Tuesday, February 4, 2020

KUWAOMBEA ADUI NI NEEMA

KUWAOMBEA MAADUI NI NEEMA

Kusali sala ya msamaha na kuwatendea mema maadui zetu wakati tukiwa bado katika giza hili nene kunadai ujasiri, neema na nguvu ya upendo. Inatudai ujasiri kukabiliana na hasira, chuki na hisia za kulipiza kisasi.

· Ni vigumu kusali wakati ni rahisi sana kulaani.

· Ni vigumu sana kuufunga ulimi wetu na kusali lakini ni rahisi kufungua ulimi wetu na kurusha makombora ya umbea, majungu, masengenyo na kejeli.

· Ni vigumu kumtendea adui yako mema lakini ni rahisi sana kuanzisha mchakato wa usaliti.

· Lakini, kwa wale wenye tabia inayojali kutokana na utambuzi wa heshima waliyonayo kwa kuumbwa kwa sura na mfano wa Mungu na kwamba wanakiri kazi ya uhulushi wa wenzao, wanawez kuvuka hivi vihunzi na kuanza maisha mapya wakiwasamehe madui zao na kuwaombea.

Fr. Innocent Bahati OFMCap,
Mwenge Catholic University (MWECAU-MOSHI)
+255 755552538// +255783942208
Itaendelea

No comments: