FAMILIA NI KITALU CHA UHAI
Familia kama chimbuko la uhai na uzima, shule ya upendo, maadili na uwajibikaji tena altare ya utakatifu, ni mahali ambapo kila mmoja anapaswa kwenda kujifunza maana ya miito iliyoratibishwa na Mungu milele yote.
Maisha ya mwanadamu kwa asili huelezwa kwa kina katika mafundisho ya Kanisa kuhusu Familia na penzi la kibinadamu kwa wanaopendana na kunuia kuishi pamoja kama mke na mume.
Uzuri na umaana wa penzi katika ndoa na tendo lenyewe la kujamiana baina ya waliooana sio tu tendo la kimwili, ila linawazamisha wahusika katika wito wa maisha ya ndoa kisakramenti na kuwaingiza kwenye taasisi ya Familia.
Ndoa na Familia kadiri tunavyoweza kuelewa ni wito maalumu kwa maisha ya wanadamu unaotupeleka kwenye altare ya utakatifu na kazi nzima ya uhulushi (uumbaji) inafanyika. Tunafahamu kwamba ujio wetu duniani uliwezekana kwa njia ya Familia
Fr. Innocent Bahati OFMCap,
Mwenge Catholic University (MWECAU-MOSHI)
+255 755552538
No comments:
Post a Comment