UMEUMBWA ILI UWAJIBIKE: TENGENEZA MAISHA YAKO
Katika haya yote, ni marufuku kukataa tamaa haijalishi tunakumbana na changamoto gani. Usikate tamaa. Wapokee wote wanatembea katika njia ya maisha yako kama zawadi.
Uwe na shukrani kwa wanaokupenda, wanaokujali na kukuthamini. Uwapokee wote kama sehemu ya darasa katika maisha, ukijifunza namna kukabiliana na hali zote katika hali ya utulivu.
Kumbuka kwamba maisha katika ujumla wake ni shule ambapo hakuna anayehitimu. Kila siku ni siku ya kukua kuelekea ukamilifu wetu kimaisha sawa sawa na mpango wa Mungu.”
Hatukuumbwa katika hali ya utupu! Mwenyezi Mungu, kusudi uweze kukamilisha mpango wake hapa duniani, alikupa zawadi ya maisha, wito, karama na vipaji, fadhila na ujasiri, uwezo wa kuona na kuamua, akikufungulia milango ya elimu na ufahamu, fursa na watu, matukio au mazingira yatakayowezesha kufikia malengo yale ambayo kwayo uliumbwa.
Katika udhaifu wetu, Mwenyezi Mungu ameweka ndani ya nafsi zetu aina ya rada ambayo inatuwezesha kusoma alama za nyakati, kuona hatari na fursa zilizo mbele yetu. Haya yote yametuwezesha kuendelea kufanya chaguzi huru za maisha, ijapo mara nyingine kwa msaada wa wengine.
Mikono iliyotufinyanga na kutuumba, kwa hakika imeacha alama isiyofutika na ujuzi wa pekee, ndio maana sisi tunaweza kushiriki, kwa ufundi mkubwa, tena tukisukumwa na upendo na uwezo wake wa Kimungu, katika kazi ya uumbaji, kutunza na kuendeleza yote sawa sawa na urari wake.
Tunaalikwa kutafakari umilele wake, ili kufurahia jinsi ambavyo anatushirikisha hata sisi, kwa kuwa tuna mwanzo lakini hatuna mwisho, kwani roho zetu kisha kuumbwa na Mungu hazifi tena.
Fr. Innocent Bahati OFMCap,
Mwenge Catholic University (MWECAU-MOSHI)
+255 755552538
Itaendelea
No comments:
Post a Comment