Tuesday, February 4, 2020

MWANAMPOTEVU

MWANAMPOTEVU ALIONJA UPENDO NA MSAMAHA WA BABA.

Upendo aliouonja mwana mpotevu ndilo pendo ambalo kila mmoja wetu anaalikwa kuung’amua maishani. Ili kung’amua hilo hakika ni lazima kuvuka vihunzi vingi.

Kishawishi kikubwa zaidi ya vyote ni kile cha kufikiri kwamba sisi hatupendwi au tusiostahili kupendwa na Mungu au na jirani kwa jinsi ambavyo tulitapanya pendo la Mungu kwa dhambi zetu.

Ni sharti tubandukane na mtazamo hasi wa maisha unaotokana na hali yetu ya kibinadamu. Kama tulipendwa kwa masharti, ni lazime tuutafute upendo kwa kufanya kazi.

·Wapo waliopongezwa walipotenda jambo jema, kukaripiwa au kuadhibiwa walipotenda jambo baya.

·Kuna nyakati tulisutwa hadharani, hata hivyo tulivaa barakoi (mask) kuonesha kwamba mambo yako shwari, ila kwenye kima na miimo ya mioyo yetu tunafahamu kwamba mambo sio shwari, na huenda tunajichukia.

Upendo wa Mungu kwetu ni lazima ung’oe hisia hizi za chuki. Ndio maana leo tunaalikwa kuwapenda maadui zetu kwani sisi tulipokuwa maadui wa Mungu basi tulisamehewa. Nayaweza yote katika Yeye anitiaye nguvu.

Fr. Innocent Bahati OFMCap,
Mwenge Catholic University (MWECAU-MOSHI)
+255 755552538// +255783942208
Itaendelea...

No comments: