Januari 10, 2019
ALHAMISI : Kumuabudu YESU wa Ekaristi.
Katika agano la kale, wana wa israeli pindi wakiwa bado katika safari yao ya wokovu (jangwani kuelekea kanaani); Muda uliwadia waliona njaa na hawakujua wapi wapate chakula na wala fikra zao hazikuweza kukumbuka ukuu na uweza wa MUNGU jinsi alivyowaokoa na mkono wa farao na kuwashusha bahari ya shamu tena walitembea kukavu kabisa.
Hivyo iliwapelekea wana wa israeli kuja na malalamiko kwa Musa mtu wa MUNGU kuwa awape chakula; Musa alifadhaika sana ila yeye alimgeukia MUNGU kwa kuwa alijua ukuu na uweza wake na kwa utii wake MUNGU alimsikiliza na kumwambia kuwa awaambie wana wa israeli kuwa alfajiri ikifika basi wataokota chakula kutoka mbinguni ambacho baadae walikiita " MANA ".
Mwisho wa yote MANA ilikwisha; Wana wa israeli baadhi yao walikufa kutokana na kutofata amri ya MUNGU juu ya jinsi ya kula chakula hicho.
Musa nae aliambiwa na MUNGU kuwa achukue hiyo MANA na kuiweka ndani ya sanduku lile ikiwemo pia fimbo yake na zile mbao mbili zenye amri kumi za MUNGU ili iwe ukumbusho wa milele kwa wana israeli kuwa walikula MANA chakula cha mbingu walipokuwa jangwani.
POINTI NI HII ;
1. Wana israeli katika agano la kale walikula chakula cha mbingu kiitwacho MANA na baadhi yao walikufa.
2. Musa alihifadhi iyo MANA ili iwe kumbukumbu ya milele.
SASA BASI TUTAFAKARI LEO;
1. Tupo agano jipya na chakula cha mbingu ni YESU mwenyewe mwana wa MUNGU na tukila chakula hicho kamwe hatutakufa bali tutapata uzima wa milele.
2. MANA iliwekwa katika sanduku ili iwe ukumbusho wa milele LAKINI leo hii tunae YESU KRISTO yu hai , yu mzima katika EKARISTI na anakaa ndani ya tabenaklo milele.
HIVYO BASI :
Tuwe na bidii kuwa safi rohoni na mwilini ili kupokea chakula cha mbingu ( YESU KRISTO ) muda wote wa uhai wetu hapa duniani.
Tumuabudu YESU wa ekaristi kila ALHAMISI katika roho na kweli.
Atukuzwe MUNGU milele na; Tumsifuni YESU KRISTO.
No comments:
Post a Comment