UPEKEE WAKO NI UPI?
Kila mmoja wetu ni wa “pekee,”-“Unique.” Katika hali ya upekee wetu hakuna aliye duni au bora kuliko mwingine. Kile kinachojiri leo hii kuwatazama wanawake kama viumbe duni sio katika mpango mzima wa uumbaji.
Thomas wa Akwino aliwahi kusema kwamba: “Mungu hakumwumba mwanamke kutoka mfupa wa kichwani mwa mwanamme, mwanamke asije akajivuna bure, wala kutoka mfupa wa mguuni mwa mwanamme asije mwanamme akamkanyaga mwanamke na kumfanya mtumwa.
Alimwumba mwanamke kutoka mfupa wa ubavuni ili wawe sawa, watembee pamoja bega kwa bega.”
Mimi na wewe ni sehemu ya maajabu ya ulimwengu. Fungua macho yako ustajabie maajabu haya.
Kila mmoja ni wa thamani kubwa, mbele ya nafsi zetu, mbele ya Mungu, hali kadhalika, mbele ya jamii, na hilo linajidhihirisha katika maneno ya Mwenyezi Mungu kwa nabii Yeremia alipomwambia: “Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, nalikutakasa, na kukuweka wakfu.”
Fr. Innocent Bahati OFMCap,
Mwenge Catholic University (MWECAU-MOSHI)
+255 755552538// +255783942208
Itaendelea
No comments:
Post a Comment