TUJIKUMBUSHE TENA HAKUNA CHAKULA NAJISI.
Warumi 14:2,14,20
2 Mtu mmoja anayo imani, anakula vyote; lakini yeye aliye dhaifu hula mboga.
14 Najua, tena nimehakikishwa sana katika Bwana Yesu, ya kuwa hakuna kitu kilicho najisi kwa asili yake, lakini kwake yeye akionaye kitu kuwa najisi, kwake huyo kitu kile ni najisi.
20 Kwa ajili ya chakula usiiharibu kazi ya Mungu. Kweli, vyote ni safi; bali ni vibaya kwa mtu alaye na kujikwaza.
Marko 7:18-19
18 Akawaambia, Hivi hata ninyi hamna akili? Hamfahamu ya kwamba kila kitu kilicho nje ya mtu, kikimwingia, hakiwezi kumtia unajisi;
19 kwa sababu hakimwingii moyoni, ila tumboni tu; kisha chatoka kwenda chooni? Kwa kusema hivi alivitakasa vyakula vyote.
Wakolosai 2:16
16 Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato;
Waebrania 13:9
9 Msipeperushwe huku na huku kwa mafundisho tofauti ya kigeni. Neema ya Mungu ndiyo inayoimarisha roho zetu na wala si masharti juu ya chakula; Masharti hayo kamwe hayakumsaidia mtu yeyote aliyeyafuata.
Share na rafiki zako.
CHANZO : Kanisa Katoliki Na Biblia
No comments:
Post a Comment