Tuesday, February 4, 2020

MAADUI WANATUIBIA UZURI WETU

MAADUI WANATUIBIA SEHEMU YA UZURI WETU-USIKUBALI

Maadui wanatuumiza na kutuibia sehemu ya maisha yetu.

Wanendelea kutuumiza nasi tunaendelea kuwagonga kila nafasi inapopatikana. Hasira na chuki dhidi yao inaendelea kukua siku baada ya siku.

Umbea, majungu, masengenyo, wivu na husuda ni ishara wazi ya chuki iliyofichika ndani yetu. 

Yesu anatuasa tuwapende na kuwaaombea maadui zetu. Haya ni mapinduzi ya kiimani ambayo hatuna budi kuyafanya ikiwa sisi ni wafuasi wa Kristo kweli.

Sala daima inatufanya tuwe na fikara njema, utulivu, kusamehe, na kuwa na mtazamo chanya.[1]

Kwa kuwapenda na kuwaombea maadui, ni utambuzi kwamba wao ni wanadamu kama sisi.

Tunaowaona kuwa maadui zetu nao pia wana matumaini, ndoto, furaha, na huzuni zao, wana madhaifu na mapungufu yao, lakini pia karama na vipawa.

Pengine wanapoumizwa kama wanavyoamini kuwa wako sawa, au wanapojisikia kutishiwa na sisi kama inavyotupata sisi.

Tukiwaombea tunatambua kuwa wao pia ni wana wa Mungu. Wao pia ni hazina, wanaopendwa sana na Mungu, wamesamehewa kwa Huruma kubwa na Mungu kama sisi pia.

[1] Prayer lowers the adrenalin levels in the body of the severely stressed person. It reduces chaotic thinking, panic reaction and calms the mind to be ready to respond maturely.

It lessens the ‘loop thinking’ syndrome i.e., repeatedly allowing the same distressing thought to go around  in one’s mind.

It induces relaxation, reduces stress, calms the body and promotes healing.

Fr. Innocent Bahati OFMCap,
Mwenge Catholic University (MWECAU-MOSHI)
+255 755552538// +255783942208
Itaendelea

No comments: