Tuesday, February 23, 2021

Discovering Yourself

 


Discovering Yourself

The greatest gift you can give yourself is to allow YOU to be YOU. Fears of all kinds stop one from acting or talking freely. Sometimes you want to please everyone but this is not possible. It will be good if you allow yourself to be spontaneous and daring. When you allow your actions to be conditioned always by what others think or say, you risk losing your personality and values.

One thing that you have to do always is to be aware of your feelings and acknowledge them. It is good for you to develop an interior peace that helps you to be confortable wit your emotions whether positive or negative. For example, emotions such as love and hate, courage and fear, discouragement and anger and so on are part of you. If you do not accept your emotions it means you are denying them. When you do this, the emotion manifests itself in destructive ways such as outbursts of anger or even physical illness eg. Headache, backache, lack of sleep, e.t.c. on the other hand if you accept your emotions positively you will be able to express them freely.

Getting to know oneself is not one day’s job. Sometimes you discover something about yourself that you do not like. Real and genuine self-knowledge can at times be disturbing, frightening and humiliating. It is possible for you to be discouraged and not want to discover this aspect of YOU, but you will be living with a false concept about yourself. You need to see yourself as you really are and accept your strengths and weaknesses, your gifts and talents.

Who you are goes beyond your name, your dreams, your career, your academic achievements and your friends. You are that irreplaceable gift that God has blessed this world with, so you have to discover yourself in order to be a gift to all. You might say, I am my body, mind, will and heart, abilities and talents, qualities, virtues, defects, character, ambition, effort, past, present and future, my relationships, attitudes and approaches, what I want to make of myself, my aims and goals. I am a being who is ever becoming. I can conclude by saying..What I am is God’s gift to me; what I make of myself is my gift to God and you society! (Dr. George Kaitholil, SSP) 

Tuesday, September 1, 2020

mwendelezo 2

 Sehemu ya pili: muendelezo wa post inayohusu "HUU NDIO UKWELI JUU YA KANISA ALILOLIANZISHA KRISTO"


PETRO ANASIMAMA KUMUWAKILISHA KRISTO MOJAKWAMOJA KWA KANISA LAKE LINALOSAFIRI HAPA DUNIANI. NDIYO KUSEMA KWAMBA KRISTO KABLA YA KUFA ALIMTEUA PETRO ALISIMAMIE KANISA LAKE HAPA DUNIANI KWA NIABA YAKE. HIVYO BASI, KANISA ANALOLIONGOZA NA KULISIMAMIA MTUME PETRO NDILO KANISA LA KWELI LILILOANZISHWA NA KRISTO MWENYWEWE. 

  KWAVILE MTUME PETRO KAMA ILIVYO KWA BINADAMU WENGINE, ALIKUFA; KWAHIYO JUKUMU ALILOKUWA ANALIBEBA LA KULIONGOZA KANISA LA KRISTO, ILIBIDI IENDELEZWE KWA KUMTEUA MTU ATAKAYE SHIKA NYAZIFA YA PETRO (YAANI ATAKAYEKIKALIA KITI CHA MTUME PETRO) MIONGONI MWA WAAMINI. UTARATIBU HUU UNGEENDELEA VIZAZI KWA VIZAZI PALE ITAKAPOTOKEA KIONGOZI HUYO AMEKUFA. 

  HIVYO, UTARATIBU HUO WA KURITHISHANA MAMLAKA KWA KITI CHA MTUME PETRO ULIENDELEZWA KARNE KWA KARNE TOKEA KARNE YA KWANZA MPAKA SASA AMBAPO KANISA ZIMA HUKAA KWA UMOJA NA KWA KUSALI HUKU LIKIONGOZWA NA ROHO MTAKATIFU LINAMCHAGUA KIONGOZI MMOJA ATAKAYESHIKA NYAZIFA YA MTUME PETRO( ATAKAYE KIKALIA KITI CHA MTUME PETRO) YAANI BABA MTAKATIFU ALIYE KHALIFA WA MTUME PETRO.

            ALAMA AU SIFA ZA KANISA KRISTO                                                   ALILOLIANZISHA


LICHA YA KUWEPO NA MFUMUKO WA MAKANISA YANAYOANZISHWA NA WATU KILAKUKICHA NA HIVYO KUPELEKEA KUWEPO NA SINTOFAHAMU JUU YA LIPI KANISA HALALI ALILOLIANZISHA KRISTO; KANISA LA KRISTO ALILOLIANZISHA LINA ALAMA ZIFUATAZO:

                   KANISA HILO NI MOJA

TUTAMBUE KWAMBA KRISTO HAKUANZISHA MAKANISA, BALI ALIANZISHA KANISA (NITALIJENGA KANISA LANGU... Mt 16:18)

KRISTO ANATUMIA NAFSI YA KWANZA UMOJA "NITALIJENGA KANISA LANGU..." KUDHIHIRISHA KUWA KANISA LAKE LITAKALO JENGWA JUU YA MWAMBA, YAANI PETRO NI MOJA TU "KANISA" NA MUANZILISHI WAKE NI MMOJA TU NAYE NI KRISTO MWENYEWE "NITALIJENGA" NA WALA SIYO NABII FULANI AU ASKOFU FULANI, AU MCHUNGAJI FULANI, N.K. 

INGAWAJE SASA KUMEIBUKA WIMBI LA MFUMUKO WA MAKANISA, KILA MTU ANAIBUKA NA KUANZISHA KANISA LAKE ANAVYOJISIKIA NA KADIRI YA MTAZAMO WAKE BINAFSI. 

   KANISA KAMA ASEMAVYO MTUME PAULO NI MWILI WA KRISTO (WALA SI MIILI YA KRISTO) KWASABABU KAMA VILE MWILI ULIVYO MMOJA UKAUNGANIKANA NA KICHWA, VIVYO HIVYO NA KANISA ALILOLIANZISHA KRISTO NI MOJA( MWILI WA KRISTO, AMBAPO KRISTO NDIYE KICHWA CHA HUO MWILI). UMOJA HUU WA KANISA UNAJIDHIHILISHA KATIKA USIMAMIZI NA UONGOZI MMOJA WA KANISA ZIMA CHINI YA KHALIFA WA PETRO YAANI BABA MTAKATIFU AMBAYE KWAKE AMEPEWA DHAMANA NA KRISTO KULICHUNGA KANISA ZIMA ALILOLIANZISHA(KRISTO) "CHUNGA KONDOO WANGU" (Yoh 21:16).

     Itaendelea katika post inayofuata(tar 4/9/2020)

Thursday, August 27, 2020

Kanisa la Yesu - Katoliki

 HUU NDIO UKWELI JUU YA KANISA ALILOLIANZISHA                                        KRISTO

           PETRO NA KANISA LA KRISTO

"WEWE NDIWE PETRO NA JUU YA MWAMBA HUU NITALIJENGA KANISA LANGU"

        

  KANISA 

NI JUMUIYA YA WAAMINI WANAO SADIKI KATIKA KRISTO, TAIFA TEULE LA MUNGU LINALOAMINI KATIKA KRISTO YESU. KWA MTUME PAULO ANALIELEZEA KANISA YAANI JUMUIYA YA WAAMINI WANAOAMINI KATIKA KRISTO, KUWA NI MWILI WA KRISTO.

  

KABLA YA KUFA KWAKE, KRISTO ALIWAHAKIKISHIA MITUME WAKE KUWA HATOWAACHA YATIMA, BALI ATAENDELEA KUWA NAO, NA KUZIENDELEZA KAZI ALIZOKUWA AKIZIFANYA.  

  KWAKUWA KAZI HIYO ILIWAHITAJI WATU, HIVYO KRISTO ALIWATEUA BAADHI YA WATU WATAKAO IENDELEZA KAZI YAKE NA KISHAWATEUA ALIWAKABIDHI MAMLAKA, HAWA SI WENGINE BALI NI MITUME KUMI NA WAWILI AMBAO KWAO MWILI WA KRISTO YAANI KANISA LILISIMIKWA. 

  

KRISTO KWA KUZINGATIA UKWELI KWAMBA KANISA ALILOLIANZISHA NI MWILI MMOJA HUSIO GAWANYIKA (MWILI WA KRISTO) ALIPENDA KUTEUA MIONGONI MWA HAO MITUME WAKE MTUME MMOJA AMBAYE ANGELETA UMOJA WA HILO KANISA ALILOLIANZISHA, NDIYE MTUME PETRO. 

  KRISTO ALIPENDA KUMTEUA PETRO KUWA KIONGOZI MKUU WA KANISA LAKE ALILOLIANZISHA AMBALO KAMA TAASISI YA WATU WA MUNGU WANAO AMINI KATIKA KRISTO YESU ILIPASWA KUWEPO NA KIONGOZI MKUU MMOJA ATAKAYESIMAMA KWA NIABA YA KRISTO HAPA DUNIANI ILI KUENDELEZA HUO UMOJA WA KANISA. 

  HIVYO BASI, NI PETRO ANAYESIMAMA KWA NIABA YA KRISTO NA AMBAYE AMEKABIDHIWA MAMLAKA JUU YA KANISA ALILOLIANZISHA KRISTO (NITAKUKABIDHI FUNGUO ZA UFALME WA MBINGUNI, LOLOTE UTAKALO LIFUNGA DUNIANI LITAKUWALIMEFUNGWA MBINGUNI; NA LO LOTE UTAKALOLIFUNGUA DUNIANI LITAKUWALIMEFUNGULIWA MBINGUNI 'Mt 16:19'), NA KUMKABIDHI UANGALIZI WA KANISA ZIMA LA KRISTO ( CHUNGA KONDOO WANGU 'Yoh 21:16'). 

  PIA NI KWAKUPITIA MTUME PETRO IMANI YA HAO WANAOMUAMINI KRISTO ITAWEZA KUIMARISHWA  (NIMEKUOMBEA WEWE ILI IMANI YAKO HISIPUNGUE NAWE...UWAIMARISHE NDUGU ZAKO...'Lk 22:32')

      Fuatilia muendelezo wake katika post inayofuata


Tuesday, April 14, 2020

NAMBA 666

FAHAMU NAMBA 666 AU 616 ILIYOANDIKWA KWENYE UFU 13:18 HAIMHUSU PAPA ISIPOKUWA ELLEN GOULD WHITE

(Anaandika Baba Titus Amigu: (Padri na gwiji/mwamba wa Theolojia).

Imbeni pamoja nami ALLELUYA! Kwa nini? Kwa sababu Mungu amenitendea makuu. Amenisaidia kukitegua kitendawili cha karibu karne mbili sasa, yaani kitendawili cha namba 666. Kwa muda mrefu tangu enzi za akina ELLEN GOULD WHITE, yaani miaka ile ya 1846, namba 666 ya katika Ufu 13:18 imekuwa ikielekezwa kwa majungu na matusi kwa Baba Mtakatifu. Ndugu zanguni, tulikuwa tunazugwa tu. Kumbe, siri ni kwamba ilikuwa inamwelekea mwenyewe aliyekuwa anaelekeza mashambulizi na matusi kwa Baba Mtakatifu, yaani ELLEN GOULD WHITE.

Nina furaha kubwa sana. Nawaalikeni mfurahi pamoja nami. Binafsi, nilikuwa napata taabu sana kujaribu kufumbua kitendawili hicho. Lakini, wakati huo huo, nilikuwa najiuliza kwa nini mashambulizi kwa Baba Mtakatifu ni makali hivyo? Kumbe, sasa tumefumbuliwa. Yote yalikuwa ni mbinu ya kutupoteza watu “maboya” tusijue kwamba namba inamwelekea mwenyewe anayetukana. Kumbe, ilikuwa ni mbinu ile ile ya mwizi kupiga kelele za “Mwizi, mwizi, mwizi huyo!” kusudi watu wamfukuze mtu mwingine na siyo yeye mwenyewe.

Acheni niwakumbusheni mambo. Nadhani nyote mna habari na mashtaka maarufu sana dhidi ya Wakatoliki kwamba namba 666 au 616 inamhusu kiongozi wetu mkuu yaani Papa au Baba Mtakatifu na kwamba namba hiyo imeandikwa kwenye mavazi yake na kofia yake. Zaidi ya hapo kuna madai kwamba namba hii ipo pia katika kompyuta na satelite. Leo nataka niwafunulieni mambo yalivyo.

Hii ni Mada ya Lugha na Hesabu Kidogo
Vijana wangu msishtuke na kuhangaika. Mada hii itahusisha herufi za Kiebrania na Kigiriki lakini zitakuwa chache tu nanyi mtaelewa yote nitakayoandika kwani ni masuala rahisi kuyafuatilia. (Kwa bahati mbaya herufi za Kigiriki zinakataa humu). Papo hapo, kutakuwa na hesabu. Hata hizo hazitawahangaisheni kwani ni hesabu za kujumlisha tu. Leo kumbukeni pia hesabu za Shule ya Msingi tulipokuwa tunatumia tarakimu za Kilatini, kwa mfano, I = 1, V = 5, X= 10, L = 50, C= 100, D = 500 na M = 1000.
Ili tuelewane, nitaanza na historia, kishapo nitakwenda nje ya Biblia ilikohamishiwa namba 666.

Mama ni Historia
Hebu nianze na jibu fupi linalolingana na historia. Wayahudi hujumlisha thamani ya kitarakimu majina ya watu na maneno mbalimbali na kuzaa namba mbalimbali. Kuhesabu kwa namna hii huitwa gematria nako kumetumika katika Ufu 13:18 na kuzaa namba 666 au katika nakala zingine za Biblia namba 616. Swali kubwa ni je, namba hiyo inamhusu nani? Ukweli ni kwamba namba 666 au 616 haimhusu Papa au Baba Mtakatifu hata kidogo. Tena haikuandikwa katika mavazi ya Papa na wala haimo katika kompyuta ama satelite.

Ukweli, kibiblia na kihistoria, ni kwamba namba hiyo ilimhusu na bado inamhusu kiongozi wa dola ya Kirumi zamani zile, yaani Kaisari Nero. Basi, namba 666 au 616 ndiyo hesabu ya jina la Nero aliyekuwa akiwadhulumu Wakristo katika karne ya kwanza ya Ukristo. Hesabu hiyo inapatikana kwa kukokotoa kigematria maneno NERON KAISAR (kwa Kiebrania - נרון קסר) au NERO KAISAR (kwa Kiebrania - נרו קסר) na KAISAR THEOS (kwa Kigiriki).

Jibu refu: Hakuna mahali po pote katika Biblia ambapo msomaji ameombwa kutumia akili isipokuwa hapa. Kwa kuwa ili kuipata hesabu hii kulihitaji kupiga hesabu, wasomaji wote wa kifungu kile walialikwa kupiga hesabu, gematria. Ndipo imeandikwa “Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili na aihesabu hesabu” (Ufu 13:18). Kumbe, kinyume na matumizi ya akili, hapa ndipo mahala wasomaji kadha wa kadha wasipotumia akili yoyote katika kusoma isipokuwa majungu na usingiziaji.

Ndugu yangu, wapo watu chungu nzima wanaoeneza tafsiri kwamba namba 666 au 616 inamhusu Baba Mtakatifu na imeandikwa kwenye mavazi yake kama nilivyosema hapo juu (rejea Ufu 13:18, 15:2). Je, mafundisho hayo yana ukweli? Najijibu mwenyewe: Si ya kweli.

Tusisahau, kitabu cha Ufunuo wa Yohane kina mazingira yake ya kihistoria ambayo ni muhimu katika kuielewa sura ya 13. Mazingira hayo ni ya historia ya Dola ya Kirumi. Wakristo walipokuwa wakidhulumiwa na dola hiyo, mwandishi wa kitabu cha Ufunuo alichukua kalamu na kuandika ili kuwaliwaza ndugu zake aliokuwa akiteseka pamoja nao (rejea Ufu 1:9). Basi, katika kuandika akatumia lugha ya mafumbo ili watesi wasifahamu wanayosemwa. Ndicho kisa, basi, joka kuu lenye pembe na kadhalika linamaanisha Dola ya Kirumi. Mkubwa wa dola hiyo naye akapewa jina la kupanga au jina la kifumbo kwa mtindo wa kucheza na namba za jina lake (gematria).

Ukitaka kupata picha kidogo ya haya, chukulia mfano wa vitabu vya marehemu Shaban Robert. Yeye aliandika mashairi mengi ya kuwatia watu hamasa wapiganie uhuru. Katika mashairi hayo, wananchi anawaita, mathalani, siafu na wakoloni nyoka. Hao siafu wanakazana kumdhuru nyoka. Aidha, kitabu chake cha Kusadikika ni kitabu cha fumbo kinachofumbia hali ya mambo katika hewa ya kikoloni. Kwa hakika wakoloni hawakuambulia lolote katika mashairi na fasihi ya Shaban Robert. Kinyume chao, wananchi walielewa mada husika na “kuwaacha kwenye mataa” wakoloni.

Ndivyo inavyotokea shuleni, mwalimu mbaya kupangwa jina ambalo mwenyewe halijui hata kama litatajwa mbele yake.
Upangaji wa jina la mtu kwa kutumia hesabu ya herufi za jina lake mwenyewe ulikuwa mtindo maarufu wa marabi na ulijulikana kama gematria. Ufu 13:18, si mahali pa kwanza kutumia gematria hata namba kumi na nne ya vizazi vilivyotajwa katika Mt 1:17 ni gematria ya jina Daudi (דוד) kwani d + w + d ni 6 + 4 + 6 = 14. Sasa ni nani katika karne ya kwanza aliyekuwa adui wa Wakristo na jina lake kigematria lilizaa namba 666 au 616? Hili ndilo swali la kuulizana. Alikuwa KAISARI NERO.

Tukitafsiri Biblia kwa usahihi huu, mtesi wa walengwa wa kitabu, aliyekuwa akifumbiwa katika 13:18 kwa kuhesabu jina lake kigematria, hawezi kuwa mtu wa karne ya tano au ya ishirini na moja. Walengwa walikuwa ni Wakristo wa karne ya kwanza na adui yao alikuwa akiishi nao kwa wakati huo huo. Basi, nani alikuwa mtesi maarufu katika mazingira ya karne ya kwanza? Wakati ule alikuwa Kaisari Nero ama Kaisari fulani aliyejidai kuwa Mungu na huyo ndiye kigematria jina lake linazaa namba 666 au 616.

Basi, gematria ikitumika kwa konsonanti za Kiebrania: נרון קסר - NERON KAISAR (yaani Kaisari Neron) au kwa maneno ya Kigiriki: KAISAR THEOS (yaani Kaisari Mungu) tunapata pasipo kuzunguka zunguka namba 666 au 616. Tazama hesabu zenyewe zinavyofanyika. (נרון קסר) r s q n w r n = 200 + 60 + 100 + 50 + 6 + 200 + 50 = 666.
k a i s a r th e o s = 20 + 1 + 10 + 200 + 1 + 100 + 9 + 5 + 70 + 200 = 616.

Angalia vyema. Hii tafsiri ya ‘KAISAR THEOS’ yaani ‘Mungu Kaisari’ ndiyo inayorejewa kwenye Biblia zenye kuandika jumla ya namba 616. Lakini vile vile 616 iliweza kupatikana kwa kuondoa “n” ya mwisho kwenye jina נרון (n w r n) katika Kiebrania. Kwa Wakristo, namba 666 ilipomtaja Neron ilisema pia kwamba ni MPINGA KRISTO kwani alikuwa kinyume cha utimilifu. Kinambari, utimilifu ni namba 777. Kumbe, yeye Kaisari Nero ni upungufu kwani hesabu yake ni 666 ambayo ni 777 kutoa 111.

Basi, kwa kuzingatia mazingira ya kitabu cha Ufunuo namba 666 au 616 haiwezi kusimama kwa ajili ya jina lingine kama Baba Mtakatifu, Mtume Mohamed au Mussolini. Haya ni baadhi ya majina wanayolazimisha watu yafanye hesabu ya 666. Na, kwa hakika, namba hiyo haimo katika mavazi wala kofia (mitra) ya Baba Mtakatifu. Hakuna mtu yeyote anayeweza kuonesha vazi hilo au kofia hiyo kwa ushahidi. Kwani ni vazi gani au kofia ipi? Basi, kama tunautafuta uzima wa milele, aheri tuache majungu na uongo kama huu. Kama ni maandishi, ni mitra yake tu yenye herufi mbili A na W yaani alpha na omega (rejea Ufu 1:8,17).

Acha tuendelee. Wanaombambikizia Baba Mtakatifu namba 666 hudai kuikokotoa nambari hiyo katika majina matatu tofauti: jina la Kilatini VICARIUS FILII DEI (Kaimu wa Mwana wa Mungu), jina la Kigiriki LATEINOS (Mlatini) na jina la Kiebrania ROMIITH (רמיית - Mrumi). Majina hayo huhesabiwa na wanaombambikizia Baba Mtakatifu namba hiyo kama ifuatavyo:

VICARIUS FILII DEI = 5 + 1 + 100 + 0 + 0 + 1 + 5 + 0 + 0 + 1 + 50 + 1 + 1 + 500 + 0 + 1 = 666.
LATEINOS = 30 + 1 + 300 +5 + 10 + 50 + 70 + 200 = 666.

ROMIITH yaani th y y m w r = 400 + 10 + 10 + 40 + 6 + 200 = 666.

Ndugu zangu, kwa misingi halali ya kusoma Biblia hatuwezi kuyapokea majina haya bila kuyafanyia tahakiki ya kihistoria. Bila kurefusha mjadala, majina haya hayajapata kutumiwa na Baba Mtakatifu yeyote, katika historia ya Kanisa sembuse wakati wa karne ya kwanza Baada ya Kristo wakati ambao hata upapa wenyewe ulikuwa haujakua. Mapapa wa karne zile hawakuwa hatari kwa mtu yeyote. Na watu wasio hatari watapewaje majina ya kupanga na ya siri? Wale wasomaji wa kitabu cha Ufunuo wangelielewaje aya ngumu inayotaja kitu kisichojulikana kwa jina hilo? Wangelifanyaje gematria kwa kutumia majina wasiyoyajua?

Aya 13:18 ilizungumzia jina ambalo wasomaji walikuwa wakilijua kama jina la adui yao aliyekuwa akiwadhulumu na si majina ya ndoto au majungu ya karne ya 20 na 21 B.K. Zaidi ya hayo majina mengine yamelazimishwa kihesabu ili jumla ya kiherufi iwe 666. Kwa ushuhuda tazama U ilivyolazimishwa imaanishe tarakimu 5. Katika Kilatini 5 ni V na wala siyo U. Zaidi ya hayo, jina “MLATINI” kama lingelitumika wakati huo, wasomaji wangelielewa kuwataja wakoloni au askari wa kirumi ambao walikuwa wakitawala ulimwengu wa wakati ule.

Hali kadhalika, kama jina “MRUMI” lingelitumika wakati huo, wasomaji wangelielewa kuwataja wakoloni au askari wa kirumi ambao walikuwa wakitawala ulimwengu wa wakati ule. Kwa hoja hizi, majina hayo ya majungu ni ya tangu karne ya 16, Kanisa Katoliki lilipoanza kupingwa kwa ari mpya na uongozi wake kukataliwa.

Nadhani hadi hapa kila mwenye kutaka kujua anajua kwamba majina waliyobuni Wasabato hayatumiwi na Baba Mtakatifu yeyote. Na zaidi ya hayo ni majina ambayo mwandishi wa kitabu cha Ufunuo hakuwa hata na habari nayo katika karne ile ya kwanza B.K. kwa vile alivyokiandika kitabu chake kwa Kigiriki na wala si kwa Kiebrania au Kilatini. Kumbe, kwa kufanya hivyo Wasabato huwa wanainyonga historia na kukizungumzia kitabu cha Ufunuo nje ya muktadha wake wa kihistoria. Hili ni kosa la kusiganisha nyakati za kikalenda (kwa Kiingereza “anachronism”).

Basi, kwa heshima ya Maandiko Matakatifu, tutafsiri namba 666 au 616 kwa gematria asilia na tukomee hapo hapo. Tusiihamishe namba hiyo na kuwapachika watu wasio na hatia. Kufanya hivyo ni kujitowelesha majungu na ni dhambi isiyo na maana yo yote. Lakini, basi namba 666 imetolewa nje ya mazingira ya Biblia na ndipo ilipowekwa sasa. Nami nimefika hapo hapo.

Namba 666 Imehamishiwa Nje ya Biblia

Ni kituko lakini ndivyo ilivyo. Watu wengine hudai kwamba namba hiyo imeandikwa shingoni kwenye nguo za Papa. Huo ndio uongo na usingiziaji usio na aibu kwa sababu nguo hizo hakuna anayeweza kutuonesha wenziwe. Siku moja niliwahi kuambiwa na wainjilisti wawili kwamba namba 666 ipo kwenye bidhaa za siku hizi, yaani kwenye kifungashio, pale inapochorwa mistari mingi mifupi na mirefu na kuandikwa namba kwa chini, na kwa namna hiyo ipo pia kwenye satelite. Siku hiyo niliwakamata kutokujua nilipowadai wanioneshe mfano. Basi, wakaleta baadhi ya bidhaa za kisasa, wakaniambia niangalie ile mistari iliyochorwa katika kifungashio cha kila bidhaa. Hapo walionesha pia mistari miwili miwili inayojitokeza zaidi kwa chini (jambo ambalo si kweli kwa kila bidhaa). Basi, hapo ndipo walipodai kuna namba 666.

Kumbe, huu ulikuwa ujinga wao mkubwa. Ndugu yangu, mistari hiyo, ndiyo bei ya bidhaa hasa kwa zile zinazouzwa „“supermarket. Katika nchi zilizoendelea watu hawaandiki bei shilingi fulani au fulani wakabandika kwenye bidhaa. Badala yake ndiyo hiyo mistari, kadiri ilivyochorwa ndivyo mashine ya kupigia hesabu inavyotambua na kutofautisha bei za bidhaa ambazo mnunuzi amezifikisha kwenye “kaunta” ya kulipia manunuzi. Na tena bei hizo hazikuingizwa katika satelite; zilivyo nyingi hazihusishwi na satelite yoyote.

Nilifanyaje? Nilichukua kauli tatu: PONYA SIKU MUHIMU YA SABA (kwa Kiingereza CURE VITAL SEVENTH DAY, kwa Kilatini CURATUS VITALE SABBATA DIES) na WOKOVU, PONYA SIKU YA SABA (kwa Kiingereza SALVATION, CURE SEVENTH DAY, kwa Kilatini SALVUS, CURARE SABBATA DIES) na VUNJA, CHUKIA UPAPA (kwa Kiingereza DEAL AXE, VIE PAPACY). Nilistaajabu sana kuona ndiyo inakuja 666 ndipo mara moja nikaingiza ugunduzi wangu katika kitabu changu KISA CHA IMANI namba 1.

Ni kweli. Kauli mbiu za Wasabato ni namba hiyo hiyo 666. Angalia gematria inavyokwenda:
CURE VITAL SEVENTH DAY = 100 + 5 + 0 + 0 + 5 + 1+ 0 + 0 + 50 + 0 + 0 + 5 + 0 + 0 + 0 + 0 + 500 + 0 + 0 = 666
CURATUS VITALE SABBATA DIES = 100 + 5 + 0 + 0 + 0 + 5 + 0 + 5 + 1 + 0 + 0 + 50 + 0 + 0 + 0 + 0 + 0 + 0 + 0 + 500 + 1 + 0 + 0 = 666

SALVATION, CURE SEVENTH DAY = 0 + 0 + 50 + 5 + 0 + 0 + 1 + 0 + 0 + 100 + 5 + 0 + 0 + 0 + 0 + 5 + 0 + 0 + 0 + 0 + 500 + 0 + 0 = 666
SALVUS, CURARE SABBATA DIES = 0 + 0 + 50 + 5 + 5 + 0 + 100 + 5 + 0 + 0 + 0 + 0 + 0 + 0 + 0 + 0 + 0 + 0 + 0 + 500 + 1 + 0 + 0 = 666
DEAL AXE VIE PAPACY = 500 + 0 + 0 + 50 + 0 + 1 0 + 0 + 5 + 1 + 0 + 0 + 0 + 0 + 0 + 100 + 0 = 666

Kuendelea Kutafuta
Basi, kwa kuwa nilikuwa namtafuta nani mwingine anayesemwa na namba 666 au 616, nikagundua kumbe ni hao hao wanaotukana. Lakini, sikukomea hapo mwaka huu 2017 macho yangu yakasaidiwa kuona zaidi. Nilichukua jina la mwasisi wa matusi mwenyewe ELLEN GOULD WHITE ndipo nikashtuka kabisa kumbe ni namba 666. Kwa kisa hiki, leo nawaomba tuimbe alleluya pamoja.

ALLELUYA! KUMBE NAMBA 666 NI ELLEN GOULD WHITE MWENYEWE
Sasa nawapeni habari njema kabisa. Tusi la namba 666 limefumbua macho yangu kwa namna ya ajabu na sasa nawatangazia wote nilichokigundua ili kiwafumbue macho ninyi pia. Kifupi, nimefikishwa kwenye ugunduzi huo kwa kupitia tahadhari ya wahenga. Wao walisema, “Unapokula na kipofu, usimguse kipofu mkono!” Msidanganyike tena, namba 666 ni ELLEN GOULD WHITE mwenyewe.

Tuamke. Jamani, Bi Ellen Gould White alikuwa anapiga kelele na kutukana kusudi tusishughulike na jina lake. Wafuasi wake wakadakia mbinu hiyo hiyo. Kumbe, Wasabato hukazania namba 666 imwelekee Baba Mtakatifu kwa sababu walitaka tusijue kwamba namba 666 inamwelekea “nabii” wao ELLEN GOULD WHITE! Walitaka tukamsake sungura katika kichaka kingine. Kumbe, Ufu 13:18 inamtaja Bi Ellen White moja kwa moja kama mnyama ambaye jina lake ukilikokotoa linakuja moja kwa moja kwenye namba 666. Yaani linakuja 666 taslimu!

Je, unaniuliza kwa vipi? Ni hivi ifuatavyo. Ukiliandika jina la Bi ELLEN WHITE pamoja na jina la asili yake GOULD unakuja kwenye namba 666 juu ya alama. Nifuatilie vyema hapa kusudi tukokotoe tarakimu pamoja. Lakini, angalia vyema, jambo lile la kuhitajika hekima, linahusisha pia kuirudisha “W” ya WHITE kwenye uasilia wake yaani V maradufu (kwa Kiingereza “double v”). Kwa taarifa yako, tangu kale “W” ni “V” mbili na ni kwa sababu ya asili hiyo Wajerumani huitamka “W” kama “V”. Umeshanielewa uzuri? Kama umeshanielewa, sasa tazama “gematria“ inavyokubali:

E L L E N G O U L D W H I T E
0+ 50 + 50 + 0 + 0 + 0 + 0 + 5 + 50 + 500+ 10+0+1+0+0 = 666

Je, unaona jinsi jina la Bi Ellen White linavyokubali kama jina la mnyama yule? Yaani sawa sawa pasipo kuacha mashaka yoyote. Kinyume chake, jiulize ni Baba Mtakatifu gani mwenye jina kama hilo? Maskini, Wasabato walisahau jambo hili la kimahesabu! Lakini nadhani wanalifahamu na ndiyo maana hufanya juhudi kubwa kulikoneshea tusi la namba 666 kwa Baba Mtakatifu. Ni janja yao lakini sasa ipo hadharani.

Narudia. Wanachofanya Wasabato ni mbinu ya kawaida tu, yaani kwamba ukitaka watu wasikuangalie wewe elekeza umakini wao kwa mtu mwingine au kitu tofauti. Ndipo, badala ya watu kuelekeza umakini kwenye jina “ELLEN GOULD WHITE” huzugwa waelekeze kwenye majina ya kubuni ya “VICARIUS FILII DEI”, “LATEINOS” na “ROMIITH”, majina yasiyo na maana yoyote kihistoria na muktadha wa kitabu cha Ufunuo.
www.radiombiu.co.tz
#RmSautiYaFaraja

Wednesday, March 4, 2020

NDOA ZA BLUETOOTH

BADO NINALIA NA NDOA ZA BLUETOOTH!
(ZILE ZA MUME YUPO SONGEA MKE ANAISHI TANGA)

Mtunzi: Hajulikani

Chanzo: Chat WhatsApp History za FHWF

Mwaliko: Hii ni sehemu ya madini yanayoendelea kutumwa ndani ya forum hiyo (FHWF) ili kuendelea kubadili fikira na mitazamo hasi kuhusu ndoa na familia. Karibu ujiunge na Jukwaa hilo, tuma maneno "MADINI YA NDOA NA FAMILIA" kwa Ma-Admin wa FHWF: +255 767 818 542 (Chief Admin), +255
716 669 895 (Co-Admin)

#MaleziYaWatoto, #NdoaZaBluetooth, #DistantLove, #DistantMarriage, #MaishaYaPamoja

--Memo hii, Ikiisha somwa, yafanyike maombi na dua maalumu---

NAKALA KWA:-

-Maparoko wote,
-Mashehe wote
-Mapasta wote,
-Maaskofu wote,
-Mnaotarajia kuingia kwenye ndoa.

DANGER! DANGER!

Hii ni memo ngumu sana inayoweza kukuudhi maana nimejifunga MABOMU kuyasema ambayo hungependa kuyasikia ukweli.

SASA TWENDENI......

Ndugu wanandoa,
Mnaomiliki ndoa za Bluetooth,
Nawasalimu salamu za kimakinikia!

Mahusiano ya wanandoa wanaoishi sehemu tofauti kwa kigezo cha kazi au masomo ni hatari Sana kwa ustawi wa ndoa yako,ni sawa na mtu anayelima shamba Iringa yeye anaishi dar ,yeye anapiga simu tu na kutegemea kuvuna mavuno kedekede.

Mme unaishi Mwanza mke anaishi mtwara halafu mnasema mmeoana.Ninakupa tahadhari kwa nguvu ya Roho Mtakatifu aliyeko ndani yangu. Eva alikuja kurubuniwa na nyoka baada ya kuona kuwa Adamu ameondoka,nina uhakika kama Eva angekuwa na mme wake nyoka asingethubutu kumsogelea Eva na kumdanganya.

Kuna mambo mengine mkiwa mnaishi pamoja mke na mme shetani hawezi kuthubutu kuyaleta ila ile kutengana shetani anapata hapo mwanya wa kuja kuwajaribu.Nimeshuhudia ndoa nyingi ambazo zimepigwa kwa jinsi hii.Ninawaonya binti zangu BHM na wale mlio kwenye ndoa tayari kuepuka jambo hili kwa garama yoyote.Msije kusema sikuwambia.

ELOI! ELOI!

Mimi nina pointi 10 nilizokuletea ili ikiwezekana uokoe hili janga lililokuzunguka

1). Kinachosababisha kufika hali hii sio serikali kukataa kuhamisha watumishi, bali ni wafanyakazi wenyewe kukataa kuhamisha akili. Shida ya kwanza kwa wengi ni kuamini kwamba ajira ni kila kitu. Shida ya pili ni vipaumbele. Ukiona unaacha mke Dar unaenda kufanya kazi Mtwara, na mke nae akawa mwajiriwa na miongoni mwenu hakuna alietayari kuacha kazi kumfuata mwingine, mjue kwamba wote wawili hakuna ambae ameweka ndoa kama kipaumbele cha kwanza!

2). Nioneshe mtu aliewahi kuthamini ajira kuliko ndoa halafu ndoa ikabaki salama kwa muda mrefu. Mnaweza kusema ohooo, tunaaminiana, mara ohooo, mke wangu/mume wangu hawezi kunisaliti, sikatai! Enhee, akishakuwa hajakusaliti what is next? Nyie ni watu wazima bana, naomba niwaeleze kwamba kuna mambo ambayo maombi yanaweza kuhamisha, lakini kuna mambo yapo mwilini huwa hayahami kwa maombi ng'oooo. Ukiamua kubisha shauri yako mwenyewe! Wewe umekomaa na ajira yako huko Mwanza mume umemuacha Dar, halafu unategemea maombi ya kwa Nabii Malisa, eti Mungu amlinde mumeo kule Dar? Subiri uvune mabua, ndio utaelewa!

3). Halafu aliewaambia kwamba mmoja akiacha ajira kumfuata mwingine, eti mtakufa na njaa nani? Shida yenu ni kwamba tukiwaelekeza ujasiriamali mnaona as if hauwahusu, ndio maana ajira mnazitetemekea kiasi cha ku-risk ndoa zenu. Aliekudanganya kwamba ukiwaachia liajira lao wanalokulipa "vilaki nane", ukamfuata mke/mme na kupiga ujasiriamali, utakosa kuzalisha zaidi ya laki nane, ni nani huyo? Unajua ninawamaindi kwa sababu, nilishawaelezaga kwamba kwenye ajira mnalipwa asilimia chini ya kumi ya mnachozalisha, sasa kinawashinda nini kuzitoa sadaka ajira ili mkaokoe ndoa? Nakuona tu unavyonibinulia midomo, na kunifyonya, lakini huu ndio ukweli.

4). Haya basi! Tuseme ninyi ni wa kisasa, so, ishu ya ndoa ya bluetooth haiwasumbui, je, hayo malezi ya watoto inakuwaje? Mke Kigoma, mume Arusha, watoto wako boarding Tabora! What a wastage of parentalhood! Shida yenu mlio wengi mnadhani ni sifa kupeleka watoto wa chekechea boarding in the name of kutingwa ama in the name of ajira. Laiti mngekielewa ambacho Mtume Paulo alimweleza Timotheo kuhusu watoto (2Tim 3:15), msingekubali mtindo huu, ama mtindo wa baba kusubiri miezi sita ama mwaka ndio akawaone watoto kwa mkewe, maana watoto wanalelewa na mama Songea baba akiwa kazini Dodoma!

5). Hadi hapa najua nimeshawakorofisha watu, maana ndoa za masafa siku hizi imekuwa ndio fasheni, kwamba mke na mume wakikutana ni spesho kwa ajili ya ujauzito na from there huyu kule mwingine huko. Hivi aliewaeleza kwamba ndoa ni just ijulikane umeoa ama umeolewa ni nani? Kwani haijaandikwa kwamba mmeoana ili muishi pamoja?

Hata hizo hela mnazotafuta (if ni nyingi kihivo) mnawezaje kuzipangia matumizi na maendeleo ya familia? Au ndio mnategemea bando la halichachi na jazwa ujazwe na WhatsApp kujadiliana kuhusu familia? Hivi mnajua kwamba kuna nguvu kubwa kupanga mambo ya ndoa na familia mkiwa mnatazamana kwa macho na mwenzi wako? Mkoje, nyieeee? Kwani maparoko, mapasta na mashehe hawawaelezi haya?

Wakinga huwa wanasema vyungu viwili huwa vinamaliza kuni haraka. Mume uko Tanga una bajeti ya nyumba, mke yuko Geita nae ana bajeti ya nyumba, hee, kwa mishahara hii ya chini ya milioni mbili, lini mtafanya maendeleo ya maana?. Ni ujinga mkubwa wa kiwango cha utoroshaji wa makinikia, wanandoa kuishi mbalimbali na ku-risk ndoa eti kwa mishahara ambayo inaishia kwenye matumizi!

By the way, who told you kwamba hata muajiriwe ajira tatu-tatu eti ndio mtakuwa na financial freedom? Wengine wananiuliza, "Je, kwa waliopo masomoni inakuwaje?". Haaa! Haaa! Mie leo naongelea mnaofanya kazi, mengine msinipangie!

6). Mmeambiwa kwamba kisiwepo cha kuwatenganisha isipokuwa kifo. Hamuoni kwamba ajira zimeshakuwa vifo? Mnapata wapi ujasiri wa kuishi na kifo mkingali hai? Nyie mnaujasiri sana. Yaani kifo kinazunguka zunguka, mpo tu mwaka wa kwanza, mwaka wa pili, mwaka wa tatu mnakitazama tu???!!!?? Kweli? Mbona mna hatari namna hiyo!

7). Pointi hii yaweza kuwa ngumu zaidi. Unajua wanaume huwa wanasisimka kwa kuona(kutazama), right? The fact is, asipokua anakiona anachokipenda mara kwa mara (yaani mke wake) ataanza kuona mibadala, hata kama ni "mlokole masalia". Mwanamke anasisimuliwa kwa kusikia (with physical expression). Ndio maana hata mke ukimuangalia usoni na kumwambia, "Nakupenda", anasisimka zaidi kuliko ukimpigia simu na kumwambia, "Nakupenda".

Mpo? Mwanamke anaihesabu "care" kwa kupima ukaribu, (yaani muda unaokua nae physically). Wanawake ni kama watoto, sio kiakili bali kwa hitaji lao la kuwa cared to the maximum. Mwanamke yeyote unaweza kumpata kiurahisi ikiwa kuna factor mbili:- mosi, ikiwa mumewe amezembea kum-care. Pili, ikiwa muwindaji utatumia sayansi ya ku-care. (Mliooa shikeni pointi hapa mnafanya uzembe halafu nyani wanakula mahindi yenu).

So, mwanamke alieolewa anapokuwa mbali na mumewe, huwa anakuwa na gepu fulani, hata kama awe anajikaza. Kuna two things hapa:- gepu hilo likiwepo ndio anaweza kuendelea kujikaza lakini ikizidi sana atakuwa anaumia na itamuathiri. Akiwa anavumilia ashukuriwe Mola. Pili ni kwamba anaweza kutafuta mbadala.

Wanaume ukiona ametafuta mbadala automatically huwa ni kwa ajili ya ngono lakini wanawake huwa wanatamani just care, baasi. The question comes, wanaume wangapi wanaweza kuwa karibu na wake za watu kwa extend ya ku-care that much halafu wawaache pasipo kuwakula? Ndio ile unakuta mke wa mtu ameshaliwa halafu anasema, "Wewe kaka Abdul nilikuwa nakuchukulia kama kaka yangu lakini umenifanya tumefanya hivi, basi iwe siri yetu".

Usidhanie ninakutisha, lakini ukatae ubishe, ni kwamba huko aliko mumeo ama mkeo ambako kuonana ni mpaka likizo hadi likizo, uwezakano wa wewe kula makombo ni mkubwa (hope mnanielewa). Jifariji uwezavyo, muone mkeo ni mlokole uwezavyo (in fact kuwa mlokole hakufuti hisia na mahitaji ya kike), mie ninakwambia fanya juu chini muishi pamoja, maana usalama ni mdogo. Sijasema usalama haupo, hapana, ila nimesema ni mdogo.

By the way (kwa wewe unaebisha) wacha tu-assume kwamba mkeo ama mumeo ambae uko nae mbali yupo salama asilimia zote kwa hiyo naomba hata usinicharukie, sawa enhee? Maana hukawii kujenga hoja unipige mawe kuhofia kujihami na uwezekano wa mali zako kuliwa hulo ziliko. We uchune tu, simuongelei mke wako/mume wako, mie nawasemea wengine. Si umenielewa etiii?

8). Baadhi ya  wanawake mlioolewa katika ndoa hizi za bluetooth mnanichekeshaga sana. Unakuta unabana kabisa pua eti, "Siwezi kuacha ajira, coz wazazi hawatanielewa maana walinisomesha", heee! Unataka kueleweka kwa wazazi ama unataka kueleweka kwa mumeo? Shida yenu (baadhi yenu), vielimu vyenu vimeshawapotezea utii na unyenyekevu kiasi kwamba mnaamua ya kwenu ndani ya ndoa as if bado mko mabachela. Mie ni mmoja ya wanaume wanaosisitiza wanawake wafanye kazi (akiwemo mke wangu), lakini niko aggressive sana linapokuja suala la mke kuthamini maslahi ya ndoa na familia kwa MAJADILIANO. Ukishabana pua yako na kuanza kuwasikiliza wazazi maana yake ni kwamba hamuwezi kufikia muafaka na mumeo kwa suala hili la ndoa ya bluetooth! OLE WAKO NIKUKUTE, maana bakora za mgongo zitakuhusu!

9). Sisemi kwamba ni lazima mmoja wenu aache kazi kumfuata mwingine, la hasha! Ila ninashauri kwamba muanze kufikiria uhamisho if upo, mkikosa kabisa alternative ya uhamisho, fikirieni mmoja anaemfuata mwingine akatafute kazi anakohamia, na hilo likishindikana ndio kufuatie KUJILIPUA, yaani kuacha ajira na kwenda kulea ndoa. Ninachofahamu ni kwamba, kama mkikomaa na Mungu na mkaziweka akili zenu kufikiri, mnaweza kuishi pamoja na kipato chenu kisiathiriwe. Ninacholilia mie ni ile watu mmekaa mbalimbali mwaka wa kwanza, mwaka wa pili, mwaka wa tatu, n.k halafu hakuna bidii za kujitoa sadaka zinazofanyika ili mkaishi pamoja. Hapa ndipo ninapomaindi zaidi!

10). Kuna kitu kwenye ndoa kinaitwa Marriage Culture (utamaduni wa ndoa) ambacho hujengwa ndani ya miaka mitatu hadi mitano baada ya kuoana. Marriage culture hutengenezeka mnapokuwa pamoja. Marriage culture ni kama msingi wa ndoa, usipojengwa siku za kwanza za ndoa you are finished maana kuna uwezekano ndoa kukosa dira. Mmetoka honeymoon, mke karudi Katavi kazini mume umeenda zako Bukoba kazini. Huu ni mwaka wa tatu, mnakutana likizo hadi likizo! Siwafichi, mnampa shetani wakati mgumu kudhani kwamba ataiacha ndoa yenu salama.

Na nyie ambao ndoa ina zaidi ya miaka mitano mkiwa pamoja then mkatawanyika mama Urusi baba, Tanzania, mna hatari kubwa maana kuna kitu kinaitwa marriage bond (muunganisho wa ndoa), kinakuwa kinasagika na ipo siku kitakatika na .mtakutana uso kwa uso na divorce hata kama mmeshaoza na kuozesha wana! Enewei siwaingilii, just nawaeleza kiaina.

HEBU TUOMBE....

Eemola wetu/mungu wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukikemea na kukomesha ndoa zote za bluetooth maana zimekuwa kiota cha michepuko na kuathirika kwa malezi ya watoto. Kabla mwaka huu haujaisha, ndoa nyingi za bluetooth zisiwepo hasa kwa huyu alienisoma na kunielewa, Ameeeen!

Baada ya maombi haya ENENDA KWA AMANI UKAJILIPUE!

MAANA....

Kuna wengine mnapolia kuhusu ndoa, kumbe inabidi tukemee tu kifo, ili mpoteze ajira mkaokoe ndoa! Naomba mtu yeyote asinimaindi kwa hii memo hata kidogo.

Ingawa najua HUU NI UJUMBE MGUMU kwenu, naombeni mnivumilie na muupokee hivo hivo. Safari hii siwadai soda maana najua  nimewachefua nyongo, japo ndio ukweli wenyewe!

NINALIA NA NDOA ZA BLUETOOTH!
(ZILE ZA MUME YUPO SONGEA MKE ANAISHI TANGA)

Sunday, March 1, 2020

FHWF Madini ya Ndoa

MADINI KUTOKA FHWF
______________________________________________

MWANZO WA UCHUMBA NI URAFIKI

Mtunzi: Charles B. Misango, Mtoa Semina kuhusu ndoa na malezi ya familia redioni (Redio Tumaini na Radio Maria) na kwenye TV (TV Tumaini)

Mhariri: Mr. Francisco Kagoma, Founder na CEO wa FHWF, Mwanafalsafa, Mwanasaikolojia na Mshauri wa Changamoto Mbalimbali za maisha zikiwemo za ndoa.

Tarehe: 29/02/2020, Jumamosi.

Chanzo/ Rejea kuu: Kitabu chake 👉🏽👉🏽👉🏽 Charles B. Misango, Nitampataje Mchumba, (Inland Press: Mwanza, 2014), uk.27-28

👉🏽👉🏽👉🏽 Washirikishe wengine nao wapate MADINI motomoto kutoka FHWF, tuma maneno "MADINI YA NDOA NA FAMILIA" kwa Ma-Admin wa FHWF: Chief Admin +255 767 818 542 na Co- Admin +255 716 669 895 ili wakuunganishe na FHWF (JUKWAA). SHEA SASA HIVI⤴️↗️

Kama ilivyo katika ndoa kuwa ni KOSA KULAZIMISHA NDOA, vivyo hivyo ni kosa kulazimisha vijana kuwa wachumba. Sheria ya Ndoa ya mwaka  1971 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002 na za Kanisa Katoliki, zinakataza kuwalazimisha vijana kuoana: wanapaswa wawe WAMEKUBALIANA KWA HIARI YAO WENYEWE. Hivyo mahusiano yaliyojengwa kwa misingi ya vitisho, ulazima, mabavu, na mambo mengine kama hayo, HAYAKUBALIKI katika mustakabali wa uchumba na ndoa.

Mwanzo wa uchumba ni urafiki. Urafiki ndio msingi au nguzo ya mahusiano bora na ndoa bora. Urafiki huleta kumfahamu rafiki yako katika mazuri na mabaya yake, kuwa jinsi ulivyo kwake na hata kujenga ukaribu ambao ni wa kweli, maana huwezi kuwa karibu kwa adui au kuwa ulivyo kwa adui yako.  Urafiki hufanya utamani kuungana zaidi kiakili, na kiroho zaidi na rafiki yako.  Mwataniana na rafiki yako, na kujikuta mkiungana zaidi: utani ni nyenzo kuu ya urafiki, hukufanya ujisikie kuwa umeunganika zaidi na rafiki yako.

Chanzo Cha urafiki ni nini? Urafiki huu baina ya binti na mvulana, mwanamke na mwanaume, unaweza tokana na urafiki baina ya wazazi wao, ama kutokana na makundi yanayowazunguka, kwa mfano, kijana anaweza kukutana na wenzake shuleni, chuoni, kanisani, kazini, na hasa vikundi vya kiroho. Kuwa MAKINI SANA NA URAFIKI UNAOANZIA KWENYE MITANDAO YA KIJAMII (MITANDAONI). Sisemi kuwa huwezi pata rafiki bora, bali uwe mwangalifu kwani wengi wameumizwa kwani wengi ni walaghai yaani si wa kweli wa nafsi zao (wa jinsi walivyo). Hivyo, rafiki huweza "kupatikana kokote na katika mazingira yoyote." (Uk.27)

Urafiki uliojengwa katika mazingira au vyanzo hivyo (sio ule wenye kufanya ngono), "utawasaidia kuwa KARIBU zaidi na zaidi, na hivyo kila mmoja KUSOMA na kujua TABIA halisi ya rafiki yake." (Uk.28)

Kupitia makundi hayo "polepole na kwa sala na maombi kwa Mungu, kijana ataanza kuona mabadiliko MIONGONI mwa rafiki zake. Wapo watakaozidi kuwa karibu naye na kila mmoja akionesha hali ya kupenda kuimarisha urafiki" (Uk.28). Hivyo asiyependa kuimarisha URAFIKI nawe, iwapo wewe umetengeneza mazingira ya urafiki na kupenda kuuimarisha, ACHANA NAYE ILI USIPOTEZE MUDA.

Nahitimisha makala hii kwa maneno yafuatayo endelea kubaki jukwaani, kwani ule uchambuzi kuhusu vivutio vya ndoa na vigezo vya ndoa bado unapikwa, ukiiva utapewa ili uutumie katika mchakato wa kumtambua rafiki /  mpenzi anayefaa kuwa mchumba na baadaye kuwa MKE au MUME.
#NdoaBora, #Uchumba, #Urafiki, #MahusianoBora

© Future Husbands & Wives Forum (FHWF), 2019 - 2020

Saturday, February 22, 2020

Saikolojia

SAIKOLOJIA YA MAISHA  Na.Fr.SIMON R.LIBERIO, MWALIMU WA SAIKOLOJIA

    MAISHA YA MWANADAMU YANAMUHITAJI MWANADAMU MWENZAKE
Saikolojia ya maisha ya mwanadamu ina Mambo mengi.Katika maisha ya mwanadamu Kuna Mambo mengi yanayokutuletea furaha au msongo kwa jina maarufu "stress". Kuna mengi sana duniani yenye kufurahisha.Kuna mengi duniani yanaweza kukukatisha tamaa.Kuna mengi duniani yanaweza kupunguza kasi na munkali wa kuleta Maendeleo tungeita KISAIKOLOJIA " kususia" au kususa. Mwanadamu ameumbwa kichwani mwake kumejaa kama stoo ya maboksi mbalimbali.
Maisha ya mwanadamu Duniani yanaweza kuwa mafupi au marefu.Mwanadamu wa Zama zetu za utandawazi, utandawizi, na utandawazimu.

MAMBO YANAYOWEZA KUKUPATIA UTULIVU WA MOYO KATIKA MAISHA.

1.FANYA UNACHOKIPENDA MAISHANI
Maishani kuna mambo mengi na vivutio hi vingi.Wataalamu husema, " Mirusi mingi humpoteza mbwa". Ukiishi bila malengo siku zote utabaki mtu wa kushika Hiki unaacha kila kitu.
2.Maishani jitahidi kufanya kazi kwa bidii na ujipatie riziki ya kila siku.Uache kuwa mtu wa kulaumulaumu.Acha kulaumu laumu watu.
3.MAISHANI ISHI MAISHA YAKO /ZAKUAMBIWA CHANGANYA NA ZA KWAKO (J.K)
Uishi maisha yako mwenyewe.Badala ya kumlaumu aliyekunyima chakula. Tafuta mbinu halari za kupata chakula chako.Azima hata madum chota maji.Uza maji hautalala njaa.Omba vibarua hata vya kulima mashambani hautalala njaa.  Ukishangaa mjini utalima lami. Dunia ni gunia hakuna atakayekuhurumia kwa uvivu na kupuuza fursa. Hata Mimi sitakuonea Huruma kwa Upumbavu wako wa kufikiri kuwa maisha ni "isidingo" au "ze comedy".

4.UWE MBUNIFU KATIKA UJASIRIAMALI
Ulimwengu huu sio wa Bibi yako. Ni ulimwengu wa watu tena wwshindani.Ujasiriamali mwingi. Biashara kwa wingi. Siasa uchwara nyingi. "Figisufigisu" nyingi. roho mbaya nyingi. roho za mtakafujo.roho za mtaka vyote. roho Mtakavitu.Ndiye anayeutawala ulimwengu wa nope nikupe. roho msakatonge.roho gombania madaraka. roho gombania vyeo. roho mchafu wivu.Dunia ina mtima nyongo. Marekani haiwezi ikacheka cheka na Taifa la uchina na kinyume chake ni sahihi. Urusi haiwezi ikachekacheka na Taifa la Amerika na kinyume chake ni sahihi.Ndio hapo tunaweza tukakibaliana kuwa adui wa bodaboda ni bodaboda. Adui au hasimu wa mfanyakazi ofisini ni mwenzake hasa wafanyakazi wavivu, wakosa ubunifu.Waiba vyeti vya mitihani.Waingia kazini kupitia migongo ya baba na wajomba zao.Watu wanamna hii usiwape taarifa za Maendeleo yako.

5.MAHATMA GHANDI ALISEMA " KAMA HAUNA SURA YA KUTABASAMU KAMWE USIANZISHE DUKA ".
Saikolojia ya muuzaji na mnunuzi ni mguso na ukaribu wa watu wawili.Mwwnye kuhitaji huduma na mwenye hitaji wa "shekeri". Mfanyabiashara anapaswa kuwa mnyenyekevu. Angalieni wachaga hapa Tanzania. Mteja si mfalme tu bali Ni ndugu alisema Baba yangu Mzee Liberio Bahanza hotelini nyumbani Mabamba.
6. TAMBUA VIPAJI VYAKO KISHA KIFANYIE KAZI KIPAJI UNACHOKIONA KINATOA MATUNDA WAZI
Kama mwanzo nilivyoandika kuwa " kichwa cha mwanadamu kimesheheni maboksi mengi yenye fikra pembuzi nyingi". Kichwa cha mwanadamu na moyo wake hujazwa na ndoto kibao. Ndoto nyingi bila kuzitekeleza ni sawa na kuwa na meno yote tena mabovu.
7. SHIKA JAMBO MOJA NA ULISHIKILIE,KIFANYIE KAZI, PAMBANA, LIWEKEA VIPAUMBELE
Maisha yanadai utulivu. Ishi kwa kutimiza ndoto zako. Ifanyie kazi ndoto yako moja ya kwanza kishapo jiulize je ninachokifanya kinanipatia raha na utulivu wa moyo? Ili kuamini kile unachokifanya  kinakupatia amani ni pale unaporidhika hapo ulipo hata kama si kwa kipato kikubwa sana, angalau unaweza ukajipatia mahitaji ya msingi  yaani :Makazi nadhifu, chakula bora, maji safi, mavazi, ada ya kulipa kwa watoto shuleni kwa wenye watoto au unaoweza kuwasaidia.

8. JITAHIDI KUWAVUMILIA WATU WENYE "TABIA NGUMU" (HARD CHARACTER PEOPLE) AU "SPECIAL CHARACTER PEOPLE /COMPLICATED BEHAVIOUR.
Ninapoandika  kuwavumilia watu wasumbufu na wenye tabia ngum. Yapo makundi mengi ya watu wenye tabia zao ngumu. Wapo walalamishi kwa kila Jambo.Wapo wanaopinga kila Jambo.Watu wa namna hii wanashida kichwani. Au uelewa wao wa kifikra ni mdogo sana. Watu wanamna hii hawana mpanuko mkubwa wa kimawaz. BeNa be hawana  "exposure" tuseme ni washamba  wa Mambo mengi. Hujifanya wajuaji wa kila jambo. Wapo wanaopenda wawajali huku wao hawana muda na wenzao. Wanaopenda kubembelezwa huku wao hawana muda na mtu. Wapo wanaopenda kuhurumiwa huku wao hawako tayari kuhurumiwa. Wapo wanaopenda waheshimiwe huku hawawaheshimu wenzao. Wapo wanaolalamikia wenzao huku wao ni mizigo kwa watu.Wapo wanaotaka kusikilizwa huku hawako tayari kuwasikiliza wenzao.

9.TIMIZA NDOTO ZAKO HAKUNA MWINGINE "WEWE"
Furaha yako itapambwa pale utakapokuwa umeishi ndoto zako, ni Kama katika Maandiko Matakatifu Mzee Simeon anatoa shukrani kwa Mungu kwakumvumilia akaishi maisha marefu sana mpaka amwone Masiha wa Bwana.Anasema "Sasa Bwana WAWEZA kumruhusu mtumishi wako aende kwa amani kwakuwa macho yangu yameuona wokovu wa Mungu wetu.
10. Epuka kujitengenezea maadui wako mwenyewe.Uwe na kauli njema. Uwe na simile. Mtu mzima hspigwi viboko. Mtu mzima huambiwa kiutu uzima.Hakaripiwi Kama dogo wa darasa la kwanza
11.Uwe tayari KUYAPOKEA Mambo magumu.Na zaidi ya yote ubaki na hekima ya Dini na Falsafa ya Watao kutambua kuwa unaweza ukavae koti au Sweta lakini hauwezi kuiondoa baridi. WAWEZA kuwasha taa na umeme lakini hauwezi kuiondoa Giza. Mwisho,Pokea hekima.@Fr.SIMON R.LIBERIO

Wednesday, February 12, 2020

AKILI

TUCHUNGULIE UBONGONI MWA MWANADAMU BILA UPASUAJI,
KAZI NZURI NI IPI DUNIANI?
MBAGALA SPIRITUAL CENTER ,DAR
@ LIBERIO S.BAVUGUBUSA C.
Swali huenda likatuchanganya kabisa,au tuseme kuna kazi mbaya? Muuliza swali huenda angeuliza kazi harali na kazi isiyoharali.
Hata hivyo ,Ni vema kuwa mwaminifu kwa muuliza swali.Nakumbuka nikiwa shule ya msingi Mabamba ,Kibondo wilayani wakati huo shule ikiitwa Misheni.
Tulikuwa tukisoma kwa mashindano ili kila mmoja awe wa kwanza darasani.Nilifuata maelekezo ya Baba yangu alivyoniambia " Kamwe Shuleni mwanangu usiwe rafiki wa mambulula" watakubwetesha. Na hapo nikajichagulia marafiki wasio "mbulula"(wenye uwezomdogo darasani).
Kati ya wanafunzi darasa la Pili na la nne waliojiweza walikuwa kama wafuatao, Valeriani Mbweja, Verasius W.Teyumwete, Julius Batromeo( mtoto wa mkulima), Victor na Dickson A. Kibala, Adili Husein Tamim, Simon Njuguma,Tausi Athuman,nk. Hao walikuwa ni vikolezo vya kuhamasishana kufanya vizuri darasani.
Mara kadhaa tulijikumbusha ule wimbo wa akina Baraka,Neema na Misa, " What are you going to be " ? Maana yake Unataka kuwa Nani? Mmoja alijibu angependa kuwa "Mwalimu", mwingine alijibu angependa kuwa "nesi" ,Mwingine alipenda kuwa "mkulima".Kwa akili zanguza kitoto niliamini kuwa kila mmoja alichagua kazi aliyoipenda zaidi kuliko ile ambayo hakuitaja.
Hiyo ni mifano hai mara nyingi ninaitumia katika kuinuana kifikra, kiuchumi na kiutendaji.
Marthin Luther Jr. Mmarekani mweusi na Mwanaharakati wa haki za watu weusina wenye asili ya Afrika na walatino aliwahi kutushauri katika maisha kwa ujumla kuwa katika maisha kuna Mambo yatakayokufanya ufike pale ambapo ungependa kufika.
Moja,Ufanye kazi unayoipenda.Kimsingi Anza na kile unachopenda japo si mbaya ukafanya kile unachopendekezewa hasa "wahenga" wakubwa wako wameonelea kipaji ndani mwako.Ninampenda sana Mheshimiwa huyu na Mwanaharakati huyu Marthin Luther Jr,mawazo yake katika pointi hii amefanana na Mzee Gotama Budha aliyewahi kusema "Tunakuwa hivi kwa KUTOKANA na mawazo yetu" ndio kusema tuko hivyo kutokana na mawazo yetu. Ambapo Mwanafasafa wa Kichina Confucius katika karne ya 5 kabla ya Kristo anasema " Ukitaka kufanya Jambo lifanye kwa moyo, na ulitaka kwenda mahali nenda kwa moyo". Kumbe hata wahenga waliliona kwa kusisitizia kuwa hatunabudi kuchagua chaguo letu wenyewe. Ukifanya kazi ya kuchaguliwa binafsi naifananisha na la kuchaguliwa mchumba ili awe mama yoyo. Kumbe ni vema kufanya kile unachokipenda.Hiyo kazi unayoipenda ndio kazi yako nzuri.Kama sio nzuri ieache ili ukalime lami.Kishapo ujipimie mwenyewe joto la jiwe.Ndipo akili zitakapokusogea na kugundua ukweli wa Falsafa ya kutafuta kazi nako ni kazi.
Kazi nzuri ni ipi, ni ile ambayo itakudai Ufanye kwa bidii tena kwa masaa kibao.Kama Wachina hufanya kazi masaa mengi,mpaka kituo cha haki za kibinadamu Amnesty huthubutu kuingilia Kati kwani wao hufanya kazi kwa Falsafa ya "punda afe mzigo ufike" ningewatania akina " hung yang ping" kwamba hufanyakazi Kama watumwa wakilenga kumkimbiza "kidume" cha Dunia ndio Waamerika ambao juzi Rais Donald Trump alijinasibu kwa ngembe nyingi kuwa katika utawala wake ameirudishia heshima tena Amerika.Ha ha ha kibwagizo cha wiki hiki.
Mwanaharakati Marthin Luther anasema, kazi uipendayo ifanye kwa muda wa kutosha na zaidi ya yote kwa ueledi mkuu.
Kazi nzuri ni ile utakayotaka kuifanya ili mwisho wa siku "utusue" utoboe ,ama uyaone matunda yake Tena waziwazi kwa kuacha Falsafa au "legacy" kwa kimombo. Usifanye kazi ilimradi utokwe na jasho, jasho haliuzwi hata ukipiga "push up" au ukala pilipili za wahindi jasho litakutoka. Kazi nzuri itakudai kuhenyeka kweli.Itakutaka uifanye kwa moyo.
Kazi nzuri ni ile utakayokuwa umejiwekea malengo ya kukukombowa.Katika Kitabu kilichoandikwa na Robert T. Kiyosaki, "Rich Dad and Poor Dad'' kinaonesha tofauti ya mtazamo wa Mtoto wa mkulima(poor Dad) tuseme yeye anakwenda Shuleni ili aajiliwe huku mtoto wa Rich Dad (Tajiri) anakwenda shule ili ailinde pesa kiusomi na sio apate kazi ya kuajiliwa na mtu.Anakwenda shule ili apate akili zaidi ya kuilinda pesa asifilisike mpaka kizazi cha nne ndio hao wafanyabiashara Waasia. Wabongo sehemu kubwa tunajua kutafuna pesa tulizoachiwa KWENYE mirathi na uzuri wa Bahati pesa za mirathi tunazitafuna bila kuzihurumia,kwa kigezo kilekile cha kuzipata kwa nasibu na bila kuzihangaikia.Ndio kisa pesa za mirathi hazilipi na hazikufanyi uumize kichwa.
Lao Tse Tzu MDAU mkubwa wa Falsafa za akina Confucius aliwahi kusema katika kazi nyepesi jiandae kukutana na magumu ili uifanye kwa ueledi mkubwa na umakini. Huyu Mwanafasafa Mchina anataka kutukumbusha tufanye Mambo kwa umakini yaani "serious". Maandiko matakatifu yametoa "ole" kwa wale wajiaminio kipumbavu. Ole wao wajiaminio kipumbavu, Upumbavu ni uparambogo,kutaka kujifanya unajua huku hujui na hutaku kujua wala kufundishwa.
Maisha na kazi ningesema ni sawa na kuwa na barabara nzuri zimetengenezwa kwa ajili ya magari huku hakuna magaru na watu wenyewe waamue kupita vichakani. Wajerumani walikuwana Falsafa ya kupiga kazi na sio kubwabwaja midomo.Ndio kusema Matakatifu Benedikto alisisitiza juu ya Sala na kazi na sio kulialia bila kupigwa.Tuchape kazi bwana.
Turudi sasa kwenye simulizi la vijana Musa, Baraka na Neema.
Yule aliyesema, ATAKUWA MWALIMU.
Huyu atapaswa kurithisha Elimu toka kizazi hata kizazi.
Huyu atahitaji awe mwema na atapasika kuwa Mfano Bora kwa watoto na jamii.
Atapaswa akwepe madeni yasiyo na tija.
Atapaswa kujiwekea uzeeni hasa kwa kutunza pensheni zake.
Atapaswa kuwakwepa walevi wa mjini na vijijini.Kwani pensheni ikiisha wao ndio watakaokuwa wakwanza kukupiga majungu na kukuona mpuuzi wa mwaka.
Atapaswa ajenge nyumba ndani ya miaka kumi ya kwanza ya kuajiliwa.
Atapaswa awekeze pesa benki ikiwa ni Maandalizi ya Kuandaa ada za watotoAtapaswa anunue mashamba walau Kama ni ekari chache ziwe kumi na tano au zaidi.Panda miti itakyokoa uzeeni. Ningekuwa Mwalimu ningefanyaje? Historia inaonesha kuwa walimu husahaulika msinite Mwanaharakati " sitaki" wengi hata walionifundisha nawaona walivyo na maisha duni.Mitazamo duni.Makazi duni.Chakula duni.Mshahara kuisha katikati ya mwezi.
Nifanyeje.Kukuruka.Fuga kuku vijana wa kazi watabaki wanawatazama kwani ukichelewa kazini ' majipu" yatashughulikiwa. Pensheni ni ya kula kidogokidogo na sio gawio la ukoo.
Wote wawili waliotaka kuwa nesi na mkulima kiufupi nesi akidhi maadili ya utabibu, mkulima naye apambane na Kilimo cha tija, kulima kwa wakati, kupanda MBEGU Bora na tena kupanda mbegu katika mvua za mwanzo kama Hayati Mwl.Julius K.Nyerere alivyowashauri watanzania.

TUSOME VITABU





FAIDA 100 ZA KUSOMA VITABU
Na.Fr.Simon R.LIBERIO
"Vitabu" ni wingi wa neno Kitabu litokanalo na neno la asili la lugha ya kiarabu " Al kitaab". Falsafa na tunu nyingi za kimaisha huhifadhiwa vitabuni. Elimu huhifadhiwa kitabuni.Hekima kedekede nazo twazikuta vitabuni.Mapindunzi ya kiuchumi na njia mbadala za ujasiriamali tunazikuta vitabuni.Sala mbalimbali majuzu, haditji za Mtume Muhamad (S.A.W) twazikuta Kitabuni. Mafundisho ya namna njema ya kuishi Duniani kadiri ya Gotama Budha, CONFUCIUS na Tao wachina Wanafalsafa nao wote tunawakuta vitabuni. Falsafa za Anthen Ugiriki takribani katika karne ya tano Kabla ta Kristo tunawasikia walimu Kama Socrates waliokuwa walimu wa Aristotle na Plato na kishapo Aristotle akawa Mwalimu wa Albert Mkuu. Msomi wa vitabu vya watangulizi waandishi wake huongeza maarifa kwake. Mafundisho ,Kazi za Yesu Kristo Mungu na Mwanadamu kwa pamoja zarekodiwa katika vitabu tena tuite Al wainjili ( Injili Takatifu)
Tujifunze kupitia mifano ya mabingwa katika kufanya vizuri.
Bila shaka ukimtazama Rais Barack Hussein Obama amekuwa hivyo baada ya ushawishi wa Mwanaharakati Marthin LutherJR Dr. Rais huyo Mstaafu wa Taifa kubwa lijiitalo "kidume" mbele ya mataifa yetu madogo ya wakata nyasi.Alimwiga Kaka yake Mbantu Marthin Jr. akiyetembelea viunga vya Alabama, Kansas akipaza sauti ya mnyonge mweusi aliyekuwa haruhusiwi kupiga kura katika Taifa alilozaliwa kwa bahati mbaya kwani alikuwepo huko ikiwa ni matokeo ya biashara chafu ya watumwa.
1.VITABU HUTUPATIA HAMASA YA KUJIFUNZA MAPYA
Hauwezi kusahau Michango ya wanafalsafa kama Aneximenes, Anaximander Wala Heraclitus katika Maendeleo ya medani za Falsafa za Anthene huko Ugiriki.Ndio maana tunasema " Let us learn from the Geneous" tujifunze kwa " Manguli" waliofanya vizuri katika tasnia mbalimbali ili tujichotee ueledi maridhawa. Padre TITUS AMIGU amekuwa hivyo Nguli na bingwa mwandishi Afrika na dunia KUTOKANA na Mwl.wake Padre Mwandishi wavitabu lukuki CHRISTIAN MUHAGAMA. Kumbe penye hatua ya maendele Kuna mtu nyuma.Nami mwandishi mchanga Tanzania, Afrika na dunia nimekuwa hivi mwandishi kwa kuvutiwa sana na kazi za Vitabu vya Padre Titus Amigu. Shikamoo Mzee Titus Amigu.Salute.
Kama Saikolojia ya makuzi ya mtoto(mwanadamu) huzaliwa Ni Tabularasa, hajui chochote, kumbe hata angekua na kujifunza mengi atabaki na deni la kutaka kujua mengi tena mengi sana. Kumbe sasa, kwa kusoma Vitabu mwanadamu atajiongezea ueledi mpana, kwa Mfano mie mwana wa mkulima Mwandishi mzaliwa wa mabonde kuinama ya kijijini Mabamba Kibondo mkoani Kigoma, ili nipasue anga vijana huita " next level" za kuwa mwandishi wa Kimataifa sina budi kukomaa na kusoma Vitabu vingi vya waandishi wa Kimataifa Kama akina CHINUA ACHEBE, WOLE SOYINKA, NGUGI WA THIONGO, JULIUS KAMBARAGE NYERERE, ASKOFU MKUU FULTON JOHN SHEEN ,SHAKESPEAR, BRIAN TRANCY, ROBIN SHARMA, BENJAMIN WILLIAM MKAPA, ROBERT KIYOSAKI, OBAMA BARACK, FR.DR. GEORGE KAITHOLILI, BILL CLINTON, ERNEST BONIFACE MAKULILO, BILL GATES, SEMZABA ,PATRUCE LUMUMBA wa Kenya niwataje tu kwa ufupi.
Kumbe sasa katika mafanikio yoyote lazima uwatazame watangulizi wako wamefanyaje.Waliwwzaje "kutoboa" waliwezaje kufanikiwa mpaka wakafikia walipofikia.Kwanini wewe nawe usifikie hatua hiyo? Kama wao waliweza KWANINI nawe usiweze? Kama wao walithubutu kwanini nawe usithubutu. Kwa maneno mengine tungesema Kama wao walijaribu kwanini nawe usijaribu?
Niseme, tu kwamba tunahitaji maono mapya, mitazamo mipya, ujuzi mpya,njia mpya za kuweza kutambua Mambo na kutatua changamoto kupitia mifano ya wenzetu waliokwishapiga hatua katika maisha.
.Elimu mpya hutupatia hamasa.
.Elimu mpya hutupatia mawazo mapya
.Elimu mpya hutupatia moyo pale tulipokata tamaa.
.Elimu mpya hutupatia fursa ya kukikosoa
.Elimu mpya hukuongezea morali ya utendaji kazi.
.Elimu mpya hukubadilisha, badala yakufanya kazi kwa mazoea.Unafanya kazi kea utalaam.
.Elimu mpya hutukosoa.
.Elimu mpya hukuimarisha katika hoja.
.Elimu mpya hukutofautisha na wenzako katika kuyakabili mazingira yako.
.Elimu mpya ni jawabu ya zile ulizoziita changamoto kuwa fursa.
2.KWA KUSOMA VITABU TUNAJIFUNZA WENGINE WALIWEZAJE AU WALIFANIKIWA KWA NJIA ZIPI NA MIBADALA MINGI WALIYOITUMIA KATIKA KUKUPAMBANA NA CHANGAMOTO KATIKA HARAKATI ZA MAFANIKIO YAO.
Ni matumaini yangu ndugu msomaji wangu,utakubaliana nami kuwa vitabu kwa sehemu kubwa vimekuwa na malengo ya kujifunza kwa wale waliofanya vizuri.Mfano mzuri ni katika Kitabu cha "RICH DAD AND POOR DADY" kilichoandikwa na Dr.Robert T.Kiyosaki, miaka ya 1997, kikitafsiriwa "BABA TAJIRI NA BABA MASKINI".Kinang'amua mitazamo miwili kinzani ya akina Baba wawili. Baba Maskini anawahimiza mwanae kuwa, "mwanangu umezaliwa katika familia Maskini,utapaswa kusoma kwa bidii sana ufaulu ili uajiliwe na upate pesa.Huo ndio msimamo wa Baba Maskini.
"Baba Tajiri" anakuja na msimamo tofauti na mitazamo mpya na wa kimapinduzi ya kifikra. Anamwambia mwanae kuwa mwanangu umezaliwa kwwnye familia tajiri,Mimi Baba yako naelekea kuzeeka, utapaswa kwenda Shuleni ukasome kwa bidii tena usome namna ya kuendesha vizuri biashara ili ukifuzu masomo urudi nyumbani uendeshe kampuni za kibiashara.Natambua ukibobobea sana katika masomo ya biashara utaendeleza vizuri Kampuni hizo bila kufilisika. Haya ndiyo tunayoyaona kwa wafanyabiashara hapa Tanzania wenye asili ya Asia akina Bakhresa, Mo,Yusufu Manji huandaa vijana wao kimasomo na hivi hata biashara zao hufanywa kisomi.Shughuli zao huendeshwa kisomi kwani vijana wao huandaliwa Kama Kijana wa " RICH DAD " alivyoandaliwa na Baba take. Ndio MAANA utajiri wao si rahisi kutoweka hapa chini ya jua. Kufilisika si rahisi. Kwani TAYARI Kuna watu waliokwishaandaliwa kiueledi katika tasnia ya biashara, masomo na matangazo.Hapa tujikubali tu, kuwa kwa kukosa mipango.
3.KWA KUSOMA VITABU TUNAJIFUNZA UVUMILIVU WA KUISHI NA WATU WA AJABU NA PIA TUNAJIFUNZA NAMNA WATU WANAVYOWEZA KUTUVUMILIA USUMBUFU WETU.
Kwa kusoma Vitabu utakutana na majina Kama akina Bokasa, Nduli Idd Amin Dadaa, akina Osama Bin Laden na wengi wengi. Majina hayo ni maarufu sana.Nilipokuwa shule ya msingi Mabamba, tukiwa tunakimbia mchakamchaka kwa mazoezi asubuhi ," tuliimba " Idd Amin akifa Mimi siwezi kulia , nitamtupa Kagera awe CHAKULA cha mamba" nilitamani kufahamu kwanini tusimulilie na zaidi ya yote maiti yake iliwe na mamba" .Nyimbo nyingi ziliimbwa "Amini aaah aaah ameolewa ,wapiii aaah huko Ulaya ,wivu aaah aaaah wamukereketa". Hiyo ilikuwa ni Falsafa ya kuonesha ushenzi wa Nduli Idd Amin.
NI KWANINI WATU HAO PAMOJA KWAMBA WALIKUWA WASHENZI WANAKUMBUKWA?
Ubabe duniani haulipi. Ubabe duniani hauna maana. Kwanini turinge.Maringo yanatoka wapi? Kwanini uvimbe pua? Kwanini uvimbe kwapa kwa mwenzio? Kwanini umkanyage mwenzio?
Maisha yetu hapa duniani , hatukuja kutunishiana misuli. Hapa duniani hatukuja kutafuta " u miss umwamba" wala hatupo kuusaka ubabe na umame". "Ubabe" ni hali, tabia, maneno au matendo ambayo yanatoka kama povu la hasira.Ubabe ni ukorofi wa akina Baba duniani.

Ambapo ukorofi wa akina mama huitwa "Umame".Duniani wapo pia akina mama wakorofi. Duniani wapo wanadamu wa ajabu.Akina Munsolini wa Italia. Akina Mao Ze Dong wa China aliyetaka aogopwe sana na kukuita "mungu". Akina Hittler wa Ujerumani nao hawatasahaulika katika masikio na historia ya waisraeli(Wayahudi) 










DEFEND YOUR FAITH AS A CATHOLIC: CHUKI NI NINI?

DEFEND YOUR FAITH AS A CATHOLIC: CHUKI NI NINI?: CHUKI NI NINI? Kadiri ya Dr.Ann Landers: “Chuki ni kama Asidi, ambayo huaribu kile kifaa ambacho imehifadhiwa na huaribu chombo ambamo ime...

Thursday, February 6, 2020

MADINI YA NDOA

MADINI KUTOKA FHWF
______________________________________________

TOFAUTI KATI YA VIVUTIO VYA NDOA NA VIGEZO VYA NDOA

Tarehe: 06/02/2020, Alhamisi.

Mtunzi: Mr. Francisco Kagoma, Founder na CEO wa FHWF, Mwanafalsafa, Mwanasaikolojia, na Mshauri wa Changamoto Mbalimbali za maisha zikiwemo na ndoa.

👉🏽👉🏽👉🏽 Washirikishe wengine nao wapate MADINI motomoto kutoka FHWF, tuma maneno "MADINI YA NDOA NA FAMILIA" kwa Ma-Admin wa FHWF: Chief Admin +255767 818 542 na Co-Admin +255 716 669 895 ili wakuunganishe na FHWF (JUKWAA). SHEA SASA HIVI⤴️↗️

Habarini za leo wanandoa waliomo katika Ndoa tayari na wanandoa watarajiwa.

Wapo tunaochanganya kati ya vivutio vya ndoa na vigezo vya ndoa kama vile vingekuwa kitu kimoja. Ni ukweli kwamba vyote vina mchango wake katika ndoa.

Utasikia maneno kama una vigezo vya kuwa MKE au mume wangu? Na mtu haulizi eti una vivutio vya kuwa MUME au mke wangu? Tayari hapo kuna maana fulani inaingia ambayo inavitofautisha "vigezo" na "vivutio."

Licha ya kwamba "vigezo" huonekana kuwa na uzito zaidi kuliko "vivutio", dunia hii ingekuwa inayokera sana kwa maana tumeumbwa kwa namna inayovutia halafu eti nje yetu kusiwepo vivutio.🤷🏼‍♂️🤷🏼‍♀️

Kifalsafa, hapa tunaongea kuhusu substance (kiini/ kigezo) (what makes something/ somebeing to be what it is, yaani _kile kinachokifanya kiwe kilivyo_) na accident (kivutio) (what adds value or falls marginally to the thing, yaani kile kinachoboresha au kinachoongeza uthamani wa kitu). Inawezekana kiini na kigezo visiwe na maana sawa mathalani maana ya ndoa - kiini cha ndoa, au vigezo vya ndoa- maana hata katika matumizi hutumika vigezo vya ndoa au vigezo vya kuoana na sio kiini cha ndoa au kiini cha kuoana. Vigezo vya ndoa hukupeleka moja kwa moja kwenye dhana ya ndoa yaani kwenye kiini cha ndoa.

Tumewahi fundisha kupitia makala mbalimbali kuhusu ndoa ni nini mfano makala ya tar. 10/02/2019 NDOA NI NINI?. Tulisema hivi ndoa ni agano kati ya mwanaume (a man) na mwanamke (a woman) kuwa wanafungamana na kuungana ili kuwa mwili MMOJA, moyo (hisia) MMOJA, akili MOJA na roho MOJA, kwa ujumla kuwa kitu kimoja katika nyanja zote na nyakati zote za maisha yao au uhai wao. Tulikwisha toa ufafanuzi wa maana hiyo katika nyakati tofauti tofauti, usitoke jukwaani tovuti (fuhuwi.com) ikikamilika utaweza rejea tena.

Leo tuone tofauti iliyopo kati ya vivutio vya ndoa na vigezo vya ndoa

1. Tofauti katika dhana au maana

Dhana ya kivutio (attractive/ exciting thing) husema kivutio ni kile kinachotakiwa kuwepo au kilichopo tayari ili kukuhamasisha kufanya kitu fulani/ kufikia jambo fulani. Na dhana ya kigezo (criterion/ requirement) husema kigezo ni kile kinachotakiwa kuwepo ili jambo fulani lifanyike au lipatikane kwa usahihi.

Hivyo vivutio vya ndoa ni yale yanayayotakiwa kuwepo  au yaliyopo tayari ili kukuhamasisha kuitafuta ndoa na kuipata yaani kumtafuta na kumpata mwenzi wa ndoa, kumtafuta na kumpata mvulana au msichana fulani na kufunga naye ndoa.  na vigezo vya ndoa ni yale yanayotakiwa kuwepo ili kuwezesha ndoa ipatikane, ifungwe na idumu.🌝

2. Tofauti katika ulazima na umuhimu.

Vivutio vya ndoa si lazima viwepo bali ni muhimu kwani ndio vichocheo kwa vijana kuingia ndani ya ndoa, huiongezea ndoa thamani na kuipa ndoa hii radha tofauti na nyingine. Ndoa ni moja ila inavyojidhihirisha kwa wanandoa hawa ni tofauti na kwa wanandoa wengine. Vivutio vya ndoa huifanya ndoa iwe na sura au taswira nyingi za kuitazama au kujidhihirisha kwa watu.

Vigezo vya ndoa ni ni vya lazima kwani vikifuatwa ipasavyo ndivyo vinavyowasaidia wanandoa kukifikia kiini cha ndoa kilichoelezwa kwenye maana halisi ya ndoa (unini wa ndoa) - muunganiko kimwili, kihisia (kimoyo), kiakili na kiroho.

3. Tofauti katika kutumikiana

Vivutio vya ndoa na vigezo vya ndoa vyote hutumikia ndoa, vina mchango wake katika kuhakikisha ndoa zinaanzishwa, zinakuzwa, zinakomaa, na kuzaa ndoa nyingine (kuzaa wanandoa wengine).

Lakini vivutio vya ndoa hutumika zaidi katika kuanzisha wazo la ndoa kwa vijana, na kulichochea. Huwezesha kuanza kutafakari vigezo vya ndoa, vya kuoana ni vipi. Hivyo huwezesha vigezo vya ndoa kutafutwa na hata kumpeleka kijana katika kiini cha ndoa.

👉🏽 Vivutio vya ndoa ➡️ Vigezo vya ndoa ➡️ Kiini cha ndoa

Vivutio vya ndoa hutumikia kiini cha ndoa kupitia vigezo vya ndoa LAKINI vigezo vya ndoa hutumikia kiini cha ndoa moja kwa moja.

Nahitimisha makala hii kwa kusema kuwa vigezo vya ndoa hubaki ndani ya kiini cha ndoa, kiini cha ndoa na  vigezo vya ndoa ni kama pete na kidole, ila *vivutio vya ndoa* hubaki nje ya ndoa, huipamba ndoa, huipa ndoa  muonekano unaovutia.

Tuvipambanue vizuri vigezo vya ndoa na vivutio vya ndoa ni vipi ili tupate kutengeneza ndoa bora.

Makala zijazo zitavipambanua vigezo hivyo na vivutio hivyo ni vipi. Baki JUKWAANI _yajayo ndani ya FHWF na FUHUWI (fuhuwi.com) yanafurahisha na kuelemisha._

© Future Husbands &Wives Forum (FHWF), 2019 - 2020

Wednesday, February 5, 2020

KANISA NA KUJINYONGA

Labda nikusaidie kupanua swali lako kwanza. Ungeuliza kwanini watu wanaojiua kwa kuondoa uhai wao, kanisa linakataa maziko yao kwa Misa Takatifu?

Kwanza tujue kujiua ni kufanya nini? Ni kitendo kilicho kinyeme na kutunza uhai wa Mwanadamu ambao sio mali yake na hivyo hana mamlaka nao. Ni kujiua moja kwa moja kwa makusudi kabisa kwa utashi wako mwenyewe.
Kanisa siku zote hata kesho, litabaki kinyume na mtu anayeondoa uhai wake mwenyewe kwasababu mbalimbali zikiwemo hizi hap;
1. Mwanadamu hana haki miliki ya uhai wala mwili wake mwenyewe bali amepewa kutunza mwili na uhai (stewardship).

2. Kujiua (Suicide) ni kosa la jinai dhidi ya wajibu wa Mwanadamu kwa jumuia yake na wale wanaomtegemea. Uhai wa Mwanadamu daima sio kwaajili yake mwenyewe bali kwaajili ya jamii nzima.

3. Kujiua ni kukiuka wajibu binafsi wa kujitahidi kufikia ukamilifu wa maisha yake ya kimwili na kiroho.  Mtu anayeondoa uhai wake anajiondolea pia uwezekano wa maendeleo yoyote ya baadae.

Kwa maana hiyo basi, kwakuwa mtu kufikia uamuzi wa kujiua anakuwa amevurugwa kiakili (mental disturbed). Kanisa kwa kuangalia mazingira yote ya kujiua na bila kuathiri imani ya watu kwa kuleta makwazo, linapaswa kuangalia namna nzuri ya kushughulikia maziko ya Mkristo aliyejiua.

Angalisho, namna ya kuangalia mazingira na kushughulikia swala hilo kichungaji, haitakuwa na ufanano kwa matukio yote wala kwa majimbo yote au tuseme ulimwengu  mzima.  Tofauti zitajitokeza na ukiziona ni vyema kuchukua muda wa kujielimisha juu ya maamuzi yaliyochukuliwa na kanisa kabla ya kulaumu au kujipa wajibu wa kuhukumu.
Mungu atuhurumie.

Frt. Nzaro

DEFEND YOUR FAITH AS A CATHOLIC: HURUMA NA MSAMAHA NI KUBWA ZAIDI KULIKO DHAMBI ZET...

DEFEND YOUR FAITH AS A CATHOLIC: HURUMA NA MSAMAHA NI KUBWA ZAIDI KULIKO DHAMBI ZET...: HURUMA NA MSAMAHA NI KUBWA KULIKO DHAMBI ZETU. TUMWIGE MUNGU KATIKA KUWASAMEHE WENGINE Maandiko Matakatifu yanaongea sana juu ya kutostahi...

DHAMBI MATOKEO YA AKILI NA UTASHI HURU WA MWANADAMU



SHUKRANI

Kwanza kabisa napenda kutoa shukurani zangu za dhati kwa Mungu wetu aliye katika Utatu Mtakatifu, aliyeruhusu yafanyike haya. Kwa maana hiyo ni kwa Neema na Upendo wake mkuu kuniwezesha, kunitia na kunipa nguvu na maarifa hata nikafanikiwa kuanza na kukamilisha uandishi wa hii kazi.
Aidha namshukuru sana Baba Askofu wangu wa Jimbo Katoliki la Kigoma Mh. Joseph R. Mlola, ALCP/OSS, kwa ushauri wake mzuri alioniambia wakati naandaa kitabu hiki.Nampongeza kwa kazi nzuri ya kuendeleza kile walichokifanya Mitume wa Yesu yaani kulichunga kundi la kondoo wa Bwana katika jimbo letu la Kigoma. Mungu Mwenyezi amzidishie na kumpa nguvu na afya njema pamoja na ulinzi wake katika Utume huo alioitiwa.
Kwa namna ya pekee kabisa napenda kumshukuru Msgr. D. H. Mbiku wa Jimbo kuu Katoliki la Dar- es salaam kwa kukubali na kutumia muda wake kuipitia kazi hii na kuiona kuwa inafaa kwa ajili ya wokovu wa Roho za watu walioko ndani na nje ya Kanisa, Baba nasema Ubarikiwe sana.
Nitakuwa mchoyo wa fadhila kama sitawashukuru Baba zangu Mapadre ambao wamekuwa pamoja nami bega kwa bega katika kunielekeza mambo mengi ya kufanya ili kazi kuwa nadhifu. Kwa namna ya pekee Pd. Vedastus Nyamurundwa (Jimbo Katoliki Kigoma), Pd. Titus Amigu (Jimbo Katoliki Iringa), na Pd. Arnold Kinyashi (Jimbo Katoliki Same).
Nawashukuru wazazi wangu ambao pia wamekuwa na mchango mkubwa kwangu katika malezi mpaka mimi kufika hapa, Mzee Joseph Lutakangwa na Mama Anatoria Yilagera; Mwenyezi Mungu mwingi wa Huruma awajalie maisha marefu na ya fanaka siku zote. Pia nawashukuru sana wadogo zangu wote kwa kunitia moyo katika safari hii ya wito, Mungu mwenyezi awasaidie katika masomo yenu na kufikia lengo la kila mmoja alilonalo katika masomo.
Shukrani za pekee kwa Frt. Innocent Banyongere na Frt. Wilhard Kangero kwa michango yao ya Mawazo katika kuboresha kitabu; nasema asanteni sana. Mwisho kabisa nawashukuru ndugu, jamaa, marafiki na waamini wale wote ambao wamekuwa wakinitia moyo katika kuandaa kazi hii, zaidi kwa majitoleo yao kiuchumi mpaka kazi kukamilika pia katika hatua hii niliyopo kuijongea Altare ya Bwana. Nasema asanteni sana, maana wanasema moyo usiyo na shukrani hukausha mema yote.
Tamati: KWAHIYO NAWASIHI, MIMI NILIYE MFUNGWA KATIKA BWANA, MWENENDE KAMA INAVYOUSTAHILI WITO WENU MLIOITIWA; KWA UNYENYEKEVU WOTE NA UPOLE, KWA UVUMILIVU, MKICHUKULIANA KATIKA UPENDO (Efe 4:1-2)

 


 

 

 

 



UTANGULIZI

Wapendwa sana ndugu katika Kristo napenda kuwakaribisha kwa moyo mkunjufu kabisa katika kukipokea kitabu hiki ambacho ni tunda la kurekebisha mienendo yetu. Ni kitabu kinachotuonyesha kwa kina zaidi namna nzuri ya kumfasa Kristo.

Katika sura ya kwanza inatoa ufafanuzi wa kina juu ya maana ya Dhambi. Pia katika sura ya pili inatupa ufafanuzi juu ya ahadi ya Mungu kwa viumbe vyake alivyoviumba, japo kwa baadae vikajakumgeuka na kuvunja yale maagano naye ya tangu mwanzo.

Katika sura ya tatu kinatueleza maisha ya sasa ya mwanadamu namna aishivyo. Sura ya nne inaeleza juu ya mabadiliko ya sayansi na teknolojia yanavyochangia kwa kiasi kikubwa katika kuendelea kumpotosha mwanadamu wa sasa katika hii dunia.

Katika sura ya tano inatupa mang’amuzi mazito juu ya kushuka kwa maadili. Sura ya sita pia inatupa somo juu ya uovu mkubwa unaoendelea katika dunia hii ya karne ya 21, japo ni marudio ya yale yaliyowahi kutendeka kipindi kilichopita katika agano la kale. Na katika sura ya saba ambayo ndiyo ya mwisho, inatueleza namna mbalimbali ya kumrudia Mungu aliyemwumba wa vyote kwa kuiga na kufata mfano wa Mungu.

Ni matumaini yangu kuwa utanufaika na mafundisho yaliyomo katika kuendelea kuimarisha nafsi yako. Kwa namna ya pekee naamini mara baada ya kupata ujumbe uliokusudiwa utakuwa chombo imara cha kupiga vita dhambi, ili hata wale ambao bado wanaendelea kuishi katika giza kuu wapate kuanza kuurudia mwanga. Na mwisho kabisa naomba baada ya kusoma kitabu hiki ujaribu kutafari ule uovu wa tangu Sodama na Gomora pia Gharika ya Nuhu; je! si ndiyo maisha yanayoendelea katika wakati huu wetu? Kwani unaona tofauti yoyote?
Hapo tunaona;
 “Tukisema kwamba hatuna dhambi tunajidanganya wenyewe, wala kweli haimo ndani mwetu. Tukiziungama dhambi zetu, yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wetu.”[1]


SURA YA KWANZA

1.0 UFAFANUZI JUU YA DHAMBI

Hakuna utata wowote juu ya uwepo wa uovu ulimwenguni. Tunaona na kusikia maovu mengi yanatendeka duniani kwa njia nyingi. Mfano: mafarakano kati ya mataifa, magomvi katika familia, magomvi mitaani, rushwa, ukabila, ujinsia, ubaguzi wa rangi, mauaji, ndoa za jinsia moja, ushoga, ukahaba na mengine mengi. Namna zote hizi za ukatili, mivurugano na utengano ambazo tunazishuhudia katika maisha ya kila siku, zinapoangaliwa kwa jicho la kiteoliojia, yote yanachipuka kutoka katika dhambi. Hivyo dhambi ipo ulimwenguni, na kunauwezekano wa kupinga upendo wa Mungu kwa namna nyingi sana.
“Biblia Takatifu inasema juu ya dhambi mara nyingi na kila mara na karibu katika kila ukurasa” alisema X. Lean-Dufour. Dhambi pia inajadiliwa kila wakati katika Katekisimu ya Kanisa Katoliki, kwa sababu mengi yaliyo kiini cha imani hayawezi kueleweka bila kuielewa dhambi. Zaidi sana, ili kufuata nyayo za Kristo, tunahitaji kuelewa vizuri madhara ya dhambi. Dhambi ina mapato mabaya sana katika maisha ya binadamu, lakini mara nyingi ulimwengu unayafanya matendo ya dhambi yaonekane yanavutia. Ndiyo maana watu wengi sana katika ulimwengu huu wa sasa, wamejikita na kuwekeza katika vitu vihusianishavyo na dhambi.

1.1 Nini maana ya Dhambi?

Dhambi ni kukataa kwa makusudi na kwa kujua zawadi ya upendo wa Mungu ya urafiki naye, ambako kunasababisha kudhoofisha au kuvunjika kabisa kwa mahusiano kati ya mtu na Mungu au kati ya mtu na mtu. Hivyo basi, kwa dhambi binafsi mtu anashindwa kuitikia kwa usahihi zawadi ya mapendo ya Mungu na urafiki usiokoma wala kubadilika maisha yote. Katika Biblia; Maandiko Matakatifu yanailezea dhambi kama nguvu ambayo ipo katika maisha yetu. Nguvu hiyo ipo duniani ambayo ina uadui na Mungu na mpango wake, maana tunaambiwa baada ya shetani kulaaniwa alishushwa kuzimu ili akatujaribu kwa namna yote ile ipingayo Mungu. Kwa hiyo dhambi inajaribu kuharibu mahusiano yetu na Mungu. Dhambi ni kinyume kabisa na upendo na upatanisho ambao Yesu Kristo anaufunua pale msalabani. Hivyo, dhambi ni zaidi ya kuvunja sheria kwa sababu ni uasi dhidi ya utu ule ambao tumeitiwa. Kwa namna nyingine, dhambi, ni kuvunja miiko fulani iliyowekwa na Mungu kwa ajili ya faida yetu wenyewe.
v   Dhambi katika Agano la Kale. Katika Agano la Kale tunaona msingi wa tabia ya dhambi, kwamba ni kuanguka kwa wazazi wetu wa kwanza (Rej. Mwa. 3:1-24). Pia dhambi inaonekana kuwa:
§    Ni kuvunja sheria ya Mungu (Mwa 3: 3 – 6 )
§    Ni dhara dhidi ya Mungu (2Sam 12:10, 15)
§    Ni (upumbavu) ujinga (Kumb 36:6, Isa. 29: 11)
§    Ni kukosa uaminifu (Isa 24:5)
§    Ni kuabudu miungu wengine (Eze 20:7-8)
Katika Agano la Kale, hakuna tamko bayana juu ya asili ya dhambi na jinsi inavyorithishwa kutoka kwa wazazi wetu wa kwanza mpaka kwa jamii yote ya binadamu. Hata hivyo habari ya kuanguka kwa binadamu katika kitabu cha Mwanzo inaeleza hali ya binadamu ya kuwa na mazoea ya kuelekea dhambi. Pale wazazi wetu wa kwanza walipotenda dhambi, ilikuwa ni kwa sababu walitaka kuwa sawa na Mungu na bila Mungu (Mwa 3:5).
v   Dhambi katika Agano Jipya. Katika Agano Jipya inaonekana kama ni mgomo au kukataa upendo wa Baba (Rej. Lk 15). Mgomo huo una mizizi yake katika moyo. Mawazo ya dhambi katika Agano la Kale yamechukuliwa na kuingizwa katika Agano jipya na kuelezwa kwa kina.
§ Agano Jipya linaeleza kuwa dhambi si kitu cha nadharia tu, bali ipo kweli, ni ugonjwa ambao kweli unahitaji tiba. Ni ugonjwa ambao unahitaji mabadiliko kamili ya maisha ya mtu. Hili linaonyeshwa bayana na mwito wa Yesu mwenyewe(Rejea Mk 1:15, 7:21-23; Mt 5:21-48)
§ Dhambi ni kitu ambacho kipo ndani ya mtu, ambacho kwacho binadamu wote wanakuwa chini yake (Rum 5:19). Dhambi ni hali ya kibinadamu ambayo tiba yake ni neema za Kimungu (Rej Rum 7:13-25).
§ Dhambi ni kama kitu cha binafsi, cha kijamii, na cha ulimwengu wote (Rej. Rum 3:9...), kwa sababu hii binadamu wote wanakuwa daima kwenye vita.

1.2 Chanzo cha Dhambi

Dhambi ya Asili. Mungu alimuumba mtu kwa mfano wake na sura yake na akamfanya rafiki yake, na alipokea neema mbalimbali za kimungu.[2] Lakini kama ilivyokuwa kwa Malaika, Adamu na Eva walijaribiwa na katika jaribio hilo iliwapasa kutii amri ya Mungu. Hii ndiyo sababu ya amri tuliyopewa mtu asile matunda ya Mti wa ujuzi, wa Mema na Mabaya:
Mti wa Ujuzi, wa mema na mabaya huonesha kwa mifano mipaka ambayo mtu kwa vile ni kiumbe amewekewa asivuke. Tena aikubali mipaka hiyo kwa hiari na aiheshimu kwa ujasiri. Sasa kwa nini Mungu alimwacha mtu ajaribiwe? Jibu ni hili kwamba, kwa Adamu na Eva kuwa kamili katika upendo wa Mungu, walihitaji utashi huru; bahati mbaya sana, zawadi hii kutoka kwa Mungu ikaja kuwa upanga wenye makali kuwili, ambao pia ungeweza kuwaelekeza kwenye uovu. Mtu akishawishiwa na Ibilisi, aliachilia tumaini alilokuwa nalo kwa muumba wake lililoko moyoni mwake, na kwa kutumia vibaya uhuru wake akakaidi amri ya Mungu. Hiyo ndiyo dhambi ya kwanza ya mtu (Rej. Mwa 3:1-11; Rom 5:19). Tangu hapo, kila dhambi itakuwa ni kumkaidi Mungu na kukosa kutumainia wema wake.
Dhambi ya wazazi wetu wa kwanza ni kukosa utii. “…kwa kuasi kwake mtu mmoja watu wengi waliingizwa katika hali ya wenye dhambi …” (Rum 5:19). Mzizi wa kukosa utii ni kiburi au majivuno.

Ø    Wazo la kwamba dhambi ya Adamu na Eva ilikuwa ni ya kuzini ni la kupingwa kabisa kwani linapingana na ( Mwa 1: 28)
Kwa dhambi hii mtu amejichagua mwenyewe badala ya Mungu, na kwa hiyo amemdharau Mungu. Mtu aliumbwa katika hali ya utakatifu ili Mungu amshirikishe kikamilifu Uungu katika utukufu. Akishawishiwa na shetani mtu huyu ametaka kuwa “kama Mungu” lakini “bila Mungu mbele ya Mungu, na si kadiri ya Mungu.”[3]
Kwa hiyo, itambulike kwamba dhambi ya wazazi wetu wa kwanza ilikuwa dhambi ya kukosa utii.[4] Ni kwa kukosa utii huko watu wote wamefanywa wadhambi. Na mzizi wa dhambi hii ulikuwa kiburi.[5] Hivyo kiburi ni chanzo cha dhambi zote. Ndiyo maana Mt. Agustino anaelezea dhambi ya Adamu kuwa ni kitu kiikubwa hata kisicholezeka.[6]

Ø    Dhambi ya Asili imo katika upungufu/ukosefu wa neema uliosababishwa na tendo huru la dhambi lililofanywa na mkuu wa jamii ya binadamu (wazazi wetu wa kwanza)
Mtaguso wa Trento unatoa maana ya dhambi ya asili kama ni kifo cha roho. Kwa namna hiyo, kifo cha roho kimo katika kukosa neema ya utakaso, hivyo ndiyo kusema, dhambi ya asili ni ile hali ya kuwa na ukosefu wa neema. Kwa hiyo, dhambi iliyorithiwa kutoka kwa Adamu kimsingi imo katika kukosa neema ya utakaso. Na ukosefu wa neema ya utakaso ambayo kadiri ya matashi ya Mungu lazima iwepo, inamaanisha kwamba hatia ya dhambi ya asili inaonesha ni kugeukia mbali kutoka kwa Mungu yaani kumwacha Mungu.[7]
Kwa maneno mafupi kabisa tunaweza kusema kuwa, Adamu na Eva waliendeleza kwa vizazi vyao asili ya kibinadamu iliyojeruhiwa kwa dhambi ya kwanza, ikiwa imeondolewa utakatifu na haki ya asili. Ukosefu wa utakatifu huu na haki ya asili huitwa “dhambi ya asili.”[8]

1.3 Uenezwaji wa Dhambi

Japo kuwa haijulikani kwa uhakika kabisa namna gani dhambi ilikujakuwa sehemu ya hali ya maisha ya binadamu, habari ya Adamu na Eva katika kitabu cha Mwanzo inafafanua kwamba binadamu wanachagua wenyewe dhambi kwa uhuru kabisa na hivyo Mungu hahusiki kabisa na dhambi ya binadamu. “Kwa maana siku utakapokula, hakika utakufa” (Rej. Mwa 2: 17).[9]
“Dhambi ya Asili inaendelezwa na asili ya kibinadamu ‘kwa kuzaliwa sio kwa kuiga,’ na hivyo ni kwa kila mmoja”, isipokuwa Yesu na Maria. Ingawa dhambi ya asili ni ya kila mmoja, hakuna mzaliwa wa Adamu anayeirithi dhambi hii kama kosa lake binafsi. Watu wote wamo katika Adamu “watu wote wameshirikishwa katika dhambi ya Adamu, kama watu wote walivyoshirikishwa katika haki ya Kristo. Hata hivyo, jinsi dhambi ya asili inavyorithishwa ni fumbo tusiloweza kulielewa kikamilifu.”[10]

1.4 Aina za Dhambi

Kuna aina nyingi sana za dhambi. Maandiko yanatuambia “Matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo; katika hayo...” (Gal 5:19-21; 1Kor 6:9-10 au rej. Rum 1:28-32). Dhambi zaweza kutofautishwa kutegemeana na kitu, kama linavyoweza kila tendo la kibinadamu, au kutegemeana na fadhila ambazo dhambi zinapingana nazo, au kwa kupita kiasi au upungufu, au kutegemea amri ambazo zinazivunja. Zaweza pia kuainishwa kutegemea yule zinayemhusu: Mungu, jirani, au mtu mwenyewe. Inawezekana kuzigawa katika dhambi za kiroho na kimwili au za mawazo, maneno, matendo na kukosa kufanya. Kadiri ya mafundisho ya Bwana, mzizi wa dhambi umo ndani ya moyo wa mtu, katika utashi wake huru, “Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati, wizi, ushuhuda wa uwongo na matukano. Hayo ndiyo yamtiayo mtu unajisi; lakini kula kabla hajanawa mikono hakumtii mtu unajisi.”[11] Moyoni pia hukaa upendo, msingi wa kazi njema na safi, ambao dhambi huujeruhi.[12]
Kuna aina mbili za dhambi ambazo hupimwa kutokana na uzito wake. Aina hizo za dhambi ni:
o     Dhambi ya mauti
o     Dhambi nyepesi
Tofauti kati ya dhambi ya mauti na dhambi nyepesi kama ilivyo wazi tayari kutoka katika Maandiko Matakatifu (Rej.1Yoh 5:16-17), iliingizwa katika mapokeo ya Kanisa. Nayo yathibitishwa na mang’amuzi ya watu.[13]
Ø Dhambi ya mauti. Hii ni dhambi ambayo huharibu upendo katika moyo wa mtu kwa uvunjaji mzito/mkubwa wa sheria ya Mungu, inamgeuzia mtu mbali na Mungu ambaye ndiye kikomo chake kwa kupendelea kitu kidogo kuliko yeye. Dhambi ya mauti kwa kuwa inashambulia ndani yetu msingi hai, yaani upendo, yataka juhudi mpya ya huruma ya Mungu na uongofu wa moyo ambao kwa kawaida hukamilishwa kwa utaratibu wa Sakramenti ya Upatanisho. Dhambi ya mauti kuithibitisha ni lazima jambo lake liwe zito/kubwa, itendwe kwa ujuzi kamili (kwa akili) na kutaka/kutenda kwa makusudi (kwa utashi).[14]

ØDhambi nyepesi. Ni dhambi ambayo haivunji agano na Mungu, kwa neema ya Mungu inaweza kutengenezeka kibinadamu. Dhambi nyepesi haimwondolei mkosefu neema ya utakaso, urafiki na Mungu, mapendo, na furaha ya milele. Mmoja anatenda dhambi nyepesi kama hashiki, katika mambo madogo, viwango vinavyoelekezwa na sheria ya maadili, au anapokaidi sheria ya maadili katika jambo zito, bila ufahamu wote au bila kutaka kikamilifu. Dhambi nyepesi yabakiza mapendo, ingawa inayaumiza na kuyajeruhi. Na hivyo ni vema zikiungamwa kwani bila kuzifanyia toba kidogo kidogo hupelekea kutenda dhambi ya mauti.[15]

1.5 Matokeo ya Dhambi

v Matokeo ya dhambi ya Asili, yako katika maneno haya kwa ufupi: kwa dhambi ya Adamu, binadamu alikoseshwa neema ya utakaso na asili yake ilijeruhiwa.[16]
Dhambi hii ni katika kutokuwa na utakatifu na haki ya asili; hata hivyo, hali ya asili ya binadamu haikuharibika kabisa: imajeruhiwa katika nguvu zake za asili, ikitiishwa na ujinga, mateso, nguvu za kifo na maelekeo ya dhambi. Kwani mwanadamu amepoteza Neema ya Utakaso na kufanya wote kurithi, pia kajeruhiwa hulka yake aliyokuwa nayo toka mwanzo.[17] “Maelekeo hayo ya dhambi huitwa tamaa mbaya”[18]
Ubatizo, unapotoa uzima wa neema ya Kristo, hufuta dhambi ya asili na unamrudisha tena mtu kwa Mungu. Lakini matokeo ya dhambi hiyo, hali ya asili iliyodhoofishwa na yenye maelekeo ya uovu inabaki ndani ya mtu ikichochea mapambano ya kiroho.[19]

v Matokeo ya dhambi ya mauti. Endapo haikuondolewa kwa toba na kwa msamaha wa Mungu, dhambi ya mauti ina matokeo yafuatayo:[20]
ü Kupoteza mapendo na Mungu na kuondolewa neema ya utakaso.
ü Kutengwa na ufalme wa Kristo.
ü Kifo cha milele cha motoni/ Jehanam.
ü Kunyimwa uzima wa milele.
ü Kutengana na Kanisa.

v    Matokeo ya dhambi nyepesi. Tukumbuke kuwa dhambi hizi lazima pia nazo zikaungamwa maana zinapoendelea kutelekezwa hupelekea kuingia katika dhambi ya mauti. Ndiyo maana hata matokeo yake hapa chini yanaonyesha bayana kwamba pia yanavunja uhusiano mzuri na Mungu.[21]
ü Hudhoofisha upendo moyoni mwa mtu.
ü Huzuia maendeleo ya kiroho.
ü Zatuandaa kidogo kidogo kutenda dhambi ya
mauti.
ü Adhabu ya muda toharani au hapa hapa duniani.
Kwahiyo, “katika macho ya Imani hakuna baya lililo zito zaidi kuliko dhambi na hakuna kilicho na matokeo mabaya zaidi kwa wenye dhambi wenyewe, kwa kanisa na kwa ulimwengu wote.”[22] Kwa sababu hiyo tunapokea mwaliko huu siku zote ili uwe msaada kwa maisha yetu yote katika Bula ya Mt. Yohane Paulo II, “Huruma ya Mungu haina mipaka, lakini yoyote anayekataa kwa makusudi kupokea huruma yake kwa kutubu, anakataa msamaha wa dhambi zake na wokovu unaotolewa na Roho Mtakatifu.”[23]


 



SURA YA PILI

2.0 AHADI ZA MUNGU

Ahadi ni neno ambalo limetumika mara nyingi katika Biblia Takatifu. Katika Agano la kale tunamwona Baba yetu wa Imani Abrahamu akiahidiwa juu ya uzao wake kuwa utakuwa kama nyota za Mbinguni japo hata baada ya kupata taarifa Sara mkewe hakuamini juu ya ahadi hiyo na kuiona haiwezekani katika uzee wao (Rej. Mwa 18:1-15). Lakini pia hata katika Agano Jipya tunaambiwa na Kristo baada ya ufufuo wake kuwa; atapaa kwenda kwa Baba yake ambapo anatuahidia kwenda kutuandalia makao ili atakakokuwa, nasi tupatekuwako (Rej. Yn 14:1-4).

2.1 Nini maana ya Ahadi?

Kulingana na maelezo hapo juu, Ahadi inaelezewa kuwa ni kiapo kinachodai utekelezaji kwa makubaliano unayokuwa umeweka na mtu. Ndiyo maana mimi nachukulia ahadi kuendana sana na kiapo, japo siyo kiapo kinachowekwa mahakamani laa hasha! bali kinachoweza kushuhudiwa baina ya wahusika; mfano mtu anamwahidi mwenzake kitu fulani wakiwa katika mazingira ya wao wenyewe, hapo Mungu anakuwa shahidi. Pia watu wengi kama mashahidi pale mtu anapoahidi kitu katika sherehe kuwa atakitekeleza hapo mashahidi ni watu wote waliokusanyika hapo, nae Mungu anakuwa katikati yao. Hivyo, Ahadi ni kiapo kutoka kwa Mungu wanachoweka watu wengine kwa jina la Mungu au kwa kusanyiko la watu kama mashahidi zikidai heshima, uaminifu, ukweli na mamlaka ya kimungu. Ahadi hizi zinapaswa kuheshimiwa kwa haki. Mungu alikuwa mwaminifu katika ahadi zake tangu kale ambapo kila alichokiahidi kwa watu wake kilitekelezwa kikamilifu.[24] Nasi kupitia Mungu alivyotenda, methali isemayo Ahadi ni deni itukumbushe kuwa tunakila wajibu wa kutekeleza kile tunachokuwa tumeahidi.
Katika ahadi tunaaswa kutumia vizuri viapo hivyo, tukirejea amri ya pili ya Mungu inayotukataza viapo vya uwongo. Kutoa kiapo au kuapa ni kumchukua Mungu shahidi wa kile ambacho mtu anakithibitisha. Ni kuutia ukweli wa kimungu kama amana ya ukweli wake mtu. Kiapo kinapokuwa kweli na halali huweka wazi uhusiano uliopo kati ya maneno ya mtu na kweli ya Mungu aliye ahadi yenyewe.[25] Kwa maana hiyo tunamfanya Mungu awe shahidi na hivyo tunaposhindwa kutekeleza basi tunathibitisha na kumfanya Mungu awe shahidi wa uwongo. 

2.2 Ahadi ya Mungu kwa Watu wake.

Ahadi ya Mungu kwetu sisi; alituahidia uzima wa milele. Ndiyo maana tangu uumbaji wa vitu vyote alisema kuwa “...akaona kila kitu alichokifanya na tazama ni chema sana...” (Mwa 1:31). Lakini pia Mwenyezi Mungu hakuishia hapo kwetu wanadamu akatuumba kwa namna ya ajabu na ya kipekee sana “...Na tufanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu... (Mwa 1:26).” Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wake Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba” (Mwa 1:27).
Wema huu alioufanya na kuuweka kwetu ilikuwa ni ishara ya kutuonyesha upendo wake mkuu ya kwamba hakutaka alichokiumba kipotee bali kiwe na urahisi wa kufikia uzima wa milele. Tunaposoma katekisimu ndogo ya kanisa katoliki katika swali la kwanza linauliza juu ya lengo la kuumbwa kwetu.[26] Hivyo lengo lake mahususi kwetu ni kuishi maisha ya kumpendeza tungali hapa duniani, nasi tukapate kufikia ile ahadi tuliyoahidiwa na Kristo mwenyewe baada ya ufufuko wake na kupaa mbinguni. Pia anatuonyesha katika hili anaposema Bwana ataniokoa na kila neno baya, na kunihifadhi hata nifikie ufalme wake wa mbinguni. Utukufu una yeye milele na milele. Amina”.[27] Kwahiyo kila mtu atambue kuwa mara baada ya kumaliza hija ya hapa duniani tumeahidiwa kupokea ile tunu ambayo ilitekelezwa na Kristo mwenyewe aliposema kuwa anakwenda kwa Baba kutuandalia makao, ili alipo yeye nasi tukapatekuwako huko.[28] Kupaa Yesu mbinguni daima tunaidhamisha ile Dominika ya 6 baada ya Ufufuko wake katika kila mwaka wa Kanisa. Na hapo ndipo anaenda kutekeleza ahadi ile ya kwenda kutuandalia makao mbinguni, ili nasi tupatefika huko.

2.3 Utofauti wa Mwanadamu na Viumbe wengine

Katika uumbaji Mwenyezi Mungu naweza kusema alimpendelea sana Mwanadamu, na hii yote ilifanyika hivyo kwa lengo maalumu. Yeye aliye kila kitu alimtambua mwanadamu kama kiumbe ambacho kilikuwa dhaifu na hivyo kwa namna yoyote alipaswa aone namna ya kuja kukikomboa baadae. Swali la kujiuliza mwenyewe kichwani, unadhani uko sawa na wanyama au viumbe wengine walioumbwa na Mungu?  Una ufanano nao? Namna ya kuona vitu unadhani uko sawa nao? Unapo mtazama mnyama unamwona kama wewe ulivyo? Katika kutafakari kwangu nimebaini vitu vifuatavyo ambavyo naona tumetofautiana navyo mbali sana. Mwanadamu kiumbe wa Pekee, Upekee wake hautokani na kuwa na roho laa hasha ila ni kutokana na ukweli kuwa ameumbwa kwa sura na mfano wa Mungu tena ametoka moja kwa moja udongoni na siyo kutoka wanyama wengine.[29] Hapa kuna haja ya kuishi kindugu kwa sababu Mungu katufanya damu moja na yote yaliyomo katika historia yanalenga umoja wa binadamu.

2.3.1 Akili na Utashi.

Katika uumbaji Mungu alimpatia Mwanadamu akili ya kuweza kufikiri na kuelewa mambo katika upana wake na hivyo aweze kutenda kulingana na ile kweli yake. Katika akili ya mwanadamu ndiko kuliko uwanja mkubwa wa mapambano kati ya nafsi na ushawishi au majaribu kutoka nje. Kama nafsi ikijeruhiwa huwa na udhaifu katika kupambana na majaribu. Kutokana na udhaifu huo vishawishi au majaribu huweza kuishinda nafsi kwa urahisi na hatimaye dhambi huingia. Nafsi iliyoshindwa na dhambi huwa mtumwa wa dhambi. Utu wa ndani uliotawaliwa na dhambi, roho yake hushindwa kuunganisha maudhui mema au baraka za Mungu kutoka kwa Roho wa Mungu. 
Pia katujalia utashi ili tuweze kupambanua mambo na kuona lipi jema na lipi baya. Utashi ni uwezo wa kipekee, Mungu alimwumbia mwanadamu wa kuwa na hiyari au ridhaa ya kuamua bila kushinikizwa. Kwa mfano; ingawa nyoka alimshawishi Eva ale tunda la mti wa katikati ya bustani ya Edeni, alikini nyoka hakumlazimisha au kumsisitiza kula tunda, ila yeye mwenyewe kwa hiyari yake alinyoosha mkono na kuchuma tunda na kulila. Ni dhahili kwamba hamna kiumbe kingine kilichojaliwa Akili na Utashi zaidi ya mwanadamu. “Bwana Mungu akasema, Basi, huyu mtu amekuwa kama mmoja wetu, kwa kujua mema na mabaya; na sasa asije akanyosha mkono wake akatwaa matunda ya mti wa uzima, akala, akaishi milele.”[30] Viumbe wengine wamejaliwa Silika(instinct) yaani ukimwona mfano mbuzi amekula majani ikafika jioni lazima awe na kiu na hivyo kitakachofanyika lazima atafute maji anywe; sasa unapomkuta anakunywa huwezi kusema huyu mbuzi ana akili kweli kisa anakunywa maji. “Lakini hao kama wanyama wasio na akili... (2Pet 2:14)” inaonyesha kweli viumbe au wanyama wengine hawana akili tangu kuumbwa kwao.
Ni kwa hali hiyo hiyo ambapo tunaona pia mfano pengine mtu ameanika nafaka nje ya nyumba na kukawa na mbuzi mazingira yale, ili kuona kuwa hana akili anaweza kuja pale kutaka kula ila ukamfukuza kwa kumrushia jiwe na akaumia ila akikimbia kidogo utamwona anaanza kugeuka nyuma na kurudi tena. Kumbe angelikuwa na akili angalijiongeza hata kwa kutumia msema usemao akufukuzaye hakwambii toka; japo kwa kumrushia mpaka jiwe yeye haoni kana kwamba humtaki. Ukisema ana akili utakuwa unakosea, kumbe anafanya hivyo kwa kuwa ndiyo silika yake au kwa lugha nyinginr ndiyo asili yake. Mwanadamu tunamtazamia atende vitu kwa kutumia akili na utashi. Muda mwingine anaweza akajisahau kama kiumbe aliyedhaifu lakini hatumtazamii afanye vitu vibaya ambavyo vinakinzana na mpango wa Mungu.
Mwanafalsafa mmoja (Jeremy Bentham, 15 Februari 1748 – 6 Juni 1832) aliwahi kusema kuwa kila kitu mtu afanyacho anapaswa kufanya kile tu kimleteacho furaha, na vile visivyomletea furaha anajiepusha navyo. Sasa swali kulingana na mtazamo huo kwamba kwa mtu kila afanyacho anakifanya akitaka kupata furaha, na yaliyomengi yampatiayo mtu furaha ni mambo zaidi ya kidunia. Je! kuna mambo mtu anafanya ila hayana maana kabisa kama kuua au kufanya matendo mengine ya kinyama kama ukatili, huyo nae tunasemaje? Nae kwa matendo hayo anapata kweli furaha? Au anatofauti gani na mnyama sasa tena mkali kama simba au chui? Swali hili likupe changamoto ya kufikiri zaidi kwamba wale watu watendao kabisa matendo yaendanayo na wanyama tena wanyama wa mwituni tunawaweka katika sehemu gani, je! Nao pia ni wanyama au wako upande gani? Mzaburi katika zaburi ya 14 anasema, “Bwana akasema, je! Wote wafanyao maovu hawana akili?[31] ni swali aliuliza. Sasa mimi na wewe tungelijibu vipi? Jibu rahisi ni kwamba: fanya mazuri na epuka mabaya (Do good and avoid evil), au fanya kile ambacho nawe wapenda ufanyiwe na wengine. Kwa kufata hiyo kanuni ya maisha utajiepusha na ugonjwa wa kanza ya kujipenda mpaka kujipendelea.

2.3.2 Mwanadamu amefanywa kidogo tu kuliko Mungu.

Kama nilivyotangulia kusema hapo juu, Mwanadamu kwa upande mwingine ndiye aliyependelewa kwa namna ya ajabu kabisa kuliko viumbe wote.[32] Lakina pia katika maisha ya kawaida kuna msemo usemao kila kizuri hakikosi kuwa na dosari au siyo kila king’aacho ni dhahabu. Licha ya yote mwanadamu aliyotendewa na Mungu bado anakuja kuonekana kuwa ni msumbufu kupita viumbe wengine wote na kumfanya Mungu aanze kujilaumu kwa kumwumba kwake na matarajio yake kwake kupitia matendo, “Bwana akaghairi kwa kuwa amemfanya mwanadamu duniani, akahuzunika moyo.”[33]
Kupitia Huruma na Upendo wake bado anaendelea kumthamini kama kiumbe wake, hakuweza kusema basi amshushe kutoka hadhi hiyo aliyokuwa nayo bali akamwacha na kuendelea kubuni mbinu zaidi za kutaka kumwokoa. Hivyo mpaka sasa Mwandamu huyu ndiye anaeendelea kutangaza utukufu wa Mungu kupitia mamlaka na hadhi aliyopewa tangu kuumbwa kwake licha ya kuwa msumbufu sana. “Umemfanya mdogo punde kuliko Mungu...” (Rej. Zab 8:4-8).

2.3.3 Kiumbe wa mwisho katika kuumbwa.

Katika uumbaji tunaambiwa kupitia masimulizi makuu mawili. Simulizi la kwanza linapatikana ukisoma Mwa 1: 1-2:4a ambapo limetajwa kuonekana katika hali ya kitaalamu zaidi kuliko simulizi la pili, tunaambiwa namna Mungu alivyoanza kuumba Ulimwengu. Mbingu na Nchi tena Nchi tunaambiwa ilikuwa ukiwa na utupu; akianzia na siku ya kwanza akaamuru iwe nuru nayo ikawa mpaka siku ya sita, siku ya mwisho katika uumbaji anapomwumba mtu na siku ya saba tukaambiwa akastarehe. Simulizi la pili juu ya uumbaji linapatikana kuanzia Mwa 2: 4b-25 ambapo tunaelezwa kuwa limetaja taratibu sana namna ya zote za viumbe vilivyoumbwa na Mungu. Viumbe vyote vyatajwa kana kwamba vingaliumbwa kwa juma moja tu. Siku ya mwisho wa juma, ndiyo siku ya saba, Mungu alistarehe.
Hivyo kutokana na masimulizi hayo mawili Mungu ametuonyesha kuwa sisi kwake tu watu wenye thamani kubwa sana kuliko viumbe wengine wote. Ndiyo kusema kwamba hakutaka tuhangaike mara baada ya kuumbwa kwetu bali tukute mambo yameshakaa safi (poa au mwake kwa lugha ya kisasa). “………ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya sita” (Mwa 1: 26-31).

2.3.4 Kutawala vyote

Ni katika hali hiyo hiyo, Mungu aliweza kumwumba siku ya mwisho ili kile alichokuwa ameshakiumba kikapate kumfaa Mwanadamu. Hapo ndipo tunaona bado ule upendo wa Mungu kwa mwanadamu na ile namna ya hali na mategemeo makubwa sana kwa Mungu kupitia kwa mwanadamu. Ndiyo kusema kwamba namna ambayo alikuwa ameshanuia kuitekeleza wakati utimiapo ilikuwa katika mpangilio mzuri na safi, hivyo Mungu hakutenda na wala hatendi vitu kwa bahati mbaya bali kwake kila kitu kinamakusudi na umaana wake.
Katika Agano la kale tunaambiwa “Mungu akawabariki, Mungu akawaambia ….mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi” (Mwa 1: 28).  Pia “umemtawaza juu ya kazi za mikono yako; umemvika vitu vyote chini ya miguu yake. Kondoo, na ng’ombe wote pia; naam, na wanyama wa kondeni; ndege wa angani, na samaki wa baharini; na kila kipitiacho njia za baharini (Zab 8: 6-8).
Mwanadamu huyu ndiye aliyepewa mamlaka hiyo ya kutawala viumbe vyote maana kwa neno lake Mungu viliwekwa chini ya miguu ya mwanadamu. “Ee Mungu wa baba zetu, Bwana mwenye kuihifadhi rehema yako, umevifanya vitu vyote kwa neno lako; na kwa Hekima yako ukamwumba mwanadamu, ili avitawale viumbe vilivyoumbwa nawe, na kumiliki ulimwengu katika utakatifu na kwa haki, na kutoa hukumu kwa unyofu wa moyo.”[34] Namna nzuri inayomwezesha kuvitawala vizuri: ni kupitia vile vitu ambayo viumbe wengine walikosa nikimaanisha kwamba tunapaswa kuvitawala kwa kutumia Akili na Utashi tulivyojaliwa; kama zawadi ya pekee tuliyopewa. Na hivyo mwanadamu ndiye aliyewekwa kuwa mfalme wa kutawala viumbe wengine wote ulimwenguni.

2.3.5 Mwenye sura na mfano wa Mungu

Mungu akasema, “Na tufanye mtu kwa mfano wetu kwa sura yetu;...[35] Tunaambiwa ya kuwa naye ameviumba kwa taratibu ya ubora wao. Ameanzia viumbe hafifu hata mwisho akamwumba mtu  mwenye sura na mfano wa Mungu, akamweka kuwa mfalme wa ulimwengu wote.
Ni kwa mantiki hiyo, tunawiwa siku zote kutendeana vizuri. Kwani sisi wote tu watoto wa Baba mmoja, tena tulioumbwa kwa sura na mfano wake. Kwa kulitambua hilo kila mtu hapa duniani ni wathamani sana mbele zake Mungu aliyetuumba. Na hivyo hatuna sababu yoyote itupasayo kuanza kudharauliana. Hatuna sababu yoyote ya kuwa na majivuno na kujiona pengine wengine ni bora zaidi kuliko wengine.




SURA YA TATU

3.0 MAISHA YA SASA YA MWANADAMU

Mara nyingi nimekuwa nikijiuliza sana swali hili; kwamba hivi ndugu, jamaa na marafiki waliotutangulia mbele ya haki mfano wakafufuka nini watakacho tueleza wanadamu wa sasa? Au watashindwa hata kutueleza chochote kufuatana na mabadiliko yaliyoko sasa na kuona kwamba kila kitu kwao ni kigeni kabisa? Mara nyingi kama una desturi ya kuongea na wazee wa zamani ambao bado tuko nao, kuna vitu mpaka sasa haswa hawavielewi na hawajui kwa hakika ulimwengu huu wa leo unaelekea wapi; maana kila wakivuta taswira ya wakati wa ujana wao na sasa maisha yaendavyo wanaonyesha bayana kuwa hii siyo dunia ile ya zamani waliyoishi katika ujana wao.

3.1 Kuongezeka kwa uovu

Uovu ni kutenda kinyume na mpango wa Mungu yeye aliyemwema siku zote. Na hivyo kuongezeka kwa uovu inatupa jibu la moja kwa moja kuwa siku hizi wanadamu hawamchi Mungu wala kumwamini na kutenda kadiri ya mapenzi yake.Ukizingatia kinachochochea zaidi ni kwamba watu wamepozea hofu ya Mungu (No sense of sin), na hapo tumeshajijengea utamaduni wa kutokuwa na aibu; yaani hatuna mshipa wa aibu tena.Mwanadamu na dhambi ni mamoja.Na zifuatazo ndizo nguzo ambazo Mahatma Gandhi alizotoa:-
·       Kwanza ni Siasa bila maadili. Madhara yake ni makubwa kweli kweli, ndipo hapo tunaanza kukutana na maneno magumu sana hata kutamkika kama vile Rushwa. Hayo yote yanapata upenyo kwa kushindwa kuwa na maandalizi mazuri, na kufanya siasa ionekene ni kitu cha kujiingiza ili unufaike kirahisi; yaani pasipo kutokwa jasho. Pia kwa kukosa uadilifu tunakutana na wanasiasa amabao wanaishia kuwa waongo kweli kweli katika ahadi zao. Kwa kushindwa kutambua umaana wa siasa watu wengine wanajiingiza huko kwa sababu wanajua kuongea sana, hivyo muda mwingi wnajikuta wakishindwa kutawala ulimi wao: ndiyo kusema kwamba wanatafuta uongozi kwa nguvu hata kwa kuahidi uongo au kutoa ahadi ya viyu ambavyo anajua hatoweza kuvitekeleza. Tuwe waadilifu na wa kweli daima (Let’s be realistic). Ni kwa namna hiyo hiyo hatuna sababu ya kutoa visingizio katika uongozi bali kuwajibika kila mmoja kwa nafasi yake. Hatutaki tena kuwa na watu wasiojua siasa wala hawawezi kuwa viongozi, maana John C. Maxwell anatupatia sifa za kiongozi; ‘Kiongozi ni yule anayeifahamu njia, anapita na kuwaonyesha wengine.’[36] Hivyo kwa kuwa na kiongozi asiyejua maadili yake, atatufanya nasi kuenenda vivyo hivyo kwa kuwa ni kiongozi; maana wanasema kipofu hawezi kumwongoza kipofu mwenzake, akimwongoza maana yake wote wanaenda kutumbukia shimoni.

·       Pili, Ndoa bila mapendo. Tafsiri ya haraka haraka ya ndoa ni upendo. Ndoa inayokosa upendo inaenda kuwa ndoano. Utakuta wengine licha ya ukristo wao wanakimbilia talaka au kujiingiza katika ndoa za mitala. Mahatma Gandhi aliwahi kusema, “Palipo na upendo pana maisha.”[37] Tulioko katika ndoa tujitahdi kupendana hata ikitupasa kujitahidi kuulinda upendo huo kwa gharama yoyote, maana ndoa ni chimbuko na kitalu cha miito yote. Hatuwezi kupata watu wakuwekwa wakfu kama familia zetu hazina upendo, maana Mungu ndiye Upendo halisi;[38] hivyo hata kupata wahudumu wa kiroho kunaambatana na baraka na neema kutoka kwa Mungu.

Tunapozungumzia ndoa ni kitu cha kipekee kabisa kwani kinahitaji umakini wa hali ya juu kabla ya kuamua. Kwa kuwa mhimili wake mkuu umejengwa na upendo, hivyo watambue kupenda ni kuchagua na kuchagua ni kuamua. Kwa mantiki hiyo, maji ukiyavulia sharti uyaoge. Sasa inashangaza kweli kweli ya kwamba, tumekuwa tukiona baadhi ya wanandoa wakiishi kama vile Mwalimu na mwanafunzi wake au mtumwa na Bwana wake; mara nyingine wakithubutu hata mmoja wao akimwita mwenzake mbwa, huna kitu, mlala hoi, mpumbavu, nilikuoa bahati mbaya tu na mengine mengi kama hayo. Lakini jiulize kwanini useme hata ulioa bahati mbaya tu? Je, hukufanya maandalizi yoyote kabla ya kuamua hivyo? Sasa kama hukuweza kumshirikisha Mungu katika kuamua kwako ulitegemea au unategemea nini? (What do you expect?)  Sasa wewe ndugu yangu unayeanza kujipanga kwa maisha ya ndoa, tafadhali mkumbuke na umshirikishe Bwana Mungu wako naye atakujazi na kukusaidia katika kufanya uchaguzi na uamuzi mzuri. Kwa hakika hakuna lisilowezekana mbele yake Mungu, kama kweli tukimwendea kwa Imani. Tukimwomba kwa Imani kwa hakika yeye atatupatia chaguo halisi; litupasalo na kutufaa kwa maisha yote mpaka hapo mwisho wa maisha yetu yaani kifo.
Sala hii itufae wote tunaohangaika na kujua ni yupi kweli nimeumbiwa kuwa mwenza katika ndoa, kama kweli tukiwa na imani na kuisali mara zote.SALA/OMBI LA KUPATA MCHUMBA MWEMA.
Ee Mwumbaji wetu, umewaunganisha watu katika ndoa takatifu. Nami natamani kupokea sakramenti hiyo na kuambatana na mwenzangu wa ndoa maisha yangu yote. Kwa hiyo, nakuomba ee Bwana, unisaidie kuchagua kwa hekima, nipate mchumba mwema, safi, mwaminifu, nifuate Zaidi uzuri wa roho kuliko wa uso, Zaidi tabia njema kuliko utajiri na umaridadi. Mioyo yetu iwe ya kulingana, nia zetu zipatane, tupate kukaa pamoja kwa amani na kulea familia kwa kukuheshimu wewe na kupata Baraka yako. Amina.[39]
Hivyo, ili ndoa izidi kusitawi inahitaji kutawaliwa na uvumilivu unaoambatana na msamaha pasipo kuchoka; Bryant H. McGill alisema “Hakuna upendo bila msamaha, na hakuna msamaha bila upendo.”[40]Kumbe kupitia ile maana ya ndoa niliyodokeza hapo juu inakuja kuthihirishwa kwa maneno hayo, hivyo ndoa iliyojaa upendo na msamaha itadumu zaidi; maana kitakachoifanya iwe ndoano kwa kuwa imeshikana kwa pendo ambalo haliwezi kugawanyika kamwe.
·       Tatu, Dini bila hofu. Kuna mtu anajiita ni mkristo ila kiuhalisia anakuwa mkristo jina (In nomine persona). Hii ndiyo imetawala sana kwa sasa, unamamwona mtu kanisani unadhani kuwa ni mwamini kweli, kumbe anatumia kigezo hicho kufichia maovu yake. Anafanya hivyo ili kufumba mambo mengine, maana wahenga walisema akumlikaye mchana usiku hukuchoma. Hivyo afanyacho ni kujaribu kuficha na kutoanika hadhalani mambo yake. Kwa mfano, mtu anajua ametenda dhambi fulani, lakini hataki kukimbilia sakramenti ya kitubio na mbaya zaidi kila adhimisho lazima ampokee Kristo. Sasa mafundisho yanasema, ampokeaye Kristo pasipo kujiandaa hupokea hukumu yake. Tujiepushe kufanya vitu kwa mazoea tafadhali, na mbaya zaidi tukivifanya kwa kulalia mgongo wa kanisa au Dini.
Waraka wa Yakobo unatueleza kuwa Mtu ajaribiwapo, asiseme, “Ninajaribiwa na Mungu”; maana Mungu hawezi kujaribiwa na maovu, wala yeye mwenyewe hamjaribu mtu. Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa… (Yak 1:13-15). Kumbe maovu yetu yanasababishwa zaidi na tamaa ambayo tamaa hupelekea mashina mabaya saba yaliyo asili ya dhambi nyingi (Mizizi ya dhambi), kwa maana ni kama mizizi inayochipukiza dhambi nyingine Zaidi.[41]
v   Majivuno, ni hali ya mtu kujisikia kuwa yeye ndiye bora. Mwenye majivuno ataka kuvuna sifa kwa ajili ya nafsi yake. Mifano: Malaika wabaya; walijivuna kwasababu ya akili na uzuri wao, mpaka wakamwasi Mungu. Mtu tajiri kwasababu ya mali yake, anamnyima Lazaro chakula. Kwa hiyo ndugu yangu kama nawe ni miongoni wa wenye majivuno tambua ya kuwa unakilema cha Unyenyekevu yaani hutaki kujishusha zaidi unataka kukaa juu tu. Pia tukumbuke kuwa ni katika hali hiyo ya majivuno (kujiona watu wa maana sana kuliko wengine) inatupelekea katika kuotesha kiburi, ambavyo vyote havipendezi machoni kwa Mungu aliye peke yake Mtakatifu.[42]

v   Choyo, ni hali ya kuwa na mkono wa birika; yaani yeye hajui kutoa bali kupokea tu. Hivyo mwenye choyo hupenda mno fedha na mali, pia anakuwa na moyo mdogo sana msimopatikana nafasi kwa wenzake. Mifano: Yuda alikuwa na choyo ambapo kutoka kwake tunaona wizi, upungufu wa Imani, uhai, ukosefu wa matumaini na mwisho kujiua mwenyewe. Pia Tajiri kushiba mwenyewe na kumnyima Lazaro. Mimi na wewe mifano hii ituimarishe na kutujenga upya, pia tukitambua kuwa mtu mwenye choyo amekosa Ukarimu. Pengine mambo mengine yanapita mbali nasi bila kuyajua maana yake, kuna msemo usemao Kadiri utoavyo ndivyo upokeavyo Zaidi.

v   Uchafu, ni hali ya kutokuwa nadhifu kiroho; yaani kuwa katika dhambi. Mara nyingi uchafu huu unahusianishwa na mambo yatokanayo na tamaa za kimwili ambayo ni makatazo kutoka kwa Mungu. Mfano: Watu wa gharika kuu, kwasababu ya uchafu wao iliwapelekea katika uuaji. Mimi na wewe tujichunguze vema na kuona ni mara ngapi tumeiheshimu na kuipa hadhi miili yetu; ambayo kwayo tunaambiwa kuwa ni Hekalu la Roho Mtakatifu?  Jibu najua unalo, hii siyo tu kwa vijana tu ambao hawajaoa; nawe uliye katika ndoa ni mara ngapi umeitendea haki ndoa yako kwa kuwa mwaminifu kupitia viapo ulivyoweka mchana kweupe mbele ya kadamunasi Kanisani? Kama majibu yako yanaonyesha kuwa bado u mchafu, tambua ya kuwa umepungukiwa au umekosa Usafi wa Moyo.

v   Wivu, ni kitendo cha kuwa na kinyongo na mtu kwa kuwa tu amekuzidi kitu fulani. Tunaambiwa ya kuwa mtu mwenye wivu huwaonea wenzake kwa sababu ya heri na mali yao. Ni katika wivu maendeleo ya kimwili pia kiroho yanakawia na kudorora hususani kwa watu waishio vijiji wakijisadikisha na ushirikina. Mifano: Kain alimwua nduguye Abel kisa wivu. Pia vijijini watu wanashindwa kujenga nyumba nzuri wakihofia kurogwa au kwenda kumwabudu Mungu wa kweli, kwa vitisho vya wazee wa mila ya kuwa mizimu itamlaani na kumwua. Sasa je! Mimi na wewe ni wapi tunajikuta na wivu usio na maana? Tukitambua kwamba mtu mwenye wivu anakosa upendo kwa wenzake. Hivyo, kama unakosa upendo kwa wenzako ujue unakilema cha wivu yaana kwa maana nyingine hutaki maendeleo ya watu wengine.

v   Ulevi na Ulafi, ni kitendo cha kutumia aidha chakula au kunywa kupitiliza. Tukiongozwa na msemo usemao kila chochote kilichopitiliza ni hatari; Kwa mantiki hiyo Mlevi hunywa sana, Pia mlafi hula sana. Katika maisha yako je! Umeweza kutumia kila kitu kadiri ipasavyo? Hivyo kama umeshindwa kujisimamia katika maisha yako mwenyewe ujue ya kuwa unakosa fadhila ya Kiasi. Maana kitu kinaonekana na kuleta madhara baada ya kupitiliza katika ule uhalisia wa kawaida.


v   Hasira, ni kitendo cha kuwa na hulika. Mtu mwenye hasira hukasirika upesi tena bure (vitu visivyomaana). Japo katika hasira tunaambiwa kuwa kuna hasira ya haki, pale unapomkaripia mtu kwa kumkuta au kumwona akifanya vibaya. Mfano; Musa alipowaona waisraeli wakiabudu sanamu alikasirika. Likini hasira nyingine ni hiyo ya bure ambayo haina maana yoyote, mfano: Kain alikasirika sana baada ya kuona sadaka ya Abeli imepokelewa ila yake ikakataliwa. Najua kama binadamu tumeumbwa kila mmoja na hulika yake, hivyo kila mmoja anajijua hasira yake ni ya aje. Kama hasira yako inakutuma katika vitu ambavyo si vya maana jua ya kuwa umekosa Upole. Kwa hiyo, mfano wa kondoo afahamikaye kama mpole tujifunze kutoka kwake, hata kama tunapokutana na maudhi makubwa basi tukubali kujishusha hapo tutakuwa kama kondoo. Ndiyo maana wanashauri kuwa hata siku moja usije ukatoa maamuzi ukiwa katika hasira au ufanye na kuamua kitu ukiwa katika hali ya hasira lolote linawezakutokea, maana wanasema ‘hasira hasara’.

v   Uvivu, ni kitendo cha kushindwa kufanya kazi zilizo ndani ya uwezo wako kwa sababu zisizo na maana (uzembe). Tukirejea maisha ya wamonaki wao walianzia Ora et labora (kazi na sala), hivyo kufuatana mwito huo wa kufanya kazi kila mmoja aone kuwa ni wajibu wake na haki. “Kwa kuwa hata wakati ule tulipokuwapo kwenu tuliwaagiza neno hili; kwamba ikiwa mtu hataki kufanya kazi, basi, asile chakula” (2The 3:10). Tunapokuwa wavivu tutambue kuwa tumekosa bidii ya kufanya vitu ipasavyo. Maana katika kufanya bidii tunajipatia maendeleo ya kimwili pia kiroho, inatuonyesha utu. Misho katika maonyo tunaambiwa kuwa “uvivu ni mama wa dhambi nyingi”
Kwa kumalizia, tunapokuwa tukisali sala ile aliyotufundisha mwokozi wetu, tuifanye na kuwa kielelezo cha sala zote (Mt 6:9-15).Kumbe daima tusalipo tusali kwa moyo mmoja ili aweze kutimiza lile ombi la tano lisemalo “Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu.”(Mt 6:13). Daima tukiendelea kuisali kwa moyo radhi wa Imani, matumaini na mapendo atatuepusha na hayo maovu.

3.2 Kukosekana kwa Upendo

Tukirejea katekisimu ndogo ya Kanisa Katoliki juu ya Fadhila za Kimungu: Mungu ametaka tuweze kuitunza neema ya utakaso vizuri na kushika ahadi ya ubatizo kwa wepesi kabisa. Kwa hiyo wakati wa ubatizo wetu ametia fadhila za Kimungu na vipaji vya Roho Mtakatifu rohoni mwetu. Hivyo kuna fadhila tatu za Kimungu: Imani, matumaini na mapendo, ambapo hatuwezi kujipatia fadhila hizi kwa nguvu zetu wenyewe, kwa maana ni vipaji vya Mungu vipitavyo tabia na nguvu za kibinadamu. Kwa hiyo, Mungu amezitia rohoni mwetu fadhila hizi mara baada ya ubatizo ikiwa ni pamoja na neema ya utakaso; pia tunayo lazima ya kuzitunza kwa sala na matendo yetu.
Tujiepushe na Maisha bila sadaka. Mtu anapenda kuishi maisha ya fahari tu, pasipo kujikatalia baadhi ya vitu ambavyo siyo vya msingi katika maisha. Kwa mfano, unamkuta ni mtu anapenda kubalisha kuvaa nguo kila baada ya masaa sita (6); hapo hapo anatokea au anahamasishwa juu ya kujitolea kuchangia watu wasiojiweza kwa kutoa kiasi chochote kadiri anavyoguswa. Ila anashindwa kuchangia chochote hata kutoa 5,000/= akifikiri kwamba akitoa tu hiyo atavuruga mipango yake ya kuendelea kununua nguo. Kumbe kinachomchochea kufanya hivyo ni kupenda sifa na kujionyesha kwa watu wengine, akidhania kuwa akionekana na wale waliomzoea akibadili nguo mpya mara nyingi watamwona ameishiwa au ni kabwela tu. Tujiepushe kufanya vitu ili tutazamwe na watu, maana tunaambiwa amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwandamu; nasi tusileweshwa kwa kupenda sifa za watu pia tuachane na umaarufu kwa vitu visivyo na maana sana katika maisha. Maana ni pale tuonapo shida au kupata ugumu fulani katika kuamua tunapata suluhisho kamili. Albert Einstein anasema “katikati ya ugumu pana fursa.” Hivyo tusiwe wagumu kutoa sadaka kwa namna yoyote ile kwa maana ni katika kutoa kuwa nasi tunapokea (It is in giving that we receive) Mt. Fransisko wa Asiz alisema.
Muda mwingine tunajisahau sana juu ya mapendo, tukisema tunampenda Mungu wakati tunawachukia wenzetu wala kweli haiko ndani mwetu; maana huwezi kusema unampenda Mungu usiyemwona wakati mwanadamu mwenzako unaemwona humpendi. Kumbe tunaalikwa kwanza kumpenda Mungu kupita yote, kwani yeye ni Mpendevu kabisa. Maneno ya Roho Mtakatifu “Mungu ni upendo, na mwenye kuishi katika upendo, anaishi ndani ya Mungu na Mungu anaishi ndani yake.”(1Yoh 4:16). Kwa sababu hiyo “Basi, tumpende Mungu, kwa sasabu yeye alitupenda kwanza.”(1Yoh 4:19). Vivyo hivyo ni kwa mapendo yake Mungu ametuumba, ametukomboa na anatutakasa.
Utamwonyeshaje basi Mungu kuwa unampenda? Ni kwa kushika amri zake. Yesu anasema “Mkinipenda, mtazishika amri zangu.”(rej. Yn 14:15). Nayo maneno ya Roho Mtakatifu yanasema: “Kumpenda Mungu, ndiko kuzishika amri zake. Na amri zake si nzito.”(Rej. 1Yoh 5:3). Kwahiyo, Mkristu hodari ataonyesha mapendo yake pia kwa matendo yasiyoamriwa, yaani yaliyo ya hiari.
Dhana msingi kabisa ya kuonyesha ukuu wa upendo ya kwamba upendo hushinda yote ni huu, katika maisha ya Yesu hapa duniani alikutana na majaribu mbalimbali mengine yakitoka kwa Mafarisayo, Masadukayo, Waandishi na Wanasheria wakimwuliza katika hali ya kumjaribu juu ya amri iliyo kuu kupita zote. Yesu anawafundisha kwa maneno haya: “Umpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote na kwa nguvu zako zote. Hiyo ndiyo amri iliyo kubwa nayo ya kwanza. Na ya pili ni sawa na hiyo: Umpende mwenzako kama unavyojipenda mwenyewe.”(Rej. Mt 22:34-40, Yn 13:34). Kwasababu hiyo kila Mkristu anaalikwa kuishi maisha ya upendo maana kwa kuishi hivyo dunia itabadilika na kuwa kitalu cha Amani pia uovu kupungua, kwa kuwa kabla ya kumtendea mwenzako chochote utaanza kujifikiria kwanza mwenyewe je! Unachotaka kumtendea, nawe utapenda au utafurahi kufanyiwa vivyo hivyo. Kumbe mwaliko kwetu sote ni kuendelea kuishi katika ile hofu ya Mungu (Rej. Rum 12:10). Maana alitueleza chochote tukitendacho katika wale walio wadogo basi tunamtendea yeye. Kwa mantiki hiyo, mapigano baina ya nchi na nchi, mapigano ya ndani ya nchi na pia migogoro, kutothaminiana na kujaliana, kuwa watu wa visasi na mafarakano ndani ya familia zetu ni ishara wazi ya kuwa watu hatupendani kabisa (hatuna upendo ndani, ndani mwetu). Hivyo basi tujitahidi kuiishi tunu hii ya upendo na itaweza kubadili maisha yetu kwa ujumla na dunia nzima. Naye mzaburi anasema katika Zaburi 133“Tazama jinsi ilivyo vyema na kupendeza, ndugu wakae pamoja kwa umoja…maana huko ndiko Bwana aliamuru Baraka, naam uzima hata milele” nasi tuone fahari kuishi kwa umoja maana katika umoja kuna upendo usiogawanyika.
Kiini chote cha mafundisho ya Imani na ufundishaji wake lazima vielekezwe kwa upendo ambao kamwe hautakuwa na mwisho. Iwe kitu kinaelezwa kwa ajili ya ukweli wa imani au kwa lengo la matumaini au wajibu wa utendaji wa maadili, upendo wa Bwana wetu hauna budi kuonyeshwa daima, ili kila mmoja aweze kuona ya kwamba kazi zote za fadhila kamili ya Kikristo hutokana na mapendo na hazina malengo mengine isipokuwa mapendo tu(Katekisimu ya kirumi, utangulizi 10, KKK 25).

3.3 Kukosekana kwa Huruma

Neno msamaha au huruma siku hizi limekuwa kama msamiati mgumu, maana watu wengi hawalijali na kuona kama linafaa. Zaidi ya hayo yote tunajibidisha na vitu tunavyosema je! vinalipa au laa! kabla ya kutenda. Neno huruma limetumika sana hata katika kuumbwa kwetu na kuwa hivi tulivyo sasa ilikuwa tu kwa sababu ya huruma ya Mungu, ndiyo maana hakutaka tuangamizwe na ghadhabu yake pindi tunapokuwa tumemkosea bali tukimbilie msamaha wake kupitia sakramenti ya kitubio (upatanisho). “Mungu hakutuumba ili tuangamizwe na ghadhabu yake… kwa maana yeye hapendi mtu yeyote apotee bali wote wafikie toba… daima yupo tayari kumpokea kila ajaye kwake yeye mwenyewe anasema; “Nirudieni mimi kwa mioyo yenu yote...” Yoeli 2:12-14. Yesu alitupenda upeo na anatupenda ndio maana alijitoa mwenyewe afe msalabani ili tupate wokovu. Kumbe basi usalama wetu upo katika huruma ya Mungu tu. “Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo” Mdo 4:12. Pasipo huruma ya Mungu mtu hana thamani yoyote.
Bwana Yesu Kristo anaita watu wote waje kwake akisema “Njoni kwangu ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami ntawapumzisha. Jitieni nira yangu mkajifunze kwangu, kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo nanyi mtapata raha nafsini mwenu; kwa kuwa nira yangu ni laini na mzigo wangu ni mwepesi.”(Mathayo 11:28-30)
“Njoni kwangu nyote” maana yake ni kwamba hambagui yeyote yule. Anayeitikia wito huu na kuja kwa Yesu hupata huruma kuu ya Mungu.  Hivyo basi mtu yeyote asiseme moyoni mwake kwamba yeye amepangiwa kutokufika Mbinguni. Bila kumbagua yeyote Yesu anatupokea, “kwa maana yeye hapendi mtu yeyote apotee bali wote wafikie toba...”2Pet 3:9.
Tuepukane na kitu kinachoitwa Ushindani bila huruma. Kwa kupoteza hofu ya Mungu, mtu yuko radhi kumwua mwenzake ilimradi tu yeye aibuke kidedea au mshindi wa tukio hilo. Daima tujifunze kuwa na wivu wa maendeleo, yaani kama unajua au unaona kitu Fulani huwezi ukubaliane na hali yako tu; kama vijana wa kisasa wasemavyo kuwa pambana na hali yako.
Kumbe sasa ni muhimu kubadili mienendo yetu inayomchukiza Mungu. Hakuna awezaye kumpendeza Mungu asipokubali kujiachilia kwa Yesu Kristo na kumruhusu ayatawale maisha yake. Ni vizuri ifikie wakati tumwambie Yesu “Bila wewe mimi siwezi”. Tujitahidi kufananisha matendo yetu na ya Kristo Yesu, hapa ndipo tutaweza kujiachilia katika huruma yake. Na huruma hii inaendana kabisa kwa ukaribu na upendo, hivyo hatupaswi kuwa kama Petro aliyemwuliza Yesu kuwa ndugu yake akimkosea yafaa amsamehe mara ngapi? Na akajipa jibu Petro lake kama kumdadisi Yesu Hata mara saba? Ila Yesu anamwambia ya kuwa bado haitoshi mara saba, bali hata saba mara sabini (Mt 18:21-22). Huyu alikuwa Petro walau yeye aliona yafaa amsamehe nduguye mara saba, je! Mimi na wewe tungeweza hata kufikia hiyo mara saba? Kwa muktadha wa sasa tuliowengi tungeishia kusema tu kuwa tusamehe mara tatu yafaa. Kwa hiyo msamaha au huruma haina kikomo wala kiasi, kila mmoja anaalikwa kusamehe kadiri awezavyo: maana tunaambiwa tumepewa bure nasi tutoe bure. Mungu katujalia kuwa watu wa huruma, nasi hatunabudi kusameheana pia kuhurumiana; tukiendelea kuchukuliana misalaba.[43] Pia tunaambiwa kuwa kadiri tufanyavyo huruma ndivyo Mungu pia atutendeavyo.[44]

3.4 Kupuuza wengine (Dharau)

Kwanini tufike mahali tudharauliane? Kama viumbe dhaifu tunasahau ya kuwa sote tumeumbwa kwa mfano na sura ya Mungu (Rej. Mwa 1:26). Bali tunapaswa kujivunia utajiri tulijaliwa na kuutumia vema. Kwa mantiki hiyo kila mmoja amejaliwa karama na talanta mbalimbali, ambazo ndizo zinazoendelea kututegemeza sisi katika kujiendesha katika maisha ya hapa duniani (Rej. 1Kor 12:4-11). Ndiyo maana hata katika utume wa mamlaka ya ufundishaji katika Kanisa umepewa kwa watu wachache ili kuhakikisha Taifa la Mungu linadumu katika ukweli ambao ndiyo unaowafanya huru. Katika kutekeleza utume huu Kristo amewapa wachungaji karama ya kutokosea katika mambo ya Imani na maadili, na utekelezaji wake una namna nyingi kulingana na ngazi kama padre, Askofu au Papa.[45] Vivyo hivyo hata katika maisha ya kitawa, ngazi ya mabikira humweka mwanamke anayeishi ulimwenguni ili akae katika sala, toba utumishi kwa ndugu zake, kadiri ya karama husika zinazotolewa kwa kila mmoja.[46] Kwa hiyo tujifunze kuthaminiana pasipo kudharauliana, tukitambua kuwa kila mmoja wetu amejaliwa kitu cha kipee ambacho mwingine hana kabisa. Tukiendelea kudharauliana kati ya mwenye nacho na asiye nacho, inamaana kwamba tunajifungia milango ya kupokea zile heri nane, na hivyo Mwinjili Luka anatueleza kinaganaga katika heri nne (Rej. Lk 6:20-22) na laana nne. Hizo laana nne ndilo tuzo la huyu mtu anaedharau wenzake wasio na kitu atakachopata itakuwa ni kilio na kusaga meno (Rej. Lk 6:24-26). Kumbe msemo usemao tujifunze kutofautiana pasipo chuki, na kuchukuliana kwa upendo. Lakini yote haya tunayafanya pasipo kujua kwamba tumeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu mwenyewe? Au kutotambua kuwa Mungu amemjalia karama na kipaji cha kipekee kila mmoja wetu? Kwanini sasa tudharauliane wakati tunajua hamna aliyemkamilifu au anayejitosheleza kwa kila kitu isipokuwa Mungu tu? Nakuachia swali hilo msomaji wa kitabu hiki, na ujaribu kujitafakari je! wewe binafsi upo sehemu gani? 


SURA YA NNE

4.0 MABADILIKO YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA

Katika ukuaji wa mambo ya ulimwengu huu yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na suala la mabadiliko ya sayansi na teknolojia. Lakini pia tukumbuke kuwa hata hawa wanasayansi nao pia wameumbwa na Mungu, na kujaliwa karama hiyo ya uvumbuzi na utengenezaji wa mambo mbalimbali. Lengo kuu ni katika kumrahisishia mwanadamu katika harakati zake za kuendesha maisha yake kwa ujumla. Mfano; utengenezwaji wa ndege, ambao unamwezesha mwanadamu takiribani kuweza kufika karibu kila sehemu apendayo. Vivyo hivyo, palipo na mafanikio changamoto hazikosi; ni kupitia mabadiliko ya sayansi na teknolojia ulimwengu umeanza kupoteza vile vitu asili vilivyowekwa na Mungu. Kumbe mabadiliko haya yamekuwa ni kama msumeno ambao hukata huku na huku, yaani mabadiliko haya yameleta matokea ambayo ni chanya lakini pia hasi kwa dunia nzima.
Mtu mmoja ambaye anapingana na falsafa (fikira), Ukristo (maadili) na Sayansi (ukweli); Friedrich Wilhelm Nietzsche (kuzaliwa 15-10-1844, kufariki 25-8-1900) alijiita Nabii kwa kutabiri kuwa kuanzia karne mbili(2)zijazo dunia itakuwa katika matarajio ya mchakato usioepukika; ukomunisti, mijini, kiwango kikubwa cha viwandani, elimu, vyombo vya habari na utamaduni, utamaduni wa kisasa, kupambana na jadi na uhuru wa kibinadamu… Na mpaka sasa kweli tumeianza karne ya pili tangu afariki dunia, na yale aliyoongelea yameshaanza kutokea. Kwa wenzetu Nchi zilizoendelea walio wengi sasa hawamtambui Mungu, na wameendelea kiasi kwamba wanaweza kubashiri na kujua ya kesho. Kwa kushindwa kutambua na kuona uwepo wa Mungu, maana yake wamejiunga na Nietzsche aliyehitimisha kwa kusema Mungu amekufa (God is dead). Sasa katika sehemu hiyo tutaona mambo yanavyoenda sasa, nawe msomaji utaona kwamba mwanadamu ni mtu wa hatari sana; mpaka ameshaanza kufanya vitu kinyume hata na mpango wa Mungu aliounuia tangu mwanzo kupitia kwa wazazi wetu wa kwanza. Hivyo katika sehemu hii tunaenda kuona jinsi gani teknolojia imechangia kwa kiasi kikubwa katika mambo yahusuyo mauaji ya watu wasio na hatia. Pia katika kutafakari janga hilo kubwa, tukumbuke kuwa mwenye mamlaka ya kuchukua uhai wa mtu ni Mungu pekee.[47]

4.1Uharibifu mkubwa wa mazingira

Tukirejea katika kitabu cha mwanzo tunaambiwa kuwa na tazama kila alichokiumba Mungu ni chema (rej. Mwa 1:31). Wema unaoongelewa hapa si kitu kingine bali Mungu aliweza kukiweka kila kitu katika hali yake ya kuweza kujiendesha.  Hali kadhalika, kila kitu kiliwekwa katika ukamilifu wake kulingana na mpango wenyewe wa Mungu. Neno mazingira lina maana ya kila kitu kituzungukacho, kama uoto, mawe, mito, bahari na mengine mengi yanayotuzunguka.
Kupitia mabadiliko ya sayansi na teknolojia, viwanda vinavyotumika kuzalisha na kutengeneza mambo ya kumsaidia mwanadamu ndivyo vinavyochafua hewa. Kadhalika moshi utokao viwandani muda mwingine hutoka na viambata vyenye sumu, ambapo huenda kuharibu anga (destruction of ozone layer) pia kuathiri mwanadamu pindi tu anapoivuta hewa hiyo iliyochanganyikana na viambata vikali vya sumu. Pia inaweza kupelekea hata kuathiri mfumo mzima wa uumbaji wa pili ambao mwanadamu amepewa na Mungu. Si hivyo tu hata moto tunaotumia kuchoma msitu, kukata miti kwa kutumia misumeno au shoka pia panga; vyote vimetengenezwa kupitia maendeleo haya ya sayansi.Kwa kutambua hilo ndiyo maana mataifa yameweka mpango mkakati wa makubaliano ya Paris juu ya mabadiliko ya tabia ya nchi, ambayo yanalenga kupunguza uzalishwaji wa hewa na gesi chafu duniani.
Viongozi wa Kanisa kama nilivyosema mwanzo kuwa Kristo amewapa karama na mamlaka ya kukosoa katika mambo ya Imani na maadili, hivyo kipindi wanapoona mambo hayaendi vizuri wanakila sababu ya kushauri na pia kukemea mapema kulingana na ule mwelekeo uonyeshao madhara. Baba Mtakatifu Francis katika mwaka wa tatu wa Upapa wake tarehe ya 24/5/ 2015 sikukuu ya Pentekoste aliweza kuzindua Bula ya Sifa kwako ee Bwana (Laudato si). Kazi yake ilitoa mwongozo wa namna nzuri ya utunzaji wa mazingira kwa ulimwengu mzima. Bula ilipokelewa vizuri sana na mataifa yenye nguvu duniani ikiwemo Marekani. Baba Mtakatifu Francis hakuishia hapo akaanda sala ya kutukumbusha na kuelewa uzuri wa ulimwengu huu ulitoka wapi, na hivyo tuone tuna kila sababu ya kuutunza.
SALA KATIKA UMOJA PAMOJA NA UUMBAJI.
 Baba, tunakutukuza pamoja na viumbe wako wote. Vyote vilitoka katika mikono yako mikuu. Vyote ni vyako, vimejazwa uwepo na upendo wako mwanana. Sifa ziwe kwako!
Mwana wa Mungu, Yesu. Vitu vyote vilitengenezwa kupitia kwako. Ulifanyizwa tumboni mwa Maria mama yetu ukawa sehemu ya dunia hii na ukautazama ulimwengu huu kwa macho yako ya kibinadamu ndani ya utukufu wa ufufuko wako, Sifa ziwe kwako!
Roho Mtakatifu, kwa mwanga wako unaongoza ulimwengu huu kupitia pendo la Baba na kuusindikiza uumbaji unapogumia kwa utungu. Unakaa ndani mioyoni mwetu pia na unatuvuvia kutenda yaliyo mema. Sifa ziwe kwako!
Bwana wa utatu, jumuiya ajabu ya upendo usio na mipaka tufundishe kukutafakuri wewe katika uzuri wa ulimwengu kwani kila kitu kinasema juu yako. Amsha sifa na shukurani zetu kwa kila kilichopo ambacho umekifanya. Tupe neema kujisikia kuunganishwa na kila kilichopo.
Mungu wa upendo, tuoneshe sehemu yetu katika dunia hii kama mikondo ya upendo wako kwa viumbe vyote vya dunia hii kwani hakuna hata kimoja kinachosahaulika mbele zako. Angalia wote wenye mamlaka na mali ili waiepuke dhambi ya kutojali, ili wapende mali yetu ya pamoja, wawasaidie wanyonge, wawutunze ulimwengu huu tunamoishi masikini na dunia vyote vinakulilia.
Ee Bwana, tuteke kwa nguvu na mwanga wako, tusaidie tulindeaina zote za maisha, Tujiandae kwa mustakabali bora kwa ujio wa ufalme wako wa haki, Amani, upendo na uzuri. Sifa ziwe kwako! Amina.
Kadhalika tunaalikwa sote kwa pamoja, kila mmoja kwa nafasi yake kutunza mazingira. Kwa kufanya hivyo tutakuwa tunaendeleza ule uumbaji wa Mungu lakini pia zaidi tukiheshimu na kuifanya kazi ile aliyotupatia kuvitawala vitu vyote. Maana tusipofanya hivyo tunaambiwa katika vitu ambavyo havina uwezo wa kutoa msamaha ni Mazingira. Kwamba ukishayaharibu mazingira usitegemee kuwa yatarejea au kurudi katika uzamani wake kama yalivyokuwa. Kumbe tutambue kuwa tunapoyakosea haki mazingira yetu kwa kuyatunza, kwa hakika lazima yatuadhibu. Ambapo baadhi ya madhara yatokanayo na uharibifu wa mazingira ni pamoja na ukosefu au upungufu wa mvua, ukame, baa la njaa, kiu, n.k

4.2 Mauaji ya makusudi.

Kuua ni kitendo cha kutoa uhai wa kitu au mtu kwa namna yayote ile aidha kwa bahati mbaya au kwa kudhamilia. Katika Maandiko Matakatifu neno kuua limetumika sana, tukianzia na Kisa cha Kaini kumwua nduguye Habili kisa wivu tu baada ya ile sadaka ya Habili ya kuteketezwa kupokelewa mbele ya Mungu (Rej. Mwa 4:1-8). Kadhalika Mungu aliwaua wazaliwa wa kwanza wa wamisri baada ya Farao kukataa kuwaruhusu wana wa Israeli (Rej. Kut 13:15).  Pia tunaelezwa juu ya Mungu kuwaua wafalme wenye nguvu akina Sihoni, Ogu (Rej. Zab 135:10-12; 136:18-22). Tunaambiwa kuua kwake Mungu ilikuwa haki yake kufanya vile ili aweze kulikomboa taifa lake teule la wana wa Israeli.
Mauaji ninayozungumzia ni yale yatokanayo na vita. Vita hii inayoonekana katika mataifa yenye migogoro ya kisiasa. Mara zote yanachochewa na ile kuwa na uhakika wa silaha ambazo ni nzito sana na zimefanyika hivyo kupitia mabadiliko ya sayansi na teknolojia. Taifa na taifa wanawekeana vitisho vya vita ili kujaribu tu kupima silaha zao walizotengeneza zinauwezo gani wa kuleta madhara. Mfano, haya ndiyo yanayoendelea katika Taifa la Korea kaskazini wakijaribu kufanya vitisho dhidi ya Marekani. Kile kinachoendelea katika nchi ya Syria, kinasababishwa na kile kiburi cha kuwa na silaha za kutosha kwa Rais Bashar Al Assad: ndiyo maana tangu mwaka 2006 vita vya wenyewe kwa wenyewe vinaendelea mpaka sasa havijamalizika, licha ya mataifa mengine kuingilia kati ili kutaka kuinusuru Syria kwa kumwondoa Rais bado hawajaweza sababu kubwa ikiwa amejiimarisha vema katika nyanja ya silaha ambazo ni zao la mabadiliko ya sayansi na teknolojia.
Na kimaadili inasema kuwa katika hali ya kujilinda unaweza kutumia vifaa vinavyoweza kumjeruhi adui yako, kuua kabisa inayosemwa ni ile inayotokea bila kudhamiria kumwua. Mfano; unafyatua risasi kwenye bunduki yako ukimlenga risasi ya miguuni adui yako lakini naye katika kujihami akawa ameinama na hapo risasi ikapiga kifua akafaa, hiyo kimaadili inaweza kuelezeka katika dhamira.
Mauaji yanayoendelea katika ulimwengu huu wa sasa mengi yanachangiwa kuongezeka kwa kasi sana silaha mbalimbali; kwani njia na vitu vitumikavyo kutekeleza unyama huo vimerahisishwa. Mfano mtu mwenye chuki au nia mbaya nawe anaweza kukuangamiza tu atakapoanza kukuwinda mara na kukuona sehemu ya maficho kidogo, kwa kutumia silaha (bunduki ndogo); ambayo inamwezesha yeye kutembea nayo na haitoi sauti kubwa wakati wa kutekeleza shambulio. Kadhalika tumeona majambazi wakitekeleza uporaji mara nyingine kuua mara baada ya kuhisi kutambulika kwa kutumia silaha aidha ziwe za jadi au bunduki. Yote haya hufanyika hivi kwa kuwa mtu akihitaji silaha ya kununua kigezo ni pesa yake, kama anayo ananunua kwa nia ya kusema kuwa ni kwa ajili ya kujilinda au usalama wake.
Pia tunaona na kushuhudia ajali za barabarani zikiua watu wasiokuwa na hatia kwa kutojali sheria na kasi wakati wa uendeshaji barabarani kwa baadhi ya madereva. Yote hayo yamesababishwa kwa kiasi kikubwa na hayo mabadiliko ya sayansi na teknolojia, lengo hasa mahususi yakilenga kumrahisishia mwanadamu katika kuendesha maisha yake. Kwa bahati mbaya sasa mwanadamu huyo ndiye anatumia vitu hivyo vibaya, kwaajili ya kutimiza haja zake binafsi.
Hivyo basi, tunapaswa kutafuta Amani ambayo ndiyo huleta heshima na maendeleo ya mwanadamu kwa ujumla. Amani hii si kutokuwako vita tu na wala haiwekwi tu kwa kushikiza usawa wa nguvu kati ya wapinzani. Amani haiwezi kupatikana duniani bila usalama wa mali na watu, uhuru wa mawasiliano kati ya watu, kujali hadhi ya watu na mataifa, na jitihada za kuishi udugu (KKK 2304).Tuungane na Nabii Isaya anayesema “Amani ni kazi ya haki na matunda ya mapendo.”(rej. Isa 32:17).  Lakini pia wale wanaoendelea kufanya mauaji hao watambue damu hiyo wanayayomwaga inawalilia, kama ilivyokuwa kwa Kaini. Mungu alimwambia Kaini “sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi” (Mwa 4:10).

4.3 Matumizi mabaya ya vifaa vya Mawasiliano

Mawasiliano ni kitendo cha kuchukua au kutuma na kufikisha ujumbe kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine au kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Mtaguso Mkuu wa pili wa Vatikano; katika hati yake ihusuyo Kanisa unatueleza namna nzuri ya kushirikishana mambo mbalimbali bila ubaguzi kwa walei wote ukisema “Zaidi ya hayo, walei kwa kuunganisha nguvu zao waweza kuponya taasisi na hali za maisha zinazochochea dhambi katika ulimwengu, hivi kwamba wote waweze kufuata kanuni za haki ambazo zinarahisisha kutenda fadhila badala ya kuwa kizuizi. Kwa kufanya hivyo wanapenyeza thamani ya maadili katika utamaduni na kazi za binadamu.”[48]
Mfano halisi ni chombo cha mawasiliano kiitwacho simu. Simu imekuwa ngangali na ngunguli katika uovu sana, nadhani kupita kitu kingine zaidi. Simu kwa sasa baada ya kutumika kuwasiliana kwa mambo yenye tija na manufaa; inatumika katika kupanga njama za uzinzi na uasherati, wizi kwa namna ya pekee katika kutekeleza uharifu ikiwemo utekaji na ujambazi, uongo ambao unatikisa na kusambalatisha mpaka familia. Na hii imekumba takribani rika zote, si vijana si watu walio tayari katika maisha ya ndoa. Ndiyo maana ndoa nyingi siku hizi tunaziona zikiharibika pasipokuwa sababu ya msingi. Zaidi utasikia wameamua kuachana baada ya Mme au Mke kuchukua simu ya mwenzake, sasa anachokutana nacho humo ndani hakielezeki kwa maana ya kuwa anaona na kujua kuwa hayuko peke yake katika ndoa bali wengi.
Kama umewahi kushuhudia ni watu wachache sana ambao wanaweza kuiacha simu tu nje nje, zaidi kama anaiacha tu unakuta kaiwekea funguo (password) yaani kaiwekea namba ya siri karibu kila sehemu. Na kwa nini haya yote kutokea katika wanandoa? Katika maisha ya sasa watu wengi hususani vijana hawatambui tena utu wao uko wapi. Hivyo kupelekea kudandia gari kwa mbele, licha ya kwamba tumeambiwa na Mhubiri kuwa kila jambo linawakati wake (Rej. Mhu 3:1-8). Kwa hiyo, wanapokuja kubariki ndoa yao wanakuwa kama watu wanaoigiza, maana hamna anayekuwa ametunza utu wake kabla ya hapo. Mbaya zaidi kwa upande wa akina Dada ndiyo zaidi wanaathirika kisaikolojia pale anapojikuta ambaye ameshiriki naye katika kumvua utu wake kwa mara ya kwanza siye aliyemwoa. Tunaambiwa katika ndoa hiyo kuna mwingine hawezi kukaa kwa utulivu, kama tujuavyo kuwa binadamu tuna hulka ya kukumbuka. Maana kinachosababisha anakuwa ameshaweka agano la nafsi na mtu aliyemtolea ubikira wake. Hivyo anapomkumbuka tu yule wa kwanza atajitahidi kumtafuta kwa namna yoyote ilimradi tu ampate na aweze kutimiza haja yake. Sasa kifaa kitumikacho kumtafuta mtu huyo tunaweza kumwita pengine mwana mpotevu ni simu kwa maisha ya sasa, atajitahidi kuuliza kila mtu ambaye anaweza kuwa na namba yake.
Hali kadhalika tunaambiwa kama vile ndoa nafsi mbili zinavyounganisha kwa pamoja au zinavyoambatana, ndiyo inavyokuwa watu wanavyofanya ngono nje ya ndoa na kuunda mshikamano wa nafsi unaopelekea kuwa utumwa wa kipepo. Muungano unatokea hapa ulianzishwa na Mungu ili kuwafanya wanandoa wawili kuwa mwili mmoja mbele zake (Mwanzo 2:24; Malaki 2:15; Mathayo 19:5-6), lakini ngono kabla ya ndoa na ile ya nje ya ndoa inaweza kwa namna ya ajabu kushikamanisha nafsi ya mtu mmoja na wengi. Kama mtu akifanya ngono na watu wengine zaidi ya mke wake, anaunda mshikamano wa nafsi unaoweza kusababisha kila aina ya matatizo (ya kimwili, kiroho na kiakili) kwa kuwa ngono si tendo la kimwili tu, lakini ni la kihisia na kiroho pia. Sasa mshikamano wa nafsi unaotokea katika mazingira haya huwa njia ambayo mapepo yanapitisha chochote wanachotaka kwenda kwa wale wahusika ili wadumu katika kifungo au kuwadhuru.[49]
Kutokana na maelezo hayo juu, ndiyo maana tunapata misamiati kama kuchepuka siku hizi. Sasa niambie pale Bwana wake atakaposhika simu ya mkewe na kuona kuna namba ameiweka ya mtu, jina lenyewe lilivyo linatia ukakasi na linaonyeha muda mwingi ndo namba hiyo inafanya mawasiliano tu; nini kitatokea? Hapo jibu rahisi ni kwamba atamfata mkewe na kumhoji juu ya mtu huyo kuwa ni nani na anapojaribu kujitetea lazima aseme uongo ili abaki salama, hapo ndipo utasikia kila siku ni fujo na migogoro tu ndani ya nyumba; mpaka kufanya uvumilivu kufika kikomo mmoja anaamua kuondoka na hapo ndoa inaishia hapo. Maana kinachoshangaza kama ni Mama amechoshwa na kipigo cha kila mara, siku akisema anarudi kwao mwanamme naye siku hiyo hiyo naingiza jiko lingine ndani. Hii ina maana kuwa wote inawezekana walikuwa na miradi sehemu mbalimbali ila kwa kuwa wanasema siku za mwizi ni arobaini; basi aliyewahi kufikia hiyo siku ya arobaini ndiye anaondoka. Hapo tujifunze fadhila ya uvumilivu na kuona kabla ya kumnyoshea mwenzako kidole kimoja, jitazame nawe kuwa kuna vidole vitatu vinakuangalia; tusiwe wepesi wa kuhukumu wengine bila kujitafiti kwanza sisi wenyewe.
Lakini yote hayo yamesababishwa na msingi mbovu wa malezi, maana watu wa zamani wao walijua na kulelewa katika misingi ya maadaili ya kabila husika. Kwao waliweza kukaa mpaka kukamilisha ndoa yenyewe siku wanapopata Baraka za wazazi, yaani kuoana rasmi.Vijana wenzangu tujifunze kubadilika, na kuwa na ule uchu wa kusema kama wa zamani waliweza kwa nini mimi nisiweze! Hiyo itatutia nguvu na kutufanya kupiga hatua mbele kidogo, japo utandawazi ndiyo dhana inayotawala sasa akili zetu pia fikira zetu kwa muda mwingi.

4.4 Chanzo cha mahusiano mabaya

Mahusiano mabaya nayaanza kutokea pale tu tunaposhindwa kutenga muda wetu kwa ajili ya kuwapa nafasi watu wengine. Nikitolea mfano wa simu, siku hizi mtu anaweza kuwa anaongea na mtu mwingine iwe ni katika stori au kuuliza kitu au kushirikishana; kinachoshangaza utakuta mtu huyu anaendelea kuongea na mtu huyu akiendelea kuchati na simu yake. Hivyo, ile ngazi ya uhusiano lazima ipungue maana mtu mwingine ataanza kumfikiria mwenzake pengine amemdharau.
(i)Uhusiano mwingine unaweza kuwa baina ya taifa na taifa, kwa kuwekeana uhasama.
Mfano: unakuta taifa hili limejiendeleza katika kutengeneza silaha za masafa marefu, taifa lingine katika kuzalisha bidhaa zitumiwazo na wanadamu kila siku. Lazima watu au mataifa haya yaingie katika uhasama, ambapo mtengeneza bidhaa atamchukia mtengeneza silaha tena kali na kuanza kujihami naye. Sasa nini chanzo cha mafarakano hayo? Unakuta ni kupitia ujuzi huu wa sayansi na teknolojia kutofautiana tu, na hapo huleta kutoelewana kati ya watu au mataifa.
(ii) Ushabiki wa kila kitu (Kiu na tamaa ya mali na maisha ya kuiga).
Unakuta kijana kila kitu kinachotoka au kutengenezwa na kuona kipya iwe ni mavazi au vifaa vingine anajikuta anashadadia, licha ya kwamba pengine hana kipato cha kutosha. Kwa kuwa anakuwa ni mtu wa ushabiki, kupenda sifa atafanya kwa namna yoyote ile ili akipate atakacho. Sasa anapoamua kutumia njia mbaya kujipatia kitu hicho, moja kwa moja anakuwa hajafanya mahusiano mazuri na mtu pengine aliyemwibia tu. Tukitambua katika suala la maadili, kwamba kile kibaya kinachotendwa na mtu mwovu mmoja aidha mwizi kinaleta madhara kwa jamii nzima; maana hakuna jamii inayomkubali mwizi. Hivyo kijana aidha ajulikane kwa tendo hilo au asijulikane moja kwa moja katika dhamira yake impe somo kuwa ameshajitenga na jamii yote inayomzunguka.

(iii) Kanisa kujibebesha agenda ya uzazi wa mpango.
Uhusiano huu unakuja kuonekana mbaya baina ya Kanisa na Waamini pindi tu matokeo yake wengine kutumia njia sahihi yaani kwa kutumia njia ya asili, lakini wengine wengi zaidi kutumia njia chafu na mbaya za kisasa. Hii inakumba watu wengi zaidi na mbaya zaidi unakuta hata wale ambao tunakuwa na matazamio nao makubwa katika kuielimisha jamii (wasomi) wanatenda kinyume kwa kufuata njia ya asili (yaani kwa kufuata mabadiko ya mwanamke katika mzunguko wake wa kila mwezi). Tuna kila sababu ya kupiga vita kwa nguvu zetu zote njia hizo za kisayansi zinazokinzana na mpango wa Mama Kanisa. Tuelimishane juu ya madhara yatokanayo na utumiaji wa vijiti, sindano, vidonge na mara nyingine kuamua kutoa kizazi eti kisa kwamba watoto uliojaliwa wametosha huhitaji wengine. Baadhi ya madhara ya kutumia njia hizo za kisayansi, zinaweza kupelekea Kansa katika mkono wanapoziingiza hizo njiti, pia Kansa ya Kizazi na muda mwingine kwa wale wanaothubutu hata kutoa kizazi huishia kupata matatizo makubwa ya mahangaiko ya tumbo mpaka kufa kwao. Kwa nini sasa tufikie mahali hayo tuyaruhusu? Kumbe tutambue kuwa Kanisa linapingana na matumizi ya vidhibiti mimba (Contraceptive) maana vinaenda kinyume na mpango wa Mungu katika kuendeleza kazi ya uumbaji.



SURA YA TANO

5.0 KUSHUKA KWA MAADILI

Siku zote uhuru humfanya mwanadamu kuwa mtu mwadilifu. Na hivyo mtu anapotenda kwa kuazimia basi anakuwa ni Baba wa matendo yake. Na hivyo matendo ya kibinadamu yanachaguliwa kwa makusudi, kufuata hukumu ya dhamiri yanakuwa na sifa kimaadili. Kadhalika uadilifu wa matendo ya kibinadamu hutegemea zaidi kitu, nia na mazingira. Katika kitu tunaona je, kilichochaguliwa ni chema ambapo utashi unajielekeza kwake kwa makusudi. Na hili ndilo jambo la tendo la kibinadamu. Nia hukaa upande wa mtu anayetenda. Kwa sababu hiyo nia hukaa katika chanzo cha hiari cha tendo la kulainisha kwa njia za lengo lake, hivyo kufanya nia kuwa kitu cha lazima katika namna ya kupima tendo kimaadili. Mfano: katika kutenda jambo jema kwa jirani haigeuzi ile nia njema, na hivyo lengo halihalalishi njia. Mazingira pia ni mambo madogo yanayochangia katika kuongeza au kupunguza uzuri (adili) au ubaya wa tendo la kibinadamu. Yaweza pia kupunguza au kuongeza wajibu wa mtendaji.
Kadhalika mazingira yenyewe hayawezi kubadili sifa adili za matendo yenyewe; hayawezi kulifanya tendo kuwa jema au sahihi ambalo kwa lenyewe ni baya.[50] Changamoto zinazojitokeza na kuchochea kuporomoka kwa maadili, sehemu kubwa inayoathirika ni mijini. Watu wakaao mijini naweza kusema ndipo kuna mizizi hii, na hivyo mizizi hiyo kuanza kuambaa mpaka vijijini; inakuwa baada ya kumaliza na kuwa imeshatapakaa sana. Hivyo baadhi ya changamoto zinazoelezwa humu kwa wakazi wa vijijini bado tunaweza tusielewe vema nini hasa inamaanisha, hususani changamoto zinazoenda hata kinyume cha asili. Ila tuyaelewe kwa moyo na tuwe tayari kuyapiga vita maana mijini sasa yapo licha ya kuwa yanafanyika chini chini.

5.1 Utandawazi

Utandawazi kwanza ni neno lililoanza kutumika miaka ya 1990, likimaanisha kukifanya kitu kuwa katika kiwango cha kimataifa na kukihamisha nje ya mipaka na kukifanya kuwa cha wazi na kikafanywa na watu wa aina yote duniani.[51] Tunaweza kusema kwa lugha nyepesi kwamba utandawazi ni mwingiliano wa kweli mbalimbali ambao umefanya ukaribu wa kweli zaidi yaani dunia kuifanya kama kijiji. Utandawazi umeleta mabadiliko makubwa kiutamaduni, kijamii, kiuchumi, kisiasa na mengine mengi. Utandawazi pia una maana ya jambo linalolenga umiliki wa fikira na wa kiutamaduni juu ya kusaidiana na kuungana yaani kuwa kitu kimoja, kuondoa mipaka na masafa kati ya nchi na nchi, kukusanyika pamoja na kuleta kitu kinachoitwa “kijiji ulimwengu.”[52] Hivyo kunapotokea mwingiliano wa jamii zenye asili na mila tofauti lazima kutatokea shida aidha pande zote au upande mmojawapo. Sasa kuna neno linatumika wakisema tunaenda na wakati, sasa je, huu wakati unaoongelewa ndiyo ule Mhubiri anasema kuwa kila jambo na wakati wake? Au ni ujinga wetu tu, kutotofautisha kati ya jana na leo yaani kutenda vitu kulingana na mazingira husika kufuatana na kanuni na taratibu za jamii yenyewe?
Mimi na wewe tuachane na Usasa bila miiko. Wanasema, hakuna marefu yasiyokuwa na ncha. Baada ya malezi kudorora tunaona kwamba, mlezi wetu mkuu sasa amekuwa ni utandawazi; ambapo daima tunadai kuwa tunakwenda na muda ila kiuhalisia hatuna utandawazi bali utandawazimu. Kwamba wewe jinsia ya kike kuvaa sketi fupi au nguo za kuonyesha maumbile yako na muda mwingine nyingine zikitoa baadhi ya viungo nje; pia jinsia ya kiume kujindanganya kuwa umevaa suruali wakati unatembea ukionyesha nguo yako ya ndani au kuvaa suruali za kubana ni kukosa adabu. Sasa lazima tutambue kuwa kila kitu kina mipaka yake, sote tupambane kutokomeza utandawazimu huu. Maana ni katika umoja tunaweza. Lakini tatizo kubwa ni kwamba tunakuwa au tunavutwa na umoja katika mambo ya upuuzi, ila yale mazuri, ya msingi tunatengana. Hii itufumbue macho na kuona kwamba kuna nguvu ya shetani ndani mwetu inayotuongoza.
Pia kwa uelewa wangu mambo hayo nayaambatanisha na suala zima la mkumbo (mob), yaani kwa kuona mtu fulani yeye yuko hivi nami nakuwa kama yeye. Haya mambo ya kushadadia vitu hivi ndiyo hutupumbaza zaidi na kushindwa kuona na kufikiri hali husika katika mazingira yako, mila na desturi na utamaduni kwa ujumla unakichukuliaje kitu au kitendo hicho. Tunahitaji kutumia busara katika kuona mambo haya na kuamua, ili kuweza kupunguza wimbi lililopo katika maisha ya sasa.
Angalia namna ya uvaaji siku hizi pande zote, je! Unaendana na uvaaji wa maisha ya zamani? Maandiko Matakatifu yametupatia majibu sahihi ya namna anavyopaswa kuvaa mwanamke, ambayo ndiyo namna nzuri na adilifu. “Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani.”(1Tim 2:9). Jiulize kweli wanawake wa sasa wanavaa nguo za kujisitiri? Asilimia kubwa ndiyo wanaokiuka hiyo: huvaa nguo fupi, za kubana na zenye kuwekewa mipasuo mirefu ya nyuma na mbele. Pia ndiyo mpango mzima sasa kwamba mwanamke nywele, kila leo mpaka fujo katika familia lazima kwende saloon kusukwa; huko ni kupoteza muda tu kwa kwenda kusikiliza na kusimulia mambo ya watu wengine (kusengenya) hiyo ndiyo hulika ya Wamama. Kadhalika, siku hizi mwanamke huyo huyo ndiye yuko tayari kulala njaa ilimradi aonekane amevaa nguo za thamani kubwa.
Tukienda mbali zaidi tumefikia hata hatua ya kuvaa nguo zisizo za sifa zetu. Naliongea hili kwa masikitiko makubwa sana, kwani uvaaji wa nguo zetu unaendana na maumbile yetu katika namna ile tulivyoumbwa. Kwa mfano uliowazi kabisa, akina Mama, Dada na Mabinti katika ujumla wake jinsia ‘Ke’; tunawaona wanavaa suruali. Suruali hizo kimaumbile tu zipo kwa ajili ya jinsia ‘Me’. Kumbe tujiepushe na mavazi yasiyotuhusu, zaidi tujikite katika mavazi ya hulka zetu kulingana na jinsia zetu na namna ya maumbile yetu yanavyoturuhusu. “Mwanamke asivae mavazi yampasayo mwanamume, wala mwanamume asivae mavazi ya mwanamke; kwa maana kila afanyaye mambo hayo ni machukizo kwa Bwana, Mungu wako.[53]
Kadhalika mwanamke anaambiwa kuwa hana ruhusa ya kumtawala mwanaume, je! ni wanawake wangapi wanatekeleza agizo hilo? (rej. 1Tim 2:11-12). Siku hizi tunawaona akinamama wanaopiga waume zao, pia tunasikia wanawake hao hao wakitafuta haki sawa kwa wote. Lakini wamesahau ya kuwa hata Maandiko Matakatifu yaliweka bayana hata shughuli zimpasazo mwanamme pia mwanamke, kama kweli ni haki sawa kwanini ziliwekwa bayana kwa kutengwa kwa kila mmoja? (rej. Mwa 3:16-19; 1Tim 2:11-14). Kwa hiyo kuna vitu vingine tunaanza kuvipigia tu kampeni aidha baada ya kusikia kwa watu wengine hususani kutoka mataifa yaliyoendelea na kuviweka kwetu, pasipo kutambua asili yake iko wapi.
Upande wa wanaume, namna ya uvaaji imeshabadilika tena. Uvaaji wa suruali za kubana, uvaaji wa milegezo (yaani kata ‘k’) na unyoaji wa mitindo ya kigeni. Katika waafrika tulikuwa na namna zinazofanana kiutamaduni tangu zamani, lakini sasa tamaduni hizo hatuna tena sasa zimetoweka. Unyoaji wa nywele ulikuwa ukitumia zaidi nyenzo tata, yaani mikasi ambapo kichwa kiliwezeshwa kunyolewa katika ustandadi wa kipimo kimoja (kiwango kimoja). Lakini sasa baada ya upatikanaji wa nyenzo rahisi sana mtu anaweza kunyoa awezavyo, ndiyo maana utaona mara mtu amenyoa kiduku. Sasa kwa nini kiduku ambacho hakikuwepo tangu zamani? Utaambiwa alimwona mchezaji wa timu fulani amenyoa hivyo naye akavutiwa kunyoa hivyo. Kumbe kinachoendelea na kutusumbua sana ni suala la ushadadiaji (ushabiki usio na maana) wa vitu pasipo kujua umaana wake.
Vivyo hivyo tusije tukakiona kila kitu kuwa ndiyo fasheni, laa! hasha mengine kwa mazingira yetu na tamaduni zetu yanatudhalilisha tu. Kwa hiyo tujiepushe sana na vitu vya kuiga tu, bali katika kuviona tujitahidi kuvijua vina maana gani kwao na kwa mazingira yako vitaonekanaje.
Siku hizi kitu kinachotumaliza ni uvivu ambayo ni moja ya mzizi wa dhambi. Watu tumekuwa wazembe sana wa kutotaka kujishughulisha na ufanyaji kazi. Mtakatifu Paulo anasema na asiyefanya kazi na asile (rej. 2 The 3:10). Sasa ile roho ya mtu kutaka vitu vya mtelemko ndiyo imekuwa sana, na kusababisha au kuwa chanzo cha matatizo mengi sana ya sasa.
Tunajikuta tunajiingiza katika hali ya maisha bila msalaba. Kuna mwanafalsafa mmoja anaitwa Plato, alisema “Uhai usiofaa haukustahili kuishi” (Unexamined life is not worthy living). Vivyo hivyo mpiganaji maarufu Bruce Lee alisema “Usiombe kuwa na maisha rahisi, bali omba nguvu za kukabili maisha magumu.”[54]


Matokeo ya kupenda vitu rahisi.
v   Ongezeko la maovu, mfano: wizi, ujambazi na kadhalika. Kwa sababu mtu hataki tena kufanya kazi ila bado anatamaa ya kuishi, atafanya awezalo kuhakikisha walau anapata mkate wake wa kila siku. Sasa katika utafutaji wake kwa kuwa ni mtu ambaye hapendi kazi, anapenda vitu rahisi tu anaweza kutumia hata njia ya kuiba ilimradi tu aokoe uhai wake. Kumbe wizi huo ni kwa sababu hapendi kujishughulisha, ambayo ni matokeo hasi yasababishwayo pengine na walezi katika kipindi cha makuzi yake. Ni mtoto amezaliwa anakuta kila kitu kipo, wazazi wanamwambia wala usifanye kazi yoyote mwanetu wewe tulia tu kula bata. Sasa waliokuwa wakimtia kiburi cha kutofanya kazi wanapotoweka na kila kitu, hapo ndipo mtu anaanza kutaabika na kushindwa kuona afanyeje; mwisho wa siku anaona kuiba itakuwa rahisi maana kushika jembe hawezi wala kufanya kazi yoyote ile itakayomfaa.

v   Mimba za kabla ya ndoa, Mfano: mimba katika hali ya uanafunzi au mimba za utotoni; huchangiwa zaidi na upokeaji wa zawadi mbalimbali kwa mwanafunzi, ambapo muda fulani anapata fursa ya kumbana ili amlipe vyake na kwa kuwa hana uwezo huo wa kurudisha basi namna iliyowazi kwake anaona bora atoe utu wake.

Haya tunayashuhudia zaidi katika shule zetu za sekondari, ambapo unakuta ni binti anasoma umbali ambao japo siyo mrefu ila kwa sababu ya kujidekeza anaamua kupanda aidha bodaboda au tax kuweza kumfikisha shule. Kwa kuwa familia zetu tunazijua ni masikini, hivyo hawawezi kuhimili gharama za kila siku na binti kwa kuwa amezoea hivyo kusema hata atembee hawezi; anafanya kila mbinu ilimradi aendelee kufika shule kirahisi na kujikuta tayari yuko kwenye mkataba na dreva tax au bodaboda sasa. Kadiri mazoea yanavyozidi, wanaamua kujihararishia ndoa mwisho wa siku utashangaa binti tayari ni mjamzito. Lakini nasi vijana tunaojiingiza katika wimbi hilo la mapenzi kabla ya muda wetu, tafadhali naomba tutambue kuwa tendo la ndoa ni marupurupu ya wanandoa tu.

v   Mimba za Utotoni
Kwa mujibu wa Mafrt. BONAVENTURA MAHEHELA na BENEDICT KAGWA mwaka 2015 juu ya mimba za utotoni, wanaanza kwa kujiuliza swali msingi hili; Nini maana ya mimba za utotoni? Mimba za utotoni ni zile zinazo tungwa kabla ya umri unaomruhusu msichana kupata mimba kwa kuwa anaelewa wajibu huo wa mzazi. Kwa hali ya kawaida, mwanamke anayeeleweka kupata uja uzito ni yule aliyefikia umri wa kuwa mtu mwenye kuweza kubeba majukumu ya mama wa familia. Sio kupata mimba msichana angali mtoto yaani anakuwa ‘mtoto mwenye mtoto!
Sababu za mimba za utotoni.
Sababu nyingi zinazoweza kutajwa katika jambo hili ni za ukurupushaji wa maadili ya Kanisa na yaliyo mema kwenye jamii. Nyingine zinatokana na utukutu au kudanganyana kati ya vijana wenyewe. Wengine wameingia kwenye matatizo ya kutaka kujaribu kila kitu maishani. Kuyakimbilia mambo bila kujua nini wanakikimbilia.
·       Maisha magumu (hali ya uchumi kwa baadhi ya familia).
Wasichana wakati mwingine hujiingiza katika mahusiano ya kimapenzi wakiwa watoto wadogo. Hii ni kwa sababu ya kutaka kutimiza mahitaji yao, kwani familia zilizo nyingi zinakuwa na uwezo mdogo wa kutimiza mahitaji ya msichana, hivyo binti anaamua kujiingiza kwenye ngono akiwa mtoto mdogo na matokeo yake ndiyo ndoa za utotoni.
·       Elimu kwa watoto wote
Katika kipengee hiki tulitazame suala hili kwa namna mbili; kwanza kabisa; katika Familia. Familia zilizo nyingi hazipati muda mzuri wa kukaa na watoto wao kwa ajili ya kuwaelimisha mambo ya duniani hapa. Familia hazina muda wa kuwaelimisha watoto wao kwamba mtoto kujiingiza kwenye mahusiano akiwa mdogo ni kosa kubwa sana. Kukosekana kwa fundisho hili kumepelekea watoto walio wengi wanajiongoza wenyewe tu. Tukijaribu kulinganisa watoto wa sasa na kipindi cha nyuma ni tofauti, maana kipindi cha nyuma vijana walikuwa pia wakipata elimu kupitia JANDO na UNYAGO.
Pili, Shule. Shule pia kwa namna nyingine zinachangia kusababisha mimba za utotoni kutokana na ufundishaji wa mfumo wa uzazi hasa shule za msingi. Kuna mafundisho mengine kwa asili yake, yanavunja ukuta wa malezi bora, yanabomoa nguzo ya malezi bora kwa vijana. Mathalani mtoto mdogo anafundishwa juu ya matumizi ya Kondomu, uzazi wa mpango kwa njia ya vidhibiti mimba kama vile vipandikizi nk. Anapo yapata haya, tukumbuke kuwa haya pati kwa nguvu ile ile yale yaliyo ya kinyume chake yaani yenye kuonesha athari zake (hususana mafundisho ya Kanisa).
·       Mitandao (utandawazi)
Mitandao ni chanzo kikubwa kabisa cha kusababisha mimba  za utotoni kwa watoto wengi kwa sasa. Hii ina jidhihirisha hasa tunapoona watoto wadogo wanaingia kwenye internet na kupakua picha za uchi na kuangalia. Hii inawapelekea kuwaka tamaa na kutaka kufanya au kujaribu na kuwasababisha kupata mimba zitokanazo na udadisi wao juu ya mambo wayaonayo mtandaoni.
·       Kupuuzia mila zetu na kufuata za kigeni (kugenishwa)
Tufikapo mahali tukayaona yakwetu kuwa ni mavi na ya wengine kuwa ni dhahabu hapo tujue kuwa tunauvua kwa kuusaliti utu wetu kama Watanzania na wenye tunu zao msingi na kunadi za mataifa mengine. Na ukweli unaonesha kuwa nyingi kati ya hizi tunazokopa kwingine ni za hovyo. Hii nayo inajidhihirisha hasa kwa watoto wa kike. Tukilinganisha kwa sasa na zamani tunagundua kabisa kuna upuuzaji wa tamaduni na mila zetu, maana watoto au wasichana wanakaa na kuvaa sketi tupu tofauti na mila zetu. Na hii inasababisha tamaa kwa wanaume walio wengi.
·       Utamu wa dhambi
Sifa mojawapo ya dhambi ni hii ya kuwa tamu. Dhambi yoyote ile iko kama dawa kali ambayo imewekwa juu yake vitu vitamu (sweet coating) ili kuleta utamu kwa mmezaji lakini ndani yake kuna uchungu. Kumbe na dhambi inaonekana kuvutia, inaonekana kubeba utamu kwa juu lakini ukishaitenda kama dhamiri iko hai, utaonja machungu ya dhambi. Kabla ya kutenda mawazo yote huleta uzuri wa jambo lakini mara baada ya kulitenda unaingia kitu kiitwacho ‘majuto.’ Na majuto siku zote ni mjukuu, yaani huja baada ya tendo baya. Kwahiyo, vijana wengi wamekuwa wahanga wa jambo hili maana waliona utamu wa mahusiano, wakahusiana kweli na mwisho wakapata malipo ya mahusiano yao (ujauzito kwa msichana kabla ya ndoa)! Utamu huu wa dhambi, umepelekea wengine kubobea katika tamaa za uzinzi, ukishabobea namna hiyo mwendo mdundo ni kutenda dhambi hii na huyu, kesho na yule. Hapo dhambi inazaa dhambi (sin begets sin) na inapata mpaka wajukuu ambao majina yao ni ‘dhambi!’
·       Kukaidi na kuvunja Amri za Mungu
Vijana kama tunamwogopa Mungu na kumpa heshima yake stahiki, tutamsikiliza asemapo ‘acha hili, tena hili, litende hivi.’ Katika amri VI ya Mungu tumekatazwa kuzini (Kut. 20:14). Kwenda kinyume na hiyo amri ndipo wenzetu (vijana) wameishia (vijana) kupata ujauzito kabla ya wakati (ndoa). Kijana ukishindwa kuitii amri ya Mungu utafanya kila aina ya uovu maana huna uoga na utii kwa Mungu, na hapo hutafaidika na lolote ulitendalo zaidi ya kupata athari za ukaidi.
·       Kupenda kujaribu jaribu kila mambo/ kitu (negative curiosity)
Kujua jambo au mambo si kosa kosa ni kujua hata kabla ya muda mwafaka wa kuyajua baadhi ya mambo. Mtoto mchanga akizaliwa anajua mambo pole pole tena kwa kiwango cha umuhimu wake. Cha kwanza kabisa ni kujua chakula chake kiko wapi (kifuani mwa mama wake), jambo la pili ni namna ya kukila chakula hicho. Sasa kwa mfano wa mtoto mchanga huo, nasi vijana tuweni na shauku nzuri ya kujua mambo na vitu. Ukiwa mwanafunzi, jua yamhusuyo mwanafunzi barabara na mengine yanayokujenga ungali mwanafunzi. Cha ajabu na cha kusikitisha ni pale mwanafunzi tunayomwona kwa nje amevalia sare safi na daftari mkononi kumbe hapo alipo anajua mambo ya ngono, mambo ya mapenzi kuliko hata walio kwenye kitengo hicho (wana ndoa). Kwanini tusiwe na kauli hii moja ya kuwa ‘ya Ngoswe mwachie Ngoswe.’ Kujaribu jaribu huko wengine wamejaribu kufanya mapenzi na matunda yake ni mimba kabla ya ndoa. Jambo hili kwangu ni ‘missing the target!’ usijaribu ukali wa sumu kwa kuilamba kijana mwenzangu. Siyo lazima ufanye mapenzi kabla ya kuoa ili uje uoe bila shida yoyote. Utunze mwili wako kwaajili ya aliyeandaliwa kwako na Mungu. Fikiria raha na furaha utakayoikuta kwa mwanamwali bikira aliyejitunza kama zawadi kwako, naye je, atafurahije akigundua yeye amekuwa wa kwanza kwako?
·       Ushawishi wa marafiki (mob/company)
Kuna ukweli kwamba kuna watu kama bendera, ‘hufuata upepo.’ Na wengine ni kama toroli, ‘lazima wasukumwe na wengine.’ Na wengine ni kama maji, ‘lazima wafuate mkondo.’ Haya siyo maisha vijana wenzangu, tusimameni wenyewe wakati mwingine. Usione fulani anafanya kitu fulani nawe bila kufikiria ukaenda kukifanya huko nyumbani ndiyo maana kwenye mieleka utakumbushwa ‘stay safe, don’t try this at home.’ Usifuatane na kikundi cha wazinzi, watakuambukiza uzinzi. Usifuatene na kampani ya watongozaji wanaojiona wao kuwa jogoo wa kila mtetea, utalazimika kuwa jogoo moja wapo la kutongoza mtetea. Usiwe katika kundi la wanaopenda tu kusikia ‘SSSSSSS’ miluzi ya wavulana ndipo wanafurahi. Hawa mimi nawaita jamvi la kila mgeni. Ukikaa nao utaishia kuwa jamvi la mgeni fulani. Tusiwe na roho ya kujaribu kila kitu mengine tuseme ‘hili jambo hata siliwezi, na hili hata kama naweza kulifanya, silifanyi.’
·       Kuogopa kuuziwa mbuzi kwenye gunia
Huu nao ni ukweli ambao nisipousema sitakuwa huru kamwe. Kuna vijana nilishaongea nao kuhusu masuala ya kufanya mapenzi kabla ya kuoa/kuolewa, walinieleza wazi kuwa ‘leo hii hakuna msichana mkweli, wala hakuna mvulana mkweli, kumbe kuwa salama na unayetaka kumwoa au kuwa na uhakika kwamba mambo ya ndoa unayaweza, kipimo ni kufanya mapenzi kadiri uwezavyo.’ Kweli inasikitisha! Na hapa kama mpo, mnanisikitisha sana, lakini kwa kuwa siwadhanii hivyo ngoja nisonge mbele nikiwatumia ninyi kama mabalozi wangu huko mwendako. Wengine wanaenda mbali zaidi na kudai hata kupata mtoto kwanza ili wajue kama wakioana wanaweza kupata watoto au la! Ukiyaweka pamoja masuala haya, utafika kituo cha mwisho ukute vijana wengi sana leo wameingia kwenye uwanja huo wa walioharibikiwa!
·       Utandawazi na athari zake hasi
Mambo yamerahisishwa sana na utandawazi. Lakini pia yameharibiwa sana kwao huo utandawazi. Ambayo hayakuwezekana zamani, leo yanawezekana. Mazuri kwa mabaya yote yanawezekana leo kwa hii sayansi na teknolojia. Hapo hata mengine kati ya tuliyoyaona hapo juu yamepata kichocheo (catalyst) chake mfano ‘negative curiosity, mob, and bad company.’ Kuna msemo huu kwamba ‘google tu utaipata mubashara, usije ukaaibika siku ya mechi kwa kuonekana huyajui mambo, google tu ujinoe, usije ukazidiwa ndani ya dakika 5 za mchezo kwa kutokuzijua njia, namna, google tu ungali kwenye zoezi ili kwenye mechi uoneshe umahiri na hutoachwa kamwe.’ Vijana wamegoogle na hakuna walichobakiza nyuma. Wamejua mambo na mambo yamewajua, wamejuana kwa maneno mengine. Ngono za kwenye simu, zimewaandaa kwa ngono mubashara siku watakapoonana. Takataka zote password yake iko kwa google. Google huyu hana huruma, amewaacha wasichana wengi wajawazito na wengine hata leo hii wanalia kilio kikuu. Sisi nasi twataka kujiunga nao?! Angalia sana kijana ‘unagoogle nini?’
·       Kudanganyika na kutaka kuudhihirisha upendo kwa ngono
Kama kweli unanipenda…’ Kinachomaliziwa hapo, ni sadaka ya mwili wako kwa mwenzako. Eti, ndugu vijana wenzangu, mimi kukupenda wewe dada mpaka tulidhihirishe hilo kwa mapenzi? Wewe kumpenda kijana wa kiume/kike mpaka mfanye mapenzi ndipo ijulikane kuwa mnapendana? Kipimo cha upendo ni kupenda bila kipimo. Kupenda bila kikomo. Na Mt. Mama Tereza wa Kalkuta anasema kipimo hicho ni kutokuwahukumu watu. Anasema ‘ukiwahukumu watu, huna muda wa kuwapenda.’ Vile vile anasema ‘penda mpaka uumie.’ Hajasema fanya mapenzi na umpendaye na hapo mtajua mnapendana. Kama kweli unampenda, utauheshimu utu wake, utaiheshimu na kuithamini kesho yake. Hutamchezea. Vijana msihadaike, hakuna upendo wa kweli kwa rushwa ya ngono. Huko kuna wengi waliofanya hivyo na wakaishia kupata uja uzito kabla ya ndoa. Je, walioana? Upendo wao je, uliendelea? Baada ya kuzini huja majonzi, huzuni, masikitiko. Msidanganyike mkaishia kubeba mikono vichwani mwenu. Mtu akikupenda na akadai uhusiano wa ngono ili kudhihirisha pendo lenu, huyo hakupendi anapenda tendo la ngono juu ya mwili wako yaani amekushusha mpaka kwenye hatua ya kuthamanishwa na ngono, bila hiyo wewe si kitu! Hii ni mbaya sana. Upendo wa kweli hauko hivyo. ‘PENDANENI KAMA VILE MIMI NILIVYO WAPENDA NINYI.’ Ni ujumbe wa Kristo tunayejiandaa kushuhudia ufufuko na ushindi wake. Wengine ni waongo, walaghai tu, madebe matupu tu ambayo hayaachi kutika.
·       Mmonyoko wa maadili
Hapo kale iliaminika kuwa msichana mwenye heshima alikuwa yule ambaye hakumjua mume mpaka alipoolewa. Ndiyo maana hata mama wetu Bikira Maria alipoambiwa atachukua mimba na kumzaa mtoto, alistaajabu na hata kumwuliza mjumbe wa Mungu “Itawezekanaje maana mimi simjui mume” (rej. Lk. 1:34)? Leo ndugu mkubali au mkatae, mgune au mnong’one, kuna hata wazazi wanao wahimiza watoto wao wakike na wakiume kuwa na maboyfriend na magirlfriend ili siku ya siku wasiwaaibishe. Wengine mpaka wanawatafutia watoto wao marafiki wa kimapenzi eti wanasema ‘ni bora awe naye mmoja wanayeaminiana kuliko awe na kijiji cha wapenzi.’ Kuna kaya nyingine msichana akitembelewa na rafiki wake wa kiume, mama kama alikuwepo anawaaga kabisa ‘kuweni huru tu watoto wangu, mimi natoka kidogo, kijana wangu jisikie nyumbani baba eee! Wangine huwaasa binti zao kufanya hima wasiwaangushe wazazi wao, yaani wafanye kitu cha ukweli.’ Katika mazingira hayo, maadili yetu yako wapi? Mama anarudi nyumbani anauliza ‘ehee Neema niambie mwanangu mkwilima wangu vitu, jogoo anawika mjini?’
Hapo tumezibiip mimba za ujanani kabla ya ndoa, na tusitegemee muujiza, lazima vema iwepo tu (mimba itiki) kama siyo kwenye tendo la kwanza basi moja wapo kati ya mtakayofanya. Watoto wataambulisha wapenzi wao bila wasi wasi kabisa eti uhuru wa kuhusiana! Ujinga uliogubikwa na giza totoro siku zote utalenga katika matendo kama hayo. Malezi mabaya katika ngazi ya familia, shuleni, na kwenye taasisi mbali mbali yatafungua njia kwa vijana wetu kuogelea katika uhuru wa kimapenzi. Vijana mtateketea huku mnaona. Mimba zitazidi kuwa nyingi kila kukicha. Mila potofu katika familia, mitaa, vijiji vyetu nazo haziko mbali katika kubomoa mahusiano kwa vijana wenzetu. Siku hizi watu hawahangaiki na malezi ya mtoto wa jirani kama ilivyokuwa kale kwamba ‘mtoto wa familia fulani alikuwa mtoto wa jamii.’ Leo mtoto wa familia ni mtoto wa baba na mama wake walio mzaa! Kweli vijana kama nanyi mna mwono huo, mnawadharau walezi, wakubwa wenu nje na wazazi wenu wa kibiolojia, mmepotoea na karibu mnaishia kabisa. SWALI: KAMA MISINGI IMBEBOMOLEWA, MWENYE HAKI ATAFANYA NINI? (Zab. 11:3). Nimetambua kuwa NILIKOSEA, NIMEKOSEA, sasa naamua SITAKOSEA TENA maana…
·       Ubakaji  na ubakwaji
Huyu mnyama aitwaye ‘ubakaji’ naye ni miongoni mwa wanaochangia mimba za kabla ya ndoa. Yeye hajui cha malengo na ndoto za kijana. Ni tinga tinga, bomoa bomoa la ndoto na malengo ya vijana. Na zaidi ya hayo linaweza kumkumba hata mama mkubwa tu. Kuna mimba nyingi tu vijana wenzangu zitokanazo na matatizo ya wanaume kuwabaka wanawake au wasichana. Tendo hili ni la kinyama. Ni dhidi ya utu, ubinadamu. Ewe kijana unaye nisikia hapa leo, nakuomba na nina kusihi sana, usiwe miongoni mwa wabakaji. Hao ni wauaji wa dada/mama wetu. Kubaka kumeacha matatizo mengi sana ya kisaikolojia, kimwili, na kiafya. Kimaisha kwa ujumla kuna vilio vingi vya wenzetu waliobakwa na hali zao kimaisha leo ni mbaya sana hata wale ambao hali zao ni nzuri wakikumbuka tu ‘lakini nilishabakwa mimi,’ wanaumia sana. Tendo hilo linaamsha mateso yote waliyoteswa na kuteseka kwayo tangu siku ya kubakwa. Wengine walijiua! Wengine waliua watoto wao tumboni! Wengine walijifungua kisha wakawatupa wachanga wao! Yote haya chanzo ni wavulana, ni wanaume. Leo, vijana wakiume mnaamua nini mkishalisikia jambo hili? Wasichana mnasemaje kuhusu kaka/baba wafanyao hili? KAULI MBIU YETU…
v Mhusika/ Wahusika
·       Wasichana wenyewe
·       Wavulana walaghai
·       Akina mama wenye malezi mabaya (walezi bora liende)
·       Akina baba ndumila kuwili (fataki)
·       Jamii kulifumbia macho
·       Serikali kukaa kimya au kutokufuatilia kwa nguvu zake zote kesi za namna hii za kuwapa mimba binti wa shule au binti wadogo
·       Wakati mwingine hata walimu mashuleni huwa chanzo (kuna walimu wana wapenda na kuwataka kimapenzi wanafunzi wao-mchungaji anakula kondoo wake mwenyewe)!

v Athari/ hasara za mimba kabla ya wakati (Ndoa)
Katika ukurasa huu, lengo letu siyo tu kutoa hofu kwa vijana wenzetu ila ni kutaka kuonesha kuwa jambo hili halikubaliki, ni hatari, linaleta maafa makubwa kwa mtu mmoja (mhusika), kwetu vijana wenzake na jamii kwa ujumla. Tukisha yaeleza madhara/athari za mimba za kabla ya ndoa, ni imani na mategemeo yetu kuwa HAKUNA KIJANA KATI YETU HAPA NA HATA TUTAKAO KUTANA NAO NA KUWASHIRIKISHA HAYA, ATAKAYEPATA MIMBA KABLA YA NDOA. Lakini hatuachi mwanya wa kutumia kila njia kuliepa hilo ati kwakuwa tumekubaliana hakuna mmoja wetu atafanya hivyo, sasa aje apatikane mmoja au wawili halafu kwa kutuogopa sisi vijana wenzao wa kongamano hili aishie KUTOA MIMBA ili tusimwone. Ndugu, kumbuka kuna anayekuona kila siku “MUNGU PEKE YAKE” na hata hivyo ana uwezo wakutuonesha yaliyofichika. Athari hizo ni nyingi, sisi leo tunakupeni hizi chache na nzito:-
¨   Kuwa mhanga wa dhambi (ulizini ndipo ukapata ujauzito)
Matunda ya uzinzi siyo matamu hata kidogo. Kila tunda la uzinzi ni angamizo kwa ustawi wa maisha ya mtu. Mimba kabla ya ndoa ni tunda moja wapo. Wasichana wengi waliojikita katiaka uzinzi, wameishia kuvuna humo uharibifu. Magonjwa na kuharibikiwa kimaisha ni kati ya matokeo. Na mimba kabla ya ndoa inatokana na uzinzi lakini yenyewe ni halali yaani huyo mtoto siyo haramu. Uzinzi kwanza (dhambi) kisha mimba (matokeo).
¨   Kuathirika kisaikolojia
Mwathirika wa mimba kabla ya ndoa anapatwa na msongo wa mawazo stress. Kila akifikiria anaona kuwa mambo hayaendi na chimbuko analiona katika tendo la kupata mimba. Hata akishindwa jambo fulani yeye fikra zake anazielekeza kwenye huo ujauzito tu. Kisingizio ‘isingekuwa hii mimba, ningefanikisha jambo hili, asingekuwa yule mvulana/baba, ningeweza kuvuka janga hili.’ Mawazo hayo na mengine mengi, hufanyika kwake wimbo wa kila siku na kila mahali. Hata ndoto zake za mchana na usiku huathiriwa na jambo hilo. Anakuwa na tabia ya kuhama hama kimawazo, katika fikra na hata kwenye maneno na utendaji wake. Ama kweli mimba kabla ya ndoa, ni ajira yenye matatizo mengi!
¨   Kuwa mama mtoto (mtoto mama/mama ambaye bado ni mtoto)
Hapa tunamwona mhanga yaani binti mdogo ambaye amebeba hadhi ya kuwa mama mtoto. Lakini umri wake unamweka kwenye kundi la watoto bado, au tuseme msichana bado wa kuwa shuleni kwa mwendo wa kawaida wa maisha. Yeye ni mtoto bado, lakini ana mtoto wa kuzaa yeye siyo mtoto wa dada au mama wake. Ni mtoto mwenye mtoto wa kuzaa! Anahitaji malezi ya wazazi wakati huo huo na yeye anapaswa kulea kichanga chake. Hapo ndipo wengine huchanganyikiwa kabisa. Hebu fikiria, unamkuta binti ana mtoto mdogo aliyembeba na analia kweli kweli pale ushindwapo kuvumilia na kwa huruma unamwambia ‘wewe binti, mpeleke mtoto kwa mama wake akanyonye. Kumbe binti huyo ndiye mama, atajisikiaje? Nawe je, ukigundua kuwa yeye ndiye mama mwenye mtoto, utajionaje? Hili ni tatizo. Mtoto kuwa mzazi, kimawazo bado hajafikia kutatua shida za wazazi, ki uchumi hajajikwamua bado, kijamii pia anaonekana kuwa kioja. Huku ni kuingia kwenye majukumu mazito na yasiyo saizi ya mbebaji maana siyo muda wake. Kweli yasiyo yetu yakiwa yetu mengine huumiza sana.
¨   Kutengwa na familia, ndugu, jamaa na marafiki
Athari hii imejikita kwenye ukweli kwamba, wale wasio pendezwa na tabia chafu namna hiyo, wengine wao hawana mshipa wa uvumilivu. Wakiwa ni wazazi, wanaweza kumfukuza nyumbani binti wao. Wakiwa ndugu, jamaa na marafiki wanaweza kumtenga na kumwacha ajijue mwenyewe. Yaani wanachukizwa na tendo lenyewe pamoja na mtu mwenyewe. Kauli chafu zote huelekezwa kwa binti huyu, ‘tuondolee hapa tumbo lako hilo kama mtu mwenye utapia mlo, loo! Mwanamke kitambi bibieee, peleka huko kitambi chako, wewe si kampani yetu, usitufuate fuate kama nzi best usije ukatutia aibu tukaoneka kama wote wazinzi jinsi ulivyo wewe.’ Hayo na mengine mengi, huwasibu vijana wenzetu. Ewe binti uko tayari kwa hayo? Wewe kijana wa kiume, kuwa mstari wa mbele kusema ‘hutakuwa miongoni mwa walaghai.
¨   Kuachwa na aliyekupatia ujauzito
Nje na kutengwa na familia, ndugu, jamaa na marafiki, kuna adha hii moja kwamba, kwa wale wanaodanganyana kwamba ‘mimi nitakuoa, nizalie mtoto nitamtunza na wewe pia,’ mambo yanapozua mambo (ujauzito ukiingia bila hodi-kabla ya ndoa) kuna kugeukiana na kuonana kama mmoja ni shetani wa mwenzake hasa mvulana au mwanamume. Fikirieni kuwa wote mnasoma halafu mmepata ujauzito, nani yuko tayari kusema ‘tuache shule tukalee mtoto wetu.’ Ni mvulana yupi atakuwa tayari kuukubali ujauzito huo kuwa ni wake? Wengi kama siyo wote wana kataa na hapo binti anabaki mbeba lawama zote kana kwamba alijipatia huo ujauzito yeye peke yake. Wengi wakifika hapo, hukata tamaa na hata kuchukua maamuzi mabaya yaliyo kinyume.
¨   Kukosa nafasi katika masomo na kazini pia
Kuna wasichana wengi walipoteza nafasi zao za masomo kwa kuwa wajawazito wangali shuleni. Wengine walifukuzwa shule. Wengine wazazi wao walikataa kata kata kuwaendeleza kielimu katika ngazi au hatua yoyote. Leo Serikali inapambana kuwapa nafasi tena wasichana kama hao. Sijui faida yake na umuhimu wake maana naogopa isije ikawa kwa upande mwingine wanaacha mwanya kwa vijana kufanya tu mapenzi maana shule ipo tu hata kwa waja wazito. Na wenye watoto. Wengine walimwaga unga maafisini kwa kuwa na ujauzito. Zote hizi ni athari hasi. Na hilo linapotokea  kuteketea kwa ndoto za kijana za maishani huwa ni pai (yaani lazima iwe hivyo).
¨   Kubaki nyuma kimaendeleo
Maendeleo yoyote yana viashiria vya kijitambua na kufanya yaliyo sahihi. Vile vile yana viashiria vya muda uliotumika vema. Kwahiyo, katika masuala ya mimba kabla ya ndoa, hatuwezi kuubeza ukweli kwamba wahusika walishindwa kujitambua wao ni akina nani (mfano, kijana ambaye hajaolewa nk), walishindwa kujua wako wapi (mathalani shuleni nk), walishindwa kutambua kuwa muda wao kwa wakati huo ulikuwa rasmi kwa kuishi maisha ya wale ambao hawajaolewa ‘kutokujihusisha na mapenzi nk.’ Kwa hiyo hawakuutumia muda wao kwa mambo msingi. Mioyo yao ilisukuma vingine siyo damu kama asemavyo MSANII LAMECK DITTO. Akili yao ilipata ajira kwa yasiyo msingi. Miili yao ilitumika kama pango la mapenzi. Katika hali kama hiyo, usitegemee maendeleo ya maana. Utabaki nyuma tu kama kitako cha bunduk, nyuma tu kama kisogo, nyuma tu kama mgongo. Utabaki kuusingizia ujauzito kwa kila anguko lako. Kweli ‘mbaazi ikikauka husingizia jua!’
¨   Kuingia kwenye maamuzi mabaya kwa mwenye mimba
Mambo yote yanaweza kuwa kenda, na kumi ni kufanya maamuzi mabaya. Ubaya wa maamuzi haya ni kwanza kwa mtu binafsi, au kwa aliyempatia ujauzito, waliomdanganya, aliyetumboni mwake (mtoto), anaweza hata kuichukia jamii kwa sababu zake binafsi na kuona kuwa haikutimiza wajibu wake katika kuwafunza vijana maadili. Mbaya zaidi, anaweza kumlaani hata Muumba wake. Chukulia mfano Mzaburi anasema “Kinacho niuma zaidi ni kwamba Mungu hana nguvu tena” (Zab. 77:10). Haya yaweza kuwa mawazo ya binti aliye katika hali hiyo. Sasa naomba niyaainishe hapa bila kusema chochote maana yanajitoshereza:-
ü Kujinyanyapaa mwenyewe (I have no any shadow of value)
ü Kukata tamaa na maisha (Nothing is possible any more for me)
ü Kutoa mimba/kuua (This is the only solution I can opt for)
ü Kutupa watoto waliozaliwa (To hell with it)
ü Kujinyonga/kujiua (It’s better I take a long and deep rest)
ü Kuwachukia wanaume wote na hata kutokuwa tayari kabisa kuolewa maishani (Single life is my vocation in life/I don’t want troubles)

v Suluhisho/ Mwarobaini
Nani sasa Amfunge Paka Kengele?
MIMI, WEWE, HATA NA YULE…
Tumekwishaona maana ya mimba kabla ya wakati (ndoa), chanzo chake, sasa tuangalie namna ya kumfunga paka kengele ili kila asogeapo, tujue kuwa yuaja adui yetu vijana, adui wa ndoto zetu na adui wa uhusiano wetu na Muumba wetu. Njia moja kubwa sana yakusuluhisha tatizo hili ni kuepa na kukaa mbali kabisa na sababu zinazopelekea vijana kuwa na mimba kabla ya wakati (ndoa). Na nyingine ni hizi tunaongezea:-
Ø Kumcha Mungu na kuwa na hofu naye
“Kumcha Mungu ni mwanzo wa hekima” (Mit. 1:7). Vijana wenzangu tukimcha Mungu, tutakuwa wana wema. Tutaishi katika nuru ambayo ni Kristo mwenyewe (Yn. 8:12). Kumcha Mungu ni pamoja na kuzishika amri zake na KUTOKUZINI ni moja wapo ya amri hizo. Usipozini utaondokana na matokeo yake yote mabaya. Utakuwa kijana jasiri na mwenye SUBIRA ivutayo heri. Anza leo. Hujachelewa. Usisubiri kesho. Kumbuka ‘ngoja ngoja yaumiza matumbo.’ 
Ø Kumwomba Mungu Roho Mtakatifu akupatie mapaji yake ili uwe na mang’amuzi sahihi (Isa. 11:2)
Mapaji ya Roho Mtakatifu ni zawadi na silaha zetu za mapambano. Omba upewe hekima, akili, shauri, imara/nguvu, elimu, ibada na uchaji wa Mungu. Ukiwa nayo haya utatenda yote yaliyo mazuri na utajiepusha na yote yaliyo mabaya. Omba pia matunda ya Roho Mtakatifu ambayo ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhila, uaminifu, upole, na kiasi (rej. Gal. 5:22-26) yakusindikize katika kuwa mwanadamu mwema kati ya wanadamu wengine wema na utaufanya ulimwengu uwe mwema pia. Hii ni misaada ya ufuasi katika maisha. Ni kinga dhidi ya dhambi na yote yaliyo mabaya.
Ø Sali daima ili Mungu akupe nguvu ya kwanza kuepa nafasi za dhambi (Lk. 22:40) pili kuishinda dhambi kwa wema na kuikimbia (Yak. 4:7-8)
Sala iliyosaliwa vizuri hufungua mioyo ya wasalio na huifungua mbingu ili aishie huko aisikie maana hupaa mpaka kwake kama moshi wa ubani (reje. Zab. 141:2). Tukimwomba Mungu katika ujana wetu, hatatuacha tuangamie kwa mahusiano mabaya. Kwake hakuna lisilowezekana kwa aombaye kwa imani (Lk. 1:37, 18:1). Kama huwezi kuacha uzinzi, Mungu hajashindwa kukutoa huko mwombe tu. Kama unaona huna nguvu za kujinasua kutoka huko, mwombe tu atakuwezesha. Tuombeni bila kukoma na hata tukipewa tuombeni tu. Tuombeni mpaka kitu kitokee hiki ndicho kirefu cha PUSH [Pray, Until, Something, Happens]. Kijana mwombe Mungu ili nguvu ulizo nazo zitumike vizuri kwa malengo mazuri. Ukiomba utapewa (omba nguvu ya kuepuka au kuacha uzinzi), ukitafuta utapata (tafuta namna ya kukaa mbali na dhambi kutoka kwa Mungu utapata), ukibisha hodi utafunguliwa, (bisha hodi kwa neema za Mungu uushinde uzinzi nawe utaushinda).
Ø Mtukuze Mungu katika mwili wako maana ni Hekalu lake (1Kor. 6:19-20, 2Kor. 6:16)
Miili yetu ni mahekalu ya Roho Mtakatifu. Tuitumieni kumwenzi Muumba wetu. Milango yetu ya fahamu itoe ushirikiano katika kumtukuza Mungu. Tuyaone yaliyo mema, tuyasikie yaliyo mema, tuyashike yaliyo matakatifu, tuyanene yaliyo asili ya wokovu wetu na wa wenzetu. Tukifanya hivyo tutajiweka pembeni ili kuepusha msongamano katika msafara wa wazinzi. Na mimba za kabla ya ndoa zitaisha kabisa kwetu na kwa wenzetu ujumbe utawafikia maana Injili ni kuishi siyo kuhubiri tu kwenye marufaa.
Ø Kushika mafundisho ya Kanisa
Kanisa Katoliki ni mama na mwalimu, tukilifuata tutafikia kule ambako Mungu ametuandalia makao maana lenyewe ni sakramenti ya watu wote wenye kuuhitaji wokovu.[55] Kanisa linakataza kile ambacho Mungu alikataza “USIZINI.” Tulisikilezeni maana halikosei katika kutufundisha sisi wana wa Mungu. Makatazo ya Kanisa ni kwaajili ya wokovu wetu na wa wenzetu.
Ø Elimu bora ya mahusiano
Kanisa na dini mbalimbali zishirikiane kuwaandaa vijana katika maisha ya uadilifu na maisha ya kimahusiano. Vijana watajua nini wafanye wanapotaka kuingia kwenye maisha ya ndoa. Na wafanye nini kabla ya ndoa. Serikali pia iwe na utaratibu mzuri wa kuwaandaa vijana ambao ni taifa la kesho. Mitaala iwe rafiki katika mahusiano siyo kuwapotosha watoto na kuwabomoa kwa mafundisho potofu kama mpango unaoendelea sasa wa kutaka kuruhusu mpango wa uzazi na vidhibiti mimba kwa vijana wa umri miaka 10 hadi 19 na kuendelea.[56] Kwa rejea tusomeni (1Kor. 7:32-33). Kila mmoja wetu leo hii namwomba sana chonde chonde, awe macho na kupinga yote yaliyo kinyume na maadili yetu kama huu mswaada wa kuruhusu mafundisho yenye kuruhusu vijana wadogo kabisa wafundishwe na waanze kutumia vidhibiti mimba chini ya mwavuli wa “SEXUAL REPRODUCTIVE HEALTH AND RIGHTS-SRHR (AFYA YA UZAZI NA HAKI)." Huu ndio mswaada wenyewe. Tukilala leo, tutaamka kesho ukiwa kazini!
Ø Semina na Warsha mbali mbali
Hizi ni nyenzo za kufundishia na kuelimishia. Leo tunatoa semina, lengo ikiwa ni kutoa rai, kutoa dira na kutoa mwelekeo mwema. Tuna imani kuwa haya yatachachusha donge zima la kujikomboa na kuondokana na mahusiano mabaya kati yetu vijana. Matumaini yetu ni kwamba baada ya semina hii, kutakuwa na kumwongokea Kristo kwa vijana wote. Amka kijana, zinduka kijana. Vuna kitu leo kwaajili ya kesho. Tupendeni kuhudhuria semina na warsha mbali mbali na tuwavuteni na wengine wengi wazipende semina ili wanufaike kama ninyi kwa juma hili. Nanyi kaweni chumvi na nuru huko (Mt. 5:13-14), mashuleni, majumbani kwa kutoa semina elekezi. Mkifanya hivyo kwanza kwa kuishi vizuri ninyi na pili kuseminisha, watu watayaona matendo yenu mema na watamtukuza Mungu Baba wa mbinguni. Kumbukeni ‘mmepewa bure, katoeni bure.’ Kumbukeni ‘ninyi si maskini hivyo kwamba hamna cha kutoa kwa vijana wengine.’


Ø Jitambue
Jitambue wewe ni nani na uko wapi, unafanya nini, kwanini, kwa wakati gani, sehemu gani, na kwa njia ipi? Kama wewe ni mwanafunzi, zingatia masomo kwanza, “MAPENZI NA SHULE HAVIPIKIKI CHUNGU KIMOJA” Neno la Mungu linasema “Mshike sana elimu, usimwache aende zake…” (Mit. 4:13). Mambo mengi sana yamefikichika kwenye siri hii ya kujitambua. Nawe itumie uvune matunda mengi katika ujana wako leo. Na utaepa na kukwepa mimba hizo.
Ø Malezi bora nyumbani
Nyumbani ni shule ya kwanza ya malezi na imani. Maadili na staha njema ya kila mtu yanategemewa kutoka nyumbani. Kama ni kuharibikiwa kwa mambo ni huko na kama ni kujenga nyumba bora ya maadili ni huko. Mahusiano mema yajengwe kwenye familia. Msingi bora wa maisha ujengwa huko. Wazazi na kaka/dada wawe mfano wa kuigwa kwa wadogo wao. Sio jambo la kifamilia baba kuleta kimada pale mama atokapo. Au mama kuleta kidume pale baba atokapo. Kwa vyovyote vile hiyo ni sumu wazazi wanayoimwaga mbele ya watoto wao. Watoto wakiulizia jibu ni ‘anti, mjomba.’ Ndiyo maana YAMOTO WALIIMBA UKWELI KABISA JUU YA ANKO JONI. Niseme nisiseme nisieme…semaaaa. Chondo chonde, vijana tuvuneni mema nyumbani hata kama mabaya yanaweza kuwa mengi zaidi. Nanyi mkija kuwa wazazi hapo kesho, kuweni kioo safi.
Ø Ilishe dhamiri yako kwa mafunzo mema, mawazo mema na matendo mema ili ikulinde katika kuenenda vema
Fuata maongozi ya roho zaidi ya yale ya mwili (Rum. 8:8-11). Dhamiri ni mwamuzi mwenye haki akitunzwa ndani ya mahakama safi na salama yaani ‘kupewa taarifa na malezi bora siku zote.’ Dhamiri haiweze kukukana kama utailea vizuri na kuikuza vema. Hii ni sauti ya Mungu ndai yetu. Ni madhabahu yetu ya kutenda matendo makuu na mazuri yenye kumpendeza Mungu na jirani. Dhamiri ndiyo itakuambia “USIFANYE HILI NI BAYA.” Ukiisikiliza utashinda hata vishawishi vya mimba kabla ya ndoa. Ukiipinga haitakulazimisha lakini mara baada tu ya tukio itasikika ikikuambia “UMEFANYA NINI? UMEFANYA VIBAYA! UMETENDA DHAMBI! LAKINI NILIKUARIFU MAPEMA HUKUTAKA KUNITII MIMI! ONA SASA!” Tupendeni kuzisikiliza dhamiri zetu. Dhamiri njema ni usukanai wa maisha.
Ø Kuacha kuiga iga kila kitu/mambo
Kuna mambo mengi sana yanatushawishi kuiga kutoka kwa watu, lakini tuweni na mipaka katika kuiga. Waswahili wanasema “Ukiiga kunya kwa tembo utapasuka msamba.” Kuna vijana wengi wameharibikiwa katika maisha na mahusiano baada ya kuona yafanywayo kwenye filamu na sehemu nyingine. Kutoka huko wanaanza nao kufanya kama walivyoona. Hapo utakuta kubusiana kila waonanapo, kutomasana tomasana kwenye maficho hasa wawapo peke yao tena kwa kuibia. Matendo hayo na mengine mengi, yanawasha moto ambao fukuto lake na joto lake linaweza kufikia kwenye hatima mbaya. Maana ndizi mbivu ukizitomasa zinaweza kudondokea kiganjani, zikifika hapo, mdomo nao utatamani kuzitia gegoni, na hapo kutafuna huwa ni ajira ya muda huo. Angalia sana, ‘safari moja huanzisha nyingine.’ Kama ni nzuri itakupeleka kuzuri na kama siyo nzuri itakupeleka kwingineko.


Ø Kuwa na subira ivutayo heri
Wahenga walisema “Haraka haraka haina baraka, haraka haraka ya mbwa huzaa watoto vipofu.” Vumilia kama una ndoto njema yakuwa baba/mama wa familia kesho. Ishi vema leo ili kesho uwe mume/mke mwema na baba/mama mzuri wa familia. Subira yavuta heri. Kuwa na saburi. Usiyakimbilie mapenzi, ukifanya hivyo utayapata na unaweza ukaovertake kabisa. Lakini ujue ajali utakayoipata siyo ndogo kamwe, ni kifo cha mende. Ukisubiri utafanya mambo yako kitaalam kwa muda mwafaka na kwa utakatifu wa masuala. Subira ni fadhila, ipalilie, ijenge, ilinde ikulinde. Ukiweza kusubiri utakuwa umepiga hatua nzuri sana katika ukombozi wako.
Ø Kuepa mahusiano ya ngono kabla ya ndoa
Epuka, jiepushe na biashara hii ya mapenzi kabla ya ndoa. Muda wa kufanya hivyo utafika utakapo kuwa mume/mke halali wa mwenzi wako. Kwanza mtafurahia maana mtakuwa ndani ya sakramenti. Na sakramenti yoyote ile ina neema iliyowekwa ndani yake na Kristo. Hapo hamtakuwa wazinzi tena bali wapendanao, wanaokula ndoa yao kwa lengo la kukamilishana na hata kupata watoto Mungu akibariki pendo lao au akikusudia hivyo kwa sifa na utukufu wake. Dawa ya moto ni moto, na dawa ya kuepa mimba za janani yaani kabla ya ndoa ni kuepa mahusiano ya kimapenzi kabla ya ndoa. Inawezekana kabisa wala usiwe na mawazo ya wachache waliokosa dira ya maisha ‘eti usipofanya mapenzi, utaugua, utashindwa kuwa mchangamfu, utakuwa zezeta, utashindwa hata ukijakuingia kwenye ndoa.’
Ø Penda kufanya kazi
Jitahidi kauli yako ioane na ya mheshimiwa Rais JPM “HAPA KAZI TU.” Nawe sema “KWANGU KAZI TU MENGI-NO SPACE, NA YA MUHIMU, MUDA UKIFIKA YATAFANYIKA.” Kumbuka wazungu wanasema “An idle mind is the devil’s workshop.” Do you want to be one of them? No please, undo your wish. Wish for good and the good will follow you. Ukipenda kazi utaepuka mawazo machafu, utatenda yaliyo mema. Waza mema, nena mema, tenda mema nayo yatakufuata nyuma yako.
Ø Palilia fadhila za kibinadamu (Busara, Haki, Uhodari/Nguvu, na Kiasi)
Kuwa nazo hizi katika kila jambo. Fanya lililojema. Ulifanyapo lifanye kwa busara, haki, uhodari na kiasi. Ukihitimu katika hili, hata mahusiano yako yatakuwa mazuri yaliyojikita kwenye busara, haki, nguvu na kiasi. Hutofanya jambo lolote bila kipimo tarajiwa, wala hutolifanya kwa kiwango cha chini.
Ø Kubali kukosolewa na wenzako
Unaweza kudhani kuwa uko kwenye njia sawa katika maisha na matendo yako kumbe uko nje ya maadili ya jamii, uko kushoto mwa ukweli. Sikiliza watu, ujitambue, watu ni kioo cha matendo yako, wasikilize wanapokuambia ukweli hata kichaa akisema kitu kwako usikibeze kwasababu yeye ni kichaa, chukua ujumbe. Ukisikiliza ushauri mzuri hutaingia katika maovu tunayoyapigia kampeni za kuyatokomeza hapa leo kwenye semina na kongamano letu.
Ø Soma alama za nyakati (Lk 12:54-56)
Katika hili jifunze kutoka kwa waliao leo. Usije nawe ukaingia kwenye kilio chao kana kwamba hukuwaona wakilia na kana kwamba hukujua kwanini wanalia. Waswahili wanasema “Mwenzako akinyolewa, zako tia maji.’ Sasa wewe kutia kwako maji ni kujihadhari na wanaume au wavulana walaghai. Ukitaka kufanikiwa waliofanikiwa watakupa hamasa juu ya nini ufanye, ufanyeje ili nawe ufanikiwe. Lakini ukitaka kufanikiwa zaidi, jifunze kwa walishindwa. Hao watakufunza viunzi vya kuruka ili usianguke au usijikwae ukaishia walipoishia wao. Habari ya Ngoswe na Mazoe kwenye Kitabu “NGOSWE: PENZI KITOVU CHA UZEMBE,” mimi ilinifunza kuwa mapenzi ni sumu ya kazi zetu. Mazoea alitumbukia katika mapenzi na Ngoswe na hatimaye Ngoswe aliunguza takwimu zote za Sensa. Ukiona vitu kama hivyo, vinakuamsha kutokufanya kama wao. Na ufanyapo kinyume chao, umefanya vizuri na hapo umeruka kiunzi. Kwa upande wa mapenzi kabla ya ndoa, umekwepa mitego ya yote yatokanayo na mapenzi hayo ‘mimba kabla ya ndoa’ ikiwa ni moja kwa kutaja. RUKA KIUNZI, KIJANA, MAKE SUCH A LONG JUMP IN LIFE.
Ø Usidanganyike (Mk 13:5)
Jitahidi kuwa mjanja katika maisha. Epuka kupenda kubembelezwa kwa kila jambo na kila wakati. Wengine walianzia huko kwa kutaka kubembelezwa, wakaishia kuwekwa kwenye mapaja kama Samsoni kwa Delila. Mwisho wake, walienda hatua kubwa zaidi kwa ubaya (mapenzi) na kwa kuwa muda ulikuwa haujafika, waliiharibu kesho yao ambayo ndiyo leo tunayoizungumzia hapa. Sema SIDANGANYIKI. Nawe kijana wa kiume usimdanganye binti wa watu. Mheshimu na heshimu utu na maisha yake. Mnapokuwa mabwenini wasichana kwa wavulana mna mengi sana ya kufanya kuliko kuwaza na kuwaka tamaa za mapenzi tu. Mtaharibu mambo. Na mtaishia kupotea. Kila mmoja aishi kwa adabu njema na hiyo iwe chombo chake cha kusafiria katika maisha, usafi uwe vazi lako. Mchana na usiku mtu asikudanganye.
Ø Usiwe mtumwa wa malimwengu na dunia hii (Rum. 12:2)
Ulimwengu una ajira nyingi sana hii ya mapenzi kabla ya ndoa ni moja wapo, usiutumikie ulimwengu katika ajira hii, mshahara wake ni mimba za utotoni, mshahara wake ni UKIMWI. Mshahara wake ni mauti. Ulimwengu una matamu mengi sana, hili la mapenzi linaweza kuonekana nambari wani, lakini ukishaonja utaona kuwa siyo ukweli kama bado dhamiri yako inasema ‘NDIYO-HAPANA, SAHIHI-SI SAHIHI, VEMA-KOSA, FANYA-USIFANYE, KAMA AMBAVYO SAA HUSIKIKA ‘TIKI, TIKI, TIKI.’


Ø Kujitambua na kutenda mambo msingi kwa muda maalum
Napenda nikupe ushauri huu bure kabisa, Wazungu wanasema “first things first” Jitahidi ufanye yaliyo ya lazima na kwa muda wake. Unaweza ukawa unafanya jambo zuri na takatifu kabisa lakini kama ni nje ya muda unaweza kupoteza lengo. Kumbuka hautabaki msichana siku zote au mvulana siku zote. Ishi vizuri muda huu ungali na nguvu nyingi kesho yaja unaweza ukutwe huna akiba ya matunda mema ya ujanani. Anza leo. Ukichezea ujana wako leo, fainali iko uzeeni, yaani kesho. Cheza vizuri leo ungali kijana. Fanya yaliyo sahihi. Hutajuta fainali ikifika.
Ø Kuwa na msimamo thabiti na simamia maamuzi mazuri na sahihi bila hofu yoyote
Usiposimama kwa lolote utaanguka kwa lolote. Simama katika ‘hapana kwenye masuala ya kipuuzi.’ Na hapana yako iwe ya kweli, siyo hapana nje kumbe ndani unasema ‘ulichelewa wapa kaka/baba?’ nilikungoja kwa shauku, loo! Sasa Mungu anipe nini? Na usisimame kwa miguu ya mwenzako, yeye ni yeye na wewe ni wewe. Usitumie vionjo vyake kuishi maisha yako. Kama anapenda ngono, siyo ufunguo wa maisha yako wewe kuishi kwa kupenda ngono. Amua sasa.
v Ushauri nasaha
“Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, yakumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana” (Rum. 12:1). Naanika ujumbe huu hadharani, kijana mwenzangu mwone kijana mwenzako kuwa dada/kaka kwako. Kwa mkubwa mwone kama mama/baba kwako. Husiana nao vizuri. Usikosee na kuwaona ‘girlfriend/ boyfriend’ ‘mume/ mke.’ Waheshimu katika mtazamo huo. Ukimwona dada/kaka ndani ya kijana mwenzako, hutomkimbilia kwa mapenzi. Utamkimbilia kwa uhusiano mwema. Na kama mmependana kwa lengo la kuoana, taratibu zipo za kikanisa, kijamii, zifuateni na ipo siku mtakuwa mume na mke nje na hapo ni uzinzi. Ni kuvunja amri ya Mungu, ni dhambi. Epa dhambi. Usikimbilie kumwona kijana mwenzako kama WIFE/ HUSBAND MATERIAL wa leo kumbe unataka kumchezea tu.
Urafiki tuujengao utusadie kukua, kujilea, kujitambua na kuhusiana. Kijana mwenzangu jenga urafiki mwema, wenye afya, wenye asili ya Kimungu “Siwaiti tena watumwa, nawaita rafiki maana yote niliyoyasikia kwa Baba yangu nimearifu” (Yn. 15:15). Epa, epuka marafiki wabaya “tufanye tu, mbona hata wengine hufanya, haiui kufanya” marafiki wa namna hii, ni kama kivuli giza likiingia wanatoweka (ukishawatimizia matakwa yao huwaoni tena). Soma neno hili la Mungu (YBS 6:7-17) likusaidie kuchagua marafiki wema na wazuri. Marafiki hao hufurahi wakikuona unaangamia nawe usijikaze huku unateketea (Rej. Mit. 1:10).
Nawaomba vijana wenzangu, kila mmoja awe mlinzi wa mwenzake, kila mmoja awe msaada kwa mwenzake kutenda mema. Kila mmoja awe mwalimu kwa mwenzake ili amfundishe kuwa ‘uhusiano kati ya mtu na mtu siyo kwa njia ya mapenzi tu. Na tujaribuni kuwaonesha wenzetu athari za mahusiano ya mapenzi kabla ya ndoa. Wakizitambua wapo watakaoacha mapenzi kabla ya ndoa na hata wakitokea wakaidi ambao hawafaidi mpaka siku ya idi kama wasemavyo Wahenga, basi kwa upande wa mwalimu, yeye ajue wazi kabisa kuwa amekuwa mtumishi mwema na mwaminifu na ametenda kwa mujibu wa wajibu wake. Hutajuta wala hutasutwa dhamiri kwenda kuungama kwa kutoa elimu hiyo, lakini ukiacha na mwenzako akapotea, sala ya kutubu kipengee cha ‘…kwa kutotimiza wajibu” kikutangulie kusema ‘nimekosa mimi, nimekosa mno...” Vijana wenzangu, tukitaka kufanikiwa katika maisha, tumwigeni Kristo aliye njia, ukweli na uzima (Yn. 14:6), yeye pekee ndiye ufunguo wa maisha yetu tukimfuata yeye tutafanikiwa katika maisha na tutazikomboa nafsi zetu.
Imetokea umechanganya mafaili na mimba imeweka vema (imeingia) ufanye nini?
a)       Usiitoe huyo kwetu wana uhai ni binadamu mwenzetu, ni mali ya Mungu, ni zawadi kutoka kwa Mungu, kwako wewe mzazi ni mtoto, na kwa Mungu ni kiumbe chake alichokijua tangu hujakibeba tumboni mwako (rej., Yer. 1:4) na amemuumba kwa sura na mfano wake kwa malengo maalum (rej., Mwa. 1:26, KKK na. 2002).

b)       Uhai wa hicho ulichokibeba ni bora mara kumi elfu kuliko ujana unaouhofia kuharibika, kuliko masomo unayofikiria kuyakosa, kuliko ajira unayohofia kuimwaga chini, kuliko kampani ya mabesti wako unayoiona iko matatani.


c)        Kumbuka umependelewa kuwa mama mtoto mtarajiwa na baada ya muda wa miezi hiyo kenda tu unakuwa. Umeshirikishwa uumbaji na Muumbaji wa kwanza na mkuu (Mungu Baba). Shirikiana naye akushirikishaye upate neema na heri kama wanawake wengine waliozipata (rejea mama wetu Maria ‘umejaa neema…umebarikiwa…Lk. 1:28, 42).

d)        Mimba siyo ugonjwa wala dhambi, ugonjwa na dhambi ni kuitoa.
Nawapeni nguzo za kuishinda njaa na kiu ya miili yetu. Tuwaigeni watakatifu vijana walioishinda dunia na matamu yake kwa usafi wa moyo. Walibaki mabikira tangu kuzaliwa mpaka kufa kwao. Mfano, mt. Terezia wa mtoto Yesu. Mwenye heri Anuarite, watakatifu akina Anyesi na wengine wengi. Hao watatufunza kuona kuwa inawezekana kuishi kiaminifu bila kuchafua usafi wa moyo. Kama kijana mpaka ninavyoongea hivi unaumia maana umeshatibua mambo yaani kwako wewe kuishi si Kristo bali ni mapenzi, nakubeba kwa upendo mpaka kwa mt. Agustino ambaye kwa maisha yake, hakuna mwanamke aliyekatiza macho yake akampendeza halafu akamwacha aende zake, lakini mwisho wa siku alimwongokea Kristo nakusema “Nimechelewa mno kuutambua uzuri wa tangu kale![57] Na hapo anatambua jambo hili lililogusa kiu ya roho yake “Umetuumba kwaajili yako Bwana, na roho zetu hazitatulia mpaka zitulie kwako.”

Kwa kuwaangalia hawa, tutafuteni majawabu ya maswali haya:
(1)               Nimejiandaaje kwa maisha baada ya maisha? Ninaendelea kujiandaa au najiandaa kwa kinyume chake?
(2)               Kwa namna ninayoishi na jinsi ninavyohusiana ana wenzangu, nikifa leo, mimi ni wa sehemu ipi kati ya mbinguni alikoenda Kristo kunitayarishia makao (Yn. 14:2) au motoni kwa shetani na malaika wake? (Mk. 9:48).
Ukipata jawabu zuri leo, usibweteke nalo nakucharaza maisha kumbuka “ajidhaniaye kuwa amesimama aangalie asianguke” (1 Kor. 10:12). Tujiulizeni maswali hayo kila siku, hata unapoenda kulala, uamkapo, utembeapo njiani jiulize. Hata uendapo kwenye utekelezaji wa appointment zako za kimahusiano kama tulivyoelezwa na msemaji wa kwanza, jiulize maswali haya. Maswali haya yatatusaidia, kuepa nafasi za dhambi zitokanazo na mahusiano mabaya. Maana kuna wakati kila ukimwona msichana/mvulana unamtamani kwa mapenzi. Hayo siyo maisha ya wana wa Mungu ndugu nakwambia.
Ifike mahali ukimwona msichana amepata sifa zote za vionjo vyako, mwonee tamaa na kiu yakumtakia siku moja kwa jinsi anavyoishi aweze kuwa mtawa/sista au ukimwaona mvulana na namna anayoishi, umwazie mema mathalani yeye siku moja kuwa padri wa kazi ya Mungu au mtawa wa kiume. Au hata mama/baba mzuri wa familia yaani kanisa la nyumbani. Na hapo utamheshimu kila mtu na hutomvunjia au kumharibia kesho yake anayoiandaa leo. LET’S BUILD TRANSFORMATIVE SELF DESIRES IN OUR LIVES. SURELY WE SHALL MAKE IT ONE DAY. GET MY WORDS CLEARLY. Ukiwa na tamaa njema yenye kubadili mwelekeo kuutoa kwenye ubaya kuupeleka kwenye uzuri, utakuwa umeanza kuishi maisha ya wana wa Mungu, maisha ya kiadilifu. Na kesho yako itakuwa yakung’ara, na mbingu itakuwa ndiyo mede uitafutayo.
Usukumani tulikuwa tunawimbo kipindi cha kulima, ambao maneno yake kwa Kiswahili ni haya:
Kiatu changu kimetangulia kwa wanawake, binti kiuno, nipe titi ninyonye, nimelogwa, nimelogewa vitu hivi.
Hapa unaweza kuona hamasa na kujitetea kutenda mabaya. Change the mind, transform your desires, transform your thoughts, the way you think affects your today and tomorrow and can affect you to the end of your life whose destiny is a complete loss! What is life if not reaching our Creator?!!
v Hasara
·       Inawezekana kupelekea mauaji (utoaji mimba)
·       Inapelekea mshichana kukosa haki zake za msingi kama msichana (kukatisha masomo yake)
·       Pia inaweza kumpelekea msichana kuathirika kimahusiano, kiafya kutokana na kupata mimba pasina kufikia umri stahiki
·       Familia wakati mwingine zinapata mizigo ya kuanza kulea mtoto aliyepata mimba pamoja na mimba yake (yaani yeye binti na kichanga chake)
·       Pia msichana mwenyewe anaweza kuingia kwenye kishawishi cha kujiua endapo atatengwa na jamii au kuonekana kioja katika jamii
·       Kuacha fundisho baya kwenye jamii (mtoto anakuwa na mtoto)

Nini kifanyike?
§  Lazima kuimarisha elimu ya msingi na sekondari na kuhakikisha wote wanaohusika wanaipata
§  Elimu ya uzazi itolewe kwa wanafunzi wa umri husika kuanzia umri wa miaka 10 n.k.
§  Walimu wa kutoa elimu ya uzazi wathibitishwe kuwa watu wenye maadili mema na wenye weledi na taaluma hiyo
§  Kukumbushia wazazi wajibu wao kwa watoto wao. Kwa njia ya semina na makongamano mbali mbali
§  Kuzuia uhamasishaji wa wazi wazi au kwa njia yoyote ile wa matumizi ya mipira (Kondomu) kwa watu wote
§  Kutambua nafasi ya mafundisho ya dini na kuyazingatia
§  Serikali izingatie kwa kuheshimu mafundisho ya kimaadili ya watu wake mfano ikikatazwa matumizi ya Kondomu. Watu wasiaminishwe na vyombo vya habari juu ya ufanisi wa vifaa hivi
§  Adhabu kali kwa wahusika (anayempa mimba msichana mdogo na msichana aliyepewa mimba kwa hiari)
§  Kuimarisha ulinzi wa watoto mashuleni, nyumbani na kokote waliko watoto wa kike kuepuka mazingira hatarishi hususani ya kubakwa. Mtoto adhaminiwe na kijiji awe mtoto wa wote katika suala la kulindwa na kutunzwa yaani mzazi na jamii kwa pamoja wafike hapa kwa kukiri kuwa “MTOTO WANGU NI MTOTO WA WETU.”
Maoni yangu
*  Mtoto wa kike aheshiwe na alindwe na wote
*  Mtoto wa kike afuate misingi na miiko mizuri ya familia na jamii mfano kutembea usiku au kwenye mazingira hatarishi
*  Akina mama wasichoke kuwafunda wana wao
*  Wavulana wawe na hofu ya kuvunja miiko ya jamii na wawaone wasichana kama dada wao au wadogo wao
*  Akina baba wawe wazazi mchana na usiku siyo kuonekana wazazi mchana na usiku wanavaa vazi la waume wa dada wetu!
*  Kuwepo na mahusiano yenye afya kati ya watu wa jinsia mbili tofauti wasiishi unyumba na kwa misingi ya sheria za sumaku yaani ncha za sumaku zisizo fanana huvutana na zisizo fanana hukwepana.
*  Michezo yenye misingi mibovu kimaadili isipewe nafasi katika makuzi ya watoto (madisko, sinema zenye kuonesha mambo ya utupu, matamasha ya hovyo kama ya wenye PSI na kampeni zao za Kondomu, vidhibiti mimba n.k)
*  Kuwepo na nidhamu ya macho (wahusika hasa wasichana na wavulana watunze usafi wa mioyo yao, waepuke kuangalia picha zenye kuamsha mihemko na hisia za kimwili mathalani kimapenzi)
*  Wasichana na wavulana wajifunze kwa walio haribikiwa kwa kuenda kinyume na misingi bora ya maisha (wasichana wengi waliopata mimba utotoni maisha yao yalisha haribika na leo wanalia ‘nigelijua,’ na wavulana walio wapa uja uzito wengine wako jela wanatumikia miaka yao 30, wengine ndiyo wameanza, wengine wako nusu ya safari, na wengine wana malizia lakini wote hao kwa pamoja wana juta kama ilivyo ‘majuto ni mjukuu,’ hata wao wana lia kila iitwayo leo ‘ningejua’).

·       Tamaa ya Pesa, Mali, Vitu
Waswahili wana msemo ‘Tamaa mbele, mauti nyuma.’ Katika umri wa ujana kuna bahari ivumayo mioyoni mwetu vijana nayo ni bahari ya tamaa ya pesa, mali na vitu vya thamani kubwa. Wengi wetu leo tunatamani, simu nzuri, gari zuri, kompyuta, mavazi mazuri, nyumba nzuri na vitu vingine vingi tu vya namna hiyo. Tamaa hiyo siyo lazima iwe mbaya kama una malengo mazuri ya kufanya kazi ili uje umiliki vitu hivyo. Sasa upande wa pili wa shilingi ndio unaoleta adha. Kama wewe mvulana unamdanganya msichana kwa kutumia vitu hivyo ambavyo vingine huna ukiwa na lengo la kumpata binti wa watu kimapenzi, hapo umekosea ndugu. Na hata ninyi wasichana kama mnaitoa miili yenu kwaajili ya kupata vitu hivyo, kupata alama nzuri darasani, na mengine mengi, wewe pia umekengeuka. Katika kuhadaana huko, ndiko kuna mavuno ya mimba kabla ya wakati na hatima yake hakuna ndoa hapo. Zaidi ya hayo kuna kuwa na kutukanana na kujengeana chuki na vinyongo. ‘Asingekuwa yeye, asingekuwa fulani, nisingekuwa na maisha mabaya namna hii!’ Wengine wanasema ‘ningejua!

5.2.1 Tamaa


Na Frt. Aresius Ngemera mwaka 2015 alikuwa na hiki cha kutueleza katika maada yake juu ya tamaa. Katika Maisha yetu wanadamu, ni mengi tunayokumbana nayo kama sehemu ya maisha yetu haya, mengine yakionekana yenye tija kwetu na mengine tukiyaona kama kikwazo katika kutengeneza maisha ambayo tunaamini Mwenyezi Mungu ametupangia. Vifo, ukame, njaa, vimbunga, magonjwa, na mengine mengi, hutufanya tuhuzunike na wakati mwingine kuwaza kuwa huenda Mungu ametuacha. Katika hali kama hiyo, tunaweza kuchukua hatua mbalimbali kutokana na hitaji la kila mtu, hatua ambazo zinaweza kuleteleza matendo yaliyo mema na pengine yaliyo mabaya. Mojawapo ya tunayoweza kuyafanya kutokana na hali hiyo ni Tamaa ya mali. TAMAA YA MALI NI NINI? Inafanyaje kazi ndani ya mwanadamu na ina matokeo yapi? Haya ni baaadhi ya maswali ambayo tunalenga kuyajibu katika makala hii, tushirikiane kwa pamoja tuone ni lipi twaweza kufahamu juu ya tamaa ya mali.

Ukiamka asubuhi ukaanza safari yako kuelekea katika kituo chako cha majukumu yako ya siku, ni wazi utapishana na watu wengine wenye safari kama hiyo ya kwako. Kadhalika utaona vitu vingi ambavyo, kati ya hivyo waweza kuona vinavyovuta hisia zako. Ni kawaida yetu wanadamu kujikuta unaiambia nafsi yako kwamba ‘nguo ile ni nzuri’ ‘huyu ana gari zuri’ ‘kile kiatu kinafaa kwa mwanangu’ ‘yule dada anapendeza machoni’ na mengine kama hayo ambapo bila kijishauri, utajikuta unajisemea tena moyoni kwamba ‘ningekuwa na pesa ningenunua ile nguo’ ‘nitatafuta pesa nimnunulie mwanangu hicho kiatu.’ ‘Yule dada angepita karibu ningemsemesha walau’ na mengine kama hayo kulingana na kile unachokiona. Tendo unalofanya mpaka wakati huu ni kujaribu kuieleza nafsi yako hisia zako kutokana na msukumo unaoupata kutoka katika uhusiano wa uliyoyaona na unayoyahitaji.
Huu msukumo ndio twaweza kuuita Tamaa kwa maneno mengine. “Nilipoona vazi moja zuri kutoka shinari kati ya nyara, shekel mia mbili za fedha na mchi wa dhahabu wenye uzito wa shekel hamsini, nikavitamani na kuvichukua, nimevificha ardhini ndani ya hema langu, na fedha iko chini ya vitu hivyo” (Yoshua 7:21).
Tamaa ni nini basi? Katika makala yake Apolinary Macha, anatwambia kwamba tamaa ni hali ya uhitaji wa kitu fulani kiasi kwamba mhitaji anaamini kwamba upatikanaji wa kitu hicho ndio upatikanaji wa furaha yake. Macha anaendelea kutuambia kwamba, unapopata ulichotamani kimoja, ghafla, uhitaji wa kitu kingine cha namna hiyo ama tofauti na hicho unakujia. Bila kuchelewa unaanza safari ya kuikamilisha tamaa hiyo kwa kukitafuta kitu hicho kadiri ya uwezo. Safari hiyo huendelea mpaka mwisho wa maisha ya mwanadamu kwani kila siku kuna kitu kipya cha kutamani. Tamaa kwa maana hiyo, haina mwisho kwani pamoja na mengine, haitupatii furaha ya kudumu. (rej. 1Yoh. 2:15-17).  Tamaa hutoka moyoni ingawa ukamilisho wake hutegemea sana utendaji wa milango ya fahamu. Na kila mwanadamu awaye yote hupatwa na tamaa (rej. Yer. 6:13). “Basi nasema: Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tama za mwili. Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka.”[58]


5.2.2 Mali


Yawezekana kuwepo namna nyingi za kuelezea maana ya mali, lakini sisi tutajikita katika kuelezea ile isemayo kuwa, mali ni kitu chochote kinachomilikiwa. Umiliki katika maana hii, unaweza kumanisha mamlaka ya mtu ama kikundi cha watu kama vile familia, ukoo, kijiji, mkoa, nchi na mengine mengi juu ya mali husika. Mali katika muktadha huu, inajikita hasa katika kumanisha kitu kinachoonekana na kitu chochote anachomiliki mtu ni mali yake.
Ø Tamaa ya Mali
Baada ya kuona maana ya tamaa na maana ya mali, twaweza sasa kujaribu kuangalia nini hasa maana ya tamaa ya mali ambalo ndo suala msingi katika mjadala wetu. Bila shaka tayari tuna dhana kuwa tamaa ni hali ya kuhitaji kumiliki kitu, na mali ni kitu chochote kinachomilikiwa na mtu. Hivyo tamaa ya mali yaweza kumanisha hitaji alilonalo mtu juu ya kitu kingine ambacho kwa wakati huo si mali yake.
Wahanga wa hali hii ya kuhitaji kumiliki mali ni watu wote ambao kutokana na mahitaji ya wakati hawajafanikiwa kuwa kitu hicho wanachokitamani, ama walichonacho hakikidhi mahitaji yao. Hali hii ya uhitaji, yaani tamaa ya mali yaweza kuendelea kwa kitu kilekile ama kitu kingine kutokana na uhitaji wa mhusika ili aweze kutimiza ile furaha yake.
§  Mgawanyo wa tamaa ya Mali
Katika upana wake, tamaa inaweza kugawanyika katika vipengele ama aina mbalimbali, japo zinaweza kuwa na uingiliano wa nama fulani. Kuna tamaa ya madaraka, tamaa ya uzima wa milele, tamaa ya kazi nzuri, tamaa ya mali, na nyinginezo. Katika mjadala wetu, tunaongelea tamaa ya mali ambayo kama sehemu ya tamaa, nayo inaweza kugawanyika katika mchanganuo wa aina mbili ambazo ni Tamaa nzuri ya mali na Tamaa mbaya ya mali. Magawanyo huu unaletwa na kile tunachokiita lengo la tamaa husika.
ü Tamaa nzuri ya Mali
Hii ni hali ambayo mtu hutamani kumiliki kitu kwa ajili ya matumizi mazuri kwake na kwa jamii inayomzunguka, na mtu huyo hutumia njia ama mbinu njema kukipata kitu hicho. Hapa tunaangalia ni kitu gani mtu anatamani na ni kwa sababu gani anakitamani, baadaye tunachunguza  uwezekano wa yeye kukipata kwa namna iliyo halali. Mfano, anayetamani kupata fedha ili anunue nguo ama ajenge nyumba na anatafuta pesa hiyo kwa njia ya kujishughulisha na kilimo anakuwa anatekeleza tamaa nzuri ya mali.
ü Tamaa mbaya ya Mali
Hii ni hali ambayo mtu hutamani kumiliki kitu, si kwa sababu ya nia nzuri ya matumizi bali kwa sababu ndugu yake ama jirani yake anacho nayeye hana. Katika hali kama hii, mtamani husika huwaza katika kuhakikisha anapata kile alichonuia ama kikubwa zaidi ya kile, kwa nia ya kumkomoa ama kumtambia mtangulizi wake. Njia za kupata ama kukidhi tamaa hii ya mali, zaweza zisiwe njema kwani, mhusika yuko tayari kutumia njia yoyote ile ilimradi atimize ama apate anachotaka. Hii yaweza kupelekea mtu mmoja kumkanyaga kanyaga mwenzake ili tu aweze kupata kile anachokitamani. Ndiyo maana mtu mmoja aliwahi kusema “Kama kusali kwako kwa kupiga magoti ni kumkanyaga mwenzako, bora uache tu.” Kama nia yako ya kupata mali inakupelekea kumuua ndugu wetu mlemavu wa ngozi, ni vema akaghairi mwenendo wako mbaya upate kulinda uhai wa mwenzako na wako pia, ni bora kuwa maskini wa mali kuliko kuwa tajiri kwa njia ya kumuua mwenzako. Hali hii yaweza kuambatana na wizi, mauaji ama mafarakano baina ya washusika. Hii tamaa ina mizizi yake katika kutoridhika na kile mtu alichonacho. Hizi tamaa zote hutokana na nini?

5.2.3 Sababu za Tamaa


Katika nafasi ya mtu mmoja mmoja, tamaa yaweza kuelezwa kuwa na visababishi vya kutosha, kwani ni mara chache tamaa ya huyu ikawa sawa na tamaa ya yule, hususani katika masuala ya lengo la tamaa hiyo. Hapa kuna baaadhi tu ya mambo yanayoweza kuwa miongoni mwa visababishi vya tama:-
¨   Hitaji la kibinadamu
Hapa tunaongelea ile hali ya uhitaji wa vitu ambayo kila mwanadamu anayo kutokana na mazingira yake. Ni hali ya kawaida mwanadamu kuhitaji chakula kizuri, malazi mazuri, mavazi mazuri na kila kitu ambacho kwacho anapata furaha anayoihitaji. Hali hii tunaweza kuiweka katika kipengele cha matendo ya binadamu ambayo anayafanya pasipo hiari na hivyo katika shughuli zake za kila siku anajitahidi kupigana ili ayapate kwa manufaa ya maisha yake ya hapa duniani.

¨   Ufahari
Hii ni hali ambapo mtu ana kiasi fulani cha mali kama milki yake lakini hajaridhika na kiwango hicho cha mali alichonacho. Katika hali ya kutoridhika, mtu huyo anaamini kuwa bado ana uwezo wa kupata mali zaidi ya ile aliyonayo na hivyo akaweza kujipatia sifa ya utajiri kutoka kwa jamii inayomzunguka. Mtu huyo atafanya kila jitihada ili aweze kupata mali nyingi zaidi akiamini atapata ufahari anaoutamani (rej. Lk. 12:16-20).
¨   Matabaka/ Utofauti katika umiliki wa Mali
Hapa tunazingatia kigezo kwamba binadamu tunatofautiana katika kiwango cha mali tunazomiliki. Kuna wenye mali nyingi na wengine kidogo, wengine wana mali bora kuliko za wengine, na wengine hawana kabisa kile wanachohitaji kama mali zao kutokana na uwezo mdogo, lakini wote tunajikuta katika mazingira ya aina moja. Katika mazingira haya, yule ambaye anajiona hana kile anachohitaji wakati anakiona kwa jirani mwenye vingi zaidi, atashawishika kufanya jitihada ili naye aweze kupata mali kama hizo au hata zaidi yake. Huku ni kujifunza kwa waliofanikiwa kupiga hatua katika maisha. Ni hali ya kuiga yaliyo mazuri na yafaayo kuigwa kwa maendeleo ya mtu binafsi na jamii nzima.
¨   Tofauti katika ubora wa Mali
Hii inaendana kwa kiasi fulani na ile ya matabaka, katika mazingira kwamba, mwenye uwezo mkubwa hutafuta kitu chenye ubora mkubwa wakati mwenye uwezo mdogo ananunua kile kinacholingana na uwezo wake; kila mbuzi hula kwa kadiri ya urefu wa kamba yake. Tofauti hizi huamsha hali  ya kawaida ya binadamu ya kuhitaji kilicho bora kwa matumizi yake. Yule mwenye kitu chenye ubora mdogo atapigana kuhakikisha anapata hicho chenye ubora zaidi kadhalika na mwenye bora anatafuta kilicho bora zaidi na hivyo tamaa inaanza kupaliliwa. Hii ni tamaa ambayo ni matokeo ya kuwa na kitu na kutamani kuwa nacho zaidi na zaidi (kwa wingi wake au ubora wake). Wana uchumi husema “Jinsi unavyokuwa na mali nyingi ndivyo unavyotamani kuwa nazo nyingi zaidi, na hata namna ya kuzipata hukua na fursa pia huongezeka.” Ingekuwa ni kuliangalia suala hii kwa jicho la Kibiblia tungeweza kusema pasina wasi wasi kuwa “Aliye nacho ataongezewa, na yule ambaye hana, hata kile alicho nacho atanyang’anywa.”

5.2.4 Faida za Tamaa


Katika lenyewe, neno tamaa halina ubaya ndani yake isipokuwa tu pale mtu anapokuwa ametumia tamaa hiyo kutekeleza yaliyo mabaya. Kutamani kitu ambacho kwa hatua halali unaweza kukimiliki ni hatua mojawapo katika kufanya jitihada binafsi za kimaendeleo. Hakuna maendeleo ya kweli bila tamaa maana hata kuendelea huja mara baada ya kuwa na tamaa ya kupata maendeleo. Hii ikikosekana, hakuna ndoto ya kumwezesha mtu kupiga hatua ya mafanikio. Hata kama angepata mchawi wa maendeleo, bado angejikuta anaogelea kwenye dimbwi lenye sumu kali ya mchawi wa kutokusonga mbele kimaendeleo. Atabaki anachapa miguu pale pale tu (mbele haendi wala nyuma harudi).
Hali hii katika maendeleo ni mbaya sana maana inaua matumaini ya kimaendeleo. Inavunja moyo wa kuyatafuta maendeleo. Inaifunika imani ya kuendelea kwenye dimbwi la kuridhika na hali iliyopo kitu ambacho ni sumu na inaua hata kama itaonekana kuwa ni kwa mwendo wa kobe maana Wahenga walishasema “Pole pole ya kobe humfikisha mbali.”  Hii ni tofauti na kutamani mali ya mtu mwingine ambayo hata Maandiko Matakatifu katika kitabu cha Kutoka 20:17, yanazuia.
Unaposhuhudia maendeleo ama mafanikio ya jirani yako, nia ya kufanya vivyo hivyo (ambayo ndiyo tamaa) inakujia na kukutia nguvu na hamasa ya kuhangaika ili kufikia hatua ya mwenzako na pengine zaidi. Hili ni zao zuri la uwepo wa hali ya kutamani maishani mwetu. Bila hii aina ya tamaa dunia isingekuwa imefikia ubunifu, udadisi, na mafanikio yaliyopo leo. Na hata kwenye jamii zetu mambo yangebaki kama yalivyokuwa enzi za zama za kwanza/za kale za mawe au hata kabla yake! Lakini kila iitwapo leo, watu wanapiga hatua mbele. Aliyeanza na simu ya tochi, leo anatamani au amesha nunua simu ya tachi au almaarufu smart phone.
Aliyekuwa na baiskeli mwaka jana, leo ana ndoto ya kununu bodaboda maana mtaani alimo wanaume wenzake karibu wote wana bodaboda na akiaangalia kuwa wengine aliwazidi kiuwezo, hapo ndipo anatamani hata kuleta pikipiki kadhaa au kilav4 chake. Aliyekuwa na mtaji wa laki tano (500,000/=) leo hii anapigia kuongeza mtaji wake ufikie Milioni moja (M1) kama jirani yake au hata zaidi. Staili hii ya tamaa ni ile inayofuata kaulimbiu ya “KAMA.” Mfano “KAMA WENGINE WAMEWEZA KWANINI MIMI NISIWEZE? KAMA YEYE AMEWEZA NA TULIKUWA SAWIA NAYE, KWANINI MIMI NISIWEZE?” Msanii aliyekuwa na nyimbo chache chini ya album, leo ana ndoto ya kuzindua album yake. Na kweli watu wamefika mbali kwa tamaa kama hii. Hata baadhi ya waandishi mashuhuri leo walianza na tamaa ya kuandika kama waandishi fulani fulani kama akina William Shakespeare, Eric Shigongo, Mhe. Pd Titus Amigu, Mhe. Pd Dk Faustine Mwikila Kamugisha kutaja japo wachache.

5.2.5 Hasara za Tamaa


Licha ya mazuri mengi tunayoweza kuyapata kutokana na kutamani, maelekeo mengi ya tamaa zetu ni katika hasara. Pengine hii ni kwa sababu ya malengo tunayokuwa nayo, ama mbinu tunazotumia kukidhi haja hizo. Tujaribu kupitia baadhi ya hasara zitokanazo na tamaa.
Ø Tamaa huondoa hofu ya Mungu
Hali hii inajitokeza pale ambapo mtu hutenda mambo yatokanayo na tamaa yake, yaliyo kinyume na mapenzi ya Mungu. Nabii Ezekiel katika Maandiko matakatifu anasema “Ndani yako wamepokea rushwa ili kumwaga damu, umepokea riba na faida, nawe kwa uchoyo umepata mapato kwa kuwadhulumu jirani zako nawe umenisahau mimi, asema Bwana Mungu” (22:12). Tunapo endekeza tamaa zetu, hatuna namna ambapo tutaepuka kutoutii uwepo wa Mungu maishani mwetu.
Ø Mauaji
Nabii Yeremia Katika Maandiko matakatifu anasema “Bali macho yako na moyo wako hauna utakalo ila kutamani, na kumwaga damu isiyo na hatia na kudhulumu na kutenda jeuri (22:17).” Tamaa ya mali inaweza kutushawishi hata kuondoa uhai wa mtu asiye na hatia, hasa pale ambapo tamaa zetu zinazidi uwezo wetu wa kufikiria; pale ambapo mafanikio ya mwenzako yanaonekana ni kikwazo kwako. Suluhisho pekee katika hali hii laweza kuwa ni kuondoa uhai wa watu wasio na hatia. Hapa ndipo usahihi wa kauli hii hujidhihirisha ‘akili na utashi wa mtu unagubikwa na tamaa ya mali, anaona lolote linalomwezesha kufika anakotaka ni jema na analifanya kwa haraka na kwa wepesi!’
Ø Wizi
Tamaa inapozidi na kutaka kutekelezeka katika namna ya haraka, mwenye kutamani anaweza kujikuta hana namna nyingine ya kupata mali hiyo anayoitamani ispokuwa kwa wizi. Kuiba ni uvunjifu wa  Amri za Mungu (rej. Kut. 20:15) na pia ni ukiukaji wa sheria za nchi zinamzozuia mtu kumnyima mwingine haki yake ya kuishi.
Ø Malumbano
Nabii Isaya anasema “Kwa sababu ya uovu wa kutamani kwake, naliona hasira nikampiga, nalificha uso wangu nikaona ghadhabu, naye akaendelea kwa ukaidi kuifuata njia ya moyo wake mwenyewe (57:17)”. Pia Nabii Mika anasema “Nao hutamani mashamba na kuyashika, na nyumba pia, nao huzichukua, nao humwonea mtu na nyumba yake, naam, mtu na urithi wake (2:2).” Mtume Yakobo naye anasema “Vita vyatoka wapi na mapigano yaliyoko kati yenu yatoka wapi? Si humu katika tamaa zenu zifanyazo vita katika viungo vyenu?... (4:1-5)”. Aya zote hizi kutoka katika Maandiko matakatifu zinaonesha ni kwa namna gani tamaa huleta malumbano na mafarakano baina yetu sisi wanadamu. Tamaa inatutenganisha mtu na mtu, ndugu na ndugu. Ni kwa tamaa mbaya ya mali namna hiyo Yuda Iskariote alimsaliti Bwana wake! Nasi leo ni akina Yuda Iskariote kwa kusaliti utu wa wenzetu, haki za wenzetu, mali za wenzetu na mambo mengi kinyume na taratibu za Kikanisa na Kiserikali. Tumejeruhi mara mia zaidi kuliko kuponya kwa silaha yetu ya tamaa. Tumeiruhusu tamaa iwe risasi yetu ndani ya bunduki yetu (akili na utashi) na hivyo kuitumia si kwa kuua wanyama, bali binadamu wenzetu!
Ø Dharau
Mwenye tamaa ya mali huambatana na majivuno na kupenda sifa za kila wakati. Mtu mwenye tamaa ya aina hii hupenda watu watambue uwepo wake katika jamii kwani anaamini mali alizo nazo ndio utajiri wa kuweza kumtiisha kila awaye chini yake. Mzaburi anasema “Maana mdhalimu hujisifia tamaa ya nafsi yake, na mwenye choyo humkataa Bwana na kumdharau” (Zab. 10:3). Tamaa ya mali inaweza kutufanya tuwaone wengine si kitu kwetu na mbaya zaidi kusahau uwepo wa Mungu katika maisha yetu. Tamaa ya mali hutufanya tuwaone wenzetu kuwa ni chombo, ni daraja la kufikia mahitaji yetu. Hiyo tamaa hutufanya tusiione thamani ya wenzetu katika maisha yetu. Hutupofusha na kutuacha maskini wa pendo la Mungu linalotualika kumpenda na jirani wetu kama tunavyojipenda sisi wenyewe.

5.2.6 Suluhisho juu ya Tamaa


Katika ufupi wake, mpaka sasa tumeona ni kwa jinsi gani tamaa ya mali ama kutamani kwa ujumla kunavyoweza kuvunja amani yetu wanadamu, hasa kama watu wanaoishi kwenye jamii moja na watu wa Baba mmoja, Baba yetu wa mbinguni. Hivyo hatuna budi kujiepusha na tamaa zetu mbaya za mali. Luka katika Injili anasema “Angalieni, jihadharini na choyo maana uzima wa mtu haumo katika wingi wa vitu alivyonavyo” (12:15). Yafuatayo ni baadhi ya mambo tunayoweza kuzingatia ili kuepuka tamaa mbaya ya mali:-
·       Upendo kwa Watu Wote
Upendo ni silaha kubwa sana tuliyonayo sisi wanadamu, inayotusaidia kutambua uwepo wa Mungu maishani mwetu na katika maisha ya jirani zetu. Amri za Mungu zinatuhimiza kupendana. (tazama Lk 10:27; Rum. 13:8-10). Tukipendana hatutafarakana kwa sababu ya tamaa ya mali. Mtume Paulo kwa Warumi anaseka kuwa; “Tumtegemee Mungu na tuachane na kupenda tamaa za dunia (13:14). Tukifanya hivi tutakuwa tunatengeneza jamii yenye furaha na upendo, yenye ushirikiano hata katika shida zetu. Hebu tuimbe kwa pamoja wimbo huu mzuri na wenye ujumbe mzuri pia:
Kiitikio
Tukipenda wenzetu, Kati yetu Mungu yupo X2
1.       Aliyetufanya tuwe ndugu, Ndiye Yesu ndugu yetu, Chuki yote na hasira, Kati yetu ziondoke.
2.       Tukipenda Mungu wetu kweli, Tuanzie na nduguze, Audhiye mmoja wao, Mapendoye si ya kweli.
3.       Tuwe moyo mmoja, roho moja, Tuwe pia kundi moja, Tupendane kama vile Yesu alivyotupenda.
4.       Furahini nyote, binadamu, Mwimbieni Mungu wetu, Amri yake ni nyepesi, Neno lake: kupendana.
5.       Kati ya ugomvi na fitina, Na katika kasirani, Mungu wetu hapapendi, Mungu wetu wa amani.
6.       Yesu Kiongozi wetu mwema, Amri yako twaijua, Washa nyoyo za Wakristu, Wapendane siku zote.[59]
·       Kuutafuta Ufalme wa Mungu
Mtume Paulo kwa Wakorintho anasema; “Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike, waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala wazinzi, wala walawiti, wala mashoga, wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang`anyi” (1Kor. 6:9-10).
Tena, Mtume Paulo anawaambia Warumi kwamba; “Dhambi isitawale ndani ya miili yenu ipatikanayo na mauti, hata mkazitii tamaa zake” (6:12). Waraka wa pili wa Mtume Petro kwa watu wote umeandikwa kuwa “Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani, ili kwamba kwa hizo tupate kuwa washirika wa Umungu, tukiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa” (1:4). Mwinjili Luka anatupa kilele cha haya mawazo yote kuwa tuutafute kwanza ufalme wa mbingu na mengine tutapata kwa ziada (12:31 soma pia Tito 2:12-13).
·       Kuridhika na kidogo tulichonacho
Kuridhika ni tabia tunayopaswa kuijenga sisi wanadamu, licha ya uhitaji wowote tunaoweza kuwa nao. Waraka kwa Waebrania unatuambia kuwa; “Msiwe na tabia ya kupenda fedha, muwe radhi na vitu mlivyonavyo, kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, sitakupungukia kabisa wala sitakuacha kabisa” (13:5). Tena katika waraka wa pili wa Mtume Petro kwa watu wote imeandikwa; “Kwa hiyo vifungeni viuno vya nia zenu na kuwa na kiasi, mkiitumainia kwa utimilifu ile neema mtakayoletewa katika ufunuo wake Yesu Kristo. Kama watoto wa kutii, msijifananishe na tamaa zenu za kwanza za ujinga wenu (1:13-14)”. Kana kwamba nataka kumuua mbu kwa kutumia greda! Yohane Mbatizaji pia alipofuatwa na makundi yale matatu ya waliohitaji msaada wake kwa kumwuliza “TUFANYE NINI?” yaani (watu wote, watoza ushuru na maaskari) aliwaambia watu, watoza ushuru, na maaskari kila mmoja “mwenye kanzu mbili ampe asiye na kanzu, mtu yeyote mwenye chakula ampe yeye asiye na chakula, msitoze zaidi ya kilichopangwa, msiwatishie watu, msiwakaripie watu, ridhikeni na mishahara yenu (rej. Lk 3: 7-14)”. Tukumbushane ule wimbo wa Msanii wa kizazi kipya anayesema mahali fulani kwenye wimbowe:
Tukipata twashukuru,
Tukikosa twalala.
Anachotufunza kijana huyu ni kuridhika na kidogo cha halali ulicho nacho. Pili, kuwa na shukrani kwa Mungu mpaji wa vyote, kidogo au kikubwa tumevipata toka kwa Mungu, tushukuru basi kabla hatujayakausha mema yote kwa kuwa na moyo uso shukrani.
Na Mzaburi ana haya ya kutuambia:
Sikilizeni jambo hili enyi watu wote, tegeni masikio enyi wakazi wote wa dunia; sikilizeni nyote wakubwa kwa wadogo, watu matajiri na fukara. Maneno yangu yatakuwa mazitomazito, nami nitasema maneno ya hekima…Watu waovu hutegemea mali zao, hujisifia wingi wa utajiri wao. Lakini mwanadamu hawezi kamwe kujikomboa mwenyewe; hawezi kumlipa Mungu bei ya maisha yake, maana fidia ya maisha ni kubwa mno. Hawezi kutoa kitu chochote kinachotosha, kimwezeshe aendelee kuishi daima, asipate kuonja kaburi. Yeye afahamu kuwa hata wenye hekima hufa, wapumbavu kadhalika na watu wajinga. Wote hao huwaachia wengine mali zao. Makaburi ni makao yao hata milele; ni makao yao vizazi hata vizazi, ingawa hapo awali walimiliki ardhi. Binadamu hatadumu katika fahari yake, atakufa tu kama mnyama. Hayo ndiyo yawapatao wanaojiamini kipumbavu, ndio mwisho wa wale wanaojivunia mali zao... Usihangaike ukiona mtu anatajirika, wala mali yake ikiongezeka zaidi na zaidi, maana atakapokufa hatachukua chochote, mali yake haitashuka huko chini pamoja naye. Ajapojikuza katika maisha haya, na kusifiwa kwa sababu ya kufanikiwa, atajiunga na wazee waliomtangulia kufa, ambao hawawezi tena kuona mwanga. Binadamu hatadumu milele katika fahari yake, atakufa tu kama mnyama (Rej. Zab. 49).

5.2.7  Ndoa za Utotoni


Lakini pia tukumbuke kuwa uovu huo tumeuendekeza sisi wenyewe kwanza kwa kukimbilia familia bila malezi. Fikiria vijana ambao wameoana katika umri mdogo, hivyo hata watoto watakaozaliwa watalelewa kitoto-kitoto. Kwa kuwa wanasema kukua ni kuona mengi, kwao hawajaona mengi ni dhahili; hata namna ya kujiweka katika maisha hawaitambui vizuri, zaidi utawasikia wakizungumzia kula bata tu (they do not have exposure to life).
Tunapokuwa na mimba za utotoni tunategemea pia kuna ndoa za utotoni pia katika maisha ya baadhi ya jamii. Kwa kuungana na Frt. Ludovick Frimi mwaka 2015, juu ya ndoa za utotoni alikuwa na haya ya kutueleza:-
Maana ya Ndoa ni makubaliano ya hiari baina ya mwanamume na mwanamke. Na haya makubaliano yasiwe ni kwasababu fulani fulani bali yawe yametoka kwao wenyewe. Ndoa za utotoni ni ndoa zinazofungwa bila makubaliano baina yao (vijana) wenyewe bali ni kwasababu mbalimbali kama vile kulazimishwa na wazazi, walezi nk. Wakati mwingine pia wahusika wanaweza kushawishiana wao wenyewe kwasababu ya kufuata mkumbo mfano, wenzao waliosoma nao wameoa na kuolewa. Kwasababu ya umaskini au kwasababu ya ujinga wa wazazi au walezi wenyewe. Ni ndoa zinazofungwa huku wahusika wakiwa chini ya umri wa kuoa au kuolewa. Wakiwa bado hawaja fikia umri wa kuwa baba au mama wa familia.

5.2.7.1 Sababu zinazopelekea Ndoa za utotoni     


Kuna sababu lukuki. Tuone japo chache:-
¨   Ujinga
¨   Umaskini
¨   Mila potofu
¨   Tamaduni za ukandamizaji
¨   Wafuata mkumbo (kutaka kutambulika katika jamii kwamba na wao wamo)
¨   Imani potofu mfano, ‘kuozesha binti mdogo kuna faida kubwa maana ana mvuto mkubwa kwa wanaume wengi wenye nia ya kuoa’
¨   Mategemeo makubwa mno ya kimapato (kuozesha binti mdogo kuna fungua mlango wa mafanikio na utajiri-ng’ombe au mahari wengi watatolewa)

5.2.7.2 Washiriki

¨   Wazazi
¨   Walezi
¨   Ndugu
¨   Jamaa
¨   Jamii
¨   Watoto wenyewe

5.2.7.3 Hasara


Hasara ni nyingi mno hata zisipo tajwa hapa zinajulikana. Lakini kwa uchache kabisa tutaje hizi hapa:-
¨   Kuvunjika kwa ndoa hizo mapema kabisa
¨   Kupata matatizo kwenye kipindi cha uja uzito na kujifungua
¨   Kuwa na familia za watoto wenye watoto wenzao
¨   Kumkosesha haki zake msingi kama elimu
¨   Mateso mengi kwenye ndoa hizo (hasa pale wanapo gundua kuwa waliingia kwenye maisha hayo wangali bado)
¨   Kutokujua masharti ya ndoa na miiko ya ndoa
¨   Kuonekana kama waigizaji tu kwa kufanya mambo ndivyo sivyo (mambo mengi ya ndoa yana kuwa hayajulikani kwao)

5.2.7.4 Dawa ya tatizo


Tusaidiane kuzibaini japo chache ili tutibu ugonjwa huu hatari kwa Taifa letu (vijana wetu):-
¨   Elimu itolewe juu ya ndoa za utotoni na matatizo yake
¨   Kuwasaidia wazazi namna ya kuondokana na umaskini kwa njia nyingine nje na hiyo ya kuwaoza watoto wadogo
¨   Kuacha mila potofu
¨   Vijana wenyewe wafike mahali hasa wale wa kike waseme ‘hapana, mimi bado, muda ukifika nitaolewa’ hata wale wa kiume kuna wanao lazimishwa na wazazi wao kuoa ili nao wajitegemee. Ngoja nikupe mfano mmoja yaliyo jiri kwenye familia moja Usukumani:
Baba: Ng’wanone ihaha wakulile ‘tolaga lulu nang’ho wizugile nose ukukilanija’ (mwanangu sasa umekuwa mkubwa, oa sasa nawe upate jiko mwishowe utapitiliza)
Kijana: Sawa baba. Lakini unkima nakumpandikila hali? (sawa baba. Lakini nitampata wapi mwanamke)
Baba: Uyukayelayela ng’wanone ukumpandika nunene umayu wako nakampandika chene (uwe unatembea tembea mwanangu utampata tu hata mimi nilimpata mama wako hivyo)
Kijana: Sawa baba intondo nakwandya kuchobha nane napandike ng’wichane (sawa baba kesho nitaanza kutafuta nami nipate mwenzangu)
Kweli kesho ilipofika kijana alimwaga babaye na kuomba baraka zote ili akafanikiwe.
Kijana: Baba uko nakaja, nakashika mhola lakini natampandikile unkima wakutola (baba kule niliko enda nilifika salama lakini sikumpata mwanamke wa kumwoa)
Baba: Pole ng’wanone. Lakini ishi wagwandyaga umhayo, ukumpandika nduhu tabu nintondo ulaje hangi nyandone (pole mwanangu. Madam umeshaianza kazi hapana tabu utampata tu na kesho tena uende tena kijana wangu)
Kesho yake kweli kijana kama siku ya jana yake alifanya vivyo hivyo. Lakini hakufanikiwa tena. Alifanya hivyo kwa muda mrefu sana hatimaye akachoka mithiri ya sungura kusema ‘sizitaki mbichi hizi.’
Kijana: Bhabha, unene nanoga lulu eshi natumpandikaga unkima uwa kutola! (baba, mimi nimechoka sasa maana simpati mwanamke wa kumwoa!)
Baba: Hama ulihaya wite ki lulu nyandone? (sasa unataka ufanyeje kijana wangu?)
Kijana: Napandikaga iwazo bhabha (nimepata wazo baba)
Baba: Iwazo ki ng’wanone? (ni wazo gani mwanangu?)
Kijana: Angu lulu usengi duhu nantole eshi atatoliwe aliyo nsoga gete kukila nabhabho naliyubhabhona ulu naja kuchola wakutola (si hata shangazi tu yamkini hajaolewa na hata hivyo ni mzuri sana kuwazidi hata wale ninao waona nikienda kumtafuta wa kumwoa)
Baba: Ulintumbafu gete nyandebhe untole llumbu lyane! (wewe ni mpumbavu sana kijana umwoe dada wangu!)
Kijana: Bhabha bhuli ubhebhe untolile umayu wane? (baba kwanini wewe umemwoa mama wangu?)
Naomba nisikuchoshe sana. Mfano huu nilio utoa usukumani inawezekana pia uko sehemu nyingine hata kwa namna nyingine. Utufunze hasa vijana, kusema ‘bado muda ukifika nitaoa tu au nitaolewa.’ Vijana kuweni na msimamo msiwe kama bendera ‘kufuata upepo.’
¨   Mtoto wa kike asitumiwe kama mradi au tega uchumi kwa njia ya kudai mahari (hasa ng’ombe)
¨   Katekesi ya kina juu ya majukumu na haki za wana ndoa-wanaofunga ndoa wafikie umri wa kuweza kuyakabili majukumu hayo

Hitimisho; Ndoa za utotoni ni haramu, si haki kwa watoto kulazimishwa kuingia katika maisha na wito huo msingi wa miito mingine kabla ya kufikia umri stahiki. Wazazi na jamii wanapaswa kupewa elimu yenye asili ya ukombozi ili watoto hasa wa kike walindwe pasina haki zao kukanyagwa kanyagwa kama mavumbi chini ya viatu vya mvaaji. Wakikua watachagua wao wenyewe ni maisha gani yatakayo wawezesha kumjua, kumpenda na kumtumikia Mungu wao. Na endapo watachagua ndoa, itakuwa safi maana umri utakuwa ni rafiki kwao kufanya hivyo na hakutakuwa na matatizo kama tulivyo yabainisha hapo juu.
Jamii imeishia kuvaa sketi fupi kimaadili kwasababu ya kukithiri katika mambo machafu kama hili la kuozesha wanajamii wake katika umri mdogo. Hili ni janga kubwa sana! Tupigeni vita ndoa za namna hii na kwa pamoja tutashinda. Jamii iziwajibishe familia zenye wazazi wanao walazimisha watoto wao kuingia katika maisha ya ndoa wangali wadogo bado. Familia pia ziseme hapana kwa watoto wanaoonesha mwonekano wa kutaka kuoa au kuolewa katika umri mdogo. Watoto wenyewe pia wawe mstari wa mbele kusema ‘nitasubiri hata kama mazingira yananilazimu kuoa au kuolewa.’
Kila mmoja wetu akitimiza wajibu wake, tutaishinda vita hii. Familia moja moja iwe kali na tayari kuwachukulia hatua wote wanao fika nyumbani kwa lengo lwa kuoa binti wadogo wadogo. Iwakamate na kuwapeleka mahakamani na huko sheria ichukue mkondo wake dhidi ya walaghali wa mapenzi kama hao, waharibuji wa maana ya wito wa ndoa kama hao. Tukumbuke yaliyotokea kwenye Biblia Kitabu cha Mwanzo pale Yakobo alipoenda kwa Mjomba wake Labani kuoa akimtaka binti mdogo amwoe kabla ya dada wake. Labani alikataa akasema “HAVITENDEKI HIVI KWETU, KUMTOA MDOGO KABLA YA MKUBWA; TIMIZA SIKU ZAKE SABA, NASI TUTAKUPA HUYU NAYE KWA UTUMISHI UTAKAONITUMIKIA, MIAKA SABA MINGINE” (Mwa. 29:26-27).[60]
Kanisa kwa nafasi ya pekee sana lina sauti ivumayo kwa nguvu sana. Likemee jambo hili. Liweke vizuizi vya hapana kwa watoto kama hao. Na isitokee kwa vyovyote vile ndoa kama hizo zikafungwa ndani ya Kanisa letu moja, takatifu, katoliki na la mitume. Itakuwa aibu kubwa sana kufanya hivyo. Nilifurahishwa sana na tukio lililooneshwa na chombo cha habari ITV juu ya uamuzi wa mahakama kuwakamata wahusika wa ndoa kati ya vijana wadogo kabisa (mvulana alikuwa amemaliza darasa la VII na msichana alikuwa darasa la VI). Jamii ililisimamia suala hili na kuhakikisha linafika kwenye ngazi ya juu.
Na ndugu wenzangu Wasukuma kuna mtindo wa msichana anapomaliza tu darasa la VII siku hiyo hiyo masaa ya jioni jioni ananyakuliwa kama kifaranga kinyakuliwavyo na mwewe. Tunaita “KUBOLWA.” Hapa ndugu Wasukuma wenzangu tumeshindwa, tuamke sasa, tuzinduke, tutoke usingizini, tuseme hapana. Nilipo fuatilia suala hili nilihakikishiwa kuwa huwa ni mpango wa muda mrefu kati ya mama na binti wake na mpenzi wake mtarajiwa. Na bahati mbaya sana kijana wa kiume awe ameshampa na Khanga mama wa binti, hapo hata binti angejifaragua namna gani ataenda tu. Wasukuma wana msemo “ATASHENG’WA TU” huu hutumika pale ng’ombe anapokuwa mkali kukamuliwa na mkamuaji anasema ‘ATAKAMULIWA TU.’ Anaweza kuhahikishiwa kuwa hata nguo zake zimeshatangulia na nyingine zitamkuta huko. Wengine nilisikitika zaidi kusikia kuwa hata kwenye mitihani yao ya shule za msingi waliambiwa wajitahidi kutokufaulu na ole wao wangefaulu yangewatokea puani. Kumbe waliandika andika tu! Bora liende.


v   Magonjwa. Kadhalika kupenda vitu rahisi imepelekea kuibuka kwa magonjwa mbalimbali, mfano: kisukari, presha, kiribatumbo, ugonjwa wa moyo na mengineyo. Haya ni baadhi ya magonjwa tunayojisabishia sisi wenyewe kwa kutojali afya zetu kupitia kazi za kufanyisha mwili mazoezi. Maana ni katika kazi, afya ya mwili na akili inajengeka vizuri. Kumbe tukirejea hata kwa Mwasisi wa taifa letu Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika moja ya hotuba zake aliwahi kusema “Kazi ni kipimo cha utu.” Hivyo kila mtu anao wajibu wa kufanya kazi kwa manufaa au kwa ajili ya kunufaisha mwili wake, katika kupambana na maradhi mbalimbali. Tuweni watu wa kujituma na siyo legevu yaani eti tunajiita watoto mayai. Kumbe tuachane na dhana potofu hiyo, tukijua kabisa hatunabudi kufanya kazi. Hii inatupelekea pia kuungana na Mhe. Dr. John Pombe Magufuli Rais wa amamu ya tano wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania katika sera yake ya “Hapa Kazi Tu”, nikiihusianisha na umuhimu wa kwamba kazi au mazoezi ni afya.

5.3 Ulegevu katika Mila na Desturi

Lazima tukubaliane tu na hali yenyewe kwamba, maisha ya sasa ni tofauti na ya zamani. Kadhalika namna ya kuelekeza na kutoa maadili kwa zamani ilikuwa kitu cha lazima, ila kwa sasa hata wazazi hawana muda wa kukaa na watoto wao kuwajuza juu ya mambo ya zamani. Na hapo utaona kuporomoka kwa taasisi msingi ya malezi ambayo ni familia, kumechangiwa na Utandawazi. Muda wa jioni au wa kupumzika wameketi barazani unakuta si Baba, si Mama wala si Mtoto kila mmoja anaendelea na shughuli za mtandaoni tu. Wakati kipindi hicho hata maswala ya Televisheni hayakuwepo na hivyo ilikuwa tu giza likikaribia wanafamilia wote wapo Nyumbani na hapo hadithi ziliweza kusimuliwa sana huku wakiendelea kuota moto. Siku watu wa nymba moja hawana muda wa kuwasalimia watu wa ndani ya nyumba yao. Zaidi anaanza na aliyeko mbali nae. Hello……umeamkaje ndugu yangu? Na pengine hata yule ambaye amelala naye hajamwambia, umelalaje?
Malezi bila mila. Ikitokea ukaulizwa mila za kabila lako hususani zile zihusuyo malezi utaweza kujieleza? Swali hilo naamini linaweza kuwa gumu, labda kwa wale wachache ambao wamekaa sana kijijini katika malezi yao. Ila asilimia kubwa imepoteza mila hizo baada ya kupita shule, yaani ni kijana ametoka chuo pengine kwa sababu ya kuingiliwa au kuvamiwa na utandawazi anaona au kujiona hana hadhi ya kuongea tena na wazee. Hali hiyo imesababisha vijana waliowengi kukosa malezi yaliyokuwa yanawaandaa kuwa watu wazuri katika maisha yao ya baadae. Kwa mfano kulikuwa kuna mila na desturi ya jando na unyago; hii iliweza kuwaelimisha vijana namna ya kuishi vizuri katika maisha yao ya ndoa. Ndiyo maana hapo awali hapakuwa na migogoro ya kifamilia sana kama siku hizi. Tuanze kurejea taratibu katika mila na desturi zetu za awali ili kunusuru kizazi cha sasa pia cha baadae, na hii iende samabamba na yale mazuri tu; mabaya tuachane nayo yakiwemo ya ukeketaji ambapo hata kibiolojia kinachofanyika ni ukatilii. Tujishikamanishe na yale yatakayojenga familia zetu upya.
Chanzo kikubwa cha kuporomoka maadili ni kutowajibika ipasavyo kwa taasisi msingi ya malezi yaani familia. Wazazi wengi sasa hivi hawajui wala hawatambui wajibu wao, anachojali tu ni kutafuta riziki ya kila siku. Ni kweli ni jambo jema, ila inafikia ni Mama wa familia eti kisa shughuli za utafutaji za hapa na pale anamaliza wiki nzima hajui watoto au mtoto anashindaje nyumbani. Kwani yeye anachofanya anaondoka alfajiri sana na kwenda katika shughuli zake akiwaacha watoto bado wamesinzia, wakati wa kurudi pia anarudi usiku ambapo anawakuta watoto wameshasinzia; zaidi akijitahidi atauliza mfanyakazi tu watoto wamesinzia wakiwa wamekula au wameoga? Huishia hapo tu baada ya kujiridhisha kuwa hawajalala njaa, kuhusu malezi mfanyakazi ndiye atakayefanya.
Kwa hiyo wazazi huwafanya wafanyakazi wa ndani kuchukua majukumu mazito ya kulea kabla ya wakati wao, kumbe malezi yanayotolewa hapo si rafiki sana ukizingatia ni mtoto analea mtoto mwenzake. Pia kwa kuwa mzazi hana muda na watoto wake hata shuleni walimu wanabebeshwa kulea watoto ambao ni wasumbufu sana, hawasikii wala kuambilikika; kwani malezi bora na msingi yanaanzia katika familia. Sasa mzazi huyu ambaye amebanwa sana na shughuli za utafutaji hata kumsahau mwanae kiasi hicho, unadhani ni lini atapata muda wa kuongea na mwanae na kumsimulia maisha yaliyokuwa wakati wao? Wazazi tujitahidi kuwa na kiasi pia kufikiria nini tunakijenga kwa watoto wetu, maana unapoendelea hivyo ujue unamharibu mtoto kwani unampatia uhuru kabla hajakomaa. Matokeo yake utaona mara ameshapata mimba, ana maambukizi ya virusi vya ukimwi; kumbe yote hayo tunayababisha wazazi wenyewe.

5.4 Elimu  ya  Magharibi

Ninapoongelea elimu ya magharibi nina maana ya elimu tuipatayo shuleni ambayo tumeipokea kutoka kwa wenzetu waliotutangulia kimaendeleo yaani Nchi zilizoendelea. Sasa kama siku zote tusemavyo kila chenye faida hakikosi kuwa na hasara. Ni kweli kwamba kile tunachokipata kinatusaidia katika kuendeleza maisha yetu kwa vitendo pia nadhalia. Lakini siyo kila tunachokisoma na kukielewa kwa nadhalia tukiweke katika matendo, maana kwa kufanya hivyo ndipo tunaanza kupata matatizo mbalimbali.
Hususani masomo ya sayansi tunapaswa kuyaelewa na kuyafanyia kazi kwa umakini wa hali ya juu. Kuna somo la Biolojia linamwelezea mwanadamu kadhalika wanyama na mifumo yao yote namna inavyofanya kazi. Mfano wa mfumo wa Uzalishanaji unaongelea namna nzima ya ile kazi tuliyopewa ya uumbaji wa pili (rej. Mwa 1:28). Sasa mwanafunzi asiyemwangalifu akishajua ahaa! kumbe katika mzunguko wake wa mwezi kuna siku ambazo yuko huru anaweza kushiriki ndoa ya kabla ya wakati na asidhulike, basi anafanya mara ya kwanza kama majaribio akisema liwalo na liwe. Hivyo inapotokea kweli hajapata ujauzito, siku nyingine atarudia tena na tena mwisho wa siku akajikuta ni gwiji katika mchezo huo. Maana tunaambiwa kuwa sumu ya penzi ukishailamba hata kwa maziwa huwezi kupona, na bandubandu huisha gogo; hivyo inaweza kumpelekea hata katika ukahaba.
Elimu bila tunu. Yaani katika maisha ya kawaida tunatazamia kumwona msomi anafanya au akitenda kulingana na alichosoma, sasa unapomwona msomi mfano mwenye shahada anatenda sawa na mhitimu wa darasa la saba; mmh! hapo lazima kuna tatizo. Kwa maana nyingine hakuna alichoambulia licha ya kusoma kwake, zaidi tutamwona kama alienda shule kutembea au kukua shuleni. Ni kwa mantiki hiyo tunataraji kumwona msomi akiishi na kuenenda kisomi katika maneno na hata matendo yake. Yaani kile alichokisoma anakiishi na kuwafanya watu wengine waige kutoka kwake yale yote ya msingi. Angalisho, siyo kusoma kwako sasa kukufanye uwadhalau wengine na kuwaona hawafai hata kuishi kwa kuwa hawajui mambo mengi. Jitahidi uishi uasili wako (be natural), usianze kujivisha pembe za majivuno mpaka kufikia kuwadhalau waliokuwezesha mpaka kufikia hapo ulipo. Hivyo tujifunze kwa Albert Einstein aliyesema ‘Elimu ni kile kinachobaki kwa mtu baada ya kusahau alichojifunza shuleni.’ Hapa alitaka kutupa somo kuwa elimu siyo kile kilichoko kwenye madaftari na vitabu bali kile kilichopo kichwani au kinachobaki ndani mwako na ukakiishi.
Kwa hiyo wito wangu kwa wazazi, wajitahidi kuwaeleza watoto wao kinagaubaga pasipo kumng’unya maneno hali halisi ya maisha ya nyakati hizi na madhara yake. Na watoto nao tuwe tayari na kuwasiliza wazazi wetu maana hao ndiyo Mungu wa pili hapa duniani. Hivyo kama tukishindwa kuwasikiliza yale wanayotuasa maana yake hatuwaheshimu, kama hatuwaheshimu tunajipunguzia miaka ya kuishi duniani; Amri ya nne ya Mungu (rej. Kut 20:12). Pia tunaaswa kuwa asiyefunzwa na Mamaye hufunzwa na ulimwengu, kumbe tuwe wasikivu siku zote na kupokea kile tunachoelezwa na wakubwa wetu. Kila mtu asiwe wa kutaka kila kitu akisikiacho akionje au kukijaribu kwanza, bali tuongozwe na busara na hekima katika kufikiri. Tuutumie msemo usemao “Fikiri kabla ya kutenda” balabala, ukimaanisha kuwa kabla ya kutenda uwe umeshaona faida na hasara zake. Na hapo ndipo ufanye uchaguzi sahihi.
Matokeo hasi ya Elimu ya Magharibi
v   Uasherati. Kulingana na ufafanuzi wa kamusi ya kisasa inasema kuwa ni kujamiana kwa hiari kati ya watu ambao hawajaoana (yaani kati ya mtu ambaye hajaoa au kuolewa). Katika agano la kale, dhambi zote za ngono ikiwemo uzinzi zilizuiliwa na sheria ya Musa na desturi ya wayahudi. Na hivyo katika Kiebrania neno uzinzi lilitafsiriwa na kutumika katika mazingira kama ya ibada ya sanamu.[61] Ndiyo maana ukisoma 2 Nya 21:10-14 tunaambiwa kuwa Mungu alimpiga Yehoramu kwa kuwaongoza watu katika ibada ya sanamu. Pia Ufu 17:1-2 tunaambiwa kuwa uasherati umeenea duniani mwote. Hivyo basi kwa maisha ya sasa tumekuwa tukishuhudia Kaka na Dada zetu walioko shuleni wakisahau na kupoteza dira yao ya kuwa shuleni. Na matokeo yake tunawashuhudia aidha kabla ya kumaliza au mara baada ya kumaliza tukiwa na matarajio makubwa juu yao, wanatuletea aibu katika familia aidha ya mimba au magonjwa. Kwa nini niiite aibu ya mimba? Mimba yenyewe kama yenyewe siyo mbaya na haina hatia, ila aibu yake iko kwa aliyebeba mimba hiyo au aliyebebesha mimba hiyo; kwa maana imepatikana kimagendo yaani ni haramu, kwa kuwa haijapatikana kihalali na kwa wakati husika.

5.4.1 Maambukizi

Tujiunge na Frt. Richard Nyonga mwaka 2015, anayetoa ufafanuzi wa Maambukizi yatokanayo na mapenzi au tokeo la ngono si salama.
Maambukizi ni hali ya ugonjwa kuenewa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine. Kuna njia mbali mbali ambazo zinaweza kupelekea kuenea kwa ugonjwa kwa kasi zaidi kama vile upepo (air borne diseases), vijidudu, maji (water borne diseases), kugusana (contagious diseases), kufanya tendo la ndoa nk.
o  Aina za maambukizi
Magonjwa yanayotokana na mapenzi yapo mengi sana. Hapa najikita kueleza yale yanayosababishwa na vijidudu (viral diseases). Maambukizi hayo ni kama yafuatayo:-
Ø Kisonono
Ugonjwa huu huenezwa na vijidudu aina ya Gonococcae. Wahanga katika ugonjwa huu ni wote wanaume na wanawake wanaoshiriki mapenzi na mmoja wao akawa ni mwathirika tayari na yule ambaye kabla ya tendo la ngono hakuwa mwathirika basi huwa yaani kwa tendo hilo, humwambukiza na mwingine. Ugonjwa huu kwa asilimia kubwa huwakumba vijana wanao wekeza nguvu zao nyingi katika mapenzi.
Ø Kaswende
Hii ni aina nyingine ya maambukizi yatokanayo na mapenzi. Ugonjwa huu pia huhusisha wote wanaume na wanawake pale mmoja kati ya washiriki anapokuwa ameathirika na ugonjwa huo. Vijana hawako nje ya maambukizi hayo. Tungeweza kusema wanacheza namba inayoongoza mashindano.
Ø UKIMWI
Ugonjwa huu pia husababishwa na kufanya mapenzi japo sababu nyingine zinaweza kuchangia kama vile kuchangia vitu vyenye ncha kali kama vile nyembe, kupewa damu ya mtu mwenye virusi vya ugonjwa huo nk. Lakini kwa asilimia kubwa sana ni kwa njia ya kufanya mapenzi na mtu mwenye VVU.
o  Mhusika/Wahusika
Ø Vijana
Ø Wanandoa wachepukaji
Ø Wanaofanya mapenzi kwa utafiti (sex for curiosity)
Ø Wanaofanya mapenzi kwa biashara (sex for business)
Ø Wanaokaa mbali na wenzi wao kwa muda mrefu mathalani madereva wa magari makubwa
Ø Wadada wanao jiuza (dada poa) na akina kaka au baba wanaishi maisha ya ufanyaji ngono na kila mtu

o  Hasara zake
Ø Maambukizi haya yanaweza kusababisha utasa kwa mwanamume na pia kwa mwanamke na kumpelekea asiwe na uwezo kabisa wa kubeba mimba kwa mfano, Kisonono.
Ø Pia mama mwenye Kisonono, kipindi cha mimba mtoto atakayezaliwa kuna uwezekano mkubwa sana wa kuwa kipofu asipopatiwa tiba mapema
Ø Mtoto anaweza kuzaliwa amekufa (still birth) hasa kwenye gonjwa la Kaswende.
Ø Hasara nyingine ambayo ni ya kiuchumi ni kupoteza hela nyingi sana kwasababu ya matibabu kwa mfano, Kisonono kinapokomaa, mgonjwa huyo hasa wa kiume mirija huziba na hupata shida katika kupata haja ndogo, hivyo mahitaji ya kimatibabu ya hali ya juu huchukua hatamu
Ø Kifo na vifo vingi katika jamii. Tumepotelewa na wapendwa wetu wengi sana katika jamii kwasababu ya maambukizi haya
Ø Ugomvi katika familia
Ø Kuvunjika kwa familia mara baada ya kugundua kuna ukosefu wa uaminifu kati ya mwenzi au kuogopa kuambukizwa hasa UKIMWI usio ponyeka

o  Mwarobaini wa tatizo
Mwarobaini pekee kwa tatizo hili ni kuvaa vazi la uaminifu, na kujiepusha na kufanya mapenzi kabla ya ndoa au nje ya ndoa kwa wanandoa na kwa wasio na ndoa kuacha kabisa kujihusisha na mapenzi. Ushauri mwingine, kwa wana ndoa ikigundulika mmoja ni mwathirika, awe na upendo wa thati kwa mwenzake asiwe mfereji wa kuiangamiza familia nzima. Wana ndoa wapime mara kwa mara ili wajue afya zao na kuendelea kuishi kwa upendo kila mmoja akidhamiria kumlinda mwenzi wake na siyo kuleta UKIMWI au maambukizi mengine nyumbani. Itambulike wazi kuwa ni kosa kubwa kujua kuwa ‘umeathirika na unakomaa mpaka na mwenzako athirike pia, huu ni uuaji wa kukusudia kabisa!’
o  Maoni yangu na ushauri
Ø Elimu siku zote ni ya muhimu sana, itolewe kuhusu maambukizi haya na namna yanavyoambikizwa ili watu wajue kuyaepa si kiujanja ujanja (kwa mfano kutumia mipira ya kiume na kike) bali kwa kuzingatia taratibu stahiki
Ø Tunu za wanandoa zisisitizwe kwa wanandoa mfano, uaminifu, upendo wa dhati kwa mwenzi wa mtu, uvumilivu nk
Ø Watu wautumie vema uhuru wao maana uhuru usio na mipaka ni utumwa na uhuru wa kufanya mapenzi bila kufuata mafundisho ya Kanisa na maongozi mema ya jamii ni kujaribu kina cha maji kwa mguu wako mwenyewe
Ø Kanisa liongeze na lipanue wigo wake wa kimafundisho ili liweze kuwafikia watu wengi na kuwanusuru na hatari hii
Ø Kila mtu awe mlinzi wa mwenzake
Ø Tusidanganyike kwa matangazo lukuki ya baadhi ya vyombo vya habari vingine ni vya serikali kabisa kuwa:-
1)  Kuna ngono salama (kwa kutumia mipira-Kondomu)
2)  Kuwa na mwenzi mmoja hata kabla ya ndoa wakupozea injini (hapa ni kama kumpelekea mbuzi wako muuza supu), vipi kama huyo mmoja uliye naye naye anawake mmoja hamtafika watatu?

3)  Matangazo mengi yanapotosha umma. Fuatilia matangazo ya PSI utagundua kuwa kuna viashiria vya kutumaliza. Wengine wanasisitiza “kama kweli unampenda utamlinda. Mpenzi wangu nakupenda nitakulinda na kinga nk, mimi na mwenzi wangu tunapendana na hivyo tunatumia Kondomu-wewe je? nk”

5.5  Ukosefu wa vitu asilia

Asilia ina maana ya mwanzo au halisi. Kulielewa neno asilia ngoja tuone Waraka kwa Wafilipi inasema “Yesu kwa asili alikuwa daima Mungu……” (Rej. Flp 2:6). Asili inaonyesha ni kitu tangu mwanzo kilikuwa na namna fulani, na hapo Yesu anaongelewa kuwa ni uhalisia kwamba tangu mwanzo kweli alikuwa Mungu.
Katika maisha yetu neno asilia limekuwa likitumika kama kitu chenye kuhusisha mambo ya tamaduni. Mifano; utasikia wakisema asili ya wachagga ni pesa tu, au asili ya wasukuma ni kupenda kula ugali, pia mara asili ya Muha ni mtu wa kufanya kazi ngumu na mengine mengi. Sasa uasilia ninaoongelea mimi umejikita katika hali ya ulaji wa chakula, ambapo kila kabila au ukoo fulani ulikuwa unavyakula asilia walivyokuwa wakivitumia kujipatia nguvu za kuendelea kuishi. Mifano; Waha walipenda kutumia Ugali wa mtama na viazi vikuu kama chakula cha asili, Wachagga ni Kimbo (huchanganywa ndizi na maharagwe); Wasukuma ni Viazi, Makande na Michembe; Wahaya ni Ndizi; Wairaqw ni Ugali na Makande; Wapogolo ni Wali; Wapare ni Makande; Wammalila ni Ndothani (viazi mviringo). Lakini sasa hivyo vyakula bado wanavitumia? Jibu ni hapana vimeshaachiliwa, kupuuzwa na kutupiliwa mbali; kwa kisingizio kwamba vimeshapitwa na wakati.
Ni katika ile hali ya kudharau vitu vya maana vya zamani, ambapo imepelekea na kuchangia katika kushuka kwa maadili. Moja ya madhara yatokanayo na upuuzwaji wa vyakula asilia ni Watoto kuanza kubarehe mapema sana. Kibiolojia mvulana anaanza kubarehe akiwa na umri wa miaka 14, na msichana kuanzia miaka 11. Sasa inatoa picha gani pale tunaposikia vyombo vya habari vikitoa taarifa ya msichana kupata ujauzito kwa kulawitiwa akiwa na umri wa miaka 8?  Kwa hiyo itupe somo kuwa vyakula hivi tunavyotumia vya kisasa vinasindikwa viwandani na utunzaji wake unaambatana na utumiaji wa kemikali. Kadhalika tunapovitumia sisi vinaenda kufanya vurugu na kemikali tulizonazo mwilini, na zinapounganika ndipo zinaenda kuharibu baadhi ya mifumo ya ukuaji wa mwanadamu. Na madhara tunaanza kuyaona mapema hata katika nyanja za ukuaji, kama ni msichana kufikisha miaka 5 tu tayari unaona baadhi ya viungo vyake vimeshachipua. Hali kadhalika kwa wavulana inakuwa hivyo, yaani unakuta bado mdogo ila anafahamu mambo mengi ya kidunia kupita hata wakubwa wake.
Tukumbuke vyakula asilia havikuwa vinapita na kusindikwa viwandani au katika upandaji wake haukuwa wa kutumia madawa ya viwandani. Kumbe kama sehemu ilionekana haina rutuba ya kutosha waliweza kutumia mbolea asilia kama samadi ambayo kwayo haikuwa na madhara kwa watumiaji. Sasa basi, kupitia mabadiliko ya mapema watu wakiwa bado watoto; hata katika ukuaji wake ukifuatilia utaona mabadiliko ya mwili yanatokea mara hata kabla ya kufikia ule muda wake. Hivyo na kujikuta maadili kuporomoka bila kujua chanzo, kinachangiwa na ulaji wa vyakula vya kisasa; ndipo tunaona kuwazia mapenzi wakiwa bado na umri mdogo. Hatupaswi kuwalaumu sana ila kuwaelimisha namna ya kujikwamua katika janga hilo pengine la ukahaba.

5.6 Uwajibikaji hafifu wa kila mtu


·       Viongozi wa Kiroho.
Mara nyingine tunaweza kuumiza na kugongagonga vichwa vyetu tukitafakari ni kwa namna gani viongozi wa dini au kiroho wamechangia katika ushukaji wa maadili. Huo ni ukweli usiopingika ya kuwa kila mmoja anaowajibu wa kufanya kulingana na nafasi yake katika jamii hata pia katika mazingira anayokuwepo kwa wakati huo. Lakini sasa tukumbuke hamna mtu mwenye wajibu mkubwa sana hapa duniani kama kiongozi wa kiroho, moja kwa moja hapa naongelea Mtawa, Shemasi, Padre na Askofu. Kwa nini naamua kusema hivyo? Kiongozi wa mambo haya ya dunianai au kimwili anashughulika zaidi na kitu kipitacho; ndiyo maana tunasikia mwili haufai kitu bali roho ndiyo itutiayo uzima. Hivyo basi Padre kama kiongozi wa kiroho anatuelekeza na kutusaidia kuufikia uzima wa milele.
Ni kwa mantiki hiyo tunajua ya kuwa, Padre ni Kristo mwingine (Alter Christus); kama ilivyokuwa kwa Kristo kuwa kazi yake kubwa mpaka kuja duniani ilikuwa kutukomboa sisi wanadamu: vivyo hivyo kwa Padre naye anashirikishwa kazi ile ile ya Kristo ya kutaka kumkomboa mwanadamu kupitia Mamlaka aliyopewa na Kanisa zaidi kabisa kupitia Masakramenti. Sasa uchangiaji wa Padre katika dimbwi hili la mporomoko wa maadili ni pale kama kiongozi wa kiroho anapoona watu wanaishi hali zisizompendeza Mungu na akaamua kupuuzia au kukaa kimya tu; asitake kukemea na kukalipia. Hapo anaonyesha dhahili na kuchangia maadili kuzidi kumomonyoka tu; kama tuonavyo ardhi ikimomonyoka hususani kipindi kama cha mvua (masika). Pia ni kwa namna hiyo Mt. Maria Viane aliona umuhimu wa Padre katika jamii na kusema “Mahali ambapo Padre anaweza kupaacha kwa muda wa miaka 20, atakuta watu wanaabudu hata miti arudipo”. Alisema hivyo kutuonyesha kuwa Padre katika mambo yahusuyo maadili na yote yampendezayo Mungu yeye ndiye mtaalam haswaa!
Changamoto inaanzia sasa wapi mpaka Kiongozi wa Kiroho asikemee? Katika somo la Litrujia Takatifu katika Utunzaji wa Litrujia katika Seminari (In ecclesiasticum Futurorum: 1979) inasema juu ya dalili kwa mseminari kuhusu jinsi ya kuundwa kwa nia mbili; kwanza: haja ya kukuza maagizo sahihi ya makuhani wa baadaye ili waweze kufanywa zaidi ya kuchagua kuelewa wazi tabia na nguvu ya Litrujia Takatifu mpya na hivyo kuyafanya maisha yao ya kiroho na katika mwenendo wao wa kila siku na kuwasiliana kwa uzuri na waamini. Hivyo wakati wanapoelewa huwapelekea kujitambua wenyewe na baadaye kugeuzwa na kuwageuza watu wengine katika mitazamao yao mibovu ya kimaisha.
Pili, msisitizo mkubwa juu ya malezi ya Litrujia katika seminari unahitajika ili kukabiliana na matatizo mapya ya mafundisho yanayotokana na kuongezeka kwa jamii; ambapo inapelekea watu kuamua kuishi maisha watakayo. Mt.Tereza wa Culcuta aliwahi kusema kuwa “Mtu anatoa kile alichonacho”. Pia mwanafalsafa mmoja (Ludwig Wittgenstein) katika kitabu chake (Tractatus Logico) anasema “whatever can be said at all can be said clearly and whereoff one cannot speak therefore one must be silent” Maneno yote ya watu hawa yanataka kutufumbua na kututafakarisha ya kuwa; Imani bila matendo imekufa, hivyo mfano mimi ningekuwa tayari ni Padre lazima tu iniwiye vigumu kukemea kitu ambacho hata mimi kukiishi siwezi. Kwa mfano mimi nakuwa Padre ambaye sina upendo kwa watu wote yaani wale niwajuwao na nisiowajua na hivyo nakuwa na ubaguzi: nachangamkia wale ninaofahamiana nao tu. Sasa itakuwa vigumu sana kusimama na kuwaambia wengine waishi upendo kwa kumwiga Kristo yeye aliyetupenda upeo. Hivyo lazima nitaona aibu na kuamua kukaa kimya pasipo kukemea. Na hapo taifa la Mungu litakapozidi kuishi kwa kujitenga na kukaa mbali na Mungu: wakati mchungaji wanae ila hatekelezi wajibu wake ipasavyo mimi kama Padre nitakuwa nahusika moja kwa moja katika kuliteketeza  taifa la Mungu kwa kushindwa kumfasa Kristo kiaminifu.
Sasa changamoto hii inatokea baada ya Kiongozi wa kiroho pengine tangu akiwa bado mlelewa hakuwa makini na kufuata kile anachofundishwa na walezi wake. Hivyo anapokuwa katika kituo cha utume wake mambo kama hayo yanatokea tu kiurahisi. Maana wahenga walisema samaki mkunje angali mbichi, sasa anapojikuta muda umeenda kuna vitu inakuwa vigumu kusema anaaweza kuvipokea na kuvifanyia kazi. Licha ya kujua kuwa Binadamu hubadilikabadilika (Man is dynamic).
·       Jamii nzima kwa ujumla.
Hatuwezi kuongelea jamii pasipo Familia. Na hivyo jamii inaundwa na familia. Sasa ufanisi wa familia kiroho na kimwili unategemea zaidi uwajibikaji baina ya wanafamilia; kwa kuwa msingi wake upo katika kutimiza wajibu. Pale inapotokea kwamba, wazijengao familia hawatimizi nyajibu zao, familia kwa ujumla na jamii nzima zinakosa mwelekeo katika nyanja zote (kiroho, kijamii pia kiuchumi). Na matokeo ndiyo hayo yanayopelekea yafuatayo kwa maadili kushuka na madhara yake yanakuwa makubwa katika familia na jamii nzima.[62]
Ø Kuongezeka kwa matendo maovu katika jamii kama wizi, ujambazi, ugaidi, ualawiti, ubakaji, n.k
Siku hizi yanazuka maovu yanayoathiri maisha ya vijana na maisha ya weneye ndoa. Nayo ni mengi. Baadhi yake ni wizi, utovu wa nidhamu, kukoseana heshima, ulevi, uasherati, makwazo kwa watoto; kudekeza watoto; kuwakatili watoto, kukosa mahitaji ya lazima; maovu ya kuzuia ama kuharibu mimba; magonjwa ya zinaa na mengine mengi.[63]
Ø Malezi duni kwa watoto. Ikumbukwe ya kuwa malezi hafifu kutoka kwa wazazi na walezi pia yanapelekea uwepo wa watoto wa mitaani, umalaya, uasherati, mimba za utotoni, matusi, uvaaji mbovu, dharau, kiburi, uvivu, n.k. Na hivyo kupelekea washindwe hata kufikiria juu ya kuoa au kuolewa kwa kuwa hawana elimu ya kutosha ya maisha ya ndoa. Maana kwa kukosekana tu heshima, mtoto anakataa na kushindwa kumsikiliza mzazi au mlezi wake anapokuwa anamweleza mambo ya kumjenga hapo baadaye.
Ø Vifo vya mapema. Tukumbuke kuwa siyo kila kifo ni mpango wa Mungu; bali vingine vinatokana na mtu au mpango na maamuzi ya mtu pale anapoamua kuishi maisha atakayo yeye, maisha yaliyokosa hofu ya Mungu na hivyo anaachana na maadili. Mfano ni ajali zitokanazo na ulevi wa pombe na madawa ya kulevya kwa baadhi ya madreva, harakati za utoaji mimba, magonjwa ya zinaa kama UKIMWI. Hayo yote naweza kusema yanakamilika kwa ule msemo usemao “asiyefunzwa na Mamaye, hufunzwa na ulimwengu”. Kwamba mtu anaposhindwa kufuata yale anayoelekezwa kutekeleza au kufanya matokeo yake ndiyo hayo kuwa lazima aingie katika matatizo makubwa, ni kwa matokeo hayo basi alililia wembe nao umemkata; maana hakutaka kuwa msikivu kwa aliyoambiwa.[64]
Sasa wito wangu kwa wote baada ya kuona changamoto hizo tena zilizo nyingi, kama Wakatoliki tunapaswa kuinuka kutoka usingizini na tuanze kujikita katika kusoma maneno ya Maandiko Matakatifu. Kwa mantiki hiyo tufanye neno la Mungu ndilo liwe chakula na kinywaji chetu, maana ni katika neno tunajipatia hekima ya Mungu. Yatupasa kuifanya Biblia kuwa kama Kitembea Nasi “VADE MECUM”. Ni vema kuhusianisha Biblia na matukio katika Biblia na maisha yetu ya sasa. Mtazamo wetu unapaswa uwe wa kisasa hasa katika kuwa na mazoea ya kufanya tafakari ya masomo katika Biblia ikiwezekana kila siku iendayo. Mwisho, wote kama Wakatoliki na wakristu kwa ujumla tunapaswa kuiga maisha ya watangulizi wetu hasa wale waliofanya mema katika ulimwengu huu. Mfano huu bora tutaupata pindi tu tutakapofuata maisha ya watu wenye kumfasa Mungu, na haya tutayapata pale tu tutakapokuwa na mazoea ya kusoma Maandiko Matakatifu. Kwa kusoma Maandiko Matakatifu tutaweza kuona ni wapi ulimwengu ulianzia, ulipitia na ulipo.
Thamani yetu machoni pa Mungu ni kubwa sana; nasi tusiipoteze kwa matendo yetu maovu, lakini thamani hii itaweza kuboreshwa endapo tutakuwa wenye kufuata mashauri ya Mungu, na mashauri haya hupatikana kwa njia ya kutafakari Neno lake yaani Biblia. Zamani zile Mungu alinena na wazee wetu na Manabii nao wakayaweka katika maandishi yale yote Mungu aliyonena nao. Waebrania waliweza kudumisha uhusiano bora na Mungu kwani hawakuweza kufahamu siku ambayo Mungu angeweza kuzungumza nao. Kadhalika nasi tunapaswa kuwa na uhusiano bora na Mungu hasa kwa njia ya sala na matendo mema yenye kujaa uangavu na maadili safi. Hatujui siku wala saa ambapo Mungu atakayotuondoa ulimwenguni humu.[65]


SURA YA SITA

Kuna mambo mengi sana ambayo kwa sasa yanaitesa dunia, na binadamu ndiye mhanga au mateka wa mambo hayo. Sasa tatizo limeshajitokeza na lipo, nini tunapaswa kufanya katika kuinusuru dunia hii? Maana katika uhalisia kamili yaliyokuwa yakifanyika kipindi cha sodoma na gomora (rej. Mwa 19:1-28) pia kipindi cha Gharika kuu (rej. Mwa 6:1-22) ndiyo sasa yameshaanza kushamili.

6.1    Utoaji mimba

Katika uuaji unaojikita katika Utoaji mimba nauona kana kwamba ni uuaji wa makusudi kwa wasichana na baadhi ya wanawake wa siku hizi. Ni kuua kwa kudhamiria mtoto aliyemo tumboni mwa mama yake kwa njia yoyote ile na kutoa nje vipande vipande vya mwili au mwili wote ukiwa maiti. Uhai wa mtoto unakatizwa kabla ya kuzaliwa; mama anamkatalia mtoto wake haki yake ya kuishi, yaani kuwa hai. Kwa lugha rahisi kutoa mimba ni kuua kama kuua kwa aina nyingine tunayoweza kufikiria. Mara zote ndiyo maana unakuta wanatoa sababu kama hizi ilimradi tu wajitetee: Afya ya mama, Mtoto anaweza kuzaliwa na ulemavu, Mimba hii imetokana na kubakwa au ni ya ndugu wa damu (Baba au Kaka), Siko tayari kuwa na mtoto sasa, Naogopa mtoto atabadilisha maisha yangu, Nimetelekezwa, Nimezaa watoto wote niliowahitaji.
Lakini mimi nasema hamna sababu yenye mashiko, maana hata hiyo ya kiafya muda mwingine mtu anaweza akadanganya ili tu aitoe mimba kwa kisingizio.
Wachangiaji wa mauaji haya ni kila mtu kulingana na nafasi yake aliyonayo. Kulingana na maelezo ya Frt. Audax Ndalahwa katika juu ya Prolife (kulinda uhai) kuwa ‘Nani washiriki wa utoaji mimba’ tarehe 03-04-2015; alikuwa na haya ya kusema:-
Akiongozwa na dhana hii “NAONA KIU” (Yn 19:28)
Kauli hii ni ya Bwana wetu Yesu Kristo akiwa Msalabani katika harakati za kuutetea UHAI wetu, ukombozi wetu, utu na thamani yetu tuliyoipoteza kwa sababu ya dhambi zetu. Ni kauli fupi kuliko kauli au maneno yote (7) aliyosema akiwa Msalabani lakini ina uzito na ujumbe mahususi sana kwetu leo. “NAONA KIU.”  Kiu ya Yesu ni kutuvuta sote kwake, ili alipo Yeye, nasi tuwepo. Yeye alisema, “Nami nikiinuliwa juu ya nchi, nitawavuta wote kwangu” (Yn 12:32; 8:28). Mimi na wewe tuna kiu gani katika dunia hii? Je, ni kiu ya kinywaji (moto/baridi), ni kiu ya kufaulu mitihani na kuwa wanafunzi bora? Ni kiu ya kuwa tu padre? Ni kiu ya kuwa na mali na vitu vingi vya thamani? Lakini zaidi ya hayo, naomba tujiulize jambo hili, “Mimi nina kiu ya KUUJUA, KUUPENDA, KUULINDA NA KUUTETEA UHAI ULIO ‘ZAWADI YA MUNGU NA MALI YA MUNGU?’” Tukiwa na Kiu ya kuulinda UHAI, karibuni tuchukue hatua.
Karibuni sasa tukiongozwa na neno hili la tano (5) la hotuba ya Yesu Msalabani, tuwaangalie WAHUSIKA/WASHIRIKI WA UTOAJI MIMBA.
Tujiulize maswali haya mawili kama gia yetu yakuondokea:-
v Nani hutoa mimba?
v Je, mtu mmoja anaweza kutoa mimba?
Majibu ya maswali haya yanaweza kutofautiana kutokana na mtazamo kati ya mtu na mtu. Karibuni sasa tusafiri pamoja katika kuyadadavua maswali haya na kuyatafutia majawabu yake.

ü Kwanza ni SHETANI
Katika orodha ya wachangiaji wengi, nimependa kumpa nafasi ya kwanza huyu mhusika. Huyu hutoa msukumo wa ndani kabisa mwa mtu. Msukumo wake ni wa namna ya kupendekeza, kama vile mtu anavyotoa ushauri kwa mwenzake. Shetani hutumia maneno lukuki matamu na yenye mvuto mkubwa. Husema, ‘fanya tu chapu! Kwa haraka na kwa wepesi, ni rahisi sana kama kumsukuma mlevi, usiogope wewe sio mtu wa kwanza kufanya hivyo, wengine wengi tu wameshafanya na wakafanikiwa, kuwa mjanja-zeeka mwili usizeeke mawazo na uamzi, usichelewe kijusi hiki kinakua, utaaibika mrembo, ona sasa unavyoonekana! Umekuwa ‘shapeless.’ Akisha kulainisha kwa maneno yake ya uongo yaliyo katika ofisi yake ya “baba wa uongo” ( Rej.,Yn 8:44), hukusindikiza mwanzo mwisho na  akisha hakikisha kila kitu kimeenda 100 kwa 100, yeye hutoweka na kubaki kando akijipa HEKO kwa utume mzuri! Je, mimi na wewe leo tunachagua kumpa kampani Shetani katika hili? MIMI SIMO, WEWE JE?

ü Pili ni  MAMA/DADA MJAMZITO
Mama wa Mtoto. Mtoto yumo tumboni mwake, ni mama yake kwelikweli; anafanya uamuzi (uwe wa hiari au wa kulazimishwa); ndiye anayemwambia mganga ua mtoto huyu; simtaki.
Huyu ni mshiriki mwingine mkubwa tu katika uovu huu usio vumilika hata chembe kidogo. Kwa kweli mama/dada mjamzito ndiye anayekuwa na dhamana ya kubeba UHAI ambao ni “ZAWADI YA MUNGU, MALI YA MUNGU.”
Lakini cha ajabu na cha kushangaza, ‘mbeba mkoba leo anadiriki kumiliki mkoba!’ Mkoba huu (UHAI) ni wa Mungu, amemkabidhi mama/dada huyu aushikilie bila mastahili. Amepewa zawadi ya kuulinda kwa muda mwafaka kwa ajili ya lengo maalum kuujaza na kuutawala ulimwengu agizo la kwanza kwanza kabisa la wazazi wetu wa kwanza (Rej., Mwa 1:28), ‘Zaeni mkaongezeke.’ Mshiriki huyu hufikia hatua au uamzi huu mbaya baada ya kusikia mashauri mabaya ya mshiriki nambari moja kama tulivyoona hapo awali. Amempa Shetani nafasi! Lakini amempa Mungu kisogo na kumwona hana jipya!
Anaichezea kwa hiari kabisa au hata kwa kushinikizwa, zawadi ambayo si wote wamewapewa na Mungu, ‘zawadi ya kuwa na kuitwa ‘MAMA (f).’ Kwa maneno mengine yeye husema, ‘UA KITU HIKI, FLASHI UCHAFU HUU, MWAGA OIL HII, SIKITAKI NA SIKIHITAJI! Na kwa hali ya kawaida hutoa sababu lukuki za uhalalishi wa uovu huu, uhalalishi huu huuitwa, ‘VISINGIZIO.’ Navyo ni pamoja na hivi: mimi bado ni msichana mdogo mno, sitaki kuwa na mtoto sasa, sitaki kuitwa mama kwasasa, mwenye mtoto (baba) amemkataa, bado niko masomoni, nyumbani hawatanielewa, nitachekwa sana, nitazeeka mapema, nitakosa thamani (market-soko), nitashindwa kula ujana, nitakosa kampani, nina hali ngumu ya kimaisha, sitaweza kumtunza mtoto huyu, nilibakwa tu, aliyenipa mimba hii ni baba yangu mzazi (kaka yangu wa damu), nina mtoto mchanga nitaambiwa ‘nazaa kama nguruwe/siyo mradi wa kujivunia kuzaa haraka haraka na kwa wingi huo.’
Visingizio vingine ni pamoja na; nimeipata mimba hii nje ya ndoa-nitampoteza mume, wazazi wamenilazimisha kutoa, nimepata mimba uzeeni. Na mengine mengi ya namna hiyo. Lakini tukubali tusikubali hakuna hata kisingizio kimoja ambacho chaweza kuwa na uzito kama sababu ya kuuruhusu mpango wa Mungu, kuupenda na kuulinda uhai utokao kwa Mungu peke yake. MAMA/DADA Yesu alikuonea wewe KIU ili aukomboe UHAI wako. Je, wewe humuonei KIU mtoto wako mwenyewe ili uje umwone siku moja alivyomzuri, akikulanda wewe/mume wako/wazazi wenu? Isikie sauti hii ya huruma moyoni na kwenye dhamiri yako “NAONA KIU.”
ü Tatu ni BABA WA MTOTO
Huyu anaweza kuwa baba kwa maana halisi ya umri wake au kijana tu amepata mwanya huu wakuwa mzazi. Huyu naye haepuki sura hii ya ushiriki/uchangiaji. Ushiriki wake waweza kuwa wa moja kwa moja au kinyume chake. Anaweza kumshawishi mpenzi wake kufanya hivyo, na hata akikataa kwakuwa yeye ameamua hivyo, anaweza kulazimisha! Anaweza kushawishiwa pia na mpenzi wake juu ya uamzi huu mchafu kabisa (ambao hata wanyama wadogo/walio chini yetu hawafanyi) kuchukua uamzi huu nayeye kwa kujidai kuonesha upendo kwa mpenzi wake (kumbe upuuzi) anaafiki na hata kutoa pesa kwaajili ya ufanikishaji wa adhma yao mbaya. Anaweza hata akamsindikiza mjamzito wake kwenye kituo cha afya ili ahakikishe kweli kuwa ameenda kutenda kama walivyokubaliana. Mchango wake ni ‘mchango-mtambuka,’ anaweza kushiriki kwa kumtelekeza mjamzito wake kama tulivyoona kisingizio kimojawapo hapo juu. Lakini liwe liwalo, atakuwa ameshiriki vizuri kabisa kufanya kitu kibaya kabisa (UUAJI). Kutupiana mpira kwa akina Adamu na Hawa na Nyoka (Rej., Mwa 3:12-13), hupata mwendelezo hapa. Huyu naye hutoa visingizio au sababu ili kuhalalisha uhitaji msingi wa zoezi hili bovu kabisa. Anaweza kudai: bado sijafikia umri wa kuwa na kuitwa baba sasa hivi, bado nasoma, nitakuwa na mzigo mkubwa sana, huyu dada/mama ni mwongo alipaswa kuniambia kuwa yuko kwenye siku zake za hatari, amelikoroga mwenyewe acha alinywe (atoe mimba), nitafungwa jela (maana binti huyu ni mwanafunzi bado/ mama huyu ni mke wa mtu), nitachekwa na vijana wenzangu, nitakosa kampani ya vijana wenzangu hata wazee hawatanipokea maana mimi damu bado ya moto, nitapoteza wasichana wengi/wanawake wengi (kama ni mchepukaji), mke wangu ataniacha na familia (kama ni mume wa mtu).
Kuna sababu nyingi mno kama walivyo wavulana na wanaume wengi tu katika uso huu wa dunia. Lakini hata hivyo sababu hizi zilizo hitimu kwa vigezo vya uovu kamwe haviwezi kuwa na mashiko yoyote ya kupelekea kuutoa UHAI (kuua). ‘NAONA KIU.’ Kijana mwenzangu, ewe baba, kiu hii ilikuwa ya Yesu kwako wewe, na ni kiu Yake kwa huyu binadamu mwenzako aliyetumboni mwa huyu mpenzi wako. Je, unataka kumpa Yesu Siki kwenye Sifongo? Huoni Kiu ya kuyaona matunda ya kazi yako? Unapenda kulima tu lakini hupendi kuvuna? Iruhusu basi kiu ya mwanao mpenzi ya kumwona baba uso kwa uso itimie baada ya mwezi wa tisa (9) ya kuwa kwenye tumbo zuri la mpenzi wako (mama wake).


ü Nne ni DAKTARI/NESI/MTOA DAWA
Huyu naye ni mshiriki wa kitaaluma. Nimsomi na kioo cha jamii. Ni tegemeo la wahitaji (wagonjwa), ni mtu anayeleta matumaini ya kuishi pale ambapo mtu amepoteza matumaini kwa ugonjwa. Je, hufanya hivyo muda wote na kwa mtu yeyote? Wewe mwenzangu unayetamani sana kuwa yeye (daktari/nesi) kwa siku za usoni, una adhma hiyo? Napasua jipu. Ukweli umejidhihirisha kuwa, hapa na pale, kwa huyu na yule wataalam hawa wamekuwa waharibifu. Mchango wa watu hawa mara nyingi ni ule wa moja kwa moja na wakati mwingine (kwa nadra) huvaa vazi la watoa ushauri. Lakini ‘tuliite koleo ni koleo tu na siyo kijiko kikubwa.’ Sababu, nia na kusudi la kumwita huyu mhusika “MUUAJI” tunayo. Hii ni kwasababu yeye ndiye anayekamilisha nia ya washiriki 2 na 3 kuwa kitendo. Kama ni vidonge (sumu) vyakunywa, ndiye anayevipitisha na hata kuvitoa, kama ni kumkatakata binadamu mwenzetu ambaye hajazaliwa bado, yeye ndiye anayevaa ‘gloves’ na kushika mikasi tayari kwa kutekeleza uovu huu. Tunamlaumu sana huyu, maana angeweza kusema ‘hapana,’ na hapana yake ikanusuru maisha ya mwenzetu.
Kwa taaluma yake, yeye ndiye anayetoa matumaini na kumwaminisha mtoa mimba kuwa, ‘utoaji wa mimba ni kitendo cha kawaida kabisa tena hakichukui muda, ni dakika sufuri tu, hakina madhara yoyote, wala hakuna maumivu yoyote ni kama kutema mate tu, hauumii bali unajisikia raha kwamba umetema mate.’ Kwa upande mwingine mhusika huyu ni halali kwa lawama zetu kwani yeye ndiye anayemhadaa mama/dada mjamzito kuwa ‘kilichoko tumboni siyo mtoto na hivyo siyo mtu, ni nyama nyama tu, ni damu damu tu sawa kabisa na damu ya mwezi (hedhi), ni mnyama fulani fulani tu, ni mlemavu nk.’ Ni huyu anayeitumia vibaya taaluma yake kwa kuwadanganya wajawazito kuwa, ‘kiumbe hicho hakijaumbika, hakijaifikia hatua stahiki ya kuwa mtu/binadamu kama sisi, ni kama kiluwiluwi chenye kichwa kikubwa na mkia mdogo! Kwa haya na mengine mengi, mganga/daktari/nesi hakwepi shitaka na kilio chetu watetea uhai kuwa ‘YEYE NI MUUAJI NAMBARI MOJA.’ Hata hivyo, ‘NAONA KIU,’ bado ni sauti tunayomuasa kuisikiliza kila mara, awe anakula, anakunywa maji, anatembea, ili ikitokea hali inayotoa msukumo, ‘asimpe nafasi mwenye risasi bila bunduki kumpa yeye risasi nakuitia kwenye bundukiye na kumuua mtu asiye na hatia’ (mjamzito mwenye nia hiyo akija kumwomba ushauri asikubali kutenda jambo hilo).
ü Tano ni WAZAZI
Wapendwa sana wazazi wetu wana ushawishi mkubwa sana karibu katika kila kitu katika maisha yetu sisi wana wao. Katika mazuri na mabaya mchango wao haukwepeki, ama wayakemee mabaya (ushiriki mzuri) au wayanyamazie kana kwamba hawayaoni (ushiriki mbaya). Katika uwanja huu wa utoaji mimba, wazazi kwa ukali wao, kutokuwasikiliza watoto wao, kutokuwasamehe katika makosa yao, kutokuwaelekeza namna ya kuingia katika utu mzima n.k  wanajikuta wako kwenye bahari na siyo tu jito ya kutoa msukumo kwa watoto wao kufanya maamuzi mabaya ya mauaji. Mathalani binti anajiuliza, ‘baba alivyomkali yule, nitabaki mtu kweli? Kama alisikia tu niko kwenye mahusiano na fulani nilitishiwa kifo! Sembuse hii leo nimeleta aibu ya kuwa mjamzito na ninasoma kwa pesa yake!’ Kwa upande mwingine wa shilingi, binti anajiuliza, ‘ni kwa maneno gani nitamweleza mama anielewe jinsi alivyokuwa mstari wa mbele wa kuniasa na kunikanya juu ya kutokujihusisha na mapenzi mpaka akaapa kuwa ikitokea tu nimepata mimba nitambue bayana kuwa sina mama na hapo ndipo utakuwa mwisho wa safari yangu ya masomo nami nikaapa nikimdhihirishia kuwa kamwe sitamwangusha. Leo hii ninavielelezo vyote na kiambatanishi vyakuwa nimeshiriki ngono, nina mama kweli? Nina shule kweli? Na yeye ndiye baba na mama wangu?
Kwa hali ya kawaida, maswali mazito kama haya humpelekea binti kuwa na msongo mkubwa wa mawazo, anakosa afanye nini na mwisho hujikuta amekuwa ‘duka la shetani’ maana ‘akili isiyo na chakujishughulisha nacho, huwa duka la shetani.’ Na hapo mshiriki nambari moja hutoa majibu kwanza, mepesi, marahisi, yanayowezekana (practical), yanayomsaidia huyu binti kutoka katika hali hiyo kama tulivyoona mwanzoni. Pili hushiriki vema kabisa mpaka kwenye ngazi ya kumwonesha njia, na daktari/mganga/nesi aliyebobea/maarufu kwa shughuli ya utoaji mimba. Kana kwamba haitoshi-humsindikiza binti huyu mpaka sehemu husika na kumpa ujasiri wote, wote kabisa akijichukulia uoga wote mabegani mwake.
Jua lizamapo, binti huyu huishia kumwua mwanae, labda mwanaye wa pekee kabisa (kama alikuwa na nafasi moja tu ya kuzaa), msaidizi wake wa kesho, mtu wa kumlea na kumtunza uzeeni mwake, kiongozi mkubwa tu wa dini au serikali n.k. ‘NAONA KIU.” Wazazi kuweni wazazi jua linapochomoza na jua linapozama. Wapokeeni watoto wenu katika hali zote na muwasaidie katika mafanikio na maanguko yao. Wahenga wanasema ‘mwanao akishika mavi, haumkati mkono la, bali unamnawisha vizuri.’ Au ‘nzi akitua kwenye maziwa yako, chukua kijiti mtoe halafu kunywa maziwa yako.’ Hii yafaa kuwa KIU yenu kwa watoto wenu na ustawi wa maisha yao.      
ü Sita ni NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI
Hawa nao ni wadau wakubwa katika janga hili. Mchango wa hawa ndugu ni ule wa kumsaidia mtu kuingia kwenye majuto kamili kwa kumzomea kutokana na ujauzito wake akiwa: mwanafunzi, msichana mrembo/mbichi/damu moto/mwenye mvuto kuliko hata wao, mke/mshikaji wa mtu mwingine, bado ananyonyesha kichanga kingine, ana umri mdogo mno (binti) au mkubwa mno (mama). Vitisho vingine ni vya kumtenga kwenye kampani yao. Wakisha mfikisha kwenye majuto ambayo ni mjukuu, humpa ushauri juu ya nini cha kufanya, namna ya kukifanya, muda wa kukifanya, sehemu ya kukifanya na sababu ya kukifanya. Wao, Shetani, yeye (mhusika) pamoja na Daktari hufikia mwisho la reli (kuua). Na hapo hata walio masikini huwa matajiri wa kutoa pesa kwa ajili ya ufanisi wa zoezi zima. ‘Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli.’ Akikufaa katika kutoa mimba huyo ni ‘adui wa kweli.’ Utanishauri nisiue kama wewe unauchukia uuaji.
Hata hivyo, ‘NAONA KIU.’ Bado ni sauti ya mchungaji wetu Bwana Yesu kwao. Anawaonea kiu ya kuwatoa katika uovu wao, anataka kiu yake ioane na kiu yao ya kuupenda na kuupa nafasi ya kwanza uhai, ‘Zawadi ya Mungu, Mali ya Mungu.’
ü Saba ni  VYOMBO MBALIMBALI
(i) BUNGE
Hiki ni chombo ambacho tunajua kina fanya kazi ya kutunga sheria za nchi. Kumbe mchango wake katika janga hili la utoaji mimba umejikita hapo hapo kwenye utunzi wa sheria za nchi. Hata hivyo huko nako kuna watu siyo malaika wanaoifanya kazi hiyo ya utunzi wa sheria za nchi.  Ni walewale tulio waona hapo mwanzo (baba/mama), na kama wamepotoka hawawezi kutunga sheria ambazo zimenyooka na ziko kwa manufaa ya wananchi. “Hauwezi kuchuma chungwa kwenye mpera, mtu au kitu hutoa alicho/kilicho nacho.’ Kama watuambiavyo Walatini, ‘Nemo dat quod non habet=No none gives what he does not have=asichonacho hatoicho/hakuna mtu atoaye asicho nacho.’
Mchango wa Wabunge bungeni uko katika kutoa miswaada ambayo hupitiwa na kuwa sheria baadaye. Miswaada hii ikipita na kuwa sheria na kama iliruhusu utoaji wa mimba, basi hapo kuua huhalalishwa. Wakati mwingine ni kushindwa kwao kutunga sheria ambazo huwalinda binadamu wenzetu hawa wasio na sauti ya kujitetea (wachanga wa tumboni). Kwahiyo kwa kutunga sheria mbovu au hata kulifumbia macho suala hili, mchango wao huwa wazi kabisa kwamba ‘nao ni wauaji.’ Na kwa mantiki hiyo, “NAONA KIU,” hubaki kuwa mwaliko kwao juu ya kuchukua uamzi mzuri wa kuulinda uhai wa ndugu zao. Binadamu ambao baada yao, wengine ndio watakao ingia bungeni na kutunga sheria za kuwalinda wao wakiwa wazee. Wabunge na mtakaokuwa Wabunge kesho, oneni kiu ya kuupenda uhai ulio ‘Zawadi ya Mungu, Mali ya Mungu.’
(ii) MAHAKAMA
Hiki ni chombo kinachosimamia sheria. Huhakikisha kuwa sheria inakidhi mahitaji ya kuwa sheria kwa kila mtu, na huhakikisha kuwa hakuna aliye juu ya sheria. Kwahiyo, chombo hiki hukakisha kila mtu ana usawa na mwenzake kisheria awe mzee kabisa, baba/mama wa makamo, kaka/dada, mtoto aliyezaliwa na aliyetumboni pia. Kinachoshangaza ni kuona kwetu pale ambapotunaitegemea Mahakama kufanya kazi za namna hiyo na nyingine nyingi za jinsi hiyo-hazifanyiki. Na pale ambapo hali iko hivyo, kinyume chake hudhihirika machoni petu. Watu wengine kuwa juu ya sheria (mathalani viongozi wa serikali na watoto au ndugu/jamaa na marafiki zao wa karibu pamoja na matajiri). Kwa mtiririko huo kuna kuwa na wenzetu ambao hawana haki yoyote kisheria, hawana utetezi (hususani watoto ambao hawajazaliwa bado na wale ambao bado wadogo hawawezi kujitetea).
Kwa mhitasari, mahakama inaweza kushiriki kwa namna zifuatazo: kushindwa kutoa hukumu zinazowalinda watoto, kupitisha sheria ili itumikie maslahi ya watetezi wa kifo, kushindwa (kwa kufumbia macho) kutoa adhabu kali pale ambapo utoaji wa mimba umetokea, kuungana na watetezi wa kifo katika mauaji ya watoto wachanga.
Kilio cha Yesu, bado kinasikika leo hii, “NAONA KIU.” Wakiruhusu kilete mabadiliko mioyoni mwao. Ili nao wapate kiu ya kuisimamia vema sheria izuiayo mauaji ya wapendwa ndugu zetu wasio zaliwa bado. Watoto hawa nao wanakiu ya kuuona ulimwengu pamoja na ndugu zao. Ni haki yao msingi kabisa kuzaliwa kabla ya haki zingine zozote (zingine hufuata baada ya hii).
(iii) MASHIRIKA (mfano PSI, USAID, MARIE STOPES)
Kauli zao nyingi ni za ulaghai na uhamasishaji mathalani “TUMIA KONDOMU, JIEPUSHE NA NGONO ZEMBE UKIMWI UNAUA.”
Mashirika haya yaweza kuwa ya Umma au ya watu binafsi. Kwa ushawishi wake wa pesa yanaweza kufanya kitu ambacho ni hatarishi kwa maisha ya mtoto aliyeko tumboni mwa mama yake.
Kwa kifupi sana haya huweza kushiriki kwa njia mbalimbali. Baadhi ya njia hizo ni pamoja na:
·       Kuhamasisha kupitia kampeni na programu mbalimbali vitendo vya utoaji mimba.

·       Kutumia fedha nyingi kuwateka watu kifikra ili wakubaliane na uamzi na maadhimio yao.

·       Kuziteka mamlaka za serikali, bunge na mahakama kwa lugha ya ulaghai na fedha nyingi ili zitumikie itikadi za utamaduni wa kifo.

·       Kutumia lugha inayomfanya duni/mnyonge binadamu aliye tumboni ili aonekane kuwa sio mtu na hivyo kuwa rahisi kumwua.

·       Kutoa taarifa zisizo za kweli juu ya wingi/idadi kubwa ya watu katika uso wa dunia, lengo likiwa ni kuhalalisha utamaduni wa uuaji wa ndugu zetu walioko tumboni mwa mama zao.
Kwa hiyo, mchango wao mkubwa ni wa ushawishi. Lakini ni ushawishi mbaya, usiolinda maslahi ya mtoto mchanga aliyeko tumboni. Je, wakuu wa Taasisi hizi, dhamiri zenu hazisikii kilio hiki “NAONA KIU,” cha Mkombozi wetu Yesu Kristo kwa kila mtu? Anaona kiu ya kila mtu kuishi huru, kwa amani kama istahilivyo wana wa Mungu Baba yetu wa mbinguni.
(iv) TAASISI NA ASASI
Sanjari na Mashirika mbalimbali, kuna nafasi ya Taasisi na Asasi lukuki ambazo kama sehemu ya jamii, zinaweza kuwa na mchango hasi katika ustawi wa maisha ya watoto wachanga. Na kwa mantiki hiyo mwisho huwa ni mbaya (uuaji). Tuangalieni kwa mhitasari mchango wa Taasisi/Asasi:
Ø Kwa kuweka na kutekeleza sheria/kanuni/taratibu za kuwafukuza wanawake wapatao ujauzito katika hali isiyo rasmi (mwanafunzi au mke wa mtu nje ya ndoa yake) na hivyo huwashauri kutoa mimba.

Ø Mgawanyo pendelevu wa kazi/ajira. Kuwabagua wajawazito kana kwamba ujauzito ni kikwazo katika kufanya kazi (mfano Bosi anayemfukuza katibu wake baada ya kupata mimba!)

Ø Kuna wakati pia wanawake wanakumbwa na changamoto ya ajira zinazoendana na masharti mazito kwa madai ya wanawake wenye maumbile fulani fulani tu. Hii huwa hatari pale wanawake nao wanapoingia moja kwa moja katika utekelezaji wa vigezo na masharti hayo yanayohitaji kuzingatiwa, na ikitokea mwanamke amepata mimba basi yuko tayari ‘kwa udi na kwa uvumba’ kuitoa mimba hiyo ili abaki na umbo linalomruhusu kuendelea kukidhi matakwa ya mwajili/waajili wake!

Ø Mitazamo ya kumwona mwanamke mjamzito kama mzinzi nambari moja katika jamii. Hali hii hujitokeza zaidi katika Taasisi za dini. Hii ni sababu nyingine ambayo nayo huchangia wanawake wengi kufikia uamzi wa kutoa mimba ili wasiabike katika kanisa kwa kufananishwa na yule mwanamke mzinzi katika Injili ilivyoandikwa na Yohane (Rej., 8:1-11).
Yesu anatuambia leo, “NAONA KIU,” kwaajili ya mabadiliko yako ya ndani, ya kiroho na kimwili ili tuupende na kuuthamini uhai “Zawadi ya Mungu, Mali ya Mungu.”

(v) WANASAYANSI
Tunamshukuru Mungu kwa zawadi ya wanasayansi katika dunia. Kwa upande wa wataalam wa mambo yahusuyo mimba na mtoto mchanga na maendeleo yake mpaka kuzaliwa. Tunawashukuru sana kwa kutufumbua macho na kutupa uelewa juu ya mimba inavyotungwa, kukua kwa mtoto tumboni mwa mama yake. Kujua umri wa mimba/mtoto na jinsia yake (wakike/wakiume), mzunguko wake tumboni mwa mamaye, kama ana ulemavu au la anavyogeuka geuka tumboni nk.
Lakini sijui ni kwasababu ya sifa zetu kwao ‘tembo wamelitia maji!’ Na mwisho wake wameleta balaa, janga, tishio na hatari katika jamii. Na kwasababu hiyo, hawa nao tunawatambua katika mtiririko wa wale wanaoshiriki kutoa mimba. Tunaweza kusema kwa haki na uhuru kamili kabisa kuwa, “hawa ndio wanaotengeneza madawa au vifaa vya kutekelezea adhma ya wale wanaotamani kutoa mimba.” Kwa upande mwingine tunausahihi kusema kuwa “wasingelikuwa hawa wataalam kwa udadisi wao wa kujaribu jaribu hiki na kile, kusingekuwepo na uhakika wa moja kwa moja juu ya utoaji wa mimba.” Wamewadhihirishia watu kuwa, jambo hili linawezekana kabisa kwa asilimia mia moja na halina madhara, mtu anaweza akatoa mimba kadiri awezavyo, ni rahisi sana kama kumsukuma mlevi tu, ni jambo la kufanya ‘body cleanliness’ na hivyo hakuna cha kuogopa wala kustaajabia. Kutokana nao tumekuwa na majanga mengi kama vile:
*  Uchaguzi wa mtoto wa kuzaa-ikitokea mahesabu hayajaenda vizuri na kuzaa mtoto wasiyemtarajia baadhi ya wazazi huishia kuchukua uamzi wa kumwua huyu ambaye hawakupanga kumpata na mara nyingi takwimu zinaonesha kuwa watoto wa kike huuawa zaidi. Tabia hii mbaya inashamiri kule ambako wanapendelea watoto wakiume tu! Chukulia nchi kama India ambako mume ni diri-hutolewa mahali.

*  Watoto wenye ulemavu-hawa nao hukumbwa na wimbi hili la mauaji ya watoto wachanga. ‘Huyu ni mkosi mkubwa katika familia na ukoo wetu, hafai kuwepo nasi, si mwenzetu, hatufanani naye kwa chochote bali tumetofautiana katika kila kitu.’ Hii ndiyo huwa litania ya wazazi wanaotaka kuhalalisha utoaji/uuaji wa mimba.


*  Uvunaji wa viinitete (stem cells)-uhitaji huu wa kisayansi hupelekea uuaji wa binadamu kwa ajili ya uchunguzi wa tiba ya magonjwa mbalimbali (bado ufaulu wake hauna mashiko sana) na mengine mengi.

Enyi wanasayansi, kumbukeni utalaam mlio nao ni zawadi kutoka kwa Mungu ambayo hutokana na uhai aliowapa Mungu. Kwanini hamtaki dunia ijipatie wataalamu wengine kutokana na watoto wanaozaliwa leo? Ndiyo maana sauti ya Kristo inajirudia tena kwa huzuni zaidi, “NAONA KIU.” Tuisikieni na tuwasheni mishumaa ya kuulinda uhai, “Zawadi ya Mungu, Mali ya Mungu,” dhidi ya giza hili totoro la mauaji ya wapendwa ndugu, rafiki na jamaa zetu.
(vi) VIONGOZI WA DINI
Unaweza kunishangaa kwamba nimepata wapi ujasiri wa kuwahusisha na viongozi wa dini katika mkanda huu wa mauaji. Nisamehe ndugu yangu, lengo ni kuutetea uhai huu siyo kufunika kombe mwanaharamu apite (kulinda sifa ya kiongozi kwa gharama ya kuutoa uhai), ili kila mtu aulinde awe ni mtu wa dini au la! Wajibu uko palepale, “Ukiona chura anaruka mchana, ujue anajambo/chura haruki mchana bila sababu,” wanatuambia Wanigeria. Kumbe nami ninajambo ambalo nataka kukujuza. Viongozi wa dini wanahusika moja kwa moja katika filamu hii ya utoaji mimba kwa njia zifuatazo:
Ukimya wao. Viongozi wa dini ni sauti ya wengi, na ‘sauti ya wengi (katika jambo jema) ni sauti ya Mungu,’ wanatuasa Walatini (vox populi vox Dei). Kwahiyo ukimya wao badala ya kukemea usiku na mchana mauaji ya watoto wachanga, huua mara dufu zaidi kuliko wahusika wengine. Maana ukimya wao huwaacha waumini wao njia panda na huwaachia maswali mengi, mfano, “Je, kutoa mimba ni dhambi mbele za Mungu?” Mbona sijawahi kumsikia kiongozi wetu akisema chochote juu ya hilo? Akina Thomaso, hawajaisha makanisani. Mpaka wasikie Paroko/Padri/Mchungaji/Kiongozi yeyote wa dini amesema nini ndipo watende bara bara.
Kushindwa kutoa katekesi toshelezi. Tatizo hili hupelekea kudumaa au hata kufa kwa dhamiri za waamini wao na hivyo kuhalalisha hata maovu kuwa mema ili wayatende pasipo kusutwa na sauti ya Mungu mioyoni mwao.
Kwamfano, tunaweza kujiuliza maswali kadhaa, “hivi watumishi wa Mungu (viongozi) walikuwa wapi wakati Bunge la Uingereza, Marekani, Afrika Kusini ilipojadili kupitisha sheria za kuruhusu kuwaua binadamu wachanga katika umri ambao wangehitaji kulindwa na kutetewa?
Kushiriki moja kwa moja. Hii ndiyo balaa kubwa zaidi kuliko inavyodhaniwa. Imeonekana hapa na pale hata kwa kusikia maana asije mtu akanishitaki kuwa kusikia tu haitoshi. Maandiko yanatuambia ‘imani huja kwa kusikia’ (Rej., Rum 10:17). Tumesikia kuwa kuna baadhi ya viongozi wa dini wameshiriki katika mapenzi na waamini wao, na ilipotokea kudhihirika kwa upendo wao (tunda la upendo wa kindoa) wameishia kuficha aibu kwa kuvunja amri ya tano (5) ya Mungu baada ya kuivunja ile ya sita (6). Tusikate tamaa wala tusione kuwa ni jambo jema kufanya hivyo maana hata viongozi wetu wanafanya! Tuipeni nafasi sauti ya Mungu isikike tena na tena katika masikio ya mioyo yao “NAONA KIU.” Na sala zetu zitawasaidia kuisikia zaidi na zaidi. Inawezekana kabisa.
(vii) MIMI NA WEWE
Ni imani yangu kuwa kama vile ulivyonishangaa hapo juu, na hapa pia utanishangaa kwamba ‘hata mimi pamoja na kuwachambua wenzangu, bado kumbe hata na mimi ni mmoja wao.’ Mimi ni muumini wa falsafa hii, Sheria ni msumeno, hukata huku na huko. Labda unaweza hata kuhamaki kuwa nimekushitaki kwa kosa usilohusika au kujiuliza, ‘amenijuaje kuwa nilitoa mimba? Ametambuaje kuwa nilimlazimisha yule rafiki wangu wakike kutoa mimba? Ni nani amemwambia kuwa mimi ndiye niliyempa wazo na hata kumpeleka kwa mtaalam?’ Na maswali mengi ya namna mbalimbali. Kumbe mimi na wewe tumo kwa namna ya pekee katika janga hili. Hii ni kwasababu:
v Mimi na wewe tumekaa kimya asubuhi mpaka jioni, Januari-Desemba. Lakini tunasikia mambo yanaendelea tena wakati mwingine kwa watu wetu wa karibu kabisa. Lakini bado tumeogopa kuambiwa “Kikulacho kinguoni mwako.” Tunabembeleza urafiki wa Kaysari!
v Mimi na wewe tumefumba macho yetu tusione yanayoendelea lakini tunawafahamu wanaofanya unyama huu. Tumetumia nguvu nyingi sana kuyawekea macho yetu mapazia meusi!
v Inawezekana mimi na wewe tumetoa fedha kumsaidia rafiki yetu/mpambe wetu kutoa mimba. Tumemsindikiza au kumpeleka kwa wataalam. Mimi na wewe tumekuwa washauri na watoa ushuhuda kuwa jambo hilo linawezekana kabisa jambo la msingi ni kusema tu ‘NDIYO,’ tufanyeni haraka iwezekanavyo!
v Tumemchukulia hatua gani ya kisheria binti/mama anayetoa mimba? Tumemchukulia hatua gani ya kisheria daktari anayeifanya kazi hiyo ya kutoa mimba na anafahamika mtaani kwetu? Tumemchukulia hatua gani kijana wa kiume/baba anayewapa mimba wasichana/akina mama kana kwamba anatoa ruzuku? Au ndo tumekuwa redio ya kumtangaza kuwa ni mtaalamu sana, akimfanyia mtu habahatishi-bali ni kawaida yake.
Mimi na wewe leo, Kristo anatualika kuisikiliza kwa utulivu mkubwa kabisa sauti ya kilio chake msalabani, “NAONA KIU.” Tuisikiapo sauti hii leo, tusiifanye migumu mioyo yetu. Tuifungue na tufanye mabadiliko leo. Nasi tuwe na kiu ya kuwaona duniani hawa watoto wachanga, wengine ni wadogo zetu na kwa wengine ni watoto wao wadamu kabisa.
Kumbe tujue na tutambue kuwa, kitendo cha kushiriki tendo la ndoa lengo siyo kutuliza tamaa za mwili bali kuendeleza uumbaji. Na hivyo inapotokea aidha mtu amepata mimba bahati mbaya hana sababu yoyote ya kutaka kuiharibu mimba hiyo, zaidi mtu akiwezakufanya hivyo basi anajaribu kukwepa majukumu tu. Tuwe mashahidi wa Kutetea Uhai, kutofumbia Macho Ukweli, tuufichue ukweli, Kuandika, kuongea na kutumia vyombo vya habari kutetea uhai. Muhimu zaidi Kusali na kuombea watu wabadilike. Kama nilivyotangulia kusema hapo juu mwenye mamlaka ya kutoa uhai wa mtu ni Mungu pekee, vitu vingine vyovyote visiwe sababu ya sisi kujichukulia mamlaka isiyotuhusu.
NINI KIFANYIKE? Kila mmoja kwanza atambue Uhai ni zawadi kutoka kwa Mungu na ametutungia sheria ya kuwa tuulinde. Mwandishi Benjamini Mbowe anasema, Ni lazima tujue sisi tumepewa tu uhai tuutunze siyo wa kwetu, hivyo yatupasa tuulinde ipasavyo hata kwa gharama kubwa.[67] Pia tunaelezwa kuwa kuua au kujiua kunapingana na mapendo ya Mungu, hivyo kila mmoja wetu atambue kuwa anawajibu tu wa kuutunza uhai; maana Mungu pekee ndiye anayetawala uhai.[68]

6.2 Mapenzi ya jinsia moja

Kuna wakati kitu hicho kinanifikirisha na kunikera sana ninaposikia baadhi ya watu wanadhubutu eti kusema ‘ndoa za jinsia moja.’ Maana kiukweli kila nikazanapo kujitahidi kusoma vitu mbalimbali ili kuongeza wigo wa kuelewa vitu katika karne hii ya 21, bado napata kigugumizi hata kuthubutu kuungana na wanaosema ‘Mapenzi ya jinsia moja.’ Ni kutokana na uhalisia kamili wa neno ‘Ndoa’ maana ni mahusiano ya Mume na mke (jinsia tofauti) na daima kunapatikana zao la mahusiano hayo kama ilivyo asili na utu wetu. Na hivyo maingiliano ya watu wa jinsia moja haipo katika kanuni yoyote ya maumbile, labda kama ni zao la sayansi fulani na tafiti zilizofanyika zikaleta zao hilo.
Hata hivyo ni kitu kisichoeleweka kwani kinaenda kinyume cha asili (Nature). Sasa kama wanadamu tuko tofauti na wanyama wengine wote kwa sababu tu kujaliwa akili na utashi, hivyo tunafikiri (Man is a rational animal). Lakini sasa kama wanyama tu wengine walioko chini yetu katika mambo yote na wahafikiri (Irrational animal), lakini hata siku moja sijawahi kuona mnyama kakengeuka asili yake; yaani dume kaambatana na dume mwenzake au jike na jike mwenzake. Na hivyo mfano huu utufumbue macho tena ili tuwezekuona vizuri, kama wanyama hawajaweza kupingana na asili (nature) na hawafikiri. Je! inakuwaje kwa mwanadamu anayefikiri kufanya vitu ambavyo hata wanyama wengine hawajawahi kutenda na sina matumaini kama watakuja kutenda kinyume na asili. Kwa mfano tumezoea kuona mtu ana miguu na mikono miwili, sasa ikitokea akapatikana mwenye mikono mitatu kwa hali ya waziwazi tunaona ni kitu cha ajabu, siyo kawaida (abnormal). Maneno yenyewe hayana hata radha kabisa kusikia mapenzi za jinsia moja. Maana yake ni kwamba ni wapenzi wa jinsi moja (mwanaume na mwanaume au mwanamke na mwanamke). Nashindwa nikuelezeje kwa undani mpaka unielewe, lakini kwangu nasema ni ndoa za kishetani kabisa. Maana haimo katika ile asilia ya Mungu, yeye aliwafanya mwanamme na mwanamke na kuwaunganisha kwa tendo la ndoa. Kumbe kitendo kinachofanyika kiko kinyume na ile asili ya Mungu, hivyo ni dhambi kama dhambi nyingine (rej. 1Tim 1:10). Licha ya baadhi ya mataifa kupitisha kuwa haki kuanzia miaka ya 2000, zaidi ni nchi za ulaya na Amerika mfano; Uingereza, Marekani, Ujerumani, Hispania na hata Afrika Kusini.[69]
Wewe unaenisikia jitahidi kupiga vita hiyo mbaya na ya aibu sana ya kumkosoa vikali Mwenyezi Mungu (rej. Mwa 2:18-19; 23-24). Daima ongozwa na Neno la Mungu, ndipo utaona ya kuwa tumesharudi sodoma na gomora (rej. Mwa 19:1-8) pia gharika kuu (rej. Mwa 6:1-4), tunaonyeshwa kuwa watu hao waliishi kama wanyama kabisa. Sasa nasi tumekwisha anza kuishi kama wanyama, na hatari zaidi inayojitokeza ni kutaka kusambaza uchafu huu kila taifa. Mataifa yaliyoendelea yanaanza kutoa masharti juu ya utoaji wa misaada kwa mataifa yanayoendelea, wakiwataka ya kuwa ili wawape misaada au mikopo yenye nafuu kwanza wahalalishe mapenzi ya jinsia moja, mara utoaji mimba pia upokeaji wa vidhibiti mimba.
Sababu na dalili zinazoweza kuchangia na kupelekea mapenzi ya jinsia moja
Kwanza kabisa ndugu zangu lazima tutambue kuwa uchafu huu hautokei ghafla kama mwizi au kama unavyoweza kuona mwanga pale tu unapowasha soketi, bali huanzia kabisa mwanzo wa makuzi ya mtoto. Hivyo, mchango mkubwa unaweza kutokana na wazazi pengine kwa kutokujua na kuwapatia malezi bora watoto. Zifuatazo ni baadhi ya sababu ambazo zinadaiwa kupelekea na kuchochea mapenzi ya jinsia moja, wazazi wasipokuwa makini na dalili hizo.[70]
v   Zawadi nyingi (zilizopitiliza) katika uhusiano wa Mtoto na Mama yake (A more rewarding relationship with the Mother). Kama Mama anakuwa na utaratibu wa kutoa zawadi kwa wanawe (wa kiume) mara nyingi, ina maana watapendelea kumpenda Mama yao zaidi. Tokea hapo wanaanza kutengeneza aina fulani ya tabia kati yao, ambapo kuna ambao watapitiliza ule upendo na kujikuta wanaanza kuwa na tabia za kike. Mara ni mvulana anapenda kukaa karibu na Mama na kujikuta anaanza kutenda kama Mama yake katika kupika, kuosha vyombo. Hapo hapo ndani ya watoto hao wapo ambao watapenda kuonekana ndiyo wanaume, na hivyo inapotokea tofauti hizo kati yao; wanaweza kujikuta wanatengeneza hali ya mvuto kati yao. Na hivyo kitakacho tokea baina yao ndiyo laana hiyo tunayoaswa kuipiga vita.

v   Upungufu wa Baba wanaokalipia (Lack of salient Fathers’). Hii ina maana ya kwamba Baba kushindwa kuonyesha ule uwanaume (Masclinity) kwa vijana wake wa kiume. Kwa mfano kuna baadhi ya makabila walikuwa na utaratibu wa Baba wa familia kuchukua mtoto wake wa kiume na kwenda nae aidha kumwonyesha namna ya kushiriki kuchinja mbuzi, kuwinda na katika aina yoyote ya utafutaji. Hii ilianza kumjengea mtoto huyo ile thamani ya kuanza kuhisi ni mwanaume tangu mapema, japo aliweza kushirikishwa aidha kwa kushika mguu wakati wa kuchuna ngozi na baadaye kupewa nyama ili azifikishe nyumbani. Sasa kama Baba anashindwa kumtengenezea mazingira ya hivyo mwanaye na kujikuta anaambatana na Mamaye muda mwingi, inaweza kupelekea tatito hilo kwa baadaye.

v   Kushindwa kuhimiza kujitawala na kufanya maamuziadilifu (Failure to encourage autonomy). Ina maana ya Baba kushindwa kumulika kwa vijana wake ile hali ya uimara wa uwanaume katika kufanya maamuzi. Hivyo Baba anapaswa kuwatengenezea na kuwamulikia vijana kwa kuwapatia mazingira ya mahusiano ya kujitegemea, na siyo kujilegeza kwa mtoto wa kiume. Kumbe, Baba anaposhindwa kumdhibiti mtoto wa kiume na akawa tepetepe au kijana wa kujilegeza basi inaweza kumpelekea katika uovu huo.

v   Kutokuwepo kwa Baba katika familia. Hali hii inapelekea katika matokeo kama ya kutegemea, ukosefu wa kukaguliwa (assessor) au ukosefu wa uimara wa uwanaume katika familia. Hayo yote kwa kuyazingatia Mama hawezi peke yake, maana yanategemea uwepo wa Baba. Sasa anapokosekana watoto wanaweza kujikuta wameendana zaidi katika mambo ya jinsia ya kike, ambayo ni hatari sana.
v   Upungufu wa shule za mchanganyiko (Lack of co-education schools). Kwa namna ya kipekee watoto wanajikuta katika dimbwi hilo wakiwa katika mazingira ya shuleni. Mfano wazazi wanaamua kumpeleka mtoto shule ya bweni kuanzia chekechea mpaka kidato cha sita ni shule hiyo hiyo na ya wavulana tu au wasichana tu. Sasa kupitia maisha hayo yanamnyima mtoto fursa wanasema ya kusafisha macho, na mbaya zaidi kwa wale wa mjini zaidi ndiyo inakuwa mbaya sana, mtoto anaporudi kwa ajili ya likizo anabaki ni wa kubaniwa ndani; kama ni mwalimu anakuja kumfundishia humo humo ndani ya geti mpaka anarudi shule ratiba yake ni hiyo tu. Hivyo, hata kisaikolojia anajikuta anaathirika, kumbe wito wangu kwa wazazi wazingatie malezi bora pia watambue kuwa malezi bora si shauri ya kumfungia mtoto ndani ya geti; ambayo mwisho wa siku inampelekea kuitwa mtoto wa geti kali. Tubadili mitazamo yetu tafadhali.
Wito wangu kwa wewe msomaji unayesoma kitabu hiki kikufumbue macho na kuona mbali zaidi. Utagunduaje kuwa umeanza kuona mbali? Ni pale tu utakapoanza kupiga vita na kukemea kitu hicho kwa nguvu zako zote, ambapo inawezakana katika kuelimisha watu ambao hawajapata nakala hii ya kitabu ili nao waweze kutambua na kujiepusha na laana hii mbaya. Nimeamua kuiita laana tena mbaya maana inakinzana na asili ya mwanadamu tangu kuumbwa kwake. Nikiamini kwa nguvu zetu wenyewe hatuwezi, tuungane sote kwa pamoja katika kumwomba Mwenyezi Mungu atuepushe na balaa hili, maana linazidi kushamili kila mahali; licha ya kuona kuwa lilianzia kwa wenzetu Nchi zilizoendelea. Pia tukumbuke kuwa hata wao wakati linaanza halikupokelewa haraka na kupitishwa na serikali, vivyo hivyo nasi tatizo hilo limeshaanza japo serikali haijahararisha au kuruhusu kitu hicho kufanyika hazalani. Tuendelee kuliombea taifa letu na nchi zote ambazo hazijakubaliana na jambo hili chafu wabaki na msimamo huo hata mwisho wa dahari.

6.3 Watu  kuuza utu

Ninapoongea juu ya mtu kuuza utu wake, nina maana ya kuufanyia mwili ambao ni hekalu la Roho Mtakatifu kama aina fulani ya udharirishaji; kwa mfano wale wanaofanya biashara haramu ya ngono. Haya ni baadhi ya mambo ambayo Mungu aliyachukia mpaka kufikia muda wa kuangamiza watu wake kama kule Sodoma na Gomora, pia kipindi cha Gharika kuu. Hivyo kadiri yanavyozidi kuenea kutoka mji na mji basi tusibaki kuyafumbia macho tukemee kwa nguvu zote, maana ni dhambi na siyo kwamba kwa kukemea tutakuwa tunawahukumu wahusika. Tukumbuke kuwa ukweli siku zote utatuweka huru (rej. Yn 8:31-32).
Kwa upande wa wanawake wale wanaojiuza au kuuza utu wao wanaitwa Makahaba, kitendo kinaitwa Ukahaba. Ukahaba limetokana na neno la kiarabu qahabatun ikimaanisha malaya. Ukahaba ni tendo la kufanya ngono nje ya ndoa au uhusiano unaokubalika katika jamii, tena na watu mbalimbali na kwa malipo.
Kwa nini niseme ni uhusiano unaokubalika katika jamii wakati kitendo chenyewe hakifai? Kwa sababu kwa ndugu zetu walioendelea zaidi kwao wamesharasimisha na hivyo ni kitu kinachoeleweka na kukubalika hata na serikali zao. Tunaambiwa baadhi ya nchi hao makahaba kwa kitendo hicho cha ukahaba kinajulikana kama biashara kama biashara nyingine halali uzifahamuzo, mpaka serikali inajivunia kodi kupitia mapato ya watu hawa. Sasa watendaji wanaopokea malipo huitwa kahaba au malaya; washiriki wanaotoa malipo huitwa wateja. Lakini kama ukahaba unaendeshwa katika nyumba maalumu mahali hapo panaitwa danguro.[71]
Aina za Ukahaba. Kimsingi kuna aina mbili za ukahaba; Malaya anajifanyia kazi mwenyewe na Malaya anafanya kazi chini ya usimamizi wa mtu mwingine.
Ø    Malaya anajifanyia kazi mwenyewe. Hapa tunajuzwa kuwa mtu huyu anaamua mwenyewe bila shuruti kufanya tu. Huyu mara nyingi utamkuta akitembea barabarani, kusubiri kwenye klabu au kwa kutangaza namba ya simu. Pia hata kupitia intaneti wanajitangaza na kukutana na wateja mahali mbalimbali.

Ø    Malaya wanaofanya kazi chini ya usimamizi wa mtu mwingine au watu wengine. Hali yao inaweza kufanan na aina ya ajira wakilipwa kwa kila tendo la ngono kutoka kwa msimamizi anayepokea fedha; au wanatakiwa kutoa malipo kwake kutokana na mapato yao. Kundi hili mara nyingi linapatikana katika danguro, lakini wako pia barabarani katika maeneo maalumu wanapotazamiwa na kuwadia. Katika kundi hili kuna hasa aina ya utumwa wa kingono, ambapo mabinti na wanawake wanalazimishwa kujiuza kwa wateja. Mwaka 2009 Umoja wa Mataifa ulikadiria kwamba 79% za watu wanaouzwa ni kwa ajili ya biashara ya ukahaba, ambayo imekuwa hivyo biashara ya watumwa kubwa kuliko zote za historia ya binadamu. Kila mwaka watu 800,000 hivi wanavushwa mipaka ya nchi zao kwa ajili hiyo, wakiwemo hasa wanawake wale wenye umri chini ya miaka 18 wakiwa hadi 50%.[72] Wazazi tujihadhari sana, usije ukakurupuka kumtoa mwanao kuwa anakwenda nje ya nchi kapata kazi ya ndani, tambua wimbi hili linaendelea na kukua siku hadi siku kwa sababu hiyo ya uwongo. Kwa hiyo mtoto anapofika huko ndipo anajikuta analazimishwa kufanya kazi hiyo, kwa kuwa hana namna nyingine ya kufanya wala hawezi kutoroka basi anajikuta ametumbukia katika giza hilo.
Watu hawa ni wale ambao siku hizi kwenye miji mikubwa unakuta ikifika jioni wanatengeneza kijiwe chao kwa biashara hiyo, na kila mmoja anabei yake kulingana na ule mwonekano wa nje wa maumbile yake. Kwa mara ya kwanza ukisikia hivyo unaweza usiamini, maana unaanza kujawa na maswali kuntu mfano: umeonyeshwa au umemwona hata mmoja wapo wa wanawake wanaojiuza namna alivyo tu, utasema hivi huyu naye na urembo wake amekosa mwanaume wa kumwoa? Au amepungukiwa nini mpaka ajidharirishe hivyo? Hayo ni baadhi ya maswali ambayo unaweza kujiuliza baada kumwona au kuwaona watu wa aina hiyo ya kujiuza.
Lakini tatizo kubwa siyo amekosa nini, bali ni tabia yake ambayo imejengeka kupitia katika kipindi chake cha malezi. Hivyo walezi wajitahidi wanao wazipitie hatua zote za ukuaji wa mwanadamu, maana wakishindwa kufanya hivyo madhara yake ni makubwa sana kwa baadaye; pia namna ya gharama ya kuweza kumsaidia inakuwa juu sana. Nimefanya utafiti wangu kwa mji wa mwanza walio wengi wanafanyia biashara yao haramu pale mjini mtaa wa makoroboi, pia katika mji mdogo wa kasulu kijiwe chao kinaitwa makaburi wazi. Kila mmoja anapaswa kupiga vita jambo hilo kama Mungu ambavyo hakulichekelea bali kulichukia na kulipiga vita sana (rej. 1Tim 1:10).
Sasa kwetu ni biashara ambayo ni haramu, yaani haijapewa utambulisho kamili na kukubalika. Lakini ukienda katika baadhi ya mataifa inatambulika kama biashara halali, na hivyo serikali inajipatia hata mapato kupitia biashara hiyo kodi ya ushuru.
Madhara yake sasa hususani kiafya, siyo siri ni chanzo kikubwa ambacho kinaweza kueneza maradhi mbalimbali ya zinaa kwa kasi zaidi.
Kwa upande wa akina Baba nao wanaojiuza wanaitwa Mashoga. Yaani ni vitu ambavyo hata kuvielezea lazima uone aibu maana siyo vitu vya kawaida kuvisikia, maana vinazidi hata unyama. Kwa mfano; mimi sijawahi kuona mnyama dume anamtafuta dume mwenzake, au mnyama jike anapoingia katika joto lake hawezi kumtafuta jike mwenzake. Sasa hawa wanaume wanaotafutana wako katika upande gani? Wafanyao mambo hayo wote wanadhambi sawa na wafiraji maana watenda hayo kinyume na maumbile (rej. Rum 1:24-27; 1Tim 1:10). Kwa hiyo mwanadamu anayeweza kutenda vitendo ambavyo asili (nature) yenyewe inakataa, hiyo moja kwa moja ni kazi ya shetani.
Kadhalika mtu huyo haanzi mara moja tu, bali tabia hii mbaya inaanzia angali mdogo sana. Hii imewaathiri zaidi wale watoto tunawaita wa geti kali, kwamba ni mtoto yeye ni wa kutoka na kwenda sehemu kwa kupelekwa na baada ya shughuli anarudi aidha kama ni mwanafunzi. Kumbe kumjengea mazingira hayo ya kumbana sana, inafika hatua wazazi wanapokuwa wametoka na kwenda sehemu basi nao wanabaki wakifanya yao. Kumbe chimbuko lake mara nyingi yanaanzia ndani ya familia kulingana na mazingira aliyopitia katika makuzi yake. Mfano; unakuta ni binti tayari ameshaolewa, ila kila anapofanya tendo la ndoa lazima amwambie mmewe tena kufanyika kinyume cha maumbile. Kumbe wito wangu kwa wazazi na walezi wawe makini na malezi wanayotoa, kumbana mwanaye siyo suluhisho la yeye kujiepusha na majanga ya sasa bali kumfanya atafute namna nyingine ya kuweza kujituliza na mahangaiko yake.
Pia kuna suala la usafirishaji haramu wa binadamu. Hili nalo liko mbioni kustawi kama nyasi, maana kasi yake ni kubwa sana ya namna ya ushawishi. Tusiwe watu wepesi wa kuamini kila mtu, ndiyo maana tunaaswa kuzijaribu roho, kwani siyo kila mtu ni mwema au anakuwazia mazuri; wengine wanakuwazia mabaya daima na furaha yao ni kuona umeshindwa (rej. 1Yn 4:1). Sasa tumefika mahali mtu anakwambia nataka nikupeleke nchi ya Oman ili uwe unanisaidia kazi za biashara, sasa unachokosea hauulizi hata swali; ila unachojua na kufurahia ni kwamba unaenda nje ya nchi. Sasa matokeo yake uliyemwamini akiishakukufikisha anakupa kazi za kukudharirisha mara ya biashara ya ngono, mara kufanya kazi za ndani kama kijakazi; kwa kuwa huna namna wala jinsi unapambana na hali yako huko. Tahadhari kwa wote, tafadhali tusiwe watu rahisi kiasi hicho cha kuonyesha ushamba uliopitiliza. Mwisho wa siku umetolewa huku ulipokuwa unafanya kazi kwa amani na kulipwa vizuri, sasa unakwenda kufanya kazi bila amani na malipo yako ni majaliwa kuyapata. Wakijua ukilipwa tu basi unaweza kurudi nyumbani, hivyo wanaamua kukukomoa. Sana sana hii imeathiri vijana wadogo ambao wanapelekwa nchi za kiarabu wakiahidiwa kwenda kufanya kazi fulani, ila wafikapo hukuta mambo yako tofauti na matazamio yao; tujiepushe na tamaa zisizo za msingi. Tujihadhari sana maana ni ukiukwaji hata wa haki za binadamu kumgeuza mtu kuwa kama biashara au bidhaa, yaani unaamua kumuuza au kuuza utu wake.

6.4  Imani potofu

“Basi Imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.”[73] Lakini katika Imani potofu inautofauti juu ya yale wanayoyaamini, kwani yako kinyume na mipango ya Mungu. Kwa nini nasema hivyo? Kwa sababu ni kupitia Imani potofu tunasikia mauaji, mafarakano baina ya familia, ambapo vyote hivyo vinakinzana na mpango wa Mungu.
Matokeo ya Imani potofu kwanza ni uchochezi wa mauaji. Tunasikia mauaji ya aina mbalimbali yanayohusisha Imani potofu za kishirikina. Mfano; mkoa wa shinyanga mara kadha zimekuwa zikitolewa taarifa za mauaji ya vikongwe wenye macho mekundu, kwa tuhuma za kuwa wao ni wachawi. Pia mauaji ya ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi yaani Albino, kwa tamaa ya kupata mali kupitia baadhi ya viungo vyao kukatwa au kuondolewa kabisa. Lakini pia tumesikia mauaji yanayosababishwa na ushirikina ikidaiwa kuwa kwa kupata kiungo fulani cha mtu utapata mali nyingi sana.
Haya yote yamechangia katika kuchelewa kwa upatikanaji wa maendeleo ya sehemu husika, maana nguvu kazi yenyewe ndiyo inazidi kuteketea. Sasa tujiulize kupitia vitendo hivyo je! kuna kweli ndani mwake? Licha ya kwamba uchawi hata Biblia inautambua kuwa upo (rej. Ufu 22:15), japo siyo kwa mantiki hiyo inayotumia mauaji eti kujipatia kitu fulani.
Pili ni kudorora kwa maendeleo. Ni katika Imani potofu sasa watu wanaimani katika ushirikina, hivyo kuna sehemu mpaka sasa kama unajipenda huwezi kujenga nyumba ya bati. Utaambiwa ukiijenga tu huwezi kumaliza siku nyingi lazima wakuloge, ili wakuone sasa mali zako utaziachia nani na kufanya wote mwonekane kama kitu sawa ndani ya jumuiya. Na wanasema maneno yanaumba, kumbe kuna vitu vinatuharibu hata kisaikolojia. Mtu anapokwenda kwa mganga wa kienyeji anaweza kuambiwa ukikutanisha macho na mtu fulani basi lazima uanguke chini kwa sababu ndiye mbaya wako. Sasa kwa kuwa maneno yanaumba na kuchanganya na hali ya kisaikolojia, kweli lazima hali itokee hivyo nawe upate kuamini. Kwa hiyo unakuta ni kama unachezewa mazingaombwe tu au viini macho.
Imani potofu inaenda mbali zaidi kwani kila mtu anayo namna ya kufikiri na kuelewa mambo, kama ambavyo Pd. Titus Amigu anavyoeleza katika kitabu chake cha Ushirikina na Imani potofu. Kuna imani kali  zilizosambaa kati ya watu. Mtu akiamka amechoka asubuhi anasema “wachawi” wamemfanyiza kazi labda amebebeshwa mizigo kama punda au kulimishwa shamba la mwingine. Wengine wanaamini kwamba  gizani wamejaa wachawi, na hivi usiku si wakati mzuri kwa mtu. Wengine wanaamini kwamba bundi, fisi na mbweha ni mifugo ya “wachawi”. Wengine  wanaamini kwamba mtu kutembea uchi usiku ni kitendo cha uchawi. Wengine wanaamini vigezo vingi vya “wachawi” hasa macho mekundu, kibiongo, mapengo, kilema na uzee mkubwa. Haya yanawatia watu hofu na hivyo wanaanza kuumwa kimwili au kisaikolojia.
Kama imani, wapo wengi wanaosadiki kila hadithi inayosikika juu ya uchawi na ushirikiana. Kumbe hadithi nyingi zinazosimuliwa ni za ubunifu tu. Ukikaba uthibitisho utagundua mambo. Hadithi zingine hazina hata majina ya wahusika. Zingine hazitaji tarehe wala mahali zilipotokea. Labda kuna mahali watu walifungukiwa mlango mlimani wakaingizwa ndani kujifunza kitu fulani. Ukiuliza wapi na nani walikuwepo, utazungushwa tu.
Bado chini ya imani kuna mambo mengi wanayoamini watu katika njaa yao ya kujipatia nguvu za pekee za pekee tu. Utawasikia watu wakisema kwamba kuna watu wanaruka usiku, wengine kwa nyungo, wengine kwa fisi, wengine kwa kuingia ndani ya pembe ndogo. kuwa na televisheni. Mambo mengine yanayowafanya wengine waamini kwamba kuna “uchawi” ni matendo ya vichaa tu. Utasikikia nimemwona mtu akikimbia msituni kwenye miiba bila kujali. Au kwamba amemwona mtu akijikatakata na kujitoa damu. Sasa mambo kama haya ni matendo ya kichaa. Ubongo wa mtu una mawimbi aina nne: alpha, beta, gamma na delta. Mawimbi haya yakitibuliwa kwa sababu ya ugonjwa au kemikali fulani mtu huonesha tabia za ajabu ajabu, tabia ambazo kwa waoga husema ni mambo ya kichawi. Kumbe si hivyo. Zaidi ya hayo, kuna wengine hudhani kuna uchawi kwa sababu ya kujikuta usiku wakipigwa, kukatwakatwa au kufukuzwa na watu au viumbe visivyojulikana au pengine vinavyojulikana kabisa. Kumbe hizo ni ndoto maalumu tu. Jina la ndoto hizo za kutisha ni majinamizi, nazo zisichukuliwe kama ushahidi wa uwepo mambo ya “kichawi”. Ni mtindo mwingine wa ubongo kufanya kazi kwa fujo kunakotokea usiku usingizini. Mambo ya kwenye mtima hujiibusha kwa fujo kutokana na kuchozwa kwa ubongo ama na ugonjwa au kemikali zenye athari.
Mambo mengine chini ya imani ni mambo ambayo msingi wake ni kudhaniana kusiko na misingi ye yote ile. Hapa utawakuta watu wakituhumiana vijijini na mijini. Karibu kila mwenye mambo ya kushangaza anadhaniwa ni “mchawi”. Mzee aliyeishi kuwashinda wenzake anadhaniwa “mchawi”. Mtu mwenye mapengo makubwa anadhaniwa “mchawi”. Mtu mwenye kibiongo anadhaniwa “mchawi”. Mtu mwenye macho mekundu anadhaniwa “mchawi”. Mtu mwenye masikio au vidole na kucha za ajabu anadhaniwa “mchawi”. Na kwa jinsi hii, kikitokea kitu cho chote kikubwa na kushangaza watatuhumiwa hao wanaodhaniwa kuwa “wachawi”. Mtindo huu wa mambo si mzuri kwani unawaonea watu pasipo ushuhuda wo wote.
Halafu chini ya imani kuna mambo mengi tunayoyasikia au kuyaona yaliyo mapato mabaya ya kuchanganya imani hasa upagani na Uislamu. Katika upagani watu wanasadiki kwamba kwenye giza wamejaa “wachawi” na hao wanatembea huko na huko kuwanga nyakati zote za usiku. Wapagani wanaendelea kusadiki kwamba usiku “wachawi” wanaruka kwa nyungo, mikeka, pembe ndogo ndogo, wanawapanda fisi kwa tumbo na kadhalika. Si hayo tu bali kwamba usiku “wachawi” wanaitana kwa milio ya filimbi ambazo ni sehemu za siri za wanaume. Pia kwamba wanafanya mikutano ya kupanga kuwaloga watu na kufanya karamu za kula nyama za watu. Haya anapoyasadiki Mkristo anachanganya imani. Ukristo haufundishi wala kuamini katika mambo kama haya. Uislamu unawaambia wafuasi wake kwamba uchawi umefundishwa duniani na malaika Haruti na Maruti. Wenyewe wanasema kwamba kiasi kilichofundishwa na malaika hawa ni asilimia kumi tu. Kwa hali hii, Waislamu wenyewe huulizana, mambo yangelikuwaje kama huo uchawi ungelifundishwa asilimia zote mia.
Mwishowe chini ya imani ni taarifa mbalimbali za filamu, video, magazeti na maelezo ya watoto. Kuna mengi ambayo watu wanasadiki kwamba yapo kutokana na filamu, video, magazeti na maelezo ya watoto. Wengine wakiona picha za ajabu ajabu za filamu au video hudhani kwamba picha hizo ni ushahidi wa uwepo wa “uchawi”. Watu hawa hawayajui mambo ya kompyuta. Kompyuta inaweza mengi sana. Inaweza kutumiwa kuunganisha picha mbili zisizohusiana kabisa. Ndipo inaweza kuweka pamoja picha mbili. Alipo mtu unaweza kuona baada ya muda mfupi pana nyani. Au unaweza kumwona mtu ndani ya chupa na kadhalika. Haya yote ni ufundi wa kuunganisha picha kwa haraka na wala si ushahidi wa uwepo wa “uchawi’. Hali kadhalika video.
Mintarafu magazeti wala hakuna lo lote la pekee. Watu wanaweza kuzusha habari za kutisha na vile vile kuziambatishia picha za kutisha. Tufahamu wote kwamba magazeti ni miradi. Kila habari inayowavutia watu inaweza kununuliwa ili kulifanya gazeti liuzike sana. Magazeti hasa yale yanayoitwa ya udaku mathalani WATU, SANI, JUMATATU na IJUMAA huwa na habari nyingi za namna hiyo.
Maelezo ya watoto nayo yanawapambisha moto baadhi ya watu hapa duniani. Huondokea katika vitambo fulani vya maisha, watoto hujitokeza na kuanza kuzungumzia habari za “uchawi” na matendo ya “wachawi”. Watoto hao husimulie eti wanavyoruka usiku na wazazi au watu wengine kutumia fursa hiyo kuwaloga binadamu wenzao. Maelezo ya watoto kama haya huwafanya  watu wengine waamini katika uwepo wa “uchawi” wakati si kweli. Kama tulilolisema kuwahusu wakubwa, tunasema hilo hilo kuhusu watoto.  
Ubongo wa mtu, hata ule wa mtoto mdogo hufanya kazi katika mawimbi aina nne: alpha, beta, gamma na delta. Kumbe mawimbi haya yakitibuliwa kwa sababu ya ugonjwa au kemikali fulani mtu huweza kuzungumzia habari ya ajabu ajabu, habari ambazo kwa waoga husema ni ushahidi wa mambo ya kichawi. Kumbe si hivyo. Wafuatilie watoto hao hao baada ya miaka walao ishirini, uwaulize habari hizo hizo, watakukatalia na wataonea aibu kuhusika nazo. Wengine wanaweza kukasirika kabisa ukiwaulizia habari walizozisimulia wakati wa utoto wao kwani hakumbuki lo lote ukubwani mwao. Mimi ninamfahamu walau mtoto mmoja ambaye alipokuwa na umri wa miaka mitatu hivi alikuwa akisema mambo ya ajabu ambayo hata sisi wakubwa hatukuyajua ameyapata wapi. Kumbe baada ya miaka ishirini hivi, tulipomuuliza habari zile zile alikuwa akikasirika sana kwa vile alikuwa hakumbuki lo lote katika hayo tuliyomwambia kuwa alikuwa akiyasema.
Pilikapilika
Chini ya pilikapilika, kuna pilikapilika nyingi ambazo msingi wake si lo lote isipokuwa elimu ya siri. Watu hujielimisha habari za siri kama vile vitu vinavyowavuta ndege kama bundi na njiwa, wadudu kama siafu na nyuki na wanyama kama vile nyoka na simba. Basi elimu hizo za siri ndizo hutumika kufugia au kuwaleta bundi, njiwa, siafu, nyoka na simba mahali. Bundi hupenda mwanga na harufu za mizoga, hivi hufika po pote penye vitu hivyo. Mwanga huwasaidia kuona panya na harufu huwasaidia kujua kilipo chakula. Hivi anapoumwa mtu sana, si mara haba bundi kufika. Hufika hapo si kwa ajili ya mgonjwa aliye mahututi bali kwa ajili ya ule mwanga ambao wauguzaji huwa nao. Yeye huja apate kusaidiwa kuwaona panya. Aidha hufika hapo kwa sababu mara nyingi mgonjwa mahututi haogeshwi na kwa namna hiyo anatoa harufu ambayo bundi hudhani ni mzoga wa kula. Basi mahali kama hapo akifika bundi na kuimba wauguzaji hudhani ameletwa na “wachawi”. Vivyo hivyo mgonjwa mwenyewe. Kumbe kwa dhana hiyo, mgonjwa hujipandishia msukumo wa damu (BP) na kumfanya asifike asubuhi. Ndipo mgonjwa akifa, wauguzaji na jamaa huanza patashika ya kumsaka “mchawi” aliyemuua mgonjwa. Wapi na wapi! Njiwa hufugwa kwa chakula. Nyoka na simba huletwa mahali kwa majani yanayonukia kama nyoka au simba jike. Kwa kuvuta nyoka huko Iringa hutumiwa majani ya mti unaoitwa mgegeluka. Kwa simba kuna majani yake. Kwa siafu ni chakula kile wanachokipenda. Kwa nyuki ni mpako wa asali yao. Mambo ya elimu ya siri hayaishii kwenye kuwaita ndege na wanyama tu. Wawindaji hujua kwamba kila mnyama dume ana eneo la milki yake. Ukipiga mluzi wa aina fulani mwenyewe atakuja pale kuangalia nani anatia fujo. Hapo mara hupigwa risasi au kupigwa mshale au mkuki. Aidha vifaru huchukia moto na ukiuwasha ni sharti waje kuuzima. Nyati huchukia mlio wa aina moja kwa mfano mungurumo wa gari linalozizima. Bais moto humvuta kifaru na mungurumo wa kuzizima humvuta nyati.
Katika kutabiri mvua, mambo ni ya namna hiyo hiyo. Wanaojidai kutabiri mvua hutaza mawe. Wakiona yana unyevu, huwaalika watu watolee sadaka. Kumbe ule unyevu ndio unaowaambia kwamba anga na mawingu yamejaa unyevu ambao punde utaanguka kama mvua. Kwa hali hiyo wao hawanyeshi mvua ye yote isipokuwa ni mabingwa wa kujua lini mvua imekaribia kwa kadiri ya maandalizi aliyoyafanya Mungu mwenyewe. Mvua ni chini ya Mungu mwenyewe na wala si chini ya binadamu fulani. Ndiyo maana wale wanaojifanya wanyeshaji mvua, hawawezi kufanya lo lote jangwani, mathalani huko Sahara, mahali ambako Mungu haandai mvua kama anavyofanya katika sehemu nyingine za dunia. Hatimaye, elimu ya siri ndiyo inayotumika katika utengenezaji wa televisheni zile zinazoitwa za asili. Wakati baadhi wakitumia nuru za maji, vioo na vivuli wengine hutumia pombe kali. Basi katika maji au vioo taswira hubanwabanwa na kumghilibu mtazamaji aone kile alichoambiwa atakiona. Zile televisheni za asili zinazotengenezwa kwa pombe kali huwalewesha watu. Kutokana na kulewa, watu huona mambo yasiyokuwapo katika uhalisia.
Chini  ya pilikapilika kuna mengi yaliyo na msingi wake katika matisho ya waoga. Lishe ya mambo ya kishirikina ni woga. Mtu anayesadiki katika mambo ya kishirikina huwa “amelogeka” walao kwa asilimia hamsini. Mtu anayemwogopa mtu fulani, akioneshwa kidole na yule anayemwogopa au akiambiwa naye, “kesho utakufa”, hushikwa na kihoro na kihoro hiyo hugeuka ugonjwa wa mwili au wa moyo wa kumkatishia maisha yake. Woga unaua. Kwa Waislamu hilo ni wazi kabisa. Shughuli za albadiri (dua mbaya) hupata nguvu katika woga wa mlengwa. Mwislamu akiambiwa atasomewa albadiri, hushikwa na kihoro cha mwaka. Halafu akisomewa kweli, huvunjika moyo na kudidimia nguvu yote. Ndipo mtu hufa. Kumbe kwa watu wasio Waislamu, labda Wakristo wasiokuwa na woga huo, albadiri hushindwa kabisa kufanya kazi kwani haiwatishi hata kidogo. Katika woga, watu wanaogopa mengi. Ukimchukua chura ukamfunga kitambaa chekundu kiunoni na kumweka chumbani kwa mwoga atashikwa na woga mkubwa kabisa. Kesho yake ukimwekea mjusi aliyefungwa miguu na kuwambwa msalabani mwoga atatishika mno. Asubuhi yake ukimwekea budi aliyevikwa shanga shingoni, hata kinyesi kitamtoka. Ukizidi hapo ukamwekea furushi lililochomekwa manyoya marefu, mtu yule atatishika hata kiasi cha kuhama kijiji au mji.
Kuna pilikapilika zingine ambazo msingi wake ni matumizi ya mapaji ya pekee ambayo wachache wamejaliwa hapa duniani. Kuna watu fulani fulani mathalani hawadhuriki na nyuki hata wakiumwa na nyuki elfu. Aidha wapo wengi hata wakipigwa na umeme volti 380 hawadhuriki. Idadi ya watu hao ni ndogo sana, labda mmoja kati ya elfu. Wakiamua kutumia mapaji ya namna hiyo kwa manufaa yao huweza. Hakika watu kama hao huweza kufanya vituko kadha wa kadha ambao sisi wengine huhitimisha kwa dhana ya kwamba ni “wachawi”.  Wasiodhurika na nyuki huweza kulala hata na nyuki au kuwachukua nyuki katika magunia kana kwamba wamechukua inzi. Wale wasiodhurika na umeme wa kiasi kikubwa kama nilichokitaja huweza kuchezea nyaya za umeme kiasi cha kutustaajabisha wewe na mimi na hata kutembea juu ya waya wa umeme bila viatu. Basi wengine wanapoyaoona mambo kama hayo hutishika na kwenda huko na huko kutangaza kwamba wameupata ushahidi wa uwepo wa “uchawi”  kumbe sivyo.
Katika pilikapilika kuna mambo mengi tunayoyasikia au kuyaona yenye msingi wake kwenye mbwembwe zilizoongezwa kwenye dawa za kawaida tu. Dawa za asili si mbaya kwa zenyewe. Mungu ameziweka kwenye majani, miti, mizizi na vyakula ili zitutibu na kuturejeshea uzima uliotetereka. Hakuna mtu mwenye busara anayeweza kuzidharau (rejea YbS 38:1-14). Hata hivyo kuna waganga wengine wanaoongeza mbwembwe nyingi na za kutisha ili waongeze bei ya dawa zao na wao wenyewe wajipatie umaarufu. Dawa ya tumbo la kawaida la kuhara ni pamoja na kutafuna majani machanga ya mpera na kunywa maji yaliyochanganya kidogo na udongo wa mfinyanzi. Lakini kwa dhamira ya faida binafsi, waganga wengine huanzia kwenye kuwaeleza watu kwamba wametiwa vitu mwilini, machoni au masikioni. Ndipo unapoweza kuwasikia watu wakiambiwa eti wametiwa mahindi machoni, au misumeno magotini, au vyungu matumboni na watu wanapikia pombe humo. Basi waganga hao hujidai kufanya madhehebu ya kuvitoa vitu hivyo pale wanaposema vimewekwa. Kwa kelele, kuimba na miruko wanafanya udanganyifu wa kutoa mahindi machoni, au msumeno magotii au vyungu matumboni. Ajabu ya watu tunaoamini ushirikina ni jinsi tunavyoshindwa kujiuliza maswali mengi. Chukulia suala la mtu kuwekewa kitu mwilini. Mbona mtu ukiingiwa na mchanga mdogo tu machoni, huwi na raha hadi mchanga huo upulizwe nje? Mbona mtu ukichoma mwiba mdogo kidoleni, huwi na raha hadi mwiba huo mdogo utolewe? Iweje basi mtu awe na punje za mahindi machoni au msumeno gotini na chungu cha kupikia pombe tumboni. Tunaaminije jambo kama hili?
Katika pilikapilika kuna mambo mengi tunayoyasikia au kuyaona yenye msingi wake kwenye namna za kuloga. Utawakuta watu wakijaribia kuwaloga wengine. Kati ya formula zilizopo za kuloga nyingi zinatumia vitu vya yule anayekusudiwa kulogwa, mathalani mate yake, nywele zake, nguo zake na kadhalika. Au zinahusisha vitu vilivyogusana naye, mathalani mchanga alioukanyaga na kuacha nyayo au maji aliyoyaoga. Vitu kama hivyo wakivipata, wenyewe wanaojidai walozi, huvifutika kwenye kitambaa na kuvidunga sindano huku wakitoa dua mbaya, kwa mfano, “Huyu mtu apatwe na kifo ghafla” au “Huyu mtu apatwe na maradhi yasiyopona, augue na kuugua””.
Basi kwa ajili ya kubahatisha kuloga hivyo, utawaona au utasikia jinsi watu wanavyotafuta vitu vya wenzao kama hivyo tulivyovitaja sasa hivi. Wengine wanachotwa mate usiku, au wanakatwa nywele usiku au nguo zao hasa zile za ndani zinaibiwa, nyayo zao za mchangani zinachotwa au maji waliyoyaoga yanachotwa huko bafuni au chooni. Sasa, ndugu yangu, ukiyaona au ukisikia mambo haya yanatendeka usidhani kuna nguvu zo zote za pekee hapo. Ni kusumbuka na upepo tu. Hakika kama mtu akavichukua vitu vyako na kufanya hivyo, wakati wewe huna habari, huwezi kudhurika wala chembe. Lakini ikiwa umegombana na mtu na mtu yule amekutisha hadharani wakati wewe unaoogopa mambo ya kishirikina, nakwambia utaanza kweli kuugua. Utaanza kuugua, si kwa sababu ya nguvu ya pekee isipokuwa kwa sababu ya woga wako mwenyewe. Kifupi, utaanza kuugua kisaikolojia kwani chakula au mbolea ya mambo ya kishirikina   ni woga wa yule anayetishwa. Anayetishwa akiwa mwamba wa kujiamini matisho yale huwa kama ngumi ya mtoto ukutani. Basi uwe mwamba wa kujiamini, ndugu yangu.
Wengine huhangaika sana wakiona nywele zao zimenyolewa usiku au nguo zao za ndani zimetoweka. Hupita huko na huko kuulizia. Kwa vyo vyote, ndugu yangu, ukipatwa na mambo kama hayo ujue mtu anayekufahamu au mtu aliye karibu nawe nyumbani au chumbani amehusika. Kama unataka kumwita “mchawi wako” wala usimtafute mbali. Ni huyo huyo mwenzi wako au jirani yako. Huyo huyo yumo katika mradi mbaya dhidi yako! Mtu wa mbali asiyekufahamu au kukukaribia hawezi kukufanyia vituko kama hivyo. Wala wewe huwezi kwenda mbali kama New York, usiku na kufanya vituko kama hivyo. Au mtu asiyeishi Washington au Marekani hawezi kumfanyia Raisi wa Marekani vituko kama hivyo. Hata White House yenyewe ilipo haijui! Au hawezi kumfanyia Malkia wa Uingereza, hata Birmgham Palace yenyewe ilipo hajui!
Tuzidi kuongea. Katika pilikapilika kuna mambo mengi tunayoyasikia au kuyaona yenye msingi wake kwenye mazingaombwe. Unajua, mazingaombwe yakiwa rasmi wanaoyafanya hujipatia fedha za viingilio wanapoyaonesha. Wafanya mazingaombwe wanafanikisha shughuli zao kwa njia tatu. Kwanza kabisa, wao huua macho ya watu yasiweze kuvifuatilia vitendo vyao vya kijanja. Basi ukiwaona wanawakazia watu macho na kusema, “pache pu” wanakusudia hilo. Nakwambia hawaanzi kucheza mazingaombwe yao mpaka hilo la kwanza lifanyike. Kwa watoto hili linafanyika kirahisi sana. Kisha kuyaua macho, wanakuja na la pili, ndiyo kufanya vitendo kwa haraka sana. Wao wanaweza kuyafanya mambo mawili au matatu wewe katika kufiwa macho ukaona kitendo kimoja tu. Kishapo kuna la tatu lao. Ni matumizi ya dawa fulani fulani, lakini si dawa zenye nguvu za ajabu sana. Wao huweza kuwa na dawa kwa mfano inayomletea mtu usingizi na hiyo hiyo kumtia kichefuchefu kiumbe. Dawa kama hiyo hutumika sana katika michezo na nyoka. Mtoto mdogo anaweza kupakwa dawa hiyo na kulala. Ndipo nyoka huweza kuanza kummeza mtoto yule. Lakini dawa ile ile itamtia nyoka kichefuchefu na hivyo kumtampika mtoto mara moja. Hayo yote yanatakiwa yatendeke ndani ya dakika 45. Muda ukizidi hapo au dawa ikiwa imeisha nguvu yake, maana yake mtoto amekwenda na maji. Kwa hali hiyo maandalizi ya mchezo kama huo lazima yafanyike kwa makini na ubora wa dawa lazima uhakikishwe. Pamoja na dawa za namna hiyo ni matumizi ya vitu vya kudanganyia. Kati ya vitu hivyo ni taa za rangi mbalimbali, michuzi myekundu ya nyanya, maboksi ya umeme na upindaji wa mikono na viganja. Taa zinasaidia sana katika michezo kama ile ya kumgeuza mtu jinsia, labda mwanaume aonekane kama mwanamke. Michuzi myekundu ya nyanya ndiyo inayotumika sana katika michezo labda ya kuchinja watu au wanyama. Maboksi ya umeme ndiyo inayotumika katika kuwashitua watu na kadhalika. Basi hayo ndiyo mambo ya mazingaombwe ya hadhara wanayolipia watu. Na haya huweza kufundishwa mashuleni watu wakajifunza. Kabla na hata wakati wa Yesu, watu waliweza kujifunza hayo huko Misri na siku hizi ukitaka unaweza kwenda kusomea huko jiji Brazaville, Kongo.
Kumbe, kuna mazingaombwe mengine ambayo watu wabaya wameyagundua wenyewe kwa utundu wao. Hayo huyaficha na huamua kuwatishia au kuwahangaishia wenzao. Hayo basi si nguvu zo zote za pekee. Mifano michache ni kama ile ya kuona mtu amegandishwa kitini au mawe yakirushwa na kudondokea mahali fulani. Kugandishwa kitini kunafanyika kwa kughilibiwa mawazo yako na matumizi ya gundi kidogo. Kurushwa kwa mawe kunafanika kama kawaida ila watu mnasadikishwa kwamba yanakotokea hakujulikani. Mkiwa makini na kupima mlalo wa jiwe linaloruka, mnaweza kugundua mara linakotokea na mkichunguza vyema mtamwona anayerusha.
Kuna bado mengi ya kusema au kuandika. Usichoke sikiliza au soma.Katika pilikapilika kuna mambo mengi tunayoyasikia au kuyaona yenye msingi wake kwenye sarakasi.  Ukisikia habari za watu kutembea juu ya paa usiku, usihangaike ni kitendo cha sarakasi tu. Wala hakuna nguvu ya pekee ye yote. Watu hutumia rungu za mianzi mirefu walizoviringishia nguo au matambara au huwaweka wanayamba wadogo waitwao komba kufanikisha hilo. Kwa rungu mwanadamu anaweza kuigiza hatua hizo au komba akitembea juu ya paa, hatua zake utadhani zinafanywa na binadamu. Hilo ni jambo la ajabu, lakini halina nguvu za pekee ndani yake kiasi cha kwamba wewe ushtuke. Na kumtoa nje binadamu aliyelala ndani wala hakuhitaji nguvu za pekee. Kuna mbinu kadhaa. Mojawapo ni kumwinda mtu anayeota ndoto za kutembea afanye hivyo siku unapotaka watu wajue. Unajua kuna wengine hutoka nje wenyewe na kutembea huko na huko wangali usingizini. Hawa watu wazuri kwa mradi wa kuwatoa watu nje ya nyumba usiku. Wanatoka nje wenyewe, kusifiwa wanasifiwa watu wanaodhaniwa kuwa wachawi! Lingine ni kuingia ndani ya nyumba ya mkusudiwa kungali mapema bado. Akifunga mlango wake na kulala, wewe ifikapo saa za manane, unafungua na kumtoa nje. Kama hajalala vizuri unamwongezea dawa ya usingizi ya majani au ya madukani. La sivyo ni kuufungua mlango wa mkusudiwa usiku wa manane. Kufungua wala hukufanyiki kwa matako kama wanavyodai wavumishaji wa habari kama hizi. Kufungua milango kunafanyika kwa funguo bandia au kwa vijijini ambako milango hufungwa kwa miti, ni kitendo cha kujua namna ya kuondoa miti hiyo tu. Kwa sarakasi kama hizi, mtu anahitaji kumfahamu sana yule mkusudiwa, mahali anapolala na jinsi anavyochoka. Kifupi, mkusudiwa na mazingira yake lazima vifahamike sana ili mkusudiwa afanyiwe “timing”. Bila “timing” sarakasi kama hizo hazifanikiwi. Mintarafu usingizi, kila mtu hulala usingizi kwa kusiganisha uzito. Mtu anaanza usingizi mzito kwa masaa mawili, halafu usingizi mwepesi kwa masaa mawili na kuendelea. Ndipo kwa kawaida, kwa walio wengi, usiku wa manane ndiyo wakati wa usingizi mzito. Hapo hata wezi wanajua na huweza kufanya vituko vyao vya wizi. Sasa kama wezi wanafanya vitimbi kwa “timing” tutashindwa mimi na wewe tukikusudia kumtisha mtu tunayemkusudia!
Zaidi ya haya niliyosema, ndugu yangu, katika pilikapilika kuna mambo mengi tunayoyasikia au kuyaona yenye msingi wake kwenye masharti magumu. Jambo hili wala halihitaji maelezo marefu. Unaweza kusikia mambo ya ajabu ajabu ambayo ndani yake hakuna lo lote. Mtu anaweza kupewa dawa akaambiwa: “Unapotumia dawa hii, mtoto wako asilie” au “Mkitaka kushinda mechi ijayo, kwanza usiku mkalale makaburini na kishapo wakati mnaingia kiwanjani  msigeuke nyuma au msipitie mlango mkubwa bali rukeni ukuta kwa upande wa kulia mwa goli”. Au unaweza kusikia: “Mkitaka kufaulu mtihani mtafute paka mweusi umtoboe macho” au “ Weka mfukoni mwako kipande cha sanda ya marehemu wa mwisho kuzikwa kijijini kwenu” na kadhalika. Sasa haya yote na mengine ya namna hii, hayana ndani yake nguvu ye yote ya pekee ni kufukuza upepo tu.
Basi ukimwona mtu anahangaika mtoto wake asilie, usidhani kuna lo lote la pekee nyuma yake, ni kama hivyo amepewa sharti gumu na mganga wa kienyeji tu kusudi mambo yasipoenda sawa na dawa aliyotoa mtumiaji amtwike lawama mtoto wake atakayelia.
Basi ukiwaona watu wanahangaika kulala makaburini kabla ya mechi, usidhani kuna lo lote la pekee nyuma yake, ni kama hivyo wamepewa sharti gumu na mganga wa kienyeji tu kusudi mambo yasipoenda sawa na dawa aliyotoa watumiaji wamtwike lawama mwenzao fulani atakayekataa kulala makaburini.
Hali kadhalika ukiwaona wachezaji wanahangaika kuingia kiwanjani pasipo kugeuka nyuma, usidhani kuna lo lote la pekee nyuma yake, ni kama hivyo wamepewa sharti gumu na mganga wa kienyeji tu kusudi mambo yasipoenda sawa na dawa aliyotoa watumiaji wamtwike lawama mwenzao atakayegoma au atakayeshindwa kufuata sharti hilo.
Ama ukiwaona wachezaji wakikataa kupitia mlango mkubwa na badala yake wanaruka ukuta kwa upande wa kulia mwa goli,  usidhani kuna lo lote la pekee nyuma yake, ni kama hivyo wamepewa sharti gumu na mganga wa kienyeji tu kusudi mambo yasipoenda sawa na dawa aliyotoa watumiaji wamtwike lawama mwenzao atakayekataa au kushindwa kufanya hivyo.
Aidha, ukimwona mwanafunzi au wazazi wa mwanafunzi fulani wakihangaika kumtafuta paka mweusi au ukisikia wamemtoboa macho macho paka mweusi, usidhani kuna lo lote la pekee nyuma yake, ni kama hivyo wamepewa sharti gumu na mganga wa kienyeji tu kusudi mambo yasipoenda sawa na dawa aliyotoa watumiaji wajilaumu wenyewe kwa kile watakachoshindwa kufanikisha kama ilivyoelekezwa na mganga husika.
Mwishowe, ukimwona mtu makaburini anahangaika kutafuta kipande cha sanda au ukisikia kuna mwanafunzi aliweka mfukoni kipande cha sanda ya marehemu wa mwisho kuzikwa kijijini kwake, usidhani kulikuwa na lo lote la pekee nyuma yake, ni kama hivyo alipewa sharti gumu na mganga wa kienyeji tu kusudi mambo yasipoenda sawa na dawa aliyotoa mtumiaji ajitwike lawama mwenyewe kwa kushindwa kutimiza kilichokuwa kigumu.
Ndipo ninakuambia, si mara haba unaweza kuwaona watu au kusikia habari za ajabu ajabu kumbe zilikuwa mahangaiko ya watu kutaka kutimiza yale waliyoambiwa na waganga wa kienyeji. Ndiyo mambo kama ya kuwabaka maajuza au kuwanajisi watoto wachanga, kukata mikono ya maalbino, kuwaua watu waliozaliwa peke yap katika matumbo ya mama zao. Au mambo ya kuzika vichwa vya ng’ombe kwenye machimbo na kuuchukua mayai ya bundi mifukoni. Hayo yote ni pilikapilika za watu wanaotafuta utajiri au bahati kwa kadiri ya ushauri wa waganga wa kienyeji. Kumbe katika hayo hakuna nguvu ye yote ya pekee bali kubahatisha bahatisha tu. Usihangae na habari zake.
Tukizidi kuweka wazi habari za pilikapilika zinazoonekana au kusikika duniani hapa, acha nikuambie kwamba katika pilikapilika hizo kuna mambo mengi yenye msingi wake kwenye mipango ya kughilibu. Kifupi, ninataka nikujuvye habari za ushirikiano watu wanaoufanya na wengine tukababaika. Unaweza kuona au kusikia mganga au mtu fulani anaweza kusema anachoumwa mgonjwa bado akali mbali. Hapo usidhani mtu yule ana nguvu za pekee. Mara nyingi mtu yule huwa amewapanga watu wa kumletea habari za wagonjwa bado wakali mbali. Ukitaka kujua hilo, nenda kwa mganga wa namna hiyo ghafla huku ungali  mzima kabisa. Hapo utaona jinsi atakavyojaribu kukuepa au kubuni buni mengi anayodhani kati yake moja wapo utalikubali kama kweli.
Aidha kwa mipango ya ushirikiano, unaweza kubaini vyema wanachofanya wale wanaojiita “wanyoa wachawi” vijijini. Timu ya watu, mara nyingi vijana wa kiume hukubaliana kumpandisha mmoja wao kama mganga mkuu. Pamoja naye wengine hujidai kuwa wasaidizi wake. Wakipita huko na huko wanakuwa makini sana kumlisha kwa taarifa mbalimbali kuhusu watu au vijiji wanavyotembelea. Kama wakitaka kujidai kufichua vifaa vya “wachawi”, hao wasaidizi ndio wanapita huko na huko kuzika vifaa vyao wao wenyewe kusudi asubuhi mganga wao mkuu ajidai kuvifichua. Basi ni hasa wasaidizi wa mganga wanaomsaidia mganga wao mkuu kuwadanganya watu. Wakitaka kucheza mchezo wa kuongeza fedha kwa mfano, ni wasaidizi wanaoleta fedha zao. Wewe ukiowaona wao wanasaidiwa kwa namna hii au ile, unaweza kudanganyika kwamba wao walikuwa wateja kama wewe na hivyo wamefaulu. Kumbe siyo, fedha ni za kikundi chao wenyewe. Wewe ukiweka au ukitoa fedha zako kuwaiga wao, ndiyo hizo watakazojichukulia kwa kadiri ya mahesabu yao. Usiwafuate watu kama hao, utakuwa mjinga ndiye aliwaye. Kwa maneno mengine, ukiyasikia au kuyaona mengine yakitendeka, ujue ni mchoro wa kitapeli uliokusudiwa utapeliwe wewe.
Mambo mengine ninayotaka kukueleza yanatupeleka karibu mwishoni mwa maelezo yangu kuhusu pilikapilika mbalimbali zilinazopatikana kati ya watu wanaojishughulisha na ushirikina duniani hapa. Ninakwambia hivi, katika pilikapilika za duniani hapa kuna mambo mengi tunayoyasikia au kuyaona yenye msingi wake kwenye kujitafutia nguvu za pekee au bahati. Watu wengi, hasa katika nchi zetu zinazoendelea wamebanwa na maisha magumu. Jinsi ya kujinasua, watu wengi hawajui. Ndipo hujaribu hiki na kile kwa fikra za mlinganisho wakidhani wataangukiwa na “ngekewa”.  Basi wengine utawasikia au utawaona wakinywa damu ya watu au ya paka. Hao hufikiri labda damu ya mtu au ya paka ni ya pekee na huenda italeta bahati. Wengine hubahatisha bahati yao kwenye kuwa, kuvaa au kubeba hirizi fulani. Hapo unaweza kuona hiziri za kila kabila, rangi na urefu. Zote hizo si lo lote. Ndani ya hirizi hakuna kitu kinacholeta bahati. Nini, kijiti, mchanga, kipande cha jiwe, punje ya nafaka, maharage au kunde?, Wengine hubahatisha labda nguvu za pekee zitatoka kwenye kumbaka ajuza fulani au kumnajisi mtoto fulani.
Wengine hubahatisha labda nguvu za pekee zitatoka kwenye ngozi ya binadamu. Basi utawaona hao wakiwachuna wenzao ngozi na kutengenezea hirizi.
Wengine hubahatisha labda nguvu za pekee zitatoka kwenye kujiacha wachafu. Basi hao utawaona wakikataa kuoga au kujitunza katika usafi.
Wengine hubahatisha labda nguvu za pekee zitatoka kwenye viungo vya akinamama. Hawa utawaona wakitafuta kwa udi na uvumba ndevu za akina au kuwakata viungo vyao kama vile via vya uzazi na matiti.
Wengine hubahatisha labda nguvu za pekee zitatoka kwenye viungo mbalimbali vya binadamu. Ndipo unaweza kuwaona au kuwasikia watu wakitafuta mapafu ya watu, au mioyo yao au via vyo vya uzazi au matumbo yao au mifuko yao ya chakula, macho, masikio na kadhalika.
Wengine hubahatisha labda nguvu za pekee zitatoka kwenye vichwa vyenye upaa. Hao ndio wanaotumia vichwa vya binadamu vyenye upaa kuvulia dagaa maziwani au labda kama huku Afrika ya Kusini kulindia stoo zao zilizojazwa bidhaa au mali.
Wengine si kwamba wanatafuta bahati ya pekee ila katika ujanja wao hujisingizia kutoka sehemu zinazoogopwa na watu. Unajua watu wengine huziogopa sehemu fulani fulani za dunia na mtu akisikika kwamba anatoka huko wengine hudhani ana nguvu za pekee. Basi kwa hilo utaona watu wakijisingizia kutoka sehemu kama hizo. Madhalani wapo wanaojisingizia kutoka Sumbawanga, wengine Baria au Gambush, wengine Malawi, wengine Msumbiji na kadhalika. Ukichunguza sana, sehemu hizi si lo lote isipokuwa ni sehemu za nyuma kielimu na kwa hali hiyo watu wake wamelimatia sana katika ushirikina. Hata hivyo, kulimatia huko, hakuwapi nguvu ye yote ya pekee isipokuwa kelele zisizo na maana. Ukiwa mbali utasikia watu wa huko wanaweza kutengeneza mvua au kutuma radi au kuwatega wanaume wanaozini na wake wa watu au kuonesha mambo katika televisheni za asili. Sasa nenda huko huko, uone mambo yalivyo kinyume. Hutakuta mvua ye yote ya maajabu. Utakuta mvua za kawaida na hata ukame unaweza ukaushuhudia. Aidha ukiwaalika waende Sahara wakawanyeshee mvua Waarabu, utawaona wakiinamisha vichwa kwa kukosa uwezo. Radi utazikuta za kawaida kabisa. Ama ukiwaalika waitume moja ikamuue Osama bin Laden wapate dau la dola milioni ishirini waliloliweka Wamarekani, utawasikia wakikuomba uache kuwaonea. Yale uliyoyasikia ya kuwatega wanaume wazinzi, hutakuta lo lote, bali utasikia pia hadithi za wanaume nyamaume wanaomendea wake wa wenzao. Kuhusu televisheni, hutakuta lo lote isipokuwa maji na vioo au pombe kali wanazoleweshana na hivyo kuoneshana maluweluwe. Ukitafuta televisheni ya asili uonee mambo ya Ulaya, wala hutapatia maana. Sasa basi, hayo yanayosikika kuhusu sehemu fulani fulani usiyachukue kama ushahidi wa uwepo wa nguvu za pekee za kishirikina. Ni hadithi zisizo na maana na wewe usikosee usingizi na wala usishiriki kuzieneza, utajiaibisha bure kijana!
Hatimaye niseme jambo la mwisho katika fungu hili la mambo. Ninasema hivi, katika pilikapilika kuna mambo mengine tunayoyasikia au kuyaona yenye msingi wake kwenye ukatili. Hapa ninayaweka mambo kadhaa pamoja. Zile pilikapilika za kusaka viungo vya watu, ukatili ndio unaofanya zitendeke. Mganga akishaagiza kupatikana kwa viungo vya binadamu, pasipo ukatili hakipo kitakachopatikana. Basi ni ukatili kumuua mtu na kuvitwaa viungo vyake. Au ni ukatili vile vile kuvipata viungo hivyo kwa kufukua maiti.  Ni ukatili kuwabaka maajuza. Ni ukatili kuwanajisi watoto wachanga na kadhalika. Ndipo basi habari za kuchunana ngozi, kukata watu viungo na kadhalika msingi wake ni ukatili. Vivyo hivyo habari za kufukua makaburi. 

Sumu: Hatimaye kuna mengine yanayosikika, kuonekana au kusomeka kuhusiana na ushirikina na pilika pilika wanayosadiki wengine kuwa ni mambo ya matendo ya giza wakati ni matumizi ya sumu tu.  Mambo hayo ndiyo yanayojenga fungu la tatu la mambo yanayotuhangaisha wanadamu, hasa sisi Waafrika. Matumizi ya sumu si uchawi kwa maana ya nguvu za pekee ya kutendea mambo ya pekee. Matumizi ya sumu kuwaua au kuwadhuru wengine ni sawa na matumizi ya sumu ya kuulia panya, kunguni, inzi, mende na kadhalika. Matumizi kama hayo tunaweza kuyafanya hata mimi na wewe. Tunapotumia dawa kuulia panya, kunguni, inzi, mende na kadhalika wala hatuna nguvu za pekee na wala hatuitwi wachawi. Vivyo hivyo, watu wanaotumia sumu kuwaulia au kuwasumisha wengine wala hawana nguvu ya pekee ya kutendea mambo ya ajabu na wala jina la wachawi haliwafai.
Ndugu yangu, sumu zipo za aina mbili: za kuua na za kusumisha na kudhuru kitu au mtu tu pasipo kuumaliza uhai. Sumu za kuua ni kali sana. Ninazijua kadhaa na ningeliweza kukutajia lakini sipendi kuchukua fursa hii kukutaji kwani wewe ukiwa mtu mbaya utakwenda kuzitumia na kuwaua watu au kuwasumisha watu. Na ukifanya hivyo, utanishirikisha mimi uovu wako wakati mimi, hadi leo hii unaposoma kijitabu hiki, watu wananifahamu kama mtu mwema. Basi ninakwambia tu kuna sumu kebakeba. Zingine za kuua ndani ya dakika chache. Zingine za kuua baada ya siku kadhaa. Zingine za kuua baada ya wiki, miezi au miaka kadhaa.
Mara nyingi ukisikia mtu fulani amekufa ghafla, kama mtu yule hakufa kwa matatizo ya moyo kama vile shikizo la damu au mshtuko (kwani wengi tunatembea tungali tukiumwa lakini pasipo kujitambua), basi tuhumu mara moja matumizi ya sumu. Humo kwenye vikao vya pombe, chunga sana. Kwenye vikao vya pombe waogope sana maadui zake wenye kucha ndefu au wale wanaoshika “kisonjo” kabla yako. Hao wanaweza kuwa wamechukua sumu ukuchani au kidoleni. Wakitaka kusumisha huweza kuigusa pombe ile kwa ukucha au kidole chenye sumu. Wewe utakapopokea pombe uifaidi, kweli “utafidi” tabaka lenye sumu na hivyo utakapoinuka pale utakuwa umekwishatumbukia matatani. Kwa kuwa wewe utakuwa ndiye aliyelimeza tabaka lile lenye sumu, usishangae ukifa wewe peke yako. Utapokuwa umelinywa lile tabaka utakuwa wakati huo huo umewaokoa wanywaji watakaokufura. Hiki ndicho kisa utasika, “Oh, fulani amekufa, lakini jana tulikuwa tunakunywa naye jioni!” Ndiyo! Ndiyo hivyo tena, ni yeye aliyelifaidi tabaka la sumu.
Sumu zakusumisha, kitu au mtu hafi, isipokuwa hujazwa sumu inayomwathiri vibaya. Ukisikia habari za misekule au ndondocha, kama kweli ipo, basi ndiyo hao watu ambao wamesumishwa na waovu. Kwa sumu ile wanakuwa viumbe dhalili karibu na wanyama na hivyo kuweza kufugika. Kutokana na sumu waliyopewa, misekule au ndondocha huwa ni punguani fulani wasio na uwezo wo wote wa maana. Misekule au ndondocha hupatikana kwa namna mbili, iwapo watu wamekusudia kufanya pilika ya kuipata. Namna ya kwanza ni watu kadhaa kula njama ya kumsumisha mtu. Basi wanajopo hao humsumisha mtu au mtoto waliyemkusudia na kisha yule mtu ataonekana kama mfu. Katika kuzimia huko watu hufanya mazishi ya haraka haraka kumbe wakati wa shughuli hizo  humwiba mtu wao na kuwafanya watu wakazike kitu ambacho si mtu. Pengine mtu huzikwa jioni jioni, na kabla hayajapita masaa sita, wanajopo hulifukua kaburi na kumchukua mtu wao. Itumike njia yo yote ile kati ya hizi mbili, huyu mtu wao akiamka huwa punguani kwa sababu ya sumu kali lakini basi huweza kutumika katika mambo ya kipuuzi kama vile kuiba mchicha, maboga, mboga, matunda bustanini au kauzu na vitu vingine vinavyouzwa katika mabanda dhalili. Misekule au ndondocha ni punguani, ndiyo maana huweza kutumwa kuiba vitu vidogo vidogo kama hivyo. Kamwe hawawezi kuiba vitu vya maana kama fedha katika benki kubwa. Ndiyo maana hujawahi kusikia benki ye yote duniani kwamba imeibiwa kimazingira. Ingekuwa misekule au ndondocha wana uwezo wangelitumwa Marekani kwenda kuiba “midole”  watu wakaachana na umaskini. Lakini, thubutu yake haiwezekani. Kwani hata Marekani kwenyewe wanakujua? Punguani aende Marekani? Kwa njia ipi!
Katika mstari huu wa sumu ambazo si za kuua, yanaingia madawa yanayoitwa limbwata. Wanawake wengine wasiojua kupenda hupita huko na huko wakitafuta dawa za kuwapa wanaume au waume zao ili wawapende wao peke yao. Hakuna lo lote nakwambia. Madawa ya limbwata yapo mengi na yana formula chafu chafu. Kuna madawa mengine yanayofanyika kwa mchanganyiko vya unga au vipande vipande wa mende. Hudhaniwa kwamba kama mende wasivyotoka jikoni, wanaume waliolishwa limbwata hawatacheza mbali na wanawake wao. Ashakumu si matusi, formula zingine huhushisha kupikia nyama au vitu ambavyo mwanamke alivificha au kuviweka kwenye sehemu zake za siri. Thu! Kinyaa!
Basi nisikupatie formula hata moja, isije ukaenda kujaribia. Inatosha nikifunga kwa kusema tu kwamba dawa nyingi za limbwata hazifanyi lo lote. Zile zinazofanya kitu fulani ni sumu tu na wala si nguvu za pekee. Ndiyo maana mtu aliyepewa dawa za namna hiyo huwa “lofa” wa kuzubaa zubaa tu. Na mara si haba utamwona akitoka mate tu na ndipo wanawake wanapoanza kuliwa wanapowaona wanaume au waume zao wakigeuka malofa na hivyo mizigo ya kuwaelemea wao wenyewe.
Ushirikina: Haya haya tuliyoyazungumzia sasa hivi ndiyo yanayoitwa na watu mambo ya kishirikina. Ni mabaya na yanawafanya watu waumwe kwa sababu yanawatia watu hofu. Hofu ya namna hiyo inawafanya watu waoga washindwe kuishi kama wanadamu huru. Wengine waogopa kujifanyia miradi ya maendeleo au kuboresha maisha yao kama vile kwa kujijengea nyumba bora kwa kuhofia “kulogwa”. Wengine wanaogopa kuishi vijijini na kujitafutia maisha kwa kilimo na shughuli zingine zinaweza kustawi vijiji na hivyo huenda kubanana na wengine mijini. Maisha ya mjini pasipo shughuli za kueleweka yanawatengeneza fukara wengi sana. Fukara ndio wanaojaribu kujinasua kwa shughuli za wizi, kuuza miili na shughuli zingine haramu kuzitaja. Basi hapo kwenye hofu za ushirikina panatengenezwa wagonjwa wengi wanaoifanya jamii yetu iugue hivi inavyougua.
Hofu juu ya laana: Wapo watu chungu mzima, hata wasomi wetu, ambao wanasadikishwa kwamba mababu zao wanaweza kuwalaani ama kwamba walikuwa na laana na wao wanafuatwa fuatwa na laana kwa mwendo wa urithi kutoka kwa hao waliokuwa na laana kabla yao. Hofu inayozaliwa katika kipengele hiki ni mbaya vile vile. Yaani kama hofu zingine zinavyodhuru, hofu juu ya laana nayo huzalisha nguvu hasi. Na nguvu hasi humuuguza mtu pasipo haki ye yote. Nani amelaaniwa? Mababu gani wanaweza kuwalaani watu? Laana inamfuataje mtu? Tuache kugonjeshana.
Kwa Wakristo, laana si jambo la kushikiliwa tena. Yesu alikuja kufanya nini kama si kumshinda shetani na matisho yake kama hayo ya laana? Binadamu hawakuahidiwa baraka kwa njia ya ukoo wa Abrahamu (rejea Mwa 12:1-3), yaani wale wanaomwamini Yesu? Basi baraka imejenga nyumba hapa duniani. Kinachotakiwa ni kumwamwini Yesu, kubatizwa na kuifanya baraka idumu nasi. Mbele ya Yesu, hakuna laana tena. Mababu kama walisema kitu cha mwono wa laana wameropoka bure. Kama kuna mtu alitishiwa laana na ye yote hapo kabla mbele ya Yesu matisho hayo yameshayeyuka. Tujiulize tu, kama maneno ya laana yanafanya kazi leo, Yesu alikuja kufanya nini? Au ubatizo una nguvu gani kama hauwezi kutufanya watoto wa Abrahamu na kutuweka huru? Yesu anacheza “madange”? Mbona tunamtania Yesu na kuidogoza kazi yake? Tangu lini Yesu anafanya miradi ya Pwagu na Pwaguzi? Tuacheni matusi!
Hofu juu ya mizimu: Mizimu ni akina nani? Fasili ya neno hilo inasema, ni mababu au wazee waliotutangulia.Wapo watu wanasadiki kwamba tunaweza kufikwa na magonjwa na madhila ya ukame na balaa zingine kama vile wadudu na wanyama waharibifu wa mazao kutokana na wazee wetu waliotutangulia. Lakini kweli hiyo? Kama walipokuwa wanadamu pamoja nasi hawakuweza kutengeneza bakteria na virusi, wakawa wanalalamika wenyewe kupatwa na maradhi ya kutatanisha, uwezo huo wanaupata wapi sasa baada ya kufa kwao? Kama walipokuwa wazima kati yetu hawakuweza kunyesha hata rasharasha, wakawa wanalalamika wenyewe kuharibikiwa mazao yao kwa ukame, uwezo wa kunyesha au kuzuia mvua katika maeneo yetu wanaupata kutoka wapi na kwa jinsi gani? Kama walipokuwa wanadamu pamoja nasi hawakuweza kutewangeneza wadudu na wanyama waharibifu, wakawa wanalalamika wenyewe mazao yao kushambuliwa na wadudu au wanyama waharibifu, uwezo wa kuwatengeneza wadudu na wanyama waharibifu wa mazao na kuwatuma dunia wanaupata wapi sasa baada ya kufa kwao? 
Basi kwa fasili hiyo mizimu hamna bao. Tunajua kwa uhakika kabisa, kwa njia ya mafundisho ya imani yetu kwamba wafu wetu hawazubaizubai mahali fulani peke yao. Wale waliokuwa wema  na watakatifu wapo katika hali ya mbinguni, wale waliokufa na nusu utakatifu wanapitia mateso ya muda katika hali ya toharani wakati wale waliokubuhu katika dhambi na kumkataa Mungu kwa imani na matendo yao wapo katika hali ya motoni kama wafungwa wa Shetani. Sasa walio watakatifu hawana silika ya kutudhuru sisi kwa kututia maradhi ama kutuzuilia mvua. Watakatifu ni roho njema nazo zinatuombea zikitaka wanadamu tujiunge nazo tuufaidi uzima wa milele pamoja na Mungu. Sasa roho zinazotukia mema zitafanyaje kazi ya kututia maradhi na kutuzuilia neema kama hiyo ya mvua!
Roho zilizo toharani zinateseka kwa muda nazo zinataka sana ziombewe na sisi wanadamu. Sasa roho zinazotaka ziombewe zitakufanyaje fujo ya kututumia maradhi na kutuzuilia mvua wanadamu? Huko si kujipiga tikitaka zenyewe? Hatimaye zile roho zilizomo katika hali ya motoni kidomodomo kimekwisha. Ni roho fungwa kwa Shetani? Mfungwa huwezaje kuwadhuru watu nje ya gereza? Wana uwezo gani wa kumtoroka bwana magereza (Shetani)? Roho kama hizo zinasubiri kihoro cha mwendelezo wa mateso ya motoni tu. Basi sisi Waafrika tunaposema eti tuwatulize wazee wetu katika hasira zao kwa kuwapikia ugali au pombe tunajisumbua tu. Ugali wale akina nani?  Mababu zetu katika hali ya mbinguni? Hawahitaji wanashiba kukaa na kumwona Mungu kama alivyo. Ugali wale akina nani?  Mababu zetu katika hali ya mbinguni? Hawahitaji, wanashiba kukaa na kumwona Mungu kama alivyo. Pombe wanywe akina nani?  Mababu zetu katika hali ya mbinguni? Hawahitaji wamekata kiu kwa  kukaa na kumwona Mungu kama alivyo.
Ugali wale akina nani?  Mababu zetu katika hali ya toharani? Hawahitaji, wanatamani kumaliza malipizi yao waende zaa kukaa na kumwona Mungu kama alivyo. Au tena ugali wale akina nani?  Mababu zetu katika hali ya toharani? Hawahitaji, wanakata kiu yao kwa hamu ya kumaliza malipizi yao kwa haraka waende zao kukaa na kumwona Mungu kama alivyo.
Hatimaye ugali wale akina nani?  Mababu zetu katika hali ya motoni? Hawahitaji, wafungwa wa Shetani hawapewi ugali wala maharage. Wao ni mateso kwa kwenda mbele tu. Na vivyo hivyo wala hawahitaji  pombe.  Basi matonge ya ugali tunayowatumia kama sadaka, tunayapoteza bure, heri tule wenyewe. Pombe tunayowamwagia, tunaipoteza bure, heri tuinywe wenyewe. Na ukipima sana sadaka za ugali za pombe zinatangaza ulafi na ulevi wetu wenyewe. Ugali tunaowatupia hao mababu, kama wangelikuwa wanakula kweli hauwatoshi, kwa maana hata kama tonge lingelikuwa kubwa kiasi gani haliwezi kuwatosha wazee wetu ambao ni wengi. Pombe tunayowamwagia hao mababu, kama wangelikuwa wanakunywa kweli haiwatoshi, kwa maana hata kama pombe ingelikuwa nyingi kiasi gani haiwezi kuwatosha wazee wetu ambao ni wengi na wengine katika yao walikuwa walevi kama shimo.
Hakika tuchofanya ni kuwadanganya tu kwani ugali mwingi na “minyama” yake tunakula wenyewe na pombe nyingi tunakunywa wenyewe. Tungelikuwa wakweli tu kwamba vitu hivyo tunajitengenezea wenyewe. Tusiwasingizie wao eti kwamba wanavihitaji. Aheri, tungeliamua wenyewe bila kujionea aibu. Siku moja tujiamulie kwamba tunataka kula ugali, basi tujipikie tujifanyie sikukuu. Siku nyingine tena, tujiamulie  kwamba tunataka kujinywe pombe, basi tujipikie tukajifanyie sikukuu.Wala dunia haitatugomea kwa maamuzi kama hayo. Waaidha kwa Wakristo, sadaka ni moja tu. Sadaka ya misa. Hayo mengine yote ni ujinga na kufukuza upepo tu.
Mapepo
Kuna tofauti ndogo isiyo na maana kati ya mapepo na majini. Wanasema eti mapepo hayaonekani lakini majini yanaonekana. Sahau tofauti hiyo, watie wote katika kundi la mashetani. Mashetani ndiyo wale malaika waliomwasi Mungu na hivyo kulaaniwa. Kwetu sisi Wakristo, tunajua fika kwamba hawana bao. Yesu amewashinda. Amemtegua kiuno shetani. Yeye ni BAUNSA WETU.
Kazi aliyojia Yesu duniani ilikuwa kuwaokomboa watu kutoka kwenye makucha ya shetani na maswahiba wake. Gharama ya kazi hiyo ilikuwa kubwa, ndiyo kujimwilisha na kisha kumwaga damu msalabani kwa ajili yetu. Kazi hii kubwa ilizaa matunda. Tumekombolewa kweli kweli kwani Yesu hakuja kufanya kazi bure. Ni sisi binadamu ambao tunaweza kufanya kazi kubwa na kuambulia mapato madogo kwa sababu ya kosa la kwanza la Adamu na Eva lakini si Mungu mwenyewe. Sasa iweje baada ya Yesu kumshinda shetani sisi tuhangaishwe na shetani kana kwamba Yesu hakufanya kitu? Basi shetani anatutazama Wakristo kwa mbali tu. Ila yeyote ambaye hajampokea Kristo yupo kwenye himaya ya shetani bado.
Ndiyo kisa mashetani (mapepo kwa majini) yanawahangaisha ndugu zetu wasio Wakristo. Ndugu zetu Waislamu ndiyo hasa yapo kwao. Basi ndiyo kisa yanavuma kati yao kwani hawana Yesu. Masimulizi yananaanza hata kwenye kuumbwa kwa majini. Wanasema yaliumbwa na kupewa jukumu la ibada kama wanadamu. Hata Mtume Mohamedi aliwasisilimu majini kwa mahubiri yake. Kwa kweli majini ni ndugu zao ndiyo maana hata majina ya majini karibu yote ni ya kiislamu. Huo ni ushuhuda tosha kwamba majini au mapepo ni jamaa ya Waislamu. Hakuna jinni John, Corbinian wala jinni Tito kwani hawana shirika na Yesu Kristo wala na  Wakristo. Sasa inasikikaje kuwa yapo kati yetu. Hapo ndipo tunapotwishwa tatizo lisilo letu. Jina la Yesu sawia na jina la Maria yanawakimbiza majini au mapepo kwa mbali kabisa. Aidha sisi kwa kubatizwa na kupakwa mafuta ya kuwingia mapepo sisi tumekuwa kama chupa zenye dawa ya kunguni ndani yake. Itakuwaje kunguni waishi ndani ya chupa hizo? Basi ikiondokea jinni au pepo kuishi ndani ya Mkristo, yaani kunguni kuishi ndani ya chupa yenye dawa ya kunguni ndani yake, basi inamaanisha dawa imekwisha nguvu, yaani “imeeksipaya”. Basi hapo lazima lije swali kwa nini dawa imekwisha nguvu? Kumbe dawa ya kiroho huisha nguvu kwa dhambi kubwa. Sasa swali, dhambi gani kubwa aliyoitenda mhusika hata kuishiwa nguvu?
Kwa muhtasiri huu, Wakristo hasa wale wanaoishi katika maeneo yenye mchanganyiko wa dini waangalie wasiishi teolojia isiyo yao. Hata mapadre na makatekista waangalie kwamba baada ya kusomea teolojia ya kikatoliki wasihubiri teolojia ya kiislamu. Wote wanaofundisha kati yetu wafundishe mambo ya kikatoliki. Si halali na kwa kweli ni hasara kubwa kusomea teolojia ya kikristo kwa miaka mingi na kishapo kuhubiri yasiyo yetu. Basi ndugu zangu, ijulikane wazi kwamba, mintarafu mapepo, majini au shetani kwa ujumla, teolojia ya Waislamu SI SAWA NA YETU hata kidogo. Acha niweke muhtasari wa teolojia ya kiislamu kuhusu majini. Kwa Waislamu mchana ni wa wanadamu na usiku ni wa majini. Wanasema hilo limefanywa na Mungu baada ya majini kuomba wanadamu watenganishwe na wao. Wanasema hiyo ilifuatia tabia ya binadamu kuchenga ibada za kumwabudu Mungu kwa udhuru za kuumwa ama kuwa na shughuli za biashara au kuwapo safari. Wanaendelea kufundisha kwamba baada ya Mungu kuwakubalia majini ombi lao, majini yanatawala usiku na binadamu mchana. Wanaendelea kusema, baadhi ya majini waliamua kutokuwa na kisasi na wanadamu na hao ndiyo majini mazuri wanaowapenda wanadamu na hivyo kuwasaidia  katika mambo ya biashara, mapenzi na bahati za aina mbalimbali. Lakini majini mengine yakaapa kuwadhuru binadamu. Kumbe hao walioapa kuwapo  wanaowapenda watu na wanaolipa kisasi kwa binadamu, wanachukua sura mbalimbali: kama nyoka, ndege hasa njiwa, mnyama, miti mirefu, binadamu hasa wanawake wazuri, kama mtu unayemfahamu, paka, panya, kuku n.k., kila mtu ana wake, wana moto, kila aya ya Qur’ani ina jinni lake, sheikh anaweza kuwaita, wanasimamia idara mbalimbali kama vile ngono, ulevi, usengenyi, wivu n.k. ni wengi mno yaani mamilioni kwa mamilioni. Pepo bawa ni majini au mapepo yanayobaka watu au kuwalawiti watu kwa nguvu. Hao si kati ya majini au mapepo mema.
Haya yote nayahesabu ubatili mtupu.
6.5 Upotevu wa dhana kamili ya Ndoa kwa Vijana wengi
Siku hizi ndoa zinazokuja kubarikiwa kanisani asilimia kubwa zinakuwa ni mtumba. Maana yake vijana wamefikia hatua ya kutaka kujaribu kila kitu kwanza. Hivyo kabla ya kuhalalisha ndoa kamili, wakiwa katika hatua ya uchumba wanadanganyana kuwa wajihakikishe kama kweli wako vizuri. Kwa hakika hii dhana ni ya kutupilia mbali, licha ya kwamba utandawazi nao unachangia kwa kiasi kikubwa katika kuwafanya vijana kuwaka sana tamaa kupitia vitu wanavyoshinda wanaona na vingine kutazama.
Hatari kubwa ipo zaidi pale wanapooana kila mmoja ana nafsi yake. Hiyo nafsi kamwe haiwezi kumwacha mtu salama, daima itamlilia tu. Wahanga wakubwa hapa ni mabinti ambao kwa hakika huwa waaminifu sana, kumbe inapotokea akashiriki tendo la ndoa kwa mara ya kwanza na mtu aliyekuwa na malengo yake. Sasa ikitokea yule mtu ameamua kuoa binti mwingine, kwa hakika ile nafsi ya yule binti wa kwanza itamlilia na kumtafuta tu mpaka impate. Ndiyo hapo tunapata masuala ya michepuko na nyumba ndogo, kumbe nayo haianzii ukubwani bali pale unapojikuta umeshiriki tendo la ndoa kabla ya muda wako. Na kuendeleza tabia hiyo hiyo ya onja onja. Hakika hata ukishaoa huwezi kuacha tabia hiyo ya udokozi. Na hivyo mhubiri anaendelea kututia shime na kutuonyesha umuhimu wa kufuata nyakati ipasavyo.[74]
Tuendelee na kujitahidi kukemea kwa nguvu zetu zote, maana ni katika kuuongea ukweli wa mambo haya na kuyaweka bayana nasi tutazifanya nafsi zetu kuwa huru.[75] Tena tuone ya kuwa wakati ni sasa wa kuvipiga vita, maana muda tulionao ni sasa; baadaye hatutapata muda huo. Hivyo tufanye kwa moyo na bidii sasa kukemea, wala tusingoje kana kwamba kuna muda ufaao utakaokuja. Kila mmoja atende kwa juhudi zake zote kadiri awezavyo ili kukinusuru kizazi hiki cha leo.[76]
Katika changamoto hizo tajwa hapo juu kwa kiasi kikubwa zimekuja kuchangia wimbi la watoto wa mitaani. Yaani mtu baada ya kujua na kuelewa juu ya kutoa mimba bila kujali ni mazingira gani kaipata, basi anaamua kuvumilia mpaka anajifungua salama. Sasa unapokuta ni binti, walio wengi anachokifanya ni kumchukua mtoto yule akiwa mdogo kabisa na kumpeleka kulelewa na bibi yake. Kitendo hicho ni kama kumtelekeza mtoto, maana mama anakwenda kutafuta au kuolewa na mtu mwingine. Sasa bibi yake asipokuwa na moyo wa nyama, atamwacha mjukuu wake akue katika maisha anayojua mwenyewe. Mwisho wa siku mtoto anajikuta anakuwa omba omba au mtoto wa mitaani.
Pia tunalowimbi la watoto yatima ambao kwayo wengine ndiyo hao wanaojikuta wamekosa mwelekeo na kuanza kulandalanda mitaani, hatimaye wanakuwa watoto wa mitaani.  Kulingana na Frt. Nini maana ya Mtoto au Watoto yatima? Hawa ni watoto ama waliofiwa na wazazi wao wote wawili (yaani baba na mama) au waliotelekezwa na wazazi wao kwasababu mbalimbali kubwa ikiwa ni ile ya kukwepa majukumu ya mzazi. Na hivyo wakajikuta wamelazimika kuishi peke yao bila mzazi au wazazi yaani kwa lugha ya leo ningeweza kusema ‘ni watoto wa bata, mama huku watoto kule, au watoto hapa mama kule.’
Ushauri wangu kwa:-
(a) Jamii
Mtoto au watoto yatima ni mali ya jamii, ni mali ya kila mtu na kila mmoja wetu. Tuwajali, tuwasaidie, tuwe nao katika dhiki yao. Familia zinaweza kuwachukua na kuwalea kama wanafamilia waliozaliwa nje ya familia. Tuwaone kama wao ni wa zizi letu lakini wanakaa nje ya zizi na hivyo tuwalete ndani ya zizi. Tuwapende, tuwape haki zao msingi mathalani haki ya kuishi, kupendwa, kupewa elimu, malezi, matunzo, malazi, chakula nk. Napenda kusisitiza haki ya kuwapenda na hii ni amri ya Mungu. Jamii ni mzazi na mlezi wa watoto hawa isiwaache kamwe bila kuwapa msaada stahiki. Jamii ni mzazi wa kila mtu, ni mlezi wa kila mtu, kila mmoja ana haki sawa na yenye uzito sawa ndani ya jamii alimo. Anapaswa kujisikia yuko nyumbani ndani ya jamii yake.
(b) M/Watoto mwenyewe
Wapendwa sana wadogo wangu, napenda kuwaambieni jambo hili ‘hamko peke yenu, hamjatengwa na watu wote, hamjaachwa wakiwa, mna baba, mna mama, mna kaka na dada, ndugu, jamaa na marafiki wanao wapendeni sana naam sana tu.’ Mungu ndiye Muumba wetu na Baba wetu sote, ni Baba mwema, ndiye mzazi wetu nambari wani. Ewe mtoto yatima usikate tamaa, usivunjike moyo, hujaachwa, hujatengwa, hujatelekezwa kwa namna yoyote.
Dawa hii nawapa, ni siri ya mafanikio ‘wapendeni na kuwaheshimu watu wote, wa dini zote, wa itikadi zote, wa kabila lolote, wa sehemu yoyote, hawa ni ndugu, jamaa, na marafiki wenu na kati yao hamtakosa mtu mwema wa kuwajali katika hitaji lenu.’ Kumbukeni kuwa ‘kwa mgonjwa mtu yeyote huonekana daktari pale anapotoa ushauri au maelekezo fulani fulani juu ya ugonjwa au tiba kwa mgonjwa.’ Kanisa ni mama kwenu-zaliweni kwalo katika sakramenti ya ubatizo, mlelewe na mkuzwe na mwimarishwe kwalo kwa masakramenti ya kipaimara, ekaristi takatifu, kitubio na mpako wa wagonjwa.
Mkidumu katika Kanisa mtakua kiroho, na kimwili mtapata humo wazazi wa kuwalea na hata kuwasaidia kuzifikia ndoto zenu. Vilevile jamii ni mlezi wenu. Jamii ina watu wema mkiiangalia katika kipimo hicho. Ubaya wa jamii ni mdogo kuliko uzuri wa jamii hasa kwenu watoto mnaopendwa sana na Kristo. Mungu Anawapenda sana, Anawafahamu kwa undani zaidi hata majina na nywele zenu zinafahamika kwake. Ninyi mmeandikwa katika viganja vyake. Kwanini mkate tamaa? Kanisa linawapenda sana ninyi watoto maana ninyi ni hazina ya Kanisa, ninyi ni tumaini la Kanisa. Jamii pia inawapenda sana maana ninyi ni nguvu na nguzo tegemezi ya kesho kwenye jamii. Ninyi ni taifa la kesho, Tanzania ya kesho haipo kama ninyi hampo leo. MSIKATE TAMAA BASI.
Upendeni ulimwengu maana wenyewe kwa wenyewe sio mbaya japo walimwengu wanaweza kuwa kinyume chake. Mfano kama kuwa kwenu yatima kumetokana na kutelekezwa, kukataliwa (jambo ambalo huumiza sana, huhuzunisha sana na hivyo hampendi kulisikia kabisa). Kwa upande mwingine kama wazazi wenu walifariki dunia nalo hili huiumiza sana roho lakini kuweni tayari kuupokea mpango wa Mungu. Katika uyatima wenu, Yeye Anakijua Akifanyacho. Hata hivyo bado mnafursa ya kuishi na wazazi wenu katika ulimwengu wa imani-waombeeni nao watawaombeeni nanyi mtapata faraja katika uyatima wenu. Mwisho hata kama katika ulimwengu huu mtaonekana na mtaishi kama yatima-msikubali kamwe kuwa yatima kiroho. Yesu anasema “SITAWAACHA NINYI YATIMA, NAJA KWENU, MIOYO YENU IJAE FURAHA” Jaeni furaha wadogo wangu katika Kristo.
Hatimaye; Matatizo haya tuliyo yaona hapo juu yanaweza kupelekea kwenye matatizo makubwa kabisa kwa mtu binafsi, kwa familia, kanisa na jamii nzima. Ninachopenda kukitolea rai ni suala la ‘watoto wa mtaani.’ Ni akina nani hao? Hivi siku hizi zetu mtaa/mitaa imepewa hadhi ya mzazi/wazazi? Na kama ndiyo ni mama/baba? Na kama siyo, mbona kuna watoto siku hizi zetu tunawaita ‘watoto wa m/mitaani?’ Nadhani hili ni kosa kubwa kijamii na kimaadili na kiasili yetu. Mtaa hauwezi kuzaa mtoto aliyeumbwa na Mungu kwa sura na mfano wake. Mtoto ni zawadi  itokayo kwa Mungu na ni tunda la upendo kati ya baba na mama (hata kama hawakai pamoja kama mume na mke). Labda kama tunauangalia mtaa au tunapoiangalia mitaa kama ‘sehemu wanamokaa.’ Wana kula na kunywa humo (mtaani), wana lala mtaani nk.
Katika masuala (matatizo) haya mtambuka, kila mmoja wetu hana budi kujiuliza moyoni mwake ‘mimi nimekuwaje sehemu ya tatizo? Nawezaje kuwa sehemu ya suluhisho? Nimefanya nini mpaka sasa? Nina mikakati ipi ya baadaye ya kusaidia? Nawapokeaje wale ambao wanasaidia katika vita hii au ndo nawakatisha tamaa kwa maneno yangu ya vijembe mtaani ‘anajipendekeza, anataka tumwone naye kuwa ana chembechembe ya upendo kwa watu lakini ni mweusi moyoni na rohoni mpaka damu yake pia.’
Ndugu kama umo kwenye baadhi ya matatizo haya hasa yale ya kujitafutia (umalaya, utoaji mimba, na uuaji mwingine kwa ujambazi nk) AMUA VEMA UPATE KUISHI, CHAGUA VEMA UISHI VIZURI. Acha ugume gume, acha ungangali, kuna kifo. Utaenda wapi na ujanja wako huu unaoukumbatia namna hii leo ungali hapa bondeni (duniani)? Mpende binadamu mwenzio, mpende Mungu wako kwa moyo wako wote. Kumbuka kuna maisha baada ya maisha. Na kama matatizo haya yana kusibu bila kuyatarajia (mfano kuwa yatima)-usife moyo, sote tunapita, leo tupo kesho hatupo. Usisononeke mno ukashindwa kupiga hatua moja mbele, inuka, songa mbele, Mungu Anakuita jinsi ulivyo. Mkumbuke mzee wetu Madiba aliposema “Watu hawatashangaa kuona umeanguka, lakini watashangaa sana kuona umeendelea kubaki ulipoangukia.” Tukiinama katika maisha, tuinuke pia, tukianguka katika maisha, tuninuke pia, tuki lala katika maisha, tuamke pia. Tusonge mbele, hatua moja mbele yatutosha.
Tuendelee kubadilika kila siku ipitayo na zaidi kujaliana na kuthaminiana, maana wanasema mtoto wa mwenzio ni wako au mwone kama mtoto wako. Tusaidiane katika zoezi zima la kulea pasipo kujali wala kuangalia huyu ni mtoto wa nani.



7.0 HITIMISHO

Kupitia maneno haya yatutie shime “Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu”, wala “figa moja haliinjiki chungu.” Kidole kimoja hakivunji chawa.” Umoja ni mzuri kwani unajenga. Ni pale tu tunapokuwa na umoja ndipo tunakuwa imara na kufanikiwa katika maisha. Katika Zaburi ya 133 mzaburi anatueleza wazi kuhusu maisha ya umoja. Anasema, “Tazama jinsi ilivyo vyema na kupendeza, ndugu wakae pamoja kwa umoja…..maana huko ndiko Bwana aliamuru Baraka, naam uzima hata milele.” Yesu aliwaombea umoja wanafunzi wake, kwani kama wangetengana ingekuwa rahisi kushindwa katika kukamilisha kazi ya ushuhuda. Yesu alisali, Baba mtakatifu, kwa jina lako ulilonipa uwalinde hawa,ili wawe na umoja kama sisi tulivyo.” Yoh 17:11b, 21. Umoja huu ulijidhihirisha katika jumuiya ya Mitume, hata kipindi cha madhulumu waliweza kuja pamoja kwa sala.

Kwa kujiunga na Mwanafalsafa Mfaransa Jean Paul Sartre (1905-1980) alisema Mtu anahukumiwa kuwa huru; kwa sababu mara moja anapotupwa ulimwenguni, yeye anawajibika kwa kila kitu anachofanya (Man is condemned to be free; because once thrown into the world, he is responsible for everything he does).[77] Watu wanahukumiwa kwa sababu wanajikuta wametupwa ulimwenguni, lakini kwa sababu kwa haraka kama wao wanajitambua wenyewe na hivyo wanawajibika kwa kila kitu wanachofanya. Kumbe tutambue kuwa licha ya kuwa huru bado tuelewe kama binadamu tuna mipaka. Kwa hiyo mimi na wewe tukiendelea kufumbia macho majanga yanayoendelea katika ulimwengu huu bila kukemea, kwa kuungana wote kwa pamoja na kuona ni vitu visivyokubalika katika jamii tutakuwa tunajitenga na upendo wa Mungu. Na hii inajidhihirisha hata katika matendo ambayo tunaambiwa tuyatendapo kwa wengine walio wanyonge wenye kuhitaji, msaada wetu wa mawazo, basi tunakuwa tukimtendea Mungu. “…Njoni, mliobarikiwa...urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu…kwani kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo mlinitendea mimi.”[78]

Hali kadhalika tunapoendelea kukaa kimya huku mambo yakizidi kuharibika, sisi tuliojaliwa kujua ukweli huu tukumbuke tutadaiwa kwa nini hatukusema ili kunusuru Roho za watu. Nabii Ezekieli anasema, “Basi wewe, mwanadamu, nimekuweka kuwa mlinzi kwa nyumba ya Israeli; basi ulisikie neno hili kinywani mwangu, ukawape maonyo yangu. Nimwambiapo mtu mbaya, ‘Ewe mtu mbaya, hakika utakufa,’ nawe husemi neno la kumwonya mtu huyo, aiache njia yake, mtu mbaya huyo atakufa katika uovu wake, lakini damu yake nitaitaka mkononi mwako. Walakini ukimwonya mtu mbaya kwa sababu ya njia yake, kusudi aiaxhe, wala yeye asiiache, atakufa huyo katika uovu wake, lakini wewe umejiokoa roho yako.”[79]

Nayakumbuka maneno ya Mwalimu wangu wa Litrujia (Pd. Kinyashi) anapenda kusema maneno yanaumba pia maneno yana nguvu. Japo yeye anapenda kusema kwa lugha ya kigeni “the power of the spoken word.” Ni kwa namna hiyo tunapofanya au kutolea maneno mazuri na ya kujenga yanaendana na baraka, lakini tunaposhindwa kusema chochote tunamkaribisha ibirisi ndiye aje kusema kupitia vinywa vyetu. Yeye mara nyingi anayaongelea maneno hayo katika kubariki vitu, kwamba unapotumia maneno na kuamulu kitu fulani kweli kinafanyika kama ulivyotamka; tofauti na kubariki kimya kimya. Anatolea mfano huu katika kubariki maji ya Baraka. Nami nimetumia maneno hayo nikimaanisha kwamba tunapoona jambo haliendi vizuri aheri kusema, kitendo cha kusema tu yatosha kulilo kukaa kimya. Kumbe watu wasipobadilika hiyo ni juu yao wenyewe, wewe huna hatia tena.
Tunaposhindwa kuelekezana na kuelimishana namna ya kuondokana na mwovu shetani na mambo yake yote, basi tunarudi kule kule kipindi kabla ya Yesu kuja duniani na kutukomboa. Sasa hatupaswi kurudi nyuma tena tutakuwa tunajichanganya maana hata miaka inazidi kusonga mbele nasi kwamba tuonekane tunarudi nyuma utakuwa uwenda wazimu. “Bali nyini ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkainge katika nuru yake ya ajabu; ninyi mliokuwa kwanza si taifa, bali sasa ni taifa la Mungu; mliokuwa hamkupata rehema, bali sasa mmepata rehema.[80] Tujifunze sala ya kuomba neema kufanya atakavyo Mungu, ili aweze kuyaongoza maisha yetu kwa kutenda yaliyo mema na mazuri. Hivyo wewe uliyekisoma kitabu hiki, ukakifundishe kwa wengine tena kwa uthabiti kabisa. Na hata Mahatma Gandhi alisema, ‘kuwa sehemu ya mabadiliko unayotamani kuyaona ulimwenguni.’ Hivyo kwa mang’amuzi uliyotoa humu kwanza yafanye kuwa sehemu ya maisha yako, hapo utaweza kuwafundisha wengine. Pia wanasema ‘watu wema wasipotenda wema, uovu unaongezeka’; nawe uliyepata bahati ya kusoma kazi hii uanwajibu wa kutenda wema huo kwa kuwamegea kile ulichojifunza kutoka kwenye kazi hii.

Mzaburi anatuambia kuwa “Jueni kwamba Bwana ndiye Mungu; ndiye aliyetuumba na sisi tu watu wake, tu watu wake, na kondoo wa malisho yake.[81] Tutambue kuwa hatufanyi sawa pale tunapoenda kinyume na mpango wake kwa kumwacha na kutenda dhambi. Kumbe kila mmoja ajitahidi kwa nafasi yake kumpiga vita shetani, kwani naamini katika hali ya kutaka kuokoa roho za watu wengine kupitia mafundisho yaliyomo, basi utakuwa unaiokoa pia roho yako (utaifanya roho yako yako iokolewe). Wala tusiogope kukemea dhambi maana alituambia yeye yuko nasi mpaka mwisho wa dahari.[82]

BIBLIOGRAFIA

Bahati Inocent, Huruma ya Mungu ni kwa wote,Uponyaji wa majeraha ya nafsi kupitia msamaha, Jamana Printers Ltd., Dar es Salaam 2016.

Biblia ya Kikatoliki Toleo la Iringa.
Bula ya Sifa kwako ee Bwana, Laudato si.

Croucher L.Sheila, Globalization and Belonging, The Politics of identity a changing world, Rowman & Littlefied, 2004.

Katekisimu ya Kanisa Katoliki, Pauline publication, Nairobi, 2000.

KangeroW.Wilehard, Njooni name nitawapumzisha, Nimekuja ili wawe na uzima tena wawe nao teleTathimini juu ya Jubilee ya kiprkee ya Huruma ya Mungu, Moshi printing, Moshi,2017.

Kinyashi R. A, Kusali ni Heri Muumba Kumpenda, Toleo la pili, Niim Computers & Graphics (T), Dar es Salaam, 2013.

Machowera Salvator, Kusali ni Heri, Hazina za Kanisa Katoliki, Moshi, 2006.

Mavumilio Rogatus, Special Ethics, Kibosho Regional Philosophicum, Moshi, Unpublished Class Notes, 2017.
Misale ya waamini.

Mbiku H. D., Uchumba na Ndoa, Toleo la Tatu.

Mbowe S. Benjamini, Thamani Yetu, Niim Printers & Media Services, Dar es Salaam, 2017.

Mtaguso Mkuu, Maelezo ya Hati 16 za Vatican II, Jimbo Kuu    Tabora, Toleo la Nne 1993.



[1]1Yoh.1: 8-9
[2]Rej., Mwa 1:26
[3]Rej., Mt. Maximus Muungama dini, Ambigua: Kur. 91, 1156C; Mwa. 3:5
[4] Rej., Rum 5:19.
[5] Rej., Tob 4:14.
[6] Rej., Ludwig OTT, Fundamentals of Catholic Dogma, J. C. Bastible (ed), P. Lynch (trans.), Tan books and Publishers, Inc, Rockford, 1960, Uk. 110-107.
[7] Rej., Ludwig OTT, Fundamentals of Catholic Dogma, J. C. Bastible (ed), P. Lynch (trans.), Tan books and Publishers, Inc, Rockford, 1960, Uk. 110-111.
[8]Rej., KKK Na. 417
[9] Rej., Ludwig OTT, Fundamentals of Catholic Dogma, J. C. Bastible (ed), P. Lynch (trans.), Tan books and Publishers, Inc, Rockford, 1960, Uk.112.
[10]Rej., KKK Na.404
[11]Mt 15:19-20
[12] Rej., KKK Na. 1853
[13]Rej., KKK Na. 1854
[14]Rej,, KKK Na. 1855-1857; St. Thomas Aquinas, STH I-II, 88, 2 corp. art.
[15]Rej., KKK  Na. 1863
[16]Rej., Rej. Ludwig OTT, Fundamentals of Catholic Dogma, J. C. Bastible (ed), P. Lynch (trans.), Tan books and Publishers, Inc, Rockford, 1960, Uk. 107. & Lk. 10:30.
[17] Rej., Michael Schmaus, Dogma, God and Creation, Volume 2, Sheed and Ward Ltd, London, 1969, uk. 195-202.
[18]Rej., KKK Na. 400
[19] Rej., KKK Na. 405
[20]Rej., KKK Na. 1861
[21]Rej., KKK Na. 1863
[22]KKK Na.1488
[23]Rej., Yohane Paulo II, DeV 46
[24]Rej., KKK Na. 2147
[25] Rej., KKK Na. 2150-2151
[26]Katikisimu ndogo ya Kanisa Katoliki Na.1“kwanini Mungu alituumba? Jibu lake ni kwamba, Mungu alituumba ili tumjue, tumpende, tumtumikie na mwisho tupate kufika kwake mbinguni”.
[27]2 Tim 4:18
[28] Rej., Yn 14:1-4
[29] Rej., Mwa 1:26-27; 2:7
[30]Mwa 3:22
[31]Rej., Zab 14:4
[32] Rej., D. H. Mbiku, Uchumba na Ndoa, Toleo la Tatu, Uk. 24.
[33]Mwa6:6.
[34] Hek 9:1-3.
[35] Rej. Mwa 1:26.
[36] Beatus Kiyabo, Tafakari Kuhusu Maisha, Nukuu 200 za Watu Maarufu, Nesmap Printing Technology, Dar es salaam, 2018, uk. 31.
[37]Ibid. uk. 20.
[38] Rej., 1Yoh 4:16.
[39] Salvator Machowera, Kusali ni Heri, Hazina za Kanisa Katoliki, 2007, uk. 12.
[40]Ibid. uk. 35.
[41]Kitabu cha Dini Katoliki, Mungu na Wanadamu, Toleo la pili, Benedictine Publications, Ndanda, 1988, Uk. 215-216
[42] Rej., Zab 75:4-5.
[43]Wilehard W. Kangero, Njooni name nitawapumzisha, Nimekuja ili wawe na uzima tena wawe nao teleTathimini juu ya Jubilee ya kiprkee ya Huruma ya Mungu, Moshi printing, Moshi,2017, p.24.
[44] Rej., Yak 2:12-13.
[45]Rej., KKK 890
[46]Rej., KKK 924
[47] Rejea, Yak. 4:11-12
[48]KKK 909, Lumen Gentium: LG 36 & 3.
[49] John Ofosu, Uponyaji wa Mti wa Familia, Laana ya Maagano ya Nafsi Madhara ya Vifungo vya Nafsi, Niim Computers & Graphics (T), Dar es salaam, 2012, uk. 1.
[50]Rej., KKK Na. 1749-1754)
[52] Sheila L. Croucher. Globalization and Belonging, The Politics of identity a changing world, Rowman& Littlefied, 2004, uk.10.
[53] Kum 22:5.
[54] Ibid. uk. 1.
[55] LG 48
[56] Haya ni mawazo ya EAST AFRICA LEGISLATIVE ASSEMBLY-EALA.
[57] Agustiono, Maungamo, 1:1
[58] Gal 5: 16-17.
[59] Kutoka Misale Ndogo (Chuo cha Waumini Jimbo la Moshi), Chapa ya nane-Novemba 24, 1991, wimbo namba 196  TUKIPENDA WENZETU, uk. 943.
[60] Kwa kweli Yakobo alimtumikia mjomba wake Labani kwa miaka 20 yaani 7 kwa ajili ya Raheli ambaye aliambiwa hawezi kumpata kabla ya mkubwa/dada wake. Kwa hiyo, miaka hiyo 7 ya awali ikawa kwaajili ya Lea. Kwa kuwa alimpenda sana Raheli, alimtumikia tena mjomba wake Labani miaka 7 mingine kwaajili ya Raheli sasa kwa awamu hii. Na hapo awali alikuwa amemtumikia kwa kuchunga mifugo wake kwa miaka 6 na ndipo neno hili linapata maana “Kwa sababu wewe ni ndugu yangu, basi je, unitumikie bure? Niambie, mshahara wako utakuwa nini?” (aya 15). Naye akajibu akasema “Nitakutumikia miaka saba kwa kumpata Raheli, binti yako mdogo” (aya 18). Utaratibu huu mimi binafsi nauona kama utaratibu uliopo leo wa ‘KUTOA/KULIPA MAHARI’ japo siyo lazima iwe kwa kuchunga na kuoa wake wawili kama ilivyo kwenye simulizi hili.
[62] Rej. Eugene Kawau, Uwajibikaji: Dawa kwa Changamoto katika Familia na Jamii, Mafundisho Huru kwa Watu Wazima, Vijana na Watoto, EKA’s Publication, Dar es salaam, 2017, Uk. 21.
[63] T.E.C, Haki na Amani katika Familia, 8.
[64] Rej. Eugene Kawau, Op. Cit., uk. 23-24.
[65] Rej. Mt. 24:36-44.

[66]Rejea, Ayu 3:16
[67] Benjamini S. Mbowe, Thamani Yetu, Niim Printers & Media Services, Dar es salaam, 2017, uk. 18.
[68] Rejea, KKK Na. 2280-2281.
[69]Pew Research Center,www.pewforum.org/2017/08/08/gay-marriage-around-the-world-2013/, retrived on 23/1/2018.

[70]Rogatus Mavumilio, Special Ethics, Kibosho Regional Philosophicum, Moshi, Unpublished Class Notes, 2017.

[71]Rej.  www.sw.m.wikipedia.org/wiki/ukahaba, oline search, 19/1/2018.
[72]Ibidem.
[73]Ebr 11:1
[74]Rej. Mhu 3:1-11
[75]Rej. Yn 8:31-32
[76]Rej. Muh 9:10
[77]Jean-Paul Sartre, Being and Nothingness, An Essay on Phenomenological  Ontology, trans. Hazel E. Barnes, , Methuen & Co. Ltd, London, 1958, Uk. 436.
[78]Rej.  Mt 25:34-40.
[79] Eze 33:7-9.
[80] 1Pet 2: 9-10.
[81] Zab 100:3.
[82] Rejea, Mt 28: 19-20.