FAMILIA NA CHANGAMOTO ZAKE
Pamoja na jitihada mbalimbali ambazo zimefanyika hata sasa, Familia nyingi zinapitia changamoto mbalimbali za kisiasa, kiuchumi, kijamii, kimazingira, kisheria, kiteknolojia, kitandawazi na kimaendeleao mamboleo, kitamaduni na vuguvugu la imani, dini, kwa kutaja machache tu.
Mabadiliko haya yote yanaelekea kuziweka Familia nyingi kwenye kipindi kigumu cha kuelewa umaana na utambulisho halisi wa Familia.
Ule utakatifu unaoendana na wito wa maisha ya Familia unazidi kufukiwa na malimwengu, na hivyo unaelekea kufifia na hata kunyauka.
Ile hali ya mshikamano wa kifamilia unazidi kudidimizwa, mila na tamaduni zilizoenziwa na kuheshimiwa zinatazamwa kama kitu kilichopitwa na wakati.
Familia nyingi leo zimepoteza utambulisho na wajibu msingi wa kuwa shule ya sala, ukweli, upendo, uwajibikaji, fadhila na tunu.
Hamasisho la Familia kukoleza Imani kwa Mungu na kuchochea ile shauku ya kukua katika utakatifu inasukumizwa kuwa jambo binafsi au ni kitu kisichokuwa na umuhimu wa ujumla.
Itaendelea....
Fr. Innocent Bahati OFMCap,
Mwenge Catholic University (MWECAU-MOSHI)
+255 755552538
No comments:
Post a Comment