Tuesday, February 4, 2020

KUSAMEHE NI HATUA

KUSAMEHE HATUA KWA HATUA 2

Kujikubali: Self-acceptance — ukuaji wowote ndani yetu unatokana na kujikubali nafsi. Hili linamaanisha tuwe na mtazamo chanya juu yetu katika kila jambo liwe jema au baya na linaloumiza. Tunapaswa kuwa na mtazamo chanya juu yetu, hata pale ambapo tunajua kwamba tumeenda kombo. Haiwezekani kukua pale ambapo tunajichukia na kujilaani wenyewe.

Kujikubali kwamaanisha pia kukubali ukweli juu ya hali yetu kwamba: sisi nasi huwa tunawakosea wengine, na tunapowakosea wengine shauku yetu ni kusamehewa.

Ni lazima tukubali kwamba kama tuna hasira ni hasira ya kweli, ikiwa tumeumizwa, tumeumizwa, kama tuna hisia za kulipiza kisasi, ni vyema kama tukazitambua na kuziweka bayana.

Hatuwezi hata mara moja kukabiliana na hali hizi kama hatujakubali ukweli juu ya hali yetu ya ndani.

Mara baada ya kuitambua hali yetu ya ndani, ndipo tu tunaweza kuanza kuruhusu zisitutawale na hatimaye kuruhusu mchakato wa uponyaji ufanye kazi.

Dr. Fitzgibbons anasema: “Watu wanapaswa kutambua kwamba wametendewa vibaya, kwa unyofu watambue kuwa wamejeruhiwa kihisia, na kwamba wana hasira.

Kisha kama wanataka kuanza mchakato wa kusamehe, wanapaswa kutofautisha nini maana ya kusamehe na kutokusamehe.”

Kusamehe ni kuondoa au kupunguza chuki na hasira na kuongeza wema na upendo kwa yule aliyetuumiza au kutujeruhi au kutotutendea kwa haki. Hili ni chaguo binafsi, tendo la utashi.

Fr. Innocent Bahati OFMCap,
Mwenge Catholic University (MWECAU-MOSHI)
+255 755552538// +255783942208
Itaendelea

No comments: