WITO WA PETRO NA YUDA ISKARIOTI
Kwa hiyo, WITO ni mwaliko wa Neema na Baraka. Lakini kama ilivyokuwa kwa yule kijana tajiri wa Injili, wale wanaopokea Neema hii ya Wito mtakatifu, wana uhuru wa kuipokea au kuikataa.
Kama ilivyokuwa kwa Petro, wanaweza kupambana kwa muda mrefu, kabla ya kujiachilia moja kwa moja kwa Kristo.
Kama ilivyokuwa kwa Yuda Iskarioti wanaweza kushawishiwa au ‘kutongozwa’ na matamanio ya ulimwengu huu (mali, sifa, heshima, cheo na uhuru nafsi) na hivyo kumsaliti Bwana wao waliyemfahamu na kumfuata muda mrefu.
Neema ya wito, inapopokelewa kwa uhuru kamili na kujitoa na kujiachilia kwa Kristo kwa ukarimu wote, tunaweza kuthibitisha kwamba, tumejitoa rasmi kuyaishi maisha mapya kwa ajili ya Mungu na kwa wokovu wa Nafsi zetu na ulimwengu wote.
Wito wetu ni matokeo ya uchaguzi huru wa Mungu kwa watu fulani.
Unapopokea zawadi ya wito unatarajiwa kujisalimisha na kujisadakisha, yaani, kuachilia yote na kushikamana na Kristo na daima kunuia kutekeleza utashi wa Mungu katika maisha yetu.
Fr. Innocent Bahati OFMCap,
Mwenge Catholic University (MWECAU-MOSHI)
+255755552538
No comments:
Post a Comment