MSAMAHA NI MAPINDUZI - CHUKUA HATUA YA KWANZA
Mara nyingi, tunajikuta tukiwasubiri wengine wachukue hatua: “Yeye ndiye aliyeniumiza, kwa hiyo awe wa kwanza kuniomba msamaha.” Lakini Yesu anasema nini?
Basi ukileta sadaka yako madhabahuni, na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno juu yako, iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako, ukapatane kwanza na nduguyo, kisha urudi uitoe sadaka.” (rej. Mt 5:23-24).
Hapa Yesu anatualika sisi tulioumizwa tuchukue hatua ya kwanza kutaka suluhu. Hii ni changamoto kubwa kweli.
Tunapotambua hali yetu ya chuki, hasira, husuda, wivu, na kadhalika na kuomba uponyaji wa Bwana kutoka katika madhaifu haya ni muhimu sana. Kwani ni katika haya, tunaweza kung’amua na kuonja fadhila za mapendo, amani, furaha, na ukarimu wa Bwana.
Kuyakung’uta na kuyaaga mapungufu yetu, huleta Uhuru wa moyo. Ndivyo ilivyo kwa mtu anayetoa msamaha. Msamaha huleta uhuru wa kweli.
Wale wenye hali ya juu ya kujiheshimu na kujienzi, wanajiona wenyewe kuwa wema, wakarimu, wapole, wanaosamehe na ujasiri licha ya maumivu yatokanayo na maaumizo.
Wanajiona wenyewe waliobarikiwa, na hawataki kuchukua sura nyingine tofauti na ile ya Mungu ndani yao, na kuachana na maumizo ya zamani.
Fr. Innocent Bahati OFMCap,
Mwenge Catholic University (MWECAU-MOSHI)
+255 755552538// +255783942208
Itaendelea
No comments:
Post a Comment