NENO UPENDO LIMENAJISIWA.
Wengi wa wanandoa vijana, mapadre na watawa vijana tumezaliwa kipindi “Ngono” inaonekana kama “Fun” (Starehe) na siyo wajibu mtakatifu. “Marupurupu ya ndoa” - LOVE ni ufupisho wa maneno: “*Legs Open Very Easily.*
Tupo chini ya utawala wa Enzi za ufalme wa chini ya kitovu.” Kimsingi Huu ni udhalilishaji wa hali ya juu na ni kuwageuza wengine kuwa vyombo au mashini za kujistarehesha.
Leo hii hatuongei kuwa ngono kuwa ni dhambi ya mauti ila tunazungumzia aina ya ngono inayokubalika kwa maana ya “Ngono Zembe na Ngono Salama.”
Binadamu amekuwa kiumbe cha ajabu. Licha ya kwamba tuna akili na utashi mambo tunayoyafanya kwa kweli yanadhalilisha hadhi yetu.
Tarehe 19/02/2016 huko Ujerumani, Radio BBC iliripoti kwamba kuna watu wawili ambao walienda mahakamani kushinikiza kwamba waruhusiwe kujamiiana na wanyama.
Baada ya majadiliano mahakama iliamua kwamba kuwalinda wanyama dhidi ya unyanyasaji wa kingono ni jukumu la kisheria. Sheria ya kuwadhalilisha wanyama nchini Ujerumani ni faini ya $27,700.
Baadhi yetu, tumezaliwa kipindi wazazi wanafanya tendo la ndoa na watoto wao, wanaume hata ndani ya ndoa wanafanya tendo hilo hadi miezi tisa ya mimba nk.
Athari zake ni kizazi cha wapenda ngono! Ndio maana kuzungumza juu ya nadhiri ya usafi wa moyo kwa wengine ni mlima usiopandika.
Ni kipindi watoto wengi wanazaliwa na wamama wazee (zaidi ya miaka 40) kwa vile Mama alikuwa akisoma na kupata degree zote kama njia ya kujikomboa na utumwa wa mfumo dume!!!
Matunda yake tuna kizazi cha wapambanaji na kuwaona viongozi katika uwajibikaji wao, ni wahafidhina na waliopitwa na wakati.
Kizazi hiki ni vigumu sana kuelewa maana ya nadhiri na ahadi ya utii, utii wa sheria pasipo shuruti.
Fr. Innocent Bahati OFMCap,
Mwenge Catholic University (MWECAU-MOSHI)
+255 755552538
No comments:
Post a Comment