Tuesday, February 4, 2020

FAHAMU JUU YA WATUMISHI WA MUNGU

NDUGU ZANGU,
AMANI NA SALAMA,
TUMSIFU YESU KRISTU!!!!.
Kuna mawazo yanatolewa na ndugu zetu wa madhehebu ya KIPROTESTANTI kuwa Kanisa Katoliki halijui na linapotosha Mandiko Matakatifu. Kwa maana hiyo wanaotoa madai hayo wanayo Elimu zaidi ya kuyajua Mandiko Matakatifu kuliko Mapadre na Maaskofu.
Hapa natoa maelezo mafupi ya namna wanavyopatikana kufikia kuitwa Padre.

UPADRE NI WITO. Ni mtu aliyejitoa sadaka kwa ajili ya huduma ya Kanisa na jamii!!!.

Hulelewa toka akiwa mdogo kwa kuzingatia malezi bora ya KIIMANI, KITAALUMA, NA KIJAMII na kufuata kazi ya ROHO MTAKATIFU. Baada ya kumaliza Elimu ya kidato cha Sita na kufaulu masomo yake vizuri sana kwa kiwango cha Daraja A, hutuma maombi (wito) kwa Padre/Askofu ya kutaka kuwa Padre , akikubaliwa , hupelekwa tena seminari kwa mwaka 1au 2 kwa ajili ya Malezi ya Upadre na kuchunguzwa kama kweli ana wito huo.

Baadaye huanza Masomo Seminari kuu. Seminari kuu lazima asome na kufaulu vizuri sana masomo ya FALSAFA (PHILOSOPHY), kwa kiwango cha DEGREE huku wakisoma kozi zote za Falsafa na TAUHIDI (THEOLOGY) kwa kiwango cha DEGREE. Wakibobea katika MANDIKO MATAKATIFU (SCRIPTURES), IMANI (DOGMA), LITULUJIA, MAISHA YA KIROHO (SPRITUALITY),, MAADILI YA KANISA ( MORAL THEOLOGY), UCHUNGAJI (PASTO THEOLOGY), SAKRAMENTI, HISTORIA YA KANISA , PASTOLOGY NA MENGINE MENGI.

Hayo masomo lazima ayafaulu kwa kiwango cha juu kabisa. Baada ya hapo hufunga NADHIRI ya kwanza na kupewa CHEO CHA FRATELA. Huendelea tena na masomo masomo na baadaye hufunga NADHIRI YA PILI ( KUISHI USEJA) NA kupewa cheo cha USHEMASI. Akishapewa Ushemasi hukaa Jimboni kwa ASKOFU  na kupangiwa majukumu kwa ajili ya huduma ya KANISA. BAADAYE hupewa DARAJA TAKATIFU LA UPADRE kwa Idhini ya Askofu na kupangiwa huduma ya Kanisa. Baadaye kidogo Hupeleka hati yake ya Upadre kwa BABA MTAKATIFU kwa ajili ya kula Kiapo cha UTII kwake na kwa KANISA.
HUYO  PADRE huendelea na masomo zaidi ya Elimu ya Kidunia ambapo husomea Taaluma mbalimbali ili aje alihudumie Kanisa Kimwili. 

Kila Padre mbali ya kuwa na ELIMU ya kiwango kikubwa cha Elimu ya THEOLOGY NA FALSAFA lakini pia Wana Elimu ya Kidunia. Kuna Mapadre WANASHERIA, MADAKTARI, WALIMU, MAINJINIA na kila aina ya Taaluma unayoifahamu wewe kwa kiwango cha MASTER'S, PHD NA UPROFESA . Lakini  vyeo hivyo vya kidunia haviluhusiwi katika Kanisa kuitana. Unaweza kuishi na Padre mtaani kwako lakini ana PhD, au ni Profesa au ana Masters.

Padre pia lazima asome na kufaulu vizuri sheria za Kanisa /Katiba ( Canon Law) ambazo ndo sheria na Katiba bora kabisa katika Dunia hii. Ukiona Nchi yeyote iko salama na inaendelea vizuri basi ujue imekopi na kupesti kutoka kwenye katiba bora kabisa ya Kanisa Katoliki. Nchi ya kwanza Kabisa kufaidika kwa kukopi na kupesti  katiba hii ni Marekani, Italy na Uingereza. Ndo maan Nchi zao ziko vizuri.

Huyo ndo PADRE /ASKOFU tunayeambiwa hawajui kitu.  Masomo hayo ya Upadre huchukua Miaka kuanzia  9 au 10.

Shemasi - Ni msaidizi wa Askofu Jimboni.
PADRE - Ni halifa wa wazee wa Kanisa waliokuwa wanachaguliwa  na Mitume kwa ajili ya kulisimamia Kanisa Mahalia.
Askofu Wakuu - mahalifa wa Mitume.
Papa - halifa wa Mtume Petro na Mkuu wa Kanisa na Askofu Mkuu wa Roma/ Vatican.

Kanisa pia linao Watawa kwa ajili ya kulihudumia Kanisa kimwili lakini Hawana daraja Takatifu.
Sister - watawa wa kike.
Mabruda / mabradha - watawa wa kiume.
Hawa Hawana mamlaka ya kutoa huduma ya Misa na SAKRAMENTI, Yaani Ubatizo, mpako wa Wagonjwa, ndoa Kitubio na Kipaimara
Wote nao kila unayemtazama ana Elimu kama hao wengine. Utofauti wao ni kutokutoa huduma ya kiroho  tu.

MWISHO;
NAOMBA MUWAULIZE WAWAPE NAMNA VIONGOZI WAO AMBAO WANADAI WANAIFAHAMU VIZURI BIBLIA NA MANDIKO MATAKATIFU WANAVYOPATIKANA. HII INAWAHUSU ZAIDI #MADHEHEBU YOTE YALIYOJITENGA NA KANISA. NA KUTUTUKANA ETI SISI NI MBUMBU HATUNA ELIMU YA BIBLIA,

MKATOLIK MWENZANGU WEWE NI NDUGU YANGU KIROHO LAZIMA NIZIDI KUKUFARIJI NA KUKUTIA NA NGUVU, NA UJIONE KUA UPO MAHALA SALAMA, FATA NA SHIKA YALE MAFUNDISHO YA BABA ZETU, SOMA BIBLIA ,HAKUNA KITAKACHOKUZUIA KUIONA MBINGU
KRISTU!!!!!.

No comments: