MSAMAHA SIYO NJIA-MKATO au UAMUZI WA SIKU MOJA
Msamaha ni mchakato unaohusiana mtiririko wa maamuzi. Si jambo la kukaa chini siku moja na kutangaza kwamba nimekusamehe. Msamaha hautendeki kivile. Wala hatuwezi kuweka mipango wiki au miezi ya kusamehe. Inachukua muda.
Baadhi, msamaha unaweza kutokea kwa asili, wakati hali ya uponyaji inaendelea. Kwa wengine inachukua muda mfupi na kwa wengine muda mrefu, inategemea madonda yaliyosababishwa na umizo lile na jinsi ya kurudisha sifa yetu iliyopotea. Hata hivyo inafaa kusamehe kwa kuwa inaleta uponyaji kamili na amani.
MSAMAHA WA KWELI
Dr. Sidney Simon, mtaalamu anayetambulika katika fani hii ya uponyaji, anatupa ufafanuzi makini kuhusu msamaha kadiri ya uelewa unaoendana na mahusiano ya wanadamu: “Msamaha ni kujiweka huru ili kutumia nguvu zetu ambazo hapo awali zilihujumiwa kutokana na shauku ya kulipiza kisasi, kushika kinyongo, na kufuga madonda yasiyoponyeka.
Ni ugunduzi mpya wa nguvu tulizomiliki na kupangilia uwezo wetu usio na ukomo katika kuwaelewa na kuwapokea watu wengine na sisi wenyewe.”
Msamaha hauelekei kutudhoofisha na kutufanya sisi kukubali kuwa wahanga wa majeraha.
Kiitikadi, msamaha unatupelekea kwenye mchakato mzima wa maridhiano, hata hivyo ili hili lifanyike ni lazima lihusishe pande zote husika (reciprocity – nipe nikupe) pale ambapo kila mmoja anatambua aliyoyafanya na kunuia kurekebisha mambo.
Msamaha unaotolewa na upande mmoja si mara zote unaendana na maridhiano. Tunahitaji kufahamu tofauti iliyopo baina ya msamaha na maridhiano (forgiveness and reconciliation).
Fr. Innocent Bahati OFMCap,
Mwenge Catholic University (MWECAU-MOSHI)
+255 755552538// +255783942208
Itaendelea....
No comments:
Post a Comment