Tuesday, February 4, 2020

MSAMAHA NA FUMBO LA MSALABA

MSAMAHA NA FUMBO LA MSALABA

Kusamehe ni kuingia katika fumbo la Kristo Msalabani. Hili ni fundisho gumu, lakini tunapaswa kulielewa. Hata pale watu wanaposamehe pasipo kufikiri sana, au wanapohiari kumtii Mungu, wanaweza kujifunua kwake.

Ni fumbo la Kristo anayesamehe watesi wake. Ni pale ambapo umeumizwa kisha ukaingia kwenye viatu vya Kristo na kujiuliza, hivi hapa Kristo angelifanya nini?

Msamaha ni kuachana na chuki, hasira na shauku ya kulipiza kisasi au kuweka kinyongo dhidi ya aliyetuudhi. Kama mmoja ametutukana au kutudanganya, tunaumia sana, na jeraha lile linabaki katika kumbukumbu zetu.

Tunapata hasira na kuelekea kuwa na hisia za kutaka kulipiza kisasi. Hii ndiyo hali tunayoiita chuki,kinyongo na hasira, na hayo yanaweza kubaki nasi kwa miaka mingi.

Chuki inatutafuna nguvu na uhuru na kuharibu uzuri wa maisha. Msamaha ni kuachilia kila aina ya chuki na kujiweka wenyewe huru.

Msamaha ni utayari wa kuachilia haki yetu ya: kuchukia, hukumu hasi na tabia ya kutokujali. Mara tu, tunaposamehe, maumivu na madonda ya zamani, hayana nafasi ya kutawala akili na hisia zetu. Hatutahitaji tena kisasi na kinyongo kuwa kwetu kama silaha ya kuwaadhibu wengine au ngao ya kujikinga dhidi ya wengine.

MSAMAHA SIO OVU KWA OVU

Msamaha ni tendo la upendo na kuyaishi maandiko kwa namna inayogusika. Martin Luther King aliwahi kusema: “Kurudisha ovu kwa ovu ni sawa na kuongeza giza la usiku katika ulimwengu ambao hauna hata nyota moja. Giza haliwezi kulifukuza giza isipokuwa tu mwanga. Chuki haiwezi kuongoa chuki isipokuwa upendo. Chuki inazaa chuki na hatimaye vurugu na vita.[1]

[1] Returning hate for hate, implies hate adding deeper darkness to a night already devouded of stars. Darkness cannot drive our darkness; only light can do that. Hates cannot drive out hate, only love can do that. Hate multiply hates and violence in descending  spiral of destruction.”
Fr. Innocent Bahati OFMCap,
Mwenge Catholic University (MWECAU-MOSHI)
+255 755552538// +255783942208
Itaendelea ....

No comments: