NI NINI KITAKACHOTUSAIDIA KUSAMEHE?
Kuna kiongozi mmoja wa kiroho ambaye alikuwa anazunguka katika miji na vijiji akihubiri juu ya msamaha na toba.
Siku moja katika mahubiri yake alikumbana na mtu aliyejeruhiwa sana na ambaye hakuwa tayari kusamehe.
Mahuburi ya kiongozi huyu yalikuwa ni mwiba nafsini mwake. Aliamua kumshambulia kiongozi huyu wa kiroho ili kumkatisha tamaa.
Wakati wenzake wakihangaika kumtuliza na kumomba kiongozi yule wa kiroho amtulize, kiongozi wa kiroho alikuwa na utulivu wa hali ya juu na tabasamu kali. Baadhi ya wana mafungo walimwuliza mbona huelekei kutikisika na kile kinachoendelea hapa? Kwa nini hujibu mashambulizi.
Kiongozi wa kiroho akauliza swali: Hebu fikiri una zawadi mkononi mwako lakini unaponuia kuitoa ile zawadi inakuwa ya nani? Wakajibu, inabaki kuwa mali ya mwenye kuitoa. Mmejibu vema. Ndivyo ilivyo hapa, sijapokea hata kidogo matusi, dharau na mashambulizi anayoyaelekeza kwangu.
Msamaha sio sana tunda la akili au maarifa tuliyosoma darasani. Zaidi mno msamaha ni zawadi ya neema na nguvu ya Roho ndani yetu. Msamaha unatiririka, kimsingi kutoka hali yetu ya kusamehewa.
Msamaha ni vigumu kwa wale ambao hawajawahi kuonja kusamehewa, hususani, katika utoto wao. Ni maang’amuzi ya kina ya jinsi tulivyoonja msamaha yatatuwezesha hata sisi kuwazawadia wengine msahama.
Msamaha ni upendo unaorehemu wale ambao wamejeruhiwa, walio dhaifu, walio na mashaka na waliosambaratisha ule muungano wa asiili.[1]
Kwa kusamehe tunafungua milango ya baraka na neema, kwa kutokusamehe tunafunga milango hiyo, tukiibua chuki, hasira, huzuni, na kwa neno moja tunajizamisha kwenye utamaduni wa majanga – hatimaye – kifo.
Kwa hivyo tunapaswa kuchukua tahadhari kuona kwamba chuki kwa maadui zetu haizamishi mizizi mioyoni mwetu ikiwa tunataka kuwa wenye afya ya roho na mwili, kisaikolojia na kijamii.
Kama tukiruhusu chuki iote mizizi, ikakua na kutoa maua ndani yetu, inaharibu wema na uzuri ndani yetu, ikituacha tuliojaa chuki, na viumbe duni tusio na furaha. Hapa ni baadhi ya misaada kutusaidia kuanzisha mchakato wa msamaha ndani yetu na katika Jumuiya......
[1] Only a deep experience of forgiveness can enable us to gift it to others. Forgiveness if the agape or compassionate love offered to another whois wounded, vulnerable, fearful and who has broken the unity.
Fr. Innocent Bahati OFMCap,
Mwenge Catholic University (MWECAU-MOSHI)
+255 755552538// +255783942208
Itaendelea
No comments:
Post a Comment