Tuesday, February 4, 2020

CHUKI NI NINI?

CHUKI NI NINI?

Kadiri ya Dr.Ann Landers: “Chuki ni kama Asidi, ambayo huaribu kile kifaa ambacho imehifadhiwa na huaribu chombo ambamo imemiminwa.”[1] Nelson Mandela aliwahi kusema: “Msamaha ni dawa na kutokusamehe ni sumu. Chuki ni kama kunywa sumu ya ukitumaini kuwa itawaua maadui zako” – alikuwa akinukuu maneno ya Anne Lamott anaposema: “Kutokusamehe ni kama kunywa sumu ya panya na kungoja ili panya afe.”

Hebu fikiri, kama hatuwasamehi ‘maadui’ zetu, nini kitakachotokea?  Ni lazima tukabiliane na madhara hasi ya kiteolojia na matunda hasi mawili ya kisaikolojia. Tuone ni nini haya madhara hasi mawili ya kiteolojia.

[1] “Hate is like an acid. It damages the vessel in which it is stored, and destroys the vessel on which it is poured."

MADHARA YA KITAUHIDI (TEOLOJIA)

Kuendekeza hasira, chuki, huzuni, shauku ya kulipiza kisasi ni kwenda kinyume na kile tunachopaswa kuwa. Kimsingi ni kuharibu sura na mfano wa Mungu ndani yetu, tena ni kwenda kinyume na Mungu ambaye ni mwingi wa rehema na huruma kwa watu wake na anayetufundisha kuwa kama yeye alivyo.

Samehe nawe utasamehewa: Kitabu cha Yoshua Bin Sira kinasema: “Umsamehe jirani yako dhara alilokufanyia, hivyo nawe utasamehewa dhambi zako wakati utakaposali.” (rej. YbS 28:2).

Ikiwa hatutawasamehe wengine, dhambi zetu hazitasamehewa. Wazo hili hili linajirudia katika Agano Jipya: “Msihukumu nanyi hamtahukumiwa, msilaumu, nanyi hamtalaumiwa, achilieni, nanyi mtaachiliwa.” (rej. Lk 6:37, Mk 11:25, Mt 5:23-24; 18:21-35).

Nanyi kila msimamepo na kusali, sameheni mkiwa na neno juu ya mtu, ili na Baba yenu aliye mbinguni, awasamehe na ninyi makosa yenu. (rej. Mk 11:25); “Tena iweni wenye fadhili, wenye Huruma, wenye kusamehe, kama Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi (rej. Efe 4:32); Mkichukuliana na kusameheana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake, kama Bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo hivyo ninyi msameheane. (rej. Kol 3:13; 2Kor 2:5-11)

Fr. Innocent Bahati OFMCap,
Mwenge Catholic University (MWECAU-MOSHI)
+255 755552538// +255783942208
Itaendelea

No comments: