheni za asili. Sasa nenda huko huko, uone mambo yalivyo kinyume.
Hutakuta mvua ye yote ya maajabu. Utakuta mvua za kawaida na hata ukame unaweza
ukaushuhudia. Aidha ukiwaalika waende Sahara wakawanyeshee mvua Waarabu,
utawaona wakiinamisha vichwa kwa kukosa uwezo. Radi utazikuta za kawaida
kabisa. Ama ukiwaalika waitume moja ikamuue Osama bin Laden wapate dau la dola
milioni ishirini waliloliweka Wamarekani, utawasikia wakikuomba uache kuwaonea.
Yale uliyoyasikia ya kuwatega wanaume wazinzi, hutakuta lo lote, bali utasikia
pia hadithi za wanaume nyamaume wanaomendea wake wa wenzao. Kuhusu televisheni,
hutakuta lo lote isipokuwa maji na vioo au pombe kali wanazoleweshana na hivyo
kuoneshana maluweluwe. Ukitafuta televisheni ya asili uonee mambo ya Ulaya,
wala hutapatia maana. Sasa basi, hayo yanayosikika kuhusu sehemu fulani fulani
usiyachukue kama ushahidi wa uwepo wa nguvu za pekee za kishirikina. Ni hadithi
zisizo na maana na wewe usikosee usingizi na wala usishiriki kuzieneza,
utajiaibisha bure kijana!
Hatimaye niseme jambo la mwisho katika fungu hili la
mambo. Ninasema hivi, katika pilikapilika kuna mambo mengine tunayoyasikia au
kuyaona yenye msingi wake kwenye ukatili. Hapa ninayaweka mambo kadhaa pamoja.
Zile pilikapilika za kusaka viungo vya watu, ukatili ndio unaofanya zitendeke.
Mganga akishaagiza kupatikana kwa viungo vya binadamu, pasipo ukatili hakipo
kitakachopatikana. Basi ni ukatili kumuua mtu na kuvitwaa viungo vyake. Au ni
ukatili vile vile kuvipata viungo hivyo kwa kufukua maiti. Ni ukatili kuwabaka maajuza. Ni ukatili
kuwanajisi watoto wachanga na kadhalika. Ndipo basi habari za kuchunana ngozi,
kukata watu viungo na kadhalika msingi wake ni ukatili. Vivyo hivyo habari za
kufukua makaburi.
Sumu: Hatimaye kuna mengine yanayosikika, kuonekana au
kusomeka kuhusiana na ushirikina na pilika pilika wanayosadiki wengine kuwa ni
mambo ya matendo ya giza wakati ni matumizi ya sumu tu. Mambo hayo ndiyo yanayojenga fungu la tatu la
mambo yanayotuhangaisha wanadamu, hasa sisi Waafrika. Matumizi ya sumu si
uchawi kwa maana ya nguvu za pekee ya kutendea mambo ya pekee. Matumizi ya sumu
kuwaua au kuwadhuru wengine ni sawa na matumizi ya sumu ya kuulia panya,
kunguni, inzi, mende na kadhalika. Matumizi kama hayo tunaweza kuyafanya hata
mimi na wewe. Tunapotumia dawa kuulia panya, kunguni, inzi, mende na kadhalika
wala hatuna nguvu za pekee na wala hatuitwi wachawi. Vivyo hivyo, watu
wanaotumia sumu kuwaulia au kuwasumisha wengine wala hawana nguvu ya pekee ya
kutendea mambo ya ajabu na wala jina la wachawi haliwafai.
Ndugu yangu, sumu zipo za aina mbili: za kuua na za
kusumisha na kudhuru kitu au mtu tu pasipo kuumaliza uhai. Sumu za kuua ni kali
sana. Ninazijua kadhaa na ningeliweza kukutajia lakini sipendi kuchukua fursa
hii kukutaji kwani wewe ukiwa mtu mbaya utakwenda kuzitumia na kuwaua watu au
kuwasumisha watu. Na ukifanya hivyo, utanishirikisha mimi uovu wako wakati
mimi, hadi leo hii unaposoma kijitabu hiki, watu wananifahamu kama mtu mwema.
Basi ninakwambia tu kuna sumu kebakeba. Zingine za kuua ndani ya dakika chache.
Zingine za kuua baada ya siku kadhaa. Zingine za kuua baada ya wiki, miezi au
miaka kadhaa.
Mara nyingi ukisikia mtu fulani amekufa ghafla, kama mtu
yule hakufa kwa matatizo ya moyo kama vile shikizo la damu au mshtuko (kwani
wengi tunatembea tungali tukiumwa lakini pasipo kujitambua), basi tuhumu mara
moja matumizi ya sumu. Humo kwenye vikao vya pombe, chunga sana. Kwenye vikao
vya pombe waogope sana maadui zake wenye kucha ndefu au wale wanaoshika
“kisonjo” kabla yako. Hao wanaweza kuwa wamechukua sumu ukuchani au kidoleni.
Wakitaka kusumisha huweza kuigusa pombe ile kwa ukucha au kidole chenye sumu.
Wewe utakapopokea pombe uifaidi, kweli “utafidi” tabaka lenye sumu na hivyo
utakapoinuka pale utakuwa umekwishatumbukia matatani. Kwa kuwa wewe utakuwa
ndiye aliyelimeza tabaka lile lenye sumu, usishangae ukifa wewe peke yako.
Utapokuwa umelinywa lile tabaka utakuwa wakati huo huo umewaokoa wanywaji
watakaokufura. Hiki ndicho kisa utasika, “Oh, fulani amekufa, lakini jana
tulikuwa tunakunywa naye jioni!” Ndiyo! Ndiyo hivyo tena, ni yeye aliyelifaidi
tabaka la sumu.
Sumu zakusumisha, kitu au mtu hafi, isipokuwa hujazwa
sumu inayomwathiri vibaya. Ukisikia habari za misekule au ndondocha, kama kweli
ipo, basi ndiyo hao watu ambao wamesumishwa na waovu. Kwa sumu ile wanakuwa
viumbe dhalili karibu na wanyama na hivyo kuweza kufugika. Kutokana na sumu
waliyopewa, misekule au ndondocha huwa ni punguani fulani wasio na uwezo wo
wote wa maana. Misekule au ndondocha hupatikana kwa namna mbili, iwapo watu
wamekusudia kufanya pilika ya kuipata. Namna ya kwanza ni watu kadhaa kula
njama ya kumsumisha mtu. Basi wanajopo hao humsumisha mtu au mtoto waliyemkusudia
na kisha yule mtu ataonekana kama mfu. Katika kuzimia huko watu hufanya mazishi
ya haraka haraka kumbe wakati wa shughuli hizo
humwiba mtu wao na kuwafanya watu wakazike kitu ambacho si mtu. Pengine
mtu huzikwa jioni jioni, na kabla hayajapita masaa sita, wanajopo hulifukua
kaburi na kumchukua mtu wao. Itumike njia yo yote ile kati ya hizi mbili, huyu
mtu wao akiamka huwa punguani kwa sababu ya sumu kali lakini basi huweza
kutumika katika mambo ya kipuuzi kama vile kuiba mchicha, maboga, mboga,
matunda bustanini au kauzu na vitu vingine vinavyouzwa katika mabanda dhalili.
Misekule au ndondocha ni punguani, ndiyo maana huweza kutumwa kuiba vitu vidogo
vidogo kama hivyo. Kamwe hawawezi kuiba vitu vya maana kama fedha katika benki
kubwa. Ndiyo maana hujawahi kusikia benki ye yote duniani kwamba imeibiwa
kimazingira. Ingekuwa misekule au ndondocha wana uwezo wangelitumwa Marekani
kwenda kuiba “midole” watu wakaachana na
umaskini. Lakini, thubutu yake haiwezekani. Kwani hata Marekani kwenyewe wanakujua?
Punguani aende Marekani? Kwa njia ipi!
Katika mstari huu wa sumu ambazo si za kuua, yanaingia
madawa yanayoitwa limbwata. Wanawake wengine wasiojua kupenda hupita huko na
huko wakitafuta dawa za kuwapa wanaume au waume zao ili wawapende wao peke yao.
Hakuna lo lote nakwambia. Madawa ya limbwata yapo mengi na yana formula chafu
chafu. Kuna madawa mengine yanayofanyika kwa mchanganyiko vya unga au vipande
vipande wa mende. Hudhaniwa kwamba kama mende wasivyotoka jikoni, wanaume
waliolishwa limbwata hawatacheza mbali na wanawake wao. Ashakumu si matusi,
formula zingine huhushisha kupikia nyama au vitu ambavyo mwanamke alivificha au
kuviweka kwenye sehemu zake za siri. Thu! Kinyaa!
Basi nisikupatie formula hata moja, isije ukaenda
kujaribia. Inatosha nikifunga kwa kusema tu kwamba dawa nyingi za limbwata
hazifanyi lo lote. Zile zinazofanya kitu fulani ni sumu tu na wala si nguvu za
pekee. Ndiyo maana mtu aliyepewa dawa za namna hiyo huwa “lofa” wa kuzubaa
zubaa tu. Na mara si haba utamwona akitoka mate tu na ndipo wanawake wanapoanza
kuliwa wanapowaona wanaume au waume zao wakigeuka malofa na hivyo mizigo ya
kuwaelemea wao wenyewe.
Ushirikina: Haya haya tuliyoyazungumzia sasa hivi ndiyo yanayoitwa na
watu mambo ya kishirikina. Ni mabaya na yanawafanya watu waumwe kwa sababu
yanawatia watu hofu. Hofu ya namna hiyo inawafanya watu waoga washindwe kuishi
kama wanadamu huru. Wengine waogopa kujifanyia miradi ya maendeleo au kuboresha
maisha yao kama vile kwa kujijengea nyumba bora kwa kuhofia “kulogwa”. Wengine
wanaogopa kuishi vijijini na kujitafutia maisha kwa kilimo na shughuli zingine
zinaweza kustawi vijiji na hivyo huenda kubanana na wengine mijini. Maisha ya
mjini pasipo shughuli za kueleweka yanawatengeneza fukara wengi sana. Fukara
ndio wanaojaribu kujinasua kwa shughuli za wizi, kuuza miili na shughuli
zingine haramu kuzitaja. Basi hapo kwenye hofu za ushirikina panatengenezwa
wagonjwa wengi wanaoifanya jamii yetu iugue hivi inavyougua.
Hofu juu ya laana: Wapo watu chungu mzima, hata wasomi wetu, ambao wanasadikishwa
kwamba mababu zao wanaweza kuwalaani ama kwamba walikuwa na laana na wao
wanafuatwa fuatwa na laana kwa mwendo wa urithi kutoka kwa hao waliokuwa na
laana kabla yao. Hofu inayozaliwa katika kipengele hiki ni mbaya vile vile.
Yaani kama hofu zingine zinavyodhuru, hofu juu ya laana nayo huzalisha nguvu
hasi. Na nguvu hasi humuuguza mtu pasipo haki ye yote. Nani amelaaniwa? Mababu
gani wanaweza kuwalaani watu? Laana inamfuataje mtu? Tuache kugonjeshana.
Kwa Wakristo, laana si jambo la kushikiliwa tena. Yesu
alikuja kufanya nini kama si kumshinda shetani na matisho yake kama hayo ya
laana? Binadamu hawakuahidiwa baraka kwa njia ya ukoo wa Abrahamu (rejea Mwa
12:1-3), yaani wale wanaomwamini Yesu? Basi baraka imejenga nyumba hapa
duniani. Kinachotakiwa ni kumwamwini Yesu, kubatizwa na kuifanya baraka idumu
nasi. Mbele ya Yesu, hakuna laana tena. Mababu kama walisema kitu cha mwono wa
laana wameropoka bure. Kama kuna mtu alitishiwa laana na ye yote hapo kabla
mbele ya Yesu matisho hayo yameshayeyuka. Tujiulize tu, kama maneno ya laana
yanafanya kazi leo, Yesu alikuja kufanya nini? Au ubatizo una nguvu gani kama
hauwezi kutufanya watoto wa Abrahamu na kutuweka huru? Yesu anacheza “madange”?
Mbona tunamtania Yesu na kuidogoza kazi yake? Tangu lini Yesu anafanya miradi
ya Pwagu na Pwaguzi? Tuacheni matusi!
Hofu juu ya mizimu: Mizimu ni akina nani? Fasili ya neno hilo inasema, ni
mababu au wazee waliotutangulia.Wapo watu wanasadiki kwamba tunaweza kufikwa na
magonjwa na madhila ya ukame na balaa zingine kama vile wadudu na wanyama
waharibifu wa mazao kutokana na wazee wetu waliotutangulia. Lakini kweli hiyo?
Kama walipokuwa wanadamu pamoja nasi hawakuweza kutengeneza bakteria na virusi,
wakawa wanalalamika wenyewe kupatwa na maradhi ya kutatanisha, uwezo huo wanaupata
wapi sasa baada ya kufa kwao? Kama walipokuwa wazima kati yetu hawakuweza
kunyesha hata rasharasha, wakawa wanalalamika wenyewe kuharibikiwa mazao yao
kwa ukame, uwezo wa kunyesha au kuzuia mvua katika maeneo yetu wanaupata kutoka
wapi na kwa jinsi gani? Kama walipokuwa wanadamu pamoja nasi hawakuweza
kutewangeneza wadudu na wanyama waharibifu, wakawa wanalalamika wenyewe mazao
yao kushambuliwa na wadudu au wanyama waharibifu, uwezo wa kuwatengeneza wadudu
na wanyama waharibifu wa mazao na kuwatuma dunia wanaupata wapi sasa baada ya
kufa kwao?
Basi kwa fasili hiyo mizimu hamna bao. Tunajua kwa
uhakika kabisa, kwa njia ya mafundisho ya imani yetu kwamba wafu wetu
hawazubaizubai mahali fulani peke yao. Wale waliokuwa wema na watakatifu wapo katika hali ya mbinguni,
wale waliokufa na nusu utakatifu wanapitia mateso ya muda katika hali ya
toharani wakati wale waliokubuhu katika dhambi na kumkataa Mungu kwa imani na
matendo yao wapo katika hali ya motoni kama wafungwa wa Shetani. Sasa walio
watakatifu hawana silika ya kutudhuru sisi kwa kututia maradhi ama kutuzuilia
mvua. Watakatifu ni roho njema nazo zinatuombea zikitaka wanadamu tujiunge nazo
tuufaidi uzima wa milele pamoja na Mungu. Sasa roho zinazotukia mema
zitafanyaje kazi ya kututia maradhi na kutuzuilia neema kama hiyo ya mvua!
Roho zilizo toharani zinateseka kwa muda nazo zinataka
sana ziombewe na sisi wanadamu. Sasa roho zinazotaka ziombewe zitakufanyaje
fujo ya kututumia maradhi na kutuzuilia mvua wanadamu? Huko si kujipiga
tikitaka zenyewe? Hatimaye zile roho zilizomo katika hali ya motoni kidomodomo
kimekwisha. Ni roho fungwa kwa Shetani? Mfungwa huwezaje kuwadhuru watu nje ya
gereza? Wana uwezo gani wa kumtoroka bwana magereza (Shetani)? Roho kama hizo
zinasubiri kihoro cha mwendelezo wa mateso ya motoni tu. Basi sisi Waafrika
tunaposema eti tuwatulize wazee wetu katika hasira zao kwa kuwapikia ugali au
pombe tunajisumbua tu. Ugali wale akina nani?
Mababu zetu katika hali ya mbinguni? Hawahitaji wanashiba kukaa na
kumwona Mungu kama alivyo. Ugali wale akina nani? Mababu zetu katika hali ya mbinguni?
Hawahitaji, wanashiba kukaa na kumwona Mungu kama alivyo. Pombe wanywe akina
nani? Mababu zetu katika hali ya mbinguni?
Hawahitaji wamekata kiu kwa kukaa na
kumwona Mungu kama alivyo.
Ugali wale akina nani?
Mababu zetu katika hali ya toharani? Hawahitaji, wanatamani kumaliza
malipizi yao waende zaa kukaa na kumwona Mungu kama alivyo. Au tena ugali wale
akina nani? Mababu zetu katika hali ya
toharani? Hawahitaji, wanakata kiu yao kwa hamu ya kumaliza malipizi yao kwa
haraka waende zao kukaa na kumwona Mungu kama alivyo.
Hatimaye ugali wale akina nani? Mababu zetu katika hali ya motoni?
Hawahitaji, wafungwa wa Shetani hawapewi ugali wala maharage. Wao ni mateso kwa
kwenda mbele tu. Na vivyo hivyo wala hawahitaji
pombe. Basi matonge ya ugali
tunayowatumia kama sadaka, tunayapoteza bure, heri tule wenyewe. Pombe
tunayowamwagia, tunaipoteza bure, heri tuinywe wenyewe. Na ukipima sana sadaka
za ugali za pombe zinatangaza ulafi na ulevi wetu wenyewe. Ugali tunaowatupia
hao mababu, kama wangelikuwa wanakula kweli hauwatoshi, kwa maana hata kama
tonge lingelikuwa kubwa kiasi gani haliwezi kuwatosha wazee wetu ambao ni
wengi. Pombe tunayowamwagia hao mababu, kama wangelikuwa wanakunywa kweli
haiwatoshi, kwa maana hata kama pombe ingelikuwa nyingi kiasi gani haiwezi
kuwatosha wazee wetu ambao ni wengi na wengine katika yao walikuwa walevi kama
shimo.
Hakika tuchofanya ni kuwadanganya tu kwani ugali mwingi
na “minyama” yake tunakula wenyewe na pombe nyingi tunakunywa wenyewe.
Tungelikuwa wakweli tu kwamba vitu hivyo tunajitengenezea wenyewe.
Tusiwasingizie wao eti kwamba wanavihitaji. Aheri, tungeliamua wenyewe bila
kujionea aibu. Siku moja tujiamulie kwamba tunataka kula ugali, basi tujipikie
tujifanyie sikukuu. Siku nyingine tena, tujiamulie kwamba tunataka kujinywe pombe, basi
tujipikie tukajifanyie sikukuu.Wala dunia haitatugomea kwa maamuzi kama hayo.
Waaidha kwa Wakristo, sadaka ni moja tu. Sadaka ya misa. Hayo mengine yote ni
ujinga na kufukuza upepo tu.
Mapepo
Kuna tofauti ndogo isiyo na maana kati ya mapepo na
majini. Wanasema eti mapepo hayaonekani lakini majini yanaonekana. Sahau
tofauti hiyo, watie wote katika kundi la mashetani. Mashetani ndiyo wale
malaika waliomwasi Mungu na hivyo kulaaniwa. Kwetu sisi Wakristo, tunajua fika
kwamba hawana bao. Yesu amewashinda. Amemtegua kiuno shetani. Yeye ni BAUNSA
WETU.
Kazi aliyojia Yesu duniani ilikuwa kuwaokomboa watu
kutoka kwenye makucha ya shetani na maswahiba wake. Gharama ya kazi hiyo
ilikuwa kubwa, ndiyo kujimwilisha na kisha kumwaga damu msalabani kwa ajili
yetu. Kazi hii kubwa ilizaa matunda. Tumekombolewa kweli kweli kwani Yesu
hakuja kufanya kazi bure. Ni sisi binadamu ambao tunaweza kufanya kazi kubwa na
kuambulia mapato madogo kwa sababu ya kosa la kwanza la Adamu na Eva lakini si
Mungu mwenyewe. Sasa iweje baada ya Yesu kumshinda shetani sisi tuhangaishwe na
shetani kana kwamba Yesu hakufanya kitu? Basi shetani anatutazama Wakristo kwa
mbali tu. Ila yeyote ambaye hajampokea Kristo yupo kwenye himaya ya shetani
bado.
Ndiyo kisa mashetani (mapepo kwa majini) yanawahangaisha
ndugu zetu wasio Wakristo. Ndugu zetu Waislamu ndiyo hasa yapo kwao. Basi ndiyo
kisa yanavuma kati yao kwani hawana Yesu. Masimulizi yananaanza hata kwenye
kuumbwa kwa majini. Wanasema yaliumbwa na kupewa jukumu la ibada kama wanadamu.
Hata Mtume Mohamedi aliwasisilimu majini kwa mahubiri yake. Kwa kweli majini ni
ndugu zao ndiyo maana hata majina ya majini karibu yote ni ya kiislamu. Huo ni
ushuhuda tosha kwamba majini au mapepo ni jamaa ya Waislamu. Hakuna jinni John,
Corbinian wala jinni Tito kwani hawana shirika na Yesu Kristo wala na Wakristo. Sasa inasikikaje kuwa yapo kati
yetu. Hapo ndipo tunapotwishwa tatizo lisilo letu. Jina la Yesu sawia na jina
la Maria yanawakimbiza majini au mapepo kwa mbali kabisa. Aidha sisi kwa
kubatizwa na kupakwa mafuta ya kuwingia mapepo sisi tumekuwa kama chupa zenye
dawa ya kunguni ndani yake. Itakuwaje kunguni waishi ndani ya chupa hizo? Basi
ikiondokea jinni au pepo kuishi ndani ya Mkristo, yaani kunguni kuishi ndani ya
chupa yenye dawa ya kunguni ndani yake, basi inamaanisha dawa imekwisha nguvu,
yaani “imeeksipaya”. Basi hapo lazima lije swali kwa nini dawa imekwisha nguvu?
Kumbe dawa ya kiroho huisha nguvu kwa dhambi kubwa. Sasa swali, dhambi gani
kubwa aliyoitenda mhusika hata kuishiwa nguvu?
Kwa muhtasiri huu, Wakristo hasa wale wanaoishi katika
maeneo yenye mchanganyiko wa dini waangalie wasiishi teolojia isiyo yao. Hata
mapadre na makatekista waangalie kwamba baada ya kusomea teolojia ya kikatoliki
wasihubiri teolojia ya kiislamu. Wote wanaofundisha kati yetu wafundishe mambo
ya kikatoliki. Si halali na kwa kweli ni hasara kubwa kusomea teolojia ya
kikristo kwa miaka mingi na kishapo kuhubiri yasiyo yetu. Basi ndugu zangu,
ijulikane wazi kwamba, mintarafu mapepo, majini au shetani kwa ujumla, teolojia
ya Waislamu SI SAWA NA YETU hata kidogo. Acha niweke muhtasari wa teolojia ya
kiislamu kuhusu majini. Kwa Waislamu mchana ni wa wanadamu na usiku ni wa
majini. Wanasema hilo limefanywa na Mungu baada ya majini kuomba wanadamu
watenganishwe na wao. Wanasema hiyo ilifuatia tabia ya binadamu kuchenga ibada
za kumwabudu Mungu kwa udhuru za kuumwa ama kuwa na shughuli za biashara au
kuwapo safari. Wanaendelea kufundisha kwamba baada ya Mungu kuwakubalia majini
ombi lao, majini yanatawala usiku na binadamu mchana. Wanaendelea kusema,
baadhi ya majini waliamua kutokuwa na kisasi na wanadamu na hao ndiyo majini
mazuri wanaowapenda wanadamu na hivyo kuwasaidia katika mambo ya biashara, mapenzi na bahati
za aina mbalimbali. Lakini majini mengine yakaapa kuwadhuru binadamu. Kumbe hao
walioapa kuwapo wanaowapenda watu na
wanaolipa kisasi kwa binadamu, wanachukua sura mbalimbali: kama nyoka, ndege
hasa njiwa, mnyama, miti mirefu, binadamu hasa wanawake wazuri, kama mtu
unayemfahamu, paka, panya, kuku n.k., kila mtu ana wake, wana moto, kila aya ya
Qur’ani ina jinni lake, sheikh anaweza kuwaita, wanasimamia idara mbalimbali
kama vile ngono, ulevi, usengenyi, wivu n.k. ni wengi mno yaani mamilioni kwa mamilioni.
Pepo bawa ni majini au mapepo yanayobaka watu au kuwalawiti watu kwa nguvu. Hao
si kati ya majini au mapepo mema.
Haya yote nayahesabu ubatili mtupu.
6.5
Upotevu wa dhana kamili ya Ndoa kwa Vijana wengi
Siku hizi ndoa zinazokuja kubarikiwa kanisani
asilimia kubwa zinakuwa ni mtumba. Maana yake vijana wamefikia hatua ya kutaka
kujaribu kila kitu kwanza. Hivyo kabla ya kuhalalisha ndoa kamili, wakiwa
katika hatua ya uchumba wanadanganyana kuwa wajihakikishe kama kweli wako
vizuri. Kwa hakika hii dhana ni ya kutupilia mbali, licha ya kwamba utandawazi
nao unachangia kwa kiasi kikubwa katika kuwafanya vijana kuwaka sana tamaa
kupitia vitu wanavyoshinda wanaona na vingine kutazama.
Hatari kubwa ipo zaidi pale wanapooana
kila mmoja ana nafsi yake. Hiyo nafsi kamwe haiwezi kumwacha mtu salama, daima
itamlilia tu. Wahanga wakubwa hapa ni mabinti ambao kwa hakika huwa waaminifu
sana, kumbe inapotokea akashiriki tendo la ndoa kwa mara ya kwanza na mtu
aliyekuwa na malengo yake. Sasa ikitokea yule mtu ameamua kuoa binti mwingine,
kwa hakika ile nafsi ya yule binti wa kwanza itamlilia na kumtafuta tu mpaka impate.
Ndiyo hapo tunapata masuala ya michepuko na nyumba ndogo, kumbe nayo haianzii
ukubwani bali pale unapojikuta umeshiriki tendo la ndoa kabla ya muda wako. Na
kuendeleza tabia hiyo hiyo ya onja onja. Hakika hata ukishaoa huwezi kuacha
tabia hiyo ya udokozi. Na hivyo mhubiri anaendelea kututia shime na kutuonyesha
umuhimu wa kufuata nyakati ipasavyo.[74]
Tuendelee na kujitahidi kukemea kwa
nguvu zetu zote, maana ni katika kuuongea ukweli wa mambo haya na kuyaweka
bayana nasi tutazifanya nafsi zetu kuwa huru.[75] Tena
tuone ya kuwa wakati ni sasa wa kuvipiga vita, maana muda tulionao ni sasa;
baadaye hatutapata muda huo. Hivyo tufanye kwa moyo na bidii sasa kukemea, wala
tusingoje kana kwamba kuna muda ufaao utakaokuja. Kila mmoja atende kwa juhudi
zake zote kadiri awezavyo ili kukinusuru kizazi hiki cha leo.[76]
Katika changamoto hizo tajwa hapo juu
kwa kiasi kikubwa zimekuja kuchangia wimbi la watoto wa mitaani. Yaani mtu
baada ya kujua na kuelewa juu ya kutoa mimba bila kujali ni mazingira gani
kaipata, basi anaamua kuvumilia mpaka anajifungua salama. Sasa unapokuta ni
binti, walio wengi anachokifanya ni kumchukua mtoto yule akiwa mdogo kabisa na
kumpeleka kulelewa na bibi yake. Kitendo hicho ni kama kumtelekeza mtoto, maana
mama anakwenda kutafuta au kuolewa na mtu mwingine. Sasa bibi yake asipokuwa na
moyo wa nyama, atamwacha mjukuu wake akue katika maisha anayojua mwenyewe.
Mwisho wa siku mtoto anajikuta anakuwa omba omba au mtoto wa mitaani.
Pia tunalowimbi la watoto yatima ambao
kwayo wengine ndiyo hao wanaojikuta wamekosa mwelekeo na kuanza kulandalanda
mitaani, hatimaye wanakuwa watoto wa mitaani. Kulingana na Frt. Nini maana ya Mtoto au Watoto
yatima? Hawa ni watoto ama waliofiwa na wazazi wao wote wawili
(yaani baba na mama) au waliotelekezwa na wazazi wao kwasababu mbalimbali kubwa
ikiwa ni ile ya kukwepa majukumu ya mzazi. Na hivyo wakajikuta wamelazimika
kuishi peke yao bila mzazi au wazazi yaani kwa lugha ya leo ningeweza kusema ‘ni watoto wa bata, mama huku watoto kule, au
watoto hapa mama kule.’
Ushauri wangu kwa:-
(a) Jamii
Mtoto au
watoto yatima ni mali ya jamii, ni mali ya kila mtu na kila mmoja wetu.
Tuwajali, tuwasaidie, tuwe nao katika dhiki yao. Familia zinaweza kuwachukua na
kuwalea kama wanafamilia waliozaliwa nje ya familia. Tuwaone kama wao ni wa
zizi letu lakini wanakaa nje ya zizi na hivyo tuwalete ndani ya zizi.
Tuwapende, tuwape haki zao msingi mathalani haki ya kuishi, kupendwa, kupewa elimu, malezi, matunzo, malazi, chakula
nk. Napenda kusisitiza haki ya kuwapenda na
hii ni amri ya Mungu. Jamii ni mzazi na mlezi wa watoto hawa isiwaache kamwe
bila kuwapa msaada stahiki. Jamii ni mzazi wa kila mtu, ni mlezi wa kila mtu,
kila mmoja ana haki sawa na yenye uzito sawa ndani ya jamii alimo. Anapaswa
kujisikia yuko nyumbani ndani ya jamii yake.
(b) M/Watoto mwenyewe
Wapendwa
sana wadogo wangu, napenda kuwaambieni jambo hili ‘hamko peke yenu, hamjatengwa na watu wote, hamjaachwa wakiwa, mna baba, mna mama, mna kaka na dada, ndugu,
jamaa na marafiki wanao wapendeni sana naam sana tu.’ Mungu ndiye Muumba
wetu na Baba wetu sote, ni Baba mwema, ndiye mzazi wetu nambari wani. Ewe mtoto
yatima usikate tamaa, usivunjike moyo, hujaachwa, hujatengwa, hujatelekezwa kwa
namna yoyote.
Dawa hii
nawapa, ni siri ya mafanikio ‘wapendeni na kuwaheshimu watu wote, wa dini zote,
wa itikadi zote, wa kabila lolote, wa sehemu yoyote, hawa ni ndugu, jamaa, na
marafiki wenu na kati yao hamtakosa mtu mwema wa kuwajali katika hitaji lenu.’
Kumbukeni kuwa ‘kwa mgonjwa mtu yeyote huonekana daktari pale anapotoa ushauri
au maelekezo fulani fulani juu ya ugonjwa au tiba kwa mgonjwa.’ Kanisa ni mama
kwenu-zaliweni kwalo katika sakramenti ya ubatizo, mlelewe na mkuzwe na
mwimarishwe kwalo kwa masakramenti ya kipaimara, ekaristi takatifu, kitubio na
mpako wa wagonjwa.
Mkidumu
katika Kanisa mtakua kiroho, na kimwili mtapata humo wazazi wa kuwalea na hata
kuwasaidia kuzifikia ndoto zenu. Vilevile jamii ni mlezi wenu. Jamii ina watu
wema mkiiangalia katika kipimo hicho. Ubaya wa jamii ni mdogo kuliko uzuri wa
jamii hasa kwenu watoto mnaopendwa sana na Kristo. Mungu Anawapenda sana,
Anawafahamu kwa undani zaidi hata majina na nywele zenu zinafahamika kwake.
Ninyi mmeandikwa katika viganja vyake. Kwanini mkate tamaa? Kanisa linawapenda
sana ninyi watoto maana ninyi ni hazina ya Kanisa, ninyi ni tumaini la Kanisa.
Jamii pia inawapenda sana maana ninyi ni nguvu na nguzo tegemezi ya kesho
kwenye jamii. Ninyi ni taifa la kesho, Tanzania ya kesho haipo kama ninyi hampo
leo. MSIKATE TAMAA BASI.
Upendeni
ulimwengu maana wenyewe kwa wenyewe sio mbaya japo walimwengu wanaweza kuwa
kinyume chake. Mfano kama kuwa kwenu yatima kumetokana na kutelekezwa,
kukataliwa (jambo ambalo huumiza sana, huhuzunisha sana na hivyo hampendi kulisikia
kabisa). Kwa upande mwingine kama wazazi wenu walifariki dunia nalo hili
huiumiza sana roho lakini kuweni tayari kuupokea mpango wa Mungu. Katika
uyatima wenu, Yeye Anakijua Akifanyacho. Hata hivyo bado mnafursa ya kuishi na
wazazi wenu katika ulimwengu wa imani-waombeeni nao watawaombeeni nanyi mtapata
faraja katika uyatima wenu. Mwisho hata kama katika ulimwengu huu mtaonekana na
mtaishi kama yatima-msikubali kamwe kuwa yatima kiroho. Yesu anasema
“SITAWAACHA NINYI YATIMA, NAJA KWENU, MIOYO YENU IJAE FURAHA” Jaeni furaha
wadogo wangu katika Kristo.
Hatimaye;
Matatizo haya tuliyo yaona hapo juu yanaweza kupelekea kwenye matatizo makubwa
kabisa kwa mtu binafsi, kwa familia, kanisa na jamii nzima. Ninachopenda
kukitolea rai ni suala la ‘watoto wa mtaani.’
Ni akina nani hao? Hivi siku hizi zetu mtaa/mitaa imepewa hadhi ya
mzazi/wazazi? Na kama ndiyo ni mama/baba? Na kama siyo, mbona kuna watoto siku
hizi zetu tunawaita ‘watoto wa m/mitaani?’ Nadhani hili ni kosa kubwa kijamii
na kimaadili na kiasili yetu. Mtaa hauwezi kuzaa mtoto aliyeumbwa na Mungu kwa
sura na mfano wake. Mtoto ni zawadi
itokayo kwa Mungu na ni tunda la upendo kati ya baba na mama (hata kama
hawakai pamoja kama mume na mke). Labda kama tunauangalia mtaa au
tunapoiangalia mitaa kama ‘sehemu wanamokaa.’ Wana kula na kunywa humo
(mtaani), wana lala mtaani nk.
Katika
masuala (matatizo) haya mtambuka, kila mmoja wetu hana budi kujiuliza moyoni
mwake ‘mimi nimekuwaje sehemu ya tatizo? Nawezaje kuwa sehemu ya suluhisho?
Nimefanya nini mpaka sasa? Nina mikakati ipi ya baadaye ya kusaidia?
Nawapokeaje wale ambao wanasaidia katika vita hii au ndo nawakatisha tamaa kwa
maneno yangu ya vijembe mtaani ‘anajipendekeza, anataka tumwone naye kuwa ana
chembechembe ya upendo kwa watu lakini ni mweusi moyoni na rohoni mpaka damu
yake pia.’
Ndugu
kama umo kwenye baadhi ya matatizo haya hasa yale ya kujitafutia (umalaya,
utoaji mimba, na uuaji mwingine kwa ujambazi nk) AMUA VEMA UPATE KUISHI, CHAGUA
VEMA UISHI VIZURI. Acha ugume gume, acha ungangali, kuna kifo. Utaenda wapi na
ujanja wako huu unaoukumbatia namna hii leo ungali hapa bondeni (duniani)?
Mpende binadamu mwenzio, mpende Mungu wako kwa moyo wako wote. Kumbuka kuna
maisha baada ya maisha. Na kama matatizo haya yana kusibu bila kuyatarajia
(mfano kuwa yatima)-usife moyo, sote tunapita, leo tupo kesho hatupo.
Usisononeke mno ukashindwa kupiga hatua moja mbele, inuka, songa mbele, Mungu
Anakuita jinsi ulivyo. Mkumbuke mzee wetu Madiba aliposema “Watu hawatashangaa
kuona umeanguka, lakini watashangaa sana kuona umeendelea kubaki ulipoangukia.”
Tukiinama katika maisha, tuinuke pia, tukianguka katika maisha, tuninuke pia,
tuki lala katika maisha, tuamke pia. Tusonge mbele, hatua moja mbele yatutosha.
Tuendelee kubadilika kila siku ipitayo
na zaidi kujaliana na kuthaminiana, maana wanasema mtoto wa mwenzio ni wako au
mwone kama mtoto wako. Tusaidiane katika zoezi zima la kulea pasipo kujali wala
kuangalia huyu ni mtoto wa nani.
7.0 HITIMISHO
Kupitia maneno haya
yatutie shime “Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu”, wala “figa moja haliinjiki
chungu.” Kidole kimoja hakivunji chawa.” Umoja ni mzuri kwani unajenga. Ni pale
tu tunapokuwa na umoja ndipo tunakuwa imara na kufanikiwa katika maisha. Katika
Zaburi ya 133 mzaburi anatueleza wazi kuhusu maisha ya umoja. Anasema, “Tazama
jinsi ilivyo vyema na kupendeza, ndugu wakae pamoja kwa umoja…..maana huko
ndiko Bwana aliamuru Baraka, naam uzima hata milele.” Yesu aliwaombea
umoja wanafunzi wake, kwani kama wangetengana ingekuwa rahisi kushindwa katika
kukamilisha kazi ya ushuhuda. Yesu alisali, “Baba mtakatifu, kwa jina lako ulilonipa
uwalinde hawa,ili wawe na umoja kama sisi tulivyo.” Yoh 17:11b, 21. Umoja
huu ulijidhihirisha katika jumuiya ya Mitume, hata kipindi cha madhulumu
waliweza kuja pamoja kwa sala.
Kwa kujiunga na
Mwanafalsafa Mfaransa Jean Paul Sartre (1905-1980) alisema Mtu anahukumiwa kuwa
huru; kwa sababu mara moja anapotupwa ulimwenguni, yeye anawajibika kwa kila
kitu anachofanya (Man is condemned to be free; because once thrown into the
world, he is responsible for everything he does).[77] Watu
wanahukumiwa kwa sababu wanajikuta wametupwa ulimwenguni, lakini kwa sababu kwa
haraka kama wao wanajitambua wenyewe na hivyo wanawajibika kwa kila kitu
wanachofanya. Kumbe tutambue kuwa licha ya kuwa huru bado tuelewe kama binadamu
tuna mipaka. Kwa hiyo mimi na wewe tukiendelea kufumbia macho majanga
yanayoendelea katika ulimwengu huu bila kukemea, kwa kuungana wote kwa pamoja
na kuona ni vitu visivyokubalika katika jamii tutakuwa tunajitenga na upendo wa
Mungu. Na hii inajidhihirisha hata katika matendo ambayo tunaambiwa tuyatendapo
kwa wengine walio wanyonge wenye kuhitaji, msaada wetu wa mawazo, basi tunakuwa
tukimtendea Mungu. “…Njoni, mliobarikiwa...urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa
ulimwengu…kwani kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo
mlinitendea mimi.”[78]
Hali kadhalika tunapoendelea kukaa kimya huku mambo yakizidi
kuharibika, sisi tuliojaliwa kujua ukweli huu tukumbuke tutadaiwa kwa nini
hatukusema ili kunusuru Roho za watu. Nabii Ezekieli anasema, “Basi
wewe, mwanadamu, nimekuweka kuwa mlinzi kwa nyumba ya Israeli; basi ulisikie
neno hili kinywani mwangu, ukawape maonyo yangu. Nimwambiapo mtu mbaya, ‘Ewe
mtu mbaya, hakika utakufa,’ nawe husemi neno la kumwonya mtu huyo, aiache njia
yake, mtu mbaya huyo atakufa katika uovu wake, lakini damu yake nitaitaka
mkononi mwako. Walakini ukimwonya mtu mbaya kwa sababu ya njia yake, kusudi
aiaxhe, wala yeye asiiache, atakufa huyo katika uovu wake, lakini wewe
umejiokoa roho yako.”[79]
Nayakumbuka maneno ya Mwalimu wangu wa Litrujia (Pd.
Kinyashi) anapenda kusema maneno yanaumba pia maneno yana nguvu. Japo yeye
anapenda kusema kwa lugha ya kigeni “the
power of the spoken word.” Ni kwa namna hiyo tunapofanya au kutolea maneno
mazuri na ya kujenga yanaendana na baraka, lakini tunaposhindwa kusema chochote
tunamkaribisha ibirisi ndiye aje kusema kupitia vinywa vyetu. Yeye mara nyingi
anayaongelea maneno hayo katika kubariki vitu, kwamba unapotumia maneno na
kuamulu kitu fulani kweli kinafanyika kama ulivyotamka; tofauti na kubariki
kimya kimya. Anatolea mfano huu katika kubariki maji ya Baraka. Nami nimetumia
maneno hayo nikimaanisha kwamba tunapoona jambo haliendi vizuri aheri kusema,
kitendo cha kusema tu yatosha kulilo kukaa kimya. Kumbe watu wasipobadilika
hiyo ni juu yao wenyewe, wewe huna hatia tena.
Tunaposhindwa kuelekezana na kuelimishana namna ya
kuondokana na mwovu shetani na mambo yake yote, basi tunarudi kule kule kipindi
kabla ya Yesu kuja duniani na kutukomboa. Sasa hatupaswi kurudi nyuma tena
tutakuwa tunajichanganya maana hata miaka inazidi kusonga mbele nasi kwamba
tuonekane tunarudi nyuma utakuwa uwenda wazimu. “Bali nyini ni mzao mteule,
ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza
fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkainge katika nuru yake ya ajabu;
ninyi mliokuwa kwanza si taifa, bali sasa ni taifa la Mungu; mliokuwa hamkupata
rehema, bali sasa mmepata rehema.”[80] Tujifunze
sala ya kuomba neema kufanya atakavyo Mungu, ili aweze kuyaongoza maisha yetu
kwa kutenda yaliyo mema na mazuri. Hivyo wewe uliyekisoma kitabu hiki,
ukakifundishe kwa wengine tena kwa uthabiti kabisa. Na hata Mahatma Gandhi
alisema, ‘kuwa sehemu ya mabadiliko unayotamani kuyaona ulimwenguni.’ Hivyo kwa
mang’amuzi uliyotoa humu kwanza yafanye kuwa sehemu ya maisha yako, hapo
utaweza kuwafundisha wengine. Pia wanasema ‘watu wema wasipotenda wema, uovu
unaongezeka’; nawe uliyepata bahati ya kusoma kazi hii uanwajibu wa kutenda
wema huo kwa kuwamegea kile ulichojifunza kutoka kwenye kazi hii.
Mzaburi anatuambia kuwa “Jueni kwamba Bwana ndiye Mungu;
ndiye aliyetuumba na sisi tu watu wake, tu watu wake, na kondoo wa malisho
yake.”[81]
Tutambue kuwa hatufanyi sawa pale tunapoenda kinyume na mpango wake kwa
kumwacha na kutenda dhambi. Kumbe kila mmoja ajitahidi kwa nafasi yake kumpiga
vita shetani, kwani naamini katika hali ya kutaka kuokoa roho za watu wengine
kupitia mafundisho yaliyomo, basi utakuwa unaiokoa pia roho yako (utaifanya
roho yako yako iokolewe). Wala tusiogope kukemea dhambi maana alituambia yeye
yuko nasi mpaka mwisho wa dahari.[82]
BIBLIOGRAFIA
Bahati Inocent, Huruma ya Mungu ni kwa wote,Uponyaji
wa majeraha ya nafsi kupitia msamaha, Jamana Printers Ltd., Dar es Salaam
2016.
Biblia ya Kikatoliki Toleo la Iringa.
Bula ya Sifa kwako ee
Bwana, Laudato si.
Croucher
L.Sheila, Globalization and Belonging,
The Politics of identity a changing world, Rowman & Littlefied, 2004.
Katekisimu ya Kanisa Katoliki, Pauline publication, Nairobi,
2000.
KangeroW.Wilehard,
Njooni name nitawapumzisha, Nimekuja ili
wawe na uzima tena wawe nao teleTathimini juu ya Jubilee ya kiprkee ya Huruma
ya Mungu, Moshi printing, Moshi,2017.
Kinyashi R. A, Kusali ni Heri Muumba Kumpenda, Toleo la pili, Niim Computers &
Graphics (T), Dar es Salaam, 2013.
Machowera Salvator, Kusali
ni Heri, Hazina za Kanisa Katoliki, Moshi, 2006.
Mavumilio Rogatus, Special Ethics, Kibosho Regional
Philosophicum, Moshi, Unpublished Class Notes, 2017.
Misale ya waamini.
Mbiku H. D., Uchumba
na Ndoa, Toleo la Tatu.
Mbowe S. Benjamini, Thamani
Yetu, Niim Printers & Media Services, Dar es Salaam, 2017.
Mtaguso Mkuu, Maelezo ya Hati 16 za
Vatican II, Jimbo Kuu Tabora,
Toleo la Nne 1993.
[4] Rej., Rum 5:19.
[5] Rej., Tob 4:14.
[6] Rej., Ludwig OTT, Fundamentals of Catholic Dogma, J. C. Bastible
(ed), P. Lynch (trans.), Tan books and Publishers, Inc, Rockford, 1960, Uk.
110-107.
[7] Rej., Ludwig OTT, Fundamentals of Catholic
Dogma, J. C. Bastible (ed), P. Lynch (trans.), Tan books and Publishers, Inc,
Rockford, 1960, Uk. 110-111.
[9] Rej., Ludwig OTT, Fundamentals of Catholic Dogma, J. C. Bastible
(ed), P. Lynch (trans.), Tan books and Publishers, Inc, Rockford, 1960, Uk.112.
[16]Rej., Rej. Ludwig OTT, Fundamentals of Catholic Dogma, J. C. Bastible
(ed), P. Lynch (trans.), Tan books and Publishers, Inc, Rockford, 1960, Uk.
107. & Lk. 10:30.
[17] Rej., Michael Schmaus,
Dogma, God and Creation, Volume 2, Sheed and Ward Ltd, London, 1969, uk.
195-202.
[19] Rej., KKK Na. 405
[22]KKK Na.1488
[23]Rej., Yohane Paulo II, DeV 46
[24]Rej., KKK Na. 2147
[25] Rej., KKK Na. 2150-2151
[26]Katikisimu ndogo ya Kanisa Katoliki
Na.1“kwanini Mungu alituumba? Jibu lake ni kwamba, Mungu alituumba ili tumjue,
tumpende, tumtumikie na mwisho tupate kufika kwake mbinguni”.
[27]2 Tim 4:18
[28] Rej., Yn 14:1-4
[29] Rej., Mwa 1:26-27; 2:7
[30]Mwa 3:22
[31]Rej., Zab 14:4
[32] Rej.,
D. H. Mbiku, Uchumba na Ndoa, Toleo la Tatu, Uk. 24.
[33]Mwa6:6.
[34] Hek 9:1-3.
[35] Rej. Mwa 1:26.
[36] Beatus Kiyabo, Tafakari
Kuhusu Maisha, Nukuu 200 za Watu Maarufu, Nesmap Printing Technology, Dar es
salaam, 2018, uk. 31.
[37]Ibid. uk. 20.
[38] Rej., 1Yoh 4:16.
[39] Salvator Machowera,
Kusali ni Heri, Hazina za Kanisa Katoliki, 2007, uk. 12.
[40]Ibid. uk. 35.
[41]Kitabu
cha Dini Katoliki, Mungu na Wanadamu, Toleo la pili, Benedictine Publications, Ndanda, 1988, Uk.
215-216
[42] Rej., Zab 75:4-5.
[43]Wilehard W. Kangero, Njooni name
nitawapumzisha, Nimekuja ili wawe na uzima tena wawe nao teleTathimini juu ya
Jubilee ya kiprkee ya Huruma ya Mungu, Moshi printing, Moshi,2017, p.24.
[44] Rej., Yak 2:12-13.
[45]Rej., KKK 890
[46]Rej., KKK 924
[47] Rejea, Yak. 4:11-12
[48]KKK 909, Lumen Gentium: LG 36 & 3.
[49] John Ofosu, Uponyaji wa Mti wa Familia, Laana ya Maagano
ya Nafsi Madhara ya Vifungo vya Nafsi, Niim Computers & Graphics (T),
Dar es salaam, 2012, uk. 1.
[50]Rej., KKK Na. 1749-1754)
[52] Sheila L. Croucher. Globalization and
Belonging, The Politics of identity a changing world, Rowman& Littlefied,
2004, uk.10.
[53] Kum 22:5.
[55] LG 48
[56] Haya ni mawazo ya EAST
AFRICA LEGISLATIVE ASSEMBLY-EALA.
[57] Agustiono, Maungamo,
1:1
[58] Gal 5: 16-17.
[59] Kutoka Misale Ndogo
(Chuo cha Waumini Jimbo la Moshi), Chapa ya nane-Novemba 24, 1991, wimbo namba
196 TUKIPENDA WENZETU, uk. 943.
[60] Kwa kweli Yakobo
alimtumikia mjomba wake Labani kwa miaka 20 yaani 7 kwa ajili ya Raheli ambaye
aliambiwa hawezi kumpata kabla ya mkubwa/dada wake. Kwa hiyo, miaka hiyo 7 ya
awali ikawa kwaajili ya Lea. Kwa kuwa alimpenda sana Raheli, alimtumikia tena
mjomba wake Labani miaka 7 mingine kwaajili ya Raheli sasa kwa awamu hii. Na
hapo awali alikuwa amemtumikia kwa kuchunga mifugo wake kwa miaka 6 na ndipo
neno hili linapata maana “Kwa sababu
wewe ni ndugu yangu, basi je, unitumikie bure? Niambie, mshahara wako utakuwa
nini?” (aya 15). Naye akajibu
akasema “Nitakutumikia miaka saba kwa
kumpata Raheli, binti yako mdogo” (aya
18). Utaratibu huu mimi binafsi nauona kama utaratibu uliopo leo wa
‘KUTOA/KULIPA MAHARI’ japo siyo lazima iwe kwa kuchunga na kuoa wake wawili
kama ilivyo kwenye simulizi hili.
[62] Rej. Eugene Kawau,
Uwajibikaji: Dawa kwa Changamoto katika Familia na Jamii, Mafundisho Huru kwa
Watu Wazima, Vijana na Watoto, EKA’s Publication, Dar es salaam, 2017, Uk. 21.
[63] T.E.C, Haki na Amani
katika Familia, 8.
[64] Rej. Eugene Kawau, Op.
Cit., uk. 23-24.
[66]Rejea, Ayu 3:16
[67] Benjamini S. Mbowe, Thamani Yetu,
Niim Printers & Media Services, Dar es salaam, 2017, uk. 18.
[68] Rejea, KKK Na. 2280-2281.
[69]Pew Research Center,www.pewforum.org/2017/08/08/gay-marriage-around-the-world-2013/, retrived on 23/1/2018.
[70]Rogatus
Mavumilio, Special Ethics, Kibosho Regional Philosophicum, Moshi, Unpublished
Class Notes, 2017.
[72]Ibidem.
[73]Ebr 11:1
[74]Rej. Mhu 3:1-11
[75]Rej. Yn 8:31-32
[76]Rej. Muh 9:10
[77]Jean-Paul Sartre, Being and Nothingness, An Essay on
Phenomenological Ontology, trans. Hazel
E. Barnes, , Methuen & Co. Ltd, London, 1958, Uk. 436.
[78]Rej.
Mt 25:34-40.
[79] Eze 33:7-9.
[80] 1Pet 2: 9-10.
[81] Zab 100:3.
[82] Rejea, Mt 28: 19-20.
Subscribe to:
Posts (Atom)
