Tuesday, February 4, 2020

FAMILIA ZILIZOJERUHIWA NI CHANGAMOTO

FAMILIA ZILIZOJERUHIWA NI CHANGAMOTO

Tunapoongea juu ya Familia zilizojeruhiwa hapa tunataka kumaanisha; Mume na mke waliotengana, Mume na mke waliotalikiana ambao hawajaoa au kuolewa,  Mume na mke waliotalikiana na kila mmoja ameoa tena au kuolewa,  Familia ya mzazi mmoja hususani mmoja anapoachika na kuachiliwa watoto.

Majeraha ya Familia ni mengi, na tena madhara na mateso kwenye Familia hizo ni makubwa. Ikiwa mmoja wa wanandoa anajikuta katika hali ya utengano, basi hali hiyo ya kushindwa katika maisha ya ndoa inakuwa ni majeraha ambayo mmoja anapaswa kuyabeba kwa maisha yake yote, hata kama anafanikiwa kuingia kwenye muungano mwingine ambao unaonekana kusitawi.

Tunapotafakari hali ya wale ambao wametengana, wametalikiana, wameachika, mateso ya wale ambao wanalazimika kusambaratisha mahusiano yao kwa sababu ya kutotendeana kwa haki, manyanyaso, vurugu na fujo, uchungu na adha wanayokumbana nayo Familia za mzazi mmoja hatuwezi kuacha kusema kwamba kilio chao ni kikubwa hata kama hakiko bayana.

Kwa upande wa Afrika, Familia isiyokuwa na mtoto inahesabika kwamba imefeli au kushindwa sana.

Jambo hili sio geni katika Maandiko Matakatifu: Mateso ya mama mtarajiwa wa Samueli, yalimfanya akeshe hekaluni kumwomba Mwenyezi Mungu ampatie mwana (rej. 1Sam 1:9-18).

Mahangaiko waliyokuwa nayo Zakaria na Elizabethi, ambao sala yao ilijibiwa na Bwana kwa kupewa mtoto (Yohani Mbatizaji) (rej. Lk 1:5-25).

Fr. Innocent Bahati OFMCap,
Mwenge Catholic University (MWECAU-MOSHI)
+255 755552538

No comments: