Tuesday, February 4, 2020

HAUPO KWA BAHATI MBAYA

HAUPO KWA BAHATI MBAYA: JIPENDE, SAMEHE, ISHI

Mwenyezi Mungu anatuthibitishia kwamba sisi ni watu wa pekee, wema, tena wa maana na wa thamani kubwa.

Kwa kweli tukitambua kwamba Mungu anatupenda na kututhamini, kwamba sisi ni wa pekee na thamani kubwa tunapaswa kujivunia hadhi hiyo mbele ya Mungu na jamii. Ni katika ukweli huo tunaalikwa kujipenda sisi wenyewe, kumpenda Mungu na jirani kadhalika.

Ili tuweze kusali ni sharti kutenda tendo la kiimani kutokana na upendo wa Mungu usio na masharti. Katika sala tunamruhusu Mungu atupende sisi.

Mwenyezi Mungu anaongea na sisi tunasikiliza kwa imani. Neno la Mungu linahuisha na kuhaisha yote. Neno hilo linatuumba na kuturudishia tena ile hadhi ya kuwa waana wa Mungu, walioumbwa kwa sura na mfano wake. Sisi ni watoto wapendwa wa Mungu.

Mwenyezi Mungu ndiye chanzo, kiongozi na mwezeshaji wa uwepo wetu tangu shughuli nzima ya uhulushi (uumbaji). Ieleweke bayana kwamba hatukutokea tu (we are not by chance).

Ni katika mpango wa Mungu tuliumbwa kwa sura na mfano wake. Kabla ya nyakati Mungu alishatuchagua, na chaguo hilo ni kwa makusudi kamili, sio kwa bahati mbaya.

Mwenyezi Mungu alikuwa na uwezo wa kuumba binadamu wa aina yeyote, kila alipoiangalia historia ya dunia.

Na kati ya mamilioni ya watu ambao walikuwa kwenye akili ya Mungu, jicho lake lilikutazama wewe kwa namna ya pekee, akapendezwa nawe, akakuumba na kukuweka hapa duniani. Aliona wote ambao wangaliweza kuwapo hapa duniani, lakini kishaamua kwamba wewe NDIYE.

Alifanya hivyo kwa sababu kuna jambo ambalo alipenda Wewe ulifanye hapa duniani, kadiri ya nyakati na hali au hadhi inayoendana na Wewe. Hayo ndiyo yanayothibitishwa hapo juu na Franklin Victor na Mt. Henry Newmann.

Fr. Innocent Bahati OFMCap,
Mwenge Catholic University (MWECAU-MOSHI)
+255 755552538
Itaendelea....

No comments: